Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ester Bulaya: Ninafuatiliwa na watu waliovaa mavazi ya kininja

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Ester Amos Bulaya, amesema kuwa yupo katika hatari kubwa kutokana na kufuatiliwa na watu waliovalia mavazi ya kininja nyumbani kwake wilayani Bunda.

Bulaya ametoa taarifa hiyo alipokuwa leo  na kusema kwamba watu hao walimfuata nyumbani kwake wakiwa na gari aina ya Noah huku wamevaa kininja.

Aidha, amesema kuwa kwa bahati nzuri wakati watu hao wakienda kwake hakuwepo nyumbani, hivyo ndugu zake wakampigia simu ili asirudi nyumbani siku hiyo aweze kuokoa usalama wake..

Hata hivyo, ameongeza kuwa watu hao waliokuwa wakimtafuta walizunguka kwa baadhi ya ndugu zake akiwemo bibi yake na kumkosa, lakini alienda kutoa taarifa polisi na mkuu wa kituo kuanza kufuatilia suala hilo, lakini haikuchukua muda akahamishwa kituo cha kazi.

Prof. Lipumba na wenzake wagonga mwamba mahakamani

$
0
0
Mahakama Kuu imekataa pingamizi lililowasilishwa na Mwanasheria wa Serikali dhidi ya maombi ya kuizuia kufanya kazi Bodi ya Wadhamini wa CUF, kambi ya mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Uamuzi huo ulitolewa jana  Alhamisi na Jaji Wilfred Dyansobera aliyetupilia mbali hoja za pingamizi zilizotolewa na wajibu maombi wakipinga maombi yaliyofunguliwa na Mbunge wa Malindi(CUF), Zanzibar, Ally Saleh.

Kutokana na uamuzi huo, Mahakama itaanza kusikiliza maombi ya mbunge huyo anayeomba zuio dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa CUF ambayo wajumbe wake waliteuliwa na Profesa Lipumba.

Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa mawakili wa CUF, Juma Nassoro kwa upande wa katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif alisema Jaji Dyansobera ameamuru usikilizwaji ufanyike kwa njia ya maandishi.

Nassoro amesema muombaji ametakiwa kuwasilisha hoja zake Oktoba 19 na wajibu maombi wametakiwa wawe wamezijibu ifikapo Oktoba 27.

Amesema Jaji Dyansobera ameelekeza iwapo muombaji atakuwa na hoja za nyongeza awe ameziwasilisha ifikapo Novemba 4 na shauri litatajwa Novemba 6.

Mbunge Saleh alifungua maombi hayo kutokana na kesi ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo akipinga uhalali wa wajumbe wa bodi walioteuliwa na Profesa Lipumba.

Anaiomba Mahakama itoe amri ya zuio la muda dhidi ya wadaiwa, wakala wao na watu wote wanaofanya kazi kwa maagizo yao kutokujihusisha kwa namna yoyote na masuala ya chama hicho mpaka uamuzi wa shauri lake la msingi utakapotolewa.

Wajibu maombi ni Ofisa Mtendaji wa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita), aliyewakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wengine ni Bodi ya Wadhamini ya chama hicho, mwenyekiti wa bodi hiyo, Peter Malebo na wajumbe wa bodi hiyo.

Aga Khan kutua nchini kwa mwaliko wa Rais Magufuli

$
0
0
Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani, Mtukufu Aga Khan anatarajia kutembelea Tanzania Oktoba 11 na 12 kwa mwaliko wa Rais John Magufuli.

Mtukufu Aga Khan atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa nne asubuhi akitokea Uganda atakakokwenda kuhudhuria sherehe za uhuru wa nchi hiyo kwa mwaliko wa Rais Yoweri Museveni.

Akizungumzia ziara hiyo leo Ijumaa, Ofisa Mawasiliano wa Baraza la Aga Khan, Shelmina Shivji amesema ziara hiyo itafungua fursa katika sekta mbalimbali na kukuza uchumi wa Taifa.

Amesema mwaliko huo wa Rais Magufuli unaonyesha uhusiano mzuri kati ya Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) na Serikali ya Tanzania.

"Mtukufu Aga Khan amekubali mwaliko wa Rais Magufuli na katika ziara yake ya siku mbili nchini atakuwa na mazungumzo na Rais na kukutana na watendaji wa AKDN," amesema.

