Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ifahamu sheria ya maandamano Kikatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

$
0
0
Maandamano ya aina yoyote ni haki ya mwananchi na yanaruhusiwa kisheria lakini maandamano hayo lazima yafuate sheria na taratibu zilizobainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheria ya maandamano inamtaka mwananchi au kundi la wananchi wanaohitaji kufanya maandamano kutoa taarifa kwa maandishi kwa Mkuu wa Polisi wa eneo husika kabla ya masaa 48 ya kuanza kwa maandamano hayo ikieleza dhumuni la maandamano hayo.

Pia wahusika wanatakiwa wawe tayari kwa jibu lolote kutoka kwa mkuu huyo kwa kuwa chochote watakachojibiwa lazima kiwe na sababu.

Endapo wahusika watakataliwa kufanya maandamano na hawatoridhishwa na sababu zilizotolewa na Mkuu wa Polisi kuna hatua mbili muhimu zinazotakiwa kufuatwa na sio wahusika kujiamulia kuandamana kilazima kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa.

Hatua hizo muhimu zinazotakiwa kufuatwa ni kuandika barua kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kumueleza kutoridhishwa na sababu zilizotolewa na Mkuu wa Polisi ili Waziri naye kwa upande wake aamue kuruhusu au kukataza.

Endapo wahusika hawatoridhika na majibu ya Waziri, waandamanaji watatakiwa kwenda Mahakamani ambapo ndipo uamuzi wa mwisho utatolewa.

Hakuna sheria inayotambua maandamano ya nchi nzima kufanyika kwa siku moja kwa sababu kila eneo lina Mkuu wa Polisi mwenye haki ya kukubali au kukataa ombi la kufanya maandamano kulingana na hali halisi ya eneo lake.

Kila jambo lina faida na hasara zake lakini kuna mambo ambayo faida huwa chache kuliko hasara, maandamano yana athari kubwa kiuchumi na kijamii kwa sababu maandamano yoyote ni lazima Jeshi la Polisi liwajibike katika kuongoza na kulinda maandamano hayo, hivyo kupelekea wanajeshi wengi kusitisha kazi zingine kwa ajili ya kuzuia vurugu zisitokee.

Athari zingine ni kusitishwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za usafiri , kufungwa kwa maduka na masoko pamoja na athari zitokanazo na vurugu zinazoweza kutokea kwa sababu ya maandamano hayo.

Hivyo itambulike kisheria hatua hizo zinatakiwa kufuatwa kabla ya kufanya maandamano, aidha maandamano kisheria ni jambo halali endapo tu litakuwa limehalalishwa kisheria.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Lewo Jumapili ya March 11

Tundu Lissu Kufanyiwa Upasuaji Wa 19 March 14

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu  Machi 14,2018 atafanyiwa upasuaji wa 19 katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji.

Upasuaji huo ni mwendelezo wa ambazo amekuwa akifanyiwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikokuwa amelazwa baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa katika makazi yake mjini Dodoma Septemba 7,2017.

Alipatiwa huduma za awali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Taarifa ya Lissu aliyoitoa jana usiku Machi 10,2018 akielezea afya yake amesema licha ya sasa kuweza kusimama bila msaada, amejuzwa na timu ya madaktari wanaomtibu kuwa kasi ya mfupa wa juu ya goti kuunga ni ndogo.

"Madaktari wangu wamesema wasipoingilia kati na kurekebisha mfupa huo itachukua muda mrefu sana kuunga," amesema.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) amesema madaktari wamemweleza hata mfupa huo ukiunga baada ya muda mrefu, hautaunga kwa namna utakaoondoa hatari ya kuvunjika baadaye.

"Kwa sababu hizi, madaktari wangu wamependekeza kufanya operesheni nyingine kwenye mfupa wa juu ya goti la kulia Machi 14,2018, nitarudi Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg, kwa ajili ya kufanyiwa operesheni hiyo," amesema.

Amesema yuko katika mikono salama ya kitabibu chini ya madaktari Profesa Stefa Nijs na Profesa Willem-Jan Mertsemakers ambao amesema ni madaktari bingwa wa mifupa wanaosifika barani Ulaya.

"Hivyo, msiwe na hofu. Mungu wetu aliyeniwezesha kuwa hai sasa, ataendelea kutenda miujiza kupitia kwa madaktari bingwa hawa," amesema.

Lissu amesema ataendelea kutoa taarifa za maendeleo ya afya yake kwa kadri itakavyohitajika akiwaomba Watanzania kumuunga mkono yeye na familia yake katika kipindi anachopitia.

Lissu yupo Ubelgiji tangu Januari 6,2018 alikopelekwa akitokea Hospitali ya Nairobi, Kenya.

