Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Aweso Amuagiza Katibu Mkuu Wizara Ya Maji Kutengua Uteuzi Wa Meneja Wa Ruwasa Mkoa Wa Mara

$
0
0


WAZIRI wa Maji, Mhe.  Jumaa Aweso (Mb) amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga kutengua uteuzi wa Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mara, Mhandisi Sadick Chakka na mwenzake wa Wilaya ya Tarime Mhandisi Marwa Murasa kwa kushindwa kusimamia vyema utekelezaji wa miradi ya maji.

Maelekezo hayo yametolewa Wilayani Tarime  tarehe 5 Januari, 2021 alipokuwa kwenye mradi wa maji wa Magoto ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani Mara.  

Awali akipokea taarifa ya miradi, Ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Waziri Aweso alisisitiza kwamba taarifa haina uhalisia na aliwaelekeza wataalam hao kueleza halihalisi ya miradi na sio kudanganya.

Akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa taarifa, Mbunge wa Tarime Vijijini na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Mwita Waitara (Mb) ambaye aliambatana na Waziri Aweso alimueleza kuhusu  adha ya huduma ya maji kwa wananchi wa Tarime.

Mhe. Mwita alisema kwamba miradi mingi ya maji Wilayani Tarime inachangamoto na hivyo alimuomba Waziri Aweso kuchukua hatua stahiki kwa wote wanaohusika kuchelewesha utekelezwaji wa miradi

Taarifa ya miradi sambamba na maelezo ya Naibu Waziri Mwita na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri kuhusu hali halisi ya miradi ya maji wilayani humo ilimsukuma Waziri Aweso  kutofuata ratiba ya kukagua miradi iliyokuwa imepangwa na wataalam hao na badala yake alielekeza kupelekwa kwenye miradi mingine yenye changamoto ambayo haikuwepo kwenye ratiba.

"Nimepitia taarifa ya wataalam wetu hapa na hii ratiba waliyopanga sikubaliani nayo, sasa nataka mnipeleke kwenye miradi mingine na siyo hii mliojipangia nyinyi ili tu kunifurahisha,” Waziri Aweso aliwaelekeza wataalam hao.

Waziri Aweso aliijadili taarifa hiyo ya utekelezwaji wa miradi Wilayani Tarime na huku akimtaka Meneja huyo wa Mkoa kueleza hali ya mradi mmoja baada ya mwingine na huku akibainisha kiasi cha fedha kilichopo kwenye akaunti ambacho kilipaswa kuwa kimetumika kutekeleza miradi.

“Bora hata kisingizio ingekua fedha kama ambavyo hua mnadanganya lakini sasa hapa Mkoani Mara tumeleta zaidi ya shilingi bilioni nane na fedha iliyopo kwenye akaunti kwa sasa ni zaidi ya shilingi bilioni 3 hivi ni nani atakuelewa watu hawana maji wewe kwenye akaunti unayo fedha ya kutosha,”  Waziri Aweso alihoji.

Alisema lengo la kuanzisha RUWASA ni kuhakikisha wananchi wanapata maji na kwamba maelekezo ya awali ni kwamba kabla utekelezwaji wa miradi haujaanza kila Meneja wa RUWASA Mkoa alipaswa kuwasilisha taarifa ya kuainisha miradi kichefuchefu yaani miradi iliyokuwa ni kero kwa wananchi lakini RUWASA Mkoa wa Mara haikufanya hivyo.

“Wananchi wanachohitaji ni maji bombani, hatutokubali kumuona Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli akiumia na kusononeka kuona wananchi wake wanateseka hawana maji na sisi tupo, hii haipendezi hata mbele za Mungu, tumemuahidi kufanya kazi na sasa tunahakikisha wananchi wanapata huduma ya uhakika ya majisafi na salama,” alisema Waziri Aweso.

Aliongeza kuwa taarifa ya hali ya miradi wilayani humo inasikitisha kwani tathmini aliyoifanya inaonyesha miradi mingi imekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 lakini haitoi maji na hivyo aliwataka wataalam kote nchini kutumia vyema utaalamu wao badala ya kujiamulia kujenga miradi kiholela.

“Haiwezekani mradi upo asilimia 98 na hautoi maji, unawezaje kujenga tenki hali yakuwa huna uhakika kama maji yapo? Ulipaswa kujiridhisha na chanzo chako kwanza ili kuhakikisha maji yapo yakutosha na hatua zingine zinafuata,” Waziri Aweso alisisitiza.

Baada ya mahojiano ya muda mrefu na Mameneja hao kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Waziri Aweso alielekeza msafara alioambatana nao kutembelea mradi wa maji wa Magoto ili kujionea hali halisi ya utekelezwaji wake.

Aidha, mara baada ya kutembelea mradi huo na kujionea hali halisi sambamba na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo, Waziri Aweso alijiridhisha pasi na shaka kwamba mradi huo haujatekelezwa kama inavyopasa.

Hali hiyo kwa ujumla na taarifa iliyowasilishwa kwake hapo awali pamoja na maelezo ya viongozi na wananchi wa Kata ya Nyakonga ilipelekea Waziri Aweso kumuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Maji kutengua uteuzi wa Mameneja hao na alimtaka kufika Mkoani Mara ili kujionea hali ya miradi sambamba na kuunda kamati itakayochunguza miradi kichefuchefu yote mkoani humo.

“Namuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Maji kutengua uteuzi wa Mameneja hawa mara moja na wapewe wengine watakaomudu majukumu haya ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya uhakika na toshelevu,” alielekeza Waziri Aweso.

Alisema miradi mingi Mkoani Mara hairidhishi na hivyo ni muhimu Katibu Mkuu akaitupia jicho RUWASA hususan watendaji wake na kwamba wasiokuwa na uwezo waondolewe na alisisitiza kwamba ni muhimu kujiridhisha uwezo wa wataalam kabla ya kuwapanga.

Waziri Aweso vilevile alielekeza miradi yote ya maji iwe shirikishi, viongozi na wananchi wa maeneo husika wawe na uelewe wa pamoja wa kinachoendelea ili kuepuka kucheleweshwa ujenzi wake.

Waziri Aweso yupo Mkoani Mara kwa ziara ya siku tatu ya kukagua miradi ya maji hususan inayotekelezwa maeneo ya vijijini.


