Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

CDA Wadaiwa Kuficha Viwanja 34,000

$
0
0
Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amedai kuwa waliokuwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) wameficha zaidi ya viwanja 34,000.

Lukuvi ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa CDA kwa miaka kadhaa, pia amesimulia jinsi wabunge wanne walivyotapeliwa na wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

Hivi karibuni, Rais Dk. John Magufuli aliifuta mamlaka hiyo na shughuli zake kuhamishia Manispaa ya Dodoma.

Akizungumza mjini hapa jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Chama cha Wapima Ardhi Tanzania (IST), Lukuvi alisema viwanja vilivyopimwa Manispaa ya Dodoma vilikuwa 60,000, lakini vilivyoonekana ni 26,000 tu huku 34,000 vikiwa vimefichwa na wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

Alisema baada ya kufanya uchunguzi, Serikali imegundua wafanyakazi wengi wameiba viwanja na kuviuza kwa watu wengine.

Lukuvi alisema kulikuwa na utaratibu wa wafanyakazi wa CDA kuuza viwanja kwa njia za panya kwa Sh milioni 5, kisha mhusika kupelekewa nyaraka mahali alipo.

Alisema kuna wabunge wanne waliuziwa viwanja kwa kutoa Sh milioni 5, lakini kesho yake rais akaivunja mamlaka hiyo na kujikuta wakitapeliwa.

Lukuvi alisema wabunge hao walikwenda kumlilia wakitaka kurudishiwa fedha hizo, lakini jambo la kushangaza hawakuwa na ‘invoice’ ya aina yoyote.

“Sasa wapo watu ambao wamewalipa hizo milioni tano,halafu kesho yake ikala kwao, Mheshimiwa Rais kaifuta CDA, ndiyo wanakuja kusema kwangu, watalipwaje? Nimewaambia nipeni risiti wanasema hawana. Nitawapa kitu gani? Majina ninayo,” alisema.

Alisema wale wote walioiba viwanja hivyo vitawatokea puani, kwani Serikali tayari inayo ripoti nzima juu ya wizi huo.

 “Serikali inakosa mapato, sasa tunataka viwanja vipimwe vingi ili tuweze kujiingizia mapato,” alisema.

Aidha Lukuvi alimbana aliyekuwa Mpimaji Mkuu wa CDA, Frank Mkomochi ambaye alikuwapo katika mkutano huo, akidai kuwa ni mmoja ya watu waliohuka kusimamia uuzwaji wa viwanja maeneo mengi.

“Viwanja Itega vilikuwa vinauzwa milioni tano, sasa vinauzwa milioni 25, hili hujalisikia wewe mtu wa CDA?” alimuhoji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa IST, Martin Chodota, aliomba Serikali kutoa kipaumbele kwa kampuni za wazawa na kuacha kuwapa nafasi zaidi wapimaji wanaotoka nje.

Hakimu Ajitoa Kusikiliza Kesi ya Godbless Lema

$
0
0
Hakimu  Mkazi, Desderi Kamugisha, amejitoa kuendelea kusikiliza moja ya kesi za uchochezi zinazomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema).

Katika kesi hizo, Lema anadaiwa kutoa matamshi yenye chuki na kuibua nia ovu kwa jamii.
 
Hakimu Kamugisha amejitoa katika kesi ya jinai namba 441/2016 ambayo Lema anadaiwa kutoa matamshi hayo Oktoba 23, mwaka jana wakati wa mkutano wa hadhara viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa.

 “Kiburi cha Rais kisipojirekebisha, Rais akiendelea kujiona yeye ni Mungu, mwaka 2020 haitafika Mungu atakuwa ameshamchukua maisha yake.

“Rais ana kiburi, Rais kila mahali watu wanaonewa, wafanyakazi wa Serikali hawana amani, wafanyabiashara hawana amani, watu wananyanyaswa,” Lema alinukuliwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Martenus Marandu.

Hakimu huyo sasa ataendelea kusikiliza kesi nyingine ya jinai namba 440/2016 ambayo pia inamhusu Lema anayedaiwa kutoa maneno ya uchochezi yenye kuleta tabaka miongoni mwa jamii Oktoba 22, mwaka jana maeneo ya Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro wakati wa mkutano wa hadhara.

