Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Jiji La Dar Es Salaam Lapata Tuzo Kupitia Mradi Wa Mabasi Yaendayo Haraka

$
0
0
JIJI  la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 duniani ambayo yamepata tuzo ya C40 Bloomberg Philantropies 2017   kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.

Katika tuzo hiyo  mwaka huu imepokelewa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Miwta aliyerejea nchini alfajiri ya Desemba 8 mwaka huu.

Jiji la Dar es Salaam limechangia tuzo hiyo  na Jiji la New York  nchini Marekani 

Mradi wa Mabasi yaendayo haraka unawahudumia abiria 200,000 kila siku kwa kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa siri ya mafanikio ya tuzo jijini hapa.
 
Tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka katika miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mahususi matano ili kutambua jitihada za majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90 duniani inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi Duniani.
Imetolewa  Desemba 10
Na Christina Mwagala , 
Afisa Habari Ofisi ya Mstahiki Meya wa jiji.

Pesa Haiendi Bure Ni Dawa Asilia Ya Kuongeza Ukubwa Wa Maumbile Ya Kiume.

$
0
0
Wanaume  wengi  wanakosa  raha  ya  kuwa  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  kwa sababu  ya  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume.

Ndoa  nyingi  zimevunjia, mahusiano mengi  yameharibika, huku  chanzo  kikuu  kikiwa  ni  tatizo  la  udogo  wa  maumbile  ya  kiume.

Uzoefu  wangu katika  tiba  asilia, umeniwezesha  kugundua kuwa,  wanawake  wengi  hulazimika  kutoka  nje  ya  mahusiano  au  kwenda  nje  ya  ndoa , pale  wanapo gundua  kuwa  wameangukia  kwenye  mikono  ya  mwanaume  mwenye  maumbile  madogo  ya  kiume.

Kitu  kikubwa  kinacho weza  kumfanya  mwanamke , kuendelea  kukaa  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  na  mwanaume  mwenye  tatizo  la  maumbile  madogo  ya  kiume, ni  pesa. 

Hapa  mwanamke  husika, hulazimika  kuendelea  kuwa  katika  mahusiano  au  ndoa  na  mwanaume  huyo  kwa  sababu  mwanaume  huyo  ana  pesa, lakini  hulazimika  kutoka  nje  ya  ndoa  pindi  anapo hitaji kufurahia  mapenzi.

Ama  kwa  upande  wa  wanaume  wenye  tatizo  la  udogo  wa  maumbile  ya  kiume. Hofu  na  mashaka  hutawala  katika  maisha  yao yote  ya  kimahusiano.

Huwa  hawajiamini  kama  mwanamke  anaweza  kuwapenda  kwa  jinsi  walivyo.

 Wivu  na  gubu  hutawala  katika  maisha  yao yote  kimahusiano. 

 Karibu  kila  kosa  linalo   fanywa  na  wenzi  wao hulihusisha  na  udogo  wa  maumbile  yao.

Kwa  mfano :  Wamekwaruzana kidogo, mke  kamnunia  au  labda  kamsonya, wao  hufikiri  wamenuniwa  au  kusonywa  kwa  sababu ya  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume.

Amempigia  simu  mpenzi  wake  au  mke  wake, halafu  bahati  mbaya  simu  haijapokelewa zaidi ya  mara  tatu, basi  moja  kwa  moja  huhisi  mke au  mpenzi  anamsaliti kwa  sababu  ya  udogo  wa  maumbile  yake  ya  kiume .  Wakati  ukweli  unaweza  kuwa  tu  labda  simu  ilikuwa  silence  kwenye  pochi.

Wakiwa  wanafanya  tendo  la  ndoa, halafu  baada  ya  kumaliza  mshindo  mmoja,  halafu  baada  ya  dakika  kadhaa, mwanamke  akawa  anataka  waendelee tena, basi  mwanaume  huhisi  kama  vile  mwanamke  huyo  anamkejeli  kwa  sababu  ana  maumbile  madogo na  yasiyo  na  nguvu  za  kutosha.

Vile vile, wakifanya  tendo moja  tu  halafu  mwanamke  akasema  amechoka, basi  jamaa  atachukulia  hiyo  kama  amedharauliwa  na  mwanamke  huyo, kwamba  mwanamke  hafurahii tendo la ndoa  kwa  sababu  ya  maumbile  yake  madogo.

Maumbile  huwa  madogo  na  husinyaa  zaidi  mara  baada  ya  kumaliza  tendo la  ndoa. Hali  hii humfanya  mwanaume huyo  kutokujiamini zaidi  na  kuvaa  taulo  ama  kaptula  haraka, ili  mwanamke  wake  asimuone  katika  hali  hiyo.

Wanapokuwa  faragha  na  wanawake  wao  huwa  hawapendi  kushikwa  maumbile  yao, hasa  yanapokuwa  bado  hayajasimama.

Kwa  ufupi  wanaume  wenye  maumbile  madogo  ya kiume, wanaishi  maisha  ya  tabu  sana  katika  mahusiano  yao.

NINI  TIBA  YA  TATIZO   LA  MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME ?

Kama  una  tatizo  la  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume, liwe  limetokana  na  kusinyaa  kwa  sababu  ya  kujichua  kwa  muda  mrefu, kuugua  chango  la  kiume  au  kurithi  kwa  wazazi  wako, tumia  tiba  ya  asili  iitwayo   PESA  HAIENDI BURE.

Ni  tiba  ya  asili  ambayo  imekuwa  ikitumika  toka  enzi  za  mababu  na  mababu  wa  mababu. 

Itasaidia  kuimarisha, kurefusha  na  kunenepesha  maumbile  yako  ya  kiume  na  kukufanya  kufurahia   tendo la  ndoa.

