Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mwijage ateua wajumbe wanne bodi ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC)

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewateua wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC).

Taarifa kwa umma ya jana Alhamisi Desemba 7,2017 iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji), Profesa Joseph Buchweishaija imesema uteuzi huo kwa kipindi cha miaka mitatu umeanza Desemba Mosi, 2017.

Uteuzi huo umefanyika baada ya  Desemba 6,2017 Rais John Magufuli, kumteua Profesa Egid Mubofu kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TFC kuanzia Desemba Mosi, 2017.

Wajumbe wa bodi walioteuliwa ni Nuru Angetile Ndile (Mchumi Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango);  Eli Nanyaro Pallangyo (Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji); Dk Kadida R.S. Mashaushi (Mhadhiri, Chuo cha Usimamizi wa Fedha -IFM); na Peter Barnabas Shao (mshauri wa masuala ya fedha katika kilimo).

Taarifa imesema bodi hiyo itazinduliwa Desemba 11,2017 saa nne asubuhi katika ofisi za Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji mjini Dodoma.

Tazama video ya Diamond Platnumz ft Rick Ross – Waka (Official Video)

$
0
0
Mwanamuziki Diamond Platnumz ameachia video ya wimbo wake ambao amemshirikisha mwanamuziki Rick Ross kutoka nchini Marekani. 

Wimbo huu ulikuwa unasubiriwa kwa hamu kubwa na watu mbalimbali, kwani hata wakati wa utayarishaji wa video hii, picha mbalimbali za Diamond akiwa na Rick Ross zilisambazwa mitandaoni, kila mmoja akiwa na lake la kusema.

Tazama video hiyo hapa chini

Tazama video mpya ya MwanaFA Ft. Maua Sama – Hata Sielewi (Official Music Video)

$
0
0
Baada ya hivi karibuni kufanya vizuri na ngoma ya Upo Hapo ambayo yumo yeye, A.Y na Fid Q, Hamisi Mwinjuma ukipenda muite Mwana FA au Binamu ameachia video yake mpya ambapo katika wimbo huo amemshirikisha mwanadada, Maua Sama.

Tazama video ya wimbo huo hapa chini.

Msikilize Mdada Glady Anayedai Kutelekezwa Baada ya Kuzaa na Diamond

$
0
0
Miezi kadhaa baada ya Hamisa Mobeto  kujitokeza hadharani na kudai kazaa na Diamond, mdada mwingine aitwaye Glady ameibuka na kudai kuwa ana mtoto wa miezi 7 aliyezaa na Diamond.

Glady ambaye ni mdada anayeishi nchini Kenya anadai kwamba alikutana ni Diamond Platnumz mwaka 2011 kupitia mtandao wa facebook ambapo walianza mahusiano na hatimaye akampa mimba.

Anasema, baada ya kubeba mimba hiyo, Diamond alikata mawasiliano, hali iliyomfanya asafiri hadi Dar es Salaam Tanzania kumweleza mama yeke Diamond ambaye naye alimkana kwa matusi


Diamond Atuhumiwa Kuwadhalilisha Wanawake.....Ni Baada ya Kumtaka Mtoto Wake wa Kiume Awatumie Atakavyo!

$
0
0
Msanii Diamond Platnumz anayetamba na Ngoma ya Sikomi ameingia matatani baada ya  watu mbalimbali kumtuhumu kuwadhalilisha wanawake kupitia ujumbe wake aliouandika katika ukurasa wake wa Instagram.

Ujumbe huo ambao ulikuwa ni maalum kwa ajili ya kumtakia heri ya kuzaliwa mtoto wake wa kiume, Nillan, ulimtaka mtoto huyo akue salama ili aje awatumie wanawake vyovyote atakavyo kwa sababu  anajituma ili amwandalie pesa ya kutumia vyovyote atakavyo atakapokuwa mkubwa.

“Nasemaje! Kua Uje kuwatembezea Baba... We swala la Kutafta ela niachie mie... Jukumu lako ni moja tu, Kupita nao.....Happy 1st Year Lanny!!!” Unasomekla ujumbe huo wa Diamond.


Ujumbe huo ulionekana kuwakera watu wengi hasa wanawake, ambao waliamua kumfungukia na kumpa makavu.

Breaking News: Mama Anna Mghwira Atangaza Kujiunga CCM

$
0
0
Aliyekuwa mgombea urais 2015 kupitia ACT - Wazalendo Mama Anna Mghwira ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, ametangaza rasmi kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM.

