Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kafulila atua rasmi CCM na Kukabidhiwa Kadi

$
0
0

Baada ya kutangaza kujivua uanachama wa CHADEMA siku ya Jumatano, David Kafulila  jana  amekabidhiwa kadi ya CCM.

Kafulila alikabidhiwa kadi ya CCM na Katibu Mwenezi wa CCM, ndg Humphrey Polepole katika mkutano wa kumnadi mgombea wa udiwani wa chama hicho, Kata ya Mbweni jijini Dar es salaam

Hapo awali Kafulila aliwahi kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendelo kisha kufuzwa baadae akajiunga na Chama cha NCCR Mageuzi ambapo alifanikiwa kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini mwaka 2010-2015 na baadaye kurudi tena Chadema 2016 na hapo juzi jumatano alitangaza kukihama chama hicho kwa madai upinzani hauna nia ya kupambana na ufisadi.

Kwa upande wa mkewe ambaye ni Mbunge Viti Maalumu kupitia chama cha CHADEMA,Jesca Kishoa juzi wakati akizungumza na wanahabari alipingana na kauli ya mumewe na kusema kwamba, mumewe anapaswa kusema ukweli na kwamba sababu alizozisema sizo zilizomuondoa ndani ya chama hicho huku akiongeza kwamba mume wake hana msimamo.

Kafulila amekabidhiwa kadi hiyo ya CCM ikiwa imebaki siku moja kabla ya kuhitimishwa kwa kampeni za uchaguzi wa marudio ya nafasi za udiwani kwa Kata 43 ndani ya Tanzania


Kinana asema hakuna waziri wa kukataa analomtuma

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema hakuna waziri mwenye ubavu wa kukataa akimtuma jambo.

Amesema hayo jana Ijumaa Novemba 24,2017 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Moita Bwawani akimnadi mgombea wa CCM wa Kata ya Moita wilaya ya Monduli, Prosper Damuni.

"CCM ndiyo chama kilichoshika dola kama kuna changamoto sehemu yoyote namwambia waziri anayehusika anafika haraka eneo hilo kusikiliza na kutatua changamoto hiyo, hakuna waziri mwenye ubavu wa kukataa nikimtuma," alisema Kinana.

Katibu mkuu huyo amewaomba wananchi katika kata 43 zinazofanya uchaguzi mdogo wa udiwani kuwachagua wagombea wa CCM akisema ndicho chama kinachoongoza dola na ahadi zinazotolewa zinatekelezeka.

Kinana amewaomba wananchi hao akisema ni wakati muafaka kwao kuacha kupiga kura kwa ushabiki.

Alisema wilaya hiyo inakusanya mapato ya ndani ya Sh2 bilioni kwa mwaka wakati bajeti yao kwa mwaka ni Sh49 bilioni kwa mwaka fedha ambazo zinatolewa na Serikali Kuu hivyo ni muhimu kuwa na diwani anayetoka chama hicho ili kurahisisha maendeleo ya wananchi.

Kinana alisema anafahamu wilaya hiyo ina changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji kutatuliwa.

"Nataka nimpe mbinu mgombea wenu akichaguliwa anatakiwa kuwa karibu sana na mkurugenzi mtendaji wa wilaya na kwa kuwa anatokana na CCM atakuwa na uwezo wa kuingia na kutoka kwenye ofisi za Serikali kutafuta fedha za maji, barabara, afya na elimu hiyo ndiyo kazi ya diwani si kukaa tu kusubiri maendeleo yaje," alisema Kinana

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wakuu wa mikoa, Mrisho Gambo wa Arusha na Christopher ole Sendeka wa Njombe waliwataka wananchi kutoyumbishwa na kelele za vyama vingine bali wamchague mgombea wa CCM.

Mgombea udiwani, Damuni aliwaomba wananchi kumchagua ili alete maendeleo kwa kuzingatia chama chake ndicho kinachotekeleza ilani ya uchaguzi iliyoshinda mwaka 2015 na kuunda Serikali.

Maagizo ya Rais Magufuli kwa Polisi baada ya ajali Singida kuua watu 12

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kufuatia vifo vya watu 12 vilivyosababishwa na ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso.

Ajali hiyo imetokea  tarehe 23 Novemba, 2017 majira ya saa 2:30 usiku katika eneo la Ighuka Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida ambapo basi dogo aina ya Toyota Hiace lililokuwa limebeba watu waliotoka kwenye sherehe ya harusi limegongana na gari dogo aina ya Noah lililokuwa linatoka msibani.

