Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli alipongeza Jeshi la JWTZ kwa kutimiza miaka 53

$
0
0
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dk. John Magufuli amelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kutimiza miaka 53 tangu kuanzishwa kwake na kwa kutimiza wajibu wake jambo ambalo limeifanya Tanzania kuwa nchi ya amani.
  
Salamu za pongezi za Rais Magufuli amezitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika, “Nalipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kutimiza miaka 53 tangu kuanzishwa kwake. Kwa kipindi chote hiki Jeshi letu limeendelea kutimiza wajibu wake akiwa ni pamoja na kulinda amani ya nchi yetu kwa uzalendo, umahiri, ushupavu, uadilifu na nidhamu ya hali ya juu na hivyo kujijengea heshima ndani na nje ya nchi yetu. Najivunia kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa JWTZ. Mungu ibariki Tanzania, Mungu libariki Jeshi letu.”

Mahujaji walioshindwa kwenda ibada ya Hijja kurudishiwa pesa zao

$
0
0
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally amesema pesa za mahujaji wote walioshindwa kwenda katika ibada ya Hijja zitarejeshwa ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo.

Sheikh Zubeiry ameyasema hayo katika Baraza la Eid Al Adh’ha na kuwa amefanya uamuzi huo baada ya baadhi ya mahujaji kushindwa kwenda Hijja kutokana na taasisi zilizoandaa safari yao kushindwa kumamilisha taratibu zote zinazohitajika.

Sheikh Zubeiry amesema ataunda kamati maalumu ambayo itakuwa ikizifuatilia taasisi ambazo zinahusika na kusafirisha mahujaji kwenda katika ibada ya Hijja ambayo inafanyika katika mji wa Makkah na Madina.

“Nimekutana na wawakilishi wa taasisi hizo mara mbili na tumekubaliana kuwa pesa hizo zitarusishwa na zitatumika kufanya maandalizi kwa Hijja nyingine labda hii haikuwa bahati yao lakini Hijja ijayo watakwenda,” alisema Sheikh Zubeiry.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika Baraza la Eid,Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi aliwataka Watanzania kudumisha amani iliyopo nchini na kuishi kwa upendo bila kubaguana kwa itikadi za kidini au kikabila.

Mmoja wa Wabunge 8 wateule wa CUF amefariki Dunia

$
0
0
Mbunge Mteuliwa wa Viti Maalum wa Chama cha Wananchi (CUF), Bi. Hindu Hamis Mwenda amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambayaimeeleza kuwa Bi. Hindu alifariki dunia jana jioni akiwa Muhimbili alipokuwa akitibiwa baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kiongozi huyo hakuweka wazi kuwa Mbunge huyo mteule alikuwa akisumbuliwa na tatizo gani, lakini alisema taratibu nyingine za mazishi zitatolewa.

Bi Hindu alikuwa miongoni mwa wabunge 8 wapya wa CUF walioteuliwa na chama hicho kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wabunge waliofutwa uanachama.

Uteuzi huo ulitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Julai 27 mwaka huu na wabunge hao nane walikuwa wanatarajia kuapishwa juma lijalo wakati wa kuanza kwa vikao vya bunge mjini Dodoma.

Lowassa Ampa Pole Uhuru Kenyatta

$
0
0
Mjumbe wa kamati kuu ya (CHADEMA) na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amefunguka na kutoa pole kwa aliyekuwa Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta kufutia mahakama ya juu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi wa Urais uliofanyika Agosti 8, 2017.

Mhe. Edward Lowassa anasema yeye bado ataendelea kumuunga mkono Uhuru Kenyatta kwani ni kiongozi mwenye kusimamia Demokrasia na mwenye maono ambaye anaweza kuisadia Kenya hivyo ataendelea kumuunga mkono tena katika uchaguzi utaofanyika upya nchini humo.

"Nitumie nafasi hii kumpa pole Uhuru Kenyatta kwa jambo lililotokea lakini nimpongeze kwa kufanya kampeni ya kiume kafanya kazi nzuri sana, ukitazama maoni ya waangalizi mbalimbali walisema uchaguzi ulikuwa wa huru na haki, lakini pia ukitazama orodha ya washindi wa wabunge Jubilee ndiye inaongoza, kwa maseneta na magavana Jubilee ndiyo inaongoza picha hizi mbili zinatoa picha, lakini ikishasema mahakama maamuzi yake ni lazima yaheshimike" alisema Lowassa

Aidha Lowassa amesema kuwa anamuheshimu sana Uhuru Kenyatta kutokana na jinsi ambavyo anaheshimu Demokrasia na kudai katika kipindi cha uongozi chake siku zote amekuwa akilinda Demokrasia ya nchi hiyo kwani wabunge wamekuwa na haki na vyama vimekuwa na haki na kila mtu ana haki.