Mamlaka ya hali ya hewa Yatoa Tahadhari

$
0
0
Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa hali mbaya ya hewa katika maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara ndani ya saa 24 kuanzia leo.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo na kudai kutakuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa ambazo zinatarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Singida, Dodoma, Morogoro, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe, Kilimanjaro, Manyara na Arusha

Mbali na hilo, TMA imesema kutakuwepo upepo mkali unaofikia kilomita 30 kwa saa kutoka Kaskazini- Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutokaa Kaskazini-Magharibi kwa Pwani ya Kusini huku hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi.

Kwa taarifa kamili angalia hapa chini



Rais Mkuu Ataka Viwanda Viajiri Wazawa

$
0
0
Rais John Magufuli amemwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhakikisha wamiliki wa viwanda vya ndani wanaajiri wazawa.

Ametoa agizo hilo leo Jumapili Machi 11,2018 akizindua kiwanda cha kufua vyuma cha Kahama Oil Mill mjini Kahama mkoani Shinyanga.

Rais amesema wananchi wazawa ndio waliompigia kura, hivyo wapewe kipaumbele cha ajira katika viwanda hivyo.

“Kama wewe ni waziri nimekuteua mimi, unaacha kuwaajiri wazawa walionipigia kura unaenda kuchukua watu wa nje hii hakubaliki,” amesema.

Rais Magufuli amesema, “Nitoe wito kwa mawaziri wangu na wakurugenzi, hakikisheni viwanda mnavyovianzisha nchini mnaajiri Watanzania, hawa ndio walionipigia kura.”

Amewataka wamiliki wa viwanda kuhakikisha wanatumia malighafi za ndani kutengeneza bidhaa badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi.

“Mwaka huu pamba nyingi imelimwa, Kahama Oil Mill pia mnatengeneza mafuta, hakuna haja ya kuagiza pamba kutoka nje wakati tuna pamba ya kutosha hapa,” amesema.

Kuhusu kiwanda cha chuma amesema malighafi inapatikana nchini, hivyo iwapo mkurugenzi wa Kahama Oil Mill anahitaji yupo tayari kumpa bure badala ya kuagiza nje.

Pia, amewataka Watanzania kununua bidhaa za ndani, huku akiwataka wamiliki wa viwanda kutengeneza zenye ubora ili kuhimili ushindani.

Wanasiasa, watumishi wa umma kupigwa ‘stop’ kuwania uongozi TLS kwazua kizaazaa

$
0
0
Mabadiliko ya kanuni za uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) zimewagonganisha viongozi wake na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) baada ya kudaiwa kuongezwa masharti yanayowanyima fursa watumishi wa umma na wanasiasa kuwania uongozi ndani ya chama hicho.

Kanuni hizo zimechapishwa juzi katika Gazeti la Serikali (GN) namba 116, jambo ambalo limekifanya chama hicho kuitisha kikao cha dharura kujadili mabadiliko hayo kwa maelezo kuwa hakikuyapitisha katika kikao cha baraza la uongozi.

Kipengele hicho kinacholalamikiwa na TLS ni cha (8)(e) kinachoeleza masharti ya mwanachama anayetaka kugombea nafasi yoyote ndani ya chama hicho kuwa asiwe mtumishi wa umma, mbunge, diwani au kiongozi wa chama cha siasa kilichosajiliwa.

Pia, Rais wa TLS, Tundu Lissu aliyeko nchini Ubelgiji kwa matibabu amedai kuwa saini yake imeghushiwa katika kanuni hizo inayoonyesha alisaini Februari 9.

Jana, Makamu Mwenyekiti wa TLS, Godwin Ngwilimi alisema, “Hiki kipengele hakikupitishwa katika kanuni za kikao cha baraza la uongozi ambazo zilikwenda kwa AG, lakini zimerudi kikiwa kimeongezwa, kwa nini aliweka muulize AG.”

Hata hivyo, alipotafutwa kwa simu kuzungumzia madai hayo, AG Dk Adelardus Kilangi alijibu kwa kifupi “sorry (samahani) sizungumzi katika magazeti.”

Kuhusu hatua ambazo TLS itachukua kutokana na utata huo, Ngwilimi alisema, “Kwanza tayari ishakuwa katika gazeti la Serikali, mimi siwezi kutoa uamuzi wangu, tumeitisha kikao cha dharura cha kujadili suala hilo. Hatujajua AG ametumia mamlaka gani kuweka hayo mabadiliko.”

Kuhusu madai ya Lissu kwamba saini yake imeghushiwa, Ngwilimi alisema saini hiyo haijaghushiwa kwani iliyotumika ni saini ya kielektroniki ambayo baada ya kikao cha baraza la uongozi kumaliza kupitisha kanuni, mmoja wa watumishi wa TLS aliiweka.

