Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mbowe amshangaa Askofu Pengo kwa Kuupinga Mchakato wa Katiba mpya

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kauli ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo kuhusu mchakato wa Katiba imewasikitisha.

Wakati Mbowe akitoa kauli hiyo, mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya maadili, amani na haki za binadamu kwa jamii ya madhehebu ya dini zote Tanzania, Askofu William Mwamalanga amemshauri Rais John Magufuli kuufufua mchakato huo uliokwama.

Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni akizungumza jana baada ya kuombwa kutoa maoni yake kuhusu msimamo wa Kardinali Pengo kwamba Katiba siyo kipaumbele chake, bali huduma za jamii, Mbowe alisema Askofu huyo ni kiongozi wa dini anayepaswa kulinda heshima aliyonayo ndani na nje ya kanisa.

Katika taarifa yake ya kufafanua kauli iliyotolewa na Askofu wa Jimbo la Rulenge mkoani Kagera, Severine Niwemugizi baada ya kukaririwa akisema kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi, Kardinali Pengo alisema hayo yalikuwa maoni yake binafsi siyo msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

“Mtu akiniambia priority (kipaumbele) ya Tanzania ni Katiba Mpya inabidi anithibitishie huo ukipaumbele maana siwezi kuona mtoto anakufa kwa njaa au kwa kukosa dawa eti kwa sababu ya Katiba Mpya. Kwangu mimi Katiba ni kitu ambacho kije baadaye, si cha haraka.

“Wanasiasa wasiache watoto wetu wafe kwa njaa kisa malumbano ya Katiba. Wasiache watoto wakose shule kwa sababu hela zote zimeishia kwenye malumbano juu ya Katiba,” alisisitiza Kadinali Pengo.

Lakini jana akizungumzia msimamo huo, Mbowe alisema, “Askofu Pengo ni kiongozi wa kanisa, anaheshimika na wananchi ambao si wale anaowaongoza tu lakini kwa kauli yake kuhusu Katiba, imetushangaza na imenisikitisha,” alisema Mbowe na kuongeza:

“Suala la elimu, chakula na maisha yetu yanalindwa na Katiba, ndiyo msingi wa mifumo ya rasilimali za Taifa. Anaposema haoni umuhimu wa Katiba anatufikirisha, anataka kusema mchakato wa Katiba uliogharimu mabilioni ya fedha leo hauna maana?”

Mbowe alisema umefika wakati mchakato wa Katiba uliokwama ukaendelezwa na hasa kuanzia katika rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti, Jaji mstaafu Joseph Warioba.

“Katiba ni maridhiano, tunahitaji kupata maridhiano ya pande zote, nirudie tu kwamba alichokisema Askofu Pengo kinasikitisha.”

Mbali ya Mbowe, Askofu Mwamalanga alisema suala la Katiba ni la Watanzania wote na si la mtu au kundi la watu hivyo mchakato huo unapaswa kuhitimishwa na si vinginevyo.

“Sisi mtazamo wetu, tuko pamoja na wale wanaotaka Katiba Mpya, suala la Katiba si la mtu mmoja. Mapambano ya ufisadi na rushwa yanapaswa kutambulika na Katiba na wananchi wanataka Katiba kwa nini wasipewe Katiba yao?

“Ni aibu kuona mabilioni yaliyotumika kwa Tume ya Jaji Warioba na Bunge Maalumu ya Katiba halafu mchakato unaishia juujuu. Nimshauri Rais (John) Magufuli kama anataka heshima kubwa ni huu mchakato uanzishwe kwani wananchi wanataka katiba yao.”

Pia, katibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Khamis Mataka ambaye aliomba kutoa maoni yake binafsi kuhusu mchakato huo wa Katiba alisema kinachopaswa kufanyika sasa ni jamii nzima kutafakari ni Katiba ipi ambayo wanaitaka.

“Vyama vya siasa, NGO (mashirika yasiyo ya kiserikali), kada za dini waendelee kuzungumza na kutafakari ni Katiba ipi tunaitaka, hii inayopendekezwa au turudi nyuma, unaweza kujiuliza ukiendelea na hii kwa kuipigia kura ya ndiyo au hapa, jibu litakuwa ni hapana hivyo tujadili ni Katiba ipi tunaitaka” alisema Sheikh Mataka ambaye pia ni msemaji wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata).

Kardinali Pengo Jumamosi iliyopita alinukuliwa akisema kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi kuwa Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni yake binafsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Alisema hilo alipotoa ufafanuzi kuhusu sitofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo si msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu sisi tuna utaratibu wetu wa kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Pata Tiba ya Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za: 
 
FUUl POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.
 
NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

Wanajeshi wawili wa Tanzania wauawa Huko Kongo

$
0
0
Askari wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, wameuawa kwenye mashambulizi makali yanayoendelea nchini Kongo.

Tukio hilo limetokea katika eneo la Beni ambako Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani wanapigana na kikundi cha waasi cha Uganda (ADF), kilichoanza vurugu na ukiukaji wa haki za binadamu kwa kuua raia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amethibitisha kuuawa kwa wanajeshi hao kutoka Tanzania, huku akitoa tarifa kuwa askari wengine 18 kutoka nchi tofauti wamejeruhiwa.

Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amehimiza mamlaka za Kongo kuchunguza haraka tukio hilo na kuwachukulia hatua wahusika.

