Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mlima Kilimanjaro waingiza bilioni 471

$
0
0
Serikali imesema hifadhi ya Mlima wa Kilimanjaro katika kipindi cha miaka kumi kuanzia mwaka 2007 hadi 2017 imeingiza mapato ya Shilingi Bilioni 471 kupitia shughuli za utalii.

Mapato hayo yameelezwa jana Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akijibu swali la Mbunge wa Vunjo, James Mbatia aliyehoji mapato ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro na matumizi yake katika kipindi cha miaka kumi mfululizo.

Hasunga alitaja matumizi ya mapato hayo, kwamba kiasi cha Sh. Bilioni 67.5 zilitumika kutengeneza miundombinu ya kuhifadhi mlima na Bilioni 46.6 kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za hifadhi katika kipindi cha miaka kumi.

Pia, alisema Bilioni 2.28 zimetumika katika utekelezaji wa miradi ya kijamii kwenye vijiji vilivyo jirani na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Mbunge Chadema ahoji utekelezwaji sera ya matibabu bure kwa wazee

$
0
0
Mbunge Viti Maalum Jimbo la Morogoro (Chadema), Devotha Minja ameihoji serikali juu ya utekelezwaji wa sera ya huduma ya matibabu bure kwa wazee.

Minja ameyahoji hayo katika kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha sita cha Bunge la kumi linaloendelea mjini Dodoma, ambapo amesema wazee katika kambi ya Fungafunga iliyoko mjini Morogoro wanakosa dawa na kulazimika kununua dawa muhimu kwenye maduka ya dawa ya nje, kutokana na uhaba wa dawa uliopo kwenye Hospitali ya mkoa wa Morogoro.

“Kambi ya Fungafunga iliyoko mjini Morogoro inayohudumia wazee wengi hivi sasa wanakosa huduma ya matibabu kutokana na hospitali ya mkoa wa Morogoro kukosa dawa za kutosha, wazee wanapewa panado na dawa nyingine wanaambiwa wakanunue kwenye famasi za nje, nataka kujua sera hii ya matibabu bure kwa wazee inatekelezeka?,” amehoji.

Akijibu swali la Minja, Naibu Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amesema serikali inatekeleza sera hiyo kikamilifu, pia kwa sasa hakuna uhaba wa dawa kwenye hospitali za umma, kutokana na kuongezeka kwa bajeti ya dawa kutoka bilioni 30 hadi kufikia takribani bilioni 270.

“Serikali kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007 imetamka wazi kwamba matibabu kwa wazee wasiojiweza yatakuwa buree na hilo tunalitekeleza kikamilifu lakini sambamba na hilo, hatuna uhaba wa dawa sasa hivi, bajeti ya dawa imeongezekasana kutoka bilioni 30 hadi  kufikia takribani bilioni 270 dawa zote muhimu zinapatikana, kama kuna suala mahsusi kuhusiana na kambi hii, devotha minja ningependa kupata maelezo ya ziada ili tushughulikie tatizo hilo,” amesema.

Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kwa sasa serikali iko kwenye mapitio mapya ya sera, baada ya sera yam waka 2003 kupitwa na wakati, ili ihuishe mahitaji ya wazee ya sasa kwa ajili ya kutunga sheria mpya.

Hizo Ndio Sababu Kwanini Pete Ya Immoring Inapendwa Na Watu Wengi.

$
0
0
Na. Dokta  Mungwa  Kabili …………….0744   000  473.
Pete  ya  Immoring  ni  pete ambayo  imejizolea  umaarufu  mkubwa  sana  miongoni  mwa  wakaazi mbalimbali  wa   nchi za  Afrika  Mashariki  na   Ukanda  wa  Maziwa  makuu  kwa  ujumla.

Nimekuwa  nikipoea  simu  na  jumbe  kutoka  kwa  watu  mbalimbali  wakitaka  niwasaidie kujua  namna  pete  ya  Immoring  inavyo  fanya  kazi  pamoja  na  kuwaelesha  uhusiano uliopo  kati  ya  pete ya Immoring  na  suala  zima  la  kusafisha, kuimarisha  na  kupandisha  nyota, kutunza  na  kukinga  nyota  pamoja  na  mwili  wa  mwanadamu  kwa  ujumla   Yafuatayo  ndio  majibu  yangu.

Kabla  sijaanza  kuelezea  kuhusu  pete  ya  Immoring  ni  vyema  nikaelezea  nyota  ni  nini ? Ili  kusudi  unapotaka  kujua  uhusiano  kati  ya  pete  ye  Immoring na  masuala  ya  nyota, uwe  unajua  kinaongelewa  kitu  gani.

Nyota  Ni  Nini  ?
Kwa  lugha  rahisi  na  nyepesi   kabisa nyota  ni  ramani  ya  maisha  ya  mtu  ambayo  ameandikiwa  na  Mwenyezi  Mungu.

Utajuaje  Kama  Nyota  Ya  Mtu   Ni  Safi  Au  Chafu ?
Utajuaje  Kama  Nyota  Ya  Mtu   Ipo  Juu  Ama  Ipo  Chini ?
Utajuaje  Kama  Nyota  Ya  Mtu  Ni  Mbaya  Au  Nzuri ?

Kiashiria  kikuu  cha  daraja  ama  hadhi  ya  nyota  ya  mtu  ni  namna  mambo  yanavyo  muendea  mtu huyo katika  maisha  yake.  Au  kwa  njia  rahisi  kabisa  unaweza  kujua  daraja  ama  hadhi  ya  nyota  ya mtu  kwa  kuangalia  kiwango  cha  riziki  anayo  ipata  katika kazi  ama  shughuli  zake  za  kila  siku  katika  maisha.

Mtu  mwenye  nyota  ya  juu  hata  riziki  yake  itakuwa  juu  pia  na  Yule  wa nyota  ya  chini riziki  yake  itakuwa  chini  pia  kama  ilivyo  nyota  yake.

Nyota  Na  Sehemu  Kumi  Na  Mbili  Za  Mwili  Wa  Mwanadamu
Kwa  kawaida  ili  mwanadamu  aishi  maisha  ambayo  watu wengine  wakiyatazama  wanaweza  kukufuru  na  kusema  mtu  huyo  kapendelewa, basi  mtu  huyo  anapaswa kuwa  na  nyota 12 ambazo  idadi yake  ni  sawa  sawa  na  idadi  ya  sehemu  kumi  na  mbili  za  mwili  wa  mwanadamu.

Katika  ulimwengu  wa  kitabibu  na  kinyota  mwili  wa  mwanadamu  umegawanyika  katika  sehemu  ndogo  ndogo  kumi  na  mbili  ambazo  zimegawanyika  katika  sehemu  kuu  mbili.

Sehemu  hizi  kuu  mbili  za  mwili  wa  mwanadamu  zinaunganishwa  na  kutenganishwa  na  kitovu. Sehemu  ya  kwanza  ni  sehemu  ya  juu  kabisa  ambayo  inaanzia  utosini  hadi  juu  ya  kitovu  ilihali  sehemu  ya  pili  ni  sehemu  ya  chini  ambayo  inaanzia  chini  ya  kitovu  hadi  kwenye  unyayo.