Shivji amesema Mtukufu Aga Khan ni mwekezaji mkubwa nchini katika sekta za afya, elimu, kilimo na maendeleo ya jamii.

Mratibu wa mawasiliano ya jamii ya Ismailia, Khan Ramji amesema maandalizi ya mapokezi ya kiongozi huyo yanaendelea vizuri kwa upande wa Serikali na Jumuiya ya Ismailia.

"Wananchi wajitokeze kwa wingi uwanja wa ndege wa JNIA kumpokea Mtukufu Aga Khan ambaye anatarajiwa kufika saa nne  asubuhi," amesema Ramji.

Julai 11, Jumuiya ya Waismailia nchini iliungana na wenzao duniani kuadhimisha miaka 60 ya uongozi wa Aga Khan ambaye ni Imamu wa 49 wa jumuiya hiyo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamoi ya October 7

Polepole: Magufuli Hakuwa na Nafasi Yoyote CCM, Lakini Kafanya Mageuzi Makubwa

$
0
0
Humphrey Polepole amefunguka na kusema Rais Magufuli hakuwahi kuwa na nafasi ya uongozi ndani ya Chama hicho na kudai ndiye alikuwa mtu sahihi 2015 kwani alipoingia ndani ya chama na serikali ameweza kuona matatizo ambayo wengine hawakuweza kuyaona.

Polepole amesema kuwa kwa jinsi ambavyo chama hicho kilivyokuwa kipindi cha nyuma kilihitaji mtu ambaye hayupo ndani ya mfumo wake ili aweze kuona mapungufu mbalimbali ndani ya chama na serikali.

"Ndugu Magufuli kama Mwenyekiti ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekuwa ni kiongozi wa kawaida na duniani kote unaposoma elimu ya mageuzi huwa inataka upate mtu ambaye ni wa kawaida labda huenda asiyetoka katika eneo ambalo linafanyiwa mageuzi ili aweze kuwa na jicho la nje, kwa sababu gani wewe unayekaa ndani unaona kama mambo yako sawa hivi, sasa ndugu Magufuli ndani ya CCM hajawahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu, hajawahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, hajawahi kuwa Mjumbe wa Sekretarieti sasa CCM ilipotafakari ni nani atakayeweza kufanya mageuzi makubwa ndani ya chama hivyo hakukuwa na mtu mwingine zaidi ya John Pombe Magufuli" alisema Polepole

Aidha Polepole amesema kuwa Rais Magufuli alipoingia serikalini na ndani ya Chama Cha Mapinduzi hakuona haya kusema madudu na uozo uliopo ndani yake

"Magufuli hajaona haya kusema kwanini dhahabu inaondoka mnaitazama, Kwanini hii Almasi inakwenda na kwanini tunashindwa kuichakata hapa, kwanini bandarini mnaruhusu mizigo inaingia bila kulipa kodi, na nyinyi CCM kwanini mali zenu zinahodhiwa na watu na fedha haziji kwenye chama, hii yote ni kwa sababu anajicho la nje ambaye anaona tofauti na nyinyi mliopo ndani ya ambao mshazoe" alisema Polepole

Mbali na hilo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa anapomsikia Rais Magufuli akisema kuwa nafasi ya Urais ni kazi ngumu anamuelewa kweli na kusema kuwa yeye anajua uongozi si kazi ya furaha bali ni mzigo mkubwa.

Breaking News: Rais Magufuli Atangaza Baraza Jipya la Mawaziri

$
0
0

Rais John Magufuli ametangaza baraza jipya la mawaziri lililoongezeka kutoka wizara 19 hadi 21.

Wizara hizo zimeongezeka kutokana na wizara mbili kugawanywa huku nafasi za manaibu wapya zikiwa tano.

Akitangaza leo Jumamosi baraza hili jipya, Rais Magufuli amesema Wizara ya Nishati na Madini imegawanywa mara mbili, sasa kutakuwa na Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.

Amesema hatua hiyo inatokana na umuhimu wa rasilimali hiyo kwa taifa na kwamba wizara hizo zote kila moja itakuwa na waziri na naibu wake.

