Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tanzania yaridhia kufuta tozo ya Dola za Kimarekani 40 kwa wasafirishaji wa mizigo

$
0
0
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. CharleS Mwijage(Mb) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania imeridhia kufuta tozo ya Dola za Kimarekani 40 (USD40) inayotozwa kwa kila stika kwenye magari yanayosafirisha mizigo kwenda nje ya nchi. Hatua hii imefikiwa kwenye Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha

Akizungumza katika Mkutano huo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema Tanzania imefikia hatua hii ikiwa ni moja ya jitihada za kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini na Jumuiya kwa ujumla.

Tozo hii imekuwa ikitozwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa malori yanoyosafirisha mizigo kwenda sehemu mbalimbali nje ya mipaka ya nchi. B

aada ya tathimini Serikali imebaini kuwa tozo hii inasababisha usumbufu na kuongeza gharama kwa wasafirishaji wa mizigo. Hata hivyo hatua hii inaendelea kuifanya Tanzania kuwa mtekelezaji mzuri wa makubaliano na itifaki mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huu uliofanyika kwa kipindi cha siku tatu tarehe 7 hadi 9 Februari 2018, pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili na kutatua vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru (NTBs) ambavyo vimekuwepo kwa muda mrefu katika Jumuiya. Mkutano huu umefikia tamati leo katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha.

Taratibu za kuanza kufuta tozo hii zinaanza kutekelezwa mara moja.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano yaSerikali,
Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki,
9 Februari 2018

Rais Magufuli ampandisha cheo na kumteua Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Februari, 2018 amempandisha cheo na kumteua Bw. Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imefafanua kuwa Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Bw. Mohamed Hassan Haji kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP), na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar kuanzia leo tarehe 10 Februari, 2018.

Kabla ya uteuzi huu Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji alikuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi Zanzibar.

Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Hamad Omar Makame ambaye amestaafu.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Februari, 2018

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya February 11

SORRY MADAM -Sehemu ya 88 & 89 (Destination of my enemies)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

   Phidaya akageuka nyuma na kuwaona askari wawili walio valia suti wakimfwata kwa kasi kitendo kilicho mfanya kuzidi kukimbia kwa uwezo wake wote. Rahab akiwa kwa mbali akamuona Phidaya akikatiza kwa kasi, mara hajakaa sawa akawaona askari wawili wakimfwata kwa kasi wakitoka katika majengo wakielekea kwenye maegesho ya magari. Rahab akafwata kwa nyuma ili kuwazuia askari hao, huku naye akiwa katika mwendo kasi.

Phidaya katika kutizama tizama kwake kwenye maegesho ya magari, akaona gari moja likisimama kwenye maegesho ya hapo hospitalini. Kwa haraka pasipo hata kuuliza Phidaya akafungua mlango wa nyuma wa gari hilo na kuingia na kumfanya muendeshaji aliyopo humo ndani kugeuka kwa kasi na kumuangalia.
“WEWE NI NANI?”  
Muendeshaji ambaye ni mwanamke mwenzake, alimuuliza kwa sauti ya ukali huku akiwasha taa ya ndani ya gari lake kuiona sura ya Phidaya vizuri.

ENDELEA
   Macho ya Agnes yakabaki yakimshangaa mwanamke huyo ambaye leo ndio mara yake ya kwanza kumuona. Kabla hajazumgumza kitu Agnes akashuhudia wanaume wawili mbele ya gari lake wakipokea kipigo kwa msichana ambaye anamfahamu fika. Wanaume hao wanao onekana kuwa ni walinzi wa kiongozi wa nchi, walijikuta makonde yao hayafui dafu mbele ya makonde ya Rahab anaye shusha kipigo kikali juu yao.

“Rahab”
Agnes alizungumza huku akiwasha taa za mbele za gari yake kushuhudia jinsi kifinyo hicho kinavyo tembea kwa wanaume hao. Ndani ya dakika tano wanaume hao wakawa wamevunjwa vujnwa viongo na Rahab aliye simama kwa kijiamini mbele ya gari la Agnes. Kwa haraka Agnes akashuka kwenye gari hukku akiwa na tabasamu usoni mwake.
“Rahab”
Agnes aliita huku akianza kumfwata Rahab sehemu aliyo simama, kabla hajamfikia walinzi wengine watatu wenye mitutu ya bunduki wakanza kuzifnyatua risasi zao sehemu alipo simama Rahab, ambaye hakuwa mzembe kwa kiasi hicho kwani hata kabla risasi hizo hazijamfikia akaanza kuruka sarakasi kuelekea naapo tokea Agnes ambaye kwa haraka akarudi kwenye gari na kujitosa kama alivyo ingia Phidaya.

Kwa haraka Rahab akaingia kwenye gari la Agnes.
“Go go goo”(Nenda ndenda nendaaa)
Rahab alizungumza kwa sauti ya juu na kumfanya Agnes kuwasha gari lake kwa haraka, akalirudisha nyuma kwa mwnedo wa kasi, akakata kona moja kali, alipo hakikisha amelilenga geti la kutokea, hakufanya kosa zaidi ya kukanyaga mafuta na kuondoka eneo la hospitali na kuwaacha walinzi hao wakifyatua fyatua risasi pasipo mafanikio yoyote. Mlinzi mmoja akarudi sehemu walipo acha magari yao akaingia kwenye gari moja na kuliendesha kwa kasi hadi sehemu walipo simama wezake, wakaingia ndnai ya gari na kuanza kuwafukuzia Phidaya na wezake.
                                                                                                                  ***
 Milio ya risasi inayo endelea nje ikawafanya watu kadhaa ndani ya hospitali waliyo isikia kuchanganyikiwa, mtu aliye toka katika chumba cha wagonjwa mahututi, akamfanya Shamsa kumtazama kwa muda, huku akiwa amemkazia macho.
“Huyu si Manka aliye mchukua Eddy”
Shamsa alizungumza huku akianza kupiga hatua za haraka kuelekea katika mlango alio simama Manka pamoja na walinzi wa wawili wa mzee Godwin.
“Huruhusiwi kuingia hapa binyti”

