Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mke wa Kafulila atoa ya moyoni uamuzi wa mumewe Kuikimbia CHADEMA

$
0
0
Mke wa aliyewahi kuwa mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, Jesca Kishoa, amemtaja mumewe kuwa ni mtu aliyeingia kundi la wanasiasa wasio na msimamo.

Kishoya amesema wakati wote mumewe amekuwa na msimamo usioyumba lakini anashangazwa kaingia katika mtego mbovu.

"Bado naamini kuwa Chadema ni mahali sahihi kabisa ambapo siwezi kufikiri siku moja nitatoka,  hivyo siyumbi kwa hilo na wanaonipigia  simu watambue hilo," amesema  Kishoya

Amesema  taarifa za mumewe kujiondoa Chadema amezipata kupitia vyombo vya habari akiwa Dodoma kwenye kampeni za udiwani lakini alimpigia wakazungumza sana na bado hakumpa sababu zilizoshiba za kuondoka kwake.

Hata hivyo amepinga madai ya Kafulila kuwa anaondoka upinzani kwa sababu ya upinzani kushindwa kusimamia ajenda ya ufisadi badala yake akasema ana mambo yake.

"Wanasiasa ambao hawana misimamo ndiyo husingizia vitu hivyo, siamini kama maneno yale yalitoka rohoni mwake, CCM siyo mahali sahihi kwa kuzungumzia mambo ya ufisadi hata kidogo, "

Mbuge huyo amesema wakati wote katika maisha yao mumewe amekuwa ni muumini mzuri wa kuhubiri habari za ufisadi ikiwemo pale alipotoa maisha yake kuhusu sakata la Escrow.

Tundu Lissu kusafirishwa kwa matibabu nje ya Afrika......Familia yataka Lissu akahojiwe Nairobi

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anatarajiwa  kusafirishwa nje ya nchi kwa matibabu mwezi mmoja kuanzia sasa.

Familia yake imesema Lissu baada ya kupata matibabu nje ya nchi amepanga kufanya mambo matano akirejea salama .

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Novemba 23, kaka wa Tundu Lissu, Wakili Alute Mughwai alisema taratibu za kumsafirisha  nje ya nchi zimeanza.

Lissu, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu na mwanasheria mkuu wa chadema amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 alipokuwa akirejea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma Septemba7.

"Awamu ya tatu ya matibabu yake ni maalumu sana kwani itahusu pia mazoezi ambayo kama haitafanyika vyema ataweza kupata ulemavu wa kudumu,"alisema.

Hata hivyo, alisema  Lissu atapelekwa nje kwa ndege ya kawaida tofauti na hali yake ya awali alipotakiwa kusafirishwa  na ndege maalumu za wagonjwa.

"Itatolewa taarifa ni lini ataondoka kwa matibabu na atakwenda nchi gani, hasa baada ya kupata ushauri wa mwisho wa madaktari katika hospitali Nairobi," alisema.

Mughwai alisema amezungumza na Lissu akiwa Hospitali Nairobi na amemueleza kuwa  akirejea tu nchini, kuna mambo makubwa matano ambayo atafanya.

Alisema jambo la kwanza, ambalo atafanya ni kwenda katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kuwashukuru madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo kwa kuokoa maisha yake siku aliyopigwa risasi.

Wakili Mughwai alisema Lissu amemwambia baada ya hapo atakwenda kanisani na msikitini kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya ibada maalumu.

"Baada ya ibada, tutaangalia utaratibu kifamilia kama itawezekana  kwenda kufanya matambiko  kwenye makaburi ya wahenga wetu 76 waliofariki katika vita miaka 200 iliyopita," alisema.

Alisema  baada ya hapo, anatarajia kuendelea kufanya kazi zake za siasa na uwakili pale alipoishia kwa ari kubwa .

Wakili Mughwai alisema  jambo la tano atahakikisha  anasimama na kupambana kisheria na watu waliotaka kukatisha maisha yake baada ya kumpiga risasi.

"Amesema atahakikisha anasimamia jambo hili kwa uwezo wake wote ili kuhakikisha wanafikishwa katika vyombo vya sheria waliohusika na uovu huo," alisema.

Familia yataka Lissu akahojiwe Nairobi
Akizungumzia juu ya upelelezi wa shauri la Lissu, Mughwai alisema bado msimamo wao upo palepale wanaomba wapelelezi kutoka nje ya nchi washirikiane na wapelelezi wa ndani kuwakamata watuhumiwa.