“Hata Lissu analijua hilo, lakini kwa kuwa kipengele hicho kimeongezwa ndiyo anasema imeghushiwa lakini kama isingeongezwa kipengele hicho sidhani kama angeongea, lakini hili nalo la saini ni moja ya mambo tutakayojadili kwenye kikao hicho cha dharura.”

Kwa upande wake, Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa Chadema alisema, “Vita ya mwaka jana inaendelea...”

“Wanajua hawaniwezi kwenye sanduku la kura za mawakili... Mimi sijashiriki kikao au shughuli yoyote ya TLS tangu wanaoitwa ‘watu wasiojulikana’ waliponipiga risasi nyingi mwaka jana,” alisema Lissu.

“Nitasaini vipi kanuni za uchaguzi zilizopitishwa na kikao ambacho sikukiendesha wala kukihudhuria?”

Ngwilimi alipoelezwa kuhusu Lissu kupinga saini yake kutumika wakati hakuwapo kwenye kikao alisema “Hilo sasa siwezi kulisemea lakini muulize yeye ni mjumbe wa baraza la uongozi, alipowauliza walimjibu nini.”

Hata hivyo, Lissu alipoulizwa swali hilo alisema “Walifanya hivyo kwa idhini ya nani? Mimi sikuwepo kwenye kikao husika, sikushiriki kwenye kufanya maamuzi haya na sikusaini au kutoa idhini ya sahihi yangu kutumika kwenye maazimio ya kikao husika.

“Sahihi yangu imetumika huko nyuma kwenye kikao gani ambacho sikukihudhuria? Hakuna, kwa kadri ninavyofahamu hii ni hoja ya ajabu kabisa. Maana yake ni kwamba wanaweza kutumia sahihi yangu ya kielektroniki kutolea pesa benki na ikawa sawa tu.”

Waziri Kigwangalla Amsimamisha Kazi Mkuu Wa Kanda - Pori La Akiba Rukwa Kupisha Uchunguzi Kufuatia Tuhuma Za Kujihusisha Na Ujangili

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amemsimamisha kazi mkuu wa kanda Pori la Akiba Rukwa lililopo wilayani Mlele mkoani Katavi kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Taarifa ya Kaimu Katibu Mkuu, Dk Aloyce Nzuki iliyotolewa jana Machi 10,2018 inasema waziri amemsimamisha kazi Emmanuel Barabara ambaye pia ni mhifadhi wanyamapori mkuu.

Dk Kigwangalla amefikia uamuzi huo kutokana na taarifa za raia wema kuwa Barabara amekuwa akishirikiana na majangili kuhujumu rasilimali za misitu nchini.

Waziri Kigwangalla katika taarifa hiyo ameagiza iundwe kamati ya uchunguzi kubaini ukweli wa tuhuma hizo.

Amesema iwapo mtuhumiwa atatiwa hatia, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma ili iwe fundisho kwa wengine.

“Tunatoa onyo kali kwa watumishi wa wizara wanaojihusisha na vitendo vya uhujumu wa rasilimali za misitu, wanyamapori na mali kale. Tunawataka waache mara moja kwa kuwa hatutosita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo, ikiwemo kufukuzwa kazi,” amesema.

Amewataka watumishi wa wizara kuzingatia sheria, kanuni, utaratibu na miongozo iliyowekwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ya uhifadhi wa rasilimali za nchi kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho. 

TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini na Saba ( 27 )

$
0
0
AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA 

Rahma akazidi kuongeza kasi ya mashambulizi ila kutokana nimesha mzoe hakunitisha sana zaidi ya mimi kuzibana sehemu zake ambazo siku zote nikimbana huwa niamshinda kwenye mechi zake.Galfa mwili wa Rahma ukaanza kukakamaa huku macho yake yakibadilia na kiini cheusi kikapotea na kukabaikia kweupe tu huku mapuvu yakiaanza kumtoka mdononi kitendo kilicho anza kunichanganya kwani tangu nimjue Rahma sikuwahi kumuaona akiwa katika hali kama hii

