Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Spika wa Bunge, Job Ndugai atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya Askari wa JWTZ nchini DRC.

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ametuma salamu za rambi rambi kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, kufuatia vifo vya askari 14.

Spika Ndugai amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya askari hao ambao walikuwa wakilinda amani nchini Kongo, pamoja na wengine 44 waliojeruhiwa kufuatia mashambulizi yanayotekelezwa na askari waasi nchini humo.

Kufuatia tukio hilo, Spika Ndugai ametoa pole kwa familia za askari hao waliouawa, na kuwaombea wale waliojeruhiwa kupona haraka na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.

Israel yaifyatulia Palestina Makombora

$
0
0
Jeshi la Israel limefyatua makombora kadhaa kuelekea eneo la Gaza, Palestina ikilenga wapiganaji wa kundi la Hamas.

Jeshi hilo la Israel limeeleza kuwa katika mashambulizi hayo lilipiga maeneo ya viwanda vya uzalishaji wa silaha na maghala ya silaha ya Hamas, mapema leo. Hata hivyo, kwa mujibu wa Independent, makombora hayo yalileta madhara katika maeneo ya makazi yakigusa pia watoto.

Hamaki kati ya Israel na Palestina iliongezeka wiki iliyopita baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Israel imekuwa ikidai Jerusalem ni mji wake mkuu wakati Wapalestina wakiendelea kudai upande wa Mashariki mwa mji huo kuwa eneo lao muhimu lililotwaliwa na Israel katika vita ya mwaka 1967.

Jana, kiongozi wa Hamas, Fathi Hammad alisema kuwa Taifa lolote litakalohamishia ubalozi wake Jerusalem litakuwa ‘adui wa Wapalestina’.

Tanzania kupitia Waziri wa Mambo ya Nje, Augustine Maige imeweka wazi msimamo wake kuwa haitahamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.

“Hatuna ulazima wa kuhamisha ubalozi wetu. Unapaswa kufahamu kuwa ubalozi wa Tanzania nchini Israel utabaki kuwa Tel Aviv na hakuna mpango wa kuuhamishia Jerusalem ingawa kumekuwa na jitihada za kutushawishi kufanya hivyo,” Waziri Maige anakaririwa na The Citizen.

Uamuzi wa Trump umepokelewa kwa hisia tofauti na mataifa mengi huku ikielezwa wazi kuwa utakwamisha mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.

Breaking News: Rais Magufuli katoa msamaha kwa Babu Seya na Familia yake

$
0
0
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, ametangaza msamaha kwa Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza (Papii Kocha) ambao waliofungwa maisha katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na kutaka waachiwe huru mara moja kutoka gerezani.

“Tanzania tuna jumla ya wafungwa 39,000 ambapo wanaume ni 37,000 na wanawake 2,000.  Wafungwa waliohukumiwa wako 522 kati yao wanaume ni 503 na wanawake ni 19. Nimeamua kusamehe wafungwa 8157, ambapo baada ya msamaha huu wafungwa 1828 watatoka leo.

“Mfano wa watu niliowasamehe ni Mzee Mganga Matonya mwenye umri wa miaka 85 amekaa Gerezani miaka 37 na miaka 7 ya kukaa mahabusu. Nimeamua kusaheme familia ya Nguza Viking jina lingine anaitwa Babu Seya na Ndugu Johnson Nguza ama Papii Kocha.

“Nimeamua kuwasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa. Lakini katika kuchunguzwa kwingi wapo wafungwa ambao wametubu dhambi zao, wamekiri makosa yao kwelikweli,” alisema Magufuli.

Mwaka 2003, Babu Seya na wanaye watatu walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kubaka na kulawiti watoto wa Shule ya Msingi Mashujaa, mwaka 2004, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar iliwahukumu wote wanne kifungo cha maisha jela.

Baada ya hukumu hiyo, walikata rufaa lakini mwaka 2005, Mahakama Kuu iliridhia hukumu hiyo ya kifungo cha maisha jela kwa wote wanne kabla ya Mahakama ya Rufaa kuwaachia huru Mbangu na Chichi Februari 2010.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Disemba 10

Mrema azungumzia uamuzi wa Rais Magufuli Kusamehe Wafungwa

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amepongeza uamuzi wa Rais John Magufuli wa kutoa msamaha kwa wafungwa na kumuelezea kama Rais mwenye upendo wa aina yake.

Mrema amesema ni wazi kuwa Rais amesikia kilio cha watu na kuamua kufanya ubinadamu ili kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.