Tukio hilo limetokea leo mjini Dodoma kwenye uzinduzi wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM (UWT), ambao umehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika mkutano huo mama Anna Mghwira amesema ameamua kufanya hivyo baada ya kuona jitihada za CCM katika kuleta maendeleo, hivyo akaona ni vyema akajiunga nao.

"Mimi baada ya kuwa Mkuu wa Mkoa kwa muda mfupi nimeona mengi ndani ya CCM na nimeona sio mbaya nikitamka kuwa naungana nanyi rasmi, ahsanteni sana kwa kunipokea na kama niliposikia hotuba ya Mwenyekiti ni kweli kuwa sisi akina mama ndiyo wenye jukumu la kubeba nchi. Na mimi naungana na akina mama wenzangu wa UWT wenye malengo ya kuendeleza taifa", amesema mama Anna Mghwira.

Mama Anna Mghwira anakuwa kiongozi mkubwa wa tatu kitaifa wa ACT Wazalendo kujiunga na CCM ndani ya mwaka huu.

Polisi Wakwama Kumhoji Tundu Lissu

$
0
0
Jeshi la Polisi limekwama kumhoji Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), akiwa hospitalini Nairobi, Kenya baada ya kiongozi huyo kusema kwamba polisi wa Tanzania hawawezi kumhoji akiwa nchini Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya nchi.

Kauli ya Lissu imekuja siku 10 tangu Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, kuiambia Nipashe kuwa wametuma askari wawili kwenda Nairobi kuchukua maelezo ya Lissu, baada ya Mbunge huyo kukubali kuhojiwa.

"Hadi sasa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania hajamwomba Mwanasheria Mkuu mwenzake wa Kenya ruhusa ya mimi kuhojiwa na Polisi wa Kenya juu ya shambulio hilo kama inavyotakiwa na sheria husika za nchi yetu," amefafanua Lissu ambaye ni mwanasheria kwa taaluma.

Aidha kwa upande wa IGP Sirro Alipoulizwa maoni yake juu ya kauli hiyo ya Lissu kuwa polisi hawawezi kumuhoji nje ya mipaka ya nchi, aliiambia Nipashe “Mimi sina jibu.”

Wiki iliyopita, IGP Sirro alisema ametuma wapelelezi Nairobi baada ya kusikia Lissu amekubali kuhojiwa juu ya tukio hilo na matarajio yao pia ni kuwapata dereva na mlinzi wake.

“Tumetuma watu wetu kwenda kuchukua maelezo yake (Lissu). Mwanzo tuliomba kwenda lakini chama (Chadema) walikataa. Juzi tumesikia wamesema wapo tayari". Sirro

Allifafanua kwamba  lengo kubwa ni kujua mazingira ya shambulio yalikuwaje na kwamba ikiwezekana wampate dereva na msaidizi huyo wa Lissu ili kurahisisha upepelezi wa tukio lenyewe.

Kanisa la Gwajima labomolewa usiku

$
0
0
Kufuatia zoezi la serikali la kupanua na kuboresha miundo mbinu mbalimbali nchini hususan ya barabara katika jiji la Dar es Salaam ambapo imelazimu baadhi ya maeneo kubomolewa ili kupisha zoezi hilo la upanuzi, Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima nalo limekumbwa na kadhia ya kubomolewa.

Kanisa hilo lililoko jirani kabisa na Barabara ya Morogoro ambayo serikali imepanga kuipanua ili kurahisisha usafiri na kupunguza foleni, lilitakiwa kubomolewa kutokana na kuwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara hiyo.

Mchungaji Biyagaza wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko chini ya Askofu Gwajima, ameeleza kuwa serikali iliwapatia notisi ya siku 30 ili wabomoe kipande cha jengo la kanisa hilo kilichopo ndani ya eneo la hifadhi ya barabara.

“Ni kweli tunayo notice ya mwezi mmoja ya kuhakikisha kwamba eneo ambalo ni hifadhi ya barabara tunaliacha. Na hifadhi ya barabara ni mita 90 kuanzia katikati. Bahati nzuri wale waliokuja kuweka alama zao walipofika hapa na wahandisi , mafundi na baadhi ya watu wa kanisani walikuwepo. Basi tukawaambia wapime mita 90 zinapoishia. Kwa hiyo wakapima mita 90 zilipoishia wakaweka alama, wakasema basi nyie mnaweza mkabomoa upande huu na upande huu mkauacha kwa ajili ya hifadhi ya barabara,” alisema Mchungaji Biyagaza.

