HATIMAYE serikali imesalimu amri na kuamua kuwalipa mishahara ya
miezi minne wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
(TAZARA) waliogoma wakishinikiza kulipwa stahiki zao.
Uamuzi wa kuwalipa wafanyakazi hao ulitangazwa jana bungeni na Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alipokuwa akitoa kauli ya serikali
kuhusu mgomo wa wafanyakazi hao ulioanza Agosti 23 mwaka huu.
↧