Sehemu  ya  juu  imegawanyika  katika  sehemu  kuu  tatu  ambazo  kila  sehemu  moja  kati  ya  sehemu  hizo  tatu  imegawanyika  katika  sehemu  ndogo  ndogo  mbili mbili  kila  moja Vivyo  hivyo  sehemu  ya  chini  nayo  imegawanyika  katika sehemu  kuu  tatu ambazo  nazo  pia  zimegawanyika  katika sehemu  ndogo ndogo mbili mbili  kila  moja.

Kila  sehemu moja  katika sehemu  hizi kumi  na  mbili  za  mwili  wa  mwanadamu  inawakailisha  na  kusimama  badala ya  nyota   moja.

Sasa  basi  ili  tuseme  mtu  Fulani  nyota  yake  ipo  juu, basi  mtu  huyo  lazima  awe  amekamilisha  idadi ya  nyota  zote  kumi  na  mbili  ambazo  zinakamilisha  idadi  ya sehemu  kumi  na  mbili  za  mwili  wa  mwanadamu.

Kwanini  ni watu  wachache  tu ndio  wanao  kamilisha  idadi  ya  nyota  zote  kumi  na  mbili?
Ni  watu  wachache  sana  duniani  ambao  wanakamilisha  nyota zote  kumi  na  mbili. Ni  mtu  mmoja  katika  maelfu . Sababu  kuu  ni  fitna  na  dhulma  zinazo  fanywa  na  wachawi  kwa  kushirikiana  na  majini  na  masheitwani wachafu   katika  kushusha  ama  kuiba  na  kuzitumia  nyota  za watu  mbalimbali.

Matokeo  yake, limekuwa suala  gumu   sana  kukutana  na  mtu  ambaye  ana  nyota  zote  kumi  na  mbili.  Sio  tu  nyota  zote  kumi  na  mbili  bali  hata  nyota  kumi  na  moja, kumi, tisa, nane au hata  saba.

Idadi  kubwa  ya  watu  tunao  waona mtaani  na  kudhani  wamefanikiwa   sana  katika  maisha, wanachezea  kwenye  nyota  nne  hadi tano.  Hawa  ni watu  walio katika  kundi la  watu  ambao  katika  ulimwengu  wa  kitabibu  na  kinyota wanajulikana  kama  watu  wanao  fanikiwa  chini  ya  kiwango chao.

Wengine  nyota  zao  hushuka  hadi  kuwa nusu, sifuri, hasi  moja,  hasi  sita na chini  ya  hapo.

Mtu mwenye  nyota sifuri  ni  mtu ambae  katika  ulimwengu  wa  kinyota  na  kitabibu anatajwa  kama  mtu  ambae  anapita duniani  bila  kuonekana. Ni  mtu  ambae  riziki yake  hapa duniani  ni  sifuri.

Mtu  ambae  nyota  yake  imeshushwa  hadi  kufikia  hasi  sita  ( -6 )  ni  mtu  ambae  katika  ulimwengu  wa  kinyota  na  kitabibu tunasema   nyota  yake  imekuwa  sawa  sawa  na  nyota  ya  mtu  aliyelala  kaburini . ( Nyota ya  Kaburi / Nyota  ya  maiti)

Wakati  mwingine  nyota  ya  mtu  inaweza  kushushwa   hadi   kufikia hasi  Arobaini  na  mbili  ( -42). Mtu  mwenye  nyota  hii  ni  mtu  ambae  katika  ulimwengu  wa  kitabibu  tunasema  nyota  yake  imechukuliwa  na nafsi  yake  imefungwa  kwenye  makaburi  saba. Mtu alie  katika  kundi  hili  anakuwa  amefungwa  kwenye  makaburi  saba  tofauti  tofauti  na  kama  ni  mwanamke  basi  tunasema  amefungishwa  ndoa  na  makaburi  saba.. Na inapotokea  mwanamke  akawa  katika  kundi  hili  basi  mara nyingi  fitna  yake  inakuwa  imetokana  na  ugomvi  wa  kugombea  mwanaume au  ugomvi  wa  mapenzi  ulio  fuatia  kuachana  kati  yake  na  mpenzi, mchumba  au  mume  wake. Mwanamke  huyu  hukusudiwa  aitulie  katika  ndoa  yake, kila  ndoa   au  uhusiano  kwake  uwe  sawa na  kaburi  na  kama  kutulia basi  atulie  kwa  mume wake  wa  saba  ambae  ni  kaburi  halisi.

Tofauti  na  mtu  ambae  nyota  yake  imeshuka  na  kufikia  sifuri, mtu ambae  nyota yake  imeshushwa  hadi  kufikia  ( -6 ) au  ( -42) ni  mtu  ambae  ramani  ya  maisha  yake  imegeuzwa  juu  chini  ama  nje  ndani.  Ni  mtu  ambae  amekusudiwa  kichawi  kwamba, aishi  maisha  yake  ya  kaburini  akiwa  hapa  duniani  na  maisha  ya  duniani  aende  kuyaishi  akiwa  kaburini.

Watu  walio  katika  kundi  hili  ndio  watu  wanaokujaga  kusumbua  sana  baadae  kama  mizimu  mara  baada  ya  maisha  yao  ya  hapa duniani  kufika  tamati.

Sababu  Kwanini  Nyota  Ya  Mtu  Inaweza  Kushushwa.
Zipo  sababu  kuu  mbili  zinazo  weza  kufanya  nyota  ya  mtu  ikashushwa:

1.    Husda, chuki  na  choyo  dhidi ya  mtu  anaeonekana  kuwa  na  nyota  kubwa.

2.    Ubinafsi  na  Tamaa  ambao hupelekea  mtu  mmoja  kuiba  nyota  ya  mwenzake  kwa  ajili  ya  kuitumia  kwa  matumizi  yake  binafsi  huku  akimuacha  muibiwa  akiwa  anahangaika ilihali  alikuwa  na  nyota  nzuri  tu.

Jinsi  Nyota  Ya  Mtu  Inavyo  Shushwa
Zipo njia  nyingi  sana  zinazo  weza  kutumika  kushusha  nyota  ya  mtu  nikisema  nizitaje  zote  hapa  ninaweza  kuandika  kitabu  kizima.  Ninacho  kieleza   hapa  ni  sababu  za  kitabibu  zinazo weza  kufanya  nyota  ya  mtu  kushuka.

Kama  nilivyo  sema  hapo  awali kuwa  mwanadamu  anapaswa  kuwa  na  nyota  zote  kumi  na  mbili  ili  asemwe  kuwa  ana  nyota  kali.  Hii  ni  kwa  sababu  mwili  wa  mwanadamu  umegawanyika  katika  sehemu  kumi  na  mbili.  Kikiongezeka  kitu  cha  kumi  na  tatu  basi  mwanadamu  huyo  lazima  apate  madhara  kwa  sababu  anakuwa  amewekwa  ndani yake  kitu  ambacho  hakina uhusiano  na  mwili  wake.