Njombe:Watu wanne watiwa nguvuni kwa tuhuma za wizi wa nyaya za umeme

$
0
0


Na Amiri Kilagalila, Njombe
WAKATI Serikali ikielekeza nguvu kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na nishati ya umeme, mkoani Njombe watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika wilaya ya kipolisi mjini Makambako kwa tuhuma za kukutwa na nyaya za umeme zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43 zinazotumika kusambazia umeme wa mradi wa REA.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema hatua hiyo imekuja baada ya jeshi la polisi kufanya upelelezi wa kuwanasa watuhumiwa hao, kufuatia aliyekuwa msimamizi wa mradi wa Rea katika kata ya Kichiwa Tarafa ya Makambako kutoa taarifa kwenye jeshi hilo alipogundua dram sita za nyaya za umeme zenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni 43 kuibwa .

“Tumekamata gari aina ya fuso na imebeba waya Rol zipatazo sita na hizi rol zipo nyaya za aina mbili tofauti zinazotumika kwenye umeme wa rea hapa mkoani Njombe”alisema Hamis Issa

Kamanda Issa amesema wamefanikiwa kukamata gari hilo kutokana na ufuatiliaji uliofanywa na vikosi vya polisi.

“Tuliweza kubaini kutokana na nyaraka iliyodondoka ya faini iliyotozwa hii gari,ikajulikana iko Dar Es Salaam,amefuatwa tajiri akasema gari iko Katavi na tulipofuatilia tuliikuta Mlele sehemu moja inatwa maji moto”alisema Kamanda Issa.

Vile vile ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuliamini jeshi hilo kwa kuwa lipo imara na watahakikisha jeshi linalinda miradi yote ya serikali hivyo wananchi wawe tayari kutoa taarifa miradi inapohujumiwa.

Waziri Mhagama: Majeruhiwa Ajali Ya Treni Waruhusiwa Wote

$
0
0


MWANDISHI WETU
Majeruhi 66 waliopata ajali ya treni iliyotokea mwishoni mwa wiki (Januari 2, 2021) wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka hospitali kutokana na  hali zao kuimarika mara baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama ametembelea Januari 4, 2021 na kuwajulia hali majeruhi hao waliokuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali hiyo ambapo hadi sasa wameruhusiwa wajeruhi wote.

Waziri alionesha kufurahishwa na huduma zilizotolewa kwa majeruhi hao na kupongeza jitihada zilizofanyika katika kuokoa maisha yao.

Alielezea kuwa, Serikali imefanya Uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya,na hivyo kuwezesha kutoa huduma kwa namna bora na weledi wenye  kwendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Akiwa wodini hapo waziri alipata fursa ya kuzungumza na majeruhi na kuwaeleza adhima ya Serikali ni kuona inaendelea kuratibu na kuboresha miundombinu muhimu ikiwemo ya barabara na afya ili pindi zinapotokea ajali kama hizo kuona jamii haipatwi na madhara makubwa kutokana na uwepo wa miundombinu rafiki inayosaidia kuondokana na madhara ya majanga.

“Kipekee ninawapa pole wale wote waliopatwa na ajali hii  iliyosababisha vifo na majeraha kwa wengine. Serikali imeguswa na ajali hili na tuwaaahidi tupo pamoja na tutaendelea kuhakikisha huduma zetu zinatolewa kwa ubora na wakati,” alisema Waziri

Waziri alieleza kuwa, Serikali kupitia Idara ya Uratibu wa Maafa itaendelea kuweka mikakati thabiti katika kuhakikisha inakuwa na mipango madhubuti ili kuyakabili majanga mbalimbali pindi yanapotokea katika kuokoa maisha ya wananchi na mali zao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe, Gerald Maganga alimshukuru Waziri kwa ziara hiyo na kupongeza shirika la Reli kwa namna walivyosaidia katika kuhakikisha walionusurika wanaendelea na safari zao.

“Niwapongeze watendaji wa shirika la Reli walivyoshiriki kwa kuhakikisha kunakuwa na mabasi yanayotoa huduma kwa abiria walionusurika na ajali hii kwa kupatiwa usafiri na kuendelea na safari zao bila usumbufu wowote,”alisema Bw. Maganga

Naye mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo Bw. Stephano Kasole alieleza furaha yake kuhusu huduma bora zilizotolewa na hospitali hiyo na kuipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu muhimu katika sekta ya afya.

“Tumepokelewa vizuri na kupatiwa huduma kwa wakati, hii imechangia kupata nafuu mapema sana, na leo nimefarijika kwa kuwa nimeruhusiwa kutoka,”alisema Kasole

AWALI

Treni ya abiria ilipata ajali tarehe 02 Januari, 2021 ilikuwa imebeba abiria 720 iliyokuwa safarini kutoka Jijini Dar es Salaam ikielekea maeneo ya Tabora, Katavi (Mpanda), Kigoma na Mwanza ilipata ajali kutokana na mvua zilizonyesha na kusababisha uharibifu wa miundombinu na kupelekea kusobwa kwa tuta la njia ya reli.Ajali ilisababisha vifo vya watu watatu na majeruhi 66.

Waziri Simbachawene Akabidhi Cheti Na Shilingi Milioni Moja Kwa Askari Wa Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji

$
0
0


 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (Wakwanza kushoto) akimkabidhi Cheti cha Kutambua Ujasiri na Utendaji Kazi Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Koplo Denis Minja, aliyeokoa maisha ya mtoto wa miaka miwili aliyekuwa ametumbukia kwenye shimo la choo Mjini Karagwe. Tukio hilo limefanyika leo katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo Mtumba, Jijini Dodoma. 

Trump apata pigo jingine Georgia.....Warnock kutoka chama cha Democratic ashinda katika uchaguzi muhimu wa maseneta

$
0
0


Mgombea wa wa chama cha Democratic Raphael Warnock ameibuka mshindi katika uchaguzi wa maseneta dhidi ya mgombea wa chama cha Republican Kelly Loeffler katika jimbo la Georgia, kulingana na vituo vya habari vya CNN, CBS na NBC leo Jumatano, Januari 6.

Raphael Warnock, mchungaji wa kanisa huko Atlanta ambapo Martin Luther King alifanya kazi, ataandika historia kwa kuwa seneta wa kwanza mweusi aliyechaguliwa katika jimbo hili la kusini.

Chama cha Democratic kinatarajia kushinda uchaguzi mwingine mdogo wa maseneta katika jimbo la Georgia kuchukua udhibiti wa Bunge la Seneti

Hili ni suala kubwa kwa utawala wa Joe Biden, ambaye atakabidhiwa madaraka Januari 20.

Donald Trump alikuja kuwaunga mkono maseneta wawili kutoka chama cha Republican wanaomaliza muda wao ambao wanawania nafasi zao katika Bunge la Seneti Jumanne hii, Januari 5.

