Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Yusuf Manji Akabidhiwa Mahakamani Tena

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemkabidhi mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumaliza kumuhoji katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa washtakiwa hao wamerudishwa kama Mahakama ilivyoamuru warudishwe baada ya Polisi kumaliza kuwahoji.

Baada ya kusema hayo, Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itaendelea na utaratibu kama ilivyo awali, ambapo ameahirisha hadi September 8, 2017.

Awali Mahakama hiyo iliruhusu Yusuf Manji na wenzake watatu kwenda kuhojiwa na Polisi kwa lengo la kukamilisha upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi wanayokabiliwa nayo.

Mbali na Yusuf Manji, washitakiwa wengine waliokabidhiwa ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda, Mtunza Stoo, Abdallah Sangey na Thobias Fwere.

Jambo La Aibu Lililo Nitokea Usiku Wa Jana Wakati Nafanya Tendo La Ndoa Na Mke Wangu.

$
0
0
Mimi  ni  mwanaume  mwenye  umri  wa  miaka  42  na  mkaazi  wa  jijini  Dar  Es  Salaam.

Mimi  nimeoa  na  nimejaaliwa  kupata  watoto  watatu, watoto  wawili  mimezaa  na  wanawake  wawili  tofauti  na  huyu  mtoto  wa  tatu  nimezaa  na  mwanamke  ambae  nimefunga  nae  ndoa na ndo  ninae  ishi  nae.

Tatizo  langu  kubwa  ni  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  ambalo  nimekuwa  nalo  kwa  muda  mrefu sasa.  Chanzo   cha  tatizo  langu  nadhani  ni  kujichua  kwa  muda  mrefu  kwani  nilianza  kujichua  mwaka 1992  wakati  huo  nikiwa  na  umri  wa  miaka  17  na  tangu  nianze  kujichua  mwaka  huo  wa  92  sijawahi   kuacha  kujichua  hadi  leo  hii.

Mchezo  huu  wa  kujichua  umenisababishia  madhara  makubwa  sana ; kwanza   maumbile  yangu  ya  kiume  yamelegea, yamesinyaa  na  kunywea  ndani  na ninapokuwa nimesimama  basi  yanakuwa  yamelegea   kweli kweli.

Pili   nisipotumia  madawa  ya  kizungu  huwa  nafika  kileleni  ndani  ya  muda  mfupi  sana, nikizidi  sana  ni dakika  moja  .

Tatu   nakuwa  sina  uwezo  wa  kurudia  tendo  . Nikishamaliza  ndio  imetoka  hiyo  mpaka  kesho  yake.

Katika  kukabiliana  na  tatizo  langu  hili  nimekuwa  nikitumia  madawa  ya  kizungu  na  kusema  ukweli  yameniathiri  kwa  kiwango  kikubwa  sana  kiasi  cha  kunifanya  niwe  tegemezi, yaani  bila  hayo  madawa  ya  kizungu  siwezi  kabisa  kufanya  tendo  la  ndoa.

TUKIO   LILILO  TOKEA  USIKU  WA  JANA
Sababu  ya  kuandika  barua  pepe  hii  ni  kukuelezea    jambo  la  aibu  lililonitokea  usiku  wa  jana  wakati  nikifanya  tendo  la  ndoa  na  mke  wangu.

Tukio  lililo  nitokea  jana  si  mara  ya  kwanza  kunitokea  lakini  kwa   mke  wangu  huyu ndio  limenitokea  kwa  mara  ya  kwanza  but  kwa  wanawake  wengine  ambao  nimewahi  kutembea  nao, limeshanitokea  mara  nyingi tu kiasi siwezi  kuhesabu.

Halijawahi   kutokea  kwa  mke  wangu  kwa  sababu  kwa  muda  wa  miaka  mitatu  ambayo  nimekuwa  na  mwanamke  huyu  nimekuwa  makini  sana  wakati  wa  kufanya  “ maandalizi “  kabla  ya  kushiriki  tendo  la  ndoa  na  mke  wangu.  Nimekuwa  nikihakikisha  nnatumia dawa  za  kizungu  za  kuongeza  nguvu  kabla  ya  kukutana  kimwili  na  mke  wangu  huyu.  Ingawa  uume  wangu  unakuwa  umesimama   ukiwa  lege  lege  lakini  at least  sijawahi  kushindwa  kabisa  kushiriki  na  mke  wangu.

Nilikuwa  nimeenda  safari  mkoani  ambako  nilikaa  kwa  muda  wa  wiki moja  na  usiku  wa  jana  ndio  nikawa  nimerudi  safari.

Kwa  bahati  mbaya  sana  nikawa  nimesahau  kubeba  dawa  zangu  za  nguvu  za  kiume na  kwa  bahati mbaya  zaidi  nakuja  kukumbuka  tayari  nimeshafika  home  na  ilikuwa  usiku  tayari.

