Mwimbaji wa bongo Flava, H Baba amelazwa hostpitali ya Taifa ya
Muhimbili baada ya madaktari kugundua kuwa ana ugonjwa wa dengue ambao
umeshawauguza watu mbalimbali.
H Baba alipelekwa hospitalini hapo jana usiku, na inaelezwa kuwa
alianza kujisikia anaumwa tangu Jumatano (June 5), wakati anajiandaa
kwenda kuuaga mwili wa marehemu George Tyson aliyefariki kwa ajali ya
gari.
↧