Rais Magufuli ametaja mabadiliko mengine katika Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambayo kwa sasa kutakuwa na Wizara ya Kilimo inayojitegemea na nyingine itakuwa ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Amesema sababu za kufanya mabadiliko hayo ni kutokana na umuhimu wa sekta hiyo inayoajiri asilimia 75 ya Watanzania nchini hivyo ni vyema ijitegemee. Kila wizara itakuwa na waziri na naibu wake.

Mabadiliko mengine ni katika wizara ya Tamisemi baada ya kuweka nafasi mbili za manaibu waziri kwa sababu ni wizara inayogusa sehemu kubwa ya wananchi.

Pia yamefanyika katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Angalia orodha ya mawaziri hao hapa

1.Wizara ya Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora.

Waziri – George Huruma Mkuchik

2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira

Waziri – January Makamba

Naibu Waziri - Kangi Lugola

3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu

Waziri – Jenista Mhagama

Naibu Waziri – Anthony Peter Mavunde

Naibu Waziri Walemavu – Stela Alex Likupa

4.Wizara ya Kilimo

Waziri - Charles John Tizeba

Naibu Waziri - Mary Mwanjelwa

5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Waziri - Makame Mbarawa

Naibu Waziri - Atashasta Nditiye

Naibu Wziri - Elias John Kwandikwa

6.Wizara ya Fedha na Mipango

Waziri - Dr Philip Mpango

Naibu Waziri - Dr Ashatu Kijaji

7.Wizara ya Nishati

Waziri - Medrad Matogoro Kalemani

Naibu Waziri - Subira Hamisi Mgalu

8. Wizara ya Madini

Wairi - Angela Kairuki

Naibu Waziri - Haroon Nyongo

9. Wizara ya Katiba na Sheria

Waziri – Palamagamba Kabudi

10. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Waziri - Agustino Mahiga

Naibu Waziri - Dkt Susan Kolimba

11 .Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Waziri - Dr Hussein Mwinyi

12. Wizara ya Mambo ya Ndani

Waziri – Mwigulu Nchemba

Naibu Waziri - Hamad Masauni

13. Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Waziri - William Lukuvi

Naibu Waziri - Angelina Mabula

14. Wizara ya Maliasili na Utalii

Waziri – Hamisi Kigwangala

Naibu Waziri - Ngailonga Josephat

15. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Waziri - Charles Mwijage

Naibu Waziri - Stella Manyanya

16. Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi

Waziri - Joyce Ndalichako

Naibu Waziri - William Ole Nasha

17 .Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Waziri – Ummy Mwalimu

Naibu Waziri – Faustine Ndugulile

18. Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo

Waziri - Dr . Harrison Mwakyembe

Naibu Waziri - Juliana Shonza

19. Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Waziri - Isack Kamwelwe

Naibu Waziri - .Juma Hamidu Aweso

20. Mifugo na Uvuvi

Waziri - Luhaga Mpina

Naibu Waziri - Abdallah Ulega

21. Wizara ya TAMISEMI

Waziri – Suleiman Japho

Hawa ndo Mawaziri Wanne Waliotemwa Baraza Jipya la Mawaziri

$
0
0
Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri kwa kuwatema mawaziri wanne waliokuwepo kwenye baraza la awali.

Mawaziri walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.

Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi,  Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.

Panga hilo limempitia pia aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye ametupwa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri tangu aingie madarakani.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Octoba 8


Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Gazi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Tatizo la Nguvu za Kiume na Chanzo cha Kuwa na Maumbile Madogo

$
0
0
Wataalam katika chuo kikuu cha tiba johns hopkins wanakili kuwa asilimia 75% ya wanaume duniani wamepatwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Tatizo hili linasababishwa na kushuka kwa TESTOSTERON kwenye damu ,kawaida testosteron kwenye damu inatakiwa iwe 400ng/d/hadi 900ng/d/.....chini ya 400ng/d/ mwanaume anapatwa na upungufu wa nguvu za kiume (erectile disfunctioning) kupungua maumbile ya kiume kwa kawaida anatakiwa kutumia dk 20_30 ndipo amalize na umbile lake liwe si chini ya nchi 7.5 .