Tiba  hii  haitakufanya  kufurahia  tendo la  ndoa  tu, bali  hata  mke  wako au  mpenzi  wako, itamfanya  pia  afurahie  tendo la ndoa  na  kuongeza  upendo  na  uaminifu  kwako.

Unapokuwa  na  uwezo  wa  kufurahia  tendo  la  ndoa  pamoja  na  kumfanya  mke  au  mpenzi  wako  kufurahia  tendo  la  ndoa, unakuwa  pia  unajiepusha  na  uwezekano  wa  kupatwa  na  maradhi  ya  kuambukizwa  kwa  njia  ya  kujamiiana  kama  vile  Kaswende, Kisonono  na  hata  V.V.U  .

JINSI  YA  KUPATA  TIBA  HII: Kupata  tiba  hii, wasiliana  na  DOKTA.  MUNGWA  KABILI  KWA  SIMU  NAMBA  :   

0744  000  473.     www.mungwakabili.blogspot.com

Uhuru Kenyatta amuandikia barua Rais Magufuli

$
0
0
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kupinga kitendo cha mauaji ya askari wake 15 waliokuwa wakilinda amani nchini Kongo, na kumpa pole kufuatia msiba huo mkubwa.

Katika barua hiyo, Rais Kenyatta amesema kushambuliwa kwa askari, ambao walikuwa wakihudumia kwa sababu nzuri ya kuanzisha amani ya kudumu nchini DRC ilikuwa mbaya, huku akiwapa pole watanzania na ndugu wa marehemu, na kuwaombea wale waliojeruhiwa waweze kupona haraka.

Uhuru Kenyatta ameendelea kwa kusema kwamba Kenya itaendelea kushirikiana na watu na serikali ya Tanzania katika kulinda amani ya Kongo na maeneo ya maziwa makuu, na kuangalia kesho bora ya maeneo hayo.

Rais Kenyatta amesema Kenya inathamini jukumu muhimu lililofanywa na watunza amani tangu imehusika katika mipango mingi ya kulinda amani.

Mwishoni mwa wiki iliyopita askari 15 wa Tanzania waliokuwa wakilinda amani nchini Kongo waliuawa na askari waasi wanaoendesha ampigano nchini humo, huku 44 wakijeruhiwa, 8 wakiwa mahututi na wawili hawajulikani walipo.

Pole Pole Amchana Lowassa.....Adai Mbona Alishindwa Kumshawishi Mhe. Jakaya Kikwete Amwachie Babu Seya

$
0
0
Humphrey Polepole ameibuka na kusema kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya nne Edward Lowassa alishindwa kuzuia Babu Seya asifungwe na kudai pia alishindwa mshawishi Mhe. Jakaya Kikwete ili awatoe watu hao.

Polepole amesema hayo baada ya watu kuanza kusema kuwa jambo alilofanya Rais Magufuli kuwatoa Babu Seya na mwanaye Papi Kocha ni jambo ambalo Lowassa aliahidi katika kampeni zake za 2015 kuwa endapo angechaguliwa kuwa Rais wa Tanzania angewaachia huru watu hao.

"Huyu mzee ambaye amezungumza kwamba hii ilikuwa ahadi yake kipindi cha kampeni ni mzee ambaye amehudumu kwenye serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kipindi ambacho Babu Seya anafungwa huyu mzee alikuwa Waziri Mkuu mwenye nguvu sana, kama alijua Babu Seya labda hakutendewa haki kwa namna yoyote kwa fikra zake angaliweza kumshauri Rais wake kipindi hicho kwamba huyu mtu hastahili kufungwa asamehewe" alisema Polepole

Polepole aliendelea kusisitiza kuwa Lowassa alishindwa kuzuia Babu Seya na watoto wake wasifungwe "Kashindwa kuzuia Babu Seya asifungwe, kashindwa mwaka wa kwanza kumshawishi Rais wake amsamehe Babu Seya, ameshindwa kufanya hivyo kwa miaka mingi iliyopita. 

"Magufuli hakuwa kwenye nafasi ya uamuzi kipindi hicho alikuwa Waziri wa kawaida kabisa baada ya tafakuri ya kina ya miaka miwili akaona katika watu ambao wamejirudi huyu anastahili msamaha, huyo mzee anaibuka oohh nilifanya mimi, huyu mzee aache hizi tabia za kinafiki, kizandiki kwani Watanzania wanataka upinzani unaojenga hoja" alimalizia Polepole.

Babu Seya na mtoto wake Papii Kocha waliachiwa huru katika kifungo cha maisha jela baada ya Rais John Pombe Magufuli kuwapa msamaha katika siku ya Uhuru wa Tanzania bara, ambapo kila mwaka Disemba 9 zinafanyika sherehe za kumbukumbu. 

==>Msikilize hapo chini akiongea

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa apandishwa kizimbani na TAKUKURU kwa makosa mawili

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma imemfikisha mahakamani aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis.

Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge, Zanzibar amefikishwa leo Jumatatu Desemba 11,2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kwa makosa mawili.

Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma, Emma Kuhanga alisema jana Jumapili Desemba 10,2017 kuwa Sadifa angefikishwa mahakamani leo.

Alisema kiongozi huyo alikamatwa nyumbani kwake akituhumiwa kwa kuwapa soda wajumbe wa UVCCM kutoka Mkoa wa Kagera kitendo ambacho ni kinyume cha maadili.

Kuhanga akithibitisha kukamatwa kwa Sadifa alisema alikamatwa Jumamosi Desemba 9,2017.

RC Gambo awavuruga CHADEMA...... Adai Mhe. Lema yupo mbioni kujiunga CCM

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewavuruga wanachama wa Chadema baada ya kuweka picha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akiwa na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na kuandika kuwa Lema yupo mbioni kurudi nyumbani.

