Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Nane ( 18 )

$
0
0
AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA Nikakata simu na kuendelea na safari yangu na kwa mbali kutoka nilipo hadi ilipo nyumba ya bibi nikaona nje kumefungwa turubai huku watu walio valia kanzu wakiwa wamekaa kwenye majamvi huku ukimya ukiwa umetawala katika endeo hilo.Nikazidi kuongeza mwendo huku akilini wazo la bibi kuwa amefariki dunia likaanza kunitesa,Kabla sijafika karibu na sehemu ilipo nyumba ya bibi nikastuka mtu akinishika mkonno kwa nyuma huku akinivuta kwa nguvu

ENDELEA
     Nikageuka na kukutana na sura yam zee wa makamo akiwa amavalia kanzu nyeupe na barakashea huku mkononi mwake akiwa ameshika mkongojo wa kumsiadia katika kutembelea
“Shikamoo mzee”
“Shikamoo yako haina msaada wowote kwangu”
Mzee alizungumza kwa hasira huku akiachia msunyo mkali hadi nikabaki ninamshangaa huku nikijiuliza nilicho mkosea ni nini
“Wewe kijana ni mbaya sana…..Kijana huna adabu shiii nkumi,kijana huna busara.Yaani umeona haitoshi umeamua kutuma majini yako kuja kumdhuru mke wangu”
“Mzee mbona sikuelewe umechanganyikiwa nini?”
“Mimi nimechanganyikiwa.PUMBAVU SANA WEWE”
Mzee akanichapa bakora moja na kunifanya nimponyoke mkononi mwake na kusimama pembeni nikiwa ninamshanga huku watu wengine walio karibu yetu wakitushangaa kwa tukio alilo lifanyia babu

“Vijana wa siku hizi hamuuna adabu sana unaniambia nimechanganyikiwa mimi?”
“Oya brother Eddy huyo mzee ni kichaa asikupotezee muda wako wewe achana naye”
   Alipita jamaa mmoja na kuniambia kuhusiana na huyo mzee ambaye kwenye macho yangu sikuwahi kumuona siku hata moja katika mtaa nilio kuwa nimekaa.Nikaamini mzee hana akili vizuri baada ya kuanza kumkimbiza kijana aliye niambia kuwa mzee huyo ni kichaa.Nikajiweka vizuri shati langu na kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye nyumba ya bibi iliyo jaa watu nje wenye kanzu nyeupe.Bibi akaniona na kuja kunifwata na kunikaribisha na kunionyesha stuli isiyo kaliwa na mtunkisha nikaichukua na tukasogea kidogo na kukaa pembeni na walipo watu wenye kanzu nyeupe huku bibi akikaa juu ya gogo la muembe ulio katwa siku nyingi
“Bibihapa kuna nini?”
“Ni maulidi ya mwanangu mmoja wa kike anayafanya kwa mtoto wake alieye zaliwa miezi kadhaa ya nyuma”

“Ahaaa mbona kumetulia sana?”
“Ahha ndio wanamalizia malizia…”
“Inamaana watu tayari wameshamaliza kula ubwabwa?”
“Ubwabwa wamekula tangua amchana hapa wanasubiri kufunga maulidi”
“Bibi bwana mimi nimekuja nina tatizo tena sio dogo nitatizo kubwa kiasi kwamba ninajikuta nimechoka kwenye tatizo lenyewe”
Bibi akaanza kucheka na kwajinsi ya meno yake kuwa pungufu mdomoni mwake na kuweka mapengo makubwa ikanilazimu na mimi kuanza kumcheka
“Eddy mjukuu wangu ile jana ulivyo kuwa unahama unakumbuka nilikupa nini?”
“Ulinipa maji kwenye kichupa?”
“Uliyatumia?”
“Bibi nisikudanganye nilisahau?”
“Hapo ndipo ulipo kosea na yule msichana uliye hama naye ndio aliye kusababishia matatizo hayo”
“Amenisababishia matatizo hayo kivipi?”
“Ngoja nikuambie kitu usicho kijua kuhusu yule msichana”
Nikajiweka vizuri kwanye stuli niliyo ikalia huku nikimtazama bibi kwa umakini 


AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 17 na 18)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA 
  
“Mama kuna nini?”      
“Kuna nyaraka za serikali ambazo ni muhimu sana, zimeibiwa. Sijui nitafanya nini mimi”
Mama alizungumza kwa unyonge huku machozi yakimlenga lenga mikono yake akiwa ameiweka kichwani, hapo ndipo taratibu nikaanza kupata picha ya mtu ambaye alitoka kasi na nilimuhisi kwamba ni mwaume wa Yudia kumbe sivyo hivyo ni mwanaume aliye kuja kuiba nyaraka muhimu za mama.
“Dany mwanangu unatakiwa kufanya kitu, la sivyo kazi sina mwanaungu”
Mama alizungumza huku machozi yakimwagika kitendo kilicho nifanya nijisikie vibaya sana moyoni mwangu.
  
