Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tundu Lissu: Nitanyamaza Nikifa

$
0
0
Mwanasheria  Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusema kuwa atanyamaza tu baada ya kufariki dunia.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alipata dhamana jana baada ya mahakama hiyo kubaini hoja za Serikali za kumnyima haki hiyo hazina mashiko.

Baada ya kutoka mahakamani, alikwenda katika ofisi za Chadema zilizopo Kinondoni, ambako pamoja na mambo mengine, alisema ataendelea kuikosoa Serikali hadi pale atakapokufa.

“Hakuna gereza litakalotunyamazisha, watu wakipelekwa mahabusu watazungumza wakiwa mahabusu, wakifungwa watazungumza wakiwa kifungoni, hivyo ili wanyamaze itabidi kwanza wafe… tutanyamaza tukiwa wafu kwa sababu wafu hawasemi,” alisema.

Lissu alisema kuna haki ya kuwasema na kuwakosoa wale waliopewa madaraka na wananchi.

Alisema katika sheria ya uchochezi ya mwaka 1953, kutoa kauli yoyote yenye lengo la kukosoa matendo ya Serikali, sera si kosa na wala kumkosoa rais na Serikali yake si kosa.

“Sasa ukisema wanakukamata, wanakushtaki kwa uchochezi, wanakupiga, wanakupeleka central (kituo kikuu cha polisi) au Oysterbay wakikupeleka sio kosa, bali unatumia akili zako kuikosoa Serikali,” alisema Lissu.

Akizungumzia kuhusu kupimwa mkojo, Lissu alisema alipelekwa na askari kwenye nyumba iliyo karibu na Ocean Road, lakini alikataa kutekeleza hilo.

“Niliwaambia nyie maaskari mimi nimeshtakiwa kwa uchochezi, unathibitishaje uchochezi kwa kupima mkojo?” alisema Lissu.

Alisema askari hao walimjibu kuwa kuna vitu wanavitaka, akawaeleza: “Nendeni mkanishtaki, hamjapata oda ya hakimu, hamtaona mkojo wangu.”

Baada ya kauli hiyo, alisema askari hao walimwambia kuwa wao wana mamlaka.

“Nikawaambia mimi ni Rais wa Mawakili (TLS). Siku ukikamatwa, ukaambiwa kupimwa damu, mkojo waambie hutaki hata kama wamekushtaki.

“Ukitoa mkojo na usiposaini hakuna dili, walichokuwa wanatafuta wapate dili ya kutengeneza ‘headline’ (kichwa cha habari), ‘huyu anasema hivi kwa kuwa anatumia dawa’, nani asiyejua polisi wanabambika? Nikakataa, nikawaambia mnataka twende kunisachi twendeni.”

Lissu alisema akiwa Segerea alikutana na wafanyabiashara James Rugemalira na Harbinder Singh Sethi wanaokabiliwa na kesi ya uhuhumu uchumi na utakatishaji fedha.

“Mwaka jana nilisema hawa lile dili (kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow) watu lazima wawajibike, waliowapa hela, waliosaini BoT (Benki Kuu ya Tanzania), walioruhusu hizo fedha kwa kusema James Rugemalira na Harbinder Singh wapewe wako wapi?” alihoji.

Lissu alihoji wapi walipo waliopewa mgawo wa fedha za Escrow.

Kabla ya kutoa uamuzi wa dhamana jana, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri, alipitia hoja za pande mbili zilizokuwa zinapingana, zilizowasilishwa mahakamani hapo mwanzoni mwa wiki.

“Hii kesi ina dhamana, hoja kwamba anakabiliwa na kesi nyingi zenye viashiria va uchochezi haina mashiko kwa sababu hakuna taarifa kuwa aliwahi kuruka dhamana.

“Kwangu mimi hiyo haitoshi kumuweka mahabusu, hoja ya kwamba aendelee kuwepo rumande kwa usalama wake, hakuna taarifa kwamba akipewa dhamana maisha yake yatakuwa hatarini.

“Mshtakiwa anawakilishwa na mawakili 18 wanaomuombea dhamana, wanafanya hivyo kwa upendo walionao dhidi ya mshtakwa, hivyo haiwezekani akipewa dhamana atadhurika.