Sababu zinazoweza kushusha testosterone homoni ya nguvu za kiume ni PUNYETO,SUKARI,BP,MAGONJWA YA FIGO,TUMBO LA CHANGO,ULEVI KUPITA KIASI,MAGONJWA YA ZINAA,U.T.I,KUTOKWA NYAMA SEHEMU ZA HAJA KUBWA,(BAWASIRI).

Wanawake pia wamekumbwa na upungufu wa hamu ya tendo la ndoa kutokana na kushuka kwa homoni estrogen, ambapo mwanamke hupatwa na kuumwa tumbo la chini ya kitovu ,maumivu anapoingiliwa,ukavu mwingi,hata kama ameandaliwa,kuyumba kwa hedhi.

Mtaalam mwingine ambaye ni mkurugenzi wa mradi wa EEP PROF RICHARD SHARP,Anabainisha vyanzo vingine vinavyoondoa mvuto wa mapenzi kuwa aina ya pepo INCUBUS wa kiume hummiliki mwanamke hadi kushindwa kutamani mapenzi na binadamu wa kawaida,mwanamke huota ndoto akifanya mapenzi na watu au wanyama,na mwanaume pia kukosa kuwatamani wanawake naye hujiwa na ndoto akifanya mapenzi nahuamka amelowa.

DR JIDONGEJA  MTAALAM WA TIBA ASILI ANAKUBALIANA NA TAFITI HIZI NA ANAKIRI KUWA WATU WENGI WENYE MATTIZO HAYA ANAWATIBU.

 PIA HUTOA TIBA ZA KISAIKOLOJIA ZA KUKUZA MVUTO KWA MTU KUPENDWA.ANAPATIKANA DAR ES SALAAM NA HUDUMA UNALETEWA POPOTE. SIMU NO 0758078280.

Zitto atoa ujumbe Baraza jipya la Mawaziri

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT -Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ametoa maoni yake juu ya Baraza jipya la Mawaziri lililofanyiwa mabadiliko jana, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook Zitto Kabwe ameandika ujumbe akiwapongeza Mawaziri hao walioteuliwa ambao wengi wao ni vijana, huku akiwataka kuchapa kazi kwa bidii.

“Uteuzi wa vijana kushika nafasi za juu ni hatua nzuri, naona vijana wengi wamepewa majukumu makubwa, ninawaombea watekeleze majukumu kwa weledi mkubwa”, ameandika Zitto Kabwe.

Jana Rais Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuongeza wizara mpya mbili, baada ya kuzivunja baadhi ya wizara ambazo zilikuwa na vitengo vingi.

CUF Ya Lipumba Yaikana CUF

$
0
0
Chama cha Wananchi(CUF), upande wa Profesa  Ibrahim Lipumba kimesema kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi wa madiwani uliopangwa kufanyika Novemba 26 lakini kimesisitiza kutoshirikiana na Ukawa.

Hii ni mara ya kwanza kwa chama hicho kuweka msimamo wake katika uchaguzi tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambapo CUF ilikuwa miongoni mwa vyama viliunda umoja huo kwa kuweka wagombea waliokubaliana.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya amesema jana  Jumamosi jijini kuwa chama hicho hakioni sababu yoyote ya kushirikiana na vyama vingine kwenye uchaguzi huo ambao unahusisha halmashauri 34.

“CUF tunashiriki kwenye uchaguzi huu lakini hatututegemei kushirikiana na umoja wowote ule, sisi hatuitambui Ukawa lakini tunajua kuna chama kama Chadema, CUF na vyama vingine,” alisema Kambaya wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni.

Alisema chama hicho kimejipanga vilivyo kuelekea kwenye uchaguzi huo na kwamba ili kuwaletea maendeleo wananchi wa maeneo hayo kunahitajika kuwa na viongozi wenye utulivu wa akili.

“Sisi tuko tayari kuelekea kwenye uchaguzi huo bila kuhusishwa na chama kingine chochote tunaamini tutafanya vizuri,” alisema.

Awali, mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho, Jafari Mneko aliwataka wana CUF kujitokeza kwa wingi katika kinyang’anyiro hicho. Amesema chama chake kimepokea taarifa kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikiwaarifu kuhusu uchaguzi huo.