Miongoni mwa maneno ambayo Lema anayodaiwa kuyatoa ni: “Rais Magufuli akiendelea na tabia ya kudhalilisha demokrasia na uongozi wa upinzani, iko siku taifa litaingia kwenye umwagaji wa damu.

 “Rais yeyote ambaye haheshimu mipaka ya sheria, mipaka ya katiba, ataingiza taifa katika majanga na umwagaji damu, watu watajaa vifua, wakiamua kulipuka polisi hawa wala jeshi halitaweza kudhibiti uhalifu utakaojitokeza.”

Jana kesi hizo mbili zilipangwa kutajwa mbele ya Hakimu Kamugisha katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, lakini Wakili wa Serikali, Alice Mtenga, alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi umekamilika, hivyo wanaomba kupangiwa tarehe ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Lakini Hakimu Kamugisha alisema haoni busara kuendelea kusikiliza kesi zote wakati kuna mahakimu wengine.
 
“Nilikuwa na kesi nne za mshtakiwa huyu huyu, sasa zimebaki mbili. Kwangu sioni kama itakuwa busara  kusikiliza kesi zote wakati kuna mahakimu wengine wanaweza wakasikiliza, najiondoa kwenye kesi namba 441, nitaendelea na kesi moja namba 440.

“Ukiangalia nature ya kesi ni ile ile moja, mshtakiwa yule yule, kwa hiyo tutaenda kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi ili apangiwe hakimu mwingine wa kusikiliza kesi hiyo ili tarehe ya kusomwa maelezo ya awali itakayopangwa, asikilize hakimu mwingine,” alisema.
 
Katika kesi hizo, Lema anawakilishwa na Wakili Sheck Mfinanga.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo hakuweza kufika mahakamani hapo jana kwa madai kuwa hawakuwa na taarifa za kesi hizo kupangwa.
 
“Nilikuwa nimesimama kwenye korido ya mahakama asubuhi nikamuona RCO, nikamuuliza kuna nini akanijibu amekuja kwenye hizi kesi, ndipo nikaamua kuja mahakamani ila Lema au wadhamini wake hawakufika,” alisema Mfinanga.

Lema alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Kamugisha Novemba 8, mwaka jana, akikabiliwa na kesi hizo.
 
Novemba 11, mwaka huo huo, alishindwa kupata dhamana baada ya mawakili wa Serikali kuwasilisha kwa njia ya mdomo kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kupinga uamuzi wa dhamana uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Lema alikaa mahabusu ya Gereza Kuu la Kisongo kwa zaidi ya miezi minne kutokana na kukosa dhamana kuanzia Novemba 11 mwaka jana kabla ya kuachiwa kwa dhamana Machi 3, mwaka huu na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

TANZIA: Mzee aliyebuni na kuchora Nembo ya Taifa AFARIKI Dunia

Kairuki: Serikali Haitaajiri Walimu wa Masomo ya Sanaa

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amefunguka na kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za sekondari.

Angela Kairuki amesema hayo leo bungeni na kudai kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao

"Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya" -alisema Angela Kairuki

Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 watumishi zaidi ya elfu tisa wameajiriwa serikalini.

"Katika mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya watumishi wa Umma 9721 wamekwisha ajiriwa kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya kila mwajiri na katika mwaka wa fedha 2017/18 serikali inatarajia kuajiri watumishi 52436 wa sekta mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa pamoja na kuimarisha kila sekta na upungufu mkubwa wa watumishi wa Umma"  -alisema Kairuki

Walemavu walioungana wampata kijana wa kuwaoa

$
0
0
Kwa yeyote aliyewahi kukutana nao, mapacha wawili ambao ni walemavu walioungana matumbo, Maria na Konsolata hatabisha kwamba pamoja na hali yao, watoto hao ni wacheshi, wakarimu na wanaoweza kukufanya utabasamu hata kama moyoni mwako, ulikuwa na huzuni

Wiki hii walifanyiwa mahojiano na Gazeti la Mwananchi na kufunguka mengi kuhusu maisha yao pamoja na ishu yao ya kufikiria kuolewa.