Wakati  tunafanya  tendo  la  ndoa  nilijikongoja  nikafanikiwa  kumaliza  round  ya  kwanza  japo  nilitumia  muda  mfupi  sana  nadhani  kama  dakika  moja  hivi.

KIMBEMBE   KILIANZA  KWENYE  KUTAFUTA   ROUND  YA  PILI
Baada  ya  kumaliza  round  ya  kwanza  nilipata  maumivu  makali  sana  kwenye  mishipa  yangu  ya  uume  na  sikuwa  na  hamu  kabisa  ya  kurudia  round  ya  pili . Hata  hivyo  nilifanikiwa  kujikongoja  kongoja  hivyo, baada  ya  kama  masaa  mawili hivi  jogoo  akafanikiwa  kupanda  mtungi  tena. Na  hii  ilikuja  baada  ya  kutomasa  sana  na  kuvuta  hisia  sana  na  wakati  nafanya  yote  hayo  nafanya  bila  wife  kushtukia  kwamba   ninajitomasa  ili jogoo  apande  mtungi. Huwa  natakaga  wife  awe  anajua   jogoo  wangu  anapanda  mtungi  bila  kuchezewa.  So  nilikuwa  nampigisha  story  wife  huku  tunatazama  kipindi  kwenye  tv  and   at the  same  time  nikawa  najitomasa.

Sasa  basi  baada  ya  kuridhisha  kuwa  jogoo  amepanda  mtungi  nikaanza  sasa  maandalizi  ya  ku-do  wife, ila  ile  najaribu  tu ku  anza  ku-do , jogoo  akawa amenywea  tena, na  jogoo  alinywea  kwa  sababu   nilipo  mwambia  wife  tuanze  ku-do  tena, wife  akasema  anaenda  maliwatoni  kwanza, kitendo  cha  wife  kwenda  maliwatoni   tu  jogoo   wangu  akanywea  tena.   Nikasema  ngoja  nijaribu  kujichezea  tena  fasta  fasta  kwa  muda  ule  ambao wife  atakuwa  ameenda  chooni  ili  atakapo  rudi akute  jogoo  yupo  vizuri, lakini  wapi  wakati  najaribu  kuanza  kujitomasa  tena, wife  akawa  amesha rejea  tena, so  ikabidi  namimi  nizuge nimebanwa  na  haja  kubwa   na  kumwambia  wife  naenda  toilet  mara  moja.

Kufika  toilet  nikaanza  kutomasa  jogoo  wangu  mithili  ya  mtu  anae taka  kupiga  punyeto, lakini wapi. Jogoo  akawa  anasimama kidogo  ananywea, anasimama  kidogo  ananywea, nikaona  hapa  mwishowe  wife  atanistukia  au  kuhihisi  vibaya   coz  zilikuwa  zinakaribia  zaidi  ya dakika  tano  hivi  kwa  kukadiria.

So nikaamua  kurudi  tu  chumbani . Kufika  chumbani  nikamkuta  wife  amekaa  kitandani. Bahati nzuri  nikiwa  nafika, movie  moja  ya  kibongo  ikawa  ndo  inaanza  kuonyeshwa   kwenye  kituo  kimoja  cha  movie  za  kibongo na  inaonekana   alikuwa  anaisubiri  kwa  hamu. So  akawa  kama  attention  yake  ameihamishia  kwenye  movie na  hiyo ndo ikawa  pona  pona  yangu  kwa  muda  huo.

 So  na  mimi nikazuga  kuvutiwa  na  ile  movie , attention  yetu sote  tukawa  tumeihamishia  kwenye  movie.

Nashukuru  Mungu  ile  movie  ilionekana  kuwa  so interested  kwake  yeye. Nilipo  ona yupo so interested   nikazuga  kumwambia  “ Ngoja  nikuache  umalize  kwanza  hiyo  movie  ndo  tuendelee”  kumbe  moyoni  mwangu  nasema “ Asante  Mungu  kwa  kunifichia  hii  aibu “.

So muda  huo  tulio  kuwa  tunautumia  kutazama  movie  nikasema  niutumie  kutomasa  jogoo  hadi  asimame.

Baada  ya  kama  nusu  saa  hivi, bahati nzuri  jogoo  akawa  amewika, nikamwambia  wife  nataka  kwenda  kulala, tumalizie  game  haraka  haraka. Bahati nzuri  nikafanikiwa   kucheza  game  na  kumaliza  japo  nilitumia  muda mfupi  sana  lakini  ni  heri  nusu  shari  kuliko  shari  kamili.  Ni  heri  nionekane  nawahi  kufika  kileleni  mapema  kuliko  nionekane  sina uwezo  wa  kupandisha  jogoo kabisa .

Nimeamka    asubuhi  nimetengeza  safari  ya  kijijini  Kisarawe  ambako  nitakaa  kwa  muda  wa  mwezi  mmoja.

 Ninataka  katika  kipindi  chote  hicho  cha  mwezi  mmoja  niutumie  kutibu  tatizo  nililo  nalo  na  kupona  kabisa  ili nitakapo  rudi  kwa  mke  wangu  niwe  na  confidence  ya  kushiriki nae  tendo  la  ndoa.