Katika salamu hizo Mhe. Rais Magufuli amemtaka Dkt. Rehema Nchimbi kufikisha salamu zake za pole kwa familia zilizopoteza jamaa zao, ndugu na marafiki.

“Ajali hii imeleta majonzi makubwa sio tu kwa familia zilizopoteza jamaa zao bali kwetu sote, tumepoteza ndugu zetu wengi ambao wameacha familia zao, wapendwa wao na jamaa waliowategemea, kwa hakika hili ni pigo kubwa”

“Naungana na familia za Marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na pia nawaombea Marehemu wapumzike mahali pema, wote walioguswa na vifo hivi wawe na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amevitaka vyombo vinavyosimamia matumizi ya barabara na usalama barabarani, kuongeza juhudi katika udhibiti wa ajali na kuwachukulia hatua kali wote wanaovunja sheria na kusababisha ajali.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
24 Novemba, 2017

Kijana wa miaka 22 apandishwa kizimbani kwa Kosa la Kuua Kwa Kukusudia

$
0
0
Mkazi wa Ipililo wilaya ya Maswa Mkoani Shinyanga, Salum Nkoja (22) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Kisutu akikabiliwa na kosa la mauaji ya kukusudia ya mtu asiyefahamika.

Hata hivyo, kwa taarifa zilizoko inadaiwa mshtakiwa huyo alikamatwa na viungo vya binadamu zikiwemo sehemu za siri wanawake. Mshtakiwa alisomewa kosa lake na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambapo amedai mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja.

Katuga alidai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la mauaji kwa kukusudia ambalo amelitenda kati ya October 1 na 30, 2017 katika sehemu isiyofahamika kati ya Ubungo Dar es Salaam na Kahama.

Wakili Katuga alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Baada ya kusomewa kosa hilo, Hakimu Mkeha alimtaka mshtakiwa asijibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi December 8, 2017.

Katika taarifa zilizopatikana inadaiwa mshtakiwa huyo alikutwa na sehemu za siri za binadamu zilizokaushwa ambazo ni za wanawake.

Rais Magufuli kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Uhuru Kenyatta

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ataungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi cha awamu ya pili.

Sherehe hizo zitafanyika Jumanne Novemba 28, 2017 jijini Nairobi, Kenya.

Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu usalama wa nchi

Video:Rais Magufuli Mgeni Rasmi Maadhimisho Miaka 56 Ya Uhuru

$
0
0
Rais Magufuli Mgeni Rasmi Maadhimisho Miaka 56 Ya Uhuru


==>Tazama video hapo chini

Profesa Lipumba asema hakutarajia Dk Slaa kuwa balozi

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amezungumzia uteuzi wa Dk Wilbroad Slaa kuwa balozi akisema hakutarajia.

Rais John Magufuli juzi alimteua Dk Slaa aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Chadema kabla ya kukihama chama hicho wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Wakati wa mchakato wa uchaguzi huo, Profesa Lipumba na Dk Slaa ambao vyama vyao vilikuwa katika umoja uliojulikana Ukawa, walijiondoa baada ya Chadema kumpitisha Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa urais.

Profesa Lipumba jana alisema, “Imekuwa kama surprise, sikutegemea kama Dk Slaa atateuliwa kwa sababu muda mwingi yupo Canada.”

Hata hivyo, Profesa Lipumba alisema hana shaka na uteuzi huo kwa kuwa Dk Slaa ni mzoefu wa siasa na mzalendo ambaye ataitumikia vyema nafasi hiyo mpya.

“Narudia, sikutegemea. Ila popote atakapopangiwa kazi Dk Slaa atafanya kwa sababu najua ni mchapakazi,” alisema.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema Rais Magufuli ana mamlaka kisheria ya kumteua mtu atakayemuona anafaa katika nafasi fulani.

“Huu ni uamuzi wa Rais sisi wengine hatuna comments zaidi ya kuwatakia kila heri katika utendaji wao wa kazi,” alisema Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza uteuzi huo wa Dk Slaa, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari alisema Rais Magufuli amemuonea huruma Dk Slaa ndiyo maana akaamua kumpa nafasi ya ubalozi.

