Jana ilikuwa kama sinema pale viongozi wa
Kamati Namba Moja ya Bunge Maalumu walipojikuta wakibishana na mjumbe
wao mbele ya waandishi wa habari, huku siri za mambo ya ndani ya vikao
zikianikwa hadharani.
Kamati hiyo inaongozwa na Naibu Waziri, Ofisi ya
Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na makamu wake ni Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, huku ikiwa imesheheni
↧