“Tumepata barua kutoka tume ambayo imetueleza kuhusu tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo na sisi tumeanza kujiandaa na ndiyo maana tunawaomba wanachama wetu wanaohisi wana uwezo wajitokeze kuomba nafasi na baadaye viongozi wa chama watachuja majina yao,” alisema.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo alionya kile alichokiita mali ya chama kutumika kinyume na sheria na akawataka wanachama kutetea maslahi ya chama chao.

“Kuanzia sasa hatutapenda kuona mali ya chama kama mihuri, bendera ikiendelea kuchezewa ovyo, tunawataka wanachama kuzingatia katiba ya chama ibara ya 12 ambayo inamtaka kila mwanachama kulinda katiba na imani ya chama,” alisema.

Mbowe Ampongeza Rais Magufuli kwa Kuitenganisha Wizara ya Nishati na Madini

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amepongeza kitendo cha Rais John Magufuli kuitenganisha Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwa kwa zaidi ya miaka saba kambi hiyo ilikuwa inaishauri Serikali kufanya hivyo.

Mbowe amesema hayo jana Jumamosi kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.

Alisema kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge zinaonyesha kuwa kambi rasmi ya upinzani ilikuwa inashauri wizara hiyo itenganishwe lakini ushauri wao haukufanyiwa kazi.

"Wizara ya Nishati na Madini ni wizara nyeti mno na mara nyingi tumekuwa tukiishauri Serikali iitenganishe wizara hiyo kwani ni kubwa na nyeti ila sasa wameona ushauri wetu unafaa na kuzitenganisha," alisema Mbowe.

Alisema suala siyo nani anafaa kuwa waziri na nani hafai kuwa waziri au ukubwa wa wizara ila suala ni kuona namna gani ya kuendesha Serikali ya Awamu ya Tano.

"Magufuli ajitafakari namna anavyoendesha Serikali kwani matakwa ya viongozi ndiyo yanakuwa maelekezo ya kuendesha nchi na hata mawaziri wanafanya kazi kwa matakwa ya mtu," alisema Mbowe.

JUKATA Kuandamana nchi nzima

$
0
0
Jukwaa la Katiba (Jukata) limemuomba Rais John Magufuli apokee maandamano ya amani kushinikiza kufufua mchakato wa Katiba mpya.

Jukata limefikia maamuzi ya kufanya  maandamano hayo ya amani nchi nzima kutokana na makubaliano ya mkutano mkuu wa dharura wa jukwaa hilo uliofanyika Septemba 29 mjini Dodoma ambao pamoja na mambo mengine ulikubaliana kuyafanyia kazi maoni ya wananchi ambayo yamekuwa yakisisitiza kuwapo kwa mchakato wa Katiba mpya.

Hata hivyo hivi karibuni Kurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ilizitaarifu taasisi za umma na zisizo za umma zinazomualika Rais Magufuli kutotangaza ushiriki wake hadi zipate uthibitisho kutoka Ofisi ya Rais.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana  Jumamosi, Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda alisema maandamano hayo ya amani yatafanyika nchi nzima Oktoba 30.

Alisema tayari wamemuandikia  barua Rais Magufuli  ya kutaka ayapokee maandamano hayo ya amani wakiwa na ujumbe mahususi kwake.

Alifafanua sababu ya kumuomba Rais apokee maandamano hayo ni kumkumbusha kuwa mambo yote mazuri anayoyafanya ikiwamo kupiga vita rushwa, kusimamia matumizi mabaya ya mali za umma, yanaweza yasilete tija na maendeleo endelevu na ya muda mrefu kwa sababu mengi yanakosa msingi wa kikatiba.

"Akumbuke kuwa yeye siyo Rais wa kudumu, kama asipojenga mifumo imara anayefuata anaweza kuyafuta kirahisi masuala yote mazuri na kuirudisha nchi kwenye hali mbaya kama ambavyo amekuwa akidai.”

"Katiba ndiyo suluhisho la kulinda mazuri yote anayoyafanya na kujenga mifumo thabiti isiyoruhusu nchi kuchezewa na watu wachache kwa manufaa yao," alisema.

Amesema kuna umuhimu wa kuyaweka masuala yote yanayofanyika sasa  katika Katiba kutokana na ukweli kwamba Katiba ndiyo sheria mama na dira ya nchi.

