Na
Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Watu wanne (wanaume) ambao bado hawajafahamika wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 35 ambao wanasadikiwa kuwa
ni majambazi wameuawa baada ya kupigwa risasi na askari Polisi. Tukio hilo
lilitokea tarehe 21.02.2014 muda wa saa 1:00 jioni katika bar moja iitwayo
Pama iliyopo maeneo ya Makao Mapya jijini hapa.
↧