Alisema ingawa familia ya Lissu iliandika barua tangu Septemba 16, kutaka wapelelezi wa kimataifa na kujibiwa na mwanasheria mkuu Septemba 20  kuwa jukumu la upelelezi ni la polisi.

 "Tunataka wapelelezi wa nje kushirikiana na wa ndani kwa sababu hatuna imani na upelelezi kutokana na kasi ndogo kwani hadi sasa wamekuwa wakieleza kukwama upelelezi kutokana na kutomuhoji dereva wa Lissu,"alisema.

Hata hivyo, alisema kwa sasa Lissu anaweza kuongea mwenyewe hivyo, jeshi la polisi linaweza kwenda Nairobi kumuhoji na atawapa maelezo yote ikiwepo watu ambao aliwatambua.

"Bila shaka Lissu atawaeleza watu hao, walimshambulia kwa sababu gani,"alisema.

Familia yaelezea gharama
Katika hatua nyingine, Mughwai alisema Oktoba 2, familia ya Lissu ilikutana na viongozi wa bunge kujadili matibabu yake ambayo ni haki yake kisheria.

Alisema baada ya mazungumzo hayo, Oktoba 8, familia iliandika barua rasmi kwa katibu wa bunge kwa kuzingatia sheria ya bunge namba 14 kifungu cha 24 kuhusu stahiki za mbunge.

Alisema barua hiyo, ilipelekwa bungeni kwa kutumia shirika la kubeba mizigo na vifurushi la DHL na kupokelewa Oktoba 19 na baadaye aliwasiliana na Spika Job Ndugai na kumweleza juu ya barua hiyo na aliahidiwa kuwa suala hilo litashughuliwa.

Hata hivyo, alisema familia haijapata mrejesho tangu wakati huo hadi Novomba 11, alipoamua kumpigia katibu mpya wa bunge baada ya kushauriwa na Spika Ndugai ambaye aliahidi kufuatilia.

"Hivyo hadi sasa bado Bunge halijaanza kugharamia matibabu ya Lissu kama sheria inavyosema na Lissu amekuwa akitibiwa kwa michango ya watu mbali mbali," alisema

Alisema michango hiyo ambayo inakusanywa katika akaunti maalumu ya Chadema  na pia kupitia chama cha mawakili(TLS) ndio hadi sasa inatumika.

"Tutaendelea kulitaka Bunge kugharamia matibabu kwani sio suala la hiari, ni haki ya mbunge lakini pia tunaomba wananchi waendelee kuchangia matibabu ya Lissu kupitia akaunti iliyotolewa na Chadema, chama cha TLS na kwa familia"alisema

Akanusha mgawanyiko juu ya matibabu
Katika hatua nyingine, Mughwai alisema, familia ya Lissu, Chadema na chama cha Mawakili wa Tanganyika(TLS), hawana mgawanyiko wowote juu ya matibabu ama hatua zinazoendelea za kumtibu Lissu.

Wakili Mughwai alisema wanasikitishwa na taarifa kuwa familia imegawanyika juu ya uamuzi wa kuliomba bunge kugharamia matibabu ya Lissu.

"Tupo kitu kimoja wote familia yetu tupo pamoja kwa yote na Lissu anajua hatua zote kwani hata makamishna wa bunge walipomtembelea Oktoba 23 aliwauliza kuhusu stahiki zake kama mbunge,"alisema.

Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nje ya nyumba yake akirejea kutoka vikao vya bunge Dodoma, Septemba 7 na kukimbizwa hospitali ya Nairobi kwa matibabu ambapo hadi sasa anapatiwa matibabu.

Rais Magufuli Mgeni Rasmi Uzinduzi wa Hospitali ya Taaluma MUHAS Kampasi ya Mloganzila

$
0
0
Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa hospitali ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Novemba 23,2017 Kaimu Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Apolinary Kamuhabwa amesema hospitali hiyo itakayofunguliwa Jumamosi Novemba 25,2017 imepewa hadhi ya kuwa hospitali ya rufaa ya Taifa.

Amesema hilo linatokana na kutoa huduma za kitabibu zinazohitaji madaktari bingwa na madaktari bingwa wabobezi, huku ikiwa imesheheni vifaa vya kisasa.