Jinsi   Inavyokuwa :  Atatumwa jinni  ambae  nguvu  yake  ya  kijini  ni  hasi  ( -6 ) kwa mfano. Jinni  huyu  atatumwa  kwenda  kukaa  kwenye  mwili  wa  mwanadamu  mwenye  nyota  kumi  na  mbili

  Kwa  sababu  jinni  huyu   nguvu  yake  ama  nyota  yake  ni  ( -6 ) na  anaenda  kuungana  na  mtu  ambae  nguvu ya nyota  yake  ni  12.  Maana  yake  ni  hii ( -6 ) inajumlishwa  na  12 ambapo  tunapata  6.   Kwa  lugha  nyepesi, jinni  huyu  atasababisha  nyota  ya mtu  huyu ishuke  kutoka  12  hadi  6 , na  linapotokea  jambo  hilo  basi  mambo  ya  mtu  huyo  yanaanza  kubadilika  taratibu ( Majini  ambao  nguvu  zao  katika  ulimwengu  wa  kiroho  ni  kuanzia  ( -1 ) na  kuendelea  ni  majini  wa  makaburini).

Mtu  huyo huyo tena  baadae  anaweza  kutumiwa  majini wengine  mfano  wawili ambao  kila  mmoja  nguvu yake  ni  ( -7 ). Hasi  7  mara  mbili  ni  Hasi 14  na  -14 jumlisha 6  ni  Hasi  8. Mtu  anapofikia  hatua  hii  basi   nyota  yake  inakuwa  imeshushwa  hadi  chini  ya  kaburi  na  mambo  yake  yataanza  kuharibika  na  kuwa  mabaya  siku hadi  siku na  asipo  shituka mapema   basi  anaweza  kuishia  hivyo  hivyo  hadi  umauti  wake.

Njia  ya  pili  ni  ile  ya  kuiba  nyota  za  mtu  au  watu  husika. Hapa  atatumwa jinni  maalumu  kuja  kuiba  nyota  zote  kumi  na  mbili  za  mtu  Fulani  na kuzipeleka kwa  mchawi  ambae  amemtuma  shughuli  hiyo. Mtu ambae nyota  zake  zimeibiwa  ataanza  kuishi  maisha  ya  mateso  na  kupata  riziki  kwake  itakuwa  ngumu  sana  kwa  sababu  nyota  zake  zinakuwa  zimechukuliwa  kwa  nguvu  na  kwenda  kutumia  na  mtu  mwingine.

Mara  nyingi  watu w anao  iba  au  kuagiza  kuibwa  kwa  nyota  hizi  ni  watu  ambao  hutaka  kupata  maradufu zaidi  ya  kile  wanacho  kitaka  ambapo  katika  ulimwengu  wa  kitabibu  watu  hawa  hulazimika  kuiba  nyota  nzuri  za  watu  wengine  na  kuzitumia  kwenye  shughuli zao  za  kutafuta  riziki.

PETE  YA  IMMORING  NA  NYOTA
Pete  ya  Immoring  ni  Nini ?
Kujua  pete  ya  Immoring  Ni  Nini fuatilia  makala  zangu za  nyuma  ambazo  niliwahi  kuandika  kwa  ufupi  kuhusu  pete  hii.

Katika  ulimwengu  wa  kitabibu  na  kinyota, pete  ya  Immoring  hufanya  mambo  yafuatayo:

1.  Pete  Ya  Immoring  Hutumika  kama  Hoza  la  Kupooza  Uchawi  au  Nguvu  Hasi  ambazo  zimeelekezwa  kuingia  kwenye  mwili  wa  mtu Pete  ya  Immoring  hufanya  kazi  kama  mmea  ujulikanao  kama  Hoza.  Mmea  huu  uitwao  Hoza  hutumika   kitabibu  kupooza  uchawi  ambao  mtu  ametupiwa.  Hutumika  kuogea, kuchanjiwa  na  kupikwa  nyungu  au  kama fusho  kwa  lengo  la  kupooza  uchawi  ama  nguvu yoyote  hasi  iliyo  tumwa  ama  kujilekeza  yenyewe  kwenye  mwili  wa  mtu  Fulani.

Pete   ya  Immoring  hutumika  kupooza uchawi  ama  nguvu  hasi (nguvu ya  majini  wabaya ) ambayo  imetumwa  kumuingia  mtu  alie ivaa.   Hii  hutokea  pale  nguvu  hiyo  inapokuwa  kubwa  kuliko  nguvu  ya  nyota  ya  muhusika .

Mathalani  mtu  ambae  nyota  yake  ni  12, akitumiwa  jinni  ambae  nguvu  zake  ni  hasi 36  jinni  huyo  atamdhuru  mtu  huyo.  Sasa  basi  inacho  kifanya  pete  ya  Immoring  ni  kuupooza  uchawi  ama  nguvu  ya  jinni  huyo na  kisha  kutoa  taarifa  kwenye  kinga  ya  mtu  huyo  kuhusu  kufanyika  kwa  shambulio  la  kiroho lililo shindwa  dhidi  ya  mtu  huyo  kwa  lengo  la  kumfanya tu  mhusika  atambue  kuwa  kuna  uadui  umejaribu  kumdhuru  lakini  umeshindwa.

2. Pete  Ya  Immoring  Hutumika  Kama  Kinga Dhidi  Ya  Shari  za  wachawi na  masheitwani  wabaya

3.Hutumika  kusafisha  na  kupandisha  nyota  Katika  kusafisha  na  kupandisha  nyota, aina  ya  pete  ya  Immoring  itakayo  tumika  itategemeana  na  kiwango  cha  nyota  alicho  nacho  mtu na  kiwango  cha  nyota  anacho  kitaka. Kwa  mfano  mtu  amabe  nyota  yake  imeshuka  hadi  sifuri  na  anataka  nyota  yake  ipande  hadi  kumi  na  mbili  basi  atalazimika  kutafuta  pete  ya  Immoring  ambayo  nguvu  yake  ni  12 . Nakadhalika.

4. Pete  ya  Immoring  husaidia  kuunganisha  nyota  ya  mvaaji  na  nguvu  ya  mungu  jua.

5.  Pete  ya  Immoring  hutumika katika  matambiko yote  ya  jua  kuanzia  tambiko  la  biashara , kinga  ya  mwili, kutibu  nguvu  za kiume  kwa  kutumia  tambiko  la  jua nakadhalika.

6.  Pete  ya  Immoring  hutumika  kama  mbadala  wa  fusho  la  jua. Fusho  la  jua  ni  fusho linalo  tumika  katika  tambiko  la  jua.

