BAADA ya jina lake kutajwa kuwa miongoni mwa watu watakaowania urais,
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amesema zipo taratibu ndani ya chama chake
za kutangaza kuwania nafasi hiyo na kusema kinachoendelea hivi sasa ni
juhudi binafsi za watu.
Pinda alisema hayo jana nyumbani kwake jijini Dar es Salaam
alipokutana na wahariri wa Mtanzania, kuzungumzia masuala mbalimbali
yanayolikabili taifa.
↧