ENDELEA
Hali ya Rahma ikazidi kuwa mbaya kitandani na kunifanya nizidi kupagawa hata sikujua nifanye kitu gani kitakachoweza kumrudisha Rahma katika hali yake ya kawaida.Nikasimaa na kuiokota suruali yangu chini na kuivaa kisha nikuitoa simu yangu mfukoni na kukuta haina chaji ikanilazimu kuitafuta simu ya Rahma na ndani ya chumba changu haikuwepo ikanilazimu kwenda sebleni na kuikuta juu ya meza ya chakula nikaichukua na kukuta meseji moja na kwabahati mbaya nikaifungua
‘WEWE RAHMA UPO WAPI TUNAKUSUBIRIA NYUMBANI KWENYE KIKAO HUYU MUME WAKO AMESHA KUJA’
Nikajikuta nikiirudia rudia meseji yake kuisoma kiasi kwamba nikajikuta nikikaa juu ya meza vizuri na kwa haraka namba iliyo tuma meseji ninaifamu ni ya mama yake ambayo alinipa siku moja shuleni.Nikabaki nikiwa nimetulia zaidi ya dakika tano huku nikijikuta rohoni mwangu nikijiwa na wivu mkali ulio andamana na hasira kali,Nikastuka simu yake iikita na kuona ni namba ya baba yake ikiingia na kubaki nikiwa nimeitazama kiasi kwamba nikajikuta nikianza kutetemeka kwa woga,Hadi simu inaka nikajikuta nikiwa kimya nisijue ninafanya nini

Wazo la kumpigia Halda likanijia kichwani na nikaanza kuifungua simu ya Rahma sehemu alipo hifadhi majina ya watu mbalimbali na kujikuta zaidi ya dakika kumi nikilitafuta jina la Hilda ila sikulipata kwani sikujua ameliandika  vipi ndani ya simu yake.Nikasikia honi ikipiga getini na kwaharaka nikajua atakuwa ni Hilda ambeye ameondoka nyumbani kwetu muda si mrefu na kwa haraka nikanyanyuka na kutoka nje na hatua ya kwanza nikachungulia dirishani kutazama ni nani anaye piga honi na kujikuta nikistuka na kajasho kembemba kakianza kunienda mbio,hii ni baada ya kuliona gari jeusi anina ya Land cruser likiwa limesimama nje kwangu huku likiwasha taa zote mbili
“Nani huyu?”
Nilijiuliza mwenyewe kana kwamba kuna mtu pembeni yangu ninaye zungumza naye kumbe nipo peke yangu.Nikamshuhudi Hilda akishuka ndani ya gari hilo na kuanza kupiga hatua za haraka kuja kwenye geti langu kidogo moyo ukanipata matumaini na kujikuta nikulifungua geti na Hilda kwa ishara akamruhusu dereva wa gari kuliingiza ndani na nikabaki nikiwa ni nimeduwaa hadi gari linasimama akashuka jamaa mmoja mweusi kiasi aliye valia vizuri na kujikuta nikirudi katika hali ya kawaida baada ya jamaa kunisalimi

“AHaaa salama tuu kaka karibuni”
Nilizungumza huk u nikiliegesha geti langu na endapo kutatoke ishu yoyote niweze kukimbia kuepukana na msala uliopo ndani
“Eddy huyu anaitwa Rashid ni dereva wao Rahma”
“Ahaa karibu ndugu”
“Asante vipi huyo bibie yupo ndani?”
Swali la dereva nikajifanya kama sijalisikia na kuongoza ndani huku wao wakinifwata kwa nyama na mimi moja kwa moja nikaingia ndani na kuukuta Rahma akiwa ametulia huku mapigo yake ya moyo yakienda taratibu kiasi kwamba nikabaki nikimtazama kwa muda.Nikasikia sauti ya Hilda ikimuita Rahma huku akionekana kuja kwenye chumba chetu ikanilazimu kunyanyuka kitandani kwa haraka na kwenye kuufungua mlango na kumkuta akiwa amesimama mlangoni kwetu
Muambie huyo Rahma kwao wanamsubiria sana na ninampigia simu hapokei”


AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 35 na 36 )

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA 
Nilizungumza hivyo huku nikishusha pumzi nyingi kwani ninahitaji kwenda kumtoa raisi kwenye gari aliloipo na kuondoka naye. Biyanka akaanza kufyatua risasi mfululizo, na kuwafanya washambuliaji kutulia kidogo, ikawa nafasi kwangu kukimbia hadi gari la raisi lilipo, kwa ishara nikamuomba afungue mlango wa gari lake kwa manaa pasipo yeye kuufungua kwa ndani mimi wa nje siwezi kuufungu. Raisi akafanya hivyo, japo ni jambo la hatari ila hakuna njia nyingine ya kufanya zaidi ya kufanya hivyo. Raisi akashuka huku kichwa akiwa amekiinamisha chini, nikaupitisha mkono wangu wa kulia kiunoni mwake, kitendo cha kugeuka na kumtazama K2 aliyopo upende wetu nyuma ya gari la raisi, nikakutana na uso wa bastola yake akiwa ameninyooshea mimi na raisi huku sura yake akiwa ameikunja akidhamiria kufanya hicho anacho kihitaji kukifanya kwa wakati huu.
      