Pia  naogopa  aibu  iliyo  taka  kunitokea  usiku  wa  jana  isije  kunitokea  tena  kwa  sababu  jambo  hilo liliniogopesha  sana   na  sitaki mke  wangu  anione  mimi ni mwanaume  wa  hivyo  ingawa  sijui  ananichukuliaje  mpaka  sasa.

IDADI  KUBWA  YA  WANAUME  WALIO  KATIKA  NDOA  AMBAO  WANAKABILIWA NA  TATIZO  LA  UKOSEFU NA UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME, WANASHINDWA   KUPATA  TIBA  YA  TATIZO  LINALO  WAKABILI  KWA  SABABU  YA  KUTOKUWASHIRIKISHA WAKE  ZAO.  WANAUME  WANAO  WASHIRIKISHA  WAKE  ZAO  HUPATA  NAFUU  YA HARAKA  SANA  KWA  SABABU  MKE  NAE  ANAKUWA  ANAJUA  TATIZO  LINALO  MSUMBUA  MUME  WAKE  NA  ANAWEZA  KUSHIRIKI KATIKA  KUMUANDALIA  LISHE  MAALUMU  KWA  WANAUME  WENYE  SHIDA  YA  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

MFANO  MZURI  TUNAWEZA  KUUPATA  KWA  TINA ( 33 ) MKAAZI  WA  DAR  ES  SALAAM, AMBAE  BAADA  YA  KUGUNDUA  TATIZO  LINALO MKABILI  MUME  WAKE  AMEAMUA  KUSHIRIKI  KIKAMILIFU  KWA  KUMUANDALIA  NA  KUMTAYARISHIA  MUMEWE   LISHE  MAALUMU  KWA WANAUME  WENYE  TATIZO  LA  NGUVU  ZA  KIUME  PAMOJA  NA  KUMUANDALIA  NA  KUMPIKIA  DAWA  YA JIKO  AMBAYO  INATIBU  NA  KUPONYESHA  TATIZO  LA  UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

KUSOMA  KUHUSU  NAMNA TINA  ALIVYO JITOLEA  KUMTIBU  MUMEWE  TATIZO  LA  NGUVU  ZA  KIUME, TEMBELEA  : http://neemaherbalist.blogspot.com/2017/08/kutana-na-mwanamke-aliye-jitolea_26.html

Hatukatazi Watumishi wa Afya kumiliki maduka ya Dawa lakini ni Lazima Yawe Mbali na Hospitali

$
0
0
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Serikali haikatazi Watumishi wa Afya kumiliki maduka ya dawa lakini ni vizuri wakazingatia kuweka maduka hayo mbali na Vituo vya Afya vya Serikali na Hospitali ili kusiwe na aina yoyote ya kutanguliza maslahi yao kwanza katika kutoa huduma za dawa kwa wagonjwa.

Ameeleza kuwa kwa sasa Serikali imejitahidi kuongeza upatikanaji wa dawa na imeamua kuanza kununua dawa kutoka kwa wazalishaji badala ya kununua kutoka kwa wafanyabiashara kama ilivyokuwa awali.

"Watendaji badala ya kuwaandikia wagonjwa dawa zilizo kwenye orodha, wanaandika dawa zao na kuwaambia wagonjwa wakanunue dawa kwenye maduka ya dawa. 

"Hatukatazi Watumishi kuwa na maduka ya dawa ila muhimu kuchora mstari wa dawa za Serikali na dawa ambazo sio za Serikali.”  Amesema  Waziri Ummy Mwalimu.

Darasa la 7 Kuanza Mitihani ya Kuhitimu Kesho na Kesho Kutwa

$
0
0
Wanafunzi 917,072 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi kesho na keshokutwa (Septemba 6 na 7).

Kati ya wanafunzi hao, wavulana ni 432,744 sawa na asilimia 47.19, wakati wasichana ni 484,328 sawa na asilimia 52.81.

Watahiniwa 882,249 watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na 34,823 watatumia lugha ya Kiingereza.

Jumla ya watahiniwa 94 wasioona wamesajiliwa  kufanya mtihani huo, wakiwemo wavulana 58 na wasichana 36.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema maandalizi yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa vifaa vinavyohitajika katika halmashauri zote nchini.

Dk Msonde amezitaka halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unazingatiwa.

"Tunataka mazingira ya vituo vya mitihani yawe salama, tulivu na kuzuia mianya yoyote inayoweza kusababisha udanganyifu,” amesema.

Spika Ndugai Atuma Salamu kwa Wabunge Waliodai Yeye ni Dhaifu

$
0
0
Mara baada ya kikao cha kwanza kwenye mkutano wa 8, wa Bunge la 11, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amesema wale waliokuwa wanamtuhumu kuwa mdhaifu katika kufanya maamuzi, sasa wataona dhahiri udhaifu wake uko wapi.