Profesa Safari alisema hawezi kumsema vibaya Dk Slaa lakini nafasi hiyo ni huruma na zawadi ya Rais Magufuli.

Amedai Dk Slaa alijaribu kuivuruga Chadema wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015 lakini hakufanikiwa.

“ Hii ni huruma. Siku zilizopita Dk Slaa aliandikwa katika vyombo vya habari kuwa anafanya kazi Super Market. Mimi nimekaa Ulaya najua maisha ya kule na Dk Slaa ni rafiki yangu sana lakini kwa kitendo alichokifanya mwaka juzi, haya ndiyo matokeo yake,” alisema Profesa Safari.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Azam TV, Dk Slaa alimshukuru Rais Magufuli kwa kumteua ili aungane naye kujenga nchi na hivyo atafanya kazi kwa uwezo wake wote.

Dk Slaa ambaye hivi sasa anaishi Canada alisema, “Ni mapenzi ya Mungu, nashukuru kwa uteuzi. Ninachoweza kusema katika hatua hii, huu ni wajibu mkubwa kwenye kipindi cha kulijenga Taifa letu.”

Credit: Mwananchi 

Dk Shika kushiriki kumnadi mgombea wa CCM

$
0
0
Katika kampeni za lala salama leo, CCM itawapandisha jukwaani aliyekuwa mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi na Dk Louis Shika, aliyejizolea umaarufu baada ya kuibuka kwenye mnada wa nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi.

Katambi aliyejiunga na CCM akitokea Chadema na Dk Shika watamnadi kwa wapiga kura wa Kata ya Mhandu jijini Mwanza mgombea wake, Constantine Sima.

Katibu wa uenezi wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Mustapha Banigwa amesema leo Jumamosi Novemba 25,2017 kuwa wengine watakaopanda jukwaani katika mkutano utakaofanyika mtaa wa Machinjioni ni waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi na mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha aliyerejea CCM akitokea Chadema.

Mkutano huo pia utahutubiwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na aliyekuwa mbunge wa Bunda, Stephen Wasira, mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe na mbunge wa Bukombe, Doto Biteko.

Uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 nchini utafanyika kesho Jumapili Novemba 26,2017.

Rais Magufuli azungumzia Pinda alivyomzuia kubomoa jengo la Tanesco

$
0
0
Rais John Magufuli amesema hakubomoa jengo la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililopo Ubungo alipokuwa waziri wa ujenzi kwa kuwa aliogopa kufukuzwa kazi.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumamosi Novemba 25,2017 alipozindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), kampasi ya Mloganzila.

Akizungumza mbele ya waziri mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mizengo Pinda aliyehudhuria uzinduzi huo, Magufuli amesema wakati huo aliogopa baada ya kuzuiwa na waziri mkuu huyo, lakini sasa yeye ndiye Rais hakuna wa kumzuia.

Akizungumzia ubomoaji unaoendelea sasa amesema, “Nilishatoa maagizo, najua Mizengo Pinda kwenye hili alinipinga wakati ule, lakini najua leo hawezi akanipinga kwa sababu mimi ndiye Rais. Wakati ule nilikuwa waziri wake, ndiyo maana nilinyamaza nilijua ninaweza nikafukuzwa, hutakiwi kumpinga mkubwa.”

 “Hilo jengo la Tanesco, narudia kama itakuwa ni kubomoa nusu, no problem (hakuna tatizo); kama ni lote hakuna tatizo, pamoja na jengo la wizara ya maji. Najua katibu mkuu wa wizara ya maji yupo hapa ananiangalia, wakaanze kulitoa eneo lililopo kwenye hifadhi ya barabara,” amesema.

Machi 6, 2011 akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Chato, mkoani Kagera, Pinda ambaye alisifia utendaji wa Dk Magufuli alimwagiza kusimamisha ubomoaji maeneo kadhaa yaliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara likiwemo jengo la Tanesco hadi Serikali itakapotoa kauli nyingine kuhusu hilo.

Pinda alikuwa akizungumzia hatua ya Dk Magufuli aliyekuwa amewaagiza wananchi waliojenga nyumba ndani ya hifadhi ya barabara kuanza kubomoa nyumba hizo na wasitarajie kulipwa fidia.

Pinda wakati huo akiwa waziri mkuu alisema spidi (kasi) ya Magufuli ilikuwa kubwa hivyo alimuagiza kusimamisha ubomoaji huo hadi suala hilo litakapojadiliwa na Baraza la Mawaziri.