Donald Trump anaendelea na msimamo wake wa kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi mpinzani wake kutoka chama cha Democratic, Joe Biden.


Hata hivyo, matokeo ya kura yalihesabiwa mara kadhaa huko Georgia na ni wazi: Joe Biden ndiye ambaye alishinda uchaguzi wa urais na ndiye ambaye alishinda katika jimbo hili kwa kura 12,000 dhidi ya Donald Trump.

Uchaguzi Uganda: Museveni ateua mwanajeshi kusimamia usalama

$
0
0


Rais wa Uganda,
Yoweri Kaguta Museveni, ameamua kumteua Brigedia Kayanja Muhanga, kusimamia masuala ya usalama wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo unaotarajiwa kufanyika tarehe 14 Januari 2021.
 

Uteuzi ho unampa nafasi Brig. Muhanga kuratibu vikosi vyote vya usalama nchini humo ambavyo vitasubiri sauti yake katika utekelezaji wa jambo lolote.

Luteni Deo Akiiki ambaye ni Naibu Msemaji wa Jeshi la Uganda amesema, Brig. Muhanga atakuwa mratibu wa operesheni za vitengo vyote ikiwa ni pamoja na vikosi vya polisi, jeshi na idara ya ujasusi na usalama.

‘Ni kweli kwamba, Brigedia Kayanja Muhanga amepewa nafasi ya kuratibu vikundi vyote vya usalama kwa madhumuni ya kuunganisha shughuli ya usalama wa pamoja hususan katika Mji wa Kampala na nchi yote,’ amenukuliwa Luten Akiiki.

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo, Tarehe 17 Desemba 2020, Rais Museveni alimteuwa mwanaye Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais (SFC).

Jenerali Muhoozi, ni mtoto wa kwanza wa rais huyo ambaye amekuwa madarakani kwa miongo minne sasa.

Kabla ya uteuzi huo, Jenerali Muhoozi, alikuwa mshauri wa baba yake – Rais Museveni – katika masuala ya ulinzi.

Meatu yafikia asilimia 90 ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa.

$
0
0

Samirah Yusuph

Meatu.
Juhudi za ziada kati ya wadau wa elimu, jamii pamoja na viongozi wa serikali katika kuhakikisha wanafikia malengo ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani hapa zimezaa matunda baada ya ukamilishaji kufikia asilimia 90.

Wilaya ya Meatu ikiwa na jumla ya wanafunzi 4,135 wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza ifikapo Januari 11,2021  inajumla ya vyumba vya madarasa 62 kati ya vyumba 92 vinavyohitajika upungufu ukiwa ni vyumba 39.

Huku madawati yaliyopo ni 2,650 kati ya madawati 4,600  yanayohitajika na upungufu ukiwa ni madawati 1,950.

Ukamilishaji huo umelenga kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika wilaya hiyo wanapata nafasi ya kuanza masomo kwa wakati.

Akizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Meatu Fabian Manoza alisema kuwa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari ni zoezi endelevu ambalo linatekelezwa kwa muda mrefu.

Isipokuwa kulikuwa na majengo hitajika ambayo yalikuwa bado hayajakamilika kutokana na sababu mbali mbali hivyo kilichofanyika ni kuhakikisha wanahamasisha  wananchi katika kukamilisha ujenzi ili wanafunzi wa kidato cha kwanza waanze masomo kwa wakati.

"Tumekuwa na ziara ya uhamasishaji kwa kushirikiana ambayo ni kamati ya ulinzi na usalama pamoja na kamati ya siasa, tumetembelea shule zote ambazo zilikuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa tukajionea wenyewe ukamilishaji wa vyumba hivyo," Alisema Manoza na kuongeza kuwa;

"Hadi sasa majengo yote yaliyokuwa yanahitajika yapo tayari na tuna uhakika wa watoto wote waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari wataanza masomo yao bila kikwazo chochote na ifikapo Januari 15 tunatarajia kutembelea shule hizo ili kujihakikishia kama watoto wote wameanza masomo".

Akielezea mafanikio hayo Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Meatu Anthony Philipo alisema kuwa ufanikishaji huo ni matokeo ya muamko wa wazazi na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha watoto wanapata elimu.

"Kilichofanya kufanikisha kwa wakati ni mwitikio wa wananchi katika kuchangia nguvu kazi katika hatua ya ukamilishaji pamoja na utakelezaji mzuri wa majukumu wa watendaji wa serikali". Alisema Philipo na kuongeza kuwa;

"Ujenzi wa vyumba vyote vya madarasa haukutumia wakandarasi umetumia mafundi wa kawaida hivyo gharama za ujenzi ni nafuu na majengo yapo katika ubora wa hali ya juu".

Huku baadhi ya wananchi wakieleza kuvutiwa kwao na utendaji wa mkurugenzi wa Wilaya hiyo jambo ambalo linafanya wamuunge mkono kwa kushiriki nguvu kazi pale wanapohitajika kufanya hivyo.

"Anaye kushika mkono na yeye mshike kama viongozi wetu wa serikali tunawaona wanatufikia na kutuelewesha kuhusu watoto wetu kupata elimu ni lazima tushiriki kwa maana tunaona mchango wa pesa pamoja na nguvu zetu katika shule hizi zinazojengwa," Alisema Saguda Mwihu mkazi wa Kata ya Itinje.

Hadi hatua hii Halmashauri ya wilaya imechangia kiasi cha tsh milioni 360 katika ujenzi wa vyumba vya madarasa, huku mwenyekiti wa halmashauri hiyo akiahidi kutoa kipaumbele cha upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo kutoka halmashauri katika vijiji ambavyo vitaonyesha ushirikiano mzuri wa nguvu kazi katika kuboresha miundombinu ya shule.


Mwisho.

Lindi Iko Nyuma Umilikishaji Ardhi-naibu Waziri Dkt. Mabula

$
0
0


 Na Munir Shemweta, WANMM LINDI
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameiagiza ofisi ya Ardhi mkoa wa Lindi kuhakikisha inatoa  elimu kwa wananchi wa mkoa huo ili waone umuhimu, faida na thamani ya kumiliki ardhi kutokana na mkoa huo kuwa nyuma katika umilikishaji ardhi.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo tarehe 5 Januari 2021 mkoani Lindi wakati akigawa hati za ardhi kwa wananchi wa kata za Mnazi Mmoja na Mingoyo katika halmashauri ya Manispaa ya Lindi akiwa katika ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi mkoani humo.