Hivi karibuni nchini Kongo kumekuwa na machafuko baada ya vikundi vya uasi kuanza tena vurugu na mauaji baada ya miaka kadhaa kupita kukiwa shwari, huku serikali ya nchi hiyo na Umoja wa Mataifa wakiishtaki ADF kwa ukiukaji wa hai za binadamu na mauaji ya watu zaidi ya 700 katika eneo la Beni, tangu Oktoba 2014.

Diwan Amchana Mbowe......Amtaka Amrudishe Dr Slaa

$
0
0
Mmoja wa Madiwani ambao wamehamia CCM wakitoka CHADEMA mkoani Arusha waliokumbwa na skendo ya kununuliwa, amemtaka Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, kumtafuta aliyekuwa katibu wake Mkuu Wilbroad Slaa, ili kuokoa jahazi kwenye chama.

Kwenye video iliyoambaa ambayo anaonekana akizungumza,  aliyekuwa diwani wa kata ya Kimandolu Mchungaji Rayson Ngowi, amesema kuna haja ya kutafuta hekima za Wilbroad Slaa, ili kukisaidia chama hicho kukaa kwenye mstari unaofaa, kwa kuwa sasa kimeanguka kwa kiasi kikubwa.

Bwana Ngowi amesema hata yeye kutoka CHADEMA ameondoka kwa kutaka mwenyewe na sio kununuliwa kama inavyodaiwa, na kwamba kuna wengine watakaofuata nyuma yao baada ya wao kuondoka kwenye chama hicho.

“CHADEMA ya leo sio ile ya Dkt Slaa, CHADEMA ya leo ni  ya maslahi, CHADEMA ganganjaa, na wakikataa mimi nitasema, sikiliza Mbowe, chama chako kina matatizo makubwa, huna viongozi, kamtafute Dkt. Slaa nafikiri ataokoa jahazi, kama mnataka kurudisha imani, kwa sababu sio mimi tu nimeondoka watakuja wengi”, amesema diwani huyo.

LHRC Wamtaka Rais Magufuli Aifute Adhabu ya Kifo

$
0
0

Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu, LHRC kimemtaka Rais Magufuli kufuta sheria ya adhabu ya kifo kwani inachangia kupoteza rasilimali za nchi ikiwa ni pamoja na kutunza watu waliohukumiwa tangu mwaka 1994.

Akizungumza leo kwenye kuadhimisha kupinga adhabu ya kifo, Mkurugenzi mtetezi na maboresho ya Sheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za binadamu Bi. Anna Henga amesema kwa kuwa Rais aligoma kusaini wafungwa wanyongwe ndivyo anavyostahili pia kufuta vifungu vinavyoanisha sheria ya kunyongwa.

Bi. Mhenga amesema kwamba gharama zinazotumika kuwahifadhi watu waliopewa hukumu ya adhabu ya Kifo ni kubwa hivyo ni upotezaji wa rasilimali ambazo zingesaidia kufanyia shughuli mbalimbali.

Aidha ameongeza kwamba kwa utafiti uliofanyika haujawahi kupunguza matukio ya kihalifu kwani wafungwa hawapewi nafasi ya kwenda kurekebisha makosa yao kwa kuwa wanaishi kuhukumiwa kifo.

"Hii sheria ya hukumu ya kifo haimpi mtu nafasi ya kwenda kurekebisha makosa yake. Kwa ujumla haisaidii chochote kwani ukigalia kuna watu kibao walihukumiwa kifo hawajapata nafasi ya kurekebisha makosa yao ya awali. Lakini pia hata pamoja na kwamba adhabu hii inatolewa bado matukio bado yanaongezeka kila siku....Bi Henga ameeleza

Adhabu za vifo nchini hazitekelezwi lakini yamerudi kwa sura tofauti kama mauaji ya watu wenye ulemavu. Mfano mtua anayetenda mauaji ameyaona maisha hayana thamani hivyo kama serikali na yenyewe itatekeleza adhabu ya kifo na yenyewe itakuwa imeungana kuona kwamba maisha hayana thamani kama muuaji.

Leo Kituo cha Sheria na Haki za binadamu LHRC imeungana na Mtandao wa kupinga adhabu za kifo Duniani kuadhimisha miaka 15 ya Siku ya kupinga adhabu hiyo.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Gazi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

TRA Yataja Makusanyo ya Kodi kwa Kipindi cha Miezi Mitatu

$
0
0
Makusanyo ya kodi kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 (Julia, Agosti na Septemba) yamefikia Sh3.65 trilioni ambayo ni ongezeko la asilimia 1.2 ukilinganisha na makusanyo ya kipindi hicho kwa mwaka uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema makusanyo hayo ni hatua nzuri kuelekea lengo la mwaka ambalo ni Sh17 trilioni.

Ametoa mchanganuo wa makusanyo hayo kwa kila mwezi ambao umeonyesha kuwa wamekusanya zaidi ya Sh1 trilioni.

“Julai tulikusanya Sh1.1 trilioni, Agosti Sh1.2 trilioni na Septemba Sh1.3 trilioni. Watu wamekuwa wakitaka makusanyo hayo yawe yanasomwa kila mwezi lakini tukitoa kila robo ya mwaka tunaonyesha kiasi kwa kila mwezi,” amesema Kayombo.

Ukizidisha makusanyo hayo mara nne ambayo ni tafsiri ya mwaka mzima jumla inakuwa Sh14.6 trilioni lakini Kayombo anasema makusanyo ya robo moja hayawezi kutoa picha ya jumla kwasababu misimu ya biashara inatofautina hivyo ana matumaini lengo litafikiwa.