7. Pete  hii  hutumika kuunganisha  nguvu  ya  mvaaji  na  nguvu  ya  bahari.

8. Pete  ya  Immoring  hutumika  katika  tambiko  maalumu  kwa kufanya  kitu  au  jambo  lisionekane  tena  kwa  kutumia  mawimbi  tisa  ya  bahari  na  mti  ulioletwa  na  mawimbi  ya  bahari  au mafuriko  na  zaafarani nyekundu.

9.Kwa  wale  wanao kwenda  baharini  kuoga  ama  kuchukua  maji  ya  bahari  kwa  ajili  ya  kutoa  mikosi  au  kusafisha  nyota  basi  pete  ya  Immoring  ni  nyenzo muhimu  sana  kwao.

10. Hutumika  kuunganisha  nyota  ya mvaaji  na  nguvu  ya  hewa

11. Hutumika  kuunganisha  nyota  ya  mvaaji  na  nguvu  ya  ardhi

12. Hutumika  kama  antenna  inayo  fanya  kazi  ya  kuvuta, kunasa  na  kuchakata  nguvu  zote  za  kiroho  zinazo  elekezwa  kwa  mvaaji

IMESIMULIWA  NA  DOKTA. MUNGWA  KABILI…0744  000  473.

Msukuma Ampa Makavu Waziri Bungeni

$
0
0
Mbunge na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amemshambulia kwa maneno Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina juu ya 'operation' anazozifanya za kionevu za kupambana na uvuvi haramu kwa kumwambia aache kufanya kazi kwa mihemuko

Msukuma ameeleza hayo katika mkutano wa 10 kikao cha sita cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati akichangia uwasilishaji wa kamati ya kudumu ya Bunge ya kilimo, mifugo na maji baada ya kupita miezi kadhaa tokea Waziri Mpina kutoa kauli yake kuachia madaraka endapo tatizo la uvuvi haramu litaendelea kuwa sugu nchini jambo ambalo kwa sasa Msukuma anadai kiongozi huyo analifanya bila ya kufuata sheria zilizopo kwa kuzuia watu wasivue dagaa na kupelekea kuwapa athari wananchi wanyonge na kumuomba aundiwe tume ya uchunguzi yeye na  timu yake.
 
"Toka nazaliwa sijawahi kuona sheria hizi zinazotumiwa na Waziri wa Mifugo Mpina, umri wangu huu nimeshuhudia awamu zote za Mawaziri. 

"Nafikilia kwamba ndio tunaanza kutunga sheria au hii ilikuwa imefichwa ndio inaibuka. Sijawahi kuona Waziri anasimama na kujisifu kwamba kwao hakuna samaki na kutamani watu wote wasile samaki. 

"Mungu ametupa neema tofauti, sijawahi kuona mtu anaenda kukamata mitego dakika mbili faini hana unachoma nyavu zake bila ya kuhakikisha kwamba ni feki au laa",alisema Msukuma.
 
Aidha, Msukuma amesema ana muhitaji Waziri huyo siku akihudhuria Bunge basi aweke wazi kuhusiana na sheria hizo anazozitumia amezitoa wapi na kama akishindwa kutokea katika kipindi basi watamsubiri katika Bunge la bajeti ili wambane vizuri juu ya hilo.
 
"Nitoe rai kwa Mawaziri kwamba Mawaziri wa aina kama hii nina washauri wapunguze mihemuko kwa sababu hata sisi tunatamani kuendelea kuwa Wabunge humu ndani lakini kwa 'dizaini' mnayoenda mtuambie mmewapanga wabunge wa kina nani ambao mnataka wawe wabunge maeneo yetu. Nina zungumza kwa wabunge wanaotoka Kanda ya Ziwa sidhani kama sisi tutarudi humu Bungeni", amesisitiza Msukuma.
 
Kwa upande mwingine, Msukuma amemtaka Waziri Mpina na timu yake kiujumla wajipange kuwafundisha wavuvi na wala sio kuwafilisi.

Serikali yawapokonya pasipoti maofisa 15 wa Nasa

$
0
0
Serikali imeamua kusitisha hati za kusafiria za viongozi kadhaa wa ngazi ya juu na wanasiasa wafuasi wa muungano wa upinzani wa Nasa ikiwemo ya gavana wa Mombasa, Hassan Joho.

Mbali ya Joho, wanasiasa wengine waliositishiwa hati zao za kusafiria ni seneta wa Siaya, James Orengo na seneta wa zamani wa Machakos, Johnson Muthama.

Mpangaji mkuu wa mikakati wa muungano huo, David Ndii pamoja na mfanyabiashara Jimi Wanjigi pia hawakuachwa katika mkumbo huo wa serikali kuzidisha kibano kwa wanasiasa wa upinzani baada ya hatua yao ya "kumuapisha” mgombea wao wa urais katika uchaguzi wa mwaka jana Raila Odinga kuwa "rais wa watu" ikiwa ni ishara ya kutotii serikali.

Katika barua waliyopelekewa viongozi hao wanaodaiwa kufikia 15, Mkurugenzi wa Uhamiaji, Gordon Kihalang'wa alisema kusitishwa kwa hati hizo kumefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Wananchi na Uhamiaji ya mwaka 2011 inayotoa sababu za kusimamishwa.

Akizungumza na Daily Nation Jumanne, Muthama alisema viongozi kutoka idara ya uhamiaji walitoa barua hiyo ya kumjulisha kuhusu hatua ya kusitishiwa hati ya kusafiria kuanzia saa 7:00.

"Tunaona udikteta ukijitengeneza. Hawaheshimu sheria kwa sababu hili ni shambulio dhidi ya Sheria ya Haki ambayo haiwezi kuachanishwa," alisema.

Seneta huyo wa zamani ambaye pia ni kiongozi wa ngazi ya juu wa upinzani alisikitishwa kwamba njia zisizofaa zinazotumika kwake tayari zimemvuruga.

"Ilikuwa nimsindikize binti yangu Uingereza leo (Jumanne) saa 10:00 alasiri lakini sasa siwezi. Hii ni njia hatari ambayo serikali imechagua na lazima isitishwe," alisema.

Kinara wa Nasa, Kalonzo Musyoka ameelezea kusimamishwa kwa hati za kusafiria kwa viongozi wa juu wa Nasa na kufungwa kwa vyombo vya habari kuwa ni sifa za serikali yenye hofu.

"Hofu ambayo imeingia kwenye utawala huu inaelezea yote. Wanaziba uhuru wa vyombo vya habari kwa sababu hawataki ukweli, na sasa wameamua kuzuia watu kusafiri. Lakini kwa nini wana hofu? Kama wako imara kama wanavyosema, hofu ya nini?"  Aliuliza Musyoka alipokuwa kwenye ofisi za makao makuu ya chama chake cha Wiper jana.

Aliyemuapisha Raiila Odinga afukuzwa nchini Kenya Usiku kwa Nguvu na Kupelekwa Canada

$
0
0
Serikali ya Kenya imemfukuza kwa nguvu na kumsafirisha kwenda nchini Canada mmoja wa viongozi wa upinzani Kenya, Miguna Miguna usiku wa kuamkia leo Februari 8 baada ya mahakama kudai aachiwe huru.

