Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Picha 3 za Tundu Lissu Baada ya Kutoka Nje Kwa Mara ya Kwanza

$
0
0
Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu imesema kwamba kwa mara ya kwanza ndugu yao alipotolewa nje kupata hewa na kuota jua kauli yake aliyoitoa alisema kuwa ni sawa na ukiwa mfungwa huoni jua, mawingu wala hupigwi upepo wa kawaida.

Katika mahojiano aliyofanyiwa Kaka wa Lissu,  Wakili Alute Mughwai Lissu amesema kwamba mara baada ya ndugu yake kutolewa nje na kukaa kwa takribani dakika 30 siyo yeye Lissu peke yake aliyefurahi bali ndugu wote waliokuwepo hospitalini hapo walifurahia mno hilo tukio.

Bw. Alute amesema kwamba awali Manesi walipanga kumtoa nje Jumamosi (Oktoba 14) na kwa kuwa Lissu alijua tunakwenda, aliwaeleza wasimtoe bali wasubiri ndugu zake wafike.

"Nilikuwa mimi na ndugu wengine. Ilipofika saa 10 jioni tulimtoa na mimi ndiye nilimtoa ICU, alifurahi na sisi tulifurahi kwa hatua hiyo,” amesema Kaka huyo mkubwa wa Lissu.

Alute ameeleza kwamba baada ya Lissu kupata upepo wa nje kwa nusu saa nzima alirudishwa wodini ambako amefafanua siyo ICU tena ingawa pia kuna ulinzi na uangalizi wa karibu na si kila mtu anaweza kumwona na kuongeza kwamba hali ya ndugu yake inazidi kuimarika huku akili  zake zikiwa  timamu.

Pamoja na hayo Alute amesema kwamba suala la kumpeleka sehemu tofauti ya matibabu ndugu yao familia ndiyo itakayoshughulika zaidi kwa ukaribu na kuongeza kwamba,  ndugu wengine wapo sehemu mbalimbali kama Kenya, Australia, Marekani, Canada ambao watabidi wajadiliane kwanza ndipo watatoa taarifa juu ya nini kinaendelea.


Kauli ya Lulu Michael Kuhusu Kesi Yake ya Mauaji ya Bila Kukusudia ya Steven Kanumba Inayoanza Tena Kesho

$
0
0
Ikiwa imebakia siku moja kuanza kusikilizwa tena kwa kesi ya mauaji ambayo inamkabili, msanii Elizabeth Michael (Lulu) amesema yupo tayari kukabiliana na kesi hiyo, ambayo alijua ipo siku itarudi tena.

Lulu ameyasema hayo leo alipokuwa  kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa alikuwa na taarifa ya kesi hiyo kabla watu hawajaipata kwenye mitandao, na utaratibu wa kisheria ulifuatwa.

“Unajua watu hawajui sheria, kesi haikuwahi kuisha ni pocedure ya kawaida ya mahakama imefuatwa na ni muda wake umefika sasa , siyo kama imeibuka tu, na kwasababu mimi ndiye muhusika nimepata taarifa kwa njia ya kisheria siyo kama nyie kwenye mitandao, na pengine niliipata kabla yenu”, amesema Lulu.

Lulu ameendelea kusema kwamba kuwepo kwa kesi hiyo kunamuathiri kwa kiasi kikubwa kwenye kazi zake na maisha yake kiujumla.

Kesi inayomkabili muigizaji huyo wa bongo movie inatarajia kusikilizwa tena kesho Oktoba 19, 2017 baada ya kuwa nje kwa dhamana kwa muda mrefu.

Elizabeth Michael (Lulu) anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo bila kukusudia cha  aliyewahi kuwa muigizaji  wa filamu nchini, Steven Kanumba, mnamo  April 7,  2012 .

Haji Mnara: Bila CHADEMA na Tundu Lissu, CCM Italala

$
0
0
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Timu ya Simba, Haji Manara ambaye ni mwanachama wa CCM amefunguka na kusema hajawahi kumshabiki Tundu Lissu wala CHADEMA lakini anaamini bila uwepo wake na CHADEMA basi chama chake CCM kitalala.

Haji Manara amesema hayo leo baada ya kuona picha ya kwanza ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiwa hospitali jijini Nairobi nchini Kenya ambapo anapatiwa matibabu kufuatia kupigwa risasi Septemba 7, 2017 na watu wasiojulikana.

"Ohhh God,mimi sijawahi kukushabikia wewe wala chama chako ila nakuombea kwa Mungu upone haraka kaka, urudi katika harakati zako nikiamini bila uwepo wenu chama changu kitalala" aliandika Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instgram.

Mbali na Haji Manara watu wengine wengi wameonyesha kufurahishwa na hali ya Tundu Lissu baada ya kumuona kupitia picha ambazo zimeanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Mbunge huyo wa Singida Mashariki anatarajiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu ya awamu ya tatu siku za karibuni.

