Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, ameteleza ulimi tena na mara hii amejikuta akimuita Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) tumbili.
Kabla ya kutoa kauli hiyo, Werema alikuwa akitoa ufafanuzi wa mwongozo ulioombwa na Kafulila, kuhusu fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambazo zimelipwa kwa kampuni ya PAP,
↧