ENDELEA
Kwa ishara nikamuomba Yudia kutoka chumbani kwa mama, naye akafanya hivyo akiwa katika hali ya woga. Taratibu nikamshika mama na kumkalisha kitandani kwake.
“Nitafanya nini mwanagu, mkataba huo ni muhimu na kesho kutwa raisi anakuja Tanga na anahitaji kuweza kuusaini”
Mama alizungumza machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. Ikanibidi kukaza roho kama mtoto wa kiume kuto kulia mbele ya mama yangu kwa maana, machozi yake yanaufanya mwili wangu wote kusisimkwa na kujihisi na mimi ninaweza kudondosha chozi muda na wakati wowote.
“Kwani mama kuna kitu watu ambao una bifu bifu nao?”
Mama akakaa kimya kwa muda, kisha akatingisha kichwa kuashiria kwamba kuna watu ambao ana ugomvi nao.
“Ni kina nani hao?”
“Kuna huyu meya mpya, wao nina uhakika kwamba ndio wanao winda hizi nyaraka, wanataka kuziteketeza ili mpango wa ujenzi wa bandari mpya usifanikiwe”

“Na huyo meya ana kaa wapi?”
“Raskazoni kule”
“Ok ngoja nianze kuifanya hivyo kazi muda huu, ila nina kuomba usilie sawa mama yangu”
“Sawa”
Nikamfuta mama machozi kwa kitambaa chake, kisha nikanyanyuka na kutoka chumbani humo. Nikakutana na Yudia kwenye kordo akiwa kama ni mtu mwenye wasiwasi na kitu fulani, ila sikutaka kumsemesha chochote kwa maana mambo ya muhimu ya mama yamesha haribika. Tukiwa hapo kwenye kordo tukasikia sauti ya kungele ya getini ikiita. Yudia kwa haraka akaondoka na mimi nikaingia chumbani kwangu.
Nikafungua kabati na kutoa begi langu la nguo, nikaitoa bastola yangu, niliyo iweka chini kabisa ya nguo zangu, nikaitazama huku nikitoa magazine yake, nikaikuta ikiwa na risasi za kutosha na wala sijaitumia muda mrefu. Nikaiweka pembeni kisha nikatoa suruali yangu ya jinzi nikaiweka pembeni, nikiwa katika hatua hizo nikasikia mlango ukigongwa, kwa haraka nikaichukua basola yangu na kuirudisha ndani ya begi na kwa mwendo wa taratibu nikaelekea mlangoni na kuufungua.

“Kaka Dany daktari amesha fika”
“Nakuja”
Nikaufunga mlango mara baada ya Yudia kumaliza kunipatia ujumbe wake, nikalifunga begi vizuri na kutoka chumbani kwangu nikakutana na daktari ambaye mama alizungumza naye muda mchache ulio pita, nikamsalimia kutokna ni mzee wa makamo ya kina mama.
“Muheshimiwa yupo wapi?”
“Amejipumzisha mama, unaweza ukaanza kunihudumia tu”
“Ok sawa ninakuomba nione kidonda chako”
Taratibu nikavua shati na kumuonyesha daktari Kidonda hicho.
“Kimeanza kukauka”
Alizungumza, huku akikigusa gusa kwa juu. Akafungua kiji begi chake kidogo cha mkononi, akatoa kichupa kidogo pamoja na bomba la sindano lililo jipya kabisa.

“Nitakuchoma sindano ya kukikausha ndani ya siku mbili hizi kitakuwa kimepona kabisa”
“Ina maana na ngozi yake itarudi kama kawaida?”
“Hapana ngozi itarudi taratibu taratibu”
“Sawa”
Akachukua pamba na kuipaka dawa ya kusafishia, kwenye mshipa wa mkono wa kushoto. Alipo maliza kufanya hivyo akanichoma sindano hiyo yenye dawa ambayo nilisha wahi kuchomwa hospitalini juzi.
“Kijana unaonekana unafanya sana mazoezi”
“Kwa nini?”
“Mishipa yako imejitokeza kiurahisi ni tofauti sana na watu wengine mishipa yao kujitokeza ni kazi sana”
“Ahaaa, huwa na fanya sana mazoezi”
Daktari akachomoa sindano yake baada ya kuisukuma damu taratibu. Akanipatia pamba iliyo na dawa nikajiziba nayo katika eneo ambalo amenichoma sindano.
“Kesho asubuhi ukija Hospitalini kwangu nitakuchoma nyingine ya kumalizia”

“Sawa sawa hospitali yako ipo eneo gani?”
“Barabara ya pili pale”
“Ahaa ok asante”
Nikamuga daktari huyo na kuingia chumbani kwangu, nikafungua begi langu na kuitoa bastola kisha nikavua pensi na kuvaa jinzi, sikuona haja ya kulivua shati nililo livaa. Nikaichomeka bastola yangu kiunoni kwa nyuma na kutoka chumbani kwangu. Nikaingia jikoni kwa ajili ya kunywa maji kabla sijaanza upelelezi wangu wa kuifwatilia nyumba ya meya ambaye mama anamtilia mashaka.
Nikiwa hapo simu ya Yudia ikaingia mesiji, mwenyewe hakuwepo nikaona bora niichukue na ili kuifungua meseji hiyo niliyo hisi labda ni mtu ambaye ni bwana wake.
(Mambo yameharibika, kaeni kwa tahadhari mjulisheni na meya)
Meseji hiyo ameituma Yudia kwenda kwa mtu huyo aliye jibu ‘SAWA’. Nilijikuta nikianza kupata mashaka makubwa, kwa haraka nikaituma namba ya mtumaji wa meseji hiyo kwenye simu yangu, nilipo hakikisha kwamba nimemaliza kuituma. Nikaifuta meseji yake aliyo tuma na niliyo jitumia na simu ya Yudia nikairudisha sehemu nilipo itoa, nikatoka jikoni humo nikiwa nimejikausha na nikamkuta Yudia akingia kwenye mlango wa sebleni akitokea nje.