Habari Zilizopo Katila Magazeti ya Leo Alhamisi ya Octoba 19

Jipatie Riwaya ya Kusisimua ya Power na You Kill Me toka kwa Mwandishi Makini

$
0
0
HABARI NJEMA KWA WASOMAJI WA HADITHI ZANGU MPYA  POWER NA AIISSII U KILL ME LEGACY

*WATUMIAJI WA WHATSAPP*
Kwa wapenzi wa hadithi zangu mpya POWER na AIISSII U KILL ME LEGACY sasa unaweza kujiunga kwenye group langu whatsapp kwa sh 3000 tu kwa mwenzi na malipo yote hufanyika kwa MPESA 0768516188 JOYCE MBWAMBO au TIGOPESA 0657072588 AZARIA MSULWA. Namba ya whatsapp 0657072588 karibu sana

*WATUMIAJI WA FACEBOOK*
Kwa wale watumiaji wa mitandao ya Facebook hatujawaacha nyuma katika kupata uhondo wa hadithi hizo(POWER na AIISSII U KILL ME LEGACY). Jiunge kwenye group langu la siri la Facebook kwa sh 3000 na utaendelea kusoma hadithi hizo kuanzia siku ya J3 hadi Jumamosi na kila siku utasoma episode mbili. Wahi sasa kwa maana nafasi ni cheche na tunawajali sana wasomaji wetu, Niandikie ujumbe wako kwenye akaunti zangu za facebook ambazo ni @storyzaeddy-tz au Eddazaria Msulwa au Eddazaria Msulwa Jr na huko kote nitapata ujumbe wako. Pia nipigie simu kupitia namba 0657072588 au 0768516188 au 0682630798

KITABU CHA PRESIDET WIFE BADO KINAPATIKANA KWA OFA YA SH 8000 TU

Naomba uendelee kuni support kazi zangu zote za uandishi zinazo zidi kusonga mbele hivi sasa. Karibuni sana.

Historia Mpya Yaandikwa Kati ya Tanzania na Barrick Mine

$
0
0
Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Barick nchini imekubali kulipa fidia ya dola milioni 300 ambazo sawa na bilioni 700 za Tanzania, pamoja na kuweka mgao sawa wa faida wa 50/50 na serikali, kufuatia mazungumzo ya ripoti ya makinikia.

Taarifa hiyo imetolewa leo na serikali wakati ikikabidhi ripoti ya mazungumzo hayo kwa Rais John Pombe Magufuli, na kusema kwamba licha ya makubaliano hayo, pia kampuni hiyo imekubali masharti yote yaliyowekwa kufuatia mazungumzo hayo, ili nchi iweze kunufaika na rasilimali zake.

Pia kwenye ripoti hiyo imekubaliwa kuwa migodi yote itaweka fedha zake kwenye akaunti zilizopo hapa nchini, na serikali kubakia na umiliki wa madini yote yatakayokuwepo kwenye makinikia, ukiondoa dhahabu, shaba na fedha ambayo yatakuwa yanamilikiwa na Barrick kisheria.

Pamoja na hayo makubaliano yaliyofikiwa yameitaka kampuni hiyo kuwapa ajira za kudumu wazawa wa eneo husika, na kuwapa stahiki zote kama wafanyakazi, na wamekubali kulipa kile kinachostahili kwenye halmashauri husika ambako migodi ipo.

Kufuatia ripoti hiyo Rais Magufuli ameipongeza timu iliyohusika kwenye mazungumzo hayo, na kuwataka Watanzania kushirikiana katika kuleta maendeleo ya nchi.

Nape Ampa Neno Tundu Lissu

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kusema amefurahi kumuona Tundu Lissu akiwa katika furaha na tabasamu na kumuomba kwa sasa asiseme lolote mpaka pale atakapona kabisaa.

Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema tabasamu la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa kwenye hospitali jijini Nairobi linatoa matumaini makubwa.

"Mjomba tunamshukuru Mungu kwa tabasamu hili la matumaini!Nakuombea afya iimarike kabla hujasema mengi! Tulia mjomba upone kabisa kwanza" alisema Nape Nnauye

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma nyumbani kwake na baadaye alipelekwa jijini Nairobi kwa matibabu zaidi ambapo mpka sasa anapatiwa matibabu huko. 

CHADEMA Wajitoa Muhanga Sakata la Lowassa

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amefunguka na kusema kwamba wanawaruhusu Chama cha Mapinduzi watumie nafasi ya Lowassa kuwepo Chadema kuwaita wao mafisadi kama jinsi wao walivyofanya kwa miaka mingi.

Salumu amesema kwamba kuwataja watu ambao waliwaita vinara wa ufisadi na leo wapo nao kwenye chama chao ulikuwa ni wajibu wao kama chama cha upinzani kutumia upenyo wa udhaidfu wa chama cha mapinduzi kuonyesha wananchi madhaifu ya serikali.

"Lazima ukubali kwamba ni wajibu wetu kuonyesha madhaifu ya serikali, Kama tulikuwa tunampinga Lowassa kwamba ni fisadi ulikuwa ni wajibu wetu Chadema. Sasa kama leo hii Lowassa yupo kwetu ni wajibu wao CCM kuwaambia watanzania kuwa Chadema kina mafisadi. Kwa sababu Lowassa amekuja Chadema ni yule yule wala hajawa malaika kama jinsi ambavyo kelele zinavyopigwa," Mwalimu amefunguka

Akizungumzia kuhusu chama kupwaya na kumtegemea mtu mmoja kuwa mkosoaji wa serikali iliyopo Madarakani, Mwalimu amesema kupanga ni kuchagua hivyo wao kama Chadema wanauwezo mkubwa wa kukosoa  lakini  huamua kuchagua nani atoe hoja kwa wakati gani na siyo kwamba wameishiwa.

