Baada ya kampeni zilizodumu kwa mwezi mmoja, hatimaye uchaguzi mdogo
wa Ubunge katika Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo, Pwani unatarajiwa
kufanyika leo ili kumpata mrithi wa Said Bwanamdogo aliyefariki dunia
Januari 22 mwaka huu kutokana na maradhi.
Katika kipindi chote cha kampeni, vyama vitano vilichuana kumwaga
sera usiku na mchana katika Kata 15 za jimbo hilo, kila kimoja
↧