Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba
ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta
kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge
Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na
habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na
Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.
↧