Mlinzi mmoja alizungumza huku akimzuia Shamsa kwa mkono, Manka akamta jicho la dharua Shamsa, kisha akaendeleak usikilizia milio hiyo ya bunduki ni wapi inapo tokea. Kwa kasi ya ajabu Shamsa mguu wake mmoja akaukanyaga kwenye paja la mlinzi huyo, akajirusha kwajuu na kumkalia mabegani, bila hata ya huruma akamvuja shingo na kuanguka naye chini na kumfanya Manka na mlinzi aliye baki kubaki wameduwaa. Mlinzi akataka kuchomoa bastola yake, ila tayari amesha chelewa kwani Shamsa alisha mfikia na kumpiga mtama ulio muangusha chini, hata kabla hajajinyanyua tayari shingo yake ilisha vunjwa.
Shamsa akanyanyuka huku akimkazia macho Manka aliye anza kurudi nyuma na kuingia chumbani huku Shamsa akimfwata kwa mbele.

Shamsa alipo muona Eddy akiwa amelala kwenye kitanda akabaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa, jambo lililo kuwa ni kosa kubwa sana kwake kwa maana Manka, alimshushia teka zito la tumbo lililo muangusha chini. Maumivu ya tumbo aliyo yapata Shamsa yakamfanya ajinyanyua chini taratibu huku akimtazama Manka aliye jiweka tayari kwa mashambulizi.
Sa Yoo na madam Merry wakakutana kwneye kordo inayo elekea kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi. Wakashuhudia walinzi wawili wakiwa wamelala chini ya sakafu nje ya chumba kimoja. Kwa haraka wakaanza kukimbia hadi kwenye mlango wa chumba hicho na kumshuhudia Shamsa anavyo pokea kichapo kutoka kwa Manka. Wote wawili wakaingia ndani na kuanza kumshambulia Manka, kila mmoja aliweza kumshambulia jinsi alivyo weza, aliye rusha kofi sawa, aliye vua kiatu na kumtandika sawa, ilimradi walihitaji kumuokoa Eddy aliye muona amelala kitandani.

“Mchukueni Eddy muondoke naye mimi ninamshuhulikia huyu”
Shamsa alizungumza huku akinyanyuka, Madam Merya na Sa Yoo hawakupoteza muda baada ya kumuona Manka amelala chini akiwa yupo hoi taabani. Kutokana kitanda alicho lalia Eddy kina matairi, walicho kifanya ni kuchomoa waya wa umeme wa mashinye ya kuhesabu mapigo ya moyo iliyopo pembeni ya kitanda hicho, na kuanza kukisukuma kutoka nje.
“Tupite njia hii”
Madam Mery alizungumza, Sa Yoo akatii wakaanza kukisukuma kitanda hicho hadi nje kwenye maegesho ya magari cha kushukuru Mungu hapakuwa na mtu hata mmoja, kutokana milio ya risasi hiyo ilisikika katika eneo hilo na raisi wote walikimbia japo ni usiku.

“Kwenye gari hili hawezi kuingia”
“Itakuwaje sasa?”
Sa Yoo akaitazama gari la wagonjwa lililopo kwenye maegesho hayo kwa haraka akalikimbilia, akajaribu kufungua mlango wa upende wa dereva kwa habati nzuri akaukuta upo wazi, kwnai ni muda mchache gari hilo limeleta mgonjwa hapo hospitalini, kingine cha kumshukuru Mungu hata dereva aliweza kusahau fungua kwneye mskani wa gari hilo. Kwa haraka Sa Yoo akaingia na kuliwasha gari hilo akalirudisha taratibu hadi sehemu kilipo kitanda, akshuka kwa haraka, akazunguka nyuma wakasaidiana na Madan Mery kumuingia Eddya kaiwa na kitanda chake kisha madam Mery akaingia nyuma na kufunga mlango na Sa Yoo akarudi mbele, akakanyaga mafuta na kuondoka eneo hilop la hospitali.

TANGA RAHA- Sehemu ya Kwanza (1)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
Ni siku ya utambulisho mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari moja jijini Tanga nikiwa mimi na mwalimu mwenzangu ambaye wa kike ambaye ndio tumetoka chuo cha ualimu na kupangiwa shuleni hapa
Akaanza mwenzangu kujitambulisha ambaye, akapigiwa makofi na wanafunzi kisha nikafwatia mimi kujitambulisha

"Mimi ninaaitwa Sir Eddy nitafundisha Biology na Chemisty"
Wanafunzi wote wakapiga makofi ma vigelegele hukt wakionekana kupendezwa na utambulisho wangu mfupi na wakueleweka.Muda wa masomo nikakabithiwa kuanza na kidato cha nne katika somo la Biology ambao ndio nao wanaanza mwezi wa kwanza wa muhula wa masomo.Nikaanza kuuliza mwanafunzi mmoja mmoja jina lake ili kuniwia rahisi kuwafundisha na kuwazoea kwa haraka
Nikaanza kipindi huku nikiwauliza uliza maswali ya mada walizo zisoma wakiwa kidato cha tabu, ili niweze kwenda nao sawia kwenye kufundishana
"Ulisema unaitwa nani, binti?"
"Rahma"
"Ehee elezea Reproduction(uzalishaji) kwa mwanadamu inakuwa vipi?"
Akanza kuelezea hatua moja baada ya nyingine kuanzia mtoto anavyo tafutwa hadi kuzaliwa bila hata kukosea.Wanafunzi wenzake wakampigia makofi huku wengine wakitaka kutokana na baadhi ya vitu alivyokuwa akivizungumza
Wakanipa ushirikiano mzuri hadi nikamaliza kipindi na kurudi zangu, ofisini nikisubiri kwenda darasa jengine
Muda wa kutoka ukawadia nikabeba begi langu lenye laptop yangu niliyo hifadhi vitu vyangu mbalimbali
"Sir ninaweza kukusaidia kubeba begi?"
"Rahma ndio unaweza kunisaidia"
Rahma yupo na mwenzake ambaye sikumuona darasani wakati nilipokuwa ninafundisha somo langu
"Unakalia wapi?"
"Maeneo sijui wanapaita Chuda, kitu kama hicho"
"Sir Eddy kwani Tanga wewe ni mgeni?"
"Nimgeni nina kama siku ya nne leo, tangu nije bado majina yana nisumbua sumbua kuyashika"

