Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Maalim Seif aitaka jumuiya ya kimataifa kuiwekea vikwazo Tanzania

$
0
0

Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kujaza nafasi nane za ubunge wa viti maalumu za CUF, kambi ya katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad imesema bado inawatambua wabunge waliovuliwa uanachama na kambi pinzani na kutaka jumuiya ya kimataifa iiwekee vikwazo Tanzania.

Kambi inayoongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba, ambayo inatambuliwa na vyombo vya Serikali, ilitangaza kuwavua uanachama wabunge wanane wa viti maalumu kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

Waliopoteza ubunge ni Halima Ali Mohamed, Khadija Salum Ally, Salma Mohamed Mwassa, Miza Bakari Haji, Rais Abdallah Mussa, Riziki Shahari Mngwali, Saumu Heri Sakala na Severina Mwijage.

Siku moja baada ya kambi ya Lipumba kupeleka majina hayo, Spika wa Bunge alikubaliana na uamuzi huo na kutangaza nafasi hizo kuwa wazi na siku iliyofuata Tume ya Uchaguzi ikatangaza wabunge wapya, uamuzi “wa mwendokasi” ambao umeishangaza kambi ya Maalim Seif ambayo imeupinga.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha dharura cha Baraza Kuu kilichofanyika ofisi ndogo za CUF zilizopo Vuga mjini Zanzibar, Maalim Seif alisema kwa mujibu wa katiba na kanuni za CUF wanachama hao bado ni wabunge.

Alisema kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe 45 kati ya 52.

Katibu mkuu huyo alisema wabunge hao wataendelea na wadhifa huo kwa kuwa waliteuliwa na vikao halali vya Baraza Kuu lililo upande wake, ambalo ndilo halali kwa mujibu wa katiba na sheria za CUF.

Pia, alisema baraza hilo lina wajumbe 52, na kati yao 25 wanatoka Tanzania Bara na 27 wanatoka Zanzibar na litakuwa hai hadi mwaka 2019. 

“Baraza Kuu la uongozi halijakutana mahali popote Jumapili Julai 23 na kufanya uamuzi wowote wa kuwafukuza uanachama wabunge wanane na madiwani wawili wa CUF kama inavyodaiwa na mtu anayeitwa Ibrahim Lipumba na kikundi chake,” alisema Maalim Seif.

Maalim Seif alisema kufukuzwa kwa wabunge na madiwani hao si mpango wa Lipumba pekee, bali ni mpango kabambe uliosukwa na dola kwa kushirikiana naye.

Alisema ushahidi wa hilo ni kufukuzwa kwao na Lipumba ambaye ni mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na papo hapo Spika wa Bunge kuridhia na NEC kutangaza majina ya wateule wa kujaza nafasi hizo.

“Baraza Kuu limeshangazwa na hatua ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kujifedhehesha na kujiaibisha kwa kusema uongo kwa Watanzania kwamba eti alijiridhisha kwamba wabunge hao wanane wamefukuzwa uanachama na chama chao na kudai kuwa tayari wamekosa sifa za kuendelea kuwa wabunge,” alisema Maalim Seif.

Maalim Seif alisema kutokana na hali hiyo ni vyema Spika akajiuzulu kutokana na kwenda kinyume cha utaratibu wa uendeshaji wa Bunge.

Alisema baraza hilo limemtaka kuandika barua kwa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), katibu wa umoja wa mabunge ya jumuiya ya Madola (CPA), katibu wa umoja wa mabunge ya duniani (IPU) kuhusu suala hilo.

Kuhusu NEC, alisema ni dhahiri imezidi kupoteza sifa na kujionyesha wazi kuwa haipo huru.

“Hata kama hawa wabunge wangekuwa wamefukuzwa kweli na baraza linalotambulika, lazima tume ifuate utaratibu uliopo kwa kuchukua orodha ya majina ya watu iliyowasilishwa ofisini kwake mwaka 2015 kujaza nafasi za uteuzi, orodha yetu ipo halali mbona hawa walioteuliwa hawamo ndani ya orodha yetu,” alihoji Maalim Seif.

Waliopitishwa na NEC ni Rukia Ahmed Kassim, Shamsia Aziz Mtamba, Kiza Hussein Mayeye, Zainabu Mndolwa Amir, Hindu Hamis Mwenda, Sonia Jumaa Magogo, Alfredia Apolinary Kahigi na Nuru Awadh Bafadhili.

Alisema kutokana na kuvunjwa katiba na sheria za nchi zilizopo ni vyema sasa jumuiya ya kimataifa ikasitisha misaada kwa Serikali ya Tanzania hadi hapo itakapokuwa tayari kufuata Katiba na hasa katika masuala ya siasa.

Alisema vitendo vinavyofanyika ni dhahiri vinaonyesha kuwepo dhuluma na udhalilishaji wa demokrasia kwa vyama vya upinzani.

“Baraza la uongozi linaunga mkono wito uliotolewa na Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) na mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu kwa jumuiya ya kimataifa kuibana Tanzania kwa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kuitenga kisiasa na kidiplomasia hadi hapo watawala watakapoamua kuheshimu katiba, sheria, misingi ya kidemokrasia na haki za binadamu na utawala bora,” alisema Maalim Seif.

Maalim Seif alisema anajiamini na yupo tayari kukamatwa kama utawala ukiona aliyosema hayafurahishi.

Alisema kukaa jela itakuwa si mara ya kwanza, akidai kuwa ameshawahi kukaa na wala haikuwa kitu, hivyo akipelekwa tena itakuwa ni kama jambo la kawaida tu kwa upande wake.

Korea Kaskazini Yafanya Jaribio la PIli la Kombora la Masafa Marefu.......Kombora Hilo Linauwezo wa Kutua na Kushambulia New York, Marekani

$
0
0
Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanya jaribio la kombora lake la  pili la masafa marefu ICBM, huku ikitoa onyo kali kwa Marekani kuwa inauwezo wa kushambulia eneo lolote lililopo nchini humo.

Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amesema kuwa jaribio hilo limebaini kuwa Marekani yote ipo katika rada ya Korea Kakazini na sasa inaweza kushambuliwa wakati wowote kwa makombora hayo.

Aidha, Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa jaribio hilo ni la kijinga na ni kitendo cha kichokozi na cha hatari kilichotekelezwa na utawala wa Korea Kaskazini, ambapo ameongeza kuwa hali kama hiyo isipodhibitiwa inaweza kusababisha athari kubwa kwa jamii.

Kombora hilo lilionekana kuwa na nguvu zaidi kuliko lile la kwanza.

Kombora hilo lililoanguka karibu na ufuo wa Japan limeshutumiwa kimataifa huku Rais Donat Trump akisema jaribio hilo lilifanywa kiholela na ni hatari.

Kombora hilo lilionekana kuwa na nguvu zaidi kuliko lile lililojaribiwa mapema mwezi huu kwa kuwa lilikuwa angani kwa zaidi ya dakika 47, kulingana na taarifa zilizotolewa na Pyongyang na ambapo lilienda kwa mwendo wa kilomita 1,000. Lilidondoka karibu na Ufuo wa Japan.

Vikosi vya kijeshi vya Marekani na Korea Kusini vilivanya zoezi la kijeshi kwa pamoja ambapo makombora kadhaa yalilipuliwa na wizara ya ulinzi kutangaza kuwa silaha maalumu zitawekwa nchini humo. 

Muda mfupi baada ya jaribio hilo, Korea Kusini, Japan na Maafisa wa Marekani waliripoti data kuhusu eneo na umbali, pamoja na muda uliochukuliwa na kombora hilo.

==>Ijapokuwa tathmini kamili haijakamilishwa, vitu kadhaa vilibainika.
Kwanza, data iliyopo inaonyesha kuwa kombora hilo lina uwezo wa kuruka umbali wa kilomita 10,400.