“Namvulia kofia kabisa, huyu ni Rais  msikivu, ana mapenzi ya kweli kwa Watanzania naweza kusema tumepata mtu ambaye tulikuwa tunamtaka,”

Mrema amesema upo uwezekano kuwa Rais alikuwa hapewi taarifa sahihi kuhusu hali ya magereza.

“Magerezani kuna uozo, wapo watu wengine wanajaa kule kwa makosa ambayo wanaweza kulipa faini tu wakatoka,”

“Nilianzisha kampeni ya kuwalipia faini wafungwa ambao walishindwa kujilipia lakini kutokana na maslahi ya baadhi ya watu nikaambiwa nisitishe kwa madai kuwa wafungwa hao hawajajutia makosa. Hii si sawa, naomba watu wa magereza wabadilike hakuna sababu ya kuwajaza wafungwa kule ambao wanatakiwa kutoka,”

Chadema wadai Rais Magufuli ametekeleza ahadi ya Lowassa Kumwachia Babu Seya

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimempongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ahadi zilizotolewa na mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa ikiwemo ya kuwaachia huru wanamuziki Nguza Viking na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.

Taarifa iliyotolewa jana  Jumamosi na chama hicho ilieleza kuwa katika ahadi zake Lowassa aliahidi iwapo Chadema ingeshinda uchaguzi angewaachia wanamuziki hao.

Vilevile chama hicho  kimetoa wito kwa  Serikali kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa sheria kuondoa nia ya kuwashtaki masheikh wa Zanzibar na mahabusu na washtakiwa wa makosa ya mtandao.

==>Hii ndo kauli ya CHADEMA
Tunampongeza Rais John Pombe Magufuli kwa ujasiri wa kuendelea kutekeleza baadhi ya ahadi zilizotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mgombea wa Urais, Mhe. Edward Lowassa, wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ambapo leo akihutubia sherehe za siku ya Uhuru wa Tanganyika, ametoa msamaha kwa waliokuwa wafungwa wa kifungo cha maisha, Ndugu Nguza Vicking (Babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha).

Kutokana na kitendo alichofanya leo Rais Magufuli kwa kutumia ibara ya 45 ya Katiba ya Nchi, kama ambavyo mgombea wetu wa urais aliahidi iwapo CHADEMA ingeshinda uchaguzi, kushika dola na kuongoza Serikali, Chama kinatoa wito kwa Serikali itumie mamlaka yake kwa mujibu wa sheria za nchi, hususan kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa utaratibu wa *Nolle Prosqui*, iondoe nia ya kuendelea kuwashtaki;

1. Masheikh wa Zanzibar wanaoshtakiwa Mahakama ya Kisutu, Tanzania Bara.

2. Mahabusu na watuhumiwa wa makosa ya mitandao.

3. Watuhumiwa na mahabusu wa makosa ya kisiasa, ikiwemo kesi za uchochezi, zinazohusisha kumkosoa Rais Magufuli, kuikosoa Serikali yake na chama chake au tuhuma zinazotokana na kutekeleza shughuli halali za kisiasa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi, ikiwemo maandamano, mikutano ya hadhara na vikao vya ndani.

Imetolewa  Jumamosi, Desemba 9, 2017 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Babu Seya na Papii Kocha Baada ya Kuachiwa Huru Jana Jioni

$
0
0
Mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wametoka katika gereza la Ukonga jana jioni  baada ya kusota kwa miaka 13.

Wanamuziki hao ‘baba na mwana’ walitoka katika kifungo cha maisha baada ya kupata msamaha wa Rais John Magufuli  jana Jumamosi Desemba 9, mwaka 2017.

JPM alitoa msamaha kwa baadhi ya wafungwa alipokuwa akihutubia Taifa kusherehea miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miongoni mwa waliopata ahueni hiyo ni Babu Seya na Papii Kocha.

“Babu, babu, babu,” zilikuwa ni kelele za mashabiki na ndugu zake waliompokea Babu Seya na Papii Kocha waliokuwa wametoka gerezani wakiwa na magitaa yao mgongoni.

Babu Seya aliyeonekana mtanashati alionekana anapunga mkono wa kulia kama mtu asiyeamini huku Papii Kocha akipunga mkono akionekana kufurahia na kuzungumza na mashabiki.

Walisindikizwa na askari magereza mpaka nje na kulikuwa na foleni kubwa kutokana na tukio hilo.

THBUB yampongeza Rais kwa kuwafutia watu 61 adhabu ya kifo

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga kwa niaba ya Tume na Wafanyakazi wote wa THBUB anachukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kufuta adhabu ya kifo kwa watu 61 waliokuwa magereza mbalimbali nchini, wakisubiri utekelezaji wa adhabu ya kifo dhidi yao.