"Niliwahi kumsikia mama mmoja akimtukana Uhuru Kenyatta matusi ya nguoni kabisaa kiasi kwamba yule mama angekuwa hapa Tanzania siku nyingi angekuwa jela lakini Uhuru Kenyatta alimsamehe na maisha yakaendelea lakini uongozi wake ni uongozi wenye malengo amerithi nchi iliyotoka kwenye ugomvi wa kivita lakini ameweza kuingoza kwa miaka mitano kimya wakifanya maendeleo, na kwa maendeleo nadhani wametupita kwa sababu Uhuru Kenyatta kwa hiyo ni mtu mwenye upeo, makini na mahiri ambaye anaitakia mema Afrika na Afrika Mashariki" alisisitiza Lowassa

Rais Magufuli na Mkewe WASALI Kanisa la Wasabato Na Kuchangia Milioni 5 na Mifuko 400 ya Saruji

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli leo tarehe 02 Septemba, 2017 wameungana na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Usharika wa Magomeni Mwembechai Jijini Dar es Salaam kusali Ibada ya Sabato.

Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania, Baba Askofu Mark Walwa Malekana aliyekuwa pamoja na Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati, Baba Askofu Joseph Mgwabi na Askofu wa Jimbo la Kusini Mashariki, Baba Askofu Albert Nziku.

Akizungumza baada ya Ibada hiyo Mhe. Rais Magufuli amelipongeza Kanisa hilo kwa kutoa huduma ya kiroho kwa waumini wake na pia kutoa huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali nchini, na amewahakikishia waumini na viongozi wake kuwa Serikali inatambua mchango huo na itaendelea kushirikiana na madhehebu yote ya dini katika kuwahudumia wananchi.

“Baba Askofu nakushukuru sana kwa mahubiri mazuri ya leo ambayo yamenigusa sana, madhehebu ya dini likiwemo hili la Waadventista Wasabato mnatoa mchango mkubwa sana kwa Taifa letu, nakuhakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nanyi” Amesema Mhe. Rais Magufuli.

Pamoja na kushiriki Ibada hiyo Mhe. Rais Magufuli amechangia shilingi Milioni 5 na mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa jipya la Waadventista Wasabato Usharika wa Magomeni Mwembechai, amechangia Shilingi Milioni 1 kwa kwaya za Kanisa hilo na pia ameendesha harambee ya papo kwa papo ya kuchangia ujenzi wa Kanisa, na kufanikisha kupata Shilingi Milioni 25.3.

Baba Askofu Mark Walwa Malekana amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuungana na waumini wa Kanisa hilo katika Ibada ya Sabato na kuchangia ujenzi wa kanisa, na ameongoza maombi ya kuliombea Taifa na Rais.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Septemba, 2017

Balozi wa China Ammwagia Sifa Rais Magufuli.....Kadai Nchi Nyingi Duniani Zinatamani Kuwa na Rais Kama Yeye

$
0
0
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas amefunguka na kusema Balozi wa China nchini Tanzania anayemaliza muda wake Lu Youqing amedai nchi nyingi duniani zinatamani kuwa na Rais kama alivyo Dkt. John Pombe Magufuli kwa jinsi anavyoongoza nchi.

Dkt. Hassan Abbas amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema balozi huyo amesema siyo nchi za Afrika tu zinazotamani kupata kiongozi kama Magufuli bali ni dunia nzima inapenda kuwa na mtu kama Rais Magufuli.

