MAJONZI na vilio vilitawala juzi katika zoezi la kuuaga mwili wa
marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ kwenye Viwanja vya Leaders lakini mmoja
wa waliotia fora katika kuangua kilio alikuwa dada mmoja mzungu
anayedaiwa kuwa alikuwa Mpenzi wa Ngwea aitwaye Misheily.
Mzungu huyo alionekana akilia kwa uchungu huku akitoa maneno
yaliyoashiria kuwa ameumia sana kuondokewa na ‘mtu’ wake huyo
↧