Wastara arejea Kutoka Kwenye Matibabu India

$
0
0
Msanii wa filamu, Wastara Juma amerejea nchini leo akitokea Mumbay nchini India alikokuwa anapatiwa matibabu ya mgongo na mguu na kuwashukuru Watanzania kwa namna walivyojitokeza kumchangia fedha za matibabu, ingawa hazikutosha na kulazimika kuuza baadhi ya mali zake.

Akizungumza leo Machi 1, 2018 nyumbani kwake Tabata ikiwa ni saa chache baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, amesema baada ya kufika hospitali alikutwa na matatizo mengine zaidi ya aliyokuwa nayo jambo lililosababisha gharama za matibabu kuwa kubwa.

Wastara alifanikiwa kwenda kwenye matibabu hayo, Februari 3, 2018 baada ya kupata michango kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Rais John Magufuli aliyemchangia Sh15 milioni.

Amebainisha kuwa matatizo aliyokutwa nayo ni pamoja na uvimbe chini ya kalio na kwamba, ndilo lilikuwa sababu ya kukaukiwa damu pamoja na kubainika kuwa na uvimbe kichwani uliotokana na kupata ajali zaidi ya mara tatu.

“Kutokana na matatizo haya ilifika mahali pesa nilizokwenda nazo ziliniishia na kulazimika kuwaomba ndugu zangu wauze baadhi ya mali zangu, ikiwemo kamera ili niweze kuendelea na matibabu,” amesema.

“Mtu umeshafika kwenye matibabu tena nchi za watu unafanyaje? Kurudi bila kutibiwa huwezi. Nililazimika kuwasiliana na ndugu zangu ili wauze baadhi ya vitu vyangu niweze kutibiwa maana afya yangu ni muhimu kuliko kamera.”

Mahakama Kuu Yapokea Rufaa ya Sugu na Mwenzake

$
0
0
 Rufaa ya kupinga hukumu ya kifungo cha miezi mitano jela iliyotolewa kwa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga imewasilishwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.

Akizungumza leo Machi 1, 2018 mmoja wa mawakili wa Sugu, Faraji Mangula amesema  tayari maombi ya rufaa yao yamepokewa leo  mchana na kupewa kumbukumbu namba 29/2018.

“Tayari rufaa yetu imeshapokewa Mahakama Kuu (Mbeya) na tunachosubiri  ni kupangiwa tarehe ya kuanza kusikiliza tu, ila tunachoshukuru watu wa Mahakama hii wapo vizuri kushughulikia suala hili,” amesema Mangula.

Mbali na kukata rufaa hiyo, lakini pia mawakili hao wanakusudia kuomba dhamana kwa wateja wao  ili waweze kuwa nje katika kipindi ambacho wanakuwa wanasikiliza rufaa yao.

Sugu na Masonga walihukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Wawili hao walitoa kauli hiyo Desemba 30 mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Urusi yajaribisha kombora jipya ....Halina Ukomo wa Masafa na Linaweza Kupenya Kizuizi Chochote cha Makombora

$
0
0
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema jeshi lake limejaribisha silaha kadhaa mpya za nyuklia ikiwemo aina ya kombora ambalo halina ukomo wa masafa na linaweza kupenya ngome ya mfumo wowote unaokabiliana na makombora.

Alikuwa akizungumza na wabunge katika hotuba yake ya taifa kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika Machi 18 nchini Russia. Putin atakuwa anatumikia awamu ya tatu kama rais na anatarajiwa kushinda na kuendelea kushikilia wadhifa wake kwa miaka sita.

Pamoja na kombora hilo, Putin amesema kuwa Urusi tayari imejaribisha kombora lake jipya ambalo linauwezo wa kufika katika mabara tofauti – linaloitwa Sarmat- ambalo ni la masafa marefu na lenye kubeba silaha nyingi zaidi kuliko lile la awali.

“Sarmat ni silaha yenye nguvu kubwa sana. Kutokana na maumbile yake hakuna mfumo uliopo wa kuzuia makombora unaweza kuwa ni kizuizi dhidi yake.”

Kiongozi huyo wa Urusi ameweka malengo ya kupunguza umaskini nchini Urusi kufikia asilimia 50 wakati wa kipindi kinachotarajiwa cha muhula wake unaofuatia na kueleza umuhimu wa kuendeleza technolojia ili kupeleka mbele maendeleo.

Vipaumbele vingine ambavyo amevigusia ni pamoja na kuboresha huduma za afya na miundo mbinu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Ijumaa ya March 2

LHRC yadai upinzani ulionewa uchaguzi mdogo Kinondoni na Siha.....Hapa Kuna Tamko Lao

$
0
0
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimedai uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni na Siha uliofanyika Februari 17, 2018 ulikuwa huru, lakini haukuwa wa haki kwa sababu vyama vya upinzani vilionewa.

Akizungumza jana Alhamisi Machi 1, 2018 Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, Anna Henga amewaeleza waandishi wa habari kuwa kulikuwa na upendeleo kwa CCM, kwamba mawakala wa vyama vya upinzani walinyimwa viapo katika vituo vingi na kusababisha vyama hivyo kukosa waangalizi.

"Sisi hatuogopi kuitwa Chadema wala chama kingine cha upinzani kwa sababu tunafuata sheria. Kama uonevu ulikuwepo lazima tuseme," alisema Henga.