    Si rahisi kufikiria maisha ya ndoa ya Maria na Consolata kwa jinsi walivyo, lakini pacha hawa walioungana wako wazi kuhusu matamanio yao ya maisha ya ndoa.

    Katika mazungumzo yao na gazeti hili, Maria na Consolata waliweka bayana mipango yao ya ndoa mara watakapomaliza elimu ya chuo kikuu.

    Ingawa ni kitu cha kushangaza, Maria na Consolata hawatakuwa mapacha wa kwanza katika maisha ya ndoa. Chang na Eng Bunker ni pacha wanaume waliozaliwa mwaka 1811 nchini Thailand ambako zamani kuliitwa Siame.

 Tofauti na mapenzi ya akina Maria na Consolata, pacha hao kila mmoja alioa mke wake na kufanikiwa kupata watoto.
Kama ilivyokuwa kwa pacha hao, Maria na Consolata wanatamani kuwa wanandoa na ndoto zao ni kuolewa na mwanaume mcha Mungu na atakayewajali.

    “Ndoa ni sakramenti takatifu, tukishamaliza masomo yetu ya chuo kikuu tunatamani kuja kuwa wanandoa,” anasema Maria.

    Kwa namna walivyo, si rahisi kwao kuolewa na wanaume tofauti isipokuwa mume mmoja na wanalijua hilo.

    Haya ndio yalikuwa mahojiano baina yangu na wao kufuatia ndoto hiyo.

    Mwandishi: Baada ya masomo, nini ndoto zenu?

    Maria: Ndoto zetu ni kuwa wanandoa. Zamani tulikuwa tunapenda tofauti, lakini kwa sasa tumempenda mtu mmoja.

    Tumegundua tuna hisia moja.

    Mwandishi: Tayari kuna mtu mmempenda nini?

    Maria na Consolata kwa pamoja: Ndio tumempenda mtu mmoja.

    Mwandishi: Nani alimwambia mwenzake kwanza kuhusu hisia za kupenda?

    Consolata: Sisi ndio tuliomwambia kwamba tunampenda, naye alitusikiliza.

    Mwandishi: Aliwajibu nini?

    Maria: Yupo kwenye tafakari, hawezi kusema akurupuke na kuingia bila tafakari. Lazima tumpe muda wa kutafakari.
    Mwandishi: Ni mwanaume wa aina gani mnayempenda?

    Consolata; Tunapenda kuolewa na mwanaume wa kawaida, mwenye tabia njema na mcha Mungu asiwe tajiri. Ikiwa tutamaliza masomo yetu, huyu tuliyempenda anafaa kuwa mume wetu. Kihalisia tunatamani mwanaume mcha Mungu, mwenye upendo na ambaye atathamini utu wetu.

    Mwandishi: Kwa nini hampendi kuolewa na tajiri?

    Consolata: Ni kwa sababu matajiri wengi huwa wanathamini pesa zao sio utu. Samahani hapa sio matajiri wote, ila wengi wao kwa hiyo sisi tunataka mtu anayeweza kuthamini utu.

    Mwananchi: Ndoa ni mume na mke mmoja kwa Wakristo. Mmewahi kutafakari hilo?

    Consolata; Ndio, Biblia inasema kwamba Mungu aliweka agano kati ya mume na mke mmoja. Sasa kwa kuwa sisi tumeungana wawili na tuna hisia moja, hatuwezi kuolewa na wanaume tofauti. Tutaolewa na mume mmoja.

    Tunatamani sana kumtumikia Mungu kupitia sakramenti ya ndoa. Mungu akitujalia tumalize masomo yetu basi tunataka kuolewa ili tumtumikie Mungu katika huo wito vizuri.

    Pacha hao waliweka bayana jina la kijana waliyempenda, ingawa kwa sababu za kimaadili tunalihifadhi. Hata hivyo, baba mdogo wa kijana huyo alikuwa tayari kuzungumza na gazeti hili.

    Baba huyo mdogo alisema ana taarifa za kijana wao kupendwa na pacha hao.