Amevitaja vyanzo vikuu vya mapatio kuwa ni viwanda, ajira na uingizaji wa bidhaa lakini amesema vyanzo hivyo hutoa kodi zaidi kulingana na wakati.

Kadhalika Kayombo amewakumbusha wamiliki wa majengo nchi kulipa kodi zao mapema badala ya kusubiri mwishoni mwa mwaka na kusababisha misongamano na usumbufu usio wa lazima.

Pia wamewataka wenye michezo ya bahati nasibu wametakiwa kulipa kodi zao kama sheria inavyoelekeza. “Anayepaswa kulipa kodi kwa wiki alipe na anayepaswa kulipa kwa mwezi au mwaka naye afanye hivyo.”

Kayombo amewataka wananchi kutumia na kuziamini takwimu zinazotolewa na mamlaka hiyo kwani takwimu zote nyingine kuhusiana na mapato ambazo hazijatolewa na TRA sio za kuaminika. 

Zitto Kabwe: Uchumi wa Nchi Umeyumba, Hali ni Mbaya Mtaani

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa uchumi wa nchi unazidi kudidimia na thamani ya shilingi inazidi kushuka huku mfumuko wa bei ukizidi kupaa.

Zitto Kabwe anasema kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambayo jana ametoa taarifa yake juu ya hali ya uchumi nchini ni kwamba hali si nzuri kwani uchumi umeonyesha kusinyaa na kudidimia huku wananchi wa hali ya chini wakiwa wahanga wakubwa zaidi.

"Taarifa hiyo inaonyesha namna hali ya uchumi wetu inavyozidi kuwa mbaya zaidi kwa wananchi wa hali ya chini , kwa mfumuko wa bei umepanda mno tangu kuanza kwa utekelezaji wa bajeti ya 2017/18, ongezeko ambalo limechangiwa zaidi na kupanda kwa bei ya bidhaa za chakula (bidhaa ambazo wananchi wengi zaidi wanazitumia)" alisema Zitto Kabawe

Aidha Zitto Kabwe amedai kushuka kwa thamani ya sarafu ya Tanzania kumezidi kuongeza maumivu kwa wananchi na ili kusaidia kupunguza ukali na gharama za maisha mishahara ilipaswa kupanda kwa asilimia 8 zaidi.

"Thamani ya sarafu ya Tanzania imeshuka, uwezo wa Tsh. 100 kununua bidhaa umeshuka hadi Tsh. 92.18. Maana yake ni kuwa mwaka 2016 shilingi 100,000 ilikupa bidhaa za shilingi 100,000. Mwaka huu 2017 shilingi 100,000 inakupa bidhaa za shilingi 92,000. 

"Kwa hiyo ili upate bidhaa za shilingi laki moja inakubidi uongeze shilingi elfu 8 zaidi. Kiuchumi, ili kulinda hali za wananchi, mishahara ilipaswa kupanda kwa asilimia 8 ili kuwapunguzia maumivu ya gharama za maisha. 

"Lakini hali hiyo inatokea katika wakati ambao mishahara haijapanda, na Rais wa nchi yetu kasema Serikali anayoingoza haitapandisha kabisa mishahara. Hali ni mbaya mno mtaani, mijini uzalishaji wa bidhaa za viwanda umeshuka kwa zaidi ya nusu, kutoka trilioni 1.5 mpaka bilioni 700 tu" alisisitiza Zitto Kabwe

Mbali na hilo Zitto Kabwe ametoa ushauri wa nini serikali inapaswa kufanya ili kukabiliana na hali hiyo na kupunguza ukali wa maisha kwa wananchi

 Zitto amedai Serikali inapaswa itazame namna inatekeleza mipango yake ya Maendeleo, Serikali isikilize na kufanyia kazi mawazo ya sekta binafsi katika kuweka sawa mazingira ya uwekezaji bila kupoka haki ya nchi kufaidi na rasilimali zake na pia ameitaka serikali ifanyie kazi haswa uchumi wa vijijini kwa kurekebisha mapungufu yote yanayoshusha uzalishaji kwenye sekta ya kilimo.

Rais Museveni amvika nishani ya heshima Aga Khan

$
0
0
Rais Yoweri Museveni amemvisha Mtukufu Prince Karim Aga Khan IV nishani ya juu ya heshima barani Afrika (Most Excellent Order of Pearl of Africa, The Grandmaster) ili kutambua miongo kadhaa ya mchango wake katika maendeleo ya Uganda.

Museveni alimvisha nishani hiyo Jumatatu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bushenyi-Ishaka katika wilaya ya Bushenyi.

Mtukufu Aga Khan, ambaye ni Imam wa madhehebu ya Ismailia, kupitia taasisi ya Aga Khan ana miradi mingi ya maendeleo katika nyanja za elimu, nishati, afya, hoteli na utalii, vyombo vya habari.

Aga Khan aliwasili nchini Uganda Jumapili kuwahi maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru na alikuwa na kikao na Rais Museveni pamoja na maofisa waandamizi wa serikali katika Ikulu ya Entebbe.

Mapema wakati wa utoaji taarifa kwa waandishi wa habari katika Kituo cha Habari Uganda, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Esther Mbayo alidokeza sababu za kumtunukia nishani hiyo ya heshima Aga Khan.

