BAADHI ya wakazi wa Mji wa Shinyanga, wamepinga vikali kitendo cha baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kumshambulia kwa maneno ya kejeli aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba wakidai mashambulizi hayo yaelekezwe kwa wananchi waliotoa maoni yao katika tume.
Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti mjini humo jana, wakazi hao wamedai
↧