    “Unajua nilishangaa kuona watu wananiita baba mkwe wa akina Maria na Consolata. Baadaye ndio nikajua kuwa kuna mahusiano baina yao (kijana na mapacha hao), japo wote wanaendelea na masomo. Kupenda ni moyo na kama ikitokea wakafikia ndoto hizo huko baadaye, basi itakuwa hivyo,” anasema.

    Mwalimu mkuu wa Shule ya Maria Consolata, Jefred Kipingi anasema hisia za kuolewa kwa mabinti hao ni jambo la kawaida na kwamba, wanapenda kuishi maisha ya kawaida kama walivyo watu wengine.

    “Uzuri wake ndoto yao ni kuwa walimu na wanasema wataolewa wakishamaliza masomo yao. Jambo hilo ni jema na hapo Mungu ndipo atadhihirisha utukufu wake zaidi,” anasisitiza.

    Ingetegemewa kwamba katika dunia ya utandawazi, taarifa za kuzaliwa kwa pacha walioungana zingetapakaa kila mahali zikipamba magazeti, redio, luninga na hata mitandao ya kijamii.

    Lakini haikuwa hivyo kwa Maria na Consolata. Hakuna chombo chochote kilichopata taarifa ya kuzaliwa kwa pacha hao wa kipekee.

    Ulemavu wao ulisababisha wafichwe hadi walipofikisha umri wa kuandikishwa elimu ya msingi katika Shule ya Ikonda na kutafutiwa mlezi wa kuwaangalia, baada ya wazazi wao kufariki dunia wakiwa wadogo.

    Habari zao zilianza kufahamika baada ya kuandikishwa darasa la kwanza na kutafutiwa mlezi aliyewalea hadi wakati walipofaulu vizuri mitihani yao ya darasa la saba mwaka 2010.

    Mlezi wao, Bestina Mbilinyi alikuwa alifanya hivyo chini ya wamisionari lakini, alikuwa akiishi nao nyumbani kwake Ikonda.

    “Niliombwa niishi na watoto hawa kwa sababu kutoka kwangu hadi shuleni sio mbali, nilijengwa choo kinachokidhi maumbile yao na niliishi nao hadi wanamaliza darasa la saba,” alisema wakati akizungumza na Mwananchi wakati walipomaliza darasa la saba

Wenger aongezwa mkataba wa miaka 2 Arsenal

$
0
0
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekubali kuchukua mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo, hatua itakayoendeleza muda ambao amekaa katika klabu hiyo.

Mfaransa huyo amekuwa meneja wa Arsenal kwa miaka 21 sasa.

Wenger na mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke walikutana Jumatatu kuamua hatima ya meneja huyo, na kisha uamuzi wao ukawasilishwa kwa mkutano wa bodi Jumanne.

Arsenal wanapanga kutangaza rasmi uamuzi huo Jumatano.

Gunners walimaliza Ligi ya Premia wakwia nafasi ya tano, mara yao ya kwanza kumaliza chini ya nafasi ya nne tangu Wenger alipojiunga nao mwaka 1996.

Walimaliza alama 18 nyuma ya mabingwa Chelsea, lakini walifanikiwa kuwachapa Blues katika fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley Jumamosi.

Mkataba wa Wenger ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Wenger aliongoza Gunners kushinda mataji matatu ya Ligi ya Premia na pia vikombe vinne vya FA misimu yake tisa ya kwanza kwenye usukani.

Mwaka 2003-04, aliibuka meneja wa kwanza tangu 1888-89 kuongoza timu iliyomaliza ligi kuu bila kushindwa.

Lakini baada ya kushinda Kombe la FA mwaka 2005, walisubiri kwa miaka mingine tisa – sawa na siku 3,283, kabla ya kushinda kikombe kingine.

Walilaza Hull City fainali ya Kombe la FA mwaka 2014 na kisha wakashinda kikombe hicho tena mwaka uliofuata.

Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakimtaka Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 67 ajiuzulu, hasa baada ya matokeo mabaya msimu huu. Shutuma zaidi zilitolewa waliposhindwa kwa jumla ya mabao 10-2 na Bayern Munich katika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi Machi.

Walimaliza msimu wakiwa wameshinda mechi tano mfululizo, lakini matokeo hayo hayakutosha kuwawezesha kuwapita Liverpool waliomaliza nafasi ya nne na kujaza