“Atatunukiwa nishani ya heshima ya juu kwa sababu ya mchango wake mkubwa wa kiuchumi alioutoa kwa nchi yetu duniani kwa ujumla,” alisema Mbayo.

Walionusurika Ajali Ziwa Victoria Wamtupia Lawama Dereva

$
0
0
Walionusurika ajali ya daladala iliyotumbukia Ziwa Victoria, wamesema iwapo dereva angesikiliza ushauri madhara yasingekuwa makubwa.

Akizungumza katika Hospitali ya Bukumbi Mission wilayani Misungwi alikolazwa, Yohana Ngabula (28) mkazi wa Kijiji cha Buyagu wilayani Sengerema amesema amepoteza mama na dada katika ajali hiyo.

Ngabula amesema walikuwa wakitoka jijini Mwanza kufuatilia mafao ya baba yao katika ofisi za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

“Nilimshauri dereva agonge hata gari lililokuwa mbele yake badala ya kulielekeza ziwani lakini hakusikia mwisho wake ndiyo hayo yaliyotokea,” amesema.

Amesema baada ya gari kutumbukia ziwani alipasua kioo na kutoka ndipo walipofika vijana wakamuokoa.

Majeruhi mwingine mkazi wa Ibisabageni, Paulo Lazaro ambaye ni mwalimu wilayani Sengerema amesema, “Tulimshauri dereva agonge vitu nchi kavu kuliko kuipeleka gari majini lakini hakusikiliza ushauri wetu, pengine tungepona wengi zaidi.”

Mwalimu huyo amesema alipita dirishani baada ya gari kutumbukia ziwani na kwamba, ana maumivu mabegani na mgongoni.

Mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo, Sophia Biambina (32) amesema amepoteza watoto wawili katika ajali hiyo.

Amesema walikuwa wakitoka kwenye msiba wa baba yake wilayani Magu na alikuwa akielekea nyumbani kwake Nyapande wilayani Sengerema.

“Baada ya ajali nilijikuta nimeshatoka nje sikujua nimetokaje, najihisi maumivu makali kwa sababu nilikunywa maji mengi. Kinachoniuma ni kuwapoteza watoto wangu, tulitoka msibani kumzika baba yangu,” amesema.

Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Bukumbi, Dk Robert Shija amesema walipokea maiti 12 na majeruhi hao watatu.

Amesema walipokea miili ya Joseph Paulo, Rehema Makalanga, Mariamu Kagosha, Pendo Msafiri, Salome Msafiri, Joyce Hamadi, Martha Makenzi, Gwanchele Mswagi na Kazungu Lukuba wote wakazi wa Wilaya ya Sengerema.

Wengine ni Martine Kamlamo mkazi wa Bukumbi, Hamadi Zahalaki wa Bukoba na Ally Abdul wa Kayenze wilayani Ilemela.

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda ameuagiza uongozi wa hospitali kuwa, ndugu watakaoshindwa kusafirisha miili wawasiliane na ofisi ya wilaya kwa ajili ya kupata msaada.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amesema walipanga kuisafirisha miili hiyo lakini tayari ndugu wameshaichukua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema hakuna miili mingine ambayo imeopolewa lakini Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kimerudi eneo la tukio.

Msangi alisema jana Jumatatu kuwa hawajapata idadi kamili ya watu waliokuwemo kwenye gari hilo.

Tamko la Wizara ya Afya katika Siku ya Afya ya Akili leo Oktoba 10

$
0
0
TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE. UMMY MWALIMU (MB) KUHUSU SIKU YA AFYA YA AKILI DUNIANI TAREHE 10 OKTOBA 2017

Ndugu Wananchi,
Siku ya Afya ya Akili Duniani, huadhimishwa duniani kote kila mwaka tarehe 10 ya Mwezi Oktoba.
 
Kaulimbiu  ya  Maadhimisho ya  Siku ya  Afya ya Akili Duniani mwaka 2017 ni “Afya ya Akili Mahali pa Kazi” Kauli mbiu hii  inalenga kuhamasisha Waajiri na watunga sera namna bora ya kuhusisha Afya ya Akili katika ngazi mbalimbali za kutengeneza miongozo ya kisera na kuifanya afya bora ya akili kuwa ni sehemu ya ustawi wa wafanyakazi.
 
Ndugu Wananchi,
Tanzania kama ilivyo nchi zingine wanachama wa shirika la Afya Duniani wanaadhimisha siku hii, ambapo Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeandaa shughuli mbalimbali za kutoa elimu kuhusu umuhimu wa afya ya akili  mahali pa kazi na kuwafanya waajiri na wafanyakazi kutambua umuhimu wa afya bora ya kiakili na  huduma za  afya ya akili.
 
Ndugu Wananchi,
Tunapozungumzia afya tunamaanisha hali ya ustawi wa mwanadamu kimwili, kiakili na kijamii. Mtu mwenye afya njema ya akili anaaminika kwa kutengemaa katika namna anavyofikiri, anavyohisi, na anavyotambua mambo, ambayo kwa pamoja hujionyesha katika matendo yake ya kila siku ikiwa ni pamoja na jinsi anavyohusiana na kushirikiana na wenzake katika familia na jamii  na mahali pa kazi kwa ujumla.
 