“Mahakama inakubali maombi ya dhamana, mshtakiwa atadhaminiwa kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili, watasaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10 kila mmoja na mshtakiwa hatakiwi kusafiri bila kibali cha mahakama,” alisema.

Baada ya kutoa masharti ya dhamana, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi kwa nusu saa ili watafutwe wadhamini hao ambao walipatikana kwa juhudi za Wakili Peter Kibatala aliyetoka nje ya mahakama kuwatafuta.

Awali wadhamini hao walishindwa kuingia eneo la mahakama kutokana na kuimarishwa kwa ulinzi kulikotokana na kuwapo kwa kesi za ugaidi mahakamani hapo.

Kwa upande wake, Wakili wa Serikali Mkuu, Simon Wankyo, alidai mahakamani kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo aliomba tarehe nyingine ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 24, mwaka huu kwa kuanza usikilizwaji wa awali.

Lissu alidhaminiwa na wadhamini wawili walioweka dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10 kila mmoja.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya July 29

Mbowe amjibu Polepole kuhusu kigogo wa Chadema anayetarajiwa kuhamia CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amejibu kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole aliyesema kuna mtu mzito wa Chadema atakayehamia chama tawala hivi karibuni.

Mbowe amesema kuwa Chadema haiwezi kutetereka kwa kuondoka kiongozi yeyote kwani imejengwa katika misingi imara kama taasisi isiyotegemea mtu.

“Kwanza kabisa sitaki kuzungumzia propaganda za Polepole ambaye najua anajifunza siasa. Wapo wazito zaidi waliohama au kufukuzwa. Lakini niseme tu chama hiki kina misingi yake, mtu awe mdogo au mkubwa ni tafsiri tu, ingawa wapo wenye mchango mkubwa,” Mbowe anakaririwa na Mtanzania.

“Mtu yoyote anaweza kuondoka lakini Chadema kama taasisi itabaki imara. Mimi kama Mwenyekiti ninajua tumejenga taasisi imara ambayo haiwezi kutetereka kwa wanachama au kiongozi wa ngazi yeyote kuondoka,” aliongeza.

Kauli hiyo ya Mbowe imekuja wakati ambapo kumekuwa na matukio ya madiwani wa Chadema kuhamia CCM katika mikoa ambayo inasadikika kuwa ni ngome ya chama hicho kikuu cha upinzani kama Arusha na Kilimanjaro.

Mwenyekiti huyo wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai amesema kuwa walifahamu hatua za madiwani hao zaidi ya 10 kufanya kile alichokiita usaliti hata kabla hawajatangaza kuhama.

Rais Magufuli na Museveni kuweka jiwe la msingi mradi wa bomba la mafuta

$
0
0
Tarehe 05 Agosti, 2017 siku ya Jumamosi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wataweka jiwe la msingi la Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Mradi huu ni moja ya miradi mikubwa ambayo nchi yetu imeipata na kuanza kutekeleza tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani tarehe 05 Novemba, 2015. Ni mradi ambao uwekezaji wake ni mkubwa wa Dola za Marekani Bilioni 3.5 sawa na takribani Shilingi Trilioni 8 za kitanzania.

Urefu wa bomba hili ni kilometa 1,445 na kati ya hizo kilometa 1,115 zinajengwa Tanzania na mafuta ghafi yatakayosafirishwa ni mapipa 216,000 kwa siku.

Inatarajiwa wakati wa ujenzi wa mradi huu ajira takribani 10,000 zitazalishwa na Watanzania watakuwa wanufaika wakubwa wa ajira hizi. Nchi zetu za Tanzania na Uganda zitapata manufaa makubwa ya kiuchumi kutokana na kodi na tozo mbalimbali, mrahaba na shughuli nyingine za kibiashara zitakazoambatana na mradi huu.

Nachukua fursa hii, kuwaalika Watanzania wote kufuatilia matangazo ya moja kwa moja yatakayorushwa na vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kwa siku hiyo ya Sherehe za uwekaji jiwe la msingi na pia kufuatilia matangazo mbalimbali na machapisho yatayotolewa na vyombo vyetu vya habari na mitandao ya kijamii kuelekea siku hiyo.