ENDELEA  
K2 pasipo na huruma akafyatua risasi moja iliyo nifanya kuyafumba macho yangu nikiamini kabisa ninakufa kwa mkono wa K2. Ila sekunde kadhaa zikapita nikafumbua macho baada ya kuwana hakuna kitu ambacho kimetokea kwa upande wangu. Nikamtazama raisi na kumkuta akiwa yupo hai, nikamtazama K2 nikakakuta akiendelea kupambana na wavamizi hawa, nikatazama nyuma yangu, kwa umbali kidogo nikamuona mvamizi mmoja aliye valia nguo nyeusi na kinyago cheusi usoni mwake akiwa amelalal chini anamwagika damu za kichwa. 
 
Hapo ndipo nikaielewa lengo la K2, kuninyooshea bastola yake kwani ameyaokoa maisha yangu na kama sio hivyo basi ningekuwa nimesha kufa. Nikaongozona na raisi kwa mwendo wa haraka hadi kwenye gari letu. Raisi huyu ambaye ni feki na watu hawafahamu kwamba ni feki, akaingia kwenye gari nikamfungia mlango wa ndani. Tukaendelea kujibu mashabulizi huku kila mmoja jasho likimwagika kisawa sawa. Nikamuona K2 anaanza kupiga sarakasi za haraka hadi kwenye gari tulipo jificha mimi, raisi na Babyanka.

“Inabidi tuondoke hapa sasa hivi, watu wangu wote wamesha kufa”
K2 alizungumza huku akigema sana, kwani shuhuli tunayo ifanya sasa hivi sio ndogo, ni kufa na kupona pasipo kufanya hivyo basi maisha yetu yanakwenda kufa. Sote tukaingia kwenye gari huku nikijirusha kwenye siti ya dereva, kwa haraka haraka nikaanza kulirudisha gari nyuma huku risasi zikiendelea kurindima, kulifwata gari letu, cha kumshukuru Mungu gari yetu haiingii risasi na hii ndio pona pona yetu la sivyo miili yetu ingejaa risasi kutoka kwa wavamizi hawa. Nilaligeuza gari kwa kasi hiyo hiyo na likageukia kule tulipo tokea.

Nikakanyaga mafuta na kuanza kurudi tulipo tokea, ndani ya gari kila mtu akawa kimya nikamtazama raisi huyu feki nikamuona jinsi anavyo endelea kutemeka kwa woga. Tukiwa njiani tukapishana na gari za jeshi zikielekea eneo la tukio. Nikafika kwenye barabara ya bagamoyo inayo elekea Dar es Salaam, nikakunja kulia kwangu na kuendelea kuendesha kwa mwendo wa kasi japo nyuma yetu hakuna gari hata moja ambayo inatufukuzia.

    Masaa yakazidi kwenda mbio, hadi inatimu saa saba na nusu tukawa tumesha ingia jijini Dar es Salaam. Moja kwa moja tukaelekea ikulu, ambapo tukakuta pameimarishwa ulinzi mara dufu. Geti likafunguliwa baada ya askari kufika karibu ya gari letu, alipo muona raisi alituruhusu. Moja kwa moja nikaelekea kwenye maegesho ya gari za raisi. Tukashuka huku walinzi wengine wanne wakifika, karibu yetu nina imani taarifa ya kushambuliwa kwa msafara wa raisi ilisha tolewa ikulu. Moja kwa moja tukaelekea ndani na kumkuta raisi mwenyewe akiwa amesimama sebleni pamoja na viongozi wengine wakionekana wakiwa katika hali ya wasiwasi. K2 akastuka baada ya kumuona raisi halisi, aliye tufwata na kutupa mikono mimi na Babyanka.

“Hongereni sana vijana kwa kazi mulio ifanya”
“Asante muheshimiwa ni jukumu  letu”
“Pole bwana mdogo kwa kukuweka katika hali ya hatari”
“Ahaa kaka wewe acha tuu, wapo wapi wale madaktari wa kichina wanivue hii sura yako”
“Wapo watakuvuaa”
Raisi feki akaondoka na kuelekea katika vyumba vingine vilivyopo hapa ikulu na kutuacha na muheshimiwa raisi.
“Huyo ni mdogo wangu anaye nifwata mimi”
Raisi alizungumza huku akitutazama sisi, akatukaribisha na kukaa kwenye sofa za hapa sebleni, akawaomba viongozi wengine kuondoka akiwemo K2 ambaye hakujua ni mazungumzo gani muhimu ambayo mimi niliye chini yake nimebaki.