Katika akaunti ya Twitter ya Serikali inayofahamika kwa jina la ‘Nexus’ iliandika katika ukurasa huo Februari, 6 saa 7:19 usiku kuwa Miguna anaelekea nyumbani Canada baada ya mahakama kuamuru aachiwe.

Serikali imeandika kuwa Wizara ya Ulinzi ilitii agizo hilo na kumpatia tiketi ya kwenda nyumbani kwake Canada ambapo ana uraia wa nchi hiyo alioupata Juni 16, 2017.

“Miguna ameelekea nyumbani. Mahamakma iliamuru aachiwe na Wizara ya Ulinzi imetii amri na imempatia tiketi ya kwenda nyumbani. Tafadhali tunasisitiza alipatiwa kibali cha kuishi Canada Juni, 16 2017” umeandika ukurasa huo.

Miguna amesafirishwa na Shirika la Ndege la KLM ambalo lilipoulizwa na wananchi katika ukurasa wao wa Twitter unaofahamika kwa jina la ‘Royal Dutch Airline’ walipendekeza maswali yote waulizwe mamlaka husika kwa sababu za kiusalama.

Miguna alishikiliwa na Polisi Februari, 2 kwa tuhuma za kushiriki kuapishwa kwa Raila Odinga kama Rais wa watu wa Kenya Januari, 30.

Mwanasheria wa Miguna, Dk John Khaminwa amesema mteja wake kwasasa hayupo nchini humo.

“Ni kweli. Ameondolewa kwa nguvu na ndege ya KLM na tunasikia ameelekea Canada. Ni uvunjaji wa haki” amesema Khaminwa.

Kuhusu sakata la uraia wake, Dk Khaminwa amesema Miguna aliukana uraia wa Kenya ila miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu aliomba tena.

“Miguna alipokamatwa Serikali ya Canada iliiandikia barua Kenya kuelezea kuwa mwananchi wao ananyanyaswa,” amesema Khaminwa.

Katika kipande kifupi cha video kinachosambaa mtandaoni kimemuonyesha kiongozi huyo akiwa katika ndege na amevalia suti, barakashia akiwa peke yake siti za mbele.

Ijue Afya Yako: Pata Tiba Asili ya Busha, Maumbile Madogo na Nguvu za Kiume

$
0
0
Tatizo hili limekuwa likiwaayhiri watu  wengi sana baada ya kujiona wako tofauti na watu wengine .Kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na maumbile  nchi-6-7 .Matatizo haya yanasababishwa na punyeto) kisukari) presha) naulevi wakupita kiasi pia na msogo wa mawazo, homoni za toka kuzaliwa 

MOMLA ni dawa inayotibu kinacho sababisha tatizo,kama vile sukari, presha, magonjwa ya zinaa, misuli kulegea na kusinyaa kwa kwasababu ya kujichuwa au punyeto na akili kudumaa kwaajili ya tendo bila kushiriki 

MBEPE nikwa wenye maumbile mafupi na membamba kwa matatizo hayo ni dozi ya siku 5 unapona kabisa 

DAGULA hii nikwaajili ya wenye busha iwe ya maji au ya utumbo kushuka inatibu bila opresheni , kuuga mifupa kwwaliopata ajari yoyote inayo sababisha uvujifu wa mifupa inatibu kwa mda wa siku 14 tayali kwa mazoizi 

LUKOMOLO ni dawa ya mvuto wa mpenzi biaashara ata kama mme mke mchumba atakutafuta mwenyewe na kutekeleza yote unayotaka mfanye akutafute mwenyewe pia tunatibu kiuno miguu aina yote tumbo la uzazi kwa kina mama na kina baba nk 

KWA WAKAZI WA DSM TUNAPATIKANA MBANGALA RANGI TATU MKABALA NA KISUMA BAA. 

KWAMIKOA YOTE MTAPATA HUDUMA HILI KWA MAWASILIANO PIGA 0767131395, 0712757594, 0787131395 MUONE DR MWANGARA

Tiba Asili ya Kuondoa Chunusi, Kupunguza Tumbo, Maziwa Makubwa na Nguvu za Kiume

$
0
0
Asilimia 90 ya wanaume hushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya  kama vile kisukari, punyeto ambayo huathiri mfumo mzima wa wa misuli inayozalisha vichocheo ashiki , kutopata choo vizuri hali ambayo huchakiwa na kula chakula kisicho na asili,tumbo kuunguruma, kujaa gesi,kiuno kuuma, mgongo na miguu kufa ganzi

SUPER HOLO; Ni dawa itokanayo na miti shamba, ipo katika mfumo wa vidonge na unga. Hutibu na kumaliza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa muda mfupi tu.,SUPER HOLO hurudisha heshima ya ndoa, itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika 15-30. Itakupa hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3. Pia itaimarisha misuli iliyosinyaa na kulegea. Dawa hii hutumiwa kwa watu wa umrii wa miaka 20- 80

NZOGIWE ni dawaya maumbile.Hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo urefu wa nchi 4-8 na unene wa sentimita 2-4 za upenyo

NZOGOMA ni dawa asili ya miti shamba, huboresha mbegu za uzazi...huzibua mirija na kusafiisha ili kuweza kushika mimba au kutia mimba.

Pia tunayo dawa ya kupunguza tumbo, unene, maziwa makubwa, kuongeza hips, makalio na kutoa chunusi

TUNAPATIKANA MTONI MTONGANI. KANA HAUNA NAFASI YA KUFIKA UTALETEWA ULIPO. WASILIIANA NA DR. MBUSI.  PIGA SIMU NAMBA:   0718 431222

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0744 594 994

Askari Magereza 11 wasimamishwa Kazi

$
0
0
Jeshi la Magereza Tanzania limewasimamisha kazi askari wake kumi na moja waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya mwanakijiji, Aloyce Makalla (41) wiki iliyopita.

Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo zinasema askari hao walisimamishwa kazi na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk Juma Malewa juzi.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, John Masunga alithibitisha kusimamishwa kwa askari hao lakini hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani zaidi akisisitiza kuwa msemaji wa jeshi hilo ni Kamishna Jenerali pekee.

Askari waliosimamishwa ambao walishafikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Korogwe mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kassim Mkwawa ni Jonas Makere, Shadrack Lugendo, Lazaro Stephen, Mussa Zuberi, Ramadhan Yusuf, Robert Alfred, Fhidirish Osmas, Alfonce Revocatus, Mbesha Naftari, Hamis Msola na Michael Elias.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa hatua ya kuwasimamisha kazi askari hao imechukuliwa ikiwa ni kupisha vyombo vya sheria kufanya kazi yake kwa uhuru zaidi na kwamba hatima yao itategemea uamuzi wa mahakama hiyo.

Askari hao wa Wilaya ya Korogwe walifikishwa katika mahakama hiyo wakikabiliwa na shtaka la kumuua, Makalla, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kerenge wilayani humo.