Dkt Mabula alisema, mkoa wa Lindi uko nyuma kwa wananchi wake kujitokeza kumilikishwa maeneo ya ardhi wànayomiliki na kumbukumbu za mkoa zinaonesha kuna  jumla ya hati 7025 zilizotolewa kwa wamiliki wa ardhi na kusisitiza kuwa idadi hiyo ni ndogo kwa kuwa wananchi wengi hawajaamka na kuona thamani ya kumilikishwa.

“Ofisi ya Ardhi Mkoa mkatoe elimu kwa wananchi umuhimu na faida za kuwa na umiliki wa ardhi, maana hapa shida haiko katika kumilikishwa kwa hati za miaka 99 pekee bali hata zile za kimila hivyo lazima mkatoe elimu hata kwa wale wananchi walio vijijini ili wamilikishwe na kupatiwa hati watakayoitumia kwa faida ya maendeleo” alisema Dkt Mabula.

Aliitaka Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Lindi kujipanga vizuri na kwenda kwenye maeneo ya kata za mkoa huo kuwaelimisha wananchi faida za kuwa na hati ya ardhi kwa kuwa tangu kuanzishwa ofisi hiyo miezi sita iliyopita ni hati 367 pekee ndizo zilizotolewa idadi aliyoieleza kuwa ni ndogo ukilinganisha na mikoa mingine.

Aliwaeleza wakazi wa kata za Mnazi Mmoja na Mingoyo katika Manispaa ya Lindi kuwa, mkoa huo una maeneo mengi mazuri ya uwekezaji na iwapo watazembea kumilikishwa kuna hatari wakayauza kwa bei ya chini kwa kwa kisingizio cha kutopimwa au kuhaulishwa.

“Mkizembea kumilikishwa maeneo yenu sasa na kupatiwa hati, mtu akitaka kuwekeza mtampa kwa bei ya chini kwa kisingizio cha kutopimwa na mwingine atalichukua na baadaye ataliuza kwa bei kubwa kwa kuwa ulimuuzia likiwa halijapimwa” alisema Naibu Waziri Dkt Mabula.

Aliwataka wananchi wa mkoa wa Lindi kujitokeza kupima maeneo yao  na kuchukua hati na kusisitiza kuwa hata kama maeneo hayo hawayahitaji wanaweza kuyapima ili kuongeza thamani na baadaye watakapotaka kuyauza wauze na kupata fedha za kutosha.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini  kuhakikisha wanasimamia ipasavyo makusanyo ya kodi ya pango la ardhi kwa kuwa mapato ya kodi hiyo ndiyo yanayotumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, idara ya ardhi ikisimamiwa vizuri na Wakurugenzi wa Halmashauri wakiiwezesha kwa kuipatia vitendea kazi na bajeti ya kutosha basi inaweza kuingiza mapato mengi kuliko sekta nyingine yoyote kwa kuwa ardhi ndiyo kila kitu.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Lindi Said Kijiji alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na ofisi yake kuhakikisha maeneo mengi ya mkoa huo yanapimwa lakini mwamko wa wananchi ni mdogo.

Alisema, ofisi yake ilishatembelea halmashauri za mkoa huo na kuonana na wakurugenzi kwa lengo la kuendesha zoezi la kupima na   kumilikisha maeneo ambapo alisema mafanikio makubwa yalikuwa katika halmashauri ya Mtama.

Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Mingoyo Manispaa ya Lindi Zakaria Michael Mwanga na Hadija Rashid Magaya waliokabidhiwa Hati ya pamoja walikuwa na haya ya kusema.


Waziri Jafo aipa tano Misungwi ujenzi wa hopsitali ya wilaya

$
0
0


Na Atley Kuni, Mwanza
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo ameoneshwa kufurahishwa na kupongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungi mkoani Mwanza kwa ubora wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.

Mpaka sasa utekelezaji wa ujenzi huo wamekamilisha majengo ya maabara pamoja na jengo la wagonjwa wanje (OPD), baada yakupokea Sh milioni 500 katika awamu ya kwanza ya ujenzi huo.

Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo, Waziri Jafo, amesema: “ miongoni mwa halmashauri zinazo nishawishi kwenda kuomba fedha zingine kwa Mhe. Rais John Pombe Magufuli ni pamoja na Halmashauri hii ya Misungwi.

“Ndugu zangu mimi, niwapongeze kwa kazi kubwa mlio ifanya, haihitaji kuwa na darubini kubaini ubora wa majengo haya, ukiangalia milango, Vigae, vioo nk. mliyotumia lakini hata uimara wa maeneo mbalimbali hii inatia hamasa sana, pamoja na kwamba hamkuwepo katika bajeti iliyopita lakini mmeitendea haki fedha iliyoletwa, hongereni sana.”

Awali akitoa taarifa ya ujenzi huo, Mkurugenzi wa Halmashuri hiyo, Kisena Mabula, amesema kukamilika kwa hospitali hiyo, itakuwa na uwezo wa kuwahudumia watu wapatao 462, 855 wa wilaya hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa mbele ya Mhe. Waziri Jafo, inaonesha hadi kukamilika kwa Hospitali hiyo itatumia kiasi cha Sh 2, 076 468, 848, ambapo katika hatua za awali halmashauri ilipokea kiasi cha Sh milioni 500 kutoka Serikali kuu, zilizo tumika kukamilisha ujenzi wa jengo la maabara pamoja na jengo la wagonjwa wanje (OPD).

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela, alimpongeza Mhe. Waziri Jafo kwa ziara yake katika Mkoa huo, huku akimhakikishia kuwa wataendelea kusimamia miradi yote kwa umakini mkubwa kadri watakavyokuwa wanaipokea.

“ Nikuhakikishie mheshimiwa waziri (Jafo) kuwa tutasimiamia kwa umakini miradi yote itakakayokuwa inatekelezwa katika mkoa wetu lakini pia tunatingatia maelekezo ya viongozi wote wa juu akiwepo Mhe. Rais mwenyewe.”

Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ni moja kati ya Hospitali 97 zinazo endelea kujengwa nchi nzima

Awamu ya kwanza ya unejzu wa hospitali za wilaya ilijumuisha kujenga hospitali 67 na katika awamu ya pili inajumuisha ujenzi wa hospitali za wilaya 28 ambazo tayari ujenzi wake umanza ikiwa ni azima ya Serikali ya awamu ya tano kusogeza huduma karibu na wananchi.