"Kulikuwa na uonevu kwa vyama vya upinzani, mawakala wao walinyimwa viapo au kupewa nakala. Tuliwashuhudia mawakala wao wakihangaika kutafuta viapo, wengine walipata saa 8 mchana.”

==>Soma Tamko lao hapo chini
 

Serikali Imetenga Shilingi Bilioni 11.4 Kuboresha Wakala Wa Ndege Zake

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuboresha Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) ambayo inasimamia na kuendesha ndege ambazo zinasafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea na kukagua utekelezaji wa majukumu ya Wakala wa Ndege za Serikali ambayo inasimamia na kuendesha ndege ambazo zinasafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali ambapo alizungumza na Menejimenti na wafanyakazi na kuwaeleza kuwa Serikali imejipanga kuboresha Wakala hiyo

Mhandisi Nditiye alisema kuwa azma ya Serikali ya Awamo ya Tano inayosimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha kuwa Taasisi za Serikali zinafanya kazi zake kwa weledi na uadilifu ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuwatumikia wananchi. 

“Serikali inatambua umuhimu wa Wakala hii na ina imani kubwa nanyi katika kuhakikisha kuwa mnafanya kazi zenu za kusafirisha viongozi kwa usalama na kwa uhakika ili waweze kutimiza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi na tayari ina nia ya kuboresha taasisi hii”, amesema Mhandisi Nditiye.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TGFA Bwana Tito Kasambala amemueleza Mhandisi Nditiye kuwa taasisi yake ina ndege nne ambazo zinatumika kusafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali katika kutimiza majukumu yao ya kuwatumikia watanzania na tayari Serikali imetenga shilingi bilioni 11.4 kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/18 kwa ajili ya shughuli mbali mbali za Wakala ikiwemo matengenezo ya ndege, mafunzo kwa wanahewa na ukarabati wa karakana.

Mhandisi Nditiye amewaeleza wajumbe wa Menejimenti na wafanyakazi wa Wakala hiyo kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wao na umuhimu wa wahandisi wa ndege na marubani wa kupata nafasi ya kuendesha ndege na kozi za mafunzo mbali mbali kuendana na taaluma zao ambapo tayari makubaliano yamefanyika baina ya Wizara na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ya kuwapatia nafasi marubani wa ndege za Wakala wa Ndege za Serikali nafasi ya kurusha ndege mara kwa mara ili kuendana na matakwa ya taaluma zao.

Ameongeza kuwa Serikali inashughulikia suala la miundo ya watumishi wa umma ambapo Wakala wa Ndege za Serikali ni mojawapo ya taasisi ambayo muundo wake unafanyiwa kazi ili kuweza kuzingatia taaluma, kada za watumishi na maslahi yao. 

“Natumaini wote mnatambua na kuelewa kuwa kipindi cha hapo nyuma kidogo utumishi wa umma uliingiwa na baadhi ya watu wachache ambao walikuwa wanafanya ujanja ujanja na kuharibu utumishi wa umma ambapo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wetu, imelifanyia kazi jambo hili na ameunda bodi maalumu ambayo inafanyia kazi suala la muundo, kada na maslahi ya watumishi wa umma,” amesema Mhandisi Nditiye.

Aidha, wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali wamemuomba Mhandisi Nditiye kuwasilisha ombi lao kwa Serikali la kuwaongezea mishahara yao kuendana na hali ya soko la ajira ya marubani ilivyo nchini kwa sasa.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0744 594 994

Wanafunzi 400 wavamia Nyumba ya Mwalimu na Kufanya Vurugu....Shule Yafungwa Wiki 2

$
0
0
Serikali imeifunga Shule ya Sekondari ya Lyamungo iliyoko Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya wanafunzi wake kuzusha vurugu kubwa huku wakivamia na kuivunja ofisi ya Makamu Mkuu wa shule hiyo.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Hai, Onesmo Buswelu, alithibitisha jana kuifunga sekondari hiyo ya kitaifa kuanzia Machi Mosi hadi Machi 17, mwaka huu.

Shule hiyo ya kitaifa hupokea wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita kutoka mikoa mbalimbali nchini.

"Ni kweli nimeifunga hiyo shule kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na sababu za kiusalama. kulikuwa na uchaguzi wa serikali ya wanafunzi na wakati unafanyika mwanafunzi mmoja aliandika matusi makubwa akiwatukana walimu.

"Baada ya kufanyika uchunguzi aligundulika huyo mwanafunzi na hapo ndiko walipoandaa vurugu hizo na kujielekeza kuharibu mali na kusababisha hasara ambayo bado haijafahamika," alisema Buswelu.

Kwa mujibu wa Buswelu, vurugu hizo ziliibuka baada ya mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) kupewa barua ya kufukuzwa shule kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Buswelu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Siha ameagiza Bodi ya shule hiyo kukutana kesho (leo) kufanya tathmini ya hali ya uharibifu na madhara yaliyojitokeza na kuiarifu serikali.

Mpaka sasa, hakuna mwanafunzi anayeshikiliwa kwa kufanya vurugu na kusababisha hasara ya mali na rasilimali za serikali.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hamisi Issah, alisema wanafunzi hao walifanya tukio hilo saa 4:30 asiku juzi.

"Hao wanafunzi wameharibu ofisi ya mwalimu huyo ambaye pia ni mwalimu wa nidhamu kwa kuvunja paa la juu, milango, madirisha na samani za ndani," alisema Kamanda Issah.