"Balozi wa China anayemaliza muda wake Dkt Lu aguswa na vita ya kimageuzi ya Rais Magufuli. Asema atamkumbuka kama mmoja wa mashujaa Afrika amesisitiza kuwa si Afrika tu bali hata duniani, nchi nyingi zinatamani kuwa na Rais kama Dkt. John Pombe Magufuli amedai Serikali ya Tanzania tangu Nyerere mpaka Rais Magufuli inasifika duniani kwa mageuzi makubwa" alisema Dkt.Hassan Abbas

Uhuru Kenyatta Ampa ONYO Raila Odinga....Amtakaa Asahau Habari za Kubadili Tume

$
0
0
Aliyekuwa Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta amefunguka na kutoa onyo kwa mpinzani wake Raila Odinga kuwa asahu kuhusu tume mpya ya uchaguzi lakini pia amemtaka Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga kutoingilia kwani wao wameheshimu maamuzi ya mahakama

Uhuru Kenyatta amesema chama chake cha Jubilee kipo tayari kwa uchaguzi huo wa marudio na sasa wanasubiri Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC iweze kutangaza siku ya uchaguzi na wanaiomba itangaze siku hiyo haraka.

Aidha Uhuru Kenyatta amesema kuwa wapinzani hao hawana haja ya uchaguzi bali ni watu ambao wanataka serikali ya mseto kitu ambacho yeye hawezi kukiruhusu hata kidogo

Mahakama ya juu nchini Kenya Septemba 1, 2017 ilifuta matokeo ya Urais nchini Kenya na kuamuru kuwa uchaguzi mpya ufanyike katika nafasi ya Urais kutokana na mahakama hiyo kubaini baadhi ya mapungufu wakati wa utoaji wa matokeo hayo ya uchaguzi uliofanyika Agosti 8, 2017.

Mtazame hapa Uhuru Kenyatta akifunguka mengi zaidi

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Septemba 3


Waziri Mkuu Kesho kuzindua mfumo wa uandaaji bajeti

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Jumanne Septemba 5 atazindua mifumo miwili itakayosaidia kuongeza ufanisi na kupunguza gharama wakati wa ufuatiliaji na uandaaji wa bajeti nchini.

Katika uzinduzi huo, mawaziri sita ambao wanafanya kazi na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) watahudhuria.

Kiongozi wa timu ya rasilimali fedha, Dk Gemini Mtei amesema uzinduzi huo utahudhuriwa na Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene; Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango; Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (sera, bunge, kazi, vijana, na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama.

Ofisa Usimamizi Mwandamizi wa Fedha Tamisemi, Elisa Rwamingo amesema mfumo huo utatumika katika halmashauri zote 185. Amesema wakuu wa vitengo katika halmashauri wamepatiwa mafunzo ya utumiaji wa mfumo huo, ambao wataenda kuwafundisha watumishi wengine.

Waziri Makamba amlilia Muhingo Rweyemamu

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amemtaja mwandishi wa habari mkongwe, Muhingo Rweyemamu kuwa alikuwa mwalimu na mshauri wake wa karibu.

Mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha wageni waliohudhuria msiba wa mwandishi huyo nyumbani kwake Mbezi Luis, January alisema alifanya kazi na Muhingo kwa karibu wakati wa uongozi wa awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete. 
 
Muhingo amewahi kuwa mkuu wa wilaya tatu kwa vipindi tofauti; Handeni, Makete na Morogoro. 
 
“Namkumbuka kwa mambo mengi alikuwa ni mtu anayepen-da kuelimisha, alikuwa akinishauri hata kusoma vitabu vya kunisaidia kunipa mwongozo,” alisema. 
 
Alisisitiza kuwa anaamini wana tasnia ya habari watamuenzi
kwa kuendelea kuandika habari zenye weledi kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla. 
 
Kaka wa marehemu, Elisa Muhingo alisema kifo cha mdogo
wake ni pigo kubwa kwa familia kwa sababu alikuwa tegemeo lao. 

“Lakini kwa jinsi alivyougua, ameteseka kwa maumivu makali, kifo chake tusingeweza kukipinga. Tunamshukuru Mun-gu amempumzisha, tunatafakari na kujipanga kuishi bila yeye,” alisema.

 Aliyekuwa rafiki wa karibu wa marehemu ambaye pia ni mwandishi mkongwe, Absalom Kibanda alisema leo wanatarajia kuuhamisha mwili kutoka chumba cha maiti cha Hospitali ya Aga Khan alikofia na kuupeleka nyumbani kwake kwa maandal-izi ya maziko. 

“Baada ya kikao cha mashauriano, imekubaliwa kwamba Rweyemamu atazikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne, Septemba 5, 2017,” alisema. 
 
Alisema shughuli za mazishi zitatanguliwa na ibada ya kumuaga ambayo itafanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tan-zania (KKKT) Mbezi, Kibanda cha Mkaa.