Walimu Wakuu shule za msingi watakiwa kusimamia fedha zinazotolewa na Serikali

$
0
0


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amewataka walimu wakuu wa shule za msingi nchini kuhakikisha wanasimamia fedha zinazotolewa na Serikali  kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu  kwa kufuata sheria na taratibu katika matumizi.

Akifungua mkutano mkuu wa pili wa umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania Bara jana , Jijini Dodoma Mhandisi Nyamhanga amesema serikali inapeleka fedha  za ruzuku mashuleni kwa kila mwezi ili ziweze kununua vifaa vya kufundishia, kujifunzia hivyo ni jukumu la  walimu  kusimamia kwa umakini na kuhakikisha wanafunzi hao wanapata elimu bora.

Mhandisi Nyamhanga anafafanua kuwa Serikali inafanya kila linalowezekana kuhakikisha elimu ya msingi hapa nchini inakuwa bora kwa kuboresha miundombinu ya elimu, hivyo ni wajibu wa Wakuu wa Shule za Msingi kuhakikisha fedha hizo zinasimamiwa kikamilifu.

“Serikali iko makini kuhakikisha suala la elimu linakuwa mbele zaidi kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maboresho ya miundombinu katika ujenzi wa vyoo,nyumba za walimu na mabweni ni kazi yenu kuhakikisha fedha hizo zinasimamiwa ili ziweze kutumika katika miradi iliyokusudiwa ,”amefafanua Mhandisi Nyamhanga

Mhandisi Nyamhanga amesema Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha elimu ya msingi na kusisitiza kuwa fedha za programu ya elimu bila malipo zitatumika kufidia malipo ya ada,posho kwa walimu wakuu pamoja na huduma nyingine za msingi.

Aidha, Nyamhanga ametumia fursa hiyo kuweka wazi kuwa Serikali inalaani vitendo vya udanganyifu wa mitihani na kuwataka walimu wakuu nchini kuendelea kudhibiti vitendo hivyo ili kuboresha elimu ya msingi.

“ Ni jambo la kusikitisha kuona katika ulimwengu huu bado walimu hamuwezi kudhibidi wizi wa mitihani,tunawakatisha tama wanafunzi wanaojituma,”amesema Mhandisi Nyamhanga.

Mhandisi Nyamhanga amesema vitendo vya udanganyifu wa mitihani bado ni tatizo ambalo lipo linatia doa  doa  kubwa kwani kwa kipindi cha mwaka jana pekee jumla ya wanafunzi 1065 walifutiwa matokeo ya mitihani kwa udanganyifu na kuwataka walimu hao wakuu kuangalia namna ya kudhibiti na kwamba hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa watakaovujisha .

Wakati huo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais –TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Gerald Mweli ametoa rai kwa umoja huo kujituma katika kutoa elimu bora kwa jamii ili kuzalisha wataalamu watakaotosha nchini.

Naye Rehema Ramole Mwenyekiti wa umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania Bara ameishukuru serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kulipa walimu mishahara yao kipindi chote shule zilipofungwa kutokana na ugonjwa wa Corana.

Wataalam Sekta Ya Maji Watakiwa Kutumia Taaluma Zao Vizuri

$
0
0


Na Mohamed Saif, Tarime

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amewataka wataalam Sekta ya Maji kote nchini kutumia utaalam wao ili wananchi wapate huduma ya uhakika na toshelevu ya majisafi na salama

Ametoa maelekezo hayo Januari 5, 2021 wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji wa Gamasara Wilayani Tarime Mkoani Mara na kuzungumza na wanufaika wa mradi huo ambao kwa nyakati tofauti walimueleza changamoto zilizopo kwenye mradi.

Miongoni mwa changamoto zilizoelezwa na wananchi hao ni pamoja na mradi kushindwa kutoa maji inavyopasa kwani kuna wakati mabomba hua hayatoi maji.

Mara baada ya kujionea hali halisi ya mradi na maelezo ya wananchi wa maeneo husika, Waziri Aweso alisisitiza kuwa dhamira ya Serikali ya Rais. Dkt. John Pombe Magufuli ni kuwafikishia huduma ya maji wananchi wake na kwamba hatokubali kuwa kikwazo cha kufikiwa kwa dhamira hiyo na hivyo aliwataka wataalm wote kwenye Sekta ya Maji kujitathmini.

Waziri Aweso aliielekeza Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mara kuhakikisha maboresho yanafanyika ili mradi uweze kutoa maji kama inavyopasa kwa lengo la kuhudumia wananchi wengi zaidi.

Alisema kuwa wananchi wanachohitaji ni maji na aliwaelekeza wataalam katika Sekta ya Maji kujiepusha na porojo badala yake wahakikishe wanajikita na kudumu kwenye falsafa ya maji bombani.

“Wataalam wetu kwenye Sekta ya Maji acheni porojo, elekezeni taaluma zenu na ubunifu katika kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero ya maji,” alielekeza Waziri Aweso.

Aliongeza “unapokuwa mtaalam lazima utoe ushauri kulingana na utaalamu wako, tunapoanzisha mradi maana yake ni wananchi wapate huduma, wataalam tutumie taaluma zetu kusaidia wananchi wapate maji,” alielekeza Waziri Aweso

Aidha, Waziri Aweso alizielekeza Jumuia za Watumia Maji kote nchini kuhakikisha zinasimamia vizuri miradi ya maji kwenye jumuia zao ikiwa ni pamoja na kuongeza umakini kwenye makusanyo kwa lengo la kuwa na miradi endelevu.

“Miradi mliyokabidhiwa inapaswa kuwa endelevu, sasa ni jukumu lenu kuhakikisha hili linafikiwa, hakikisheni mnashirikiana, mnaitunza na mnisimamia vizuri,” alielekeza Waziri Aweso.

Viongozi Sekta Ya Afya Tatueni Kero Za Wananchi- Mganga Mkuu wa Serikali

$
0
0

Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma

Wizara ya Afya ipo tayari kupokea kero na malalamiko ya wananchi endapo itaonekana wameshindwa kusikilizwa ama kusaidiwa na viongozi wao wa ngazi za chini na wale wa vituo vya kutolea huduma za afya kwenye maeneo yao.

Hayo yameelezwa leo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi mara baada ya kufanya kikao na Viongozi wakuu wa sekta ya afya kwa njia ya mtandao”ZOOM” kilichowajumuisha Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya,Wajumbe wa kamati ya usismizi wa huduma za afya za mikoa(RHMT) na wilaya (CHMT) pamoja na Wakurgenzi wa hospitali za Taifa,Kanda na Maalumu.