"Umetokea wapi?"
"Arusha"
Tukatembea njia nzima huku tukizungumza mambo mengi, kuhusiana na mji huu ambao nyumba zake zimepangika vizuri kwa mpangilio wa mistari mistari, nitofauti sana na mji kama Dar es Salaam.Tukafika nyumbani kwangu na nikawakaribisha na sote tukaingia ndani kuingia ndani
"Ehe sir Eddy umejitahidi?"
Rahma ni muongeaji sana kiasi kwamba hakuwa anampa mwenzake nafasi, ya kuzungumza na mimi japo hata kuchangia mada ya jambo tunalo lizungumzia
"Nimejitahidi vipi?"
"Chumba chako ni kizuri"
"Asante"
"Sir acha sisi twende tutakuja kukutembelea jumamosi"
"Sawa karibuni"
Wakaondoka na kuniacha nikiendele na shughuli zangu za kawaida, ikiwemo kupika chakula cha mchana, nilicho kijumlisha na chakula cha usiku.Nikaendelea kufanya kazi kwa juhudi siku zote za kazi yangu, huku upendo wangu wa kuipenda kazi yangu ukizidi kuongezeka kadri ya siku zilivyozidi kukatika

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 12

NEC: Maandalizi Ya Uchaguzi Yanakwenda Vizuri

$
0
0
Zikiwa zimebaki siku 6 kabla ya Uchaguzi Mdogo wa Majimbo ya Siha, Kinondoni na Kata 8 kufanyika, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi huo yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na ufumbuzi wa changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi RAMADHANI KAILIMA amesema mara baada ya mkutano wa Watendaji wa Tuma na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni Bwana Aron Kagurumujuri.

Bwana Kailima amesema Tume inafuatilia kwa karibu maandalizi ya Uchaguzi Mdogo yanayoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuwa ni wajibu wake na kwamba Maafisa wa Tume wako maeneo mbalimbali yanayojiandaa kwa Uchaguzi huo Mdogo utakaofanyika jumamosi Februari 17, Mwaka huu.

‘Tumekuja kukutana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ili kupata taarifa juu ya maendeleo ya Maandalizi. Tumekuja hapa kwa sababu hapa ni rahisi kufika’ amesema Bwana Kailima na kuongeza kuwa maafisa wa Tume wapo katika maeneo mbalimbali yanayofanya Uchaguzi kwa kuwa Tume ina wajibu wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Uchaguzi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi Tume imejiridhisha kuwa maandalizi yanayoendelea  vizuri na amepongeza jitihada zinazofanywa na Msimamizi wa Uchaguzi pamoja na Wasaidizi wake katika kuhakikisha kuwa changamoto zozote zinazojitokeza zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Aidha amewashauri Wasimamizi wa Uchaguzi kuendelea kukutana na Wawakilishi wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya kutoa taarifa katika kila hatua ya kuelekea Uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha kuwa Vyama vinapata taarifa ya kila hatua ya maandalizi ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya mchakato mzima wa Uchaguzi.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi amesema Tume imejipanga kuanza kutoa vipindi vya Elimu ya Mpiga Kura mfululizo hadi siku ya Uchaguzi, Elimu itakayohusu mada mbalimbali za Uchaguzi zikiwemo Haki na Wajibu wa Mpiga Kura, Wakala wa Vyama vya Siasa na Msimamizi wa Uchaguzi pamoja na taratibu zote za Upigaji Kura.

‘Nawasihi sana watu watembelee Online ya Tume Tv, website ya Tume, kwa jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, facebook na instagram lakini pia App ya Tume, kwa hiyo tumeanza Elimu ya namna hiyo kama eneo la kuelimisha Umma kuelekea tarehe 17 siku ya Kupiga Kura’ amesema Bwana Kailima.

Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo ya Kinondoni mkoani Dar es salaam, Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro na Udiwani katika Kata 8 za Tanzania Bara, unatarajiwa kufanyika Siku ya Jumamosi Februari 17, Mwaka 2018.

Watanzania Waaswa Kuwa Wazalendo Wa Kweli Zoezi La Uandikishaji Vitambulisho Vya Taifa Unaoendelea Nchini

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dr. Mwiguli Lameck Nchemba awewataka watanzania kuwa wazalendo wa kweli kwenye Usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaoendelea kwenye mikoa 19 ya Tanzania kwa kuwafichua wale wote wanaojipenyeza kutaka kusajiliwa kama Raia.

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizindua shughuli za Usajili na Utambuzi wa Watu katika Mkoa wa Morogoro Jumamosi katika viwanja vya Shujaa mkoani humo na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu Andrew Massawe akisoma taarifa ya zoezi la Usajili na Utambuzi  wa Watu kwa mikoa 19 inayoendelea na Usajili; alisema mkoa wa Morogoro unakusudiwa kusajili zaidi ya wananchi 960,000 wenye umri wa miaka 18  na kuendelea. Zoezi ambalo limepangwa kukamilika kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili,2018.