"Hata kwenye timu ya mpira wapo mastaa wengi wanaofanya vizuri lakini huangaliwa ni nani wa kuibeba timu, ndivyo hata Chadema ilivyo, mnaweza kuwa wengi lakini kupanga ni kuchagua, Tundu ni Mwanasheria Mkuu wa chama hivyo chama kinaanda ajenda lakini atachaguliiwa mmoja wa kuifikisha ajenda hiyo huku wengine tukitoa sapoti, inategemea ajenda hiyo pia inatolewa wakati gani, mbona hapa katikati mengine yametokea kwani tumemuinua Lissu kitandani atusaidie kusema. si tulisema wenyewe. ? hivyo hakuna mtu mmoja anayeibeba Chadema bali tunashirikiana pamoja", Mwalimu ameoneza.

Huu ni utaratibu wetu hata kipindi cha kina Mh. Zitto Kabwe pamoja na Dkt. Slaa wote agenda zilikuwa ikitengenezwa na watu ndani ya chama na wanaozipeleka mbele huwa ni wachache siyo kwamba eti chama kimepwaya.

Katika hatua nyingine Mwalimu amesema lengo la chama cha upinzani ni kushika dola na siyo kusikiliza jinsi ambavyo watu wengine wanavyokosoa na kusisitiza kwamba Chama chao kilianzishwa kwa malengo ya kuja kushika dola.

TUCTA Wamjibu Msenaji Mkuu wa Serikali

$
0
0
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA limesisitiza  kuwa madai ya wafanyakazi  iliyowasilisha serikalini ni halali na litaendelea kufuatilia ili wahusika wapate stahiki zao.

Akizungumza jijini  Arusha Rais wa TUCTA Tumaini Nyamhokya amesema wamesikitishwa na kauli ya Msemaji  Mkuu wa Serikali ya kutaka madai ya wafanyakazi yapuuzwe na kwamba kauli hiyo haikuwa na busara yoyote.

Nyamhokya amesema kwamba madai yao wameyafanyia utafiti wa kina na wanaendelea kusisitiza kuomba serikali itekeleze ahadi zake za nyongeza ya mshahara, upandaji wa madaraja kwa wafanyakazi, nyongeza ya mshahara ya kila mwaka ambayo ipo kisheria na madai ya wafanyakazi yatokanayo na mishahara na yasiotokana na mishahara.

"Tuna madai halali yaliyofanyiwa utafiti wa kina na bado tunahitaji utekelezaji wake kwa haraka ili kuleta nafuu ya wafanyakazi nchini," amesema.

Nyamhokya amesema TUCTA inaendelea kutambua dhamira ya kweli ya Rais John Magufuli katika kutatua changamoto za wafanyakazi nchini na hawataki malumbano na Serikali zaidi ya kushirikiana kutatua kero zilizopo.

Amesema hawahitaji malumbano na serikali na wao kazi yao ni kufuatilia maslahi ya wafanyakazi na sio chama cha siasa kama ilivyodaiwa karibuni na msemaji wa serikali Dk.Hassan Abasi kuwa madai yao yapuuzwe na kwakuwa  TUCTA wanafanyasiasa

Amesema si sahihi kuhusisha TUCTA na wanasiasa kwa kuwa wao jukumu lao kubwa ni kutetea masilahi na haki za wafanyakazi tofauti na ajenda za vyama vya siasa kutaka kushika dola.

Rais Magufuli: Mwekezaji Ambaye Hataki Atupishe na Kutuachia Madini Yetu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameitaka Tume iliyofanya mazungumzo na kampuni ya uchimbaji ya madini Barrick Gold Mining, kuandaa mazungumzo maalumu ya  aina hiyo hiyo kwenye madini ya Tanzanite na Almasi ili nchi ipate faida na kama wamiliki hao wakikataa basi waondoke moja kwa moja.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati alipokuwa akipokea taarifa maalum ya mazungumzo kati ya timu ya wataalamu aliyoiunda na timu ya wataalamu kutoka kampuni ya Barrick Gold Mining kuhusu madini ya dhahabu.

 "Baada ya tume hii ya dhahabu nataka mfanye 'negotiation' ya namna hii kwenye almasi lakini pia mfanye negotiation kama hii kwenye Tanzanite, Mpangee mapema, muanze haraka. Hakuna kulala. Zege hailali. Lazima tufanye kwa spidi  ili Almasi nayo muingie kwenye majadiliano yake tuweze kupata faida. Atakaye kataa kuja kufanya majadiliano atupishe atuache moja kwa moja na madini yetu. Kamati hii imeonyesha njia.... Atakayekataa atupishe. Tutafanya hivyo kwenye madini yote na nyinyi mmeshaonyesha njia," Rais Magufuli .

Pamoja na hayo  Rais Magufuli amesema amekubaliana na  mapendekezo yaliyotolewa na Waziri Prof. Kabudi kuwa iendelee kufuatilia madai yote kwa ajili ya pande zote mbili.