Pinda, ambaye alikuwa waziri mkuu kuanzia 2008 baada ya kujiuzulu kwa Edward Lowassa alisimamisha ubomoaji huo ili kutoa nafasi kwa Serikali kujipanga upya.

Alisema Serikali inamuamini Magufuli kuwa kiongozi mwenye uwezo na ndio maana ilimpa nafasi akawabane makandarasi wazembe.

Dk Magufuli akiwasilisha bajeti bungeni mwaka 2012/13, alizungumzia ubomoaji akisema siasa iachwe akisisitiza sheria zimepitishwa ikiwamo Sheria namba 13 ya mwaka 2007 na ya hifadhi ya barabara iliyoanza tangu mwaka 1932.

Alizungumzia jengo la Tanesco alisema liko kwenye hifadhi ya barabara na kwamba hata kama asipolibomoa yeye kuna siku litabomolewa vinginevyo sheria ibadilishwe.

Novemba 15 akitokea Chato alipokwenda kwa mapumziko baada ya ziara ya Uganda, Magufuli alimuagiza wakala wa barabara nchini (Tanroads) kuweka alama ya X katika jengo la Tanesco na Wizara ya Maji, sehemu zilizo katika hifadhi ya barabara.

Chadema wataka wapiga kura wakae mita 100

$
0
0
Chadema wamewataka   wapiga kura kukaa umbali wa mita 100  wakati wa kusubiri matokeo yao kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyia kesho katika kata 42 nchini, ili kulinda kura zao.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Jeshi la Polisi lilipinga wapiga kura kukaa umbali wa mita 100 na baadaye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuhitimisha sakata hilo kwa kutamka kuwa kukaa umbali wa mita 200, baada ya kupiga kura hairuhusiwi.

Akielezea mwenendo wa uchaguzi huo, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema,  Benson Kigaila amesema  sheria inaruhusu wapiga kura kukaa umbali huo ili kulinda kura zao.

“Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 inataka wapiga kura kusimama umbali wa mita 100, kwa hiyo tuwaambie wapiga kura wetu wakishamaliza kupiga kura wakae umbali wa mita hizo, waongeze na nyingine moja walinde kura zao,” amesema

Kigaila amewataka  wapiga kura hao kwenda kwenye vituo vya kupigia kura na kutimiza wajibu wao bila kuogopa kitisho chochote na baadaye walinde kura zao hadi zitakapotangazwa.

“Waende wakapige kura wasiogope kitisho chochote,” amesema na kuwataka baadaye waende kwenye makao makuu ya kata yatakako tangazwa matokeo hayo kuhakikisha, washindi wanatangazwa kwa haki.

Kiongozi huyo wa Chadema amesema kumekuwa matukio ya uvunjaji wa haki kwenye mikutano yao ya kampeni ikiwamo makada wake kuvamiwa na kupigwa.

“Upinzani ukishinda utatangazwa wapende wasipende, ambaye atatangaza matokeo tofauti ashughulikiwe kama mwizi mwingine wa kawaida kwa sababu wezi huwa wanashughulikiwa,”

“Kwa hiyo watu waende walinde haki yao ya kikatiba, wapige kura na walinde matokeo. Yatangazwe matokeo sahihi.” amesema  kiongozi huyo wa  Chadema

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Novemba 26

Rais Magufuli Akataa Kupewa Sifa Ujenzi Hospitali ya Mloganzila

$
0
0
Rais wa Serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa sifa na pongezi kwa rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha ujenzi wa hospitali ya Mloganzila.

Rais ametoa pongezi hizo jana wakati akihotubia wananchi waliohudhuria ufunguzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila jijini Dar es salaam.

“Wakati ujenzi wa Hospitali hii unaanza mimi nilikuwa naagizwa tu na niliambiwa nikatafute eneo kubwa nikawaza nitalitoa wapi lakini baadae mzee Jakaya akanipigia tena simu  akaniambia kuna eneo huko Mloganzila ni la serikali nenda kaangalie na ujenzi uanze haraka, ndio nikaja hapa”, alisema Rais Magufuli.

Rais magufuli aliongeza kuwa “Watu tunapenda sifa lakini hizi sifa sio zangu ni za rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwani mimi nilikuwa naagizwa tu nikiwa waziri wa Ujenzi, ndio maana nimeona niseme wazi kuwa sifa zote zimwendee mzee Kikwete”.