Prof. Makubi amesema kuwa wananchi wana matumaini na Serikali yao hivyo wanayo haki ya kusikilizwa na kutatuliwa kero zao kutoka kwa watendaji kwenye vituo vyote vya huduma za afya nchini hivyo kamati zote zinapaswa kufanya tathimini za kero zote kwa muda wa wiki nne na kuzitatua pia kuwasilisha ripoti Wizarani pamoja na TAMISEMI .

“Tunaanzisha utaratibu ambao sisi viongozi wa sekta ya afya tunaenda kutafuta kero kutoka kwa wananchi na kuzitatua,Hili ni agizo na tumekubaliana wasambae kwenye ngazi zote kuanzia zahanati,vituo vya afya na kwenye hospitali,tunatakiwa kuhakikisha wananchi wapate huduma bora licha ya kuwa tumeboresha huduma kwenye vituo vyetu”.

Aidha, amesema utaratibu huu utaweza kurahisisha kutatua kero za wananchi na kuweza kupunguza kero hizo na zingine sio lazima zimfikie Mhe. Waziri hivyo kama watendaji wanatakiwa kujitafakari wanaweza kutatua vipi changamoto wazipatazo wananchi.

“tumekubalikia suala la kuimarisha suala la uongozi, uwajibikaji na usimamizi kwani kila mmoja ameona kuna mapungufu kwenye usimamizi wa huduma za afya nchini,hivyo tumekubaliana kila kiongozi kuanzia Taifa hadi vijijini kusimamia sehemu zenye mapungufu kwani wananchi wanahitaji mazuri kutoka kwetu,hatuwezi kuwaridhisha kwa kila kitu lakini tutapunguza matatizo yao.

Upande wa kuimarisha vitengo vya huduma kwa wateja, Mganga Mkuu huyo wa Serikali amesema kitengo hicho kinatakiwa kuboreshwa na hivyo wanapaswa kuchakata kero zote na kuzifanyia kazi na hivyo kuzibandika kwenye ubao wa matangazo wa vituo vyao pia wanapaswa kuwa hai wakati wote kwakuwa mwananchi wanataka huduma za afya jinsi wanavyohitaji.

“Viongozi hao pia wanatakiwa kukagua ndani ya hospitali zao kwenye maeneo ya kutolea dawa na stoo kuona kama dawa zipo na zinawatosheleza wananchi,kama kuna wizi tuweze kuchukua hatu,waende kwenye wodi na OPD kuwasalimu wagonjwa na kama wana kero waseme ili wazitatue,pia maabara kuweza kuona kama vipimo vinafanyika”.Alisisitiza
Hata hivyo wamekubaliana kuwepo na magroup ya ‘Whatsap’ ambayo watapokea na kushughulikia kero kwenye kila wilaya au mkoa husika ili kila mwananchi awezo kutoa kero zake.

“Tumeagiza kuwe na namba ambazo zitatangazwa kwa wananchi,pia wawashirikie wananchi kupitia mikutano na kutaja namba zao ili wananchi wajue wanawasilisha vipi malalamiko yao ”.

Aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kujenga imani na kuwaamini watendaji wote wa sekta ya afya, na kusema kuwa baada ya Mhe. Waziri kutangaza namba yake ya malalamiko kwa muda wa wiki mbili ameweza kupokea kero elfu tatu kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Kikao hicho kwa njia ya mtandao kimehudhuriwa na washiriki wapatao 220 na ajenda kubwa ilikuwa ni jinsi ya kupunguza kero za wananchi zinazousiana na huduma za afya nchini ambazo wanatuma kupitia namba ya malalamiko iliyotangazwa na Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima mwishoni mwa mwaka jana ambayo ni 0734124191.
-MWISHO-

Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa China Kutua Nchini leo

$
0
0


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China mhe. Wangi Yi atawasili nchini Tanzania leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 7 na 8 Januari 2021.

Prof. Kabudi ametoa kauli hiyo wakati anaongea na waandishi wa Habari jana Wilayani Chato mkoani Geita, ambapo amesema kuwa Waziri Yi atakapokuwa nchini atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuzindua Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) katika wilaya ya Chato mkoani Geita.

“Hapo kesho ( leo)mara baada ya Mhe. Yi kuwasili hapa Chato, atazindua Chuo cha VETA cha wilaya ya Chato ambacho kimejengwa kwa fedha za watanzania,” alisema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa “sababu ya kumuomba afungue chuo hicho ni utamaduni wetu wa kumpa heshima mgeni anapokuja hapa nchini kwetu, sambamba na kutambua elimu ya mafunzo na ufundi stadi ilivyopiga hatua huko nchini China.”

Pamoja na mambo mengine, Prof. Kabudi amesema kuwa  Serikali ya China itajenga Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) mkoani Kagera ikiwa ni namna ya kufikia lengo la  Serikali  ya Awamu ya Tano ya kujenga VETA kila Wilaya hapa nchini.

Waziri Kabudi ameongeza kuwa shughuli nyingine zitakazofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, kuwa ni  mazungumzo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, pamoja na kufanya  mazungumzo rasmi kati yake na ujumbe wake kutoka nchini China.

Aidha, shughuli nyingine atakazofanya Waziri Yi ni pamoja na kutembelea mwalo wa Chato ili kuona shughuli za uvuvi, ikizingatiwa kuwa ziwa Viktoria ni ziwa la pili kwa ukubwa dunia Pamoja na kusaini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tano kutoka Mwanza hadi Isaka chenye urefu wa km 341 ambapo kitagharimu kiasi cha Shilingi trilioni 3.0617

Waziri Kabudi ameogeza kuwa, Februari mwaka huu Serikali ya Tanzania inatarajia kuanzisha  safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Guanzhou  nchini China ili kukuza sekta ya utalii.

Historia ya mahusiano ya kidiplomasia kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya watu wa China ulianza mwaka 1965.

Watu wanne wamefariki baada ya wafuasi wa Trump kuvamia bunge

$
0
0


 Watu wanne wamefariki Dunia Nchini Marekani kufuatia fujo zilizotokea baada ya Wafuasi wa Rais Donald Trump kuvamia Bungeni wakipiga kelele kuwa kura za Trump zimeibiwa na kwamba wanataka Trump abaki madarakani.

Waliofariki ni Mwanamke mmoja ambaye alipigwa risasi pamoja na wenzake watatu, Polisi wamethibitisha na kusema pia wamewakamata zaidi ya Watu 50 kutokana na fujo hizo.