Kwa upande mwingine Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Barick nchini imekubali kulipa fidia ya dola milioni 300 ambazo sawa na bilioni 700 za Tanzania, pamoja na kuweka mgao sawa wa faida wa 50/50 na serikali, kufuatia mazungumzo ya ripoti ya makinikia yaliyofanyika kwa zaidi ya miezi mitatu,

Serikali Yawapa Siku 7 Wavamizi Nje ya Nchi

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kuwapa siku saba wavamizi ambao wapo kwenye pori tengefu la Loliondo kuondoka mara moja ndani ya siku hizo kwani wasipofanya hivyo baada ya hapo mali zao zitataifishwa na serikali.

Kigwangalla amesema uwepo wa wavamizi hao ambao wana ng'ombe zaidi ya 6,000 na matrekta zaidi ya 200 kutoka nchi ya jirani imekuwa sababu kubwa ya chanzo cha mgogoro wa ardhi baina ya vijiji na hifadhi hiyo.

"Kuna taarifa kwenye eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu la Loliondo, kuna ng'ombe zaidi ya 6,000 na trekta zaidi ya 200 toka nchi jirani, yote kinyume cha sheria! Uwepo wao siyo tu unahatarisha uhai wa mfumo wa ikolojia ya Serengeti-Mara, bali pia unapunguza eneo la kuchungia kwa wenyeji wa Loliondo. Hivyo kuleta kiu ya wananchi wa Loliondo kuingia ndani zaidi ya eneo la hifadhi kutafuta malisho na hatma yake kuhatarisha uhai wa Serengeti. Uvamizi huu wa wenzetu kutoka nchi jirani ni moja ya sababu kubwa (zilizojificha) za mgogoro wa ardhi baina ya vijijj na hifadhi kukolea moto" alisema Waziri Kigwangalla

Aidha Waziri huyo amesema wakati wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu wamewataka wavamizi hao kuondoka katika maeneo hayo

"Wakati tukiendelea kutafuta suluhisho la kudumu, tutaondoa makando kando kama haya haraka. Leo tumetoa siku saba kwa wavamizi wote toka nchi jirani waliopo eneo la Loliondo bila kufuata taratibu za kisheria waondoke na mali zao la sivyo tutazitaifisha" alisisitiza Kigwangalla.

Ujumbe mzito alioandika Zitto Kabwe kwa Tundu Lissu

$
0
0
Na Zitto Kabwe.
Jana nimefarijika kukusikia tena sauti yako tangu nikusikie nilipokuja kukusabahi hospitalini. Sauti yako sasa imeboreka na kurudi sauti ile ile uliyokuwa nayo kabla hujashambuliwa kwa risasi nyumbani kwako Dodoma. Watanzania wamefarijika sana kuwa bado uko hai na utaweza kuungana nasi tena kuendeleza mapambano ya kujenga demokrasia yetu.

Siku ile nimekuja kukusabahi uliniuliza nini kinaendelea nyumbani. Nilikwambia tu Watanzania wanakuombea. Ukanitazama kwa lile jicho lako la kiMarx, ukacheka na kusema “Taifa la Waomba Mungu”.Tukacheka. Ni kweli Watanzania wamekuombea sana, na ni jambo la kushukuru kuwa Mola amewasikiliza maombi yao.

Ninafuraha kuwa unaendelea vizuri sana tofauti na nilipokuja kukuona. Tutazidi kumwomba Mola afya yako iimarike zaidi. Tuna kazi kubwa sana mbele ya safari, na kwa hakika ni lazima tuifanye kwani tusipoifanya nchi yetu itaanguka kiuchumi na kidemokrasia, na watu wetu kuendelea kuwa maskini zaidi kuliko ilivyo sasa.

Ilikuwa ni lengo la waliokushambulia kutunyamazisha. Tumewaambia kuwa hatutanyamaza kamwe. Kama ulivyoniambia ukiwa kitandani kuwa “tumeshashinda. Tutashinda”. Hakika ushindi ni dhahiri na ndio maana wanatapatapa kuzuia uhuru wa mawazo na fikra.

Ndugu yangu, nisikuchoshe na barua ndefu kwani najua bado hujawa na nguvu za kutosha. Nilikuletea kitabu nikamwambia mkeo awe anakusomea. Naamini anafanya hivyo. Juzi tulisherehekea miaka 50 tangu kuuawa kwa komredi Che Guevara. Najua unavyompenda Che tungekutana ubalozi wa Cuba hapa Dar siku ile.

Shambulio la kutaka kukuua limetuonyesha watu wanaoumizwa na ‘INJUSTICE’ na wasioumizwa nayo. Wengi wasioumizwa na ‘Injustice’ wanadiriki hata kuhoji kwa nini eti tunapaza sauti kuhusu suala lako. Jibu letu kwao ni nukuu hii ya komredi Che Guevara, nukuu ambayo huniongoza katika maisha yangu ya mapambano ya haki.

“If you tremble with indignation at every injustice, then you are a comrade of mine” (Kama unaumizwa na kila uonevu, popote pale duniani, basi wewe ni mwenzangu).