Maneno aliyoambatanisha RC Gambo na picha aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram yalisomeka “Msituko yupo mbioni kurudi nyumbani!” jambo ambalo liliibua utata kwa baadhi ya wafuasi wa Chadema.
A post shared by Murriet (@mrisho_gambo) on
 
Tazama baadhi ya maoni ya wadau na wafuasi wa Chadema walivyopokea taarifa hiyo.
  • rexmyic—lema; mwenyewe sisi ccm hatumtaki mana hana sifa yakuwa huko@RC hide my ID
  • upendojlyahoo.co.uk—; Gambo acha we*u mchaga hadanganyiki wewe labda albat msando
  • jazzaluis_jr—; Acha kulisha watua maneno.kakuambia anarudi?amnaga kazi zakufanya
  • seif_71—; Badala ya kuongelea maendeleo kila siku kila mnawaza kuamisha wanachama kutoka kutoka huku kuingia huku mpk uchaguzi utafika ni hvy hvy tu!
  • momnathan2013–; Nunua wavulana wenzio sio Godbless Lema,mwanaume anaejitambua.
  • remmymosha—; Kuandika kwenyewe shida jembe letu haliwezi kwenda fisiem eti msituko badala ya mshtuko
  • neema7888; Old news …Tushawachoka sasa, WaTz tunataka maendeleo sio kuona watu wazima mkishindana kuhama vyama…old fools.!
Hata hivyo mpaka sasa Mhe. Lema hajaongea chochote kuhusu kauli hiyo ya RC Gambo. 

Je, kwa maoni yako unadhani Lema anaweza kuungana na CCM kama alivyofanya aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CUF, Maulid Mtulia. ?

Miili ya askari waliouawa DRC kurejeshwa leo

$
0
0
Miili ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa na waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inarejeshwa nchini leo.

Taarifa ya ofisi ya habari ya JWTZ imesema miili ya askari hao itawasili nchini leo Jumatatu Desemba 11,2017 saa kumi na mbili jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Awali, akizungumzia na waandishi wa habari jana Jumapili Desemba 10, 2017 Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali James Mwakibolwa alisema miili ya askari hao ingerejeshwa nchini kati ya Jumanne Desemba 12, au Jumatano Desemba 13,2017 kwa ushirikiano kati ya Serikali na Umoja wa Mataifa (UN).

Mwakibolwa alisema askari hao walivamiwa kambini na waasi wa ADF na mapigano yalidumu kwa takriban saa 13. Alisema askari 14 wa JWTZ waliuawa, 44 wamejeruhiwa na wengine wawili  hawajulikani walipo.

Alisema tukio hilo lililotokea Desemba 7,2017 katika kambi ndogo iliyopo katika daraja la Mto Simulike, kaskazini mashariki mwa Wilaya ya Beni, Jimbo la Kivu nchini DRC.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne yya Disemba 12


Herry James Mwenyekiti Mpya Wa UVCCM , Makamu Wake Ni Tabia Maulid Mwita

$
0
0
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umemchagua Kheri James kuwa mwenyekiti wake kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

James amepata kura 319 kati ya kura 583 zilizopigwa akimwacha kwa mbali mpinzani wake, Thobias Mwesiga aliyepata kura 127.

Uchaguzi huo uliofanyika Jumapili Desemba 10,2017 ukihusisha wagombea saba kwa nafasi ya mwenyekiti.

Katika uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa UVCCM, Thabia Mwita ameshinda kwa kupata kura 286 dhidi ya mpinzani wake Rashid Mohamed Rashid aliyepata kura 282.
Msimamizi wa uchaguzi huo alikuwa William Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Wagombea wengine waliochaguliwa ni mwakilishi wa vijana katika jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT), Dotto Nyirenda; mwakilishi wa vijana kwenda Jumuiya ya Wazazi, Amir Mkalipa na wawakilishi watatu wa Tanzania Bara kwenda Baraza Kuu la UVCCM ambao ni Rose Manumba, John Katarahiya na Secky Kasuga.

Wengine ni wawakilishi wawili wa Zanzibar kwenda Baraza Kuu la UVCCM ambao ni Nasra Haji na Abdallah Rajabu.

Pia, wajumbe wawili kutoka Zanzibar wanaokwenda Halmashauri Kuu ya Taifa, Abdallaghari Idrisa Juma na Maryam Mohamed Khamis.

Wengine waliochaguliwa ni wajumbe watatu kutoka Tanzania Bara wanaokwenda Halmashauri Kuu ambao ni Sophia Kizigo, Mussa Mwakitinya na Keisha.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, mwenyekiti James amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii na kutekeleza maagizo yaliyotolewa na mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Ameagiza viongozi wa umoja huo hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa  akifungua mkutano wa tisa wa UVCCM ichapishwe na nakala zisambazwe kwa vijana mikoani na wilayani ili kutekeleza maagizo aliyoyatoa ikiwamo kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za jumuiya hiyo.

PICHA: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Akimpongeza Mwenyekiti Mpya Wa UVCCM

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa UVCCM Kheri James, nje ya Ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma Desemba 11, 2017 (katikati) ni Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Serikali Yasaini Mikataba Minne Ya Ujenzi Wa Barabara kilomita 402 za Lami

$
0
0
Serikali imesaini mikataba minne na kampuni nne za ujenzi wa barabara yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 702 kwa ujenzi wa kilomita 402.

Tukio hilo la kusaini mikataba hiyo limeshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Mandeleo ya   Afrika (AfDB), MarieHellen Minja, wabunge ambao miradi hiyo ya Barabara itapita majimboni mwao, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na wakandarasi walioshinda zabuni.

Akizungumzia utiaji saini huo, Waziri Mbarawa amesema fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami  kutoka Tabora (Usesula)- Koga hadi Mpanda yenye urefu wa kilomita 335 na kilomita 67 kutoka Mbinga hadi Mbamba Bay mkoani Ruvuma.