Uwekezaji Morogoro wawaweka matatani raia watatu wa China

$
0
0
Siku moja baada ya agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa agizo kwa uongozi wa Mkoa wa Morogoro kufuatilia utendaji wa kampuni ya Zhong Fenq, umeviagiza vyombo vya ulinzi kuwakamata raia watatu wa China wanaodaiwa kuendesha shughuli za uwekezaji kinyume cha sheria.

Juzi, Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kwenda katika kijiji cha Maseyu kufuatilia utendaji wa kampuni hiyo kama inafuata sheria, kanuni na utaratibu. 

Dk Kebwe jana alitoa agizo kwa vyombo vya ulinzi kuwakamata raia hao na kuamuru warudishwe kwao mara moja baada ya kugundulika kujihusisha na uchimbaji wa madini ya kutengeneza marumaru bila kufuata utaratibu, kanuni na sheria za nchi.
 
Waziri mkuu alitoa agizo hilo kutokana na malalamiko ya mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba kuwa wawekezaji hao kutoka China wanaendesha shughuli za uchimbaji bila ya kuwa na kibali.
 
Mgumba alisema tangu mwaka 2011 wawekezaji hao wameendesha shughuli zao bila kulipa kodi za Serikali na tozo za halmashauri, hivyo kuikosesha Serikali mapato.

Mbunge huyo ambaye machimbo hayo yako jimboni kwake,
alisema licha ya uongozi wa mkoa kwenda eneo hilo na kuizuia kampuni kuendelea na uchimbaji hadi itakapopata vibali ilikaidi na kuendelea na shughuli zake.

Majaliwa alisema iwapo wahusika watabainika kuwa hawajafuata sheria, kanuni na utaratibu hatua zichukuliwe dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika eneo hilo chini ya ulinzi na kuwasiliana na ubalozi wa China nchini.

Akitoa agizo jana, Dk Kebwe alimtaka kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro na kamanda wa Uhamiaji wa mkoa kuhakikisha wanawakamata na kuwasafirisha    raia hao wa China hadi jijini Dar es Salaam  na utaratibu wa kuwaondoa nchini ufanyike  mara moja. 

“Nawaagiza kuhakikisha  mnaorodhesha vifaa na vitu vyote vilivyopo  katika mgodi huo,” alisema Dk Kebwe.
 

Raia hao wa China kwa sasa wanashikiliwa na polisi wakisubiri kukamilishwa  kwa utaratibu wa kuwarudisha kwao, huku  mali za mgodi huo zikiwa chini ya uangalizi  wa jeshi hilo.
 

Katika hatua nyingine, Dk Kebwe aliagiza  polisi kuwakamata mhasibu wa halmashauri  ya Wilaya ya Morogoro, ofisa biashara,  mtendaji wa kata ya Maseyu na mtendaji wa  kijiji hicho kwa kushindwa kutoa taarifa za  raia hao wa kigeni kuendelea na uchimbaji  huo.

Pia, Dk Kebwe alisema waliendelea kuwatoza kodi ya huduma hadi Juni mwaka huu  licha ya kujua kuwa hawana kibali.


Akizungumzia kuchelewa kuondoka kwa  Wachina hao, ofisa madini mkazi Mkoa wa  Morogoro, Bertha Luzabiko alisema mamlaka ya Wizara ya Nishati na Madini ndiyo  ilikuwa ikishughulikia suala lao.


Mkuu wa uhamiaji Mkoa wa Morogoro,  Safina Muhindi alisema mpaka sasa hajaona  pasipoti wala vibali vya kufanya kazi nchini  vya rais hao, hivyo ufuatiliaji unaendelea.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema walichofanya ni kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa la  kuwakamata
 

Mwaka 2016 mgodi huo ulizuiwa kufanya  shughuli za uchimbaji wa madini na uzalishaji wa marumaru baada ya kubainika kuwa  wawekezaji hao hawana vibali, huku bidhaa  zilizokuwa zikizalishwa na kampuni hiyo  zimekuwa zikiandikwa kuwa zinatengenezwa China. 

Imeelezwa uongozi wa mgodi  ulisitisha shughuli kwa muda na baadaye  ulirejea kuendelea na uzalishaji.