Tume inampongeza sana Mhe. Rais kwa uamuzi wake huo kwani unaendana na Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Na. 62/149 la tarehe 18 Desemba 2007 linalozitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kufuta au kusimamisha utekelezaji wa adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala.

Tume inatambua kwamba, kama alivyosema Mhe. Rais, msamaha huu haufuti adhabu ya kifo katika sheria za nchini.

Hivyo, kutokana na mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 130(1) (g), Tume inapenda kuchukua nafasi hii kuishauri Serikali kuona uwezekano wa kufuta adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala, ili iendane na Azimio la Umoja wa Mataifa  lililotajwa hapo juu.

Pia, Tume inaisihi Serikali, hususan Idara yake ya Ustawi wa Jamii kuwasaidia, na Wananchi kwa ujumla kuwapokea, wale wote waliopewa msamaha ili waweza kuendelea na maisha yao kama raia wema katika jamii.

Imetolewa na:   
Mhe. Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Desemba 9, 2017

Mnyika aungana na Rais Magufuli

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika kuomboleza vifo vya askari 14 waliouawa nchini Kongo na wengine kujeruhiwa, huku akiwapa pole wafiwa wote.

Mbunge wa Kibamba ameitumia Jumapili ya leo Disemba 10,2017  kuwaombea mashujaa hao na kuwapa pole wanafamilia wote ambao ndugu zao wamepoteza maisha katika tukio hilo.

"Kwa kipekee naitoa ibada ya leo kuwaombea Mashujaa wetu,askari 14 wa JWTZ waliojitoa mhanga na maisha yao kuitetea amani Congo, 44 ambao wamejeruhiwa na wale wawili (2) ambao hawajulikani walipo. Mungu awajalie pumziko jema kwa wale waliopoteza uhai kupigania amani

"Awape uponyaji majeruhi na kusaidia kupatikana kwa Askari wawili. Aijalie faraja na ustawi familia za wahanga na wote ambao wameguswa kwa moja kwa moja au namna ingine yeyote na tukio baya hilo" aliandika John Mnyika

Mwenyekiti UVCCM ashikiliwa na Takukuru

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma inamshikilia Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis kwa tuhuma za kugawa rushwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi.

UVCCM leo Jumapili Desemba 10,2017 inachagua viongozi wapya wa ngazi ya Taifa watakaoongoza jumuiya hiyo ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano.

Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge, Zanzibar amekamatwa nyumbani kwake karibu na mnada wa zamani mkoani Dodoma.

Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma, Emma Kihanga amethibitisha kukamatwa kwa mwenyekiti huyo na kwamba watatoa taarifa zaidi baadaye.

"Ni kweli tumemkamata tangu jana usiku tumekesha tunafanya uchunguzi, nitatoa taarifa baadaye kuhusu tukio hilo," amesema.

Mkutano mkuu wa uchaguzi wa UVCCM unaendelea mjini Dodoma na miongoni mwa waliohudhuria ni Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akifunga mkutano mkuu wa uchaguzi wa Umoja wa Wanawake (UWT) jana Jumamosi Desemba 9,2017 alisema hawajapokea malalamiko mengi kutoka umoja huo na kuzitaka jumuiya nyingine za CCM kujifunza UWT.

Rais Magufuli atia saini nyaraka za kuachiwa Babu Seya na wenzake

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba, 2017 ametia saini nyaraka za msamaha alioutoa jana kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking (Babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela.

Mhe. Rais Magufuli ametia saini nyaraka hizo Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kuwapongeza Jeshi la Magereza kwa kazi nzuri wanayoifanya kurekebisha tabia za wafungwa wa makosa mbalimbali.

Mhe. Rais Magufuli amesisitiza kuwa pamoja na kutolewa kwa msamaha huo, vyombo vya dola viendelee kusimamia sheria, na kwa Jeshi la Magereza amelitaka kuhakikisha linawatumia wafungwa kuzalisha mali ikiwemo kuzalisha mazao ya kilimo na kufanya kazi za ujenzi.

“Nimeona nitumie kifungu hiki cha Katiba (Ibara ya 45 {1}) ambacho nilipewa na Watanzania, ingawa kilikuwa hakijawahi kutumika, unajua mtu ambaye alihukumiwa kunyongwa halafu baadaye anaachiwa, ni kitu kinashangaza kwa sababu hakijawahi kutokea, lakini nimeona nifanye hivyo kwa ajili ya Watanzania”

“Mimi nikuombe tu, muendelee kusimamia wajibu wenu na kusimamia sheria, mtu anayehukumiwa kufungwa afungwe kweli, na nilishatoa wito kwa magereza, pasiwepo wafungwa wa kukaa tu na kupumzika, wafanye kazi, kufungwa sio kustarehe” Amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutoa msamaha huo wa kihistoria na kubainisha kuwa wafungwa na Maafisa Magereza wameipongeza hatua hiyo, ambayo itasaidia kuwatia moyo wafungwa wanaorekebishwa tabia katika magereza mbalimbali nchini.