“ Mkoa wa Morogoro zoezi litahusisha Wilaya zote isipokuwa Kilombero ambayo ilikuwa Wilaya ya kwanza ya mfano kufanyiwa usajili mwaka 2012 na hivyo idadi kubwa ya wananchi wake tayari wana Vitambulisho vya Taifa na kwasasa wanaosajiliwa ni wale wanaotimiza umri wa miaka 18 na wanaohamia “ alisisitiza

Aidha ndugu Massawe amlimweleza Mhe. Waziri mbali na Usajili Mamlaka kwa kushirikiana na wadau wengine imeanza matumizi ya Vitambulisho vya Taifa ikiwemo Usajili wa Makampuni unaofanywa na Brella ambao kwa sasa unataka kila anayesajili Kampuni kuwa na Kitambulisho cha Taifa. Huduma nyingine ambazo kwa sasa huwezi kuzipata bila kuwa na Kitambulisho cha Taifa ni upatikanaji wa Hati za kusafiria(Passport), Usajili wa namba za simu na huduma nyingine za kifedha n.k

Katika hotuba yake Mhe. Waziri alikemea vikali tabia ya baadhi ya watendaji na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji kudai posho au kuhusisha michango na tozo mbalimbali wakati wa kuwasajili wananchi wakati zoezi hilo ni bure. 

Alisisitiza Mamlaka  zote za Serikali kuhakikisha zinasisimia na kutoa ushirikiano kwa NIDA kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa kwa wakati wakiwemo Wageni na Wakimbizi kwani shughuli ya usajili kwa sasa inahusisha makundi yote.  Pindi wakati utakapofika kwa wale wote ambao watakuwa hawakusajiliwa watakuwa na cha kujieleza kwanini hawakusajiliwa Vitambulisho vya Taifa wakati Serikali imewekeza fedha nyingi kukamilisha zoezi hili.

Alisisitiza Usajili Vitambulisho vya Taifa si hiyari ni wajibu wa kila Raia, Mgeni na Mkimbizi kusajiliwa kwa kufuata taratibu, sharia na kanuni za Usajili zinazosimamiwa wakati wa utekelezaji wa Usajili.

“ Kama mnavyofahamu Serikali ya Awamu ya Tano chini Mhe. Dr. John Pombe Magufuli ina vipaumbele vingi na mahitaji kwa wananchi ni mengi. Sasa Rais ameacha mambo mengine akaamua kuwekeza kwenye Vitambulisho vya Taifa mradi unaoigharimu Serikali fedha nyingi sana; sasa ole wao ambao hawatasajiliwa kwa visingizio visivyokuwa na msingi” alisisitiza

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dr. Kebwe Steven Kebwe aliwataka wananchi wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kwenye Usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaoendelea maeneo mbalimbali ya mkoa huo na kusisitiza hatowafumbia macho wale wote watakao husisha zoezi hilo na itikadi za vyama au dini, au kudai rushwa kuwahudumia wananchi pindi wanapojitokeza kwenye vituo vya kusajiliwa.

Zoezi la Usajili wanachi Vitambulisho vya Taifa linakusudiwa kumalizika mwezi Desemba mwaka huu kwa wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kuwa wamesajiliwa na kupata namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) wakati hatua za Uzalishaji zikiendelea sambamba na kuvigawa kwa wananchi.

TRA Yakamata Bidhaa Mbalimbali Zikitokea Nchini Kenya.....Kuna Mirungi, Vifaranga 5000, Mayai Kasha 416

$
0
0
Na: Veronica Kazimoto,Arusha
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata na kutaifisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na tani moja ya sukari na chumvi, majani ya chai mifuko 18, mirungi kilogramu 16, vifaranga vya kuku 5000 na mayai kasha 416 katika mpaka wa Namanga mkoani Arusha zikitokea nchini Kenya kupitia njia zisizo rasmi.

Akizungumza mara baada ya kukamata bidhaa hizo, Meneja Msaidizi wa Forodha mkoani hapo Edwin Iwato alisema bidhaa hizo ni mali ya Joseph Sekino, Innocent Minja na Andrew Lyimo wote wakiwa ni wafanyabiashara kutokea Tanzania na watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

“Tumewakamata wafanyabiashara watatu ambao ni Joseph Sekino akiwa amepakia tani moja ya sukari na chumvi na majani ya chai mifuko 18 kwenye gari Na. T 785 AWV, Innocent  Minja akiwa na mayai kasha 416 na mirungi kilo 16 kwenye gari Na. T 443 CQU na Andrew Lymo akiwa na vifaranga vya kuku 5000 kwenye gari Na. T 441 DHW wote wakitokea nchini Kenya kuja mkoani Arusha,” alisema Iwato.

Iwato alieleza  kwamba, wafanyabiashara hao waliingiza baadhi ya bidhaa hizo kwa kutumia vifungashio vya bidhaa nyingine za nchini Tanzania ili kuficha uhalisia wake huku wakiwa hawana vibali wala kulipa ushuru wa Serikali kama inavyotakiwa.

Alifafanua kuwa, mirungi ilikamatwa ndani ya mifuko ya plastiki maarufu kama Rambo ikiwa imefichwa kwenye boneti ya mbele ya gari aina Noah Na. T 443 CQU sehemu ya injini.

Naye, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Richard Kayombo alisema, tabia ya wafanyabiashara hao siyo tu inawahujumu wafanyabiashara wenzao bali inakwamisha azma ya Serikali ya kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo ya kila mwananchi.

“Tabia ya wafanyabiashara hawa siyo nzuri kwa kuwa inakwamisha ukusanyaji mapato ya Serikali na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ili iwe fundisho kwa wengine wanaofikiria kufanya biashara pasipo kutumia njia rasmi na kulipa ushuru ipasavyo”, alisema Kayombo.