Kijana wa Miaka 18 Asimulia Jinsi Alivyowateka Watoto Wanne Arusha

$
0
0
Matukio ya utekaji watoto mjini Arusha yameanza kupata mwelekeo wa ufumbuzi baada ya kijana wa miaka 18 kukiri kuwateka watoto wanne alipokamatwa katika mji wa Katoro wilayani Geita alikofanya tukio jingine la utekaji.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari akiwa chini ya ulinzi wa polisi jana, kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Samson Petro alisema watoto wawili aliwarudisha kwa wazazi wao baada ya kupewa Sh300,000.

Alisema wengine wawili aliwatelekeza mtaani baada ya wazazi wao kutotoa kiasi cha fedha walichotakiwa kumpa.

Samson alisema alianza ‘shughuli’ hiyo ya utekaji watoto kutokana na mahitaji ya fedha na kwamba, aliacha shule akiwa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lutozo iliyopo Katoro.

“Naishi na wazazi wangu, lakini nao ni masikini, nilifanya hivi ili nipate fedha na nilikuwa nikimchukua mtoto naandika ujumbe kwenye karatasi, naandika na namba ya simu napeleka karibu na familia ili wanitafute,” alisema Samson.

Awali, kamanda wa polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema walimkamata kijana huyo katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu iliyopo mjini Katoro juzi saa mbili usiku.
 
Mwabulambo alisema polisi mkoani Geita kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha walifanya uchunguzi na kubaini mtuhumiwa alikuwa Katoro.

Alisema walipata taarifa za kutekwa Justin Ombeni (2) Septemba Mosi nyumbani kwao katika eneo la Shilabela ambako mtuhumiwa alikwenda na kuwakuta watoto wanne wakicheza nyuma ya nyumba.

Alisema aliwagawia pipi na kuondoka na Justin. Kamanda huyo alisema polisi ilipata taarifa kuwa kijana huyo yupo chumba namba 103 katika nyumba hiyo ya wageni ambako waliweka ulinzi kuizunguka.

Alisema walipoingia katika chumba hicho walimkuta akiwa na
mtoto huyo. Mwabulambo alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika. 

Ombeni Mshana ambaye ni baba wa Justin alisema mtekaji huyo alimpatia ujumbe mtoto wa jirani uliomtaka kutuma Sh4 milioni na walipokuwa wakiwasiliana na mtuhumiwa alishusha kiwango hadi Sh1 milioni. 

Alisema polisi walimtahadharisha kwamba asitume fedha hizo.Kamanda Mwabulambo alisema tukio la kutekwa Justin ni la pili katika kipindi cha miezi minne baada ya mwingine kutekwa. 
 
Kesi kuhusu tukio hilo la kwanza inaendelea mahakamani baada ya mtoto kupatikana.
 
Katika hatua nyingine, kikosi kilichoundwa na wananchi mkoani Arusha kikiongozwa na mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Kata ya Olasiti, Daudi Safari na familia za watoto wawili waliotekwa kimewakamata watuhumiwa wawili na kuwafikisha polisi.

Watoto hao ambao bado hawajapatikana ni Moureen David (6) anayesoma darasa la kwanza shule ya msingi Lucky Vincent na Ikram Salim (3).

Wakizungumza jana nje ya kituo kikuu cha polisi Arusha baada ya kuwafikisha kituoni watuhumiwa hao, Safari na wazazi wa watoto hao, David Njau na Salim Kassim walisema kwa nyakati tofauti wameanzisha msako baada ya
kuona siku zinakwenda bila watoto kupatikana.

Moureen alitekwa Agosti 21 saa 11 jioni akiwa anacheza nyumbani kwao eneo la Olasiti, wakati Ikram alitekwa Agosti 26 saa 12 jioni akiwa anacheza na watoto wenzake nyumbani kwao, Burka - Olasiti.

Safari alisema wamemkamata mtu mmoja (jina linahifadhiwa)
ambaye simu yake ilitumiwa na watekaji kuomba fedha kwa mzazi wa Ikram Salim.

Alisema pia wamemkamata wakala wa fedha wa kampuni moja ya simu (jina tunaihifadhi) aliyetoa Sh300,000 kwa watekaji baada ya fedha kutumwa na mzazi wa Ikram.

Imeelezwa kuwa wakala huyo amekamatwa kwa kuwa fedha hizo zilitolewa pasipo kuorodheshwa popote na mpokeaji hakuonyesha kitambulisho chochote.

Akizungumzia operesheni hiyo, Njau alisema hawatapumzika mpaka watoto wao wapatikane.
 