Waziri Mbarawa amesema ujenzi wa barabara hizo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na ahadi za Rais John  Pombe Magufuli wakati wa kampeni.

Aidha, Waziri Mbarawa ametumia nafasi hiyo kuwataka wakandarasi walioshinda zabuni kujenga barabara zenye ubora na viwango kwa kuzingatia muda wa ujenzi.

Profesa Mbarawa ameongeza kuwa nia ya Serikali ni kuona ujenzi wa barabara hiyo unakamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

“Naomba TANROADS msimamie ujenzi wa barabara yenye ubora kwani wakandarasi wengi ni wajanja na ikitokea mtu ameharibu asipewe nafasi kabisa ya ujenzi wa barabara hapa nchini,” amesema Waziri Mbarawa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, amesema kuwa wakandarasi waliopewa kazi wametokana na uchambuzi mkubwa uliofanyika kati ya wakandarasi 129 waliojitokeza mwaka 2016 kuomba zabuni za ujenzi wa barabara hizo.

Mhandisi Mfugale amefafanua kuwa ili kurahisisha ujenzi wa barabara hizo wamegawa kwa wakandarasi wanne ambapo barabara ya Usesula hadi Komanga kilomita 108 itajengwa na Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering Group Corporation Limited ya China kwa gharama ya zaidi ya Sh.Bilioni 158 na itajengwa kwa miezi 36.

“Komanga hadi Kasinde kilomita 108 itajengwa na Mkandarasi Kampuni ya China Wu Yi Co. Limited kwa zaidi ya sh.billioni 140 na Kasinde hadi Mpanda kilomita 105 Mkandarasi Kampuni ya China Railway Seventh Group Co.Ltd kwa sh. Bilioni 133,” amesema Mhandisi Mfugale.

Mhandisi Mfugale ameongeza kuwa barabara ya Mbinga hadi Mbamba Bay kilomita 67 inajengwa na Mkandarasi China Henan International Corporation Group Co.Ltd (Chico) kwa sh. Bilioni 129.

Amesema TANROADS imejipanga kusimamia ujenzi huo kwa kufuata viwango vinavyohitajika vya ujenzi wa barabara nchini.

Mwakilishi Mkazi wa AfDB,  Bi. Minja amesema ofisi yake itaendelea kutoa mchango kwa serikali katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini pale watakapo hitajika.

Bi. Minja amesema kuwa matarajio ya AfDB ni kuona Tanzania inapata maendeleo kwa haraka na njia rahisi ni kupitia miundombinu.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye barabara ya Tabora hadi Mpanda inapita jimboni kwake ambapo amesema kuwa ujenzi huo utafungua fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, amesema barabara hiyo itakuwa kiungo muhimu kati ya Tanzania, Msumbiji na Malawi.

Amesema kuwa Nyasa ina vivutio vingi vya utalii hivyo ujio wa barabara hizo utakuwa njia rahisi ya kuwafikisha watalii eneo hilo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Bei Mpya Ya Mafuta Kwa Mwezi Wa Disemba

$
0
0
MAMLAKA ya udhibiti wa huduma za nishati na maji( ZURA )  imetoa taarifa juu ya bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia leo  Jumanne tarehe 12-12-2017.

Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Maisara Kaimu Mkurugenzi masuala ya wateja Mussa Ramadhani Haji  alisema kuwa bei hizo Zura imepanga kufuatia mambo yafuatayo;-

Wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations) katika mwezi wa Novemba 2017 , kwa lengo la kupata kianzio cha kufanyia mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi wa Disemba 2017.

Pia thamani ya shillingi ya  Tanzania , gharama za usafiri , Bima na’ Premium ‘hadi Zanzibar  . Kodi za serikali  na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.

Alisema bei za rejereja ya mafuta ya Petroli kwa mwezi wa Disemba, 2017 imepanda kwa shillingi (100) kwa lita kutoka shilling 2,130 Mwezi wa Novemba , 2017 hadi shilling 2,230 kwa lita katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.5%.

Pia alisema bei ya rejereja ya mafuta ya Dizeli kwa Mwezi wa Disemba , 2017 imeshuka kwa shilling (90) kwa lita kutoka shilling 2,280 kwa lita katika mwezi Novemba hadi shilling 2,190 kwa lita katika mwezi wa Disemba, 2017 sawa na  asilimia 4%.

Aidha alisema bei ya reja reja ya mafuta ya Taa kwa mwezi wa Disemb 2017 imepanda kwa shilling (80)  kwa lita kutoka shillingi 1.539 kwa lita katika mwezi wa Novemba , 2017 hadi shilling 1,619 katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.9%

Vilevile bei ya reja reja ya mafuta ya Banka kwa mwezi waDisemba,  2017 imeshuka kwa shilling (90) kwa lita kutoka shillingi 2,122 kwa lita katika mwezi wa Novemba, 2017 hadi shilling 2,032 katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.4%.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

IGP Sirro Akagua Na Kushiriki Mazoezi Ya Ukakamavu Na Askari Wa Mkoa Wa Tabora

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu kutoka kushoto akiangalia  mmoja wa askari wa Jeshi la Polisi akiwa katika mazoezi ya utayari kupita juu ya kamba mkoani Tabora jana. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu toka kulia jana asubuhi alishiriki  mazoezi ya utayari na kuwatia hamasa Askari wa  Mkoa wa Tabora,  katika ziara yake ya siku moja mkoani humo, hatua hiyo ni kutokana na kuwataka askari wa Jeshi la Polisi kuwa na utayari wakati wote .

 Picha na Jeshi la Polisi

UKAWA Watishia Kususia Uchaguzi Jimbo la Nyalandu.....Watoa Masharti Tume ya Uchaguzi

$
0
0
Vyama  vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimetishia kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo matatu, likiwamo la Singida Kaskazini la aliyekuwa mwakilishi Lazaro Nyalandu, endapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haitotangaza kuuahirisha na kuupangia tarehe nyingine.