Kamishna Jenerali Malewa amesema wafungwa waliopatiwa msamaha wa kuachiwa huru, waliruhusiwa kutoka magerezani tangu jana na Maafisa Magereza wamewaasa kwenda kuonesha mfano bora kwenye jamii watakakwenda kuishi.

Katika hatua nyingine Mhe. Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kutekeleza agizo lake la kutengeneza viatu kwa ajili ya askari wake badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi.

Jeshi la Magereza linazalisha jozi 150 za viatu kwa siku katika kiwanda chake cha Karanga kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, na kwa kushirikiana na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF limeanza kuboresha kiwanda hicho ili kufikia uzalishaji wa jozi 450 kwa siku.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino, Dodoma

10 Desemba, 2017

JWTZ Wazungumzia Vifo vya Wanajeshi 14

$
0
0
Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania limesema kikundi chake cha ulinzi na usalama kilichopo DRC kwaajili ya kutekeleza jukumu la ulinzi na amani kilivamiwa na Waasi waliojilikana kuwa ni ADF na kusababisha mauaji kwa wanajeshi 14.

Amesema kwamba tukio hilo lilitokea katika eneo la kambi iliyopo daraja kwenye mto Simulike barabara ya kutokea Oicha kwenda Kamango mpakani mwa nchi ya Uganda Kaskazini Mashariki ya wilaya ya Beni Jimbo la Kivu Kaskazini.

Akithibitisha mauaji hayo muwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania (CDF) Luteni Jenerali James Mwakibolwa amesema shambulio hilo lakuvamiwa lilizusha mapigano baina ya kikundi hicho na kile cha waasi na yalidumu kwa takribani masaa kumi na tatu (13) na kusababisha vifo vya askari wa Tanzania 14 na wengine 44 kujeruhiwa na askari wawili bado hawajulikani walipo ambapo jitihada zaidi za kuwatafuta zinaendelea.

Amesema shambulizi la tarehe 7 kuamkia tarehe 8 Desemba lilikua baya zaidi kuwahi kuitokea tangu vikosi hivyo vianze kushiriki ulinzi wa amani nchini DRC mwaka 2011 kwakua limeleta madhara makubwa, hata hivyo kikundi hicho ambacho bado kipo huko kinauwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu husika kwa uhodari wa hali ya juu ,ushupavu, weledi mkubwa na umahiri stahiki.

Kwa niaba ya mkuu wa majeshi Luteni Jenerali Mwakibolwa amewathibitishia watanzania kuwa tukio hilo halitawavunja moyo na kamwe Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania halitatetereka kupeperusha bendera yake ndani na nje ya nchi kwani tukio hilo limewaongezea nguvu, ari ,ushupavu na uhodari zaidi katika kutekeleza majukumu yake.

Aidha amesema nchi pia iko salama na itaendelea kuwa salama na yeyote ambaye anataka kuwajaribu atashughulikiwa ipasavyo kwani historia ya jeshi inadhihirisha uwezo thabiti.

Kuhusu taratibu za kusafirisha miili ya marehemu kuirejesha nchini zinafanyika chini ya utaratibu wa Serikali na umoja wa mataifa na JWTZ na serikali wanaendelea kuchukua hatua stahiki kufuatia tukio hilo ikiwemo kufanya uchunguzi katika eneo husika sambamba na kuangalia taratibu za kuwajulisha familia za wafiwa zimekamilika na ndio maana hawakuweza kutoa taarifa hizo bila kuwaweka sawa familia za mashujaa hao.

Kwa umoja wa watanzania amewataka kuwaombea dua roho za mashujaa hao zipumzike mahali pema peponi kwa amani na majeruhi wote wapone haraka iwezekanavyo ili warejee kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ulinzi wa taifa na dunia nzima.

Msando Awalipua UVCCM Mbele ya Rais Magufuli

$
0
0
WAKILI Alberto Msando, ambaye alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea chama ACT-Wazalendo, leo akiongea kwenye mkutano wa UVCCM Taifa, unaoendelea Dodoma, amefunguka na kuwachana vijana wa chama hicho (UVCCM) baada ya viongozi wake aliodai walimdanganya Mwenyekiti wa CCM,  John Pombe Magufuli juu ya idadi wa vijana wao.