Dawa Asilia Inayo Saidia Kushusha Sukari Iliyopanda.

$
0
0
Je ! Sukari  yako  ipo  juu ? Unatafuta tiba  asilia  ya  kushusha  sukari ?
Kama jibu  lako  ni NDIO basi  hii  ni HABARI NJEMA  SANA  KWAKO.
Ipo tiba  asilia  inayo  saidia  kushusha  sukari iliyo  panda.

JINSI  INAVYO  TUMIKA :  Dawa  hii  huchemshwa  na  kuachwa  ipoe  kabisa  kisha  mhusika  anatumia  kunywa  nusu  glasi  yenye ujazo wa  milimita mia mbili  na  hamsini ( 250 mills ) .

Asubuhi  atakunywa  nusu  glasi  na  usiku  atakunywa  nusu  glasi. Atafanya  hivyo  kwa  muda  wa  wiki mbili  hadi  tatu.

BAADA  YA  KUMALIZA  DOZI : Baada ya  kumaliza  dozi  mhusika anashauriwa  kwenda  hospitali  kupima  ili  kuona  sukari  yake  imepungua  kwa  kiasi  gani na  kupata  ushauri  wa  kitaalamu  kutoka  kwa  Daktari.

Tiba  hii  pia  inasaidia  kuimarisha  afya  ya  mwili  kwa  ujumla.
N.B : Tiba hii  haiwafai  watu wenye  sukari  ya  kushuka  ama  sukari  iliyo  chini  kwa  sababu inashusha  sana  sukari mwilini.

Kwa  watu wenye  sukari  ya kushuka  ambao  wanatafuta  tiba  ya  kupandisha  sukari, bado  hatujapata  dawa  ya  uhakika  inayo  weza  kusaidia  kupadisha  sukari.

Jaribu  kutumia  tiba  hii  uone  namna inavyo weza  kukusaidia  kudhibiti  kiwango  cha sukari kwenye  damu.

Kwa wewe  ambae  sukari  yako  ipo  juu  na  unataka  kutumia  tiba  asilia  ya kushusha  sukari  yako, jaribu  kutumia  tiba  hii  ili  badae  uweze  kutoa  ushuhuda wa  namna  tiba  hii  ilivyo  kusaidia.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma ya jengo  la  UBUNGO PLAZA.

Wasiliana nasi kwa  simu  namba  0766 53 83 84.

Kwa  Makala  mbalimbali kuhusu  tiba  asilia  za  magonjwa  na  matatizo  mbalimbali  yanayo  msumbua  mwanadamu, tutembelee  kila  siku  kupitia  blogu yetu : wwww.neemaherbalist.blogspot.com 

TCRA Yazindua mfumo wa usajili laini za Simu kwa kutumia alama za vidole

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA)  imezindua mfumo wa kusajili laini kwa kutumia alama za vidole.

Mfumo huo ujulikanao kama Baiometria utawezesha kupata taarifa sahihi za wateja wa kampuni zote za simu nchini, ilielezwa.

Mfumo huo umeanza kwa majaribio katika mikoa sita ya Dar es Salaam, Tanga, Singida, Pwani, Iringa na Zanzibar, ilielezwa zaidi na kila mmmoja utakuwa na kituo kimoja cha usajili.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba, alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwapo vitendo vya watumiaji wa huduma kugushi vitambulisho au kutumia vitambulisho vya watu wengine.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo, TCRA kwa kushirikiana na watoa huduma za simu za mkononi na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) waliazimia kuanzisha mfumo huo.

"Mfumo huu ni wa usajili wa laini za simu kwa kutumia Baiometria; yaani mfumo wa kuchukua taarifa za wahusika kwa njia ya alama za vidole. Kama tunavyojua kila mtu ana alama pekee za vidole zisizofanana na za mtu mwingine yeyote duniani," alisema Kilaba.

Alitaja faida za kutumia mfumo huo kuwa ni kupata takwimu sahihi za watumiaji wa simu za mkononi na huduma za fedha ambao ni takribani milioni 22, kwa ajili ya kuweka mipango sawa ya kuendeleza sekta na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Alisema faida nyingine ni kujenga imani kwa watumiaji wa huduma na kudhibiti matumizi ya laini za simu kufanya uhalifu.

Alisema namba inayosajiliwa kwa majina bandia inaweza kutumika kutapeli au kutuma ujumbe mfupi wa maneno au simu za matusi na kuudhi.

"Hii itarahisisha huduma za kuhamia mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine wa simu bila kubadili namba yako, ambayo ilizinduliwa mapema mwaka jana," alisema Kilaba.

"Kwa upande wa watoa huduma, usajili utawawezesha kuwajua wateja wao na kuwahudumia kwa ufanisi zaidi."

Vitambulisho vitakavyotumika kusajili alama za vidole ni cha Taifa, mpiga kura, leseni ya udereva, kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi na hati ya kusafiria.

Moto wa Mshumaa Waua Watoto Wanne Wa Familia Moja

$
0
0
Watoto wanne wa familia moja wamefariki dunia kwa kuteketea kwa moto walipokuwa wamelala chumbani katika tukio lililotokea mtaa wa Geita Road Kata ya Nyatukala mjini Sengerema.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amesema tukio hilo lilitokea saa tano usiku wa Februari 28, 2018 na kuwataja watoto hao kuwa ni Redia Elias (10), Modesta Elias (9), Steven Deogratias (9), na Kizengela Elias mwenye umri wa miaka ninane.

