Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza
Mukandala amekanusha taarifa zilizozagaa zinazodai kuwa msanii wa Bongo
Fleva Diamond Platnumz atatunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) kutokana na
mchango wake kwa jamii.
Akizungumza na Power Jams ya East Africa Radio, Prof. Rwekaza
Mukandala ambae yupo nje ya nchi kwa sasa amesema taarifa hizo si za
kweli ni uzushi tu.
↧