Profesa Kamuhabwa amesema uwepo wa vifaa vya kisasa na madaktari wa kutosha utasaidia hospitali kupunguza kwa kiasi kikubwa wagonjwa kwenda nje ya nchi kupata tiba.

"Hospitali hii itasaidia kuongeza idadi ya madaktari bingwa kwa kuwa imewekewa mazingira rafiki kwa ajili ya kufanya uchunguzi na utafiti ili kuboresha huduma na matibabu," amesema.

Amesema ujenzi wa hospitali hiyo ni mwendelezo wa Kampasi ya Mloganzila ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha chuo hicho.

Naibu makamu mkuu wa chuo na mwangalizi wa huduma za hospitali, Profesa Said Abood amesema hospitali hiyo ina mfumo wa Tehama katika kutuma na kupokea sampuli hivyo kurahisisha kasi ya majibu na huduma.

Amesema huduma zote za hospitali zipo katika jengo moja, hivyo hakutakuwa na usumbufu wa mgonjwa kuzunguka kufuata utaratibu ili kupata matibabu.

"Tuna vifaa vya kisasa ambavyo ni vichache nchini au havipo kabisa, mfano kifaa cha kuvunja mawe kwenye figo bila upasuaji," amesema.

Waziri Mkuu: Chuo Kikuu Ardhi Marufuku Kukodi Makampuni

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekipiga marufuku Chuo Kikuu Ardhi kukodi makampuni ya kufanya kazi mbalimbali kwa niaba yake.

Amesema kitendo hicho kinaharibu kazi na sifa ya chuo hicho kwa kuwa baadhi ya makampuni wanayoyapa kazi hayakidhi vigezo.

Waziri Mkuu  ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 23, 2017) kwenye ufunguzi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo Kikuu Ardhi.

“Kama kuna umuhimu wa kufanya kazi na kampuni ni bora muanzishe kampuni ya kwenu itakayofanya kazi vizuri ili kujiepusha na matatizo.”

Pia Waziri Mkuu amekiagiza chuo hicho kufanya tafiti zenye kuleta majibu ya maswali na changamoto mbalimbali zinazolikabili Taifa na Dunia.

Ametaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni mabadiliko ya tabia nchi, ujenzi holela, uharibifu wa mazingira na majanga ya asili kama mafuriko.

Amesema Serikali inaamini kuwa matokeo ya kazi zinazofanywa na chuo hicho zikiwemo tafiti ni chachu ya maendeleo ya taasisi za elimu ya juu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Dira ya Maendeleo ya Taifa imeweka mkazo wa kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kupato cha kati ifikapo 2025, hivyo wanahitajika wataalamu wa kutosha na wenye weledi.

“Hivyo Chuo Kikuu cha Ardhi kama taasisi ya Serikali inawajibu mkubwa wa kutayarisha wataalamu mbalimbali wa sekta za ujenzi, ukadiriaji majenzi na uhandisi wa mazingira.

Pia Waziri Mkuu amewataka watumie fursa hiyo ya kuadhimisha miaka 10 ya chuo hicho kujitafakari na kuona ni kwa namna gani wanaweza kuwekeza zaidi ili kuongeza tija ya uwepo wa taasisi hiyo kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

“Wekeni mikakati madhibuti itakayowezesha chuo kupiga hatua kubwa zaidi katika kipindi cha miaka 10 ijayo. Siku zote mjikite katika kutafuta kuwa na ubora zaidi ya wakati uliopita.”

Awali, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema Serikali inakkitegemea chuo hicho katika kufanikisha ajenda yake ya uchumi wa viwanda kwa kuwa kinatoa wataalamu wengi.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Mkuu wa chuo hicho ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya, Mwenyekiti wa Baraza la chuo Bibi Tabitha Siwale, Makamu Mkuu wa chuo Profesa Evaristo Liwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, wanafunzi na watumishi wa chuo hicho.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, NOVEMBA 23, 2017.

BREAKING NEWS:.Rais Magufuli amteua Dkt. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Novemba, 2017 amemteua Dkt. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi.

Dkt. Wilbrod Peter Slaa ataapishwa baada ya taratibu kukamilika.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Novemba, 2017

Kafulila: "Ndoa yangu haihusiani na siasa"

$
0
0
Daudi Kafulila ambaye hapo jana amekihama chama cha CHADEMA, amesema suala la mke wake kuridhia au kutoridhia kwa yeye kuhama chama wakati yeye ni Mbunge wa chama hiko, ni suala ambalo halihusiani na ndoa yao.