Kombora hilo linaweza kurushwa na kufika mji wa New York.

Pili Marekani iliripoti kwamba Korea Kaskazini ilirusha kombora hilo kutoka Mupyong -ni Korea Kaskazini.

Eneo hilo lilikuwa tofauti ikilinganishwa na taarifa za awali ambazo zilifanikisha jaribio yaliotabiri kurushwa kwa kombora la Kusong.

Hata hivyo, China imeshutumu jaribio hilo huku ikitaka pande zote zinazoshutumiana kuvumiliana na kutoendelea na majaribio hayo kwani yanaweza kusababisha madhara makubwa na kuhatarisha usalama wa eneo husika.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 31

NEC yatoa ufafanuzi kuhusu uteuzi wa wabunge CUF

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefafanua juu ya uteuzi wa wabunge wapya wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi (CUF).

Imesema kuwa imesikitishwa na kushangazwa na taarifa za Baraza Kuu la Taifa la chama hicho kwamba tume hiyo imekiuka kanuni zake katika uteuzi wa wabunge wanane wa chama hicho ili kujaza nafasi za wazi zilizotokea hivi karibuni.

Aidha, imesema chama husika kilipewa fursa ya kupendekeza na kilifanya hivyo, kabla ya NEC kuanika majina ya wabunge wapya wa CUF katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yamo katika taarifa ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani aliyoitoa jana jioni, akizungumzia tuhuma dhidi ya tume hiyo, inayodaiwa kukiuka kanuni katika uteuzi wa wabunge wanane wa viti maalumu wa CUF.

Sehemu ya Taarifa ya CUF katika mitandao ya kijamii inayoituhumu NEC inasema; “Kanuni walizojiwekea wenyewe Tume katika uteuzi wa watu wa kujaza nafasi hizo zinasema uteuzi huo unafuata mpangilio wa majina, kama ulivyokuwa umewasilishwa na chama husika wakati wa uteuzi wa wagombea wa ubunge wa viti maalumu wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

“CUF ilipeleka orodha yake ambayo haihusishi majina yaliyotangazwa, hivyo ndiyo kusema hata kama hicho kinachoitwa kufukuzwa uanachama wabunge hao kingekuwa halali (jambo ambalo si halali kama ilivyokwishaelezwa hapo juu), basi kwa Kanuni za Tume yenyewe, watu wa kujaza nafasi hizo wasingekuwa hao waliotangazwa.”

Kailima, katika taarifa yake, alisema taarifa zinazotolewa katika mitandao zikihusisha NEC kukihujumu chama hicho ni za kushangaza na kwamba Baraza Kuu la Uongozi la CUF, linataka kuupotosha umma kuhusu utekelezaji wa kazi za Tume.

“Chama husika ndicho kinaweza kujua ni nani siyo mwanachama wa chama hicho kwa kipindi cha kujaza nafasi wazi inapotokea,” alieleza Kailima na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa majina manane yaliyopendekezwa na CUF kujaza nafasi wazi za wabunge wa viti maalumu ni miongoni mwa majina 55 yaliyowasilishwa na chama hicho kwa barua yenye kumbukumbu Namba CUF/AK/DSM/ KM/003/1A/2015/14 ya Septemba 28, 2015 iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.

Waziri Mkuu awaonya madiwani Kyela.....Awapa siku mbili kumaliza tofauti zao, Vinginevyo Atalivunja Baraza Hilo

$
0
0
Serikali imewapa siku mbili Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya kumaliza tofauti zao zinazokwamisha utendaji wa Halmashauri hiyo na kuendelea kufanya kazi walizotumwa na wananchi.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa jana Julai 29, 2017 wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya.

“Baraza la Madiwani limegawanyika,mnamgogoro tunataka uishe na mshirikiane na mshikamane katika kufanya shughuli za maendeleo ili wananchi waweze kupata manufaa. Mkiendeleza migongano hatutawavumilia Serikali inauwezo wa tutalivunja baraza.”

Majaliwa amesema ikifika Jumatatu Julai 31, 2017 Madiwani hao wawe wamemaliza tofauti zao na wawaite wakuu wa Idara na kuwapa taarifa hiyo ili shughuli za maendeleo ziendelee kutekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo.

Tofauti hizo ambazo zimedumu kwa takriban mwaka mmoja zimesababisha Madiwani hao kushindwa kufanya vikao jambo linalokwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi katika Halmashauri hiyo.

Amesema baadhi ya Madiwani hao wanawatetea watumishi waliosimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiibia Serikali mabilioni ya fedha jambo ambalo halikubaliki na halivumiliki. “Naombeni mmalize tofauti zenu mara moja kabla sijaondoka.”

Aidha, Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya kuhakikisha watumishi wote waliohusika katika kula fedha za umma wanachukuliwa hatua kama alivyopendekeza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG).

Jeshi la Polisi Dar lakamata vifaa mbalimbali vya magari na Wezi 73

$
0
0
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, limewakamata watuhumiwa 73 wa wizi wa magari pamoja na vifaa vya magari katika oparesheni yake maalum inayolenga kuwakamata wezi na wanunuzi wa vifaa vya magari.

Taarifa ya jeshi hilo, iliyotolewa jana na Kaimu kamanda wa Polisi kanda maalum Dar es Salaam, (DCP) L. J Mkondya inaeleza kuwa tarehe 21/07/2017 walifanikiwa kuwakamata wezi wa vifaa mbalimbali vya magari, ikiwa ni pamoja na wanunuzi wa vifaa hivyo katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.

Katika Operesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 73 wamekamatwa baada ya kupekuliwa walikutwa na vifaa mbalimbali vya magari ikiwemo, Side mirrors, taa za gari, bampas, left pump, milango ya magari, vitasa vya magari, power windows, radio, injector pump, starer na seat cover.

Watuhumiwa waliokamatwa katika mkoa wa kipolisi Kinondoni ni 29, Ilala 33 na Mkoa wa kipolisi Temeke ni 11, watuhumiwa hao walishindwa kuvitolea maelezo vifaa hivyo, na kuwa upelelezi bado unaendelea ili kubaini mtandao unaojihusisha na wizi huo ambapo watafikishwa mahakami mara tuu uchunguzi utakapo kamilika.

Kwa ujumla vifaa vyote vilivyo kamatwa ni, Radio 12, Taa za magari aina mbalimbali 105, side mirrors 92, vitasa vya gari 109, switch 7, Bampa 4, Left Pump 3, Air Cleaner 1, Booster 3, Show grill, Mashine ya kupandishia vioo 1 na Tyre used 2.

Waziri Mkuu Azindua Meli mbili zilizonunuliwa na Serikali Mkoani Mbeya

$
0
0
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa amezindua Meli mbili za mizigo za Mv Njombe na Mv Ruvuma zitakazotumika katika kusafirishia mizigo kwenye Ziwa Nyasa na kuonya kwamba zisitumike kama eneo la kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya.

Amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Meli hizo zilizogharimu sh. bilioni 11.253 ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli alizozitoa ikiwa na lengo la kutatua changamoto ya usafiri wa abiria na mizigo katika Ziwa Nyasa.

Amesema kuwa ni jambo la faraja na la kujivunia kwa Serikali na wananchi kwa pamoja kushuhudia meli zilizotengenezwa na Mtanzania, zikiwa zimekamilika tayari kwa kuanza kazi ya kuwahudumia wananchi, ambapo awali suala hilo lilikuwa likifanywa na raia wa kigeni.

Waziri Mkuu amezindua meli hizo zilizojengwa na kampuni ya Kitanzania ya M/S Songoro  Marine Transport  jana katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya.