Amesema wakati moto huo uliotokana na mshumaa kushika chandarua na kuunguza godoro walilokuwa wamelalia, mama yao alikuwa amelala kwenye nyumba nyingine ya familia hiyo.

“Watoto wote ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Pambalu na wanatarajiwa kuzikwa leo,” amesema Kipole.

Mmoja wa majirani wa familia hiyo, Amas Juma amewataka wazazi kuwa makini pale wanapolazimika kuwawashia watoto mishumaa kwa kuhakikisha inazimwa kabla ya kulala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuchukua tahadhari watoto wanapobaki wenyewe nyumbani.

Mvua kubwa kunyesha Arusha, Manyara na Kilimanjaro

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuanzia usiku wa  jana Machi 1, 2018  hadi  leo  Machi 2, 2018 kutakuwa na vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi ya nyanda za Juu Kaskazini Mashariki.

Taarifa ya TMA iliyotolewa  imebainisha maeneo hayo kuwa ni mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro ambapo mvua hizo itazidi milimita 50 ndani ya saa 24 huku ilieleza hali hiyo inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua.

TMA imewashauriwa wakazi wa maeneo husika kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zinazotolewa.

Kabla Sijafa - Sehemu ya 02( Simulizi ya Kweli)

$
0
0
Mwandishi: Grace G. Rweyemam
“Ninaandika wosia huu siku chache kabla ya kifo changu, ikiwa ni njia pekee ninayoweza kuonyesha ni jinsi gani nisingependa kilichonitokea kimtokee mtu mwingine yeyote. Kwa kila atakayebahatika kusoma, naomba ajue kwamba nimeandika kwa lengo la kumsaidia kujua kuwa humu duniani tunapita, na hata kama unadhani unamiliki dunia, ipo siku utaiacha. Ninafariki nikiwa na miaka 40, ninamuacha mke na watoto wangu wawili ambao bado wananihitaji sana kama baba.

Ninamuua mke wangu na kumkatishia ndoto zake, mwanamke msomi na mwerevu sana. Siwezi kumlaumu kwa lolote, ingawa mwanzoni nilihisi kama ni sahihi kutoka nje ya ndoa aliponiudhi kidogo au sana. Sasa najiuliza, ni mara ngapi yeye nilimkosea ila hakutoka nje ya ndoa. Uzinzi ni kama kulamba sega la asali, na ukishaanza kamwe si rahisi uache.

Mara ya kwanza kabisa kutoka nje ya ndoa ni wakati ndoa yetu ikiwa na miaka mitatu. Nakumbuka siku moja mke wangu alikuwa amenuna. Sikumbuki ni sababu gani hasa ilimfanya anune, ila nakumbuka mara kadhaa alininunia endapo ningemuudhi.

Tabia ya kununa iliniudhi sana, ingawa hakuninyima chakula wala kuacha kufanya majukumu yake. Kilichoniudhi zaidi ni vile ambavyo nilitumia nguvu nyingi kumfanya anipe haki yangu ya tendo la ndoa. Mwanzoni aliponuna, nilijitahidi kumbembeleza na kujipendekeza, baada ya muda akawa sawa. Lakini siku zilivyosogea, nilikuwa nikikereka sana akininunia, hivyo hata kama ningekuwa na kosa, ningejifutia na badala yake kumuhesabia yeye kosa.

Siku hiyo aliponinunia, niliamua nitaondoka nyumbani na kwenda sehemu yoyote ile bila kumuaga. Mida ya saa mbili na nusu usiku nilitoka, siku ya ijumaa, nikaenda kwenye baa moja, haikuwa mbali sana na maeneo tuliyoishi. Mimi si mnywaji kabisa, hivyo niliagiza maji tu nikawa nakunywa. Ghafla alinishika bega mtu, nikageuka na kuona ni mwanadada tunayefanya naye kazi ofisi moja, serikalini.


Diamond Kupiga Shoo Kombe La Dunia 2018 Nchini Urusi

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz anatarajiwa kushiriki katika wimbo maalumu wa Kombe la Dunia nchini Russia. Wimbo huo utakuwa unawakilisha bara la Afrika.

Wimbo huo  umedhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, Diamond atashirikiana na wasanii wengine kama Sami Dani kutoka Ethiopia, Ykee Benda kutoka Uganda na Lizha James kutoka Msumbiji.

Hapo awali msanii wa Marekani Jason Derulo alidokeza juu ya wimbo huo ambao unakwenda kwa jina la Colors ambao utatoka Machi16 mwaka huu.

Leo Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti picha inayoashia ushiriki wake katika Fainali za Kombe la Dunia ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Urusi kuanzia June mwaka huu.

Serikali Yaomba Ushirikiano Zaidi Na Benki Ya Dunia Ili Kuharakisha Maendeleo Ya Nchi

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Dkt. Felipe Jaramilo katika ofisi za  Wizara ya Fedha na Mipango Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Waziri wa Fedha na Mipango aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Joseph Magufuli  katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maedeleo hapa nchini.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa uchumi wa nchi umeendelea kukua kwa kiwango cha  kati ya asilimia 6-7 kwa muda na hivyo kuiwezesha Serikali kuendelea na utoaji wa huduma za jamii na kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa  pomaja na nia ya  kuendeleza mafanikio mazuri yaliyopatikana katika awamu za Serikali zilizopita, Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kwa dhati kujenga uchumi imara kwa kuendeleza viwanda na kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuvutia wawekezaji wa ndani na wale wa nje   kuja kuwekeza nchini , kujenga miundombinu  ya barabara, reli, umeme , viwanja vya ndege na kuongeza uwekezaji katika utoaji wa huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji.