Kafulila ameyasema hayo leo na kueleza kwamba linapokuja suala la ndoa hapo ndio huwa lazima wafikie makubaliano, lakini ikija suala la kisiasa kila mtu ana uamuzi wake ambao hawaingiliani kwani ndoa yao ilifngwa kanisani na sio kwenye chama.

“Haya ni maamuzi ya kisisasa, sisi ndoa yetu ilifungwa kanisani haikufungwa kwa mwenyekiti wa chama au kwenye chama, kwa hiyo ndoa ni jambo jingine na harakati ni mjambo jingine, yeye ni mke wangu lakini haimaanishi tunakubaliana kwenye kila kitu, tunakubaliana kwenye mambo ya ndoa, kwenye siasa kila mtu anaweza akatazama jinsi anavyotazama yeye na sio shida”, amesema Kafulila.

Hivi sasa kumekuwa na mvutano kati ya wanandoa hao baada ya Kafulila kuhama CHADEMA, huku mke wake akisema hakuwa na taarifa zozote, na hata hizo sababu zake za kuhama hazina ukweli na kumtaka aweke wazi sababu rasmi za kufanya hivyo

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Novemba 24

TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia

$
0
0
Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Peramiho, Songea.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho amethibitisha msiba huo.

“Nimepata taarifa jana usiku (Alhamisi Novemba 23,2017) kuwa Gama amefariki kwa kuugua shinikizo la damu,’’ amesema na kuongeza;
 

“Tunawasiliana na familia ili kujua utaratibu wa mazishi. CCM tunasikitika kwa msiba huu, msiba ni wetu sote.”

Gama enzi za uhai wake amewahi kuwa Mkuu wa wilaya za Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala kabla ya kuwa Mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Dk Slaa amshukuru Mungu kwa Kuteuliwa Kuwa Balozi

$
0
0
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua kuwa Balozi wa Tanzania na kusema kuwa yuko tayari kutoa mchango wake katika kulijenga taifa la Tanzania.

“Kwa sababu Ubalozi uko kwenye Idara za moja kwa moja za mkuu wa nchi, na bila shaka hakukuwa na sababu mkuu wangu kutotaka kuniteua, ninamshukuru kwa uteuzi huo kwa kuniona, ninachoweza tu kusema katika hatua hiyo ni kwamba ninao wajibu mkubwa hasa katika kipindi hichi cha kulijenga taifa letu,” amesema Dkt. Slaa.

Dkt. Slaa ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, na ambaye aliwahi kugombea nafasi ya Urasi kupitia chama hicho, alijiuzulu nafasi yake hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuondoka nchini.

Muda mfupi baadaye Dkt. Slaa alitangaza kutojihusisha tena na siasa za hapa nchini na akawa anaishi nchini Canada pamoja na mpenzi wake Josephine Mushumbusi.

Dk. Slaa, ambaye kwa sasa anaishi nchini Canada alikokwenda kwa masomo, tangu alipotangaza kuachana na siasa Septemba 1, mwaka 2015 aliweka wazi kuwa anafanya kazi zaidi ya mbili ili aweze kujipatia kipato kitakachomuwezesha kumudu gharama za maisha nchini humo.

Alitaja kuwa kwa sasa anafanya kazi ya Mshauri wa Mauzo (sales Advisor) pamoja na kutoa ushauri (consultancy).

“Mimi ninafanya kazi PWD/CDS/COSTCO kama Sales Advisor, baada ya kumaliza masomo yangu hasa Interpersonal Communication. Costco ninakofanya kazi ina members (wanachama) 10,000. Kwa siku wanaofika Warehouse ni kati ya 5,000 hadi 7,000,” alisema Dk. Slaa.

Kufuatia uteuzi huo wa Dkt. Slaa kuwa Balozi uliofanywa na Rais Magufuli, taaarifa kutoka ikulu imeeleza kuwa zoezi la kuapishwa kwake litafuata baada ya kukamilishwa kwa taratibu.

Zitto Atoa Neno Kwa Wanaohama Vyama Kila Kukicha

$
0
0
Kufuatia vuguvugu la hivi karibuni  la wanasiasa kuhama vyama vyao na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) huku wengine wakitoka CCM na kuhamia upinzani, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameamua kutoa ya moyoni kuhusiana na sarakasi hizo za kisiasa.