Aidha, Kayombo aliongeza kuwa, bidhaa zote haramu zilizokamatwa zitateketezwa kwa mujibu wa Sheria, zile zinazofaa kwa matumizi ya binadamu zitagawiwa kwa taasisi mbalimbali za Serikali zenye uhitaji kwa mujibu na taratibu zilizowekwa na TRA na magari yote yaliyotumika kusafirisha bidhaa hizo yametaifishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Utaifishaji wa magari na bidhaa ambao usafirishaji wake haufuati sheria na taratibu, unalenga kukomesha shughuli za magendo nchini ambazo kwa kiasi kikubwa zinakwamisha juhudi za Serikali katika ukusanyaji wa mapato.

Salum Mwalimu apangua tuhuma za Uzanzibar

$
0
0
Mgombea Ubunge  wa jimbo la Kinondoni (CHADEMA), Salum Mwalimu asesema kwamba hoja ya Uzanzibar inayokuzwa na wapinzani wake kwenye siasa hasa kipindi hiki cha uchaguzi si jambo jema na haifai kuingia kwenye mjadala kwani inaweza kulipasua Taifa.

Akizungumza  kuhuhusu tuhuma za U-zanzibar dhidi yake, amesema kwamba anajua kwamba wakati wa vita zinatumika silaha mbalimbali lakini ni vema kwenye hili la la kuleta Utanganyika na U-zanzibar likatumiwa kwa tahadhari ili lisije kuleta madhara.

Akiweka wazi utambulisho wake wa Uzaa, ndg Mwalimu amesema kwamba hajawahi kuuficha utambulisho wake wa kwamba yeye ni ni mzaliwa wa Zanzibar na wala haoni kama ni jambo la ajabu.

"Sifa kubwa ya kuwa mgombea wa ubunge ni uwe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hapo ikimaanisha Tanganyika na Zanzibar. Sasa kama chokochoko hizo zimeanza basi watuambie kwamba Zanzibar nchi yenu hii hapa na Tanganyika tuione ili wazanzibar wawe wanagombea Zanzibar na Watanganyika wagombee bara. Mimi ni Mzanzibar na wala hilo siyo jambo la ajabu" Mwalimu

Hata hivyo Ndg. Mwalimu ameshangazwa na hoja hii kunyooshewa vidole kwake na kuhoji au huenda yeye siyo mtoto wa Kigogo wa Serikali au CCM ndiyo maana imeelekezwa kwake na kusema mbona wapo viongozi kibao kama Waziri Mwinyi na wengineo waliwahi kuwa viongozi bara huku wakiwa na asili ya Zanzibar na wengine wenye asili ya Tanganyika wakiwa viongozi huko Zanzibar.

Makamu wa Rais atoa neno kuhusu kupunguza foleni Hospitalini

$
0
0
Makamu wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  amesema Serikali inajitahidi kujenga na kutanua vituo vya Afya ikiwa na lengo la kupunguza msongamano kwenye hospitali za Wilaya.

Makamu wa Rais ameyasema hayo  jana  wakati wa kuweka jiwe la msingi  la upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole kilichopo mjini Mafinga.

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Iringa ambapo jana  alitembele wilaya ya Mufindi na kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ikiwa mmoja ni wa kujenga maabara ya kisasa na madarasa na kidato cha tano na cha sita katika Sekondari ya Mgololo na upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.

Akiwahutubia wananchi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi  la Upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole , Makamu wa Rais alisema katika kila kituo cha afya kinachopanuliwa ama kujengwa Serikali imezingatia  huduma za mama na mtoto ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto, kuborsha huduma za upasuaji .

Serikali imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho na kutumia mafundi wa kawaida kujenga ilikuweza kusaidia kutoa ajira kwa vijana zaidi wa eneo husika.

Makamu wa Rais amezitaka halmashauri zisimamie utoaji na matumizi ya fedha wanazotoa kwa Vijana asilimia 5 na Wanawake asilimia 5 ili kuleta tija kwenye shughuli za maendeleo.

Makamu wa Rais alisema  “tunapozungumzia uchumi wa viwanda lazima tuwaandae Vijana tangia wadogo, tuhakikishe wanafundishwa  yale yanayohitajika”.

Makamu wa Rais aliwaambia wakazi wa Mafinga, watakapokuja tena kwenye kampeni watawataka wananchi waseme Serikali yao imewafanyia nini.

Mapema jana  Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na madarasa  ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Mgololo, ujenzi ambao utagharimu  shilingi milioni  450 za kitanzania chini ya ufadhili wa kiwanda cha Mufindi Paper Mills.

Atiwa Mbaroni kwa Kumlawiti Mtoto wa Kiume Mwenye Umri wa Miaka Minne

$
0
0
Na Masanja Mabula -Pemba 
BAKAR Khamis (25) mkaazi wa Mitondooni Wilaya ya Wete, anadaiwa kumnajisi (kumlawiti) mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne huko Shehia ya Piki Wilaya hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baba mzazi wa mtoto huyo alisema   mtuhumiwa alimchukuwa mwanawe hadi Bahanasa na kuingia kwenye gari ya abiri na kumpeleka bonde la Hindi na kumfanyia ulawiti.

Alisema   mtuhumiwa ni mgeni katika shehia hiyo, alikwenda kwa kutembea, ingawa alichokifanya ni kumchukua mtoto wake na kwenda kufanyia kitendo cha ulawiti, jambo ambalo linamtia huzuni kila anapofikiria.

“Huyo mtuhumiwa ni mgeni hapa kijijini kwetu, alipoona tu washamzoea watoto ndipo alipoamua kumchukua mwanangu kwenda kumlawiti na huko kwao tumesikia kaondoshwa kwa kuwafanyia watoto kitendo hicho”, alisema baba huyo.