Albert Msando aliomba nafasi kwa Rais Magufuli ili aweze kuwasema vijana hao wa CCM baada ya moja ya taarifa yao kusema wapo vijana wa CCM zaidi ya milioni sita,  jambo ambalo linapingana na taarifa zao wenyewe.

“Nimeazima taarifa ya utekelezaji na mpango mkakati naona mmesema kwamba UVCCM mpo milioni sita.  Je, ni kweli? Kama vijana mtakuwa mnafanya mambo kama haya, tutakuwa na nchi ya hovyo sana na chama cha hovyo sana.  Mmeandika takwimu zinazoonyesha kuwa idadi ya vijana wenye umri kati ya 14 na 35 ni asilimia 34 ya watu wote nchini. Mara tu baada ya ukurasa wa nane, ukurasa wa tisa mmeandika kundi la vijana ni kubwa, takwimu zinaonyesha sasa wamefikia asilimia 65 ya idadi ya watu nchini.  Ina maana hatujijui tupo wangapi?” alihoji Msando

Akiendelea kuonyesha mapungufu hayo, Msando alisema:

“Kwenye kitabu hiki mmemwambia Rais Magufuli kuwa vijana wa UVCCM mnafika milioni sita lakini kwenye jedwali la kweli mmeandika idadi ya vijana wa UVCCM kila mkoa tangu 2013 hadi 2017 jumla walio hai ni milioni moja laki sita,  wasio hai ni laki nne.  Sasa kwa nini mmdanganye Rais? Tukafanye kazi na hizi ndiyo takwimu zenu,  sasa hivi mnamwambia Rais tunakaribia milioni sita.  Mnataka Rais aondoke akiwa na picha ya kuwa mpo zaidi ya milioni sita wakati mpo milioni moja laki tano?  Jamani hatuendi hivyo,  tunakata CCM mpya ya vijana wachapa kazi,  Wanachama wote ambao hawapo hai warudi, tupate wanachama wapya, ” alisema Msando.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu yya Disemba 11

Fahamu Uhusiano Uliopo Kati Ya Unene & Uzito Kupita Kiasi ( Overweight & Obesity ) Na Tatizo La Ukosefu & Upungufu Wa Nguvu Za Kiume.

$
0
0
Unene  na  uzito  uliozidi  ( Obesity )  ni  miongoni  mwa  vyanzo  na  visababishi  vikuu  vya  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Kwa   mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitabibu, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wenye   unene  na  uzito  uliozidi, wanakabiliwa  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

KWANINI  WANAUME  WENYE  UNENE  NA  UZITO  ULIOZIDI  WANAKABILIWA  NA  HATARI  KUBWA  YA  KUPATWA  NA  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Wanaume  wenye  uzito na  unene  uliozidi  wapo  katika  hatari  kuu  ya  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuna  uhusiano mkubwa  kati  ya  unene/uzito  uliozidi  pamoja  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.

Kama  tulivyo elezea  katika  makala  zetu  za  nyuma,  SUALA  LA NGUVU  ZA  KIUME NI  SUALA  LA  KIMFUMO.  Mfumo  wa  nguvu  za  kiume  unahusisha  ogani  mbalimbali  katika  mwili  wa  mwanadamu.

Ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, ni  lazima  ogani  zote  zinahusika  katika  mfumo, ziwe  imara  na  zenye  afya  njema, na  pia  ni  lazima  ziwe  na  ushirikiano  imara.

Kudhoofishwa  kwa  ogani  moja  wapo  kati  ya  ogani  hizo  kutasababisha  mhusika  apatwe  na  tatizo  la  ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Kwa  kukumbushia  tu,  mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa   nguvu  za  kiume  yapo  matano  ambayo  ni

1. Ubongo  imara  na  wenye  afya  njema

2. Mishipa  imara  ya  kusafirishia  damu  mwilini

3. Mfumo  imara  na  wenye  afya  wa usafirishaji  damu  mwilini.M .3

4.Mishipa  na  misuli  ya  uume  iliyo  imara na  yenye  afya  njema

5.Pamoja  na  uhusiano  imara  na  wenye afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyo katika  ubongo  ( nerves),mishipa  ya kwenye  uti  wa  mgongo  ( spinal  cords ) pamoja  na  mishipa  & misuli  ya  kwenye uume.