Magonjwa ya akili ni magonjwa ambayo yanaathiri au yanapelekea mabadiliko katika kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda, na hivyo kuwa na mabadiliko ya kitabia au mwenendo uliotofauti au usioendana na jamii husika kiimani, kimila, desturi, na nyanja nyingine za kijamii. Tabia hizo zinatokana na ugonjwa wa akili kuathiri ufanisi na shughuli za mtu husika (mgonjwa) pamoja na kuathiri uhusiano wake katika jamii na hivyo huathiri jamii nzima inayomzunguka.
 
Visababishi vya magonjwa ya akili vimegawanyika katika sababu za kibaolojia, kisaikolojia na kijamii na mjumuiko  wa visababishi hivi ndivyo vinavyopelekea mtu kuwa na dalili  za ugonjwa wa akili.
 
Ndugu Wananchi,
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha kuwa kati ya watu wazima wanne mmoja kati yao alishapata au alishaona mtu mwenye matatizo ya kiakili, ambayo hutokana na mila na desturi zilizopitwa na wakati, unyanyasaji, unyanyapaa na kutengwa au kubaguliwa kwa namna yeyote.
 
Hali kadhalika hata katika nchi yetu tumekuwa tukikabiliwa na matatizo kama hayo ya mila na desturi zisizo rafiki, unyanyapaa na ubaguzi ambao unasababisha pia ufinyu wa bajeti, uhaba wa wataalamu katika vituo vya kutolea huduma, uhaba wa vifaa tiba na dawa kwa wagonjwa wenye matatizo ya kiakili, kijamii na kisaikolojia. 

Tunapaswa kukumbuka kuwa hakuna afya njema ya kimwili kama hakuna afya ya akili; na pia nchi yetu ikiwa na wafanyakazi wenye afya bora ya akili ni hazina kubwa kwa Taifa letu.
 
Ndugu Wananchi,
Katika kukabiliana na ukweli huu jitihada mbalimbali zimefanywa za kutoa huduma za afya ya akili ikiwa ni pamoja na kutengeza Mwongozo wa kisera wa afya ya akili ya mwaka, 2006 na Sheria ya Afya ya Akili ya mwaka 2008 ambavyo unatoa mwongozo wa namna ya kutoa huduma. 

Aidha, serikali inaendelea kuhamasisha waajiri kuwekea mkazo mambo mbalimbali ya kuimarisha huduma za afya ya akili katika mipango yao, na kuhakikisha kila Mkoa unaimarisha huduma hizi katika ngazi ya Mikoa yote Tanzania Bara.
 
Vilevile serikali inaendelea kuwajengea uwezo watoa huduma za afya ya akili nchini ili waweze kutambua na kubaini mapema dalili za magonjwa ya akili na kutoa matibabu stahiki au rufaa kwa wakati muafaka. 

Pia, tumeimarisha matibabu ya magonjwa ya akili na saikolojia katika hospitali za mikoa na rufaa hii ikiwa ni pamoja na kupeleka wataalamu wa afya ya akili wakiwepo madaktari bingwa na wauguzi bingwa ili kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje na wale wa ndani/ waliolazwa.
 
Ndugu Wananchi,
Watu wengi wamekuwa na uelewa mdogo kuhusu magonjwa ya akili, na kufikia hatua ya kuhusisha na laana, kurogwa, kuwa na mapepo au kutupiwa majini; Magonjwa ya akili ni magonjwa kama yalivyo mengine na yanaweza kumtokea mtu yeyote wa rika lolote na muda wowote, hivyo basi wananchi, wanafamilia na jamii kwa ujumla tunapaswa kujua na kutambua dalili za magonjwa ya akili na kuwasaidia kupata matibabu, kupunguza unyanyasaji, unyanyapaa na kuwatenga wagonjwa wa akili. Taarifa ya afya na magonjwa ya akili ya mwaka 2015/16 inaonyesha kuwa takribani wagonjwa 611,789 wameweza kuhudhuria kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya nchini.
 
Katika kukabiliana na wimbi la ugonjwa wa Afya ya akili wataalamu na waajiri wataendelea kuelimisha jamii juu ya magonjwa ya akili na kupinga vitendo vya unyanyasaji, unyanyapaa na kuwatenga wagonjwa hivyo, kuwawezesha kufikishwa maeneo ya utolewaji wa huduma na tiba mapema ili wasaidiwe kama walivyo wagonjwa wengine.
 
Ndugu Wananchi,
Dhamira kuu ya maadhimisho ya mwaka huu 2017, ni kuhakikisha afya ya akili inakuwa sehemu ya agenda kila mwaka mahali pa kazi na kwamba waajiri na waajiriwa waweze kuweka mikakati/mipango ambayo itazuia/ itapunguza au kuondoa visababishi vya magonjwa ya akili na uwezeshaji wa utambuzi wa mapema kwa walio na dalili za magonjwa ya akili na hivyo kupatiwa tiba.
 
Aidha, dhamira pia inalenga kuhakikisha kuwa mahali pa kazi ni mahala salama na pasipokuwa na visababishi/vichochea/vihatarishi vinavyopelekea waajiri na waajiriwa kupata dalili za magonjwa ya akili kwa sababu ndio sehemu ambayo mwajiriwa/waajiriwa wanakaa muda mrefu kuliko muda wa majumbani.
 