“Sisi baada ya hapo tukaona tujipange kwa ajili kuachia eneo la barabara ili shughuli nyingine ambazo ni mpango wa maendeleo ya serikali ziweze kuendelea na sisi tuweze kuendelea na eneo letu vizuri. Kwa hivyo kile kipande chote ambacho ni cha barabara na tukaongeza ndani kidogo chote tumekiondoa. Na hili eneo linalobaki tunapaimarisha ili nyumba ya Bwana iweze kufanya kazi yake ya kutoa huduma za kiroho,” aliongeza.

Mchungaji Biyagaza alieleza japokuwa eneo la jengo limepungua, eneo lililobakia linaimarishwa ili kanisa hilo liweze kuendelea kutoa huduma za kiroho kwa waumini wake.

Aidha kufuatia zoezi hilo la upanuzi wa barabara ya Morogoro ambalo linaenda sambamba na ujenzi wa barabara za juu (fly-over) katika makutano ya barabara eneo la Ubungo, umepelekea kubomolewa kwa majengo mbalimbali ikiwemo majengo ya wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na jengo la Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania ambayo yamebomolewa kufuatia agizo la Rais Dkt. John pombe Magufuli.

Rais Magufuli awapa neno wajumbe wa Baraza Kuu wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT)

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli amewataka wajumbe wa Baraza Kuu wa Umoja wa Wanawake CCM(UWT) kuchagua viongozi ambaye atakuwa anajali wanawake na siyo kujali tumbo lake.

Akizungumza na wajumbe hao leo Ijumaa wakati akifungua mkutano huo Rais Magufuli amesema watakapokuwa wanachagua viongozi leo Ijumaa wasiangalie wamepewa kanga kiasi gani, wala amelipiwa hoteli ya aina gani.

“Nataka mchague kiongozi wa kujali wanawake na sio kujali tumbo lake na awe mtetezi na shida zao wala habagui,” amesema Rais Magufuli.

Amesema anawapenda akina mama hivyo wachague mtu kwa matakwa yao.

“Viongozi wa jumuiya hii wanatakiwa kujua historia na kuipigania jumuiya hii muhimu kwa CCM,”

“Wanawake ndio wapigaji kura waaminifu na ukiahidiwa kura nao jua utashinda.”

Amesema, “Chama tunakata kiwe cha wananchi na sio cha mtu binafsi na kiongozi atakayechaguliwa aendane na mabadiliko ya ndani ya chama.”

Msigwa Awachana Wapinzani Wanaohamia CCM

$
0
0
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema wanasiasa wanaohama kutoka vyama vya upinzani kwenda CCM, wanafanya uamuzi huo kutokana na uoga.

Msigwa amesema hay oleo Ijumaa wakati akihojiwa katika kipindi cha Morning Trumpet kilichorushwa na televisheni ya Azam akiwa na Mbunge wa Temeke, (CUF) Abdallah Mtolea.

Msigwa amesema kufanya siasa ndani ya CCM kuna urahisi kuliko kufanya nje ya chama hicho kwa sababu unafanya siasa ukiwa unazungukwa na polisi na unakuwa unalindwa lakini unapokuwa upinzani unakuwa kama yatima, hali inayopelekea wengine waoga kushindwa na kuamua kwenda CCM.

“Hawa wenzetu wanaochukuliwa mi naamini kuna uoga na kuna kununuliwa, mtu akisema sisi wapinzani tuwananunua watu wa kutoka CCM, unawanunua watu wa CCM waje kufanya nini upinzani, kuna mabomu, kuna dhiki, yani mtu atoke CCM ambapo analindwa aje upinzani kwenye dhiki? Kwa hiyo hii propaganda kuwa upinzani nao unanunua watu ni ya kutaka kupotosha umma tu,” amesema Msigwa.

Msigwa ameongeza kuwa gharama za kuwa upinzani ni kubwa ndio maana hata idadi ya wanasiasa wanaohama kutoka upinzani kwenda CCM ni wengi kuliko wanaotoka CCM kwenda upinzani na ndio maana hata baadhi ya wanasiasa hao baada ya kuona hali ya joto kisiasa imezidi kuwa kali wametangaza kurudi nyumbani CCM.