Hata hivyo, tume hiyo imesema itaendelea kutekeleza majukumu yake ikibainisha kuwa katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya kikatiba, haitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya serikali au maoni ya chama chochote cha siasa.

Nyalandu, waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, alitangaza kuachia ubunge wa Sindiga Kaskazini na kuihama CCM Oktoba 30, mwaka huu kisha kujiunga na Chadema kutokana na kile alichodai kutoridhishwa na mwenendo wa sasa wa chama tawala.

Ukawa umeitaka tume hiyo kuusogeza mbele uchaguzi huo ili kwanza kuwe na majadiliano baina ya tume, vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi kuepuka ilichodai kasoro zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata 43 uliofanyika Novemba 26, mwaka huu.

Umoja huo unaundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

Hata hivyo, CUF kwa sasa imegawanyika katika makundi mawili - moja likimuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na jingine likiwa upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Mapema mwezi huu, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Hamid Mahmoud Hamid, alitangaza kuwa uchaguzi mdogo katika majimbo matatu ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini, na kata sita za Tanzania Bara utafanyika Januari 13.

Hata hivyo, zikiwa zimebaki siku 32 kabla ya kufanyika kwake, Ukawa jana ulitangaza tishio la kutoshirika katika uchaguzi huo endapo NEC haitauahirisha na kupanga tarehe nyingine na pia kutoa nafasi kwa vyama vyote na wadau husika kukaa pamoja kujadili na kuzipatia majibu "kasoro" zilijitokeza katika uchaguzi mdogo uliopita.

Ukawa umedai uchaguzi huo ambao chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitangazwa mshindi katika kata 42 kati ya 43 zilizoshindaniwa, haukuwa huru na wa haki hivyo kuna haja kuitishwa mkutano wa wadau kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi huo na kuzitafutia utatuzi kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mwingine.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, viongozi wa Ukawa walidai tayari wameshaiandikia barua NEC kuomba uchaguzi huo usogezwe mbele igawa bado hawajajibiwa.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe, akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake, alibainisha mambo kadhaa ambayo yamewalazimu waombe uchaguzi huo usogezwe mbele ikiwa ni pamoja na kutangaza uchaguzi katika Jimbo la Longido ilhali bado kuna kesi kwenye Mahakama ya Rufani inayolihusu.

"Jimbo la Longido Kaskazini kwa mujibu wa sheria za uchaguzi haliko wazi," Mbowe alisema, "bado halijaiva kwa ajili ya uchaguzi kwa sababu rufani yake bado iko mahakama ya rufani na imekatwa kwa kufuata utaratibu, inakuwaje utangaze uchaguzi wakati rufani imekatwa?"

Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema sababu ya pili ni kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo katika kata 43 mwezi uliopita, akidai kuwa pamoja na mambo mengine, NEC ilishindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kusababisha uchaguzi huo kutokuwa huru na wa haki.

Mbowe alisema sababu ya tatu iliyoulazimu Ukawa kuomba kusogezwa mbele kwa uchaguzi mdogo wa majimbo matatu ni kutumika kwa nguvu kubwa ya vyombo vya dola katika uchaguzi mdogo uliopita, huku wanachama, viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na wabunge wakikamatwa ovyo.

“Tumeona umwagaji wa damu katika uchaguzi huo mdogo na mambo hayo yanafanyika ikiwamo kwa kutumia silaha za asili na za moto," Mbowe alisema na kueleza zaidi:

"Tumeona viongozi wa mikoa wakifanya kampeni na wakati mwingine kuwaamrisha polisi nini cha kufanya katika uchaguzi huo japokuwa hawaruhusiwi kufanya hivyo, wasimamizi wa uchaguzi nao hawakubaki nyuma, Nec wamejidhihirisha kushindwa kutekeleza wajibu wao.

“Katika nchi hii tukiendelea tunavyoendelea, hakuna uchaguzi utakaofanyika kwa kufuata sheria na kanuni zilizopo. Mazingira ambayo sheria haziheshimiwi, tukishajenga tabia hiyo hakutakuwa tena na uchaguzi huru."

'Kigogo' huyo wa Ukawa alidai kukimbia moja kwa moja kwenda katika uchaguzi katika mazingira hayo kunaweza kuleta mpasuko na pia umoja huo ukifanya hivyo, hautakuwa unalitendea haki taifa.

“Kwa mantiki hiyo, uchaguzi huo unastahili kuahirishwa," Mbowe alisema, "ni rai yetu kwa serikali na NEC kuona umuhimu wa kuahirisha kwanza uchaguzi huo ili wadau mbalimbali wa vyama vya siasa na washiriki wa shughuli hizo, kutafakari wamepata funzo gani katika uchaguzi wa kata 43.

"Kuna mazingira gani ya kufanya siasa katika nchi  yetu inayotupa 'justification‘ (uhalali) ya kwenda kwenye kufanya chaguzi, kuendelea kushiriki chaguzi za kuumiza watu, kufunga watu, za kuvunja amani, hazitujengi kama taifa isipokuwa tunaongeza mpasuko na ufa kati yetu.

“Kwa sisi, rai yetu kama viongozi wakuu wa kitaifa wa Ukawa ni kwamba, muda uliotolewa na kutangazwa uchaguzi huu bila kufanya ‘consultation’ (majadiliano) na vyama vya siasa japo NEC wanaweza kujitetea kwamba sheria inawapa mamlaka hayo, lakini tunaamini kwa upande wa pili uongozi ni pamoja na kusoma ‘between the line’ (kutafakari kwa makini) kwamba kuna viashiria vyote vya kupoteza amani katika taifa.