Aidha, ameeleza kuwa katika kufikia malengo hayo , Serikali imefanya juhudi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato, kusimamia vizuri matumizi ya fedha za Serikali, kuongeza bajeti ya maendeleo hadi kufikia asilimia kati ya 35 na 40 ya bajeti nzimat, kuongeza ufanisi katika utendaji wa umma  na kupambana na rushwa pamoja na mambo mengine.

Pamoja na ukuaji mzuri wa uchumi, Dkt. Mpango alisema kuwa Taifa bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana, kiwango cha umasikini bado kiko juu, ukuaji  mdogo wa Sekta ya kilimo ambayo imeajiri takribani asilimia 70 ya watanzania unaosababishwa na ukosefu wa mbegu bora, miundombinu ya umwagiliaji na soko la uhakika, na kupungua kwa mikopo ya benki za biashara kwa sekta binafsi pamoja na mambo mengine.

Katika kusaidi juhudi za Serikali kupambana na changamoto mbalimbali , Dk. Mpango aliiomba Benki ya Dunia kupitia kwa Dk. Felipe kuisadia Serikali mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 150  kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi na utoaji huduma ( Growth and Service Delivery) amabao uko katika hatua ya maandalizi.     

Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Dkt. Felipe Jaramilo, kwa upande wake aliipongeza Serikali ya awamu ya tano ya  Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi nzuri inayofanya ya kusimamia uchumi mpana, kuongeza makusanyo ya ndani ambayo yanasaidia upatikana fedha kwa ajili ya kugharamia uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo, kupambana na rushwa, kusimamia matumizi ya fedha za umma, na kuongeza ufanisi katika utendaji  wa kazi za umma.

Aidha, Dkt. Felipe aliishauri Serikali kuwekeza zaidi katika rasilimali watu na miundombinu  ili  kulifanya Taifa kuweza kuhimili ushindani  wa kimataifa dunia na kujenga uchumi unaokua  na  endelevu.

Vile vile aliieleza kuwa katika kipindi cha miaka  mitatu iliyopita uwekezaji kutoka nje umekuwa zaidi katika Sekta ya madini, hivyo alishauri Serikali kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuwavutia wawekezaji kutoka nje kuwekeza katika sekta za viwanda na utoaji huduma ili kuongeza wigo wa shughuli za kiuchumi na kuchochea ukuaji wake.

Kigwangalla kumshauri Rais kuunda jeshi maalumu kwa wanyamapori na misitu

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamis Kigwangalla amesema wizara ipo kwenye mchakato wa kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda Jeshi jipya litakalokuwa maalumu kwa usimamizi wa wanyamapori na rasilimali za misitu nchini ili kuboresha utendaji kazi katika sekta hiyo.

Amesema hatua hiyo inalenga kudhibiti na kusimamia sekta ya maliasili kutokana na kuingiliwa na majangili wanaosababisha rasilimali hiyo kuteketea.

"Vikosi vya majeshi vilileta ushauri huo na sasa wizara tumeona jambo hilo lina tija kweli, hivyo tupo kwenye mchakato huo na tumefikia hatua nzuri tukikamilisha tunampelekea Rais kwa kumshauri aanzishe jeshi jipya kwa ajili wanyamapori na misitu, tunaamini jambo hili litazaa matunda,” amesema.

Amefafanua kuwa jeshi litakaloundwa litakuwa chini ya Rais mwenyewe na litasaidia kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji na kujenga nidhamu kwa watumishi.

Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Misitu Tanzania,(TFS) Professa Dos Santos Silayo amesema kwa sasa wameimarisha utendaji wa wakala huo tofauti na ilivyokuwa awali wa kusimamia mapato  tu.

Amesema hatua ya kubadili wakala huo na kuwa mamlaka kamili ya misitu itaongeza ufanisi na utendaji kazi katika sekta hiyo.

"Mbali na kuweka mifumo mizuri ya udhibiti lakini tumeanza ushirikishwaji wa wananchi wanaoishi karibu na misitu ili kuweka ulinzi wa rasirimali hizo.”

Tanzania yakanusha kuminya demokrasia....Yashutumu Matamko ya Marekani na Umoja wa Ulaya

$
0
0
Serikali ya Tanzania imekanusha tuhuma kwamba inaminya demokrasia nchini humo na kusema kuwa imesikitishwa na matamko kadhaa yaliotolewa na Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) na kuungwa mkono na baadhi ya balozi za nchi za Magharibi.

Taarifa ya serikalli ya Tanzania imefuatia matamko yaliyotolewa na nchi za magharibi wiki za hivi karibuni yakielezea wasiwasi wao kutokana na matukio ya kiusalama ambayo wameeleza yanatishia utawala wa kisheria na maadili ya kidemokrasia nchini Tanzania.

Katika wiki za hivi karibuni polisi wa Tanzania wameshutumiwa kwa kutumia nguvu za kupita kiasi kushughulikia mivutano ya kisiasa na pia wanasiasa kadha wa upinzani wakiwemo wabunge mara kwa mara wameitwa polisi kwa mahojiano kutokana na madai ya kufanya mikutano isiyo halali.