Kwa upande wake mama wa mtoto, alisema  aliondoka na kwenda mazikoni, ambapo mara baada ya kufika alipigiwa simu na kuambiwa kuwa mwanae amemfuata na ndipo alipofanya haraka ya kurudi, ingawa alipofika hakumkuta.

“Alimpelea katika bonde la Tangoni – Hindi na wakati anamlawiti wakatokea watoto wanaochuma mabungo na mtuhumiwa akakimbia, ndipo walipomuuliza anapoishi na kusema na wakamleta nyumbani”, alisema mama huyo.

Alieleza mara baada ya kufika mtoto wao walimuhoji na kusema kuwa kaka Bakar, alimchukua na kwenda kumfanyia kitendo cha ulawiti na kisha kumpa maandazi, ambapo aliporudi alikuwa nayo kwenye mfuko.

“Walikuja wazazi wa upande wa mtuhumiwa tufanye suluhu ili tusiifikishe kesi Polisi, lakini kwa kitendo alichofanyiwa mwanangu siwezi kusamehe, kwani huu ni ukatili”, alisema mama huyo.

“Huyu mtoto ana kawaidi ya kucheza na mwanangu, sasa alikuja mwanangu na kilio na kuniambia kaka ananikimbia, nikatoka nje nikamwita lakini na mtuhumiwa ikawa anamwita, sasa ikawa kama tunavutiana, ingawa sikuwa na wasiwasi nae nikaona labda anamfuata tu kwa vile washamzoea”, alisema jirani wa mtoto huyo.

Nae, kijana mmoja anaeishi mtaa huo, alisema alimshuhudia mtuhumiwa akiingia kwenye gari na mtoto huyo maeneo ya Bahanasa na kuteremka Mzambarauni majira ya saa 3:00, ingawa hakujua alikompeleka kutokana na yeye alikuwa anaenda Wete.

“Mimi sikufanya wasiwasi maana nilijua ni mdogo wake wa maduguni, kwa hiyo niliporudi ndio nikapata taarifa hiyo na ndipo nilipokumbuka wakati nilipomuona anapanda nae gari”, alisema kaka huyo.

Mratibu wa shehia ya Piki, Bikombo Shazil Makame, alisema tukio hilo limetokea katika shehia yake na tayari wameshalifikisha kituo cha  Polisi  Wete, ambapo aliwataka wazazi kuwa mstari wa mbele kwenda kutoa ushahidi mahakamani, ili kesi iweze kupata hatia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji, alisema tukio hilo lilitokea Januari 2 mwaka huu saa 6:00 mchana huko Piki, mtuhumiwa huyo alimnajisi mtoto wa kiume mwenye miaka minne shehia ya Piki Wilaya ya Wete.

Kamanda huyo, alisema mtuhumiwa huyo ameshakamatwa na Jeshi hilo linaendelea na upelelezi, ambapo watampeleka mahakamni mara baada ya uchunguzi kukamilika kujibu tuhuma zinazomkabili.

Matukio ya udhalilishaji kwa watoto ikiwemo ulawiti yamekuwa yakiongezeka kila siku, kutokana na sababu mbali mbali, ikiwemo wanajamii kukataa kutoa ushahidi pamoja na kesi kukaa muda mrefu mahakamani bila ya kupatiwa hukumu.

Chadema yamlalamikia msimamizi wa uchaguzi Kwa kutaka Kuwajumu

$
0
0
Chadema imemlalamikia msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni ikidai anaashiria kuharibu uchaguzi wa Februari 17,2018.

Chama hicho kimedai kutowapa viapo mawakala juzi Februari 10,2018 kunaashiria njama za kutaka wasishiriki shughuli za upigaji na kuhesabu kura.

Viongozi wa Chadema wamesema hayo jana Februari 11,2018 walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi  mdogo katika jimbo hilo na la Siha pamoja na kata tisa.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema sheria inataka mawakala wa upigaji kura kula kiapo cha kutunza siri siku saba kabla ya kupiga kura na wanapaswa kupewa kiapo hicho.

"Anayeapisha ndiye anayesaini, hawezi kuapa mbele ya mtu mmoja na kusaini mwingine, kwa kila mwapishaji katika kila kata anakuwa na sababu zake, msimamizi wa uchaguzi anatumika," alidai Kigaila.

Kigaila alisema, "Kinachoendelea Kinondoni ni tofauti na Siha, kule Siha wameapa jana na kila wakala ameondoka na kiapo chake, sasa sijui sheria inayotumika Siha ni tofauti na inayotumika Kinondoni. "

Meneja kampeni wa Chadema Kinondoni, Saed Kubenea alisema kila linalopangwa kutaka kuuharibu uchaguzi huo hawatalikubali.

Lowassa Awapongeza Maaskofu Akimnadi Mgombea wa CHADEMA

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa amewapongeza maaskofu kwa kuunga mkono mambo aliyosema wamekuwa wakiyapigania.

Lowassa ametoa pongezi hizo  jana Februari 11,2018 akimnadi mgombea ubunge jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu katika Kata ya Kijitonyama.

“Leo kwenye magazeti wameandika kwamba Baraza la Maaskofu wamezungumzia mambo ambayo tumekuwa tunayasema kila siku, kuhusu kuzuia uhuru wa kuzungumza na suala la maadili. Ninawashukuru sana maaskofu, ninawapongeza sana kwa kuunga mkono ambayo tumekuwa tunayasema,” alisema Lowassa.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limetoa ujumbe wa Kwaresima wa mwaka 2018 ndani yake likitoa msimamo kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini.

Lowassa akimnadi Mwalimu alisema anamfahamu kwamba ni kijana shupavu na mchapa kazi ambaye akipewa kura wananchi wa Kinondoni watapata maendeleo.

“Kinondoni msilale mpaka kieleweke. Mchagueni Salum Mwalimu akawaletee maendeleo,” alisema.

Mwalimu akiomba kura alisema Kinondoni ni watu ambao wanajitambua.