"Kwa hiyo, tunaiomba serikali chaguzi hizi zisogezwe mbele, wadau tukae kwanza, vyama vya siasa na wadau wengine tukae tuzungumze. Hivi kweli tumechagua uchaguzi ukawe ni wa mapanga, visu na rungu? Hivi kweli tumekubaliana kwamba mawakala watolewe vituoni?

“Na tukishakubaliana juu ya haya, maadili na kwanini yalikiukwa? Kwa sababu si kila jambo lazima liende mahakamani japo wao wanasema mkiona hamjaridhika muende mahakamani, ila wakumbuke kwamba mahakamani pia ni kuchelewesha haki na mambo ya kisiasa hayako hivyo.

"Ni vema wakaangalia namna uchaguzi huu uahirishwe ili wahusika wakae na kutafakari tulikotoka na tuliko na tunakotaka kwenda, kama Tume na serikali itapuuza rai yetu, sisi kama umoja wetu wa vyama hivi hatutakuwa tayari kushiriki uchaguzi huo."

Katibu Mkuu wa NLD, Toz Matwanga, aliyekuwa amefuatana na Mbowe kwenye mkutano huo, alisema sheria inavipa haki vyama vya siasa vyote kufanya siasa kwa amani, hivyo kuvinyima haki hiyo ni kosa.

Katika mkutano huo, mbali na Matwanga, Mbowe pia alifuatana na viongozi wa NCCR-Mageuzi na CUF kutoka upande wa Maalim Self.

Picha za kombora jipya la Korea Kaskazini Hwasong-15 Linaloweza Kuitandika Marekani

$
0
0
Korea Kaskazini imetoa picha za jaribio la kombora lake jipya ambalo inadai kuwa linaweza kushambulia popote pale nchini Marekani.

Picha hizo zinaonyesha kiongozi wa Korea Kaskazini Ki Jong un na maafisa wengine kadha ya ngazi za juu jeshini wakisherehekea kombora la Hwasong-15 wakati likipaa. 
 
Wengi wameshangazwa na ukubwa wa kombora hilo. Picha hii ambayo haijulikanai ilichukuliwa lini na iliyotolewa na vyombo vya habari vya taifa inaonyesha Kim akilikagua kombora hilo.
Kim akikagua Hwasong-15 
 
Michael Duitsman, mtafiti katika kituo kimoja alisema kuwa kombora hilo ni kubwa kuliko kombora la kwanza la Hwasong-14 "ni nchi chache tu zinaweza kuunda kombora kama hilo na Korea Kaskazini imejiunga nazo."

Pia linaonekana kuwa na kichwa kikubwa ikimaanisha kuwa linaweza kubeba bomu zito la nyuklia kwenye kichwa chake.

Yote haya yanaashiria kuwa kombora hilo lina uwezo kwa kusafirisha bomu la nyuklia kwa muda mrefu.
Hwasong-15 likipaa
Maandalizi ya kulifanyia majaribio Hwasong-15
 
Lilisherehekewa kwa sigara
Kim mwenye furaha anaonekana akicheka kwa furaha  wakati kombora hilo linapaa. Linaaminiwa kuwa kombora la kwanza la Korea Kaskazini lililopaa mbali zaidi katika kilomita 4,475.
Bw Kim na wenzake walionekana wakisherehekea  mafanikio ya jaribio hilo kwa sigara.

Credit: BBC

Majonzi miili 14 ya Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ikipokelewa

$
0
0
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana ulikuwa eneo la majonzi makubwa baada ya miili ya askari 14 wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), waliouawa na waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), kufika nchini hatimaye.

Miili hiyo ilirejeshwa majira ya jioni na kupokelewa na umati wa askari wa JWTZ wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo.

Ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wengi kiasi hicho wa JWTZ kuuawa katika misheni ya kulinda amani, kwa mujibu wa Jenerali Mabeyo aliyekuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari uwanjani hapo.

Miili hiyo ililetwa na ndege maalum ya Umoja wa Mataifa huku ikiwa imefunikwa bendera ya UN.

Baada ya kuwasili, kwa huzuni wanajeshi walianza kuchukua mwili mmoja baada ya mwingine na kuhamishia katika magari maalum yaliyokuwa yameandaliwa.

Kila mwili ulibebwa na wanajeshi nane wakati wa kuhamishia katika magari hayo kwa ajili ya kusafirisha kwenda kuilaza katika Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo, jijini.

Jumla ya magari saba yalitumika kubebea miili hiyo, kila moja ikibeba miili miwili na kusindikizwa na kundi la wanajeshi.

Akizungumza kabla ya kuanza safari hiyo ya kwenda Hospitali ya Lugalo, Dk. Mwinyi alisema miili hiyo inatarajiwa kuagwa Alhamisi katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi, eneo la Upanga.

Pia alisema tukio la kuuawa kwa wanajeshi hao wamelipokea kwa masikitiko makubwa na kwamba wataendelea kuchukua tahadhari ili kuzuia kutokea kwa tukio kama hilo tena.

Kwa upande wake, Jenerali Mabeyo alisema tukio kama hilo ni la kwanza kutokea na kwamba hawajatetereka.

“Unavyolinda amani, lazima utegemee lolote, na tukio hili ni la kwanza katika kipindi cha miaka mitano," alisema Jenerali Mabeyo. "Hatuna hofu."

"Isipokuwa unaposhambuliwa, unajitazama umekosea wapi halafu unajirekebisha."

Aidha, mkuu wa majeshi alisema hali ya wanajeshi waliojeruhiwa ambao wako Kinshansa, DRC na nchini Uganda inaendelea vizuri na kwamba mmoja aliyepotea kati ya wawili amepatikana.