Alisema ufuatiliaji walioufanya kupitia minara ya kampuni za simu unaonyesha wahusika walikuwa eneo la Kwa Mrombo jijini Arusha walipopiga kuomba Sh4.5 milioni ili wamwachie Doreen na kiasi kingine kama hicho kwa ajili ya Ikram.

Watekaji hao kupitia ujumbe waliotuma nyumbani kwa Njau walidai kama wasipopewa fedha wangempoteza mtoto huyo japokuwa hawana nia hiyo.
 
Kassim Salim ambaye ni babu wa Ikram alisema, “tunaendelea kuomba msaada zaidi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na vyombo vya dola watusaidie tuwapate watoto wetu.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema juzi kuwa watu watatu wanashikiliwa wakihusishwa na tukio hilo akiwapo dereva wa bodaboda mkazi wa Olasiti aliyetumwa kuwarejesha watoto wawili waliokuwa wametekwa.

Matukio ya utekaji yalianza kuibuka Agosti 21 baada ya kutekwa watoto wanne. Watoto wawili Ayoub Fred na Bakati Selemani wakazi wa eneo la FFU, kata ya Murieti jirani na kata ya Olasiti walirejeshwa

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Septemba 4

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Septemba 5

Askari ya FFU akamatwa sakata la utekaji watoto

$
0
0
Wakati Mtuhumiwa wa matukio ya utekaji watoto, Samsom Petro (18), ambaye jana alifikishwa Arusha kwa ajili ya kuonyesha sehemu alipowaficha watoto, amebainika kuwa anaishi na kaka yake ambaye ni askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha mjini hapa.

Inadaiwa kuwa askari huyo pia anashikiliwa na polisi kwa mahojiano tangu Agosti 27 wakati kikosi maalum cha polisi kilipozingira nyumba aliyopanga.

Petro, ambaye alikamatwa juzi akiwa Katoro mkoani Geita, anatuhumiwa kuwateka watoto wawili, Moureen David(6) na Ikram Salim(3) na hadi jana jioni alikuwa ameandamana na polisi katika eneo la Njiro ambako alidai aliwatelekeza watoto hao.

Lina Kajuna ambaye ni mmiliki wa nyumba ya aliyekuwa amepanga askari huyo wa FFU, alisema ana miaka miwili tangu ampangishe.

Kajuna alisema mtuhumiwa wa utekaji, Samson Petro alifika Arusha mwezi Juni na amekuwa akiishi na kaka huyo na tangu amefika amekuwa akimuona kuwa na tabia ambazo sio nzuri, kama wizi wa kuku.

“Alipofika muda mfupi tulianza kuona matukio ya wizi nikaibiwa kuku na pesa mimi nikamlalamikia kaka yake lakini akasema tuendelee kumchunga,”alisema

Alisema baada ya hali ya wizi kuendelea, alikwenda kulalamika kwa balozi wa eneo wanaloishi ambalo ni Mtaa wa Olkeria, Daniel Kichau kutaka wamchunguze.
 
Hata hivyo, alisema wakati akichunguza, ndio matukio ya utekaji yakaanza na tangu Agosti 25 alitoweka nyumbani hadi jana walipopata taarifa kuwa amekamatwa.
 
Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Daudi Safari alisema jana kuwa kikosi chao cha wananchi walifika kwenye nyumba hiyo na kubaini alikuwa anaishi na askari huyo wa FFU .
 
“Tumemuhoji mama mwenye nyumba ametupa ushirikiano mkubwa na ni kweli Samson alikuwa anaishi kwenye nyumba yake na kaka yake ambaye alikamatwa tangu Agosti 27,” alisema.
 
Katika msako wa jana, polisi walikwenda peke yao na mtuhumiwa na kuwaacha wazazi wa watoto hao wakiwasubiri kituo kikuu cha polisi. Baadhi ya askari walisema wanaendelea na msako wa watoto hao

Yusuf Manji Atinga Mahakamani na Muonekano Mpya.....Polii Wapewa Onyo

$
0
0
Mfanyabiashara Yusuf Manji, anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, jana alitinga Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiwa na muonekano mwingine tofauti na wiki chache zilizopita.

Manji alionekana kuwa tofauti kwani alivaa suti nyeusi na kunyoa ndevu tofauti na siku nyingine ambako amekuwa akitinga mahakamani akiwa amevaa fulana nyeusi ya mikono mirefu na suruali ya ‘jeans’ rangi ya bluu huku akiwa na nywele pamoja na ndevu nyingi.