Akichangia mada katika mjadala huo kuhusu wimbi la wanasiasa wanaohama vyama vya siasa Mtolea alikosoa wanasiasa wanaohama vyama na kuacha ubunge kwa kutoa sababu za kuunga mkono juhudi za Serikali.

“Hawa wanaosema kwamba wamefurahishwa na kazi ya Rais, hivi kumuunga mkono Rais ndio umtie hasara, kwa sababu ukijivua ubunge, jimbo lile unaliacha wazi na uchaguzi lazima ufanywe kwa matakwa ya sheria, leo kurudia uchaguzi kwa jimbo moja ni takriban Sh70bilioni, sasa Je unamsaidiaje Rais kwa kuitia hasara Serikali kwa kurudia uchaguzi kwa gharama hizo.”

Mtolea amesema baadhi ya wanasiasa waliotangaza kuondoka upinzani kwa kudai upinzani umeishiwa ajenda, wasichokifahamu ni kwamba vyama vya siasa haviendeshwi kwa ajenda bali vinaendeshwa kwa itikadi au misingi iliyosababisha kuundwa kwa chama cha siasa ili waweze kumaliza kero mbalimbali nchini na njia ya haraka ya kufikia maendeleo ya nchi.

Mtolea alitolea mfano tatizo la kukatika kwa umeme kuwa linaweza kuwa ajenda lakini tatizo hilo likiisha, ajenda hiyo inakua imekwisha, lakini itikadi ya chama inabaki.

Askari wa 14 wa JWTZ wauawa katika shambulio nchini DR Congo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kuuawa kwa askari 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopo katika operesheni ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Pamoja na askari hao kuuawa, askari wengine 44 wamejeruhiwa na 2 hawajulikani walipo.

Kufuatia vifo hivyo Mhe. Dkt. Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Salvatory Mabeyo, Maafisa na Askari wa wote JWTZ, familia za marehemu na Watanzania wote kwa kuwapoteza mashujaa waliokuwa wakitekeleza wajibu wao.

“Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na vifo vya vijana wetu, askari shupavu na mashujaa waliopoteza maisha wakiwa katika majukumu ya kulinda amani kwa majirani zetu DRC” amesema Mhe. Dkt. Magufuli.

Amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kuwa watulivu na kuwa na subira wakati Serikali ikiendelea kuchukua hatua zinazostahili baada ya kutokea tukio hilo, na pia amewaombea majeruhi wote wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kawaida.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino, Dodoma
08 Desemba, 2017

Wabunge wa CHADEMA waachiwa kwa dhamana

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro imetupilia mbali hati ya kiapo cha kupinga dhamana ya wabunge Suzan Kiwanga(Mlimba), Peter Lijualikali (Kilombero) na washtakiwa wengine 37 waliofikishwa mahakamani hapo kwa makosa nane.

Mbele ya Hakimu, Ivan Msaki mahakama ilitupilia mbali kiapo hicho na kueleza kuwa washtakiwa wote dhamana yao iko wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja watakaosaini dhamana ya Sh 5 milioni na pia barua za dhamana lazima zisainiwe na wenyeviti wa vijiji ama maofisa watendaji.

Katika kiapo kilichowasilishwa awali mahakamani hapo na upande wa mashtaka kupitia wanasheria wa Serikali, Sunday Hyera na Edga Bantulaki ulieleza sababu walizodai kuwa ni za msingi za kupinga dhamana na kwamba kuwepo nje kwa washtakiwa  kunaweza kuharibu upelelezi wa kesi hiyo.

Kufuatia hoja hiyo upande wa utetezi unaowakilishwa na mawakili wanne wakiongozwa na wakili Peter Kibatala uliamua kuwasilisha hati ya kupinga kiapo hicho kwa madai kuwa  kiliandikwa bila ya kuzingatia misingi na matakwa ya kisheria.

Wakili Kibatala alidai kuwa miongoni mwa mapungufu yaliyokuwemo kwenye kiapo hicho ni pamoja na kutokuonyesha majina ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Malinyi (OCD) ambaye alitajwa kwenye kiapo hicho kama chanzo kilichotoa taarifa zilizotengeneza mashtaka yanayowakabili wabunge hao na wenzao.

Alidai kuwa mapungufu mengine yaliyokuwepo kwenye kiapo hicho ni utofauti wa tarehe ya kuandika kiapo hicho na kusainiwa na hivyo waliiomba mahakama kuzingatia mapungufu hayo.