Sasa  basi, hitilafu  yoyote  katika  mojawapo  kati  ya  mambo  matano  tajwa  hapo  juu, itamfanya  mhusika  apatwe  na  tatizo  la  ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

UNENE  NA  UZITO  ULIOZIDI   UNA  SABABISHA  VIPI  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA/AMA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kwa lugha nyepesi  na  yenye  kueleweka  kwa  kila  mtu,  mtu mwenye  unene  na  uzito  uliopitliza, maana  yake  ni  kwamba  ana  mafuta  , sukari  na  kolestrol  nyingi  katika  damu  yake.

Kwa  maana  nyingine, ni kwamba  kama  wewe  una  unene  uliopitiliza, maana  yake ni  kwamba, ogani  zilizomo  ndani  ya  mwili  wako  zinaogelea  katika  mafuta  yaliyomo  ndani  ya  mwili wako.

1.  Kolestrol   nyingi   katika  damu, huathiri  mfumo  usafirishaji  damu  katika  mishipa  ya  inayo  tumika  kusafirisha  damu  katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili  ikiwamo  katika  mishipa  ya  kwenye  uume. Matokeo  yake  basi  , kolestrol  hiyo  husababisha  kuziba  kwa  ateri  ambayo  ndio  njia  itumikayo  kupeleka  damu  katika  mishipa  na  misuli  ya  kwenye  uume, na  kama  damu  haitaweza  kusafirishwa  hadi  kwenye  mishipa  ya  kwenye  uume, maana  yake  ni  kwamba, mwanaume  huyo  hatokuwa  na  uwezo  wa  kusimamisha  uume  wake  kwa  sababu, damu  ndio  inayo  ufanya   uume  uweze  kusimama.

2. Kama  ilivyo  kwa  kolestrol, sukari  na  mafuta  mengi  katika  damu  huathiriki  utiririkaji  wa  damu   mwilini  na  hivyo  kufanya  vigumu  damu  kutiririka  kuelekea  kwenye  mishipa na misuli   ya  uume  ambayo  ndio  inahusika  na  kuufanya  uume   usimame.

3. Unene  na  uzito  uliopitiliza  una  uhusiano  mkubwa  sana  na  ugonjwa  wa  kisukari. Na  ugonjwa  wa  kisukari nao  una  uhusiano  mkubwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, kwa  sababu  unaathiri  mfumo  mzima  wa  nguvu  za  kiume  kama  ifuatavyo : Kwanza;unashambulia  na  kudhoofisha  mishipa  ya  ubongo  na  kuifanya  ishindwe   kuwa  na  uhusiano  mzuri  na  mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo, pamoja  na  mishipa  na  misuli  ya  kwenye  uuume. Pili unashambulia na  kudhoofisha  mishipa  ya  usafirishaji  damu  mwilini na  tatu  unasababisha  kudhoofika  kwa  ogani  muhimu  katika  mwili  wa  mwanadamu  kama  vile  figo.

Hivyo  basi, mwanaume  mwenye  unene  na  uzito  ulio zidi, yupo  katika  hatari  kubwa  sana  ya  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, kuliko  inavyo weza  kufikiriwa.

4. Unene  na  uzito  uliopitiliza  una  uhusiano  mkubwa  na  tatizo  la  shinikizo  la  damu. Kwa  lugha  nyingine  ni  kwamba, watu  wanene  wapo  katika  hatari  kubwa  sana  ya  kupatwa  na  tatizo  la  shinikizo  la  damu,. na  tatizo  la  shinikizo  la  damu  nalo  lina  uhusiano  mkubwa  sana  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Shinikizo  la  Damu husababisha  mishipa  ya  ateri  ambayo  hutiririsha  damu  iingiayo  kwenye  uume  kuziba  na  kushindwa kutanuka  kwa  kiwango  inachotakiwa  kutanuka.

Pia  huifanya  mishipa  laini  katika  uume   kushindwa  ku-relax  na  hivyo  kushindwa  kuizuia  mishipa  ya  vena  ya  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  kwenye  maeneo  mengineyo  ya  mwilini.

Matokeo  yake  kunakuwa hakuna  kiasi  cha  kutosha  cha  damu  iingiayo  kwenye  uume  na  hivyo  kufanya  uume  ushindwe  kusimama.

Vile  vile  hata  kiasi  kidogo  cha  damu  kinacho  ingia  kwenye  uume, kinashindwa  kuendelea  kuhifadhiwa  ndani  ya  uume  wakati uume  ukiwa  umesimama, na  matokeo yake  ni  uume  kusinyaa  ndani  ya  kipindi kifupi  sana  tangu  usimame.

Kama  hiyo  haitoshi, tatizo  la  unene  na  uzito  kupita  kiasi  lina  weza  kupelekea  mhusika  kupatwa  na  magonjwa  ya  presha  na   moyo  ambayo  nayo  yanachangia  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  kiasi  kikubwa  sana.