Aidha, alisema kuwa Meli hizo zitumike katika kukuza uchumi wa wananchi kwa kusafirisha mizigo na biashara halali kati ya nchi za Tanzania na Malawi na zisitumike kama eneo la kuingiza wahamiaji haramu pamoja na dawa za kulevya nchini.

“Changamoto ya usafiri wa mizigo katika ziwa Nyasa itakuwa historia kwani meli hizi zitarahisisha usafiri na kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania nan chi za Malawi na Msumbiji, hivyo tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kutoa ahadi hii ambayo leo utekelezaji wake umekamilika.”

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Karim Mataka alisema kuwa ujenzi wa meli hizo ulianza Juni 2015 na zina uwezo wa kubeba tani 1,000 za mizigo kwa kila moja.

Uwanja wa Ndege Songwe Chupuchupu Kuungua

$
0
0
Taharuki imewakumba wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (Sia) mkoani Mbeya na wananchi wanaofanya shughuli kando mwa barabara kuu ya Tanzania -Zambia baada ya moto kuwaka ndani ya eneo la uwanja huo.

Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika ulitokea jana mchana na kaimu meneja wa uwanja huo, Jordan Mchami alisema iliwachukua takriban nusu saa kuuzima.

Alisema moto huo ulianzia katika eneo la barabara kuu ya Tanzania - Zambia umbali wa mita 600 kutoka maeneo yalipo majengo na eneo la kurukia ndege.

“Tumefanikiwa kuuzima, hakuna madhara yoyote katika eneo letu na si sahihi kusema uwanja umeungua. Ifahamike kwamba uwanja huu una eneo kubwa ambalo ni kama vile pori tu. Moto umetokea barabara kuu ya Tanzania -Zambia umbali wa mita 600 hivi hadi tulipo sisi,” alisema baada ya kuenea taarifa katika mitandao ya kijamii na maeneo ya jirani kwamba uwanja huo umewaka moto.

Alipoulizwa kuhusu cha moto huo Mchami alisema ulionekana kuanzia barabarani na walipofuatilia kwa kuwauliza kina mama wanaofanya biashara ndogondogo kando mwa barabara hiyo waliambiwa kuwa waliona lori lililokuwa limeegeshwa eneo ulikoanzia hivyo wanahisi huenda mtu au watu waliokuwa katika gari hilo walirusha kipande cha sigara na kusababisha nyasi kuwaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mpinga alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, simu yake ilipokewa na msaidizi wake aliyesema kamanda yupo kwenye msafara wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Hata hivyo, taarifa za ofisa mmoja wa polisi aliyekuwapo eneo la tukio ambaye aliomba jina lake lisiandikwe  kwa kuwa si msemaji alisema, “Tumefanikiwa kuuzima moto ambao ulienea eneo kubwa. Tunashukuru haukuweza kufika maeneo ya kurukia ndege au kuharibu mali za uwanja huu.”

Uwanja huo umeongeza wigo wa fursa za kibiashara na kurahisisha huduma za usafiri wa anga kwa wakazi wa Mbeya, huku ukianza kuunganisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na maeneo mengine duniani.

Kadri siku zinavyokwenda, watu kutoka nchi jirani za Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Malawi wamekuwa wakiutumia uwanja huo.

Wageni hao ambao huingia nchini kwa ajili ya shughuli za biashara na utalii, wamezidi kuifungua kibiashara mikoa ya Songwe na Mbeya na kuonyesha ishara chanya kuwa uwanja huo unaelekea kuwa kitovu cha biashara kati ya Tanzania na nchi za kusini mwa Afrika.


Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Gazi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Jipatie Dawa za Asili za Kuongeza Maumbile, Nguvu za Kiume......Kuondoa Mvi na Mkanda kwa Ajili ya Kupunguza Tumbo

$
0
0
OFFER Ya punguzo la %10 kwa kila product zetu.
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na maumbile kuwa madogo ni kwa watu wengi sana.
 
Lakin NATURAL BEAUTY imepata uvumbuzi wa matatizo hayo na tiba zake zilizotengenezwa kwa mimea na matunda hazina kemiko wala madhara yoyote. Pia bidhaa zetu zote ni guarantee na risiti.
 
Pata bidhaa hizi uweze kufurahia matokeo mazuri.
Tunazo za÷👇👇
   🥝🥑🥒🧀🍉🍅🍓🍇
1.HANDSOME UP ni kifaa kinachoongeza maumbile ya kiume  kwa 99% kwa size uipendayo wewe na kuimarisha misuli ya uume kifaa hiki kinapatikana kwa @200,000/= tuu. 
 
2. MAX MAN PILLS 60. Hii ni maxman mpya kabisa yenye vidonge 60 na sasa inasambazwa na kampuni ya NATURAL BEAUTY Inapatikana kwa @170,000/=
 
3.MEN GELY YA KUPAKA. Hii inaongeza kwa wastani wa inch 6.5 na inapatikana kwa @130,000/=.  
 
4. SHARK POWER. Hii pia ni kwa ajili ya kuongeza maumbile  wastani wa inch 7.5 kutoka size uliopo inapatikana kwa @140,000/=.
 
5. MAX MAN 2. Ni vidonge kwa ajili ya nguvu ambavyo vinasaidia sana hata kwa watu wenye kisukari na waliokua wakifanya sana master blashion. Pia huongeza hamu ya tendo la ndoa inapatikana kwa @140,000/=
 
6.DISCREET. Hii ni ya kuondoa mvi na zisiludi tena milele inapatikana kwa @130,000/=
 
🍅🍇🍉🍅🍍🍓🥒🥑🍒
Tupo DAR ES SALAAM  kariakoo na kinondoni kanisani.
Kwa mawasiliano zaidi piga  0759029968 au 0659618585. 
 
Popote ulipo utapata huduma zetu.
Pia bidhaa zetu zote ni guarantee na hakikisha ununuapo bidhaa kampuni hii unapewa risiti harisi ya natural beauty
 
Follow us Instagram
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
                            Karibu

Waziri Mkuu Atoa ONYO Kwa Wapiga Dili

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya kwenda nchi za nje hivyo ameagiza ulinzi uimarishwe katika mipaka yote ya nchi na kuwa wale watakaobainika watachukuliwa hatua kali.

Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa kituo cha forodha cha Kasumulu kilichopo mpakani mwa Tanzania na Malawi wilayani Kyela,.

Amesema kuwa kunatabia ya baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kuitumia Tanzania kama njia ya kupitisha dawa za kulevya kwa ajili ya kupeleka nchi za  Afrika ya Kusini, Malawi na Zambia.

“Endeleeni kufanya upekuzi wa kina wa magari, watu na mizigo yote yote katika mipaka yetu. Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya na Serikali haitakubaliana na jambo hilo.”

Aidha, Majaliwa amewataka viongozi hao kuhakikisha biashara zote za magendo zinazofanyika mipakani, zikiwemo za kubadilisha fedha zinadhibitiwa kwa kuwa zinaikosesha Serikali mapato.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ni vema yakawepo maduka ya kubadilishia fedha katika maeneo hayo ili kudhibiti biashara hiyo ambayo kwa sasa inafanywa kimagendo huku Serikali ikikosa kodi.

Sakaya Amvaa Maalim Seif

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya, amesema kuwa maamuzi ya kukurupuka yanayofanywa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad yanaonyesha ni namna gani kiongozi huyo anavyopungukiwa na uwezo wa kufikiri.

Amesema kuwa, Maalim Seif kwa sasa hajielewi kwani CUF inaendeshwa kwa kufuata misingi ya Katiba ya chama hicho si kama Maalim anavyofikiria kukiongoza chama hicho cha upinzani.

Ameyasema hayo mara baada ya kikao kinachodaiwa kuwa cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la chama hicho kilichofanyika mjini Unguja na kuwafukuza wanachama saba wa chama hicho akiwemo Sakaya.