"Imethibitika bila shaka,  nchi zenye Katiba bora ustawi wa Taifa huwa wa hali ya juu kuliko nchi zilizokuwa na migogoro kutokana na kukosa Katiba zenye misingi ya uongozi," amesema Mwakagenda.

Mwakagenda alifafanua kuwa  maandamano hayo katika ngazi ya kitaifa yatafanyika jijini Dar es Salaam na yataanzia kwenye ofisi za Jukata na kumalizikia viwanja vya Mnazi Mmoja.

Alisema kwa upande wa mikoani nje ya Dar es Salaam kila wilaya ya Tanzania wameshapeleka taarifa kwa wakuu wa Polisi wa Wilaya kuwafahamisha kuhusu njia yatakapopita maandamano hayo ya amani.

"Lengo la taarifa hiyo mikoani ni kuwaomba wakuu wa wilaya ambao ni wawakilishi wa Rais kwenye wilaya husika kuyapokea," alisema Mwakagenda.

Mwakagenda alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki kwenye maandamano hayo ya amani.

Alisema maandamano ni njia mojawapo ya wananchi kuwasiliana na viongozi wao ambao wamepewa dhamana ya kuongoza Taifa kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.

Alieleza Jukata wana imani watapata ushirikiano wa kutosha kutoka Jeshi la Polisi nchini ili maandamano hayo yafanyike katika hali ya amani na utulivu.

Alisema ana imani wananchi pia watapokea kwa mtizamo chanya kusudio la kufanya maandamano hayo yenye lengo la kurudisha hamasa ya wananchi kushiriki kwenye michakato ya kidemokrasia.

“Hamasa imepungua, iwapo wananchi watapoteza hamasa hiyo kabisa, ipo hatari huko mbele michakato mingine kama uchaguzi kukosa ushiriki  kutokana na wananchi wengi kutoona umuhimu wa kushiriki mambo muhimu ya nchi yao,”alisema.

Alisema Tanzania itakuwa nchi ya viwanda ikiwa kipaumbele kitakuwa Katiba mpya yenye mifumo imara ili kusafiri katika njia sahihi wananchi waitakayo.

“Bila Katiba mpya na bora ni sawa na kujenga nyumba nzuri juu ya mchanga ambayo inaweza kuangushwa hata na upepo, ” alisema Mwakagenda.

Kadinali Pengo Amkana Askofu Niwemugizi

$
0
0
Baada ya Askofu wa Kanisa Katoliki nchini kusikika akidai Katiba mpya ndio kipaumbele cha sasa kwa wananchi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo amewataka waumini wa Kanisa hilo na Watanzania kwa kuyachukulia maoni hayo kuwa si msimamo wa Kanisa Katoliki. 

Akizungumza mwishoni mwa wiki hii, Kadinali Pengo amesema kuwa kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge, Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi ni maoni binanfsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Mwadhama Kadinali Pengo amesisitiza hilo wakati akitoa ufafanuzi juu ya sintofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa Kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo sio msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimao wa kanisa kwa sababu sisi tunataratibu zetu za kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Pengo amefafanua kuwa kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndio msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge, Ngara lakini kimsingi kauli ile imekosa vigezo vya kuichukulia kama msimamo wa Kanisa au Jimbo anakotoka.

Akizungumzia juu ya suala la katiba mpya ambalo baadhi ya wanaharakati na wanasiasa wanajaribu kuligeuza kuwa ajenda kuu kwa sasa, Kadinali Pengo alisema yeye binafsi kipaumbele chake ni kuona huduma za jamii kama zile elimu na afya zinaendelea kuboreshwa kwa kasi kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. Magufuli ilivyoanza kufanya.

“Mtu akiniambia priority (kipaumbele) ya Tanzania ni katiba mpya inabidi anithibitishie huo ukipaumbele maana siwezi kuona mtoto anakufa kwa njaa au kwa kukosa dawa eti kwa sababu ya katiba mpya. Kwangu mimi katiba ni kitu ambacho kije baadae, si cha haraka, Pengo"

“Wanasiasa wasiache watoto wetu wafe kwa njaa kisa malumbano ya katiba. Wasiache watoto wakose shule kwa sababu hela zote zimeishia kwenye malumbano juu ya katiba,” Kadinali Pengo amesisitiza.