Katika chama chake cha ACT-Wazalendo, Zitto amepoteza wanasiasa kama Samson Mwigamba, Dkt. Kitila Mkumbo na wanachama wengine 10 ambao wametimkia CCM huku aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Mama Anna Elisha Mghwira akijiuzulu nafasi hiyo na kusalia kuwa mwanachama wa kawaida baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto ameandika yafuatayo;

“Kuhama au kubadili Chama cha Siasa sio jambo geni katika siasa zetu, na ni haki ya kikatiba ya Mtanzania yoyote kufanya ivyo. Kitu cha msingi ni kitendo hicho kuongozwa na imani thabiti kwenye misingi ya chama unachokwenda.

Siku zote ninaamini kuwa vyama vinapaswa kujengwa juu ya misingi ya Itikadi. Sisi ACT Wazalendo itikadi yetu imejengwa kwenye Azimio la Tabora kuhusu Siasa ya Ujamaa wa Kidemokrasia. Tutaendelea kufanya siasa za masuala na kuimarisha mfumo wa Vyama vingi nchini kwetu.

Mimi Binafsi na Wanachama wenzangu wa ACT wazalendo tunawatakia heri na mafanikio wenzetu waliojiunga na vyama vingine. Sisi wengine tutaendelea kujenga Vyama kama Taasisi muhimu za Maendeleo katika Nchi yetu. Kamwe hatuwezi kuruhusu nchi yetu kuwa ya chama kimoja. Kwa mazingira ya kisiasa ya sasa, kuwa mwanachama wa Chama cha Upinzani ni uzalendo uliotukuka.

Ni dhahiri kuwa Chama kuondokewa na wanachama wake sio jambo jema. Lakini ukitazama watu wanaohama vyama ni wanasiasa wale wale wa siku zote na walikuwa kwenye vyama vingine kabla na kuhamia vyama wanavyotoka sasa. Kwangu mimi kuna somo moja kubwa nalo ni kuandaa aina Mpya ya wanasiasa, wanasiasa wanaojengwa kwenye itikadi na misingi. Kazi kubwa iliyopo mbele yangu kama Kiongozi ni kuandaa kizazi kipya cha Viongozi wa kisiasa wajamaa. Hiyo ndio kazi ninayofanya sasa. Forward Ever, Backward Never.”

Zitto Kabwe, Mb
Mtwara
23/11/2017.

Serikali yakanusha tarifa ya uteuzi wa wakuu wa wilaya inayosambazwa mitandaoni.

$
0
0
Serikali imekanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, kuhusu uteuzi wa wakuu wapya 10 wa wilaya na kueleza kuwa siyo ya kweli na ipuuzwe mara moja.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa hafla ya kuwaaapisha walioteuliwa pamoja na kuwapangia wilaya zao za kazi itafanyika Ikulu siku ya Jumatatu, Novemba 27, 2017.

Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, kupitia ukurasa wake wa Twitter ameeleza kuwa taarifa hiyo haijatolewa na ikulu ila imetengenezwa na wahalifu wenye nia mbaya na serikali.

Hapa chini ni taarifa iliyokanushwa.

Waziri Mkuu Ampa Ofisa Ardhi Mwezi Mmoja Kufidia Wananchi

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa mwezi mmoja Ofisa Ardhi wa wilaya ya Namtumbo Bw. Maurus Yera awe ametafuta ardhi ya kuwafidia wakazi wa kijiji cha Lwinga wilayani Namtumbo.

Wakazi hao 21 mwaka 2008 eneo lao lenye ukubwa wa ekari 101 lilitwaliwa na Serikali kupitia halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya kupisha ujenzi wa shule ya sekondari ya mkoa wa Ruvuma na waliahidiwa kulipwa fidia.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Novemba 23, 2017) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Lwinga akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma.

Alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao kupitia mabango, ambapo walimuomba awatatulie kero hiyo ya madai ya fidia ya ardhi iliyodumu kwa miaka 10 bila kupatiwa ufumbuzi.

Waziri Mkuu alisema haoni sababu ya Halmashauri hiyo kushindwa kuwafidia wananchi hao sehemu ya ardhi kwa muda wote huo ukizingatia wilaya hiyo ina hifadhi ya ardhi.