Kama ambavyo viongozi wa Mkoa wa Tanga wanafanya, tunataraji wananchi wa Tanga watajitokeza kwa wingi kuungana na Rais wao Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe hii kubwa na kwa mradi huu mkubwa katika nchi zetu.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Julai, 2017

Rais Magufuli Amtumbua Kigogo wa Uhamiaji kwa Kuingiza Wasomali Nchini

$
0
0
Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo kwa tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi kinyume cha taratibu.

Kauli hiyo imetolewa  jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini.

Alisema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.

"Idara ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu." alisema Waziri Mkuu

Waziri Mkuu alisema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini

 "Tulidhani ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa hii ni dosari hatuwezi  kuivumilia. Hawa Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao" alisisitiza Majaliwa

Dongote ameporomoka kwenye Orodha ya matajiri wa Dunia

$
0
0
Bilionea raia wa Nigeria Aliko Dangote ameporomoka kwenye nafasi za watu tajiri duniani hadi 105 kutoka nafasi ya 51. 

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes limeripoti kwamba utajiri wa Dangote umepungua kutoka dola bilioni 15.4 mwaka 2016 hadi dola bilioni 12.2 mwaka huu kutokana na kushuka thamani kwa pesa ya Nigeria.

 Dangote alijipatia utajiri wake kupitia uzalishaji wa saruji, sukari, na unga wa ngano. Aligonga vichwa vya habari 2016 wakati aliposema kuwa alitaka kuinunua klabu ya soka ya Arsenal katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Hapo juzi  Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos alimpiku Bill Gates kwa muda mfupi kama mtu tajiri duniani kabla ya kushuka hadi nafasi ya pili.

Waandishi wa TBC wafukuzwa kwenye mkutano wa Tundu Lissu

Bulaya Ambwaga Tena Wasira Mahakamani

$
0
0
Mahakama ya Rufani imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na wapiga kura wanne wa Jimbo la Bunda Mjini Mkoani Mwanza ya kupinga ushindi wa Mbunge, Esther Bulaya katika uchaguzi Mkuu wa Wabunge, Madiwani na Rais wa Tanzania ulifanyika Oktoba 25 mwaka 2015.

Wapiga kura hao ambao wanampigania aliyekuwa Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika na mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Bunda Mjini, Stephen Wasira, wapo wanne ambao ni; Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila.

Uamuzi huo umetolewa jana na  Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Elizabeth Mkwizu ambapo alisema, upande wa walalamikaji uliwasilisha hoja 10 za kupinga ushindi wa Bulaya, lakini hoja hizo hazikuwa na mashiko, hivyo zinatupiliwa mbali.

Miongoni mwa hoja zao ni “Stephen Wassira, hakualikwa katika mchakato wa kujumlisha kura suala hili linaweza kuathiri matokeo ya uchaguzi kwa kushindwa kumtambua mgombea wala chama chake,”

Baada ya maamuzi hayo Mbunge huyo kupitia ukurasa wake wa twitter aliandika maneno machache ambayo alimshukuru Mungu kwa kitendo cha kushinda kesi hiyo dhidi ya wapiga kura hao.

"Wana bunda wameshinda tena na tena, asante Mungu", aliandika Bulaya.

Wema Sepetu Akerwa Ndugu Yake Kupigwa na Polisi Mahakamani

$
0
0
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ametoa yake ya moyoni na kutoa tuhuma kwa jeshi la polisi nchini kufuatia baadhi ya polisi kumpiga ndugu yake ambaye juzi alikwenda naye mahakamani kusubiri kesi ya Tundu Lissu.

Wema Sepetu anasema kuwa ndugu yake huyo kwa sasa anapatiwa matibabu hospitalini kufuatia kipigo alichopata kutoka kwa polisi hao kwa kile anachosema kuwa kijana huyo alipigwa kufuatia kupita katika mlango wa mahakama.

