Nuh Mziwanda jana alijikuta katika wakati mgumu mjini Tabora baada ya
Shilole kuwauliza wakazi wa mkoa huo anakotokea iwapo Nuh Mziwanda
anafaa kuwa mume wake.
Shilole ambaye ni mchumba wa Nuh alifunguka mbele ya mashabiki wa
Tabora waliokuwa wamefurika kushuhudia show ya Serengeti Fiesta kutaka
kujua kama wanamtaka Nuh Mziwanda awe shemeji yao kitu ambacho mashabiki
hao walikataa.
↧