Spika Ndugai ameeleza hayo wakati akiwakaribisha wabunge 7 wapya wa Chama cha Wananchi (CUF) waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya wabunge nane ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

“Taratibu zote zilifuatwa kwa wabunge hawa kuingia hapa bungeni, wapo baadhi ya lile kundi wiki mbili kabla ya mambo haya kutokea walisema Spika dhaifu, nikasema sasa udhaifu wangu ndiyo utaonekana. Kama una akili yako maneno kama haya hayana umuhimu”, alisema Spika Ndugai.

Sambamba na hilo, Spika Ndugai amewakaribisha wabunge walioapishwa huku akiwafunda wabunge wengine, kwamba kiapo walichokula wenzao leo kiwakumbushe utii na uaminifu kwa kwa tiba ya nchi.

“Kiapo hiki cha uaminifu kina tukumbusha wengine ambao tuliapa utii wa Katiba na kiapo chetu kwa ujumla wake, kuhusiana na uaminifu na utii.  Ni vizuri kuisoma Katiba na kuipitia ili uweze kujua nafasi ya vyama vya siasa na uhusiano wa mbunge na chama cha siasa”, alisisitiza Spika Ndugai.

Wabunge hao ambao wameapishwa leo wanatarajiwa kupangiwa kamati na kuanza kazi mara moja, kama ambavyo Spika amewataka kufanya hivyo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Septemba 6

MAJONZI: Watoto Waliotekwa Wakutwa Wamekufa Chooni

$
0
0
Watoto 2 Ikram na Maureen, kati 4 waliotekwa wamepatikana wakiwa wamefariki dunia katika shimo la choo ambacho  bado halijaanza kutumika.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian huko Olasiti jijini Arusha, Daudi Safari, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Jeshi la Polisi limeopoa miili ya watoto hao  jana jioni.

Inadaiwa kuwa mtekaji aliwatumbukiza ndani ya shimo hilo wakiwa hai kabla ya kuondoka na kuelekea Geita ambapo amekamatwa na kusema walipo watoto hao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha taarifa za kukamatwa kwa mtekaji huyo aliyetambuliwa kwa jina la Samson Petro mwenye umri wa miaka 18.

Kamanda Mwabulambo amesema kijana huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungului iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na mtoto mdogo mwenye miaka miwili.

Alisema mtuhumiwa alimficha mtoto huyo katika chumba namba 11 cha nyumba hiyo ya kulala wageni wakati akisubiri mpango wake wa kutaka alipwe shilingi milioni nne na wazazi wa mtoto huyo Ombeni Mshana na Elizabeth Ombeni.

Mwigulu Nchemba Ataja Sababu za Masheikh wa Zanzibar Kushitakiwa Bara

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefunguka na kusema kuwa mtu yoyote akifanya makosa ya nchi nzima atachukuliwa na kupelekwa sehemu yoyote ambapo mamlaka zinazofanya jambo hilo zitaona panafaa.

Mwingulu Nchemba amesema hayo  jana wakati akijibu swali la Mbunge Dkt. Suleman ambaye alihoji uhalali wa baadhi ya Masheikh kuhamishwa kutoka Zanzibar na kuletwa Tanzania Bara kuhukumiwa katika mahakama za Tanzania bara na kusema ni kinyume na sheria.

"Mhe Spika spingani na muuliza swali kwenye upande wa vipengele vya sheria  lakini naomba nimwambie tu kwamba kuna makosa ambayo 'specifically' siyo ya kijiografia mfano watu wakifanya makosa ya kung'oa michikichi Kigoma hilo unaweza kulitaja ni kosa la Kigoma, kama watu watang'oa karafuu Pemba ni kosa ambalo unaweza kusema la Pemba.

".... lakini yanapofanyika makosa ya nchi nzima Mtanzania yoyote au raia yoyote awe wa Tanzania au nje ya Tanzania atachukuliwa na taratibu za kufuata haki na sheria zitafanyika pale ambapo mamlaka inayofanya hatua hizo inaona ndipo panafaa" alisema Mwigulu Nchemba

Ongeza Hips, Makalio Na Mapaja, Kuwa Mweupe Na Softi...... Ongeza Maumbile Ya Kiume, Nguvu Na Hamu Ya Tendo

$
0
0
Natural beauty product Tunakuletea bidhaa bora zenye matokeo ya uhakika na haraka zisizo na kemikali wala madhara. Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa kiafya. 
 