"Ninachojua mimi ni kwamba binadamu ana haki ya kwenda mahakamani kusikiliza kesi ya ndugu yake... Imeniuma sana kilichomtokea kaka yangu jana, Only now nakuja kujua kwamba alichukuliwa na polisi wakaenda kumpiga mpaka sasa yupo hospitali amelazwa. Kosa lake ni kupita pale mlango wa mahakamani na akasema kabisa yupo pamoja na mimi na mama yangu" alisema Wema Sepetu

Hata hivyo Wema Sepetu anasema wakati anasubiri kesi ya Tundu Lissu juzi  mahakamani alikuja kuitwa na polisi na kuambiwa kuwa aondoke eneo hilo na arudi nyumbani kwake

"Maana jana tulivyokuwa tumekaa tunasubiri kesi ya Mh. Tundu Lissu itajwe, Nilikuja kuitwa walitaka niondoke eneo hilo na nirudi nyumbani... Nilikuwa mkali kidogo, wakanijia na huyo kaka yangu ambaye alisema kuwa yupo pamoja na mimi" alisema Wema Sepetu

Mbali na hilo Wema Sepetu alisema kuwa namna ambavyo jeshi la polisi linafanya si jambo zuri na kusema matendo ya namna hii yanaweza kuleta shida au matatizo siku za usoni

Mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka huu msanii Wema Sepetu alifanya maamuzi magumu na kuamua kuhama chama kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya msanii huyo kutuhumiwa na serikali kuwa anajihusisha na Uuzaji na matumizi ya madawa ya kulevya ambapo mpaka sasa bado kesi yake inaendelea katika Mahakama Kuu Tanzania (KISUTU)  

Kutana na Mtaalamu wa Kusafisha Nyota........Anatoa Mvuto wa Biashara, Kupandishwa Cheo, Kurudishiwa Mali Uliyoibiwa na Mengne

$
0
0
Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..

CHIEF SULTAN ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
 
Je unasumbulia na Mapenzi..?
(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na CHIEF SULTAN Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.
Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
 
Wasiliana na CHIEF SULTAN Kwa Majibu ya Maswali yako..
Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)
KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA..
Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.
 
Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.)Humaliza Kesi za Muda mrefu ndani ya siku 14 tu.
Anatoa NDAGU Zisizokuwa na Masharti.. Kwa maelezo Zaidi wasilina nae kwa

whatsapp +255 0658 316 976
Call +255 755 911 233

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Pata Tiba ya Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za: 
 
FUUl POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.
 
NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM .HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Gazi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Mahakama Yaamuru Harbinder Singh Sethi Akatibiwe Muhimbili

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mshtakiwa, Harbinder Singh Sethi apelekwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kupata huduma ya matibabu.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alitoa amri hiyo jana  Ijumaa Julai 28 baada ya Sethi kuieleza mahakama hiyo kuwa hali yake kiafya bado ni mbaya na kwamba aliongea  na Magereza ili aweze kupata tiba toka kwa daktari wake, wakampeleka katika Hospitali ya Amana.

Amedai kuwa kutokana na maradhi yanayomkabili kuhitaji mtaalam ameshindwa kupata matibabu, hivyo ameomba asinyimwe haki ya kupata matibabu.

Baada ya kutolewa maelezo hayo, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Vitalis Peter alieleza kuwa ni kweli mshtakiwa ameieleza mahakama kuhusu hali yake lakini hakuna nyaraka zinazounga mkono kutoka kwa mtaalam kuelezea hali yake.

Amebainisha kwa kuwa kutibiwa ni haki yake na kuwa wapo madaktari katika Hospitali ya Taifa  ya Muhimbili na Magereza.

Hakimu Shaidi alisema kusiwekwe kikwazo chochote kuhusu afya ya mshtakiwa hivyo aliamuru Magereza kumpeleka Muhimbili kwa ajili ya matibabu na tarehe ijayo watoe taarifa kama amri aliyoitoa imetekelezwa.

Upelelezi wa kesi hiyo hadi sasa haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Agosti 3, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Awali, Julai 14, 2017, wakili wa Sethi, Alexi Balomi aliifahamisha mahakama kuwa Sethi anaumwa na hali yake imeendelea kuwa mbaya na alikuwa hawezi kupata usingizi kwa wiki nne.