Rais Donald Trump alilazimika kuwatuliza wafuasi wake walioandamana na kuwataka warejee majumbani mwao lakini katika ujumbe wake huo wa video alikazia kuwa uchaguzi ulitawaliwa na wizi: ”najua mnaumia, naumia pia ila tunataka Amani”.

Bunge la Congress lamthibitisha Joe Biden kuwa Rais wa Marekani

$
0
0


 Mabaraza ya bunge la Marekani yamemthibitisha rais mteule Joe Biden kuwa mshindi wa rais katika uchaguzi uliofanyika Novemba.

Mabaraza hayo mawili yalitupilia mbali matakwa ya wapambe wa Trump kwamba matokeo katika majimbo ya Arizona na Pennsylvania yabatilishwe. 

Baada ya kukamilika kwa mchakato huo, seneta Amy Klobuchar alisema wameweka rekodi kwamba Biden atakuwa rais na Harris makamu wake kulingana na kura ambazo wamepewa.

Punde baada ya ushindi wa Biden kuidhinishwa, Rais Trump ametoa taarifa akiahidi makabidhiano ya amani ya madaraka huku akidokeza kuwa atasalia kwenye siasa, hatua inayoibua gumzo kwamba atataka kuwania tena urais mwaka 2024.


Mume Auawa Baada ya Kumfumania Mkewe na Mwanaume Mwingine

$
0
0


Mtu aliyetambuliwa kwa jina la Juma Kitemango (48) mkazi wa Matundasi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, ameuwawa kwa kushambulia na vitu vyenye ncha kali na mgoni wake, Juma Sunzima (40) baada ya kuwafumania na mkewe wakiwa ndani ya chumba chake. 


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Jerome Ngowi,  amewaambia waandishi wa habari Januari 6 jijini humo kuwa tukio hilo lilitokea Januari 4 wilayani humo, baada ya marehemu kufika nyumbani kwake na kumkuta mkewe Merry Daimon, akiwa na mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake. 


"Marehemu aliwafumania mkewe na mtuhumiwa wakiwa wanafanya yao ndani ya nyumba yake waliyokuwa wakiishi na mkewe na ndipo ulipotokea mzozo na mtuhumiwa kumjeruhi na vitu vyenye ncha kali na sehemu za kichwani na utosini na kusababisha kifo chake," alisema.


Asema mara baada ya tukio hilo mke wa marehemu na mtuhumiwa  walikimbia  na kwamba  jeshi la polisi linaendelea na msako ili wafikishwe mikononi mwa sheria.


Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mareheme kabla ya umauti kumkuta walikuwa na migogoro isiyokwisha na mkewe ya kimahusiano iliyohusihwa na wivu wa kimapenzi.

Polisi wanne wasimamishwa kwa utovu wa nidhamu Arusha

$
0
0


Na Woinde Shizza ,ARUSHA
Jeshi la Polisi nchini limewafukuza kazi kwa fedheha askari wake wanne kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu ,rushwa na wizi.

Akiongea na vyombo vya habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha ,Salumu Hamduni alisema kuwa askari hao wametimuliwa kazi jana januari 6,Mwaka huu .


Alisema kabla ya kufukuzwa  kazi kwa askari hao ,walifikishwa kwenye mahakama ya kijeshi na kukutwa na hatia na kwamba watafikishwa mahakamani Kama vibaka wengine wanaojihusisha na matukio ya uhalifu


“Askari hao tumewafukuza kazi baada ya kuwafikisha kwenye mahakama ya kijeshi na watashtakiwa Kama vibaka wengine wa kawaida”alisema Kamanda


Aliwataja askari hao kuwa ni pamoja na  askari mwenye namba G. 5134 DC Heavenlight Mushi  aliyekuwa Askari kitengo Cha Intelijensia Mkoa wa kipolisi kinondoni jijini Dar es Salaam,H.125 PC Gasper Paul kitengo Cha Intelijensia makao makuu Dodoma na H.1021 PC Bryton Murumbe aliyekuwa askari wa kawaida mkoani Dodoma.


Kamanda alifafanua kwamba askari hao wamefukuzwa kazi kutokana kwa kosa la kumteka mfanyabiashara wa Madini jijini Arusha,Sammy Mollel ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Germs and Rocks Venture ya jiji Arusha na kujipatia kiasi cha sh, milioni 10 kinyume cha sheria.


Alisema askari hao wakikamatwa desemba 24,2020 katika ofisi za mfanyabiashara huyo baada ya kufika kwa ajili ya kuchukua mgao wa pili wa shilingi milioni 20 kati ya milioni 30 walizohitaji na kupatiwa sh,milioni 10.


Mwingine aliyefukuzwa kazi ni askari mwenye namba F.1445 CPL Koplo William Joseph mkazi wa Muriet jiji Arusha ambaye alikamatwa jana nyumbani kwake akiwa na na bidhaa mbalimbali haramu ikiwemo misokoto ya bangi.


Alisema kuwa askari huyo alikutwa na misokoto 20 ya bangi bhangi kwenye gari lake ,kukiunganishia umeme wa wizi kinyume cha sheria,kupatikana na pombe ya gongo lita tano na lita mafuta ya Dizel Lita 85.


Pia alikutwa na vyuma vya bomba kinyume na taratibu,pombe ya viroba boksi 84 iliyookatazwa na serikali,chupa 9 za konyagi na pakti 3 za pombe aina ya kiroba .


Kamanda alisema kuwa upelelezi wa matukio hayo umekamilika na majalada yamepelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi na majalada hayo yakirudi watafikishwa mahakamani.


Ukaguzi wa Dawa kwenye vituo vya kutolea Huduma – Rukwa

$
0
0


Nteghenjwa Hosseah, Rukwa
Mkurugenzi wa huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Dr. Ntuli Kapologwe amewaagiza waganga wafawidhi wote wa vituo vya kutolea huduma za Afya kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa dawa (Medicine Audit) kila robo mwaka kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Dr. Ntuli ameyasema hayo wakati alipokua akiongea na timu za usimamizi wa huduma za afya Mkoani Rukwa wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi mkoani humo tarehe 02/01/2020.

Akizungumza katika kikao hicho Dr.Ntuli amesema hakutakuwa msamaha kwa kituo cha kutolea huduma ambacho hakitafanya ukaguzi wa dawa na taarifa ya kila Mkoa kuwasilishwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

“ Kwa kufanya ukaguzi wa dawa tutaweza kujua namna dawa zilivyotumika, dawa gani eneo fulani inatumika sana na kwanini na hivyo kubaini mahitaji zaidi kwa wakati unaokuja.

