Wakati vikosi vya Umoja wa Mataifa vikisitisha kwa muda
operesheni ya kukabiliana na Kundi la M23 Mashariki kwa Jamhuri ya
Demokrasia ya Congo, ili kupisha mazungumzo ya amani, kundi hilo
limesema liko tayari kuweka silaha chini.
Mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mapigano kati ya kundi hilo na Jeshi la DRC, yalitarajiwa kuanza jana mjini Kampala,Uganda.
↧