Jana usiku wadau wa filamu na vipindi vya TV walipatwa na mshituko
baada ya kupata taarifa kuwa muongozaji mahiri wa filamu na vipindi vya
runinga, George Tyson amefariki katika ajali ya gari.
DJ Choka alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa kwenye msafara mmoja na
timu ya The Mboni Show na marehemu George walioelekea Dodoma kutoka Dar
es Salaam Alhamisi (May 29) na kurudi wote (May 30).
↧