Picha za ajali iliyotokea asubuhi ya leo huko Makongo jijini Dar es
Salaam ambapo lori lililokuwa limebeba mchanga lililiangukia gari dogo.
Juhudi za Askari wa Jeshi la Wananchi wakishirikiana na kikosi cha
zimamoto na uokoaji zilifanikisha kumnasua kutoka kwenye mchanga dereva
wa gari dogo mwendo wa saa moja u nusu hivi asubuhi baada ya kuwemo ndani ya gari hilo tangu saa 11 afajiri.
↧