Mbunge wa upinzani Joseph 'Sugu" Mbilinyi na afisa mwingine wa chama cha Chadema mjini Mbeya walihukumiwa kifungo cha miezi mitano gerezani mwishoni wa Februari baada ya kukutwa na hatia ya kumkashifu Rais John Pombe Magufulu

Taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania pia imesema kuwa tayari nchi hiyo imechukua hatua kukubaliana na vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini. Nchi za magharibi ziliishutumu Tanzania kwa kukiuka vikwazo hivyo.

Hata hivyo Tanzania imesema tuhuma kwamba imekiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya silaha za nyuklia za Korea Kaskazini na programu yao ya makombora ya balistika hazijaweza kuthibitishwa..

Taarifa hiyo imeeleza kuwa suala la utawala wa sheria na demokrasia katika tamko hilo la mabalozi linaonyesha sintofahamu iliyoko juu ya usalama na changamoto za kisiasa ambazo Tanzania imekuwa ikikabiliwa nazo kwa kipindi cha miezi 18 na kwamba matamko hayo yamekuwa sio tafsiri sahihi ya hali ya kisiasa na usalama iliyopo Tanzania.

“Ni kawaida kwa wanadiplomasia wa kigeni kufuatilia na kuripoti hali ya kisiasa na usalama inayoendelea katika nchi walizotumwa. Lakini tunashangazwa na ukimya uliowazi katika kipindi cha nyuma wa mabalozi hawa juu ya vitisho vya uvunjifu wa amani uliokuwa haujawahi kutokea na changamoto nyingine ambazo Tanzania imekuwa ikikabiliana nazo katika maeneo matatu ya Kibiti-Mkuranga –Rufiji yanayopakana,” limesema tamko hilo.

Wizara hiyo imeeleza kuwa vitisho hivyo vimewauwa watu wasio na hatia na kwa sadfa ya ajabu, wengi wa waliouwawa walikuwa kutoka chama tawala.

Mauaji hayo yalikuwa yametanguliwa na matukio kama hayo ya uvunjifu wa amani katika maeneo mbalimbali ya nchi yakiwa ya aina yake yalihusisha uvunjifu wa amani.

Kwa mujibu wa tamko hilo pamoja na kuwepo taarifa za matukio haya ya uvunjifu wa amani yalitolewa na vyombo vya habari nchini, hakukuwa hata na tamko lililolaani vitendo hivyo kutoka kwa mabalozi hao.

Wizara imehoji kuwa ni hivi sasa tu ndio EU inataja juu juu shambulizi la silaha lililotokea Mkoa wa Pwani katika kipindi cha miaka miwili.” Kuchelewa kutolewa kwa matamko hayo baada ya muda mrefu na wakati mgumu unastaajabisha.

Moja ya matamko yaliyotolewa na mabalozi wizara imesema ni jambo zuri kwa mabalozi wametambua wito wa Rais Magufuli akitaka uchunguzi ufanyike wa matukio mengine ya uvunjifu wa amani katika wimbi la operesheni ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji.

Lakini wizara imesema kuwa matamko hayo ya mabalozi hayakutambua uhusiano uliokuwepo kati ya hatua za kishujaa ambazo zimechukuliwa na Rais Magufuli kuondoa ufisadi, madawa ya kulevya, ukwepaji kodi, ujangili wa nyara za serikali na kuhakikisha uwajibikaji katika sekta binafsi na za umma, na matukio ya usalama.

“Hatua za serikali ya awamu ya nne bila shaka zimewakasirisha watu wenye nguvu ndani na nje ya nchi ambao wanamaslahi binafsi katika hali ya uzembe iliokuwa inaendelea hapo awali nchini,” taarifa hiyo imesema.

Chadema yamsimamisha kazi Mwenyekiti wa Bavicha

$
0
0
HALI si shwari ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya chama hicho kuchukua hatua ya kumsimamishwa uongozi Mwenyekiti wa Baraza la Vijana, Dickson Kibona.

Kibona alisimamishwa kazi Februari 28, mwaka huu, ikiwa zimepita siku 11 tangu kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa kiti cha ubunge Jimbo la Siha, ambalo Chadema iliangushwa na Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi huo.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Katibu wa Chadema, Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, imeeleza kuwa Kibona anasimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

Waraka huo kwa umma haujaeleza wazi kwamba Kibona anasimamishwa kazi kupisha uchunguzi gani.

Sehemu ya waraka inasema: "Ofisi ya Chadema Kanda ya Kaskazini, ambayo ni mamlaka ya nidhamu na uwajibishaji kwa viongozi wa mikoa, ilimwandikia barua Kibona ambaye ni Mratibu wa Bavicha Kilimanjaro, kwa mujibu wa ibara ya 6.5.2 ya kanuni za chama ya utaratibu wa kuchukua hatua ya kinidhamu sehemu ya kazi kuhusu tuhuma zinazomkabili kama kiongozi na kama mwanachama wa Chadema."

Kwa mujibu wa maelekezo hayo ya Golugwa ambayo yanasema kwa uzito na unyeti wake, Ofisi ya Kanda imeelekeza Kibona kusimama na kupisha uchunguzi.

Imeeleza kuwa hatua hiyo ni ya kiutawala na itatoa fursa kwa kipindi ambacho Kibona ameelekezwa kwenye barua aliyopewa kujibu tuhuma kuhusu ama aachishwe uongozi au afukuzwe uanachama kwa mujibu wa ibara ya 6.3.4 (b) na (c).
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images