Zitto Kabwe Atoa NENO Kushuka kwa Mapato ya Nchi

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi  ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kutoa sababu kwanini mapato ya serikali yameshuka na kusema serikali inapaswa kutazama upya utendaji wake vinginevyo itabidi ikope ili kulipa mishahara kwa watumishi.

Zitto Kabwe amesema kuwa kwa miezi ya Julai na Agosti mwaka huu mapato ya serikali yalishuka mpaka shilingi 600 bilioni na kusema ni maporomoko makubwa hivyo madhara yake ni makubwa.

"Ni mporomoko mkubwa Sana na sio jambo la kushangilia hata kidogo. Madhara ya kushuka kwa mapato ni makubwa kwani mishahara ya watumishi wa Umma peke yake ni Shilingi 570 bilioni Kwa mwezi" alisema Zitto Kabwe

Aidha kiongozi huyo ameelezea sababu kubwa iliyopelekea mapato ya nchi kushuka 

"Mzee Harry Kitilya alipata kuniambia mwaka 2013 " Mwenyekiti, TRA inatoza kodi kutoka kwenye shughuli za biashara zinazozalisha mapato na sio kutoka kwenye biashara tu ". Kitilya alikuwa na maana kuwa kama hakuna shughuli za biashara ( business transactions), huwezi kutoza kodi. Maelezo haya yanaeleza kwanini mapato ya serikali yameshuka. Shughuli za biashara zimeshuka sana nchini na hivyo kupelekea kuporomoka Kwa mapato" alisema Zitto Kabwe

Zitto Kabwe aliendelea kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili la kuporomoka kwa mapato ya serikali

"Kodi inayoingiza mapato mengi Serikalini ni PAYE ( kutoka mishahara ya wafanyakazi). Kitabu cha mapato ya serikali kuu cha mwaka 2016/17 kinaonyesha kuwa wafanyakazi wote wa sekta ya Umma na sekta binafsi walichangia jumla ya shilingi trilioni 3 kwenye mapato yote ya Serikali. Hivi karibuni tumeshuhudia makampuni yakipunguza wafanyakazi na mengine kufungwa. Pia Serikali yenyewe ilipunguza watumishi iliyowaita hewa na wenye vyeti feki. Hivyo eneo kubwa la kodi ya PAYE limeathirika" alisisitiza Zitto Kabwe

Mbali na hilo Zitto Kabwe aliitaka serikali kutazama upya utendaji wake ili kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji nchini na kudai kama serikali haiatafanya hivyo itafika mahali itabidi ikope pesa ili kulipa mishahara ya watumishi mbalimbali.

Tundu Lissu Kufanyiwa Upasuaji wa 15

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefanywa upasuaji mara 14 na ataendelea kufanyiwa upasuaji mwingine wa  15  ndani ya wiki mbili zijazo.

Mbowe amesema hayo jana kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.

Alisema hali ya Lissu inaendelea kuimarika lakini aliumizwa sana kama walivyokuwa wanaeleza mara zote lakini na jambo la kumshukuru Mungu kwamba ameendelea kuimarika.

"Ameendelea kupata afya, akili zake ni timamu, madaktari kule wanafanya kazi kubwa kwelikweli kuendelea kumuudumia na ni matumaini yetu kuwa baada ya muda Mungu atamrejesha katika wajibu wake wa kulitumikia Taifa,"

Mbowe alizungumza hayo baada ya kueleza kuwa alitokea Nairobi kuangalia afya ya mbunge huyo ambaye alipigwa risasi Septemba 7 mwaka huu akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.

Pata Tiba ya Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za: 
 
FUUl POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.
 
NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Lema: Hakuna jipya baraza la mawaziri

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa baraza jipya la mawaziri lililotangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli halina jipya kwani sura zilizobaki ni zile zile.

Ameyasema kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter, ambapo amesema kuwa ameona mabadiliko ya baraza la Rais Magufuli lakini bado fikra ni zile zile na watu ni wale wale na kudai katiba mpya ndio suluhisho la vyote.

“Nimeona Mabadiliko ya baraza la JPM. Watu ni wale wale, fikra zile zile. Katiba Mpya yenye fikra mpya ndio tumaini kwa mabadiliko sahihi ya nchi na watanzania kwa ujumla,”ameandika Lema

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images