             NB. Matokeo ni uhakika na garantii na risiti
🍉🌿🍅🍍🍒🍉🍓🍅🍒
          BIDHAA ZETU:-
  
1.Kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @130,000/=
2.Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa:-
(a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200,000/=
(b)Vidonge  @180,000/=
(c)BOTCHO 10× ya kupaka @170,000/=
3.Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:-
(1)Mafuta  @130,000/=
(11)Vidonge @150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5.Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a)SHARK POWER gely ya kupaka (Inaongeza inch 6-7) @150,000/=
(b)Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
(C)HANDSOME UP ORIGINAL- kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo @250,000/=
6.Kuondoa mvi milele zisiludi tena @150,000/=
7.Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula  @130,000/=
8.Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @130,000/=
(b)Mkanda wa kawaida @120,000/=
(c)Micro-computer belt wa umeme @200,000/=
9.Kupunguza  maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @130,000/=
10.Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) na kuondoa vigimbi @130,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @120,000/=
12.Kurudisha usichana  (bikra) @120,000/=
        Wasiliana nasi :- (+255)
             0759029968 au.       
                0659618585
 
  TAHADHARI: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
👉🏻Ili kuona bidhaa zaidi na shuhuda za waliotumia bidhaa zetu. ...............
     Follow us on instagram  @natural2162
@natural2162
            
                              [ WELCOME ALL]

Wizara ya Ardhi yaanza kutoa hati ya miaka 99 kwa wakazi wa Dodoma

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  imeanza kutoa hati mpya za ardhi zenye umri wa miaka 99 tofauti na zile zilizokuwa zikitolewa awali za miaka 33.

Akizungumza na wanahabari jana  Mjini Dodoma Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema  zoezi hilo la ubadilishaji wa hati kwa wakazi elfu 25 wa mkoa huo limeanza rasmi ambapo wakazi hao wanatakiwa kufika Wizarani wakiwa na nakala za hati zao za zamani ambazo zimelipiwa kodi zote za ardhi.

“Ubadilishaji wa hati hizi ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipoivunja Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ambapo aliiagiza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kubadilisha hati zilizokuwa zikitolewa na mamlaka hiyo kutoka umiliki wa miaka 33 na kuwa miaka 99,” alifafanua Lukuvi.

Aliongeza kuwa hati hizo za miaka 33 zilikuwa zikiwanyima fursa wakazi wa Dodoma kupata wawekezaji kutoka nje ya nchi kutokana na hati hizo  kuwa za muda mfupi tofauti na hati zinazotolewa na miji mingine hapa nchini.

Aidha hati hizo pia zilikuwa kikwazo kwa wamiliki kushindwa kupata mikopo mikubwa ambayo hutolewa kwa watu wenye umiliki wa ardhi wa kuanzia miaka 50 na kuendelea.

Lukuvi amesema kuwa mabadiliko hayo ya hati hayata athiri mipaka ya viwanja vitakavyobadilishiwa hati bali kinachofanyika ni kubadilisha umri wa umiliki wa ardhi.

==>Msikilize hapo chini

Serikali yakanusha ugonjwa wa Ebola kuwepo nchini

$
0
0
Serikali imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za kuwepo ugonjwa wa Ebola nchini zinazodai kuwa ugonjwa huo umeingia nchini kupitia nchi jirani ya Rwanda.

Agizo la Makamu wa Rais wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam

$
0
0
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amemtaka Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa kuhakikisha kanda yake inatokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Mama Samia ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika Tamasha la 14 la Jinsia lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo.

“Bado takwimu za Jeshi la Polisi zinaonyesha ukatili wa kijinsia unaendelea. Kamanda Mambosasa tunakuachia wewe suala hili, likitokea tunakubana wewe na wewe utawabana wenzako,” alisema.

Mama Samia alisema serikali inaendelea kutekeleza Mpango mkakati wake wa miaka mitano wa kutokomeza ukatili wa jinsia ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto unapungua kwa asilimia 50.

“Bila wanawake kuzitumia sera na sheria za wanawake na jinsia zilizotungwa na serikali hatutafanya lolote. Isipokuwa tutazifungia na kuziweka katika makabati na hatutafika kokote,” alisema.

Hata hivyo, Mama Samia alisema serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwakomboa wanawake ikiwemo kufufua Benki ya Maendeleo ya Wanawake nchini (TWB).

“Serikali imechukua hatua mbalimbali kumkomboa mwanamke kiuchumi ili aweze kusaidia jitihada za serikali za kuleta maendeleo. Tuna Mpango wa kufufua benki ya wanawake, ni wajibu wenu kuhakikisha haifi. Watu wenye uwezo waisaidie serikali kuitafutia mitaji,” alisema.

Aidha, Mama Samia aliwataka wanaume kutowanyanyasa wanawake kwa kuachana na mila na desturi potofu zinazokandamiza haki za wanawake na jinsia.

Pata Tiba ya Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za: 
 
FUUl POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.
 
NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

ACACIA Yaanza Kufungasha Virago.....Yakabidhi Uwanja wa Ndege wa Buzwagi

$
0
0
Baada ya Acacia kutangaza kupunguza operesheni zake Bulyanhulu, kampuni hiyo imeanza kuikabidhi Serikali baadhi ya mali zake kwenye Mgodi wa Buzwagi ambao unatarajiwa kufungwa miaka mitatu ijayo.