Aahh! Ndugu yangu nilisema nisikuchoshe. Nikuache upumzike, uwe imara zaidi. Basi pumzika na hili pia;

“We cannot be sure of having something to live for unless we are willing to die for it”  (Hatuwezi kuwa na uhakika wa kulipambania jambo mpaka kwanza tuwe tayari kufa kwaajili ya jambo hilo) – Ernesto ‘Che’ Guevara.

Wewe umetuonyesha hilo kwa vitendo na ndio maana upo hospitali Nairobi. Sisi sote twapaswa kuwa Tundu Lissu.

Pole sana Komredi, Mola akupe afya njema.

Samson Mwigamba Aibwaga ACT- Wazalendona Kujiunga CCM

$
0
0
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba na wanachama wengine 10 wametangaza kujiunga na chama cha CCM baada ya kujivua uanachama wa ACT Wazalendo leo.

Taarifa za Mwigamba kujiunga na CCM zimetolewa leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, na kusema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kujitenga na upinzani unaokerwa na maendeleo ya nchi, na pia kuunga mkono juhudi za serikali za mapambano dhidi ya rushwa.

“CCM ya sasa ndicho chama kinachotekeleza kwa karibu itikadi, falsafa na sera za ACT Wazalendo ambazo mimi na wenzangu tulishiriki kukiasisi, nchi yetu ndio kinara wa mapambano dhidi ya rushwa sasa hivi, sera ambazo ndio misingi ya ACT Wazalendo, tumeamua kujitenga na upinzani unaokerwa na mafanikio ya nchi ili tuendelee kuwa sehemu ya mapambano katika kurejesha nchi kwenye misingi yake”, amesema Mwigamba.

Samson Mwigamba atakuwa kiongozi wa pili ACT Wazalendo kujivua uanachama wa ACT Wazalendo kwa mwaka huu baada ya Prof. Kitila Mkumbo ambaye naye alifanya hivyo wiki kadhaa zilizopita.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Octoba 20

Kikwete Amfariji Tundu Lissu

$
0
0

Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete amefunguka na kusema kuwa amefurahi kumuona Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiwa mwenye tabasamu na furaha na kuzidi kumuombea apone kabisa na kurudi kupambana.

Ridhiwani Kikwete amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram na kusema Mungu siku zote anatenda wema kwa watu kufuata kushambuliwa kwa risasi nyingi Tundu Lissu na hatimaye kuweza kupona na sasa furaha yake kuanza kurejea.

"Mungu utenda wema siku zote. Ashukuliwe yeye kwa kazi ya kurejesha tabasamu katika sura yako na afya kwa wanaokuuguza. Nimefurahi kukuona tena msomi, Kiongozi wangu na mwana kamati mwenzangu wa Bunge ukitabasamu na mwenye Afya njema. Mungu akulinde na akusimamie katika matibabu yako .Looking forward to see you back into your good shape" aliandika Ridhiwani Kikwete

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mnamo Septemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma na kisha baadaye kusafirishwa na kupelekwa jijini Nairobi Kenya kwa matibabu ambapo mpaka sasa yupo nchini Kenya akiendelea kupatiwa matibabu.

Nyalandu Ajitoa Muhanga Sakata la Katiba Mpya

$
0
0
Wakati mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu akieleza kuwa anakusudia kuwasilisha hoja ya muswada binafsi kwa Spika utakaoweka sharti la kurejea upya mjadala wa Katiba mpya, utafiti umeonyesha kuwa wananchi wawili kati ya watatu wanasema Tanzania inahitaji Katiba mpya.

Pia, nusu ya wananchi wanasema mchakato wa Katiba uanze upya na tume mpya.

Jana kupitia katika akaunti zake za mitandao ya kijamii ya Instagram, Twitter na Facebook Nyalandu aliandika, “Nakusudia kuwasilisha kwa Spika wa Bunge, mheshimiwa Job Ndugai azma yangu ya kuleta muswada binafsi wa sheria katika kikao kijacho cha Bunge itakayoweka sharti la kurejea upya mjadala wa Katiba mpya ya Tanzania, kwa kuzingatia rasimu ya Katiba ilivyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba.”

Nyalandu alisema muswada huo anatarajia kuuwasilisha kwenye kikao kijacho cha Bunge.

Akizungumza  kwa simu baada ya kuandika maneno hayo, Nyalandu alisema amekusudia kupeleka muswada huo kwa sababu mchakato wa Katiba mpya haukufikia mwisho.

“Nitafurahi sana kama jambo hili litafanikiwa kwa kuwa lina umuhimu wake kwa kila mtu. Suala hili pia halina itikadi za vyama vya siasa na lina masilahi, kwa sababu Katiba ina uwezo wa kukaa zaidi ya miaka 100,” alieleza Nyalandu.

Mbali na Nyalandu kueleza hayo, mwezi uliopita asasi za kiraia zaidi ya 80 zilijitokeza hadharani na kutoa tamko zikisema kwamba huu ni wakati mwafaka wa mchakato wa Katiba kuanza upya ili ifikapo 2020 iwe imepatikana.

Kabla ya asasi hizo kutoa tamko, Jukwaa la Katiba lilijitokeza na kusema litaandaa maandamano ya amani kumueleza Rais John Magufuli umuhimu wa kuandika Katiba mpya.