“Nataka wananchi hawa wawe wamelipwa fidia yao ya ardhi kabla ya siku kuu ya Krismasi ya mwaka huu. Serikali haiko tayari kuona wananchi wake waliotoa ardhi kupisha maendeleo wakisumbuliwa.”

Waziri Mkuu alisema Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inataka kila mtumishi ahakikishe anatumia taaluma yake vizuri kwa kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua kero zinazowakabili kwa wakati.

Pia Waziri Mkuu alitoa wito kwa wananchi hao kuhakikisha hawakubali kutoa rushwa pale wanapohitaji kupata huduma mbalimbali kutoka kwa watumishi kwa kuwa ni haki yao kuhudumiwa.

Aliwataka wananchi kuwa na imani na Serikali yao na kuiunga mkono katika mapambano dhidi ya rushwa kwani vitendo hivyo vinakwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watendaji kuhakikisha miradi wanayosimamia inakuwa na thamani inayolingana na kiasi cha fedha kilichotolewa na iwapo watabainika kwenda kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

“Lazima kiasi cha fedha kinachotolewa kugharamia mradhi kilingane na thamani ya mradi husika. Mfano tumetoa sh. milioni 70 kugharamia mradi na kukuta mradi uliojendwa ni wa sh. milioni 30 aliyeshughulikia ujenzi huo nasi tutamshughulikia hatutamuacha salama.”

Awali, Waziri Mkuu alifungua ghala la kuhifadhiia mpunga na mchele katika wilaya ya Namtumbo lililojengwa na MIVARF na kisha alizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo na kuwataka wafanye kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bibi Christine Mndeme alisema mkoa huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa masoko kwa mazao ya mahindi na mbaazi, ambapo Waziri Waziri Mkuu alisema sula hilo linashughulikiwa hivyo wananchi waendelee kuwa na subira.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
iJUMAA, NOVEMBA 24, 2017.

Mbunge Gama kuzikwa Jumatatu

$
0
0
Aliyekua mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama anatarajiwa kuzikwa Jumatatu katika makaburi ya familia yaliyopo Kijiji cha Likuyufusi mkoani Ruvuma.

Gama aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Novemba 24,2017 atazikwa Jumatatu Novemba 27,2017 katika makaburi hayo yaliyopo umbali wa kilomita 25 kutoka Songea mjini.

Issa Fussi ambaye ni msemaji wa familia na mdogo wa Gama amesema amefariki usiku wa kuamkia leo akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho.

Amesema Gama alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na alipelekwa hospitalini hapo Jumatano Novemba 22,2017 usiku na kulazwa hospitalini hapo .

Fussi amesema msiba huo ni pigo kwa familia kwa kuwa Gama alikuwa nguzo akitegemewa katika masuala mbalimbali ya maendeleo na kifamilia.

Amesema mwili wa marehemu Gama umehifadhiwa katika Hospitali ya Peramiho na utaratibu wa mazishi unaendelea.

Onyo la serikali kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini

$
0
0
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inawataarifu wananchi kuhusu orodha ya viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kama ilivyo sasa. Lengo ni kuwawezesha wananchi kuwafahamu viongozi wa vyama vya siasa, kwani imedhihirika kuwa wananchi wengi hawawajui viongozi wengi wa vyama vya siasa na nafasi zao.

Napenda watanzania wafahamu kuwa, orodha ya viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa hubadilika pale ambapo muda wa uongozi wa viongozi wa kitaifa umeisha na viongozi wengine kuchaguliwa/kuteuliwa, kiongozi kujiuzuru, kufariki au kuondolewa katika uongozi au uanachama.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ndiyo yenye dhamana ya kuhifadhi taarifa za viongozi wa kitaifa wa kila chama siasa. Hivyo, imekuwa na utaratibu wa kuujulisha umma mara kwa mara na kwa njia mbali mbali, kuhusu orodha ya viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa mara panapotokea mabadiliko ya uongozi.

Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 8A na 8B cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 [RE: 2015] kama ilivyorekebishwa mwaka 2009, ni kosa la jinai kwa mtu yeyote ambaye hatambuliki na Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa ni kiongozi wa kitaifa wa chama cha siasa, kufanya shughuli za chama au siasa kwa niaba ya chama chochote cha siasa.

Msajili wa Vyama vya Saisa anawaasa wanachama wa vyama vya siasa kuheshimu Sheria za nchi, hasa Sheria ya Vyama vya Siasa.