Katika utekelezaji wa makabidhiano hayo, jana kampuni hiyo iliikabidhi Serikali uwanja wa ndege uliopo katika mgodi huo. Huu ni mgodi wa pili kufungwa na kampuni hiyo baada ya ule wa Tulawaka ambao iliuuza kwa Shirika la Taifa la Madini (Stamico) mwaka 2013.

Jana, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Zainab Telack alisema hiyo ni hatua ya awali katika mchakato wa mgodi huo kusitisha shughuli zake za uchimbaji madini kwa mujibu wa mkataba uliopo.

“Tumeanza na uwanja wa ndege baadaye tutakabidhiwa majengo na vitu vingine kama ulivyo utaratibu,” alisema Telack.

Alisema Desemba mwaka huu utakuwa mwisho wa shughuli za uchimbaji na baada ya hapo wataanza kusaga mawe yaliyochimbwa kwa miaka mitatu mfululizo mpaka 2020.

Juzi, kampuni hiyo ilitoa taarifa ikibainisha lengo lake la kupunguza operesheni zake kwenye Mgodi wa Bulyanhulu baada ya kuzuiwa kusafirisha mchanga wa dhahabu tangu Machi hivyo gharama za uendeshaji kuwa juu kuliko ilivyotarajia huku mapato yakishuka.

Kwa miezi sita ya kutosafirisha mchanga huo, Acacia imedai kuwa imepoteza zaidi ya Sh583 bilioni.

Katika utekelezaji wa mkakati wake wa kubana matumizi, kampuni hiyo inatarajia kupunguza wafanyakazi na kandarasi mbalimbali ilizonazo. Kwa sasa, ina wafanyakazi 1,200 na wakandarasi 800 kwenye Mgodi wa Bulyanhulu.

Taarifa hiyo pia ilibainisha kucheleweshwa kwa leseni za wakandarasi wa machimbo ya chini ya ardhi kwenye Mgodi wa Buzwagi jambo linaloongeza changamoto.

Ingawa mazungumzo baina ya Serikali na kampuni ya Barrick inayomiliki asilimia 64 ya hisa za Acacia bado yanaendelea, uamuzi wa kupunguza operesheni kwenye mgodi huo unatarajiwa kupunguza uzalishaji kwa karati 100,000 kutoka kati ya karati 850,000 hadi 900,000 zilizokadiriwa awali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu, bei ya hisa zake kwenye Soko la London (LSE) ilishuka kwa asilimia sita mpaka Pauni 1.94 huku kwenye Soko la Dar es Salaam (DSE) ikishuka kutoka Sh5,940 mpaka Sh5,400 jana mchana. Tangu kutolewa kwa zuio hilo, bei ya hisa hizo imepungua kwa asilimia 65.

Taratibu za kupunguza operesheni zake kwenye Mgodi wa Bulyanhulu zitakamilika ndani ya miezi mitatu na kampuni hiyo inaamini itatengamaa kuanzia mwakani.

Mahakama Yawapa Kinga Wabunge 19 wa CUF

$
0
0
Baada ya wabunge wanane wa viti maalumu wa CUF, kuvuliwa uanachama wa chama hicho na kisha kupoteza nyadhifa zao, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewapa kibali wabunge 19 wa majimbo wa chama hicho kuomba kuwekewa kinga.

Mahakama hiyo imetoa kibali hicho kwa wabunge hao baada ya kukubaliana na maombi yao waliyofungua mahakamani hapo dhidi Bodi ya Wadhamini wa CUF, mwenyekiti wa CUF na katibu mkuu wa chama hicho.

Katika maombi hayo namba 69 ya mwaka 2017, wabunge hao wanaowakilishwa na Wakili Mohamed Tibanyendela walikuwa wakiiomba mahakama iwaruhusu kufungua maombi kuomba kinga ili wasiguswe kutokana na mgogoro wa kiuongozi unaoendelea ndani ya chama hicho.

Wakiongozwa na Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea, wabunge hao walifungua maombi hayo ya kibali cha kuomba kinga Agosti 25 na yalisikilizwa upande mmoja (waombaji pekee) Agosti 31 na kutolewa uamuzi huo juzi na Jaji Wilfred Dyansobera.

Tibanyendela alisema jana kwamba baada ya kupata kibali hicho, watafungua maombi hayo mahakamani hapo baada ya kukamilisha taratibu zote.

“Ndio nakamilishakamilisha hapa kuandaa maombi haya na baada ya hapo itabidi kwanza wateja wangu wote wasaini. Kama unavyojua kwa sasa wote wako Dodoma, bungeni, lakini tutafanya utaratibu ambao utawawezesha wote kusaini kisha tutayapeleka mahakamani,” alisema.

Katika maombi watakayofungua, wabunge hao wataomba kupewa kinga ili wasiguswe kwa namna yoyote na wajibu maombi au watu wanaofanya kazi kwa maelekezo yao, ili kutokuathiri haki na masilahi yao.