Baada ya mlango wa kutokea sebleni kufungwa raisi akashusha pumzi nyingi huku akitutazama kwenye nyuso zetu.
“Kimtazamo munaonekana kwamba mumechoka sana na pilika pilika za hapa na pale”

==>>Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

$
0
0
Super nzoka IKEMEKO TRDITONAL clinic Ni dawa ya Asili ya vidonge iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 

Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji maji ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara kwa mtumiaji yeyote hata wa umri wa miaka 80 na kuendelea.... inaongeza hamu, urijali kwa wanaoshindwa kuendelea na tendo la ndoa.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 kwa tendo la kwanza itakuwa unauhakika wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuhisi kuchoka 

SILYA; inakuza uume uliosinyaa kurefusha umbile dogo urefu inchi (6-9)na unene wa cm 4 za upenyo kwa wenye kasoro za kimaumbile na walioathiriwa na kupiga punyeto pamoja na matatizo ya kiafya

Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0716343218 TUNAPATIKANA BUGURUNI SOKONI STENDI ya musanga

Tiba Asili ya Kuondoa Chunusi, Kupunguza Tumbo, Maziwa Makubwa na Nguvu za Kiume

$
0
0
Asilimia 90 ya wanaume hushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya  kama vile kisukari, punyeto ambayo huathiri mfumo mzima wa wa misuli inayozalisha vichocheo ashiki , kutopata choo vizuri hali ambayo huchakiwa na kula chakula kisicho na asili,tumbo kuunguruma, kujaa gesi,kiuno kuuma, mgongo na miguu kufa ganzi

SUPER HOLO; Ni dawa itokanayo na miti shamba, ipo katika mfumo wa vidonge na unga. Hutibu na kumaliza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa muda mfupi tu.,SUPER HOLO hurudisha heshima ya ndoa, itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika 15-30. Itakupa hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3. Pia itaimarisha misuli iliyosinyaa na kulegea. Dawa hii hutumiwa kwa watu wa umrii wa miaka 20- 80

NZOGIWE ni dawaya maumbile.Hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo urefu wa nchi 4-8 na unene wa sentimita 2-4 za upenyo

NZOGOMA ni dawa asili ya miti shamba, huboresha mbegu za uzazi...huzibua mirija na kusafiisha ili kuweza kushika mimba au kutia mimba.

Pia tunayo dawa ya kupunguza tumbo, unene, maziwa makubwa, kuongeza hips, makalio na kutoa chunusi

TUNAPATIKANA MTONI MTONGANI. KANA HAUNA NAFASI YA KUFIKA UTALETEWA ULIPO. WASILIIANA NA DR. MBUSI.  PIGA SIMU NAMBA:   0718 431222

Tiba Bora ya Nguvu za Kiume, Kisukari, Ngiri, Miguu Kuvimba

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume yanawaathiri watu wengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wengine. Kawaida mwanaume anatakiwa kuwa na uume kuanzia nchi 6- 8, vinginevyo mtu huwa na matatizo. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo. 

Baadhi ni upungufu wa vichocheo hivi; Homoni za getrogen ambazo mwanaume anapobalehe, vichochea hivi huchochea ukuaji wa uume.

Ngiri; Hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na hufanya tumbo kuunguruma na kujaa gesi. Sababu zingine ni korodani moja kuvimba, kupopata choo vizuri.

Sababu hizi na zingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara kwa mara husababisha kukosa tendo ya kurudia tendo na baadae kushindwa kabisa

SILYA: Ni dawa inayozalisha homoni zxa Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka hadi nchi 6-8
 
WET POWER: Ni dawa bora ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba na matunda ambayo huongeza nguvu za kiume kuanzia miaka 15-95 na hukomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi, ina imariisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara mbili bila hamu kuisha na pia itakuchelewesha kufika kileleni

Pia tunatibu kisukari, presha, ngiri, miguu kuvimba na kuwaka moto

Wasiliana na Sheikh Khatib akutatulie matatizo yako. Namba zake; 0785 234 837  au 0656 551 093  au 0746473974

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Moto wateketeza wanne wa familia moja

$
0
0
Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuteketea moto.

Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Magwira, Kata ya Bwilingu wilayani Chalinze usiku wa kuamkia leo Machi 11,2018.

Chanzo cha moto hakijajulikana ingawa imeelezwa kulikuwa na tatizo la umeme kuzima na kuwaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shanna amethibitisha tukio hilo akiahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0744 594 994

Kubenea kudai Tume huru ya uchaguzi

$
0
0
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amemtaka Waziri wa Katiba wa Sheria na Katiba Prof. Paramagamba Kabudi kubeba hoja yake binafsi aliyowasilisha Bungeni siku za hivi karibuni ili kuweza kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi kabla ya chaguzi zijazo.

Kubenea ametoa kauli hiyo leo (Machi 11, 2018) wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema lengo la yeye kupeleka hoja binafsi ni kutokana na kutokuwepo kwa tume huru itakayoweza kujiendesha yenyewe mambo yake bila ya kutegemea kupata msaada serikali huku akitolea mfano suala la bajeti la kuendesha tume wakati wa chaguzi.

"Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lijadili na kuazimia serikali ipeleke Bungeni mswada wa marekebisho ya Katiba ili kuruhusu kuundwa kwa chombo huru kitakachoweza kusimamia uchaguzi kitachoitwa Tume Huru ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", amesema Kubenea.

Pamoja na hayo, Kubenea ameendelea kwa kusema "suala la tume huru ya uchaguzi ni kilio cha watu wengi sana wakiwemo viongozi wa serikali, asasi za kiraia na vyama vya kisiasa. Kwa hiyo ni matarajio yangu kuwa watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii wataungana na mimi na kuunga mkono hoja yangu na hivyo taifa taifa hili litaweza kupata tume huru kabla ya uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2020.
 
"Tume iliyoongozwa na Jaji Warioba ambayo Prof. Kabudi alikuwa kamishna ilileta mapendekezo ya kuwepo tume huru ya uchaguzi. Leo Prof. Paramaganda Kabudi ndiyo Waziri wa Sheria na Katiba wa serikali ya Rais Dkt. John Magufuli, ni matarajio yangu Prof. Kabudi atabeba hoja yangu kwa nguvu zote kuishawishi serikali, wabunge wenzetu waikubali na ije na maadhimio hayo".

Kwa upande mwingine, Kubenea amesema ni matarajio yake Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai atatumia busara zake zote na mamlaka aliyopewa ili kuruhusu hoja aliyoipeleka Bungeni ipite na izae matunda mazuri ndani yake.

Mbunge wa CCM ajitosa jimbo la Lissu, aanza kutoa misaada

$
0
0
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (CCM) ametoa msaada wa vitanda vya kujifungulia katika jimbo linaloongozwa na Tundu Lissu (CHADEMA).

Amesema kuwa ametoa msaada huo mara baada ya kufuatwa na kuombwa msaada na siyo kisiasa kama inavyozungumzwa na watu wengine.

Kingu ameeleza kuwa katika jimbo linaloongozwa na Lissu wapo madiwani wanaotoka katika chama chake (CCM) na ndiyo waliomfuata kuomba msaada kwake na wala hakuwa na nia ya kufanya kazi ndani ya jimbo hilo bali ni moyo tu.

Amesema kuwa asingeweza kwenda kutoa misaada katika majimbo ya wana CCM kwa kuwa hawakumuomba na kama ikitokea siku wakahitaji msaada wake yupo tayari kuwasaidia kwa kadri ya uwezo wake.

“Mimi sioni ubaya. Watu wameomba msaada wa vitanda kwamba kina mama wanateseka. Marekani leo wanaisaidia Tanzania haina maana kwamba Marekani mambo yako supa. Lakini Marekani inatoa misaada ya mabilioni. Mimi kwenda kutoa msaada jimboni kwa Lissu haina maana kwangu nimemaliza changamoto za kwangu,” amesema Kingu

Hata hivyo, Katika hatua nyingine Kingu amesema anamuombe Lissu ambaye amemtaja kama Kaka yake apone ili aweze kurejea kwenye majukumu yake.

Maandamano Yamwibua John Cheyo....Ataka Mabaraza ya Vyama Yatumika Badala ya Watu Kuandamana

$
0
0
Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo amesema mabaraza ya vyama vya siasa yakitumika kikamilifu yanaweza kuondoa malalamiko ya wananchi na viongozi wa upinzani.

Amesema hayo leo Machi 11,2018 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu vuguvugu la maandamano yaliyopangwa kufanyika Aprili 26,2018 yanayoratibiwa kupitia mitandao ya kijamii.

Cheyo amesema maandamano hayo ni uchochezi na uvunjifu wa amani na kwamba, mambo yanayolalamikiwa yangeweza kutatuliwa kupitia mabaraza hayo.

"Tusitake kufika hatua ya kuandamana barabarani ili kudai haki, Katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi. Tukifikia huko amani iliyopo Tanzania tutashindwa kuipata tena na wananchi watakosa nchi nyingine yenye amani ya kukimbilia," amesema.

Cheyo amesema kama tatizo ni fedha kwa ajili ya mabaraza hayo kukutana, Rais John Magufuli anapaswa kutoa fedha kuyawezesha kufanya vikao.

"Siungi mkono hoja za kudai kuwepo mikutano ya hadhara hata kama ni kwa ajili ya kuongeza wanachama kama wanavyodai wengine, naamini kwa sasa mitando ya kijamii ina nguvu kuliko kitu chochote nchini," amesema Cheyo.