Vilevile, dhamira inalenga  kuongeza thamani, heshima na utu wa mgonjwa wa akili, kuzifanya  huduma za afya ya akili kama sehemu muhimu ya huduma ya mwili wa binadamu, kupunguza unyanyapaa, kutengwa na kunyanyaswa, kuifanya jamii kuongeza uelewa na kutambua magonjwa ya akili kama magonjwa mengine na hivyo kuyapa kipaumbele.
 
Ndugu Wananchi,
Serikali imeendelea na utekelezaji wa Sera ya Afya ya mwaka (2007) ambayo inalenga kutoa huduma bila malipo kwa wagonjwa wa akili na magonjwa mengine yasiyoambukiza.
 
Aidha Sera ya Mwongozo wa Huduma za Afya ya Akili inasisitiza utoaji wa huduma za Afya ya Akili bila malipo.  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kutambua uwepo wa maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili duniani kama sehemu ya uhamasishaji kwa jamii kama ilivyo kwenye nchi zote duniani.
 
Ndugu Wananchi,
Ili kuboresha hali ya afya ya akili Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kwamba: – inaongeza uelewa wa jamii kuhusu visababishi, dalili na huduma zinazohusiana na afya na magonjwa ya akili ikiwemo:
  • Watumishi wa afya wanapatiwa mafunzo maalum ya namna ya kuchujua/kuchunguza dalili za magonjwa ya akili na kutoa huduma stahiki kwa wagonjwa wa akili.
  • Kufanya tafiti mbalimbali zinazosaidia kuboresha huduma za kuzuia na kudhibiti magonjwa ya akili katika jamii.

Raila Odinga ajiondoa kwenye uchaguzi mkuu wa marudio Kenya

$
0
0
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kuwa hatashiriki kwenye uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.
 
Bwana Odinga anasema anataka kufanyika uchaguzi mpya jinsi ilivyoamuliwa na mahakama ya juu.

Uchaguzi huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Bw. Odinga anasema amejiondoa ili kuipa tume ya uchaguzi IEBC muda wa kutosha kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha kufanyika uchaguzi kwa njia nzuri.

Awali tume ya uchaguzi ilikuwa imemtangaza rais wa sasa Uhuru Kenyatta kuwa mshindi.Ilisema kuwa Bw. Kenyatta alishinda uchaguzi huo kwa kura milioni 1.4.

Upinzani nchini Kenya awali ulikuwa umetangaza wazi kuwa ungeshiriki kwenye uchaguzi mkuu ikiwa mabadiliko yanayostahili yangefanyika.

Upinzani unaamini kuwa uchaguzi unastahili kufutwa baada ya Odinga kujiondoa, na kutoa muda wa kutosha kufanyika mabadiliko yanayostahili ili uchaguzi kufanyika kuambatana na sheria na katiba.

Serikali imekuwa ikisema kuwa uchaguzi utafanyika na rais kuapishwa.Bw. Odinga pia ametoa wito kwa watu kuandamana  Jumatano hii kwa kutumia kauli mbiu "hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi".

Mwezi Septemba mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya Keriako Tobiko, aliamrisha polisi na tume ya kupambana na ufisadi kuchunguza ikiwa wanachama wa tume ya uchaguzi walihusika na uhalifu wowote.

Alitaka wachunguzi kuchunguza madai kuwa maafisa wawili wakuu wa upinzani walikuwa wamedukua mitandao ya tume ya uchaguzi.

Waziri Kairuki Aelezea Vipaumbele Vyake Wizara ya Madini

$
0
0
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ameeleza vipaumbele  vyake katika Wizara kuwa ni pamoja na  udhibiti wa utoroshaji wa madini nchini, maslahi kwa wafanyakazi huku akiwataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu.

Kairuki ameyasema hayo jana tarehe 10 Oktoba, 2017 jijini Dar es Salaam  alipozungumza na  watumishi wa Wizara ya Madini pamoja na taasisi zake, waliopo Dar es Salaam na Makao Makuu  ya Wizara Dodoma. 

Lengo La kikao hicho lilikuwa ni kufahamiana na kupanga mikakati  ya kushirikiana ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa Uchumi wa nchi.

Taasisi zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na  Wakala wa Jiolojia  Tanzania (GST), Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO), Chuo cha Madini Dodoma (MRI) pamoja na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini na Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji (TEITI).

Alisema kuwa Sekta ya Madini  inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwataka wataalam wa madini kubuni mbinu za ukusanyaji wa maduhuli pamoja na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye uchimbaji madini.

Katika hatua nyingine aliwataka wataalam hao kubuni mikakati  ya kuzuia utoroshaji wa madini nchini ili nchi ipate mapato stahiki.

Aliwataka watumishi kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuwa wabunifu ili  sekta hiyo iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Naye Naibu  Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo aliwakumbusha  watumishi kuzingatia Dira na Dhima ya Wizara  ikiwemo kufanya kazi kwa tija ili hatimaye  sekta ya madini iweze kuchangia katika uchumi wa nchi kwa kuwa mchango wa sekta husika bado ni kidogo.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH....Anatoa Pete za Bahati, Anasafisha Nyota, Anazuia Chuma Ulete na Mengine

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH CHIEF SULTAN MAKATA Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
 
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Chief Sultan Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
 
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Chief Sultan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
 
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. 

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp/Calls 0658316976
0755911233
 
Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote

Kesi Ya Msukuma Na Madiwani Nane Yapigwa Tarehe

$
0
0
Kesi inayomkabili Mbunge wa Geita na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Mkoani Geita Joseph Kasheku Msukuma na madiwani nane imesogezwa mbele baada ya upande wa mashitaka kudai upelelezi haujakamilika.