“Naona sasa uwezo wa kufikiri wa Maalim Seif unazidi kupungua, sijui sasa anafukuza watu kwa mara ya ngapi, hajui anachokifanya kwa sasa, kila siku amekuwa akikurupuka tu katika kutoa maamuzi,”amesema Sakaya.

Hata hivyo, amesema kuwa CUF ni chama kimoja chenye Mwenyekiti na Katibu mmoja huku manaibu katibu wakuu wakiwa wawili na kila maamuzi yanafanyika kwa kufuata Katiba ya chama hicho.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya July 31

CHADEMA Kutoa Tamko Zito Leo

$
0
0
Kamati Kuu ya CHADEMA   imekutana kwa siku mbili, tarehe 29 hadi 30 Julai, 2017 katika Hotel ya Double Tree, jijini Dar es Salaam kujadili hali ya siasa nchini pamoja na ukandamizwaji wa demokrasia .

Taarifa iliyotolewa  jana  na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema inasema kwamba katika mambo ambayo Kamati Kuu imejadili ni pamoja na kamata kamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA maeneo mbalimbali nchi nzima.

Hata hivyo kikao hicho kilijadili na kufikia maadhimio na hatua za kuchukua katika ajenda  ambapo ni pamoja na  kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha kwa watanzania, ambapo  taarifa kamili juu ya maadhimio hayo na hatua zitakazochukuliwa na chama itatolewa leo  Jumatatu tarehe 31 Julai 2017, kwenye kikao na waandishi wa habari kitakachofanyika jijini Dar es salaam.

Punyeto Ilisababisha Ninusurike Kwenda Jela

$
0
0
Mimi ni kijana  mwenye  umri  wa  miaka  32.Tabia ya  kujichua  ilisababisha  nisurike  kwenda  jela.

Ni  hivi, nilianza  kujihusisha  na tabia  ya kujichua mwaka  2004  nikiwa  na umri  wa  miaka  19.

Tofauti  na  vijana  wenzangu, mimi  niliingia  kwenye  tabia  ya  kujichua  sio  kwa  sababu  ya  kukosa  msichana, la  hasha  ila  kwa  sababu, nilikuwa  naogopa  sana  ukimwi

Niliamini  kujichua  ndio  njia  pekee  na  ya  uhakika  ambayo  ingeniepusha  na hatari  ya  kupata  maambukizi  ya  virusi.
Kabla  ya  kuanza  kujichua  tayari  nilikuwa katika  mahusiano  ya kimapenzi  na  wasichana  kadhaa.

Baada  ya  kujaribu  kujichua, nikawa  addicted. Kujichua  ikawa  ndio  mchezo wangu wa  kila  siku .

 Ilifikia  kipindi  nikawa  najichua  asubuhi  mara  tatu na  usiku najichua  pia.

Kama  ikitokea  mida ya  mchana  nimepata  sababu  ya  kujichua,na  nipo  maeneo ya  karibu  na  nyumbani, basi  nitaenda  chumbani  fasta, na  kama  nikiona  mazingira  hayaruhusu nitazuga  kama  naenda  kuoga  na  nikiwa  bafuni  namaliza  shughuli  huko  huko.

Pamoja  na  kwamba  nilikuwa  najichua, lakini  pia  ilikuwa  ikitokea  nikipata  msichana  ninakuwa  nae.

Pamoja  na  yote  hayo  cha  ajabu ni kwamba, hata  kama  nimetembea  na  msichana  siku  hiyo, usiku  lazima  nijichue.

 Ilikuwa  haiwezi kupita  siku    bila  kujichua.Niliendelea  na  tabia  hii  hata  nilipokuwa  chuo.

Wakati  nipo  chuo, mara  nyingi  nilikuwa  nachelewa  vipindi  vya  asubuhi, kwa  sababu  ilikuwa  ikifika  asubuhi ilikuwa ni  lazima  nijichue  na  nisingeweza  kufanya  hivyo mbele  ya  room mates  wangu, na  nisingeweza  kwenda  kufanyia bafuni  kwa  sababu  bafuni kulikuwa  na  foleni mida  hiyo  ya  asubuhi plus  mabafu yalikuwa  hayana  milango , so nikawa  nasubiria  roommates  waondoke  kwanza ili nijichue  kwanza, kisha  baada  ya  hapo ndio  niende darasani.

Wakati mwingine  nilikuwa  najichua  nikiwa  kwenye  internet  café. Hasa  hasa  zile  internet  café  zenye  vyumba .Hii  ilikuwa  inatokea  kama  nikiwa  natazama pornography, basi nitafanya  namna  yoyote  ile  hadi  nijichue

Nilipomaliza  chuo nilifanikiwa  kupata  kazi  kwenye  taasisi moja.Siku moja  nikiwa  mkoani  kikazi  nilikutana  na  mdada  mmoja, tukapendana.

Nilimkubali kwa  sababu  alikuwa  wife  material.Niliporudi  Dar  nilirudi  nae, tukaanza  kuishi  kinyumba.Hiyo  ilikuwa  mwaka  2013.

 Pamoja  na  kwamba  nilikuwa  naishi kinyumba  na  mwanamke, lakini  bado  nilikuwa  siachi  kupiga  punyeto.

Wakati mwingine  nilikuwa  namuacha  amelala  kitandani  naenda  bafuni  kujichua.

Wakati mwingine  nilikuwa  nakataa  kushiriki  nae  unyumba,  na  tukiwa  tumelala, usiku  wa  manane  akiwa  amelala, nitajichua  bila  yeye  kustukia.

Nilikuwa  nimeshazoea  asubuhi lazima  nijichue, sasa  kuishi  kinyumba  na  mwanamke  kukawa  kikwazo  kwangu. Nikawa  nashindwa  kujichua  asubuhi.

Hivyo basi, ilikuwa  ikifika  weekend, asubuhi  ilikuwa  lazima  nimtume  aende  dukani  au hata  sokoni  mtaa  wa  tatu  au  mjini, lengo  likiwa  kupata  nafasi  ya  kujichua.

Ilifika  kipindi  Yule  mwanamke  nilikuwa  naweza  kukaa  nae  hata  miezi  miwili  bila kukutana  nae  kimwili. Na  hata  nikikutana  nae  kimwili  nilikuwa  nafanya  mara  moja  tu halafu nalala  hadi kesho  yake  asubuhi.

Kingine  naomba  niseme  ukweli, nilikuwa  mkorofi kidogo  kwa  huyu  dada, kwa  hiyo  wakati  mwingine  nilikuwa  nakuwa  mkali  sana  kwake  bila  sababu.

Nilifungua  duka  la  nguo, na  kumpa  dada  huyo  kazi  ya  kulisimamia.

Baada  ya  kuwa  mzoefu kidogo, nikawa  namuagiza  yeye  kwenda  kuchukua  marobota  ya  nguo za  kuuza  ofisini.

Baada  ya  kukaa na dada  huyu kwa  kama  mwaka  mmoja  hivi, siku  moja, kuna  kitu  aliniudhi  nikampiga.

Baada  ya  kumpiga , dada  huyo  alichukua  vitu  vyake, akaita  bajaji  na  kuondoka  zake.

Mimi  nilijua  ameondoka  na  atarudi tu mwenyewe  baadae  lakini haikuwa  hivyo.

Baada  ya  siku tatu  nikasikia  amepanga  chumba ambako anaishi  na  kijana  wa  kiume  aliyekuwa  anafanya  kazi  ya  bodaboda.

Pia  nikaambiwa, dada  huyo  amefungua  duka  la  nguo, na  kwenye  duka  hilo  anafanya  huyo  kijana  wa  kiume.

