Kesi ya aliyejifanya askari polisi wa usalama barabarani, James Hassan (45) imeendelea kupigwa kalenda kutokana na mshitakiwa kutofika mahakamani hapo licha ya kuwepo kwa mashahidi wawili.
Kesi hiyo iliyofikia hatua ya kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imekuwa ikipigwa kalenda mara kwa mara kutokana na mshitakiwa huyo kudai kwamba anaumwa hivyo kukwamisha kesi hiyo
↧