Sisty L.  yahoza
Kny: MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
23 Novemba, 2017

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kifo cha Mbunge wa Songea Mjini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mhe. Leonidas Tutubert Gama.

Mhe. Leonidas Tutubert Gama amefariki dunia jana tarehe 23 Novemba, 2017 saa 4:25 usiku katika hospitali ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho, iliyopo Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma ambako alikimbizwa kwa matibabu baada ya kuugua ghafla.

“Nimepokea kwa mshtuko na majonzi taarifa za kifo cha ghafla cha Mhe. Leonidas Tutubert Gama, nakupa pole Mhe. Spika Job Ndugai, Wabunge na wafanyakazi wa ofisi yako, na kupitia kwako naomba ufikishe salamu zangu za pole kwa familia ya Marehemu, wananchi wa Jimbo la Songea Mjini na Mkoa mzima wa Ruvuma, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amempa pole Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Ndg. Oddo Mwisho na wana CCM wote kwa kumpoteza kada wao aliyeiwakilisha vizuri CCM kwa nafasi yake ya ubunge.

Mhe. Rais Magufuli amesema Mhe. Leonidas Tutubert Gama ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa na Mbunge, alikuwa kiongozi hodari, aliyefanya kazi kwa kujiamini na aliyependa kupigania maslahi ya wananchi bila kuchoka.

Amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi na pia ameiombea familia yake iwe na subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
24 Novemba, 2017

Taarifa ya Bunge kuhusu kifo cha Mbunge Leonidas Gama

CCM Yamlilia Mbunge Leonidas Gama

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi, kimetoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekwa Mbunge wa Songea Mjini kwa tiketi ya chama hicho Ndg Leonidas Gama kilichotokea usiku wa kuamkia leo.

Uongozi wa CCM chini ya Mwenyekiti wa Chama hicho Ndg, John Pombe Magufuli umetoa salamu hizo kupitia kwa Katibu Mwenezi, Ndg Humphrey Polepole imesea kwamba chama kimepokea taarifa za kifo hicho kwa mshtuko mkubwa na huzuni.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kwamba kipindi chote cha uongozi wake alikuwa sehemu ya viongozi wa kisiasa ambao waliamini katika uelewa wa pamoja na matarajio, siasa safi na za kimaendeleo, uongozi bora na umuhimu wa kuweka maslahi ya nchi na taifa mbele.

 Mhe. Leonidas Gama amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Peramiho, Ruvuma.

Mwanariadha Pistorius aongezewa kifungo hadi miaka 13 kwa kumuua mpenzi wake

$
0
0
Mahakama ya rufaa nchini Afrika Kusini imemuongezea adhabu ya kifungo mwanariadha mwenye ulemavu Oscar Pistorius kutoka miaka 6 hadi miaka 13 na miezi mitano kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Hatua hii inafuatia madai kutoka upande wa serikali kwamba adhabu aliyopewa awali ya miaka sita ilikuwa ndogo. 
 
Pistorius alishtakiwa kumuua mpenzi wake kwa kumpiga risasi 4, katika siku ya wapendanao mwaka 2013, na baadaye Pistorious alisema alifyatua risasi hizo kwa kujua ni mwizi.

Familia ya Reeva Steenkamp imeeleza kuwa wamefurahishwa na uamuzi wa mahakama na inaonesha kuwa haki inaweza kuendelea kutendeka nchini humo Afrika Kusini.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Novemba 25

Profesa Kabudi atoa kauli hatua ya majadiliano na Barrick

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamaganda Kabudi amesema majadiliano yanayofanywa na Serikali pamoja na Kampuni ya Dhahabu ya Barrick kuhusu mchanga wa dhahabu (makinikia) yamefikia mahali pazuri na kwamba Taifa litajulishwa hivi karibuni.

Kwa upande wa Tanzania timu ya majadiliano iliyoundwa na Rais John Magufuli ilikuwa iliongozwa na Profesa Kabudi wakati timu ya Barrick iliongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Richard William.

Kamati hiyo ambayo ilianza majadiliano hayo rasmi Julai 31 mwaka huu ilenga kujadiliana madai ya Tanzania kwenye biashara ya madini.

Akizungumza na wakuu wa taasisi, idara na vitengo vya sheria Serikalini mjini hapa, Kabudi alisema Taifa litataarifiwa kuhusu maendeleo ya majadiliano hayo hivi karibuni.