Nguo  hizo  zilikuwa  zinatangazwa  kupitia  instagram.Nilipatwa  na  uchungu  na  hasira  sana, kwa  kuona  kumbe  huyo  mwanamke  alikuwa  ananisaliti  na  huyo kijana.

Nikaingiwa  na  nia  ovu.Nikatafuta  namba  mpya  na kupiga  simu ya ofisi  ya  duka  la  huyo  mdada, akapokea  kijana  huyo, nikamwambia  alete  nguo  Buguruni, ambapo  akakubali  bila  hiyana.

Nikiwa  Buguruni, nikatafuta  nondo. Lengo  langu  lilikuwa  Yule  kijana  atakapo  fika   hapo  Buguruni sokoni, nimpigie  kelele  za  mwizi  halafu  nimpige  na  hiyo nondo.
Nilikuwa  na  hasira  kweli  kweli.

Sijui  kitu  gani  kilitokea, wakati namsubiria  huyo  kijana  kwa  hasira  na  uchungu, nahisi  malaika  wa Mungu  waliniambia  hebu  ongea  na  hawa  watu.

Pale  Buguruni Rozana, siku hiyo  kulikuwa  na  vijana  kama kumi hivi,  wanao husika  na  magari, makonda  na  madereva.

Nikawafuata  wale  jamaa  kijiweni  kwao, nakuwaambia, bana, kuna  mtu  anatembea  na  mke  wangu, wanaishi pamoja  na  kufanya  biashara  pamoja, nimempigia  simu  huyo  mwanaume  anaishi na  mke  wangu  alete  nguo  hapa Buguruni, nataka  akifika  hapa  nimpige  na  nondo  kichwani  halafu nimuitie  mwizi.

Braza  mmoja  mwenye  hekima  na  busara  akaniambia  mdogo  wangu  usijaribu  kufanya  kitu  kama  hicho. Ukifanya  hivyo, utamuua  halafu utakamatwa  na  kuwekwa  ndani  au  wanachi  wenye  hasira  nao  watakuua. Usijaribu  kabisa mdogo wangu, tena  na  hiyo nondo  yako  ilete hapa.

Akaniambia, ni bora  useme   ameshirikiana  na  mkeo  kuiba  hela halafu  umweke  ndani  lakini sio  kumpiga.

Kidogo  ushauri wa  Yule  braza  ambao  uliungwa  mkono  na  watu wengine  walio kuwa  pamoja  kijiweni  ukanipa uwoga.

Lakini  hata  hivyo bado  nikawa  na  uchungu  na  kijana  Yule.
 So  nikafanya  maamuzi  mapya, kwamba, sitampiga  na  nyundo, nitampiga  na  ngumi  huku  nikimuita  mwizi.

Nikaondoka eneo  walipokuwa  wale  jamaa nilio waomba, na  kusogea hadi maeneo ya  karibu na  Sewa  Bar  pale. Nakumbuka  ilikuwa  siku  ya  Jumamosi.

Yule  kijana  alivyo  fika  tu, hata  sikuuliza, nikamuitia  mwizi  huku nikimpiga  ngumi. Nilifanikiwa  kumpiga  ngumi  kama  mbili  hivi  za  kichwani.

Bahati nzuri, pale  walikuwepo  “Polisi Jamii”, wakanizuia nisiendelee  kumpiga, wakamkamata  na  kwenda  kituoni  huku  wakinitaka  na  mimi  niende  nao.

Kufika  kituoni  baada  ya  maelezo  yetu  kusikilizwa, nikaonekana  mimi  ndio  nina  makosa

So nikawekwa  ndani, nikisubiria  kufunguliwa shitaka la  shambulio la  kudhuru  mwili.

Bahati nzuri  Yule  kijana  alikuwa  mstaarabu  sana, akasema  hana shida  na  kesi  na  amenisamehe.

Kama hiyo haitoshi  akampigia  simu Yule  mwanamke  niliyekuwa  naishi  nae ambae  yeye ndio  aliekuja  kunitoa  polisi.

Baada  ya  kuchimba  ukweli nikaja  kugundua  kwamba, kumbe  Yule  kijana  ni mtoto  wa  dada  wa  Yule  mwanamke  niliye kuwa  naishi  nae  na  sio kweli  kwamba  walikuwa  wanaishi  nyumba  moja, ila  kuhusu  kwamba, kijana  alikuwa  anamsaidia  kusupply  nguo  kwa  wateja  wake  ni  kweli kwa  sababu  alikuwa  na  bodaboda  na  kipindi  hicho  bodaboda  zilikuwa  zinaruhusiwa  kuingia  hadi mjini.

Nilijaribu  kumbembeleza  Yule  mdada arudi  tusihi lakini  hakukubali bila  kutoa  sababu  yoyote  ile  ila  ninajua sababu  kuu ni mimi  kutokuwa  na  uwezo  wa  kushiriki  nae  tendo  la ndoa

Tangu  tukio  hilo  litokee sijafanikiwa  kuonana  tena  na  mdada  huyo, coz  alibadilisha  namba  zake za  simu  na  kurudi  kwao  mkoani…

Kila  ninapo ona  suala  la punyeto huwa  ninaogopa  sana, kwani  nalihusisha  na  mambo  mengi  mabaya. Upigaji  punyeto  unaweza  kumsababishia  mtu madhara  makubwa  kuliko  anavyo weza  kufikiria.

Kwa  mfano  huwa  najiuliza, kama  ningempiga  Yule kijana  na  ile nondo, halafu  akafa  sasa  hivi  si  ningekuwa  naozea  jela?

Upigaji  punyeto  ni  jambo  baya  sana. Kibaya  zaidi  kwa  upande  wangu, mpaka  wakati  huu  bado ninajihusisha  na  upigaji  punyeto, na  sidhani  kama  ninaweza  kuacha.

Nimekata  tama  ya  kuwa  na  mpenzi, kwa sababu  najua  hakuna  mwanamke  anaweza  kuishi  na  mwanaume  kama  mimi.



Kuacha  upigaji  punyeto  ni  changamoto  kubwa  sana. Hata  hivyo, unaweza  kujaribu  njia  ifuatayo. Njia  hii haijathibitishwa  kisayansi kumsaidia  addict  wa  punyeto  kuacha  punyeto, ila inaweza  kukusadia  ama  kukulazimisha  kuacha  punyeto.

Jinsi  njia  hii  inavyo  fanya  kazi, inasaidia  ku incapacitate viungo  vya  mwili vinavyo  husika  na  upigaji  punyeto.

Ni njia  ambayo  inahitaji  ushirikiano  wa  kutosha  wa  mwathirika.

Kufahamu kuhusu njia  hiyo, tafadhali tembelea :


Vile  vile  kama unataka  kufahamu  jinsi  punyeto  iinavyo sababisha  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu za  kiume  na  jinsi  unavyo weza  kutibiwa  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  ambalo  limetokana  na  upigaji  punyeto, tembelea :


Vile vile, kama  na  wewe ni muathirika  wa punyeto, na  unataka kushare  nasi  jinsi  punyeto  ilivyo  athiri  maisha  yako, usisite  kutuandikia : neemaherbalist@gmail.com

Kisa  chako  kinaweza kuwa  na mafundisho  mazuri  na  chaweza  kuwa  msaada  kwa  mamilioni  ya  vijana  ambao  watapata  nafasi  ya  kusoma  story  yako.

ACT Wazalendo yawakingia kifua wakulima wa korosho ......Yamtaka Waziri wa Kilimo ajiuzulu

$
0
0
Chama cha ACT-Wazalendo kimemtaka Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba kujiuzulu kwa kushindwa kuwapelekea wakulima wa korosho pembejeo kama alivyoahidi.