Mbali na kutinga akiwa ‘ametokelezea’  kwa kuvaa suti hiyo sambamba na tai shingoni na viatu vyeusi, mshtakiwa huyo pia alionekana kuwa amechangamka tofauti na siku nyingine.

Manji na wenzake watatu walifikishwa jana mahakamani hapo kwa hati ya kutolewa mahabusu kwa ajili ya kwenda kuhojiwa polisi.

Tayari, Mahakama imeruhusu Manji na wenzake kwenda kuhojiwa na polisi kuhusiana na kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili kwa lengo la kukamilisha upelelezi.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama kuwa waliomba hati ya kuwatoa washtakiwa mahabusu ili kufanyiwa mahojiano katika kesi namba 33/2017 na kwamba washtakiwa hao walikabidhiwa mikononi mwa polisi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alisema aliandikiwa barua na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO), akiomba washtakiwa hao waende wakahojiwe polisi.

Alisema Mahakama imekuwa ikisisitiza kesi za uhujumu uchumi zikamilishwe upelelezi ili ziweze kusikilizwa.

“Tusingeweza kukataa maombi hayo kwa sababu tutapingana na kauli yetu ya kukamilisha upelelezi. Ndiyo maana tumetoa hati ya kuwatoa mahabusu kwa ajili ya mahojiano na hii si mara ya kwanza kuwatoa washtakiwa mahabusu kwa ajili ya upelelezi,” alisema Hakimu Shaidi.

Hakimu Shaidi aliwataka polisi kuzingatia haki za washtakiwa kwa kuhakikisha wanakuwa na afya njema na wapate uhuru wa kuwakilishwa na mawakili wao kwenye jambo lolote na isiwe kificho.

Hakimu aliwakabidhi washtakiwa hao kwa Koplo Dotto kama barua inavyoelekeza kwa kuwa Sajenti Mkombozi ambaye alitakiwa kukabidhiwa hakuwepo. Washtakiwa hao wanatakiwa kurudishwa kesho (leo) katika muda wa kazi.

Mbali na Manji, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Deogratius Kisinda (28), Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43).

Akiwasilisha maombi hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi aliomba mahakama iruhusu washtakiwa wakabidhiwe kwa polisi ili kutimiza matakwa ya upelelezi.

Kishenyi alidai kwamba Kifungu cha 59 (1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kinawapa mamlaka polisi kufanya upelelezi.

Akijibu hoja hizo, wakili wa utetezi, Hudson Ndusyepo alidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri kama ilivyoombwa na upande wa mashtaka kwa sababu shauri hilo halijapata hati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuipa mamlaka kusikiliza shauri hilo.

Ndusyepo alidai kuwa mahakama hiyo imefungwa mikono ya kutoa amri dhidi ya maombi hayo.

Pia alidai kifungu cha sheria kilichotajwa na upande wa mashtaka, kinazungumzia ufanyaji wa upelelezi kwa ujumla.

Wakili mwingine wa utetezi, Hajra Mungula alidai kuwa washtakiwa hao wako chini ya ulinzi na kwamba upande wa mashtaka uliwashtaki huku ukijua kwamba haujakamilisha upelelezi na umetoa hati ya kuzuia dhamana.

“Tunaomba ombi hili likataliwe na upande wa mashtaka uelekezwe kuzingatia sheria na haki za washtakiwa,” alisema Mungula.

Hata hivyo, Wakili Kishenyi alisema Mahakama imekuwa ikisisitiza kukamilisha upelelezi na kwamba wanachofanya ni sehemu ya kuukamilisha.

Pia alidai kuwa washtakiwa hao wanayo haki ya kuwakilishwa hivyo maombi yao yakubaliwe.

Hakimu Shaidi alikubaliana na ombi la upande wa mashtaka na kuwaruhusu washtakiwa hao kwenda kuhojiwa.

Tundu Lissu Aikana Habari ya Kualikwa Kwenye Mkutano wa Wanasheria Bingwa Duniani

$
0
0
Rais wa  (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameikana taarifa inayosambaa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kuwa amealikwa kwenye Mkutano wa Mawakili Bingwa wa sheria nchini Marekani na kusema yeye mpaka sasa hajapata mwaliko huo.

Tundu Lissu alisema hayo  jana baada ya kutoka mahakamani katika kesi yake ya uchochezi ambapo alisema kuwa hata yeye anaona taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii na kusema hajapata huo mwaliko na kudai anasubiri.