SULUHISHO  LA  TATIZO  NI  NINI?
Kama  wewe  ni  mwanaume  mwenye  tatizo  la  unene  na  uzito  ulio zidi, unapaswa  kufanya  mambo  yafuatayo:

i.  Kupunguza  kolestrol   mwilini: Unaweza  kupunguza  kolestrol  na  mafuta  mengi   mwilini  kwa  kufanya  mazoezi  na  diet  ama  kwa   kutumia   dawa  mbalimbali    za  asili  ama  vyote  kwa  pamoja.

ii.  Unapaswa  kupunguza  unene  na  uzito  : Unaweza  kupunguza  unene  na  uzito  kwa  kutumia  mazoezi na  diet  ama  kwa  kutumia  dawa  asilia  ya  MKATAA  KITAMBI  ambayo  inasaidia  sana  kupunguza  mafuta  mwilini, kupunguza  unene  na  uzito.

TIBA  ASILIA  YA  NGUVU  ZA  KIUME  KWA  WANAUME  WENYE  UNENE & UZITO  ULIOZIDI.
Kwa  mwanaume  mwenye  unene &  uzito  uliozidi  ambaye  pia  ana  sumbuliwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, anashauriwa  kutumia  dawa  zifuatazo kwa  pamoja

1.  Dawa  ya  kuondoa  kolestrol  na  mafuta  mengi  kwenye  damu.

2.  Dawa  ya  kupunguza  unene  na  uzito  pamoja  na

3. Dawa  asilia  ya  nguvu  za  kiume  iitwayo JIKO  ambayo  inatibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  ukosefu na/ama upungufu  wa  nguvu  za  kiume  ndani  ya  siku  thelathini  tu.

Dawa  ya  JIKO  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI.

Dawa  ya JIKO  pamoja  na  dawa  za  kuondoa  kolestrol   & mafuta  mwilini, kupunguza  unene  na  uzito  zinapatikana  katika  duka  la  kuuza  dawa  asilia  la  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM, katika  eneo  la  TABATA  MAKOKA  karibu  na  Shule  ya  Sekondari ya  Mt. ANNUARITE.

AU 

Ubungo  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING, nyuma  ya jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  wateja  waliopo  jijini  DAR  ES  SALAAM, ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu,  watapelekewa  dawa  mahali  walipo  ( DELIVERY )

Kwa  wateja  wa  ZANZIBAR  watatumiwa  dawa  kwa   njia  ya  boti.

Kwa  wateja  wa mikoani, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya   MABASI na

Kwa  wateja  wa  ughaibuni, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya   POSTA  au DHL.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu   tiba  asilia  ya  magonjwa  mbalimbali, tembelea  kila  siku :www.neemaherbalist.blogspot.com

Ado Shaibu : “Sijaona hoja yoyote ya maana ya kunifanya niondoke ACT”

$
0
0
Ikiwa vuguvugu la kuhama kwa wanasiasa limepamba moto nchini, Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema haoni hoja ya msingi itakayo mshawishi kukihama chama hicho.

Ado aliyasema hayo Novemba 9, 2017 siku moja baada ya aliyekuwa Mgombea kiti cha Urais kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia ACT ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa chama hicho, Mama Anna Mgwira kuhamia CCM, uamuzi alioutangaza kwenye Mkutano wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) uliofanyika mjini Dodoma.

Ado alifunguka kuwa, katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ambacho hakuwepo kwenye mitandao ya kijamii na kupatikana kwenye simu iliyozoeleka, kuna baadhi ya watu baada ya kurejea hewani, walimtumia jumbe zenye kuhoji kama ameshahamia CCM kutoka ACT.

“Jibu langu kwao lilikuwa jepesi. Siasa halisi si mzaha Kama mchezo wa komborera. Kwamba Leo ujifiche hapa kesho pale Kisha ubutue. Siasa ni itikadi. Siasa ni falsafa. Siasa ni sera. Siasa ni hisia za watu waliokuamini na kukuheshimu. Ukiheshimu Itikadi, falsafa, sera na hisia za watu waliokuheshimu na kukutumaini ndani na nje ya chama, hauwezi kuhama hovyo Kama wacheza komborera wanavyobadili maficho yao,” alisema na kuongeza.

“Kuhama Chama ni lazima kusukumwe na hoja za msingi na zenye mashiko. Kwa sasa, sijaona hoja yoyote ya maana ya kunifanya niondoke Act Wazalendo.”

Siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa la wanasiasa wa vyama vya upinzani kuhamia chama Tawala CCM kwa madai ya kumuunga mkono Rais John Magufuli kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wake, miongoni mwao wapo waliokuwepo Wabunge, madiwani, viongozi kwenye vyama vya upinzani na wanasiasa mashuhuli.

Godbless Lema ampongeza Rais Magufuli.....Amshauri Awaangalie na Waliokaa Mahabusu Muda Mrefu

$
0
0
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema amempongeza Rais John Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa.

Pia, amemshauri kuwaangalia mahabusu waliokaa muda mrefu gerezani pasipo kupata haki.

Katika maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara)  Jumamosi Desemba 9,2017mkoani Dodoma, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 8,157 kati yao 1,828 waliachiwa huru kuanzia siku hiyo.

Rais John Magufuli jana Jumapili Desemba 10,2017 ametia saini nyaraka za msamaha alioutoa kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking na Johnson Nguza (Papii Kocha) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela.

Msamaha huo umeonekana kumgusa Lema ambaye ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Lema   amesema kuna mateso wanayopata mahabusu ambayo yanahitaji kuangaliwa.

“Rais Magufuli, Mungu akubariki kwa msamaha uliotoa jana kwa wafungwa na hasa wale waliokaa magereza muda mrefu pamoja na wazee, msamaha ni ibada,” amesema Lema ambaye pia ni mbunge wa Arusha Mjini (Chadema).

“Ni msamaha muhimu kwao, mtu aliyehukumiwa maisha au kifo akipata msamaha ni jambo jema sana, ninafurahi wamesamehewa sasa hawatakuwa tena magereza maisha yao yote,” 

“Nimefurahi kwamba hata wale waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa hasa wazee pia wamepata msamaha, kwangu ninaona ni jambo jema na zuri, kwa mtu anayejua huzuni ya magereza atakubaliana nami.”

Kuhusu mahabusu, Lema amesema, ‘’Wako mahabusu wamekuwa magereza kwa muda mrefu bila kesi zao kukamilika. Mheshimiwa  Rais fuatilia watu kama hawa pia.”

PICHA: Rais Magufuli Akiangalia Kiatu Kinachotengenezwa Na Kiwanda Cha Magereza Cha Karanga

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ubora wa kiatu cha Mrakibu Msaidizi wa  Magereza Melkior Komba, Katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Viatu hivyo vimetengenezwa na kiwanda cha Jeshi la Magereza Karanga kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Jeshi la Magereza linazalisha jozi 150 za viatu kwa siku katika kiwanda chake cha Karanga kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, na kwa kushirikiana na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF limeanza kuboresha kiwanda hicho ili kufikia uzalishaji wa jozi 450 kwa siku.

PICHA NA IKULU

Takukuru kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma imesema Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis atafikishwa mahakamani leo.

Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma, Emma Kuhanga jana alisema Sadifa atafikishwa mahakamani leo  Jumatatu Desemba 11,2017.

Alisema kiongozi huyo alikamatwa nyumbani kwake akiwapa soda wajumbe wa UVCCM kutoka Mkoa wa Kagera kitendo ambacho ni kinyume cha maadili.

UVCCM jana Jumapili Desemba 10,2017 ilichagua viongozi wapya wa ngazi ya Taifa watakaoongoza jumuiya hiyo ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano.

Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge, Zanzibar alikamatwa nyumbani kwake Mailimbili mjini Dodoma.

TANESCO Yawatoa Hofu Wateja Wake Juu Ya Mfumo Wa Ununuzi Wa Luku

$
0
0
Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa Umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua
katika mifumo iliyozoeleka.

Akizungumza jana  jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA) wa Tanesco, Demetruce Dashina alisema kuwa kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku kutokana na wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakihamisha mitambo hiyo kutoka ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine.

“Jana tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa luku kwenda katika ofisi zetu mpya hivyo ikawalazimu wateja wetu kupata usumbufu kidogo, lakini kuanzia saa saba(jana) mfumo huo umekaa sawa na wateja wanaweza kununua umeme kama walivyokuwa wanafanya hapo awali bila shida yoyote mara baada ya marekebisho ya kiufundi” alisema Dashina

Alisema kuwa shirika lilijipanga kuwahudumia wateja wake kama kawaida wakati wa kuhamisha mitambo hiyo lakini Wananchi wengi wakapata taharuki hivyo kufanya mfumo wa
ziada kuzidiwa kutokana na watu kununua umeme kuliko Kawaida.
 
Kwa upande wake Kaimu Meneja  Uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji aliwaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka.

Muhaji alisema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo   kuwataka watanzania kuwa na Imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya kuwahudumia  kama inavyohitajika.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images