Akizungumza na Waandishi wa habari, jana Julai 30, 2017 jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT, Ado Shaibu alisema Serikali iliahidi kuwapa wakulima wa korosho dawa ya kuua wadudu sulpher bure ili waongeze uzalishaji, hivyo chama hicho kinaitaka serikali kutimiza wajibu wake kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo na kama haiwezi kufanya hivyo itangaze taarifa halisi za upatikanaji wa pembejeo hizo kwa wakulima.   

”Sisi kama chama cha siasa kwa kuzingatia falsafa ya chama chetu cha siasa ni maendeleo tunaendelea kusisitiza kuwa serikali ni lazima itimize wajibu wake wa kulinda maisha na hali za wananchi kwa kuhakikisha hakuna uhaba wa pembejeo kwa wakulima hawa wa korosho nchini, kuhakikisha kuwa pembejeo husika zinapatikana kwa bei ambayo watanzania wanaimudu na zinapatikana kwa wakati. 

"Ni muhimu tukumbuke kuwa unapohujumu zao la korosho unawahujumu wakulima zaidi ya 50,000 wanaojishughulisha na kilimo hicho,” alisema na kuongeza.

“Serikali itoe taarifa za uhakika mapema kuhsu upatikanaji wa pembejeo badala ya kutoa taarifa za hadaa. Ni bora ieleze wazi juu ya uwezo wake ili wakulima waweze kujiandaa mapema kwa kujiwekea akiba kwa ajili ya kununua pembejeo.

"Iwapo serikali itakuwa haina uwezo wa kugawa salfa yote bure kama inavyoonekana ieleze kwa undani kiwango inachoweza kutoa bure na iimarishe mfumo wa pembejeo.”

Pia ameitaka serikali ichukue hatua kali dhidi ya wafanyabiashara wa pembejeo wanaopandisha bei kila siku bila kuangalia maslahi ya wakulima.

“Serikali ifanye uchambuzi wa kina wa mahitaji halisi ya kila mkulima na kuwa na uhakika wa bajeti yake ndipo itangaze kutekeleza mfumo wa salfa ya bure isikurupuke kwa lengo la kutaka sifa

"Seriklai ifanye haraka kutimiza ahadi yake ya kufikisha pembejeo ya bure kwa wakulima wa korosho kwa kuhakikisha pembejeo ya bure kwa wakulima wa korosho kwa kufikisha kiwango kinacholingana na mahitaji yaliyoko,” amesema.

Kampeni ya ‘MAGUFULI BAKI’ Kuanza Nchi Nzima Hivi Karibuni

$
0
0
Kampeni ya ‘MAGUFULI BAKI’ iliyoanzishwa karibuni na mwanaharakati ambaye pia aliwahi kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Sengerema kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, Laurence Mabawa, inatarajiwa kuanza karibuni.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana , Mabawa alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupigania rasilimali za wananchi wanyonge na masikini na kuunga mkono juhudi anazozifanya na hivyo kampeni hiyo inahamasisha yeye kubaki katika msimamo wake pasipo kusikiliza maneno ya watu.

“Napinga kwa nguvu zote, kama nilivyokwisha kufafanua toka mwanzo ,kampeni ya ‘Magufuli Baki’ ina lengo la kumtia moyo Rais Magufuli na kumwomba abaki katika msimamo wake wa kutetea maskini, wanyonge na kupigania rasilimali za taifa letu,

“Nirudie tena wito wangu kwamba nitazunguka nchi nzima kwa gharama zangu kupata fursa ya kuwasikiliza wananchi kupitia kampeni yangu inayojulikana kwa ‘Magufuli Baki’ kuhakikisha wananchi wanatoa maoni yao juu ya rais kuendeleza msimamo wake wa kiutendaji na sitavunjwa na propaganda za baadhi ya vikundi vinavyonikejeli mitandaoni pasipo kuthamini maendeleo anayoyafanya,” alisema.

Aidha alieleza kwamba toka aitangaze kampeni yake kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wanasiasa na wananchi ambao hutoa lugha za maudhi na kejeli kwa baadhi ya Watanzania wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.

Alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 kifungu kidogo cha (1) na (2) kinatupa haki na fursa ya kutoa maoni na kueleza fikra zetu, hivyo amewaomba wanasiasa wasitumie kifungu hicho cha katiba kukivunja kwa kutoa maoni yenye kuudhi na kejeli, kwa hiyo, alisema, kitendo cha kushambuliana kwa maneno makali ni kosa kisheria.

Alisema kampeni aliyoianzisha itaweza kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao ambayo yatasambazwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kuanzia mwezi ujao.

Waziri Mkuu Awaasa Watumishi Wanaofanyakazi Viwandani

$
0
0
WAZIRI MKUU  Mhe. Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaofanya kazi katika viwanda mbalimbali nchini kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu.

Amesema Tanzania imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda hivyo ni vema watakaopata fursa ya ajira katika viwanda hivyo kuwa waadilifu.
 
Ameyasema hayo Jumapili, Julai 30, 2017 wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha gesi cha Ikama kilichoko wilayani Rungwe.
 
Waziri Mkuu amesema wakati Serikali ikiendelea kuwakaribisha wawekezaji nchini, wananchi walioajiriwa kwenye maeneo hayo wawe waaminifu.

“Mnatakiwa muwe waaminifu, msibebe kitu chochote ndani ya kiwanda bila ya ridhaa ya wamiliki kwa kuwa mtaonyesha taswira mbaya kwa wawekezaji.”
 
Amesema uaminifu wao ndio utawezesha Watanzania wengi kupata ajira kwenye viwanda hivyo ambavyo vimejengwa katika maeneo yao.
 
Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya TOL Gases, Mhandisi Harold Temu alisema kiwanda kinauwezo wa kuzalisha tani 46 kwa siku.

Alisema gesi inayozalishwa kiwandani hapo ni ya Carbon Dioxide ambayo inauzwa nchini na nchi jirani za Zambia, Malawi, Zimbabwe na Congo.

Mhandisi Temu alisema wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda vya kutengenezea soda, bia na pia hutumika katika kuhifadhia chakula na kwenye vifaa vya kuzimia moto.

Mapema Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kuchakata majani ya chai cha Katumba, ambapo alisema Serikali inaimarisha Ushirika wa zao hili ili wakulima waweze kupata tija. 

Sehemu 2: Ufafanuzi Wa Dokta Mungwa Kabili Kuhusu Mwanamke Aliyemlisha Mume Wa Mtu Limbwata La Nyama Ya Bundi.

$
0
0
THEOFLIDA   ALIVUNJA   MWIKO   KUHUSU  “ WATOTO  WA  MISUKULE “

Na. DOKTA   MUNGWA   KABILI ……………………..0744   000  473

Hii  ni  sehemu  ya  pili  na  ya  mwisho   ya  ufafanuzi  wa  Dokta  Mungwa  Kabili, kuhusu  mwanamke  aliye  mlisha  mume  wa mtu  limbwata  la  nyama  ya  bundi.

Kuisoma  sehemu  ya  kwanza  ya  ufafanuzi  wa  dokta  Mungwa, bonyeza  : http://mungwakabili.blogspot.com/2017/07/ufafanuzi-wa-dokta-mungwa-kabili-kuhusu.html

Kwa  ufupi  kilicho  sababisha  mpaka  Theoflida  apate  matatizo  yote  hayo  aliyo yaandika  kwenye  waraka  wake  ni  kuvunja   MWIKO  KUHUSU  WATOTO  WA  MISUKULE.

Nirudi  kwenye  mada  yetu. Theoflida  alivunja  mwiko  mkubwa  sana. Mwiko  ambao  haupaswi  kuvunjwa  kwa  sababu, namna au  jinsi yoyote  ile.

Ni hivi, baada  ya  kufika  kilingeni kwangu  na  kunielezea  shida  na  matatizo  yake, niligundua  Theoflida  ni  mwanamke  ambaye  aliumizwa  na  kunyanyaswa  sana  na  wanaume.