“Kinondoni ni watu mnaojitambua, ni watu ambao mlijitoa mwaka 2015, wengine waliachika. Ninawapenda sana, ninajua nina deni kubwa la kuwalipa,” alisema.

Mwalimu alisema, “Ninapozungumza najua ninazungumza na wajanja ambao hawadanganyiki. Tangu juzi, wenzangu wameleta fedha hapa Kijitonyama kwa ajili ya kununua shahada.”

Alisema waliposikia anagombea ubunge walipata hofu kubwa, vikao vikawa haviishi wakitafakari itakuwaje nikienda bungeni.

Wabunge, Mawaziri Waungana Kumuombea Kura Maulid Mtulia Kinondoni

$
0
0
 Wabunge na mawaziri kutoka CCM wamejitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni kumnadi mgombea ubunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia.

Waliohudhuria mkutano huo uliofanyika jana  Februari 11,2018 katika mtaa wa Idrisa, Magomeni ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson; Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako; na Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile.

Wabunge waliohudhuria ni Hussein Bashe wa Nzega Mjini, Azzan Zungu (Ilala), Livingstone Lusinde 'Kibajaji’ (Mtera), Halima Bulembo (Viti Maalumu) na Oliver Semuguruka (Viti Maalumu).

Wengine ni Sixtus Mapumba (Mbinga Mjini), Steven Ngonyani 'Profesa Majimarefu' (Korogwe), Joseph Musukuma (Geita Vijijini) na Rita Kabati (Viti Maalumu).

Kabla ya viongozi hao kupanda jukwaani, burudani ilitolewa na vikundi vya ushereheshaji huku waliohudhuria mkutano huo wakisimama kucheza na kuwatuza waliokuwa wakiburudisha.

Halima lisema mwanzoni Mtulia alikuwa mbunge wa upinzani na katika baraza la madiwani hakuweza kushauriana na meya lakini sasa yuko CCM hivyo kuwaomba wananchi wamchague.

Mapunda alisema wananchi wa  Kinondoni hawakuwa na tatizo na mchezaji bali timu anayochezea.

“Mchezaji mzuri akitoa pasi inaharibika na ndiyo maana Mtulia ni mchezaji mzuri na sasa amekuja timu bora ya CCM mleteni tumalize mchezo mapema,” alisema.

Mbunge Zungu alisema wabunge wa CCM hawana ujanja bali ni ilani ambayo imejenga kuwajali wananchi.

Dk Ndugulile ambaye pia ni mbunge wa Kigamboni alisema, “Mtulia nitampa ushirikiano katika kutatua matatizo ya afya, wazee na maendeleo ya jamii yatapatiwa ufumbuzi kwa kumchagua Mtulia.”


Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Tamko La Maaskofu Katoliki Kuhusiana na Hali ya Kisiasa, Kiuchumii na Kijamii Hapa Nchini

$
0
0
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa ujumbe wa Kwaresma wa mwaka 2018 ndani yake likitoa msimamo kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini.

Ujumbe huo ulioandikwa na maaskofu wote 36 wa TEC wakiongozwa na Rais wake, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa upo katika kitabu cha kurasa 20 ikiwa ni maandalizi ya ibada hiyo ya siku 40, kipindi ambacho ni cha mfungo wa sala kukumbuka siku 40 za Kristo kufunga na kwenda jangwani.

Hali ya kisiasa
Katika ujumbe huo, TEC imesema uamuzi wa Serikali kuzuia maandamano, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni kwenda kinyume cha Katiba ya nchi.

Baraza hilo pia limeonya hatua ya Serikali kuvibana vyombo vya habari ikiwa pamoja na kuvifungia kwa sababu mbalimbali.

“Kufungiwa huku kwa vyombo vya habari kumeenda sambamba na kuminya uhuru wa Mahakama na Bunge kwa njia ya kuminya haki wabunge na kutowapa nafasi ya mikutano ya hadhara kama haki yao ya msingi ya kikatiba.”

“Kikatiba, nchi yetu inafuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katiba na sheria mbalimbali zimeainisha utaratibu wa kazi na shughuli za vyama vya siasa. Ili kuhakikisha kwamba shughuli za vyama vya siasa zinakuwa endelevu, vyama vyenye kukidhi vigezo hupewa ruzuku kupitia bajeti ya Serikali inayopitishwa na Bunge,” unaeleza ujumbe huo.

“Hata hivyo, shughuli za, siasa bado zinaendelea kuzuiwa kwa kutumia vyombo vya dola. Maana yake ni kwamba shughuli za kiuenezi za vyama vya siasa, kama vile mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na hata mikutano ya ndani, ambayo ni haki ya kila raia, zimekoma mpaka uchaguzi mwingine. Kisheria, huu ni uvunjifu wa Katiba na sheria za nchi.”

Kuhusu vyombo vya habari, TEC imesema Serikali imepunguza wigo wa uhuru wa wananchi wa kupata habari na maoni ya kujieleza na kueleza kwamba kwa ujumla wake, mazingira hayo yatasababisha jamii kufarakana na hata kujenga chuki.

“Kumekuwapo pia hali ya vurugu katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi hizi zinaacha nyuma uchungu, hasira, tamaa ya kulipa kisasi na hata kususia chaguzi nyingine,” unasema ujumbe huo wa TEC na kuonya kuwa kama hali hiyo itaachwa, itakuja kusababisha mifarakano mikubwa itakayobomoa amani na umoja wa kitaifa.

Kuhusu uchumi, TEC imetoa mambo sita ya kujiuliza; “Tunazitumiaje mali na rasilimali nyingine tulizokabidhiwa na Mungu kama mawakili wake? Tunalipa kodi stahiki kwa ajili ya kugharamia huduma za jamii ambazo Serikali inapaswa kutoa kwa ajili ya wananchi?”