Aidha rais Magufuli aliweka wazi kuwa wakati anakwenda kuona eneo la Mloganzila wala hakukuwa na barabara lakini aliambiwa na rais Kikwete aanze ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara haraka iwezekanvyo na alifanya hivyo sambamba na waziri wa maji amnbaye naye aliagizwa kuanza ujenzi wa miundombinu ya maji.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila jijini Dar es salaam ni mpango na jitihada za rais wa awamu ya nne.

Rais Magufuli Aishukuru China kwa Meli ya Matibabu Bure

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameishukuru serikali ya watu wa China kwa msaada wao walioutoa kwa wananchi wa Tanzania wa kuwapatia matibabu bure, akisema jambo hilo ni upedo usio elezeka.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipoenda kutembelea meli yenye madaktari bingwa kutoka China ambayo imetia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam, na kutoa huduma za vipimo na matibabu kwa wakazi wa Dar es salaam bila gharama yoyote.

"Tunapenda kusema shukrani kwa dhati kwa serikali ya China kuamua kuituma meli na madaktari kuja Tanzania, tunafurahi kwa huduma zao, wameokoa maisha ya watanzania zaidi ya elfu 6,400, huu ni upendo wa pekee unaogusa, ndio maana leo nimeshindwa kuvumilia nimeona bora nije nishukuru, nimeguswa mno na ndugu zetu wachina, yapo mataifa mengine matajiri, yenye mali nyingi lakini hayajaguswa", amesema Rais Magufuli.

Sambamba na hayo Rais Magufuli amewakabidhi madaktari hao barua maalum kwenda kwa raisi wa nchi yao Xi Jinping pamoja na kinyago kama zawadi kwake, kumshukuru kwa mchango wake na ukarimu wake kwa watanzania masikini.

Pia Rasi Magufuli amewatakia safari njema madaktari hao na kuwaomba kurudi tena wakati mwengine, na kuwataka kukaa kwa muda mrefu zaidi ili waweze kutoa huduma kwa watanzania wengi hata watakaotoka mikoan

Rais Magufuli Avamia Bandarini Leo na Kuiua Uozo Mpya

$
0
0
Rais John Magufuli ametoa siku saba kwa Mamlaka ya Mapato( TRA), Mamlaka ya Bandari(TPA), Takukuru na Wizara ya Fedha kuhakikisha inatoa taarifa ni nani alihusika kuagiza magari 50 kupitia mgongo wa Ofisi ya Rais.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo Jumapili Novemba 26 baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini mara baada ya kutembelea meli ya Wachina iliyofanya matibabu kwa Watanzania kwa muda wa siku 5.
 
Magari hayo aina ya ambulance ambayo mpaka leo yapo bandarini, yaliagizwa mwaka 2015 kupitia majina ambayo hayatambuliki na Ofisi ya Rais.

Kabla ya kutoa maagizo hayo, Rais amewahoji IGP, Waziri wa Fedha, Kamishna Mkuu wa TRA na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ambao hata hivyo hawakuwa na mujibu kuhusu nani hasa mwagizaji wa magari hayo.

“Natoa onyo kwa mawaziri na wateule wale wote waliotangaza, sitaki mpaka nije kubaini uozo mimi mwenyewe ninataka mpigane kuhakikisha uozo wote unaondoka, safari nyingine nikigundua jambo lolote na wewe ni eneo lako hautapona,” amesema.

Ameongeza, “Ninatoa siku saba, nataka aliyeagiza haya magari kwa mgongo wa Ofisi ya Rais atambulike ni nani na ninatoa maagizo hata kama ni mtu mkubwa kiasi gani atambulike nahitaji mujibu.”

Wakati huohuo Rais Magufuli ametembea umbali wa zaidi ya mita 700 ili kukagua magari ya polisi ambayo yaliingizwa nchini mwaka 2015 lakini bado zaidi ya magari 50 yameendelea kubaki eneo la bandari.

"Kule Polisi kuna mambo ya hovyo. Polisi Mnadai hizi gari ni zenu, kwanini hamzifuatilii tangu 2015? Kuna magari yamekaa miaka 10 lakini sheria inasema gari likikaa zaidi ya siku 21 yapigwe Mnada, kwanini hampigi mnada? IGP kwenye Majambazi upo safi lakini huku kwenye Ufisadi bado sana. Kama mtu anakunanihii mtwange. Nilikuchagua ulikua such good guy lakini unaniangusha. Polisi kuna Uchafu mwingi sana".