Pia, wabunge hao wataiomba Mahakama iwalazimishe wajibu maombi hao kumaliza tofauti zao kwa mujibu wa katiba ya chama na sheria za nchi.

Wabunge hao wa majimbo wamestuka na kuchukua hatua hizo baada ya wenzao wanane kupoteza nyadhifa zao kutokana na uamuzi wa chama hicho upande wa Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kuwavua uanachama.

Chama hicho kimekuwa katika mgogoro wa kiuongozi kwa muda mrefu tangu Profesa Lipumba alipotangaza kujiuzulu mwaka 2015 na baadaye kubatilisha uamuzi wake huo mwaka jana.

Kurejea kwake kwa kuandika barua ya kutengua ile ya kujiuzulu, kulisabisha kuibuka kwa makundi mawili ya wanachama wa chama hicho, moja likiongozwa na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad linalompinga na jingine linalomuunga mkono.

Katika mwendelezo wa mgogoro huo, kambi inayoongozwa na Profesa Lipumba ilitangaza kuwahoji na kuwachukulia hatua wanachama na viongozi mbalimbali wakiwamo wabunge kwa tuhuma mbalimbali zikiwamo kukihujumu chama kwa kushirikiana na vyama vingine.

Kundi la kwanza kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa na Baraza Kuu la Uongozi ni wabunge hao wa viti maalumu ambao wako kambi ya Maalim Seif.

Wabunge hao wanane ni Severina Mwijage, Saumu Heri Sakala, Salma Mohamed Mwassa, Riziki Shahari Ngwali, Raisa Abdallah Mussa, Miza Bakari Haji, Hadija Salum Al-Qassmy na Halima Ali Mohamed ambao hata hivyo, hawakuitikia wito huo na matokeo yake walivuliwa uanachama na kupoteza ubunge.

Wabunge 19 wa majimbo ambao pia wako kambi ya Maalim Seif,  kwa mujibu wa taarifa hiyo lilikuwa ni kundi la pili kuitwa kuhojiwa na kisha kufuatiwa na kundi la tatu ambalo ni viongozi wa ngazi za juu.

Mafuta ya Taa Yashuka....... Petrol, Dizeli Bei Juu

$
0
0
Mamlaka  ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya ya bidhaa za mafuta ya petroli nchini, ambapo kuanzia leo bei za rejareja za bidhaa hizo zimepanda kwa Sh 10 kwa lita, ikilinganishwa na bei iliyopita huku bei ya mafuta ya taa ikishuka.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Godwin Samwel, kuanzia Septemba mwaka huu, bei za rejareja za petroli na dizeli zimeongezeka kwa Sh 10 kwa lita sawa na ongezeko la asilimia 0.53 na Sh 57 kwa lita sawa na asilimia 3.10.

Hata hivyo, bei ya mafuta ya taa imepungua kwa Sh 19 kwa lita sawa na asilimia 1.04. 

Aidha, ilisema kuwa kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za petroli na dizeli, nazo zimeongezeka kwa Sh 10.41 kwa lita sawa na asilimia 0.56 na Sh 56.74 kwa lita sawa na asilimia 3.30.

Alisema kwa upande wa mafuta ya taa, bei ya bidhaa hiyo imepungua kwa Sh 10.01 kwa lita sawa na asilimia 1.11. 

Alifafanua kuwa ongezeko la bei za petroli na dizeli kwenye soko la ndani, limetokana na ongezeko la bei za mafuta hayo katika soko la dunia na ongezeko la gharama za usafirishaji wa mafuta hayo (BPS premiums).

Kupungua kwa bei ya mafuta ya taa kunatokana na kupungua kwa gharama za usafirishaji wa mafuta hayo, ijapokuwa bei ya mafuta hayo imeongezeka katika soko la dunia. 

Alieleza kuwa kutokana na mabadiliko hayo mapya ya bei za bidhaa za mafuta, bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote katika mkoa wa Tanga, nazo zimebadilika, ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe Agosti 2, mwaka huu.

Katika mkoa huo, kuanzia Septemba mwaka huu, bei za rejareja za petroli zimeshuka kwa Sh 13 kwa lita sawa na asilimia 0.65 wakati bei za Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa Sh 14 kwa lita sawa na asilimia 0.78 na Sh 106 kwa lita sawa na asilimia 6.21.

Aidha, bei za jumla za petroli zimeshuka kwa Sh12.98 kwa lita sawa na asilimia 0.69 wakati bei za dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa Sh 14.47 kwa lita sawa na asilimia 0.83 na Sh 105.88 kwa lita sawa na asilimia 6.65).

Samwel alifafanua kuwa kupanda na kushuka kwa bei za mafuta mkoani Tanga, kunatokana na mabadiliko ya bei za mafuta hayo katika soko la dunia na ongezeko la gharama za usafirishaji wa mafuta hayo.

Alisema vituo vyote vya mafuta, vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango, yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta.

Hashim Rungwe Anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Siku 4 sasa

$
0
0
Aliyekuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Hashim Rungwe anashikiliwa na polisi kwa siku nne sasa.

Rungwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Chaumma anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo anashikiliwa akituhumiwa kughushi nyaraka.

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema jana Septemba 5 kuwa, Rungwe anashikiliwa kituoni hapo kwa siku nne.

Hata hivyo, Kamanda Mambosasa hakutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo akisema hana taarifa za kutosha.

Waziri Mkuu Atoa ONYO Dosari Uaandaji wa Bajeti

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua mifumo miwili ya kielektroniki itakayosaidia kuandaa bajeti kwenye ngazi ya serikali za Mitaa huku akitoa onyo kali kwamba mifumo hiyo isitumike kukwamisha shughuli au utaratibu wa kazi za serikali .

Waziri Majaliwa amezindua mifumo hiyo jana  mjini Dodoma na kusema lengo la mifumo hiyo mipya ni kuongeza uwajibikaji na ufanisi na kamwe isiwe kikwazo katika utoaji wa huduma kwa jamii.

"Napenda kutumia fursa hii kuwafahamisha viongozi na watendaji pamoja na wananchi wote kwamba, lengo la matumizi ya mifumo ya TEHAMA ni kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi wa shughuli za serikali na isitumike kukwamisha shughuli au utaratibu wa kazi za serikali. Ni muhimu mifumo hiyo itumike kwa ufasaha ili kuleta tija inayotarajiwa na kila muhusika kwa ahakikishe anailinda, anaitunza na kuitumia mifumo hiyo ili iweze kudumu na kuwa endelevu kwa manufaa ya taifa", alisema Waziri Majaliwa.

Pia Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa mikoa na Halmashauri na vituo vya kutoa huduma za elimu na afya kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa mamlaka zinazohusika kwa wakati.

"Ngazi zote za mamlaka za serikali za mitaa zitoe taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi wanaowahudumia kupitia mikutano, mbao za matangazo, tovuti, vyombo vya habari na njia nyinginezo", alisisitiza Waziri Majaliwa.

Waziri Mkuu alisema kwa sasa serikali haitarajii kuona kituo chochote cha kutoa huduma za elimu na afya kilichopo chini ya Halmashauri kinakuwa na matumizi yasiyozingatia taratibu na kanuni za fedha za umma.

"Hatutarajii kuona viongozi wa mikoa na Halmashauri wakibadilisha matumizi ya fedha bila kuwasiliana na Mamlaka husika. Matumizi ya fedha yafanyike kutegemea chanzo cha fedha kilichopokelewa kwa wakati na kwa mujibu wa bajeti iliyotengwa kwa mwaka husika. 

"Serikali ina matarajio makubwa na mifumo hii, na nitapenda Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Ofisi yangu zipate taarifa zote za mipango, bajeti pamoja na taarifa za fedha zinazopelekwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa wakati na zikiwa katika ubora wa hali ya juu." alisema Waziri Majaliwa

Mifumo iliyozinduliwa jana ni mfumo wa kupanga mipango, kuandaa bajeti na kutolea taarifa za hatua za utekelezaji wa bajeti (Planning, Budgeting and Reporting System- PlanRep) pamoja na mfumo wa kufanya malipo na kutoa taarifa za fedha ambazo zimetumwa kwenye vituo vya kutoa huduma (Facility Financial Accounting and Reporting System-FFARS).

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Tatizo la Nguvu za Kiume Latua Bungeni

$
0
0
Sakata la upungufu wa nguvu za kiume ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa baadhi ya wanaume miaka ya sasa, limeibua sintofahamu bungeni baada ya mbunge wa Konde, Khatibu Saidi Haji (CUF) kutaka kujua serikali imejipanga vipi katika kukabiliana nalo.

Akijibu swali hilo Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangala amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema  serikali haina jibu la moja kwa moja kuweza kuwapa wananchi, kwani tendo la ndoa hufanyika faragha baina ya wanandoa.

Dkt. Kigwangala aliendelea kusema kwamba pamoja na usiri uliopo kuhusu tatizo hilo, lakini kuna vitu wanaweza kufanya ili kukabiliana nalo, ambapo huweza  likasaidia kuokoa ndoa yao na kuweza kuwapatia watoto.

"Nianze kukubaliana na Mhe. Hatibu Said Haji kwa swali la msingi, changamoto za ukosefu wa nguvu za kiume zinazowapata wanaume wengi sasa hivi, zinatokana na ukosefu wa furaha, msongamano wa mawazo na ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama kisukari, shinikizo la damu, ukiwa na matatizo haya huwezi kuwa na furaha katika tendo la ndoa", alisema Dkt. Kigwangala.

Naibu huyo wa Wizara inayohusika na masuala ya Afya aliendelea kwa kuwataka wananchi watafute furaha binafsi ili kuweza kuwa na hamasa ya kufanya jambo hilo, na kuacha kuamini kwenye dawa za asili ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela bila kuzingatia usalama wake kwa afya ya mtumiaji
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images