Mbali na hayo, jana matokeo yaliyotolewa na Twaweza katika utafiti uitwao ‘Zege imelala?’ yameeleza kuwa wananchi wawili kati ya watatu wanasema Tanzania inahitaji Katiba mpya, huku nusu yao wakisema mchakato wa Katiba uanze upya na tume mpya.

Utafiti huo umesema muhtasari unatokana na takwimu kutoka sauti za wananchi ukiwa ni utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.

Mkurugenzi mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze alisema, “Wananchi wanataka Katiba mpya. Wengi wao wanataka mchakato uanze upya na tume mpya katika ukurasa mpya. Hata hivyo, wapo wananchi ambao wapo tayari kusonga mbele kwa kutumia rasimu iliyoandaliwa na tume iliyotangulia.”

Pia, alisema kuwa wananchi wanaunga mkono kipengele kilichoongeza madaraka ya Bunge katika suala la kuwapitisha mawaziri walioteuliwa na kinachowapa wananchi haki ya kuwaondoa wabunge wanaozembea kazini.

Eyakuze alisema utafiti umedhihirisha uwajibikaji wa siasa kwenye uhalali wa mchakato wa Katiba.

“Matokeo yameonyesha dhahiri kwamba wananchi wengi wanatatizwa katika kutofautisha kitendo cha Ukawa kugomea Bunge la Katiba na migomo mingineyo. Ushabiki wa kisiasa huwafanya watu wengi kutozingatia uhalali wa jambo husika,” alisema.

Eyakuze alisema, “Hivyo basi; vyovyote tutakavyofufua mchakato wa Katiba ni muhimu kwa wahusika wakuu kuheshimu na kutambua kwamba sheria mama ya nchi ni ya thamani zaidi kuliko tofauti za kisiasa. Tanzania inahitaji mchakato wa Katiba utakaozingatia uhalali na ujumuishi wa Watanzania wote.”

Taarifa ya Twaweza kwa vyombo vya habari ilisema asilimia 67 ya Watanzania wanasema ni muhimu kwa Tanzania kupata Katiba mpya na asilimia 56 wanasema toleo la mwisho la rasimu ya Katiba lipigiwe kura na wananchi.

Hata hivyo, asilimia 48 ya wananchi wanasema kwa maoni yao, Katiba mpya haitapatikana ndani ya miaka mitatu ijayo.

Taarifa hiyo ilisema wananchi wanaendelea kuunga mkono kwa nguvu kubwa uundwaji wa Katiba mpya inayotilia mkazo suala la uwajibikaji.

Ilisema asilimia 79 wanataka mawaziri wanaoteuliwa wapitishwe na Bunge na asilimia 64 wanataka wawe na uwezo wa kuwaondoa wabunge katikati ya mihula yao iwapo hawatatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Hata hivyo, wananchi wamegawanyika kwenye baadhi ya hatua za uwajibikaji zilizopendekezwa ikiwamo kuzuia viongozi na watumishi wa umma kuwa na akaunti nje ya nchi (asilimia 52 wanaunga mkono), kuwapo kwa ukomo wa ubunge (asilimia 52 wanaunga mkono) na kuweka kanuni za uwazi na uwajibikaji kuwa sehemu ya tunu za Taifa (asilimia 48 wanaunga mkono).

Hivyo vyote ni vipengele vya rasimu ya Katiba ambavyo viliondolewa na Bunge Maalumu la Katiba.

Twaweza ilisema wananchi pia wanaunga mkono kuondolewa kwa kipengele kinachotaka kuchunguza na kudhibiti ofisi ya Rais (asilimia 55) na mawaziri kuchaguliwa kutoka nje ya Bunge (asilimia 62).

Matokeo hayo taasisi hiyo imesema yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,745 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye utafiti huu) Juni hadi Julai 2017.

Kuhusu muundo wa Serikali ni moja kati ya vipengele vilivyoibua mjadala mzito wakati wa mchakato wa kuunda Katiba mpya na hatimaye kuwagawa wananchi. Asilimia 42 ya wananchi wa Tanzania Bara waliunga mkono muundo wa Serikali mbili.

Twaweza imesema muundo wa Serikali moja ulikubalika kwa asilimia 25 na ule wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ulipendwa na asilimia 16.

Mchakato wa Katiba mpya ulisimama Oktoba 2014 baada ya Tume ya Uchaguzi kudai kuwa ungeiliana na Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Mdogo wa Steven Kanumba Atoa Ushahidi Mahakamani Jinsi Kanumba Alivyofariki

$
0
0
Kesi ya mauaji inayomkabili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael (Lulu) imeendelea kusikilizwa  jana katika Mahakama Kuu jijini Dar es salaam, kwa upande wa mshataka kuanza kutoa ushahidi wao.

Akitoa ushahidi ndugu wa marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco, alisimulia mahakama jinsi ilivyokuwa siku ya tukio, na kwamba aligundua kuwa kaka yake hapumui baada ya kugombana na mpenzi wake Lulu.