Kutokana na mvutano huo wa kisheria baina ya pande hizo mbili Hakimu Msaki aliamua kupitia hoja za msingi za kisheria na hivyo kubaini mapungufu yaliyopo kwenye kiapo hicho na kueleza kuwa mapungufu hayo hayawezi kurekebishwa na kwamba kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria na si kufundisha namna ya kuandika kiapo.

Kwa msingi huo Hakimu Msaki alitupilia mbali hati hiyo ya kiapo cha kupinga dhamana na kueleza kuwa washtakiwa hao watakuwa nje kwa dhamana wakati kesi yao ikiendelea.

Kabla ya kupewa dhamana washtakiwa hao walikaa rumande kwa siku 12 hali iliyosababisha kesi hiyo kuvuta hisia za watu hususani viongozi na wanachama Chadema waliokuwa wakifulika mahakamani hapo.

Zitto Kabwe azungumzia hatima ya ACT- Wazalenddo

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amefunguka kuwa  ndani ya chama chake (ACT) kuna watu wengi wakiwemo wanachama wa kutosha  akimaanisha hajabaki mwenyewe.

Zitto amefunguka hayo akimjibu mfuasi wake wa kwenye mtandao wa kijamii ambaye alitoa maoni yake kwa kumuuliza Mh. Kabwe haoni kama amebaki peke yake, ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mgombea urais wa chama chake Anna Mghwira kujiunga na CCM huko Dodoma.

Akimjibu mfuasi huyo Zitto amesema "Chama chetu ACT Wazalendo kina madiwani 42, kina wenyeviti wa mitaa, vitongoji na wajumbe wa Serikali za Vijiji/Mitaa 507, Viongozi kila mkoa na jimbo, wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Ni dhahiri tuna watu wengi na wanachama wengi wa kutosha"

Hivi karibuni CCM ilijivunia wanachama wapya ambao waliwahi kuwa na nafasi ya uongozi ACT Wazalendo ambapo baadhi yao ni Prof Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba, Alberto Msando na jana  Anna Mghwira.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Nkasi atumbuliwa kwa tuhuma za rushwa

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jafo amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wilaya ya Nkasi, Julius Kawondo kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya yaliyoisababishia Serikali hasara ya Sh 7 bilioni

Jafo amewaambia waandishi wa habari jana Ijumaa kuwa Kawondo ameshindwa kusimamia kile alichopaswa kukifanya kwa wakati katika eneo lake la utumishi.

"Natumia Sheria ya Serikali za Mitaa Sura ya 4 kifungu cha kwanza hadi tano pamoja na Sura ya 287 ya sheria hiyo ambavyo vinanipa mamlaka hayo," alisema Jafo.

Alisema fedha hizo zilikuwa za mradi wa maji wa Kijiji cha Kamwanda ambako mkurugenzi alishirikiana na mmoja wa maofisa kutoka wizara ya maji.

Jafo alimuomba Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe kumchunguza mmoja wa watumishi katika wizara yake ambaye alishirikiana na mkurugenzi huyo kuhujumu mradi wa maji katika Kijiji cha Kamwanda wilayani humo.

Taarifa ya SUMATRA kwa wamiliki wa mabasi kuhusu usafiri mwisho wa mwaka


Waziri Kigwangalla ateua kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Tanzania

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangalla  jana Desemba 8,2017 Mjini Dodoma, ameunda kamati ya kuongoza maandalizi ya namna watanzania na wageni wa Tanzania watakavyosherehekea Utanzania wao  kwenye mwezi maalum utakaojulikana kama ‘TANZANIA HERITAGE MONTH’.

Akielezea wakati wa kutangaza kamati hiyo iliyojumlisha wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari, wanamichezo na wadau wengine mbalimbali na wafanyabishara, alisema:

“Kwenye mwezi huu kila kitu kitakuwa cha kitanzania na tutataka kwenye kila ofisi ya umma, ofisi binafsi, shule, chuo, hotel, balozi zetu n.k mtu akifika tu, ‘utanzania’ wetu uonekane!” alieleza Dk.Kigwangalla.

