Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitawapima mwezi ujao Waziri Mkuu mstaafu,
Edward Lowassa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Benard Membe ili kujua ni kwa kiasi gani wametekeleza masharti
yatokanayo na adhabu wanazotumikia kutokana na kukiuka kanuni na
taratibu za chama hicho kwa kutangaza kabla ya wakati juu ya nia yao ya
kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu 2015.
↧