Mvua
kubwa ziliyonyesha mfululizo kuanzia juzi maeneo mbalimbali jijini Dar
es Salaam zimesababisha vifo vya watu kumi na kuharibu miundombinu ya
barabara ikiwamo madaraja sita kubomoka.
Aidha, mradi wa mabasi yaendayo kasi (Dart) umelazimika kusimamisha
shughuli zake, baada ya ofisi zake za Jangwani kukumbwa na mafuriko na
kusababisha hasara ya zaidi ya Dola za Kimarekani 30,000.
↧