"Mimi mwenyewe nimesikia nimealikwa sehemu fulani wakili pekee barani Afrika bado nausubiri huo mualiko sijauona bado ila nimeusikia mtandaoni, sijui watu ambao huwa wanasambaza uongo kama huu inawasaidia nini, mimi naona inanipandisha 'chat' nisizo stahili mimi nataka nipande 'chat' nazostahili " alisema Tundu Lissu

Katika taarifa hiyo ambayo imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii  ilikuwa inasema kuwa Mwanasheria huyo wa CHADEMA ni wakili pekeee kutoka barani Afrika ambaye atahudhuria Mkutano wa Mawakili Bingwa wa Sheria nchini Marekani utakaofanyika katika Jiji la Washington DC siku ya Ijumaa ya tarehe 15/09/2017

Wabunge wa Upinzani Wagoma Bungni na Kutoka Nje

$
0
0
Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni wamesusia kuapishwa kwa wabunge saba Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi (CUF) katika mkutano wa nane Bunge la 11 kwa madai hawakufurahishwa na maamuzi ya kufukuzwa wabunge 8 wa Viti Maalumu wa chama hicho.

Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania umeanza leo Mjini Dodoma na moja ya mambo yaliyopo kwenye ratiba ya mkutano huo ni kuapishwa kwa wabunge wapya 8 wa Viti Maalumu ambao wameteuliwa kuziba nafasi za wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofutwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba baada ya kupoteza sifa ya kuwa wabunge.

Wabunge ambao wamekula kiapo cha uaminifu siku ya leo Septemba 5 ni pamoja na  Alfredina Kaigi, Kiza Mayeye, Nuru Bafadhili, Rukia Kassim, Shamsia Mtamba, Sonia Magogo na Zainab Amir.

Aidha, CUF kimewaapisha wabunge saba badala ya nane kama inavyotakiwa kutokana na mbunge mmoja mteule Hindu Mwenda kufariki siku ya Ijumaa Septemba Mosi  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kwa upande mwingine, wabunge wa upinzani waliingia bungeni baada ya wabunge hao kumaliza kuapishwa na Spika Job Ndugai.

Tume Ya Uchaguzi Kenya Yatangaza Tarehe ya Uchaguzi wa Rais

$
0
0
Tume huru ya uchaguzi nchini Kenya IEBC imetangaza rasmi tarehe ya uchaguzi wa urais, ambao utakuwa wa marudio baada ya Mahakama kuufuta wa awali

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tume hiyo kwa vyombo vya habari kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo wa twitter, IEBC imesema Oktoba 17 ndiyo tarehe rasmi ya kufanyika uchaguzi huo.

"Uchaguzi mpya utafanyika Oktoba 17 mwaka 2017, kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu wa kufuta uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 8, 2017, hakutakuwa na wagombea wapya, wagombea ni Raila Odinga na mwenzake Kalonzo Musyoka, pia Uhuru Kenyatta na mwenzake William Ruto", iliandika taarifa hiyo.

Uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika ndani ya siku 60 tangu uamuzi wa Mahakama ya juu wa kuufuta ule wa awali kutolewa, Septemba 1 mwaka huu.

Mwijage Kutua India Kuisafisha Tanzania

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage  amekiri kupokea wito wa kwenda nchini India kwa ajili ya kusafisha jina la Tanzani baada ya watu wanaodaiwa ni madalali tapeli wa zao korosho kulichafua.

Mh. Mwijage ameyasema hayo jana ambapo amedai kuwa anaoushahidi  kuwa kampuni hizo za udalali zilichafua jina la nchi hivyo ni lazima awafikishe katika mikono yua sheria.

“Vitendo hivi vinavyofanywa na makampuni haya havivumiliki kwani mchezo huu ni mauti kwetu na nitahakikisha wanachukuliwa hatua kwani ninao ushahidi unaotosheleza,”alisema Mwijage.

Mh. Mwijage amefafanua kwa kusema kwamba watu wametapeliwa kwa kuambiwa pindi wanapoagiza mazao watoe pesa ya kianzio ambayo ni kuanzia dola za Marekani 123,000, sawa na Sh275 milioni na dola 200,000 sawa na Sh448milioni za kitanzania.

“Nimepokea wito kutoka India kwa ajili ya kwenda kusafisha jina la nchi kutokana na taswira iliyosababishwa na uwepo wa matapeli hao,”alisema Mwijage.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>