Kufuatia vifo hivyo, Rais John Magufuli ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu alituma salamu za rambirambi kwa Waziri Mwinyi, Jenerali Mabeyo, maofisa wote wa Jeshi na kwa familia zote za marehemu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika salamu hizo Rais Magufuli alisema: “Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kuuawa askari wetu kumi na wanne na wengine arobaini na wanne kujeruhiwa, na wawili hawajapatikana huko DRC wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani.

"Natoa pole sana kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na familia, (na) wakati tukisubiri taarifa kamili kutoka DRC niwaombe Watanzania tuwe na subira."Mungu wetu yuko pamoja nasi."

Taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres Ijumaa ilisema shambulio hilo ndilo baya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa umoja huo katika historia yake miaka ya karibuni.Pia alielezea kusikitishwa na tukio hilo.

“Ningependa kueleza kusikitishwa kwangu na shambulio hilo lililotekelezwa usiku wa jana (Alhamisi) dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC," alisema katika taarifa hiyo.

"Shambulio hilo lilitekelezwa kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki, eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.Taarifa ya UN ilisema pia wanajeshi watano wa Jeshi la DRC (FARDC) waliuawa kwenye shambulio hilo. 

Sababu Zilizofanya Mwenyekiti wa UVCCM , Sadifa Juma Khamis kurudishwa Rumande

$
0
0
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Juma Khamis ambaye alipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Mkoa wa Dodoma kwa makosa mawili yanayohusu rushwa, amekosa dhamana mpaka Jumanne ijayo kwa hofu ya kuingilia mchakato wa uchaguzi mkuu wa umoja huo .

Sadifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar alifikishwa mahakamani hapo majira ya 4:55 asubuhi na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Akisoma kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Joseph Fovo, mwendesha mashtaka wa Takukuru, Biswaro Biswaro alisema mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo Desemba 9, mwaka huu akiwa nyumbani kwake maeneo ya kata ya Mnadani, Manispaa ya Dodoma.

Alisema katika kosa la kwanza, Sadifa akiwa nyumbani kwake alitoa rushwa ya vinywaji kwa wajumbe ili wamchague mgombea wa nafasi ya Makamu mwenyekiti wa UVCCM, Rashid Mohamed Rashid.

Biswaro alisema kosa la pili analokabiliwa nalo Sadifa ni kutoa ahadi ya kuwalipia gharama za usafiri wajumbe hao kutoka Dodoma–Kagera kama zawadi kwao baada ya kumpigia kura mgombea huyo.

Wakili huyo aliwataja wajumbe hao kuwa ni Kadogo Shabani, Abdallah Hamimu, Octavian Andrea, Didas Zimbihile, Tasinta Nyamwiza, John Lufunga, Mtwawafu Kantangayo, Haleluya Ivody, Deocres Kagunila, Emmanuel Shitobelo, Happiness Rynyogote, Adolf Andrew, Adinani Musheruzi, Editha Domisian na Hashim Abdallah.

Biswaro alisema mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15(1)(b) na (2).

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu Fovo alimhoji mshtakiwa huyo ambaye alikana kutenda makosa yote mawili.

Biswaro alisema upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na upande wa Jamhuri unaweka pingamizi la dhamana kwa mshtakiwa.

Mwendesha mashtaka Biswaro alisema sababu za kuzuia dhamana ya mshtakiwa huyo ni kutokana na mkutano mkuu wa uchaguzi UVCCM kuwa wa siku mbili mfululizo, juzi na jana na pia matokeo yakiwa bado hayajatangazwa.

Alisema endapo Sadifa atakuwa nje kuna uwezekano wa kuingilia uchaguzi huo.

“Naomba Mahakama itambue uchaguzi bado unaendelea na mshtakiwa hadi sasa hajakabidhi uongozi... bado ni mwenyekiti,” alisema Biswaro.

Aidha, Biswaro alisema sababu nyingine ni kuwa mashahidi wengi ni viongozi ambao ni wenyeviti na makatibu na endapo akiachiwa kwa dhamana ana kila aina ya ushawishi unaoweza kuvuruga upelelezi.

Kufuatia maelezo hayo, wakili wa utetezi, Godfrey Wasonga alipinga kuzuiwa kwa dhamana na kudai kuwa ni haki ya mtu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alibainisha kiapo cha kuzuia dhamana hicho kilichowasilishwa mahakamani ambacho kimetolewa na Kamanda wa Takukuru mkoa wa Dodoma, Emma Kuhanga, hakina mashiko.

“Uchaguzi wa UVCCM umeshaisha na mshindi tayari ameshapatikana na hakuna uchaguzi mwingine wa kuingilia au kama kuna uchaguzi utafanyika, kiapo kingesema,” alisema Wasonga.

Alihoji sababu za kupelekwa mahakamani kwa kesi ambayo upelelezi wake haujakamilika na kuzuia dhamana kwa mshtakiwa.

Alisema mshtakiwa huyo hataweza kuingilia uchunguzi kwa sababu walizozitoa.“Hawa mashahidi atawezaje kuwashawishi wakati mtu ameshatoka madarakani?" Alihoji wakili Wasonga."Mteja wangu ni Mbunge, ni mtu makini na anaaminiwa. Asihukumiwe kwa kuwekwa ndani kwasababu zisizo na mashiko.”

Aliomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo na mshtakiwa apewe dhamana kwa kuwa hataweza kuingilia uchaguzi kwa kuwa uchaguzi mwingine wa UVCCM utafanyika mwaka 2022.

Kutokana na mvutano huo wa kisheria, Hakimu Fovo aliahirisha kesi hiyo hadi Jumanne ijayo ndipo mahakama itatoa maamuzi kuhusu suala hilo. Alisema mshtakiwa ataendelea kuwa rumande.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH....Anatoa Pete za Bahati, Anasafisha Nyota, Anazuia Chuma Ulete na Mengine

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH CHIEF SULTAN MAKATA Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
 
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Chief Sultan Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
 
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Chief Sultan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
 
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. 