"Siku ya tukio marehemu Kanumba alinambia nisitoke nyumbani anataka tutoke wote kuanzia saa sita usiku, akaja Lulu na Kanumba ndiye aliyemfungulia mlango Lulu, alipofika ndani nikasikia akimuuliza Lulu kwanini anaongea na boyfriend wake mbele yake? Katika malumbano yao Kanumba alikuwa akimvuta Lulu arudi ndani na Lulu naye alikuwa anataka kutoka nje, wakati wakiendelea kugombana mlango wa chumba changu sikuufunga”, alisikika Seth akiisimulia Mahakama.

Seth aliendelea kusimulia kuwa …..”Baada ya ugomvi Lulu alikuja chumbani kwangu akilia, akanambia Kanumba kadondoka amejaribu kummwagia maji haamki. Na ilikuwa mara ya kwanza kuona ugomvi kati yao, nilipoingia chumbani nilimkuta Kanumba chini kaegemea ukuta nikamlaza chali nikamtafuta daktari wake, Dk Kageiya, alipofika alimfanyia chek up akanambia ameshafariki ila akashauri tumpeleke hospitali ya Muhimbili”..

Hata hivyo, alipoulizwa na moja wa wazee wa Baraza, Rajabu Mlawa baada ya kutoa ushahidi wake, kama anajua aliyesabisha kifo cha msanii huyo, shahidi huyo alisema hajui.

Mzee wa Baraza: Katika kumchunguza kwako marehemu baada ya tukio hilo, ulibaini kwamba marehemu alipata madhara gani?

Shahidi: Madhara niliyoyabaini ni kukosa pumzi

Mzee wa Baraza: Hayo madhara ya kukosa pumzi yalisababishwa na ugomvi ule?

Shahidi: Kwa hilo mimi siwezi kujua nini kilisabisha kukosa pumzi.

Mzee wa Baraza: Umesema kuwa ulipokwenda chumbani kwa marehemu ulimkuta ameanguka akiwa ameegemea ukutani, unajua ni nani alisababisha tukio la kuanguka?

Shahidi: Siwezi kujua ni nani aliyesababisha kwa sababu mimi sikuwemo mle ndani

Wakati akihojiwa na wakili wa mshtakiwa, Peter Kibatala, kama alikuwepo wakati sampuli za mwili wa marehemu zikichukuliwa kwa ajili ya vipimo vya maabara, kama ilivyoandikwa kwenye maelezo yake, alisema hakuwepo.

“Mimi sikuwepo wakati wa kuchukua sampuli za mwili wa marehemu. Alikuwapo ndugu yangu mwingine, mimi nilikuwepo kwenye mostmortem (taarifa ya kitabibu ya chanzo cha kifo) ya kawaida.”

Wakili Kibatala: Kwa hiyo aliyeandika hapa alikuwa akibuni?

Shahidi: Siwezi kusema kuwa alikuwa akibuni, labda kama ungemuuliza mwenyewe.

Wakili: Katika maelezo yako Polisi ambayo uliyaandika muda mfupi tu wakati wa tukio, kuna mahali ulipoeleza polisi kwamba ulipokwenda kumfuata Dk Paplas ulimwambia mshtakiwa abaki na marehemu?

Shahidi: Hakuna mahali ambapo kuna kipengele nilipomweleza polisi kuwa nilimuacha Elizabeth Michael na marehemu (Baada ya kusoma maelezo yake)

Hata hivyo, alipoulizwa tena na Wakili wa Serikali, George kuhusu kuwepo kwa tofauti ndogondogo katika maelezo yake aliyoyaandika polisi na yale aliyoyatoa kwenye ushahidi wake mahakamani, shahidi huyo alieleza kuwa yeye alikuwa akihojiwa tu na aliyekuwa akiandika ni askari.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Sam Rumanyika iliahirishwa na itaendelea tena leo kwa mashahidi wengine wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao.

Awali Wakili George aliieleza mahakama kuwa alitegemea kuwa na mashahidi wawili jana, akiwemo Dk Kageiya, lakini wakati wakifanya mazungumzo na shahidi huyo, aliwaeleza kuwa hajisikii vizuri na kuomba atoe ushahidi wake kesho.

Pia Wakili George aliileza mahakama kuwa wataomba kuongeza shahidi mwingine ili wafikie watano.

UN yatoa Dola Milioni 160 Kusaidia Miradi ya Maendeleo Nchini

$
0
0
Umoja wa Mataifa (UN) umetoa Dola 160 milioni za Marekani kati ya Dola 200 milioni zinazitakiwa kutolewa mwaka huu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwamo kuwahudumia wakimbizi waliopo kambi mbalimbali Kigoma.

Nusu ya fedha hizo zimeelekezwa kwenye mradi wa Kigoma wa kuwahudumia wakimbizi na kiasi kingine kimeelekezwa kwenye miradi mingine ya maendeleo inayofadhiliwa na mashirika mbalimbali ya UN.

Oktoba 24, UN itaadhimisha miaka 72 tangu kuanzishwa kwake na sherehe za maadhimisho hayo kitaifa zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 500 wakiwamo na mabalozi, wanafunzi na vyombo vya ulinzi na usalama.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ‘Maendeleo ya Viwanda na Utunzaji Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.’

Akizungumzia maadhimisho hayo jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kimataifa na kikanda, Dk Susan Kolimba alisema wameamua kuunganisha kauli mbiu ya Serikali ya kuendeleza viwanda na mpango wa UN wa kutekeleza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Mratibu mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez alisema programu ya Kigoma imebuniwa ili kukidhi vipaumbele vya maendeleo ya mkoa huo na hasa kuzilenga jamii katika wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko.