“Juzi na jana tumefikia katika hatua nzuri ambayo nisiseme lakini Taifa litataarifiwa hivi punde juu ya maendeleo ya utekelezaji wa tuliyokubaliana,”alisema.

“Baada ya hapo nilidhani nitapumzika nifanye kazi nyingine lakini mheshimiwa Rais amenipa jukumu jingine la kusimamia madini ya Tanzanite na Almasi.”

Alisema shughuli hizo ndizo zimemfanya iwe vigumu kuwatembelea na kuongea nao tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo mwanzoni mwa mwaka huu.

Alisema miongoni mwa sababu ambayo iliwafanya wasiweke hadharani wajumbe wa tume hiyo wanaoenda kukutana na kampuni ya Barrick kuepuka watu kuwachambua kwa faida ya upande wa pili.

Alionya tabia ya wataalam wa sheria kutoa maoni ya kisheria haraka sio nzuri katika kushughulikia maslahi ya Taifa.

“Tutashindwa, tutalipa fedha nyingi wakati wake si huu. Tutalipa mabilioni ya fedha tukienda mahakamani. Kwa hiyo alipwe sio wakati wake. Na kwa unyenyekevu mkubwa tulipoanza majadiliano haya tuliambiwa kuwa Barrick watawashtaki,”alisema.

“Mtalipa fedha nyingi, wametushtaki? Nawaulinza nyinyi ndugu zangu wametushtaki Barrick? Tumelipa hela nyingi? Lakini sio ndio ilikuwa mazungumzo hayo? Kwamba hapo simesaini (Makubaliano). Subirini mtashtakiwa, mtalipa fedha nyingi.”

Alisema wengine walisema kuwa Barrick hawatafika katika mazungumzo hayo na kuhoji kama walikuja ama la.

“Mazungumzo yamevunjika. Sasa mlitaka tuyafanye hadharani? Moja ya sababu ya wale kufichwa isipokuwa mimi nifahamike wala ilikuwa hatuwaogopi sana wale. Nyinyi Watanzania maana mngeanza kuchambua huyu darasa la nne alifeli,”alisema.

“Kwa hiyo mngeanza kuchambua watu kwa faida ya yule (Barrick) badala ya kupeana. Hatukukutana na watu wadogo. Jana tulikuwa na Richard Willison (Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick… komandoo yule (Willison) lakini pamoja na ukomandoo wake si tulipambana naye bwana?”

Alisema ni lazima kusimamia maslahi ya Serikali bila woga wowote na kwamba inakera kusikia mwanasheria akisema kesi ni ngumu nakwamba Serikali ilipe fedha haraka sana.

“Tutashtakiwa sasa wewe umeajiriwa kwasababu gani? Si uende upambane. Nasema hili mjue nyakati zimebadilika. Mjiulize zimepitishwa sheria mnazifahamu zilizopitishwa si za wizara yako?”alihoji.

Pia alisema kuwa kwa muda wote wa majadiliano ya makinikia wajumbe wa timu hiyo hawakukaa majumbani kwao kutokana na uhalisiana wa suala hilo.

Profesa Kabudi alisema majadiliano kuhusu mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya upakuaji makontena bandarini ya Tanzania (TICTS) yamewezesha kampuni hiyo kuongeza mapato.

“Tulifanikiwa kukaa na wale wa Hong Kong na kufanikiwa kuubadilisha mkataba ule mara ya kwanza ulikuwa ni mkataba ambao kwa mwaka kodi ya pango ni dola milioni 7 lakini sasa ni dola milioni 14 zinazoongezeka kwa asilimia tatu kila mwaka,”alisema.

Alisema fedha hizo zitalippwa mwanzo wa mwaka zote na kwamba mwaka huu wamelipa dola za kimarekani milioni 17.3

Alisema anza kutoa Dola za Marekani milioni 14 kila mwaka badala ya dola za marekani milioni 7 kila mwaka kama kodi ya pango.

Alisema awali mkataba ulikuwa hautoi nafasi ya kuongeza kodi sasa unatoa ongezeko la asilimia la asilimia tatu.

“Tumekubaliana wawe wanalipa kwa mkupuo mwanzo wa mwaka wa fedha na Julai mwaka huu badala ya kulipa oktoba wamelipa Dola za marekani milioni 17.3,”alisema Kabudi. 
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images