MWENYEKITI wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta ameanza kazi na kuwaonya wajumbe wa bunge hilo ambao wamekuwa na tabia ya kupayuka ovyo kwenye vipaza sauti, kuwa wasimlaumu kwa vile atawabana kwa kutumia kanuni walizozitunga wao wenyewe.
Sitta ameanza kazi huku wajumbe wengi wakiwa na imani naye kuwa ataliendesha Bunge hilo lenye mchanganyiko wa watu kwa haki na kwa viwango na kasi;
↧