KAMATI ya Mazishi ya aliyekuwa Msanii wa Bongo Fleva, Albert Mangwea
‘Ngwea’, mpaka jana mchana ilikuwa imekusanya jumla ya Sh milioni 32
kutoka kwa wadau mbalimbali.
Kamati hiyo inahitaji Sh milioni 50 kwa
ajili ya kusaidia kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Afrika Kusini
mpaka Morogoro kwa ajili ya mazishi. Fedha hizo pia zinahitajika kwa
ajili ya kuratibu shughuli nzima ya mazishi.
↧