Utanzania huo ambapo kila mwezi huo utakapofika ambapo moja ya mambo hayo ni pamoja na aina ya mavazi maalum, vyakula,  na mambo mengine yanayobeba na kujumuisha Utanzania.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Disemba 9

Jinsi Kitambi Kinavyopatikana na Jinsi Kinavyoondolewa na Dawa ya Mkataa Kitambi

$
0
0

Kitambi  ni  ile  hali  ya  tumbo  kuwa kubwa  na  kuchomoza  kwa  mbele  na  wakati mwingine  kufikia  hatua  ya  kunin’ginia.

JINSI  KITAMBI  KINAVYO  PATIKANA
Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati  ya bilioni 50  hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili wa binadamu.

 Kwa wanawake  seli hizo  zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye  nyonga, kiunoni na kwenye makalio.

Kwa upande  wa  wanaume seli  hizo zinapatikana  sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia.

Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:

i.Njia  ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi

ii.Na  njia  ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

SABABU ZA KUPATA KITAMBI
Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika  mwili  wa  mwanadamu, hali  inayo  sababishwa  na  mtu  kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.

VYAKULA  VINAVYO  CHANGIA KULETA  KITAMBI

Vyakula vinavyochangia  kuleta  kitambi ni  pamoja  na :
i.Vyakula  vyenye  mafuta  mengi  kama  vile  nyama nyekundu  (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama  ya  kuku  wa  kizungu  ( iwe  ya  kuchemsha, kukaanga  ama  kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi ya kukaanga kwa  mafuta  (chips) pamoja  na  pizza.

ii.Vyakula vyenye wanga mwingi kama  vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate  mweupe.

iii. Vyakula  na  vinywaji  vyenye  sukari  nyingi  iliyo  ongezwa( added  sugar ), kama  vile  soda  na  keki.

iv. Vyakula  vilivyo  tengenezwa  kwa  ngano  na  sukari kama  vile  keki, skonzi, chapatti, maandazi, mkate  mweupe  nakadhalika

v. Pamoja  na  vinywaji  vilivyo  tengenezwa  kwa  kutumia  ngano  kama  vile  bia  za  aina  mbalimbali  na  kadhalika.

Vyakula  vilivyo  tajwa  hapo  juu, vikitumiwa  bila  kuzingatia  kanuni  za  mlo  kamili, huchangia  kuleta  tatizo  la  kitambi.

vi. Sababu nyingine ni  kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na  viungo(  physical  exercises  )  kwa  muda  mrefu.

JINSI YA KUJUA KAMA UNA KITAMBI
Kitambi kinaweza kuonekana kirahisi kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya vipimo vya kiuno(waist) na nyonga (hips).

Mzingo wa kiuno ukiwa >102 cm au 40  kwa wanaume na >88 cm au 35  kwa wanawake, na uwiano wa kiuno na hips(Waist-Hip Ratio) ikiwa >0.9 kwa wanaume na >0.85 kwa wanawake.

BMI ya 30 au zaidi inaashiria 'Obese' uzito kuzidi kiasi. Kuwa na mzingo uliozidi kawaida ni kiashiria hatari cha matatizo ya kimetaboliki, kuliko hata cha BMI.

Kipimo kingine cha kitambi ambacho kimeonyesha uwezo zaidi kuliko BMI katika kutabiri uwezekano mkubwa wa magonjwa ya moyo ni Index Of Central Obesity(Waist-To-Height Ratio-WHtR) ambapo uwiano ukiwa sawa na 0.5 au zaidi, hii ikimaanisha mzingo wa kiuno angalau ni nusu ya kimo cha mtu.

Kipimo kingine ni Body Volume Index, kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.

MAMBO  YANAYO  MUWEKA  MTU  KATIKA  HATARI  YA  KUPATWA  NA  KITAMBI
Tumekwisha  ona  hapo  juu jinsi  kitambi  kinavyo  patikana  na  vyakula  pamoja  na  sababu  nyinginezo  zinazo  sababisha  kutokea  kwa  kitambi, sasa  tutazame  mambo  yatakayo  kufanya  uwe  katika  hatari  ya  kupatwa  na  kitambi.

Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za kitaalamu, mambo  yafuatayo  huwaweka  watu  katika  hatari  kubwa   ya  kupatwa  na  kitambi :

1. Ulaji  mbovu  wa  chakula; Ulaji  mbovu  wa  chakula  ni  ulaji  usio  zingatia  kanuni  za  mlo  kamili. Hapa  mtu  hufululiza  kutumia  chakula  cha  aina  fulani  pekee  bila  kuzingatia  aina  nyinginezo  za  chakula.  Mfano; mtu  anaweza  kuwa  anakula  mlo  ufuatao :

Asubuhi :  Mchemsho  ama    supu  ya  ng’ombe , chapatti  tatu  na  soda  moja.  Mchana :   Ugali  nyama  choma anashushia  kwa  maji  na  soda.