Wakili Balomi aliiambia mahakama kuwa Sethi anasumbuliwa na uvimbe tumboni wenye ukubwa kama  puto ambao unahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari wataalam na kwamba anahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari.

Katika kesi hiyo, Sethi na James Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 309 bilioni.

LHRC Yasikitika Wabunge wa CUF Kuenguliwa Huku Kukiwa Bado Kuna Kesi Mahakamani

$
0
0
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, (LHRC) kimetoa taarifa yake kwa vyombo vya habari kikisikitishwa na jinsi Bunge, lilivyotengua uteuzi wa wabunge wa viti Maalum juzi.

“LHRC inafuatilia mwenendo wa demokrasia nchini na kinatambua uwepo wa mzozo wa kiutawala ndani ya CUF, mzozo ambao umepelekea mgawanyiko ndani ya chama hicho na kufikia hatua ya wanachama kufikishana mahakamani kwa ajili ya usuluhishi,” imesema.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga imesema LHRC ilitaraji kuona Bunge likiheshimu mhimili wa mahakama ambao bado haujatolea uamuzi shauri la Bodi ya Wadhamini ya CUF dhidi ya maamuzi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya kumtambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti.

“Kwa maamuzi haya bunge limedharau mhimili wa mahakama ambacho ni chombo huru kwa mujibu wa Katiba. LHRC kinalitaka Bunge kurejea maamuzi yake na kusitisha maamuzi hayo mpaka mahakama itakapochukua hatua.” Imesema taarifa hiyo.

Tamko la Serikali kuhusu homa ya Ini,

$
0
0
Serikali imesema kuwa inatarajia kuanza kutoa Chanjo ya Homa ya Ini kwa wananchi wote bila kujali kigezo cha umri wala uwezo wa kifedha kwa wale wote wenye dalili za ugonjwa  au wenye ugonjwa wa Ini.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza kuhusu maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya ini duniani.

“Katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini duniani tumedhamiria kuhakikisha chanjo ya ugonjwa huu inapatikana kwa watu wote nchini ambao wana hatari ya kupata maambukizi ya homa ya ini au tayari wamepata ugonjwa huo, watapata chanjo kwa bei nafuu kwa mswaka wa bajeti 2018/2019” alisema Ummy.

Alisema kuwa ili kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini mpango wa damu salama unatakiwa kuhakikisha wanapima damu zote za wachangiaji kabla ya kuwawekea wagonjwa wanaohitaji huduma ya damu.

Aidha, Ummy alisema kuwa asilimia 50 ya wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano wana maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini hivyo amewataka watanzania kutojihususha na matumizi hayo na kuepuka ngono zembe.

Hata hivyo, Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamad Bakari Kambi alisema kuwa virusi vikubwa vya ugonjwa wa ini ni A,B na C ambapo vimelea A huletwa na mtu asiye na maambukizi kula chakula kisicho salama na kunnywa maji yasiyo salama.

Diamond Kampeleka Zari Mombasa na Kuwachamba Wanaomsema Vibaya

$
0
0
Diamond Platnumz ameamua kuwaumbua waliokuwa wakisema kwamba penzi lake za Zari limekufa.

Pia amewajibu wanaotaka mpenzi wake abaki akiwa mnyonge baada ya kupata matatizo ya kufiwa na mama yake mzazi wiki chache zilizopita.

“Kuna vichupi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa Misiba ya watu…. Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo, anatakiwa apelekwe sehem tulivu apetiwepetiwe adekezwe apate faraja!…sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo, Msijifanye ni Tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia… Pambaneni na Mahusiano yenu…! Nina siku 5 za kumpetipeti… leo ndio kwanza Ya kwanza 😛.” ameandika Diamond Instagram.

Diamond amefikia hatua hiyo baada ya watu kumponda mpenzi wake Zari The Boss Lady, ambaye siku ya jana alikuwa Instalive na mkali huyo wa Eneka wakijiachi kimahaba, hali iliyofanya mitandao ya kijamii kumponda kuwa anaonyesha hana uchungu wa kufiwa na mzazi wake, kazi yake ni kujiendekeza na mapenzi.