Ilidaiwa mahakamani hapo na mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Saraji Iboru kuwa Januari 22 saa 9.30 katika kitongoji cha Mapangoni Kijiji cha Kerenge, washtakiwa hao kwa pamoja walimuua mwanakijiji huyo.

Iboru ambaye alikuwa akisaidiana na mwendesha mashtaka kiongozi, Shosa Naiman alidai kwamba siku ya tukio, washtakiwa hao walikwenda nyumbani kwa Makalla wakimtuhumu kwamba Januari 15 alimjeruhi askari mwenzao aitwaye Sajenti Stephen.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji. Hakimu Mkwawa aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 15 itakapotajwa tena.

Hatua utakazotakiwa kuzifuata ili kupata 'passport' mpya ya kielektroniki

$
0
0
Tarehe 31 Januari, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli alizindua mfumo wa uhamiaji mtandao (e-Immigration) ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, kudhibiti ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuimarisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa raia wa Tanzania na wageni wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali.

Kabla ya kuzindua mfumo wa uhamiaji mtandao Rais Magufuli alikagua teknolojia iliyotumika katika mfumo huo ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa alama za vidole na baadaye kupatiwa pasipoti mpya ya kielekektronikia (e-Passport) ambayo pia ilianza kutolewa siku hiyo hiyo.

Passport hizo, zitamrahisishia mmiliki wake kuweza kupata huduma kirahisi zaidi katika nchi mbalimbali duniani ikilinganishwa na ilivyokuwa passport ya kawaida iliyokuwa inatumika hapo awali.

Wakati wa uzinduzi wa Passport hiyo, ilielezwa kuwa itapatikana kwa gharama ya shilingi 150,000/- ambayo ni tofauti na kiasi cha shilingi 50,000/- iliyokuwa ikitolewa kwa passport za zamani.

Tazama video hapa chini kujua hatua za kufuata ili kupata passport hii mpya ya kielektroniki.

Lipumba kufukuza Madiwani Wote wa CUF Dar es Salaam

$
0
0
Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF kwa upande wa Maalim Seif, Mbarala Maharagande amefunguka na kuweka wazi kuwa Profesa Lipumba pamoja na genge lake wamepanga njama kuwafukuza madiwani wote wa CUF Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari Mbarala Maharagande amesema kuwa Lipumba amepanga njama za kuwafukuza madiwani wa CUF Dar es Salaam wakiwepo wastahiki Meya kutokana na madiwani hao kutokuwa na ushirikiano na Lipumba na kundi lake.

"Lipumba amepanga njama za kutaka kuwafukuza uanachama madiwani kwa tiketi ya CUF-Chama cha Wananchi mkoa wa Dar es salaam; wakiwemo wastahiki Manaibu Meya, kutokana na madiwani hao kukataa kumsaidia msaliti Lipumba na genge lake katika kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni.

" Lipumba na watu wake wamejikuta katika wakati mgumu kwa uamuzi wao wa kusimamisha mgombea wakipingana na uamuzi wa UKAWA wa kusimamisha mgombea mmoja kutoka miongoni mwa vyama washirika. 

"Uamuzi huo wa Lipumba ambao umetafsiriwa kuwa ni mpango wa kutaka kuzigawa kura ili kuisadia CCM ishinde, umeshitukiwa na wananchi wa jimbo la Kinondoni na kusababisha kususiwa mikutano yao ya kampeni na wadau mbalimbali"

Mbali na hilo Maharagande amedai kuwa chama hicho kimejipanga vyema kukabiliana na njama hizo zinazotaka kufanywa na Profesa Ibrahim Lipumba

"Tayari jopo la wanasheria wa Chama (CUF TAASISI) wamejipanga kukabiliana na hujuma hiyo vilivyo. 

"Tutaendelea kutoa taarifa kwa wanachama wote na umma wa Watanzania kwa ujumla juu ya kila kinachoendelea kwa wakati muafaka. 

"Tunatoa wito kwa wanachama wote, wapenda mabadiliko na demokrasia kwa ujumla kuzidi kuwa wastahimilivu na kuongeza kasi ya ushiriki wa shughuli mbalimbali za CUF Taasisi katika hatua hizi za mwisho za kumalizana na Wasaliti wa Mabadiliko na Demokrasia nchini" alisisitiza

Bei mpya ya mafuta ya Petroli itakayoanza kutumika leo Februari 7, 2018 kote nchini

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta zinazoanza kutumika leo Februari 7, 2018 huku bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa zikipanda.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzinyangwa Mchany imesema bei za rejareja zimeongezeka kwa petroli ikiwa ni Sh59 sawa na asilimia 2.70, dizeli Sh46 (sawa na asilimia 2.30), na mafuta ya taa kwa Sh24 (sawa na asilimia 1.17).

Amesema bei za jumla nazo zimeongezeka ambazo kwa petroli ni Sh58.57 sawa na asilimia 2.85, dizeli kwa Sh46.48 (sawa na asilimia 2.44) na mafuta ya taa kwa Sh23.75 (sawa na asilimia 1.24).

Mchany amesema ongezeko hilo linatokana na bei kuongezeka katika soko la dunia.

“Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia Bandari ya Tanga nazo zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la Januari 3. Bei za mafuta ya taa hazijabadilika kwa sababu hakuna yaliyoingizwa nchini kupitia bandari hiyo Januari,” amesema Mchany.

Amesema bei za rejareja katika mikoa ya Kaskazini zimeongezeka, ambazo petroli ni kwa Sh15 sawa na asilimia 0.70 na dizeli kwa Sh47 sawa na asilimia 2.29. Bei za jumla zimeongezeka petroli ikiwa ni kwa Sh15.36 sawa na asilimia 0.73 na dizeli Sh47.18 sawa na asilimia2.42.

“Ongezeko la bei za mafuta ya petroli na dizeli katika Mkoa wa Tanga linatokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji,” amesema Mchany.

Kaimu mkurugenzi mkuu huyo amesema sehemu ya shehena kubwa ya mafuta yaliyopokewa katika Bandari ya Dar es Salaam ni yenye bei ya soko la dunia za Novemba, 2017 wakati iliyopokewa katika Bandari ya Tanga ni ya bei ya soko la dunia ya Desemba 2017.

Amesema bei za mafuta katika soko la dunia kwa Novemba 2017 ziko juu kwa zaidi ya asilimia sita ikilinganishwa na bei za Oktoba 2017, wakati bei za Desemba zina mabadiliko tofauti.

Amesema bei ya petroli imepungua kwa asilimia 0.2 na ya dizeli na mafuta ya taa imeongezeka kwa asilimia 2.7 na asilimia 1.9.

“Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ili mradi tu bei hizo zisivuke  bei kikomo kama ilivyokokotolewa na kanuni iliyopitishwa na Ewura,” amesema Mchany.