Pia itawezesha kufahamu kiasi cha Fedha kilichopatikana kutokana na mauzo ya dawa ambacho kitatumika tena kurudi kununua dawa MSD’ alisisitiza Dr Ntuli.

Aliongeza kuwa ukaguzi wa dawa ukifanyika kikamilifu itasaidia Kubaini upotevu wa dawa pamoja na wizi wowote uliotokea katika kituo husika.

Dr. Ntuli alisistiza umuhimu wa kufanya ukaguzi wa dawa kuwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kufanya mlinganisho wa kiasi cha dawa kilichotumika sambamba na wagonjwa halisi waliohidumiwa na kuwa na takwimu halisi za Serikali katika kutoa Fedha za dawa.

Aidha Dr. Ntuli aliwakumbusha wataalam wa afya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Joseph Pombe Magufuli mwezi Novemba 2020 alitoa shilingi Bil. 41 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na fedha hizo zimeelekezwa MSD.

‘Fedha hizo zitawezesha kila kituo kupata dawa za kutosha sasa ni jukumu la kila kituo kuhakikisha kinazungusha(REVOLVE) fedha baada ya kuwa wametoa huduma kwa kurejesha MSD ili upatikanaji wa dawa uwe endelevu na wananchi waweze kupata dawa wakati wote watakapohitaji” alisisitiza Dr Ntuli.

Walimu Wahamasishwa Kujiendeleza Kielimu

$
0
0


 Na Veronica Simba
Serikali imewahamasisha Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini, kujiendeleza kielimu katika ngazi mbalimbali ili kuboresha zaidi utendaji wao wa kazi.

Wito huo umetolewa jijini Dodoma leo, Januari 7, 2021 na Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Moses Chitama wakati akizungumza na Wajumbe wa Mkutano wa Pili wa Umoja wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara.

Akifafanua, amesema kuwa, kujiendeleza kielimu ni haki ya msingi kwa watumishi wote wa umma wakiwemo walimu, ndiyo maana Serikali kupitia Tume imekuwa ikiwahamasisha kuitumia fursa hiyo ipasavyo.

Chitama amekemea tabia ya baadhi ya Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania Bara, ambao hukataa kutoa ruhusa kwa watumishi walio chini yao wenye nia ya kujiendeleza kielimu.

Hata hivyo, Kaimu Katibu huyo amesisitiza kuwa Walimu wote wa shule za umma wenye nia ya kujiendeleza kielimu, wanapaswa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Mamlaka ikiwemo kufuata Mpango wa Mafunzo.

Aidha, amewasisitiza kuhakikisha wanapata ruhusa ya maandishi kutoka kwa Wakuu wao, kabla ya kwenda masomoni kwani kinyume chake watakabiliwa na mashtaka ya utoro kazini ambayo adhabu yake ni kufukuzwa kazi.

 “Tumekuwa tukipata rufaa nyingi za kesi za Walimu ambao walitoroka kazini na kwenda masomoni hivyo kufukuzwa kazi. Serikali inapenda walimu msome lakini fuateni taratibu zilizowekwa,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira na Maendeleo ya Walimu kutoka TSC, Mecktildis Kapinga, akifafanua kuhusu utaratibu wa kupanda vyeo, ameueleza Mkutano huo kuwa, kanuni inaelekeza kutompandisha cheo mtumishi yeyote wa umma akiwa masomoni, hadi pale anapohitimu ndipo mchakato wa kumpandisha hufanyiwa kazi.

“Naomba mtambue kuwa utaratibu huo ni kwa watumishi wote wa umma, na siyo kwa walimu pekee kama ambavyo baadhi yenu mmekuwa mkinung’unika,” amefafanua Kapinga.

Mkutano huo wa siku tatu, ulianza Januari 5, 2021 huku ukiongozwa na kaulimbiu isemayo uongozi na usimamizi makini wa elimu, utaimarisha Tanzania katika uchumi wa kati.

Tume ya Utumishi wa Walimu ni Mamlaka ya Ajira na Nidhamu kwa walimu wa shule za msingi na sekondari Tanzania Bara, walio kwenye utumishi wa umma.

Zaidi Ya Watanzania Milioni 12 Waishio Vijijini Wafikiwa Na Huduma Za Mawasiliano

$
0
0


Na Celina Mwakabwale, UCSAF
Mtendaji Mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema mpaka sasa zaidi ya wananchi millioni 12 waishio maeneo ya vijijini na yasiyo na mvuto wa kibiashara pamoja na wale wa mipakani na kanda maalum wamefikiwa na huduma mbalimbali za mawasiliano ikiwemo simu, runinga, radio pamoja na mawasiliano ya posta.

Bi. Mashiba ameyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile aliyetembelea tasisisi hiyo na kufanya kikao na wajumbe wa bodi, menejimenti pamoja na wafanyakazi. Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Zainab Chaula, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Jim Yohazi pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo.

Dkt Ndugulile ameipongeza UCSAF kwa kufikisha huduma za mawasiliano kwenye maeneo mbalimbali nchini huku akiitaka kuwekeza zaidi katika teknolojia yenye gharama nafuu ili kuyafikia kwa haraka maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma za mawasiliano. Hivi sasa UCSAF inatumia shilingi milioni 350 kujenga mnara mmoja wa mawasiliano.

Ameongeza kwa kusema kuwa, sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari inabadilika kwa kasi hivyo ameitaka wizara kukamilisha uandwaaji wa sheria ya TEHAMA ili kuendana na kasi ya mabadiliko hayo.

Akizungumza na wajumbe wa bodi Dkt Ndugulile ameagiza kuwepo na utaratibu mzuri wa kufanya kazi kwa ukaribu na kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) na UCSAF ili kuongeza kasi ya upelekaji wa huduma mbalimbali za mawasiliano katika maeneo wanayoshirikiana.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula ameipongeza UCSAF huku akiitaka kuendelea kufikisha huduma za mawasiliano ili kuendana na malengo ya kuanzishwa kwa wizara hiyo.

Hadi sasa mfuko wa mawasiliano kwa wote umefanikiwa kufikisha huduma mbalimbali za mawasiliano ikiwa ni pamoja na kuwasha minara katika kata 633 zenye vijiji 2,320, kuunganisha mtandao wa intaneti na kutoa vifaa vya TEHAMA kwa shule 711, kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu 2,213 wa shule za UMMA kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara pamoja na kujenga vituo 10 vya TEHAMA visiwani Zanzibar.

 Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF)

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>