Jioni :  Mchemsho  wa  kuku  na  bia  mbili  nakuendelea.

Usiku  :  Chips  mayai  au  chips  kuku  au  chips  mishikaki  na  bia.

Mtu  huyu  akiendelea  na  utaratibu  huu  kwa  muda  mrefu, ni  lazima  atapatwa  na  kitambi.

2. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  mafuta  mengi

3. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye wanga  mwingi  

4.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  sukari  iliyo  ongezwa ( added  sugar  ).

5.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vya  ngano.

6.Ulaji  mfululizo  wa   vinywaji  vyenye ngano  na  sukari.

7.Kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na viungo  ( physical  exercises  ).

Mhusika  anapokuwa  katika  makundi  yote  yali yotajwa  hapo  juu, hali  huwa  mbaya  zaidi. 

NJIA ZA KUONDOA KITAMBI
Kuwa  na  kitambi  ni  lugha  ya  mwili  ( body-language )  inayo  leta  ujumbe  kwako  kwamba  “ Mwili    wako  haupo  salama  tena “

Kama  una  kitambi   maana  yake  una  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini, mwili  wako  unatumika  kuhifadhi  mafuta  usiyo  yahitaji.

Hali  hii  kitabibu  imaanisha  kwamba, ogani  nyinginezo  zilizomo  ndani  ya  mwili  wako  zinao gelea  kwenye  mafuta( fats  )  yasihotika  yaliyomo ndani  ya  mwili  wako,  jambo  linalo  kuweka  katika  hatari  kubwa  sana  ya  kushambuliwa  na  magonjwa  hatari  kama  vile  shinikizo  kubwa  la  damu, kiharusi  na kisukari  na  kwa kutaja  machache.

Hivyo  basi  ili  kuondokana  na  hatari  hiyo, yakupasa   kupambana  kuondoa  hayo  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini  mwako.

NJIA  ZA  KUONDOA  KITAMBI.
Unaweza  kuondokana  na  kitambi  kwa  kufanya  diet  pamoja  na  mazoezi ya  mwili  na  viungo.

Vilevile  unaweza  kuondoa  kitambi  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  dawa  asilia  ya  kuondoa  kitambi  na  kuondoa  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

DAWA   ASILIA  YA  KUONDOA  KIAMBI  NA  MAFUTA  MWILINI.
Hii  ni  njia  ya  uhakika  kabisa  ya  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

 Unaweza  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  DAWA  ASILIA   IITWAYO YA  MKATAA  KITAMBI.

 Dawa   hii  ni  ya asili  kabisa
“  Pure  Herbal “, ambayo  haijachanganywa  na  kemikali  yoyote, haina  side  effect kwa  mtumiaji  na  inaondoa  kabisa  tatizo  la  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

JINSI  DAWA  YA  MKATAA  KITAMBI  INAVYO  FANYA  KAZI.
1.Huyeyusha  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

2.Husaidia  kupunguza  hamu  ya  chakula.

3.Inazuia  kutengenezwa  kwa  seli  za  mafuta  ( fat cells  ) katika  mwili  wa  mwanadamu. Unapokula  chakula  chenye  mafuta  mengi, dawa  hii asilia  hupambana  kuyafanya  mafuta  hayo  yasitengeneze  seli  za  mafuta  mwilini  mwako. Hali  hii  huuepusha  mwili  wako  kuhifadhi  mafuta   yasiyo  hitajika  mwilini.

4. Husaidia  kupunguza  uzito wa mwili  kwa  haraka  sana  endapo  itatumika  pamoja  na  diet  ya  kabechi.

UFANISI  WA  DAWA.
Ufanisi  wa  dawa  hii  ni  wa  asilimia  mia  moja. Dozi  ya  dawa  hii  hutumika  kwa  muda  wa  siki  ishirini  na  moja.