PICHA: Mwigulu Nchemba aongoza uchomaji moto shamba la bangi ekari sita

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameongoza operesheni ya kuteketeza ekari sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu uliopo kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Uteketezaji huo umefanyika leo Februari 7, 2018 ambapo Mwigulu, Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo na baadhi ya askari wamelazimika kutembea kwa miguu umbali wa kilomita 2 kwenda katika msitu huo, huku wamiliki wa mashamba wakitokomea kusikojulikana.

Bangi hizo zilivunwa kutoka shambani, kurundikwa sehemu moja na kisha kuchomwa moto.

Mwigulu amesema Serikali itaendelea na operesheni hiyo nchi nzima na haitasita kuwakamata wahusika wote na kutaifisha magari yanayotumika kusafirisha bangi.

Amewataka polisi kuongeza juhudi kupambana na wanaotengeneza dawa za kulevya viwandani.

Kwa upande wake Mkumbo amesema ekari sita za mashamba ya bangi zimeteketezwa na kusisitiza kwamba operesheni hiyo ni endelevu katika mkoa wa Arusha na wilaya zake.

Amesema kwa sasa wanaolima bangi wamebuni mbinu ya kulima katikati ya misitu ili kukwepa kukamatwa.

“Wananchi wanapaswa kubadilika kwa kulima mazao yenye tija badala ya bangi. Polisi kama walinzi wa usalama hatutakubali kuona vijana wanaathirika kwa matumizi ya dawa za kulevya,” amesema.

“Walidhani kulima bangi katikati ya misitu hatutawabaini. Polisi tuna mbinu nyingi na hatutakubali kuona vijana wetu wanaharibikiwa kwa sababu ya bangi.”

Dr Slaa Aeleza Sababu za Kutompa Pole Tundu Lissu

$
0
0
Balozi mteule, Dk. Willibrod Slaa ameeleza sababu za kutompa pole Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, mwaka jana.

Dk. Slaa ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, alitoa kauli hiyo jana wakati akihojiwa na kipindi cha 360 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Clouds.

“Suala la Lissu nilishachokozwa sana kwenye mitandao ya kijamii kuwa kwanini sijatoa pole sasa mimi sioni kama pole inalazimishwa.

“Kama binadamu hakuna anayependa mwenzake aumizwe lakini matukio ya kuumiza yametokea mara nyingi sana nchini, sasa mimi si chombo cha dola kunyooshea kidole mtu, sheria inasema kama kuna mtu unamhisi unaenda polisi,” alisema.

Alipoulizwa endapo amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema: “Nitaongea naye vipi na mwenyekiti wa chama wakati mimi nilishaachana na siasa za vyama.”

Alipoulizwa iwapo Mbowe akimpigia atakubali kuonanana naye alisema: “Sasa itategemeana na mazingira ya kuonana.”

Akizungumzia mwenendo wa siasa za upinzani hapa nchini, Dk. Slaa alisema haumfurahishi kwa sababu alishiriki kujenga upinzani lakini haoni chama chenye sera zilizonyooka.

“Mwelekeo wa siasa za upinzani nchini haunifurahishi, baada ya uhuru mwaka 1963 kulikuwa na vyama vingi, baadaye vikaanza kufa vyenyewe kwa sababu vilikatisha tamaa wananchi na baadaye vikaondoka kisheria.
 
“Sasa naona tena dalili hizo za mwaka 1963 kwa sababu hatuelekei pazuri…wanaongea juu juu lakini mikakati ya utekelezaji hakuna.

“Sioni uimara wa vyama na mkakati wa kutupeleka mbele, wanachofanya wanasubiri kiongozi wa serikali atoe kauli halafu wanakuja na kusema hili sio lakini hakuna sera mbadala,” alisema Dk. Slaa.

Kuhusu kuzuiwa mikutano ya siasa alisema hakubaliani na marufuku ya siasa kwa kuwa Bunge ndiyo ilipitisha lakini pia hakuna hati yoyote iliyotolewa na Rais John Magufuli kwamba mikutano ni marufuku.

“Sikubaliana na taratibu kuwa mikutano imepigwa marufuku, lakini mara kadhaa nimekuwa nahoji hawa wanasiasa wanionyeshe hati yoyote iliyotolewa na rais  kuwa mikutano imepigwa marufuku kwa sababu rais anafanya kazi kwa kufuata sheria,” alisema.

Prof. Jay azuiliwa kumuona Sugu

$
0
0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Nyasa kimedai kuwa mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof. Jay na mkewe wamezuiliwa kuwanona Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga katika Gereza la Ruanda ambako wamewekwa mahabusu.

Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’ akiwa ameambatana na Mkewe Grace Haule amefika Mbeya jana na leo tarehe 07 Februari 2018 ameenda katika Gereza la Ruanda mkoani humo kwa ajili ya kuwaona Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga ambapo amekataliwa kuwaona na uongozi wa Gereza hilo

Viongozi hao Sugu na Masonga wanaoshikiliwa kwa kunyimwa dhamana kesho Alhamisi tarehe 08 Februari 2018 watafikishwa mahakamani kwa ajili ya muendelezo wa kesi yao ambayo wanatuhumiwa kwa kutoa maneno ya fedheha.

Habari – CHADEMA
Kanda ya Nyasa
O7 Februari 2018.

Chadema Kanda ya Nyasa.

Tanzania Kinara Utawala Bora Afrika Mashariki....Pia imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika.

$
0
0
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani (2017 Democracy Index) iliyozinduliwa Februari 2,  mwaka huu  na kuchapishwa na  jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist  imeitaja  Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika maswala ya Utawala Bora kwenye  ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alisema kuwa Tanzania kuwa    nchi ya kwanza kwenye masuala ya Utawala bora imeweza kusaidia ukuaji wa Uchumi wake.

“Utawala Bora ni kigezo muhimu cha ukuaji wa uchumi na hata ustawi wa jamii, kama ambavyo Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani iliyotolewa na  jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist imeitaja Tanzania ni ya kwanza katika ukanda wa EAC, ikifuatiwa na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC.

Pia, ripoti ya Foresight Afrika  na taarifa ya  Uchumi ya Benki ya Dunia vyote vimeitaja Tanzania kuwa katika nchi tano Bora za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi katika mwaka 2018, nchi hizo ni Ghana, Ethiopia, Kodivaa , Senegali na Tanzania”.

Aidha, Dkt. Abbasi alisema kuwa ukuaji huo wa uchumi ni dhamira isiyoyumba ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, ikiwa ni   pamoja na kuhakikisha uchumi mkuu unaendelea kujiakisi katika maisha ya watanzania kupitia utoaji wa huduma kwa wananchi na kuboresha sekta mbalimbali.

Katika sekta ya Afya, Dkt. Abbasi alisema kuwa pamoja na ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea nchi nzima na uboreshaji wa hospitali, Serikali imetenga  bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka Bilioni 31 mwaka 2015 hadi Bilioni 269. Aidha, bajeti ya sasa imewezesha Serikali kuboresha  usambazaji wa dawa hadi kufikia asilimia 86 ya uhakika wa kupatikana dawa muhimu.