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp/Calls 0658316976
0755911233
 
Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote

Rais Magufuli Akerwa Wasanii Kuvaa Nusu Uchi Majukwaani

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amekerwa na mamlaka zinazohusika na maadili kutochukua hatua dhidi ya wasanii wanaoimba majukwani wakiwa na mavazi ya utupu.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumanne wakati akufungua mkutano mkuu wa tisa wa jumuiya ya wazazi CCM utakaofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma.

Rais Magufuli amehoji vyombo vya habari, wasimamizi wa maadili, wizara na taasisi zinazodhibiti zimeshindwa kushughulikia maadili ya vijana.

Msingi wa kauli hiyo ilikuwa ni kumtaka kiongozi wa jumuiya hiyo atakayepatikana kuhakikisha anakwenda kusimamamia maadili ya vijana na Taifa kwa ujumla.

Rais Magufuli aliwataka wazazi hao kusimamia maadili ya Watanzania.

"Hii ni jumuiya ya wazazi lakini maadili yameanza kupotea na jumuiya ipo kwa ajili ya kukemea, mimi nimekuwa shabiki mzuri wa muziki, wanaovaa utupu ni wanawake, wanaume wanacheza wakiwa wamevaa, sana sana wataachia kifua wazi tu ili waonekane 'six pack', lakini wanawake, walio wengi wanaachia viungo vyao,”

"Jumuiya imefika wakati wa kukemea, tunawafundisha nini, je akicheza bila kuvua nguo hata furahisha wimbo? Sasa ni jukumu lenu jumuiya ya wazazi, kwa kumtanguliza Mungu kwa sababu hata Adam alipotenda dhambi alijikuta yupo uchi, lakini kwenye muziki hawajioni wako uchi na wanacheza hadharani.”

Rais Magufuli amesema wakati umefika bila kujali itikadi za vyama kuungana katika ujenzi na ulinzi wa maadiili ya Watanzania.

Tume ya Uchaguzi Yawajibu UKAWA Kuhusu Kuahirisha Uchaguzi

$
0
0
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhani amesema chama cha siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume iuahirishe kwa kuwa haiko kumshawishi mtu au chama kushiriki.

Akizungumza leo Jumanne Desemba 12,2017 jijini Dar es Salaam, Kailima amesema chama kushiriki uchaguzi ni jambo la hiari na NEC ipo kwa ajili ya kuweka na kutengeza mazingira yatakayofanya vyama vya siasa kushiriki uchaguzi.

Kailima katika taarifa iliyotolewa na NEC amesema iwapo kuna chama kitaamua kutoshiriki uchaguzi, kitakachoshiriki hata kama ni kimoja mgombea wake atapita bila kupingwa.

“Ikitokea vyama vikasusa vyote kushiriki kwenye uchaguzi hapo ndipo unaweza kuahirishwa kwa kuwa hakutakuwa na mgombea,” amesema alipozungumza na waandishi wa habari waliotaka ufafanuzi wa NEC kuhusu tamko lililotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Kailima ameviasa vyama vya siasa vinavyotishia kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo matatu na kata sita Januari 13,2018 kufuata mifumo ya kisheria ya kushughulikia malalamiko ya uchaguzi.

Juzi Mbowe alitishia kuwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) havitashiriki uchaguzi iwapo changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 Novemba 26,2017 hazitafanyiwa kazi na NEC.

Akizungumzia hoja hiyo, Kailima amesema katika orodha ya vyama vilivyopo NEC, Ukawa si moja ya vyama vya siasa.

“Niwasihi vyama vya siasa watumie mifumo iliyopo ya kawaida ya kuwasilisha malalamiko kwenye kamati za maadili; kujaza fomu namba 14 kabla ya kura kuanza kupigwa; fomu 16 wakati kura zinapigwa; na kuwasilisha malalamiko mahakamani baada ya kura kuhesabiwa,” amesema Kailima.

Amesema hiyo ndiyo mifumo iliyowekwa kisheria katika kushughulikia changamoto za uchaguzi zinapojitokeza na kuhoji wanayotaka wao ni ipi.

“Kama kuna mgombea hakuridhika mahakama zipo aende maana wamepewa siku 30 za kufungua kesi,” amesema.

Amesema NEC haiwezi kuahirisha uchaguzi kwa kuwa sheria inatamka kuwa uchaguzi unaweza kuahirishwa iwapo tu kuna mgombea amefariki; kutokuwepo mgombea; zikitokea ghasia na fujo au wagombea wakifungana kwa kura.

“Je kuna mgombea amefariki? Haya mambo yote manne hayajatokea, sasa tutaahirishaje uchaguzi?” amehoji Kailima.

Kuhusu jimbo la Longido ambalo Mbowe alidai shauri la uchaguzi bado liko mahakamani na wameiandikia NEC kuhusu suala hilo na barua kutojibiwa, Kailima amesema madai hayo si ya kweli kwa kuwa barua zote walizoandikiwa wamezijibu.

Amesema jimbo hilo liko wazi kwa kuwa Mahakama ndiyo imeiandikia NEC kuitaarifu kumalizika kwa kesi iliyokuwepo mahakamani.

Kailima amesema NEC itasimamisha uchaguzi wa jimbo hilo iwapo tu Mahakama itawaeleza wasimamishe mchakato huo.

“Nimesikitishwa na kauli kwamba eti wametuandikia barua sisi Tume ya kusimamisha uchaguzi wa Longido eti hatujawajibu. Tulipata barua kutoka kwa ole Nangole (Onesmo) tukamjibu, tukapata barua kwa wakili wa Ole Nangole nikamjibu; tukapata barua kutoka kwa katibu wa Chadema tukamjibu na nikaongea naye kwenye simu, sasa leo wanaposema hatujawajibu kwa kweli kauli hiyo imenisikitisha,” amesema
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images