SERIKALI imesema kuwa ndege zinazoonekana mpakani mwa Tanzania na
Malawi ni maalumu kwa ajili ya kufanya utafiti na vyombo vya udhibiti
wa anga vimezipa vibali vya kuwa katika maeneo hayo.
Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison
Mwakyembe wakati akijibu mwongozo wa Mbunge wa Ileje, Aliko Kibona
(CCM), aliyetaka ufafanuzi wa uwepo wa ndege hizo
↧