Bajeti hiyo imewezesha  ukarabati wa  wodi 5 za ICU na kuongezwa vitanda kutoka 21 mpaka 75,  kununua  mashine mpya za CT-Scan yenye uwezo mkubwa imenunuliwa katika hospitali ya Muhimbili na Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya fahamu (MOI)  zenye uwezo mkubwa ambapo wastani wa wagonjwa wanaopimwa imepanda kutoka 20 hadi 50 kwa siku.

Vifaa vingine vilivyonunuliwa ni pamoja na mashine 14 za upasuaji (diathermy machines) na mashine za kuchuja damu kwa ajili ya wagonjwa wa figo zipatazo 25 na kuongeza uwezo wa kuhudumia wagonjwa kutoka 68 kwa siku hadi 126.

Uboreshaji huo wa sekta ya afya umeifanya  Muhimbili kuwa hospitali ya kwanza ya umma katika ukanda wa Afrika Mashariki kutoa huduma za juu za kibingwa hasa oparesheni ya kuweka vifaa vya kusaidia kusikia  ambapo watoto 5 waliokuwa awali hawasikii kabisa walifanyiwa oparesheni mwaka jana na kusikia kwa mara ya kwanza katika maisha yao.  Wengine 6 wamefanyiwa wiki iliyopita.

Katika sekta ya Sekta, Msemaji  huyo wa Serikali alisema kuwa lengo la Serikali ni  kufikisha huduma ya maji kwa asilimia 85 vijijini ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 67.7 mwaka 2015, makao makuu ya mikoa asilimia 95, Dar es Salaam asilimia 95 na  miji mikuu ya wilaya asilimia 90 ifikapo 2020. 

Ambapo hadi sasa kwa ujumla kuna takribani miradi 1,423 imekamilika na kuna vituo vya maji 117,190 vyenye uwezo wa kuhudumia watu milioni 29 sawa na asilimia 79. Katika miaka hii miwili pekee zaidi ya miradi 388 ilikamilishwa.

Dkt. Abbasi, anafafanua kuwa katika usambazaji wa umeme mijini na vijijini kazi imeendelea kwa kasi kubwa. Katika kutekeleza Mradi wa REA III, kiasi cha shilingi bilioni 985.9 zitatumika kuwafikishia wananchi umeme katika programu maalum iliyoanza kutekelezwa.

Alisititiza kuwa, “Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, imedhamiria kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi si tu  kwa maneno bali kwa vitendo, mfano namna ambavyo Serikali imeongeza wigo wa barabara vijijini na mijini, pamoja na kuundwa kwa  wakala maalum (TARURA) ambao utajikita zaidi katika kuharakisha ujenzi wa barabara za vijijini”

Aliongeza kuwa mwaka huu Serikali inakusudia kutekeleza upanuzi wa njia za mwendokasi jijini Dar es Salaam kwenda njia za barabara ya Kilwa kwenda Mbagala yenye urefu wa  kilomita 19 na barabara ya Uhuru kwenda Gongolamboto yenye urefu wa kilomita 23.9.

Aidha, Dkt Abbasi amewakumbusha watanzania  kuwa wazalendo, kuunga mkono jitihada za Serikali kufanya kazi kwa bidii,  kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano inasisitiza wananchi kufanyakazi ili kuijenga Tanzania uitakayo.

Serikali yatangaza kuboresha mishahara

$
0
0
Serikali ya Tanzania imeahidi kuanza kuboresha maslahi ya watumishi ya walimu ikiwemo mishahara yao kipindi hiki kutokana na kumaliza zoezi la muda mfupi la uhakiki wa wafanyakazi hewa katika sehemu mbalimbali za ajira.

Hayo yamewekwa wazi na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Joseph kakunda leo (Jumatano) katika mkutano wa 10 kikao cha saba cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa alipotaka kujua ni lini serikali itawapandishia mishahara walimu.

"Utaratibu huu ambao ulikuwa umesimama kwa kipindi kifupi cha miaka kama miwili hivi kupisha uhakiki wa watumishi ambapo ni zoezi lililofanywa kwa umahiri na ueledi mkubwa, baada ya kuwa tumelikamilisha sasa tutaingia kwenye awamu ambayo ni ya kuboresha maslahi ya watumishi ikiwemo mishahara yao", amesema Kakunda.

Kwa upande mwingine, Mhe. kakunda amewatoa hofu walimu wote ambao hawakupandishwa madaraja yao kutokea mwaka 2016 hadi 2017 na kudai katika mwaka huu wa fedha wameshafanya matayarisho wa kupandisha madaraja hayo.

Msigwa amchana Kigwangala Bungeni

$
0
0
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe. Peter Msigwa amefunguka na kumchana Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala na kudai kuwa anafanya kazi kwa mizuka na mihemko na kuisumbua sekta ya Utalii na Maliasili nchini.

Msigwa amesema hayo wakatii alipokuwa akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, mjini Dodoma na kudai kuwa Mawaziri vijana wamekuwa na mihemko.

"Niwashauri hawa Mawaziri vijana fursa 'opportunity is atrracted by talent, skills, perfomance and abillity. Show your talent and abillity,m people will love you' 

"Hawa Mawaziri wa zamani hawa kwa mfano Lukuvi, Tizeba tunawaona wakijibu hoja wanajibu hoja siyo za kimihemko kiasi kwamba unaridhika hata Waziri akikujibu unapenda lakini Mawaziri vijana wengi mnaonekana mnayofanya katika Serikali hii kiasi kwamba Serikali ijayo muonekane hamna tija" kwa sababu mna mihemko sana"

Mbali na hilo Msigwa alikwenda mbali zaidi na kumnyooshea mkono Waziri wa Maliasili na Utalii na kudai amekuwa na maamuzi ya ajabu jambo ambalo linapelekea kiongozi huyo kuivuruga Wizara hiyo.

"Utalii huu umejengwa kwa muda mrefu sana na akitokea mtu mmoja anaamua kufanya tu kwa kutafuta umaarufu atauvuruga kwa muda mfupi sana

" Utalii kwenye pato la taifa unaingiza asilimia 20 na forex ni kubwa inatokana na utalii kwa hiyo hicho si kitu kimoja mtu anaweza kuamka leo anasema nimeharibu na hii diplomasia ya kiuchumi inategemea sana na kutabirika, wawezekaji huko nje wanataka kuona kunatabirika wao kufanya biashara zao. 

"Haiwezekani huyu Waziri anatoa amri mpaka mapolisi wanamkataa anashindwa hata kuwasiliana na Waziri wake wa Mambo ya Ndani, huyu huyu Waziri anatoa amri anapingana na Waziri wa Ardhi, huyu huyu Waziri mmoja anapingana na Waziri wa Uvuvi hatuwezi kuwa na Mawaziri ambao wanakuwa na mizuka na kufanya kazi kwa mizuka wote kama tunalipenda taifa letu tufanye kazi kwa kupendana" alisisitiza Mchungaji Msigwa

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya February 8

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images