Kesi hiyo ambayo ilikuwa isikilizwe jana imepangwa kutajwa tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu ambapo washitakiwa wote wapo nje kwa dhamana.

Kwa upande wake wakili anayewatetea washitakiwa Bw Deo Mgengeli alielezea hatua ambayo imeendelea siku ya jana  mahakamani hapo kuwa shauri limekuja na kwamba limetajwa na hadi sasa hakuna mshitakiwa ambaye ameongezeka hivyo mahakama imeamua tarehe Kumi mwezi wa 11 wawasili mahakamani kusikiliza tena kesi hiyo.

Aidha wakili Mgengeli alizungumzia suala la madiwani wengine waliokamatwa na jeshi la polisi na kutofikishwa mahakamani  akasema kuwa kukamatwa  kwa madiwani hao  ni jambo la kawaida  kwani ni swala la upepelezi kwa makosa ya jinai na kwamba alhamisi wanatakiwa kwenda tena polisi ili kujua ni kipi ambacho kinaendelea ila hadi sasa hawana kosa lolote.

 Awali washitakiwa hao kwa pamoja walifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita Septemba 19 mwaka huu

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka ya kufanya mkutano bila kibali, kuziba barabara na uharibifu wa bomba la maji linaloelekea kwenye mgodi wa dhahabu wa GGM.

Uhuru Kenyatta Amvaa Raila Odinga

$
0
0
Rais Uhuru Kenyatta amemjia juu Kiongozi wa NASA Raila Odinga baada ya kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini Kenya na kusema hata kama amejitoa Katiba ya Kenya haijazuia uchaguzi kutofanyika

Kenyatta amesema kuwa Odinga alitaka uchaguzi urudiwe jambo ambalo limeigharimu nchi ya Kenya fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara, zingeweza kutumika kujenga mahospitali na kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi, lakini anashangaa mtu ambaye ametaka uchaguzi kurudiwa anajiengua tena.

"Rafiki yangu nasikia sasa umesema umejitoa baada ya kutupeleka peleka zaidi ya shilingi bilioni 12 hivi sasa zinatumika ili tufanye uchaguzi, pesa ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara, zingetumika kujenga hospitali ya wananchi sasa zinatumika kwa uchaguzi ambao yeye ndiye aliitisha na sasa anasema hataki, kuna haki hapa jamanii, si mahakama ilisema IEBC haina makosa hayo masharti yote unatoa lakini tume hii si ndiyo imefanya viongozi hawa wengine wote kupatikana" alihoji Kenyatta

Mbali na hilo Kenyatta amesema kuwa wao wataendelea na mchakato wa uchaguzi kama kawaida na kusema huenda awepo au asiwepo Odinga uchaguzi utafanyika kama kawaida kama ambavyo tume ya uchaguzi ilitangaza.

Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu mifupa ya Binadamu iliyokutwa kwenye bwawa mkoani Shinyanga

$
0
0
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule amethibitisha kuokotwa kwa viungo vya mwili wa binadamu katika bwawa la maji la Jomu wakati watu wakitafuta maji huko Tinde mkoani Shinyanga.

Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule alidai kuwa iku ya Jumatatu  watu walipoona viungo hivyo vya binadamu ilibidi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi na wao walifika na kukuta viungo hivyo.

"Fuvu la kichwa limepatikana hapo bwawani, taya ya binadamu, mbavu za binadamu kumi na nne.

"Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo jeshi la polisi lilichukua hatua za haraka kufika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa awali tukishirikiana na daktari mtaalam wa viungo vya binadamu 

"Katika tukio hilo tulikuta viungo hivyo ikiwa pamoja na mfupa mmoja wa sehemu ya paja, mifupa ya mikono na mifupa ya sehemu ya bega ya binadamu" alisema Simon Haule

Aidha Kamanda Haule alisema kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ikiwa pamoja na kufungasha mifupa yote na kupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kufanya vipimo kubaini vinasaba na jinsia ya mtu ambaye amefariki.

==>Msikilize kamanda akiongea hapo chini

CHADEMA yapata pigo lingine Iringa

$
0
0
Chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa kimeendelea kujiimarisha kwa kuvuna wanachama watano kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Iringa wakiwa na mikakati ya kuja kulikomboa jimbo la Iringa mjini ambalo lipo chini ya chama cha CHADEMA.

Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama hao kutoka kata ya kitwiru mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya aliwapongeza wanachama kwa kutambua kazi inayofanywa na chama cha mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano DR John Pombe Magufuli.

“Mimi nimefurahi sana nyie kurudi nyumbani maana mtakuwa na msaada mkubwa sana katika kukijenga chama hapa manispaa ya Iringa ili tuweze kulikomboa jimbo hili katika uchaguzi ujao na hii ndio mikakati yetu” alisema Rubeya.

Rubeya aliwaambia wanachama hao kuwa sasa wapo katika mikono salama ya kisiasa tofauti na walipokuwa kwenye chama cha awali na kuwasihi wasiwe waoga katika kufanya kazi za kukijenga chama cha mapinduzi.

“CCM ndio chama tawala hivyo ondoeni hofu na mzidi kutupa maarifa mliyotoka nayo huko na kukisaidia chama hiki kuzidi kupata wananchama wengi kutoka vyama vya upinzani na mkiwa CCM mtapikwa vizuri na kuwa viongozi wazuri” alisema Rubeya.