“Wale ambao tu waajiri, tunawajali wafanyakazi na wahudumu wetu kwa kuwalipa mishahara ya halali? Wale ambao tu wafanya biashara, tunalipa kodi zote kihalali?”

“Wale ambao tumepewa jukumu la kukusanya kodi, ushuru na ada nyingine kama tunafanya hivyo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu husika? Tunaepukaje na kishawishi cha rushwa, hongo, mulungula, magendo au aina yoyote ya ufisadi?”

Katika eneo la kijamii TEC imesema bado kuna kishawishi cha kupingana na azma ya kuboresha maisha ya kijamii.

“Hii inajidhihirisha kwa njia ya uhasama, ugomvi, ukatili kwa watoto na wanawake, ujambazi, na maovu mengine kama hayo miongoni mwa jamii yetu. Kama wamisionari tunaopaswa kuleta habari njema kwa ndugu zetu, kwa nini turuhusu roho ya namna hii ambayo kwa kweli ni roho ya Kaini inayouliza kwa jeuri kabisa,” unasema ujumbe huo.

Katika ujumbe wake, Baraza hilo limesema, “Kwa mwaka huu wa 2018 kipindi hiki ni cha kujitafakari mbele ya Mungu na kufanya toba hususan uhai wa amani yetu kwa njia ya matendo ya huruma, haki upendo na amani kwa jirani zetu.”

Limesema hiki ni kipindi chenye upekee wa aina yake kwake sababu ya mambo matatu;

“Ni katika mwaka huu ambapo Kanisa Katoliki Tanzania linaadhimisha na kusherehekea miaka 150 ya Ukatoliki Tanzania Bara, na kilele chake kitakuwa tarehe 2 Oktoba.

Mwaka huu pia utakuwa ni mwaka wa 50 tangu Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania watoe tamko rasmi kuhusu mwelekeo na hatima ya nchi yetu na Mwaka huu ni mwaka wa maandalizi ya utekelezaji wa haki ya msingi ya kidemokrasia ya raia wote ya kuchagua viongozi wa Serikali zetu za mitaa, vijiji na vitongoji hapo mwakani 2019.”

Kwa sababu hizo tatu, TEC imesema, “Ni vyema tafakari yetu ya Kwaresima ikalenga katika swali ambalo, kwa namna moja au nyingine, linahusu sababu hizo tatu. Kwa njia ya swali hilo mwanadamu hudiriki kumhoji na kumuuliza Mungu na Muumba wake kuhusu hali ya binadamu mwenzake. Swali hilo ni Je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” (Mw. 4:9).

LIVE: IGP Simon Sirro amuapisha Kamishina wa Polisi Zanzibar kwa niaba ya Rais Magufuli.

$
0
0
February 10, Rais alimpandisha cheo Mohamed Hassan Haji  kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP), na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. 
 
Leo, February 12, IGP Simon Sirro amuapisha Kamishina huyo  kwa niaba ya Rais Magufuli. 

Tazama tukio hilo hapo chinii

Zitto Kabwe Amtembelea Tundu Lissu Ubelgiji

$
0
0
Mbunge Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe amemtembelea Tundu Lissu nchini Ubelgiji anakoendelea na matibabu ya viungo na saikolojia tangu Januari 7, 2018.

Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki anapata matibabu hayo baada ya kushambuliwa kwa risasi  Septemba 7, 2017 akiwa nje ya makazi yake mjini Dodoma. 

Awali mbunge huyo alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Dodoma siku hiyohiyo kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Nairobi alikotobiwa hadi Januari 6, 2018 alipohamishiwa Ubelgiji.

Katika picha mbalimbali zilizotoka jana Februari 11, 2018  ziliwaonyesha wawili hao wakiwa kwenye mwonekano tofauti wa mazungumzo.

Leo Februari 12, 2018, Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS) amesema, “Zitto amekuja kunijulia hali na kwa ajili ya kubadilishana mawazo kuhusu hali ya nchi yetu kisiasa, kiuchumi na kijamii.”

Hata hivyo, Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT- Wazalendo amesema hawezi kuzungumza zaidi kuhusu kile walichoteta na Lissu huku akiahidi baadaye kutoa taarifa.

Tiba Asili ya Kuondoa Chunusi, Kupunguza Tumbo, Maziwa Makubwa na Nguvu za Kiume

$
0
0
Asilimia 90 ya wanaume hushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya  kama vile kisukari, punyeto ambayo huathiri mfumo mzima wa wa misuli inayozalisha vichocheo ashiki , kutopata choo vizuri hali ambayo huchakiwa na kula chakula kisicho na asili,tumbo kuunguruma, kujaa gesi,kiuno kuuma, mgongo na miguu kufa ganzi

SUPER HOLO; Ni dawa itokanayo na miti shamba, ipo katika mfumo wa vidonge na unga. Hutibu na kumaliza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa muda mfupi tu.,SUPER HOLO hurudisha heshima ya ndoa, itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika 15-30. Itakupa hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3. Pia itaimarisha misuli iliyosinyaa na kulegea. Dawa hii hutumiwa kwa watu wa umrii wa miaka 20- 80

NZOGIWE ni dawaya maumbile.Hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo urefu wa nchi 4-8 na unene wa sentimita 2-4 za upenyo

NZOGOMA ni dawa asili ya miti shamba, huboresha mbegu za uzazi...huzibua mirija na kusafiisha ili kuweza kushika mimba au kutia mimba.

Pia tunayo dawa ya kupunguza tumbo, unene, maziwa makubwa, kuongeza hips, makalio na kutoa chunusi

TUNAPATIKANA MTONI MTONGANI. KANA HAUNA NAFASI YA KUFIKA UTALETEWA ULIPO. WASILIIANA NA DR. MBUSI.  PIGA SIMU NAMBA:   0718 431222
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images