Mchungaji Christopher Mtikila amechafua hali ya hewa bungeni, kwa kumtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Kificho
amueleze ni kwanini tangu jana amekuwa akimnyima nafasi ya kuzungumza
bungeni.
Mchungaji Mtikila alisimama ghafla na kusema: Mwenyekiti kwanini
unaninyima haki yangu ya kuzungumza, nataka kujua kwanini unaninyima
haki ya kuzungumza. Kuzungumza ni haki yangu.
↧