Hivyo  basi  baada  ya  kumtengeneza  na  kumpa  dawa  ambazo  zilimsaidia  kuwapata  wanaume  anaowataka  na  kuwahitaji   akaona  sasa  imefika  zamu  yake  kuwaumiza  na  kuwanyanyasa  kimapenzi  wanaume  aliokuwa  anawataka.

Hivyo  basi  mara  kwa  mara  akawa  anakuja  kilingeni kufuata  dawa  za  kuwatengeza  wanaume  mbalimbali  aliokuwa  akiwataka .

Hata  hivyo  pamoja  na  mambo  yote  hayo, Theoflida  hakuridhishwa  na  jambo  moja. Nalo  ni maumbile  yake .

Theoflida  hakuwa  akiridhishwa   na  muonekano wa  maumbile  yake  hasa  hasa  sehemu  yake  ya  makalio.

 Hivyo basi  kwa  muda  mrefu  alikuwa  akitaka  nimsaidie  kumpa   dawa  ya  kuongeza  ukubwa  wa  makalio  yake.

Mara  kadhaa  akiwa  ofisini  kwangu, alishuhudia  wanawake kadhaa  wakifika  ofisini kwangu  kwa  ajili  ya  kutoa  shukrani  zao  mara  baada  ya  kutumia  dawa  za  asili  za  kuongeza  ukubwa  wa  makalio.

Kwa  sababu  hiyo  na  yeye  akashawishika  na  kuniomba  nimtengenezee  dawa  hiyo  ya  kuongeza  ukubwa  wa  makalio.

Hata  hivyo  sikuwa  tayari  kumpatia  dawa  hiyo, kwa  sababu  moja  kubwa . Nayo  ni  kwamba, Theoflida  alikuwa tayari  amechanjiwa  dawa  nyingine  ambayo  haiendani  na  dawa  hiyo ya  kuongeza  ukubwa  wa  makalio.

  Ni mwiko  na nuksi kubwa  sana  kwa  mtu  kuchanjiwa  dawa  hizo  zote  mbili  kwa wakati  mmoja. Ukifanya  hivyo  utafanya  mwili  wa  mtu  huyo  utumike  kama  uwanja  wa  mapambano  kati  ya  majini  kutoka  koo  mbili  za  kijini  zilizo  kula  kiapo cha  uadui  hadi siku  ya  kihama.  Na  endapo jambo  hilo  litatokea  basi itakuwa  shida  sana kwa  mhusika.

Kabla  sijauelezea  mwiko  huo, ngoja  nikufafanulieni  kidogo  kwanza :

Ni hivi  Wachawi  ni  washenzi  sana.  Katika  ulimwengu  wa  wachawi  kuna  viumbe  wanaitwa  “ watoto  wa  misukule “.

Watoto  wa  misukule  wapo  wa  aina  mbili. Aina  ya  kwanza  ni  ya   mtoto  wa  msukule  aliyezaliwa   baada  ya  mtu  wa  kawaida  kumuingilia  mwanamke  msukule  na  mtoto  kuzaliwa  na  aina  ya  pili  ni  mtoto  wa  msukule  anaezaliwa  baada  ya  msukule  wa  kiume  kujamiiana  na  msukule  wa  kike .

Katika  ulimwengu  wa  wachawi, watoto  hawa  wa  misukule  hujulikana  kama  “ WATU WANAOPITA  DUNIANI  BILA  KUONEKANA “.

Katika  viumbe  waliombwa  na  Mwenyezi Mungu, hakuna  viumbe  wanaoishi maisha ya  mateso  kama  watoto  wa  misukule .

  Usiombee  kuchukuliwa  msukule,.usiombee  ndugu yako  kuchukuliwa  msukule.usiombee  kabisa.. ni hatari  sana …na  ndio  maana  katika  kinga  zote  za  kiganga  anazo  takiwa  kupewa  mwanadamu, hakuna  kinga  kubwa  na  muhimu, kama  kinga  dhidi  ya  kuchukuliwa msukule.

Wachawi  wa  nchi  wanawatesa  na  kuwatumikisha  viumbe  hawa  katika  shughuli  zao  za  kichawi.  Baadhi  ya  mambo  hayo  ni  mfano,  watoto  wa  kike  wa  wa  misukule  wanapofikia  umri  wa  miaka  saba  huwa  wanakeketwa, vile visimi  au vinembe  vyao  hukaushwa  halafu  mwisho wa  siku huchanganywa  na  madawa  mengine  ya  kichawi  ili  kutengeneza  uchawi  wa  kimapenzi.

Watoto  wa  misukule  hutumiwa  kwenye  uchawi  wa  chuma  ulete.

Watoto  wa  misukule  hutumiwa  katika  uchawi  wa  majini  mahaba, ambapo  hutumika  kuwaingilia  kimapenzi  wanawake  na  kuwafunga  kwenye  vifungo  vya  kichawi kama  vile  kuwasababishia  utasa  nakadhalika

Watoto  wa  misukule  hutumika  katika  kuwalisha  uchawi  watoto  wadogo  wa  kiume  kwa  lengo  la  kuwasababishia  uhanithi  na  kuyafunga  maumbile  yao  ya  kiume  yasikue.

Hii  mara  nyingi hutokea  kwenye  ndoa  za  mitaala, hasa  hasa  pale  inapotokea  mwanamke mmoja  akawa  na  watoto  wa  kiume  na  mwingine  akawa  na  watoto  wa  kike  tu. Pamoja  na  mambo mengine  mengi.

Ikitokea   mtoto wa  msukule  amefariki dunia, basi  lile  kaburi  lake  hutumika  katika  mambo mengi  sana,  baadhi  ya  mambo  hayo  ni pamoja  na  kuzika  nyota  ama  vivuli vya  watu  nakadhalika. USIOMBEE  NYOTA  YAKO  AU KIVULI  CHAKO  KIZIKWE  KWENYE  KABULI  LA  MTOTO  WA  MSUKULE.

Watoto  hawa  wa  misukule pamoja  na  mambo mengine, ndio wanao  tumiwa  na  wachawi  kuiba  nyota  za  watu, kwenye  uchawi  wa  chuma  ulete  nakadhalika.  ( MADA  KUHUSU  WATOTO  WA  MISUKULE  NI  NDEFU SANA, SIKU  NIKIPATA  NAFASI  NITAIELEZEA  KWA  UREFU  ZAIDI)

Sasa  basi  watoto  hawa  wa  misukule  wanapo fariki dunia,  huwa  wanazikwa  porini   saa  sita  usiku au  saa  saba  mchana. Ukipita  porini  saa  saba  mchana  au  saa sita  usiku, ukasikia  harufu  ya  pilau  basi  ujue  siku  hiyo  kuna  mtoto  wa  msukule  anazikwa. Na  mara  nyingi  inapokuwa  inafanyika  shughuli  ya  kuwazika  watoto  wa  misukule  huwa  inaendana  na  zoezi  la  kuzika  nyota  za  watu au  vivuli  vya  watu .

Sasa  basi  katika  makabari  wanayo  zikwa  watoto  wa  misukule, huwa  yanawekwa  juu  yake  mashahidi  saba  ya  kaburi .

 Katika  ulimwengu  wa  wachawi,  mashahidi  ya  kwenye  makaburi  ya  misukule hujulikana  kama  SHAHIDI LA  MSUKULE  au  SHUNGE.

Shahidi  la Msukule  hukatwa  kwenye  miti  saba  tofauti  wala hayaingiliani  na  mashahidi  ya  makaburi  kwenye  makaburi  ya  kawaida.

Katika  miti  hiyo  inayo wekwa  juu  kwenye  kaburi  la  msukule, upo mti  mmoja wenye  matumizi  mengi   katika  uganga, ambao  pia  wachawi  huutumia  katika  mambo yao  ya  ulozi.