Amesema kabla ya kudai haki ya kuandamana, zipo nyingine wananchi wapaswa kuzipa kipaumbele zikiwemo haki ya kuishi, kupata maji safi na salama, elimu na afya.

"Hatuwezi kufika mahali tuseme nchi hii imepotea na hakuna demokrasia kisa tumekosa haki ya kuandamana, haki ya kufanya mikutano ya hadhara. Kila mtu alishuhudia mikutano ya kampeni za uchaguzi wa ubunge wa marudio katika majimbo ya Kinondoni na Siha ilivyogeuka sehemu ya kutukanana," amesema Cheyo.

"Kama kitu mnachokidai kiliweza kusababisha watu kugombana na askari hadi mauaji yakatokea hicho kitu hakitusaidii kama nchi," amesema.

Cheyo amesema yanayodaiwa kwa nguvu hayana faida na manufaa ya kila siku kwa sababu watu wanahitaji kupata wakati wa kulima na kuvuna.

"Hiyo mikutano iliyoshupaliwa sasa na kuhitajika kwa nguvu zote si kweli kwamba kila siku watakuwa barabarani kuhutubia wananchi, fedha tutatafuta saa ngapi, tutalima saa ngapi, hivyo ni vyema tutambue kila kitu kinachofanyika kupitia mambo ya siasa kisiwe kisingizio cha kusema nchi haina amani, haina uhuru," amesema Cheyo.

Amesema viongozi wa dini wanapaswa kuwa kiunganishi cha wananchi na viongozi wa vyama vya siasa na si kufanya kinyume cha hilo.

Jeshi la Polisi lawapiga marufuku ACT Wazalendo kufanya mikutano ya ndani

$
0
0
Jeshi la Polisi wilayani Mvomero Mkoani Morogoro limekiamuru chama cha ACT Wazalendo wilayani humo kusitisha kufanya mikutano ya ndani

Katika barua iliyosainiwa na SSP Julius S. Lukindo ambaye ni Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo imeelezwa kuwa Jeshi la Polisi kwasasa linashughulikia kesi nyingi za kisiasa hivyo ACT Wazalendo wanashauriwa kufanya mikutano hiyo siku za baadae

Mwigulu aonya atakayeandamana ‘hata kuzunguka kitanda’

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza na kumuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote ambao wamepanga njama za kutaka kuwauwa watanzania katika maandamano ambayo wameyapanga kuyafanya

Mwigulu ametoa hiyo wakati alipokuwa akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli aliyopo Mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ambapo leo hii (Machi 11, 2018) amezindua kiwanda cha Alizeti Mkoani humo na kusema kinachotafutwa katika maandamano hayo ni namna ya watu wanatawanywa ili kusudi waje kulalamika kuwa serikali ndio imeuwa watu wake.

"Njama hiyo tumeiona na mimi nimemuelekeza IGP Sirro kwamba hata kupanga njama ya kuua ni kosa, wachukue hatua kwa wale watu wanaopanga mipango ya aina hiyo na kuchafua taswira ya nchi yetu ama kwa mipango yao au ya wale wanaowatuma. 

"Watu wanataka mikusanyiko ili wafyatue na kuuwa watu  ili kuchafua taswira ya nchi yetu na tunayo mifano wa maeneo waliwahi kufanya jambo la aina hiyo na hatua zitachukuliwa", amesema Mwigulu.

Pamoja na hayo, Mwigulu ameendelea kwa kusema "Mhe. Rais ndio maana unaona vinyago vinyago vingi hivi kama hivi juzi alitokea kijana mdogo amesema ametekwa, eti ametekwa na akapata muda wa kutafuta pafyumu na nguo za kubadilishia kule atakapokuwa ametekwa. 

"Unatowa wapi muda wa kujiandaa ?, watu wanatafuta njia za kuchafua taswira ya nchi yetu, na jambo hili Mhe. Rais kama ambavyo ulishatoa maelekezo, si jambo ambalo tutacheza nalo wala mjadala, hakuna sababu ya maandamano wala hakuna sehemu ya kuandamania na hakuna ruhusa ya kuandamana".

Aidha, Waziri Mwigulu amesema endapo ikatokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba zao bado sheria itachukua mkondo wake dhidi ya watu hao.

"Ikitokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba wakazunguka kitanda na akatokea mtu akaumia, yule aliyeitisha waandamane pale atawajibika kwasababu watu wanafanya mzaha na maisha na dira ya nchi yetu ambapo Rais umejitoa muhanga kwa ajili ya kutengeneza urithi wa watoto wa Tanzania", amesisitiza Mwigulu.

Kwa upande mwingine, Waziri Mwigulu amesema yeyote atakayethubutu kutaka kuharibu taifa la Tanzania kwa kufanya vitendo vya uovu hawatoweza kumuacha salama.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images