MATOKEO  YA  DAWA:
Dawa  hii  huondoa  kabisa  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

BEI  YA  DAWA :
Dawa  hii  inaoatikana  kwa  kiasi  cha  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU  (Tshs. 50,000/=)

MAHALI  TUNAPO  PATIKANA.
Tunapatikana  jijini  DAR  ES  SALAAM, katika  eneo  la  UBUNGO  karibu  na  SHULE  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

KWA  WATEJA  WASIO  WEZA  KUFIKA  OFISINI  KWETU.
Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu  Tabata, tunao  utaratibu  wa  kuwafikishia  dawa  mahali  popote  walipo  ndani  ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  DAR  ES  SALAAM.
Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  Dar  Es  salaam, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  MABASI.

Kwa  wateja  wa  ZANZIBAR  tunawatumia  dawa  kwa njia  ya  boti.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  NCHI:
Kwa  wateja  wa  nje  ya  nchi, tunatumia  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA : 0766  53 83 84

TUTEMBELEE:

Mamia wajitokeza siku ya Uhuru, uwanja wafungwa

$
0
0
Wakazi wa mji wa Dodoma na viunga vyake mapema leo Jumamosi, Desemba 9, 2017 wamejitokeza kushuhudia maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Taratibu za ukaguzi wa kiusalama, zilifanya misururu mirefu baada ya kutumika geti moja kuingilia ndani ya Uwanja wa Jamuhuri.

Hali hiyo ilifanya misururu mrefu kuanzia geti la kuingilia uwanjani kufika katika barabara inayoelekea Nkuhungu.

Mabasi makubwa yanayotoka katika wilaya za jirani yalionekana yakishusha watu tangu saa 11.00 alfajiri kuwahi foleni.

Watu walianza kuingia uwanjani huku vikundi mbalimbali vya burudani vikitumbuiza.

Saa 2:00 asubuhi, gwaride maalumu lililojumuisha vikosi vya ulinzi na usalama viliingia uwanjani.

Viongozi mbalimbali walianza kuwasili uwanjani kuanzia saa 1:00 asubuhi wakiwemo mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mama Fatma Karume, mke wa Rais ya Kwanza wa Tanzania Mama Maria Nyerere na aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais, Mohammed Gharib Bilal.

Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema ni baadhi ya viongozi wa kisiasa walioonekana uwanjani hapo.

Viongozi wengine waliofika asubuhi uwanjani hapo ni Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, mke wa Rais, Janeth Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, majaji wakuu wa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, Spika wa Bunge Job Ndugai, mawaziri na wabunge.

Tayari Uwanja wa Jamhuri umejaa na wananchi wamezuiwa kuingia katika uwanja huo na milango yote imefungwa.

Umoja wa Mataifa walaani kuuawa wanajeshi wa Tanzania nchini DRC

$
0
0
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio lililotekelezwa katika kambi ya walinzi wa amani iliyopo Semuliki, Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kupelekea vifo vya wanajeshi 20 huku wengine 53 wakijeruhiwa.

Kambi ya jeshi hilo la ulinzi wa amani (MONUSCO) ilishambuliwa Disemba 7 jioni na kupelekea vifo vya wanajeshi 15 wa Tanzania na 5 wa DRC.

Wajumbe hao wametuma salamu za pole kwa familia za wafiwa, serikali ya Tanzania na DRC lakini pia MONUSCO huku wakiwatakia majeruhi afya njema na wapone haraka.

Aidha, katika taarifa hiyo wajumbe hao wameeleza kuwa kushambulia kambi za walinzi wa amani ni tukio ambalo linachukuliwa kuwa ni uhalifu wa kivita katika sheria za kimataifa na kwamba wahusika hawawezi kusamehewa kwa matendo hayo.

Serikali ya DRC imetakiwa kuhakikisha kuwa wahusika wa tukio hilo wanakamtwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kutaka makundi yote ya kihalifu kusitisha mapigano.

Pia, wamewashukuru wanajeshi na watu mbalimbali ambao wanahatarisha maisha yao kila siku kwa ajili ya kuhakikisha amani inakuwepo duniani, na kwamba tukio kama hilo la kusikitisha linaikumbusha dunia kuwa ni kiasi gani watu hawa wameweka maisha yao hatarini kwa faida ya wengi.

Shambulio hilo la DRC ni kubwa zaidi kuwakumba walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa kwa miaka ya hivi karibuni.

Baraza la Usalama alimesema kwamba litaendelea kushirikiana kwa karibu na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN nchini DRC na MONUSCO kuhakikisha kuwa wanatekeleza ipasavyo malengo yao.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>