Mti  huu  hutoa  utomvu, utomvu  wa  mti  huu, una  matumizi  mengi  sana  katika  tiba  na  mambo mengineyo, kwanza  unatumika  kutibu  vidonda  ndugu,  pili utomvu  huu  ni dawa  nzuri  sana  inayotibu  marahi  ya  degedege  kwa  watoto.

Kama  mtoto  ameshikwa  na  degedege, basi  unampaka  utosini  na  kwenye  paji  la  uso. Mtoto  huyo  atapona  degedege  hapohapo  na  hatougua  tena  degedege. 

Kama   mtu  anasumbuliwa na  ulevi  ulio  pitiliza  hasa  hasa  ule  ulevi  wa  kichawi, utomvu  huu  ndio  tiba  yake  sahihi.

Ili  kujua  kama  ulevi  wa  mtu  ni  wa  kawaida  ama  kulogwa, unatakiwa  kufanya  mambo  yafuatayo : Kwanza : Chukua  yai  la  kunguru, pasulia  kwenye  pombe  anayo kunywa  mlevi, halafu  subiri ndani  ya  siku  saba, kama  atarudi  kunywa  pombe, basi  jua  huyo  ulevi wake  ni wa  kulogelezewa,  njia  ya  pili  chukua  mavi  ya  njiwa    mweupe yaliyo  kauka, yasage, chukua  mavi ya  binadamu  yaliyo kauka, yasage, changanya  na  karafuu  maiti, mkubashengelo, mfalme wa  pori, ndaze  nyeusi  zilizo  sagwa  pamoja  mzungu pori, vitu vyote  hivi  visagwe  kwa pamoja, hlafu chukua  kiasi kidogo  sana  cha  mchanganyiko  wako  kisha tia kwenye  pombe  anayo tumia  “mlevi” wako, halafu subiria  kwa  muda  wa  siku  saba. Ndani  ya  hizo siku  saba, akinywa  pombe , basi  jua  huyo ulevi  wake  ni  wa  kulogwa  na  hivyo  atatakiwa  kutumia  utomvu  huu.

Kitu kingine  utomvu  huu  huwa  wanautumia  wanawake  wenye  wanao  nyonyesha  watoto  wachanga  ili  kujua  kama  mume  ametoka  kulala  na  mwanamke  mwingine.

Utomvu  unachanganywa  na  dawa  nyingine  ahalafu  inafungwa  kwenye  kitambaa cheusi  kama  hirizi, anavikwa  mtoto. Baba  akitoka  kwenye  matembezi  yake  usiku, akitaka  tendo  la  ndoa, mtoto  ataanza  kulia, na  hata  kama  amelala  ataamka na  kuanza  kulia  sana..Tendo  la ndoa  halitafanyika  siku  hiyo ( NI NUKSI KWA MWANAUME  KUFANYA  TENDO  LA NDOA  NA  MKEWE  ANAE NYONYESHA  BAADA  YA  KUTOKA  KULALA  NA  MWANAMKE MWINGINE )

Vile  vile  utomvu  huu  hutumika  kuongeza  ukubwa  wa  makalio.. mtu akichanjiwa  utomvu  huu kwenye  makalio  na  kujipaka, baada  ya  siku  kadhaa, makalio yake hunenepa  na  kuwa  makubwa.

Turudi  kwa  Theoflida,  mwanadada  huyu alitaka  na  yeye  achanjiwe  utomvu  huu wa  asili  wa  kuongeza  makalio…

Hata  hivyo  sikuweza  kumkubalia  kwa  sababu  matumizi  ya  dawa  hii  yanaendana  na  miiko  na  taratibu  zake.

Theoflida  alikuwa tayari  amechanjiwa  dawa  nyingine  ya  kinga  ambayo  haiwezi  kukaa  pomoja  na  dawa  hii  ambayo  pia  huongeza  ukubwa  wa  makalio.

Ili  atumie  dawa  hii  kwa  ajili  ya   kuongeza  ukubwa  wa  makalio, alitakiwa  asubiri  kwanza  hadi  ipite  miezi  36( miaka  mitatu )  kwa  sababu  dawa  hiyo  aliyo chanjiwa  ilikuwa  inakaa  mwilini  kwa  muda  wa  miaka  mitatu.

Baada  ya  miaka  mitatu, ndipo  angeweza  kutumia  dawa  hiyo  ya  makalio  aliyo  kuwa  anaitaka.

Siku  moja  Theoflida, alifika  ofisini kwangu  akiomba  nimpatie  dawa  hiyo  ajili  ya  rafiki  zake. Nilimpatia  dawa  huku  nikimsisitizia  asijaribu  kutumia  dawa  hiyo  yeye  mwenyewe  na  kama  angefanya  hivyo  basi  angepata  madhara  makubwa  sana.

Hata  hivyo  kwa  sababu  ya  kuwa  na  kiu  kubwa  ya  kutaka  kuwa  na  makalio  makubwa, Theoflida  pamoja  na  kuwapa  rafiki  zake  dawa  hiyo, yeye  mwenyewe  alienda  kutumia  dawa  hiyo, na  matokeo  yake  baada  ya  siku  saba, madhara  ya  kuvunja  mwiko  wa  kutumia  dawa  hiyo  ya  kaanza  kuonekana.

Theoflida  alianza  kuugua  magonjwa  ya ajabu  ajabu, kwa  kuwa  alikuwa  anajua  alicho kifanya, alishindwa  kuja  kwangu  kwa  sababu  alijua  nisinge  mpokea,.  Mwisho  wa  siku  akaamua  kwenda  kufafuta  msaada  kwenye  imani  nyingine  ambako  nadhani ndio  walio mshawishi  aongee  mambo ambayo  hakupaswa  kuyaongea.

Nadhani  mpaka  hapo, mtakuwa  mmepata  ufafanuzi, hivyo maswali  kuhusu  Theoflida, na  imani  hayatakuwepo  tena.

Kufahamu  kuhusu  mambombalimbali  yanayo  endelea  katika  ulimwengu usio onekana. Tembelea  kila  siku  :  www.mungwakabili.blogspot.com

Taarifa za upotoshaji kuhusu mfunzo ya vitendo kwa wanafunzi

$
0
0
Kumekuwepo na upotoshaji wa mafunzo ya utarajali (Internaship programme) bila malipo yaani fedha za kujikimu wakati wa mafunzo hayo kwa baadhi ya wanaotarajia kuanza mafunzo kwa vitendo mapema mwaka huu.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwajulisha kwamba kwa sasa hakuna ‘intern’ aliyepangiwa kuanza mafunzo hayo kwani tunasubiri watoke waliopo kwenye mafunzo.

Barua iliyodukuliwa na kusambaa kwa lengo la kupotosha wataraji hao ilikuwa ni kwa ajili ya wataraji (intern) kutoka nje ya nchi ambao kwa sheria hawalipiwi na Serikali ya Tanzania.

Aidha wapo ‘intern’ wawili ambao wanasoma nchini China na mwingine Algeria masomo yao yalihitaji mafunzo kwa vitendo kabla ya kumaliza na kwa kuwa ilikua lazima warudi vyuoni mwezi Oktoba waliomba kufanya mafunzo hayo  kwa kujigharimia  pamoja na kuwa ni watanzania na wazazi wao walikuwa wameridhia hilo kwa maandishi ili warudi  mapema kumalizia program yao ya udaktari.

Hivyo ni watanzania wawili tu wameshapata barua yenye kuwataka  kujilipia kwa mazingira hayo hakuna wengine waliyepewa barua ya kuruhusiwa kwenda mafunzo ya utarajali (internship) bila malipo.

Imetolewa na;

Nsachris Mwamwaja
Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Afya
30/7/2017
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images