SIKU chache baada ya Waziri wa zamani na Mbunge wa Urambo Magharibi,
Profesa Juma Kapuya (CCM) kutuhumiwa kumbaka na kutishia kumuua binti
mdogo wa miaka 16, kiongozi huyo ameibuka na kutoa utetezi wa
kujikanganya.
Akizungumza kupitia kwa wakili wake, Yasin Memba, mbunge huyo
alitishia kuliburuza gazeti la Tanzania Daima mahakamani endapo halitamwomba msamaha
ndani ya siku saba.
↧