Aidha Rubeya aliwaambia kuwa CCM hutoa madaraka kwa mtu yeyote yule mwenye weledi katika nafasi aliyogombea, hivyo huku hakuna kuteuana huku kuna nafasi za kugombea na kuchaguliwa na wanachama wa chama cha mapinduzi tofati na kule mlikokuwa mnateuna kwa maslai ya mtu mmoja.

Naye katibu wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa Marko Mbaga aliwataja wanachama waliohamia chama hicho kutoka CHADEMA ni Baraka Kimata aliyekuwa katibu mwenezi na Diwani wa kata ya Kitwiru,Theodora Mbata aliyekuwa matroni wa wanawake kata ya Kitwiru, Erick Muyungo na  Raymond kimata aliyekuwa kiongozi wa redbrigad manispaa ya Iringa na katibu mwenezi wa kata ya kitwiru.

“Hii ni mwanzo tu watakuja wengi mno kwa kuwa CCM manispaa ya Iringa wanachapa kazi hata kama halmashauri ipo kwa wapinzania lakini wao wataendelea kufanya kazi kwa kutekeleza ilani ya chama chetu ili kuwamaliza wapinzani wetu wote warudi kwenye chama tawala” alisema Mbaga

Edwin bashir ni katibu wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa alisema kuwa sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa wananchi na wananchi waendelee kuwa na Imani na chama cha mapinduzi ili waje kufanikiwa kulikomboa hili jimbo ambao lipo upinzani.

“Mimi najua vijana wengi muda sio mrefu wataanza kurudi nyumbani kwao kwenye chama wananchokipenda na kuondokana na siasa za maji taka kwa kuwa CCM ni tanuli za kuwahoka viongozi bora na sasa manispaa tutafanya kazi kweli kweli na kuwamaliza wapinzani kwa nguvu zote” alisema Bashir.

Baraka Kimata,Theodora Mbata, Erick Muyungo na  Raymond kimata walisema kuwa watakitumikia ipasavyo chama cha mapinduzi kama walivyokuwa wanakitumika chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na kuhakikisha CCM wanashinda chaguzi zote watakazo kuwa wanashiriki katika manispaa ya iringa.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati aliwapongeza viongozi wote wapya waliochaguliwa hivi karibuni na kuanza kufanya kazi inayoonekana machoni mwa wakazi wa manispaa hiyo.

“Juzi mmechaguliwa lakini kazi imeanza kwa kuwapata wananchama wapya wanaotoka upinzani kurudi CCM hiyo sio kazi ndogo kwa kweli hiyo ni kazi kubwa sana ambayo mmeanza nao nichukue nafasi hii kuwapongeza kwa mnachokifanya kuhakikisha tunapata wanachama wengi kutoka upinzani” alisema Kabati.

18 Watiwa Mbaroni kwa Mauaji

$
0
0
Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya mkoani Mara, linawashikilia watu 18 kwa tuhuma za mauaji baada ya kumshambulia kisha kumchoma mishale yenye sumu mkazi mmoja wa kitongoji cha Mwara Bw. Magige Mesenda na kusababisha kifo chake.

Kamanda wa Polisi Kanda ya Tarime na Rorya, SACP Henry Mwaibambe, amesema kuwa kikundi hicho kimekuwa kikijihusisha na mauaji ya watu mbalimbali kimekamatwa kikiwa na silaha za jadi ambazo zimekuwa zikitumika kufanya vitendo hivyo vya mauaji.

Mke wa Sheikh Jumuiya ya Uamsho Ambaye mumewe yuko Mahabusu AJINYONGA

$
0
0
Mke wa Sheikh Suleiman Othman mmoja wa wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho wanaoshikiliwa mahabusu Tanzania Bara amejiua kwa kujinyonga.

Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja imesema Rahma Mussa Koki (28) alijiua kwa kujinyonga Jumapili

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hasina Ramadhan Taufiq amesema watu watano wamehojiwa wakiwemo wazazi wake kuhusu tukio hilo.

Amesema katika mahojiano bado hawajatambua sababu za mwanamke huyo kujinyonga.

“Katika hatua za awali tumesikia alianza kuugua maradhi ya akili na huenda yakawa chanzo cha yeye kuijua,” amesema Taufiq.

Amesema licha ya watu hao kuhojiwa, hakuna wanayemshikilia.

Kamanda Taufiq amesema kazi ya Jeshi hilo ni kuhakikisha wanaendelea na upelelezi na utakapokamilika watatoa taarifa.

Wakati huohuo, Safia Kombo Sheha, mama mzazi wa Rahma amesema kabla ya kifo chake alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili na alipatiwa matibabu mara kadhaa.

“Kabla ya kifo chake kama wiki nzima alikuwa akisema nitajinyonga nasi tukawa karibu naye kila wakati kwa kujua ni
mgonjwa. Jumapili asubuhi tulikuwa pamoja ila niliondoka kidogo. Niliporudi nilikuta mlango wa chumbani kwake umefungwa, tulipouvunja tulikuta akiwa amejinyoka kwa kutumia kamba,” amesema.

Safia amesema baada ya ndugu na majirani kufika walibaini alishafariki. Tukio hilo amesema lilitokea saa nne asubuhi, eneo la Kigunda, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Rahma ameacha watoto watatu, wawili wakiwa wa kike.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images