Wema Sepetu Ataja Sababu Zilizomfanya Asiende Kumuona Tundu Lissu

$
0
0
Mrembo wa Tanzania na Kada wa Chadema Wema Sepetu ametoa ya Moyoni kwa nini hakwenda kumuona mapema Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi septemba 7  ni kwamba asingeweza kumuona akiwa kwenye maumivu.

Wema ameweka wazi maneno hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni baada ya dakika chache tangu kuachiwa kwa picha za kwanza za Mbunge huyo akiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Wema ameandika "Kisichokuua kinakufanya uwe na nguvuz zaidi....Utarudi tena ukiwa na nguvu kuliko ulivyokuwa awali...Shujaa wetu. ... Picha hii imenifanya nipate hisia. Sasa naweza andaa safari ya Nairobi kuja kukuona.. Awali nisingeweza kuvumilia kukuona ukiwa kwenye maumivu".

Wema Sepetu ametajwa na Chama cha  Chadema kama mmoja wa wahamasishaji  aliyeweza kuhamasisha watu kutoa michango kwa ajili ya matibabu ya Mbunge Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa kwenye gari lake nje ya makazi yuke huko mjini Dodoma.

Ni Ushindi MKUBWA Kwa Taifa Letu........Hiii Hapa Hotuba Ya Rais Magufuli Baada Ya Kukamilika Majadiliano Kati Ya Tanzania Na Barrick

$
0
0
Majadiliano kati ya Tanzania na timu ya wawakilishi wa kampuni ya Barrick Gold inayomiliki migodi ya madini hapa nchini yamekamilika na makubaliano kati ya pande hizo yametiwa saini jana tarehe 19 Oktoba, 2017 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Timu ya Barrick Gold Corporation ilikuwa imeongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo Prof. John Thornton wakati timu iliyowakilisha Serikali ya Tanzania imeongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.

Miongozi mwa mambo waliyokubaliana ni kutekeleza mwelekeo mpya wa biashara ya madini ambapo kutakuwa na mgawanyo sawa wa faida (yaani Tanzania kupata asilimia 50 na Barrick Gold Corporation kupata asilimia 50 ya faida) na kuundwa kwa kampuni ya ubia wa usimamizi wa migodi ya madini iliyopo Tanzania ambayo itakuwa na makao makuu yake Mwanza na ofisi ndogo Dar es Salaam nchini Tanzania badala ya nchini Uingereza.

Mengine ni kufunga ofisi za uhasibu na fedha zilizopo Johannesburg Afrika Kusini na kuhamishia Tanzania na kutekeleza masharti yote ya mabadiliko ya sheria mpya ya madini na rasilimali za nchi ya mwaka 2017.

Aidha, Barrick Gold Corporation imekubali kuwepo kwa wawakilishi wa Serikali katika bodi za migodi yake yote hapa nchini, kazi mbalimbali za kwenye migodi kufanywa na kampuni za Kitanzania, Migodi kutoa ajira za kudumu kwa wachimbaji, wachimbaji hao kuishi majumbani kwao badala ya kuishi kwenye makambi ya migodi na mashauri yote ya kesi mbalimbali kufanywa hapa nchini.

Kampuni ya Barrick Gold pia imekubali kutoa Dola za Kimarekani Milioni 300 sawa na takribani Shilingi Bilioni 700 kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kupitia biashara ya kampuni hiyo.

Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo Prof. Thornton amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa msimamo wake unaojenga misingi ya biashara ya kuaminiana na uwazi, ambayo ni muhimu na ya namna yake kwa biashara katika karne hii ya 21.

Prof. Thornton amesema Barrick Gold Corporation watazingatia makubaliano haya na wanaamini kuwa yamefungua ukurasa muhimu utakaowezesha kufanya biashara kisasa.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amezipongeza timu zote mbili yaani Tanzania na Barrick Gold Corporation kwa kazi kubwa ziliyofanya kufikia makubaliano hayo na kwa kipekee amempongeza Prof. Thornton kwa nia yake thabiti ya kukubali kufanyika kwa mazungumzo na kukubali mambo yaliyofikiwa.

Mhe. Rais Magufuli amesema makubaliano hayo yataisaidia nchi kuzalishaji ajira zaidi, kupata manufaa mbalimbali yanayostahili ikiwemo fedha za kugharamia huduma za kijamii kwa wananchi na yanajenga msingi imara ambao utaiwezesha Tanzania kunufaika na rasilimali zake za madini.

Mhe. Dkt. Magufuli amemuagiza Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Kabudi kuunda timu zitakazoshughulikia biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi pamoja na migodi mingine ya dhahabu haraka iwezekanavyo ili nchi iweze kunufaika ipasavyo.

“Nataka machimbo yote ya dhahabu mchakato kama huu ufanyike, pia nakuagiza Prof. Kabudi biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi nako ni lazima kufuate utaratibu huu, asiyetaka aondoke” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Pia Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi hizi badala ya baadhi yao kuzibeza kwa kuwa zina manufaa kwa taifa na wananchi wake.

==>Msikilize  Hapo Chini
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images