Mbowe aagiza wagombea wa Chadema kujitoa kata tano Arumeru Mashariki

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameagiza wagombea wote wa udiwani wajitoe kwenye uchaguzi wa kata tano Arumeru Mashariki, mawakala na viongozi wote watoke vituoni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili alisema tayari amewasiliana pia na Tume ya Uchaguzi kwa kuwa Arumeru sio uchaguzi ni vurugu watu wanatekwa kama Mbunge wa Babati Mjini, Paulina Gekul hadi sasa ametekwa na hajulikani alipo

Kutokana na hali hiyo Mbowe ametaka Tume ya Uchaguzi kuitisha uchaguzi mpya.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya leo Jumatatu ya Novemba 27

CCM Yaikamata Kaskazini...... Yashinda Kata Nne Jimboni za Arumeru Mashariki

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeshinda kata nne za Arumeru Mashariki ambazo wagombea wa Chadema wamejitoa. Kata hizo na matokeo yake ni kama ifuatavyo, Makiba Samson Laizer (CCM) kura 2,029 na Joyce Martin (Chadema) kura 608.

Kata ya Ambuleni, Jasephat Jackson (CCM) kura 2,057 na

Dominick Mollel (Chadema) kura 1,201. Kata ya Leguruki

Andason Sikawa (CCM) kura 3,023 na Daniel Mbise(Chadema) kura 287.

Kata ya Maroroni, Yoha Kaaya (CCM) kura 3,568 na Asanterabi Mbise (Chadema) 1,201.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH....Anatoa Pete za Bahati, Anasafisha Nyota, Anazuia Chuma Ulete na Mengine

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH CHIEF SULTAN MAKATA Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
 
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Chief Sultan Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
 
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Chief Sultan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
 
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. 

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp/Calls 0658316976
0755911233
 
Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote

Lowassa Apangua Kauli za Mkuu WA Mkoa...Akanusha Kutaka Kurudi CCM

$
0
0
Aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA 2015 Edward Ngoyai Lowassa ambaye alihama CCM, ameweka wazi taarifa za kutaka kurudi CCM, na kusema kwamba hana mpango kabisa na wala hafikirii kurudi CCM.

Lowassa ameyasema hayo kufuatia kauli iliyotolea na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho ambo, kwamba Lowassa ana mpango wa kurudi CCM kama baadhi ya wananchama wengine wa CHADEMA walivyofanya, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote na haitakuja tokea.

“Hizo habari ndio nazisikia kutoka kwenu, taarifa hizi si za ukweli na uongo mtupu, sijaomba kukutana na rais, nashangaa kwa nini mkuu wa mkoa mzima anasema uongo mkubwa kiasi hicho, na anaachiwa bila kuchukuliwa hatua”, amesema Edward Lowassa.

Edward Lowassa ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha Mrisho Gambo ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha kusema hadharani kwamba Lowassa amemuomba amkutanishe na Rais Magufuli kwani anataka kurudi kwenye chama, ni kitendo kisichofaa kwa kiongozi mkubwa kama yeye, na kumtaka aache mara moja kwani yeye sio msemaji wake.

“Ni jambo la jabu sana, nataka kumwambia Mrisho Gambo aache uongo sina mpango wa kurudi CCM na siihitaji CCM, wananchi wapuuze maneno hayo, ni uongo, anastahili kuchukuliwa adhabu, nasikitika sana Gambo anataka kuchukua wajibu ambao sio wake, haihitaji kuwa msemaji wangu na wala simuhitaji kuwa msemaji wangu, naiheshimu sana ofisi ya mkuu wa mkoa nategemea atashughulika na ofisi ya mkuu wa mkoa inayomuhusu, badala ya kutoa maneno ya uongo mtaani”, amesema Edward Lowassa.

Hivi karibuni Mrisho Gambo alisikika akisema kwamba amefuatwa na baadhi ya watu ambao wametumwa na Lowassa, kumuomba amsaidie kukutana na Rais Magufuli ili aweze kurejea CCM, kwani uamuzi ambao aliufanya mwaka 2015 wa kuhama chama ulikuwa ni uamuzi wa hasira.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images