Picha zilizozua mijadala mitandaoni.

Trump Amtumbua Mkuu wa Utumishi Serikalini

$
0
0
Rais Donald Trump wa Marekani amemteua Waziri wa Mambo ya Ndani, John Kelly kuwa mkuu wa utumishi wa Serikali baada ya kumwachisha kazi Reince Priebus.

Priebus amefanya kazi kwenye Serikali hiyo kwa muda wa miezi sita tu.

Baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuhusu hatima ya Priebus, Trump ametangaza uamuzi wake kwenye mtandao wa Twitter akiwasili mjini Washington.

Awali, Trump alitoa hotuba jijini New York ambayo aliitumia kummwagia sifa Kelly kwa kazi anayofanya katika wizara hiyo.

Amesema ,"Nina furaha kuwafahamisha nimemteua waziri John Kelly kuwa mkuu wa utumishi wa Serikali katika Ikulu."

Mwenyekiti wa Kijiji Jela Miaka Mitatu kwa Rushwa ya Sh.20,000

$
0
0
Mwenyekiti wa Kitongoji cha German, Kijiji Machochwe wilayani hapa Mkoa wa Mara, Ibrahim Magere amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh500,000 kwa kosa la kuomba rushwa ya Sh20,000.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu wa Wilaya ya Serengeti, Amalia Mushi alisema mshtakiwa ametiwa hatiani katika kesi ya jinai namba 37/2017 kufuatia ushahidi uliotolewa upande wa Takukuru kutoacha shaka.

Kabla ya hukumu hiyo, Wakili wa Takukuru, Eric Kiwia alidai kuwa mshtakiwa aliomba Sh20,000 kutoka kwa Joseph Rhobi mkazi wa kijiji hicho aliyekamatwa kwa madai kuwa alikuwa akitafutwa na polisi.

Aliendelea kuwa Rhobi mwaka 2012 alikamatwa na askari wa Kituo kidogo cha Polisi Machochwe, lakini alitoroka akiwa amefungwa pingu ambazo baadaye alizisalimisha kwa mtendaji wa kijiji.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Rhobi alihitaji barua ya utambulisho kutoka ofisi ya kijiji, hivyo mwenyekiti huyo alitoa taarifa polisi na mtuhumiwa alikamatwa.

Hata hivyo, Rhobi aliachiwa kwa dhamana hivyo Mwenyekiti wa Kitongoji alimdhamini huku akimdai Sh20,000 kumaliza suala hilo hali iliyosababisha kutoa taarifa Takukuru na kufanikisha kukamatwa.

Mshtakiwa alipelekewa magereza baada ya kushindwa kulipa faini ya Sh500,000.

Wakili wa Lissu, Fatma Karume amburuza kortini askari Polisi Aliyemshika Mkono Mahakamani....Anadai Fidia ya Bilioni Moja

$
0
0
Wakili wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Fatma Karume amefungua kesi ya madai Mahakama Kuu ya Tanzania dhdi ya Inspekta wa Polisi Eugene Mwampondela wa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es salaam.

Fatma amesema kuwa Inspekta Mwampondela alimshika mkono na kumvuta kwa nguvu hali iliyomsababishia maumivu makali, hivyo anadai alipwe kiasi cha shilingi bilioni moja kwa kosa la kumwingilia mwilini mwake na kumbughudhi kwa kumzuia kufanya kazi yake.

“Aliniambia kuwa ameagizwa na wakubwa kutoka juu, hivyo namfikisha mahakamani ili amweleze jaji ni nani aliyemtuma, na mimi sitaki kushikwa shikwa mwili wangu kwa hiyo naomba anilipe shilingi bilioni moja ili liwe fundisho kwa wengine,”amesema Fatma.

Fatma ambaye ni mmoja wa mawakili wa Mbunge wa Singida Mashariki alikumbana na kadhia hiyo wakati akiwa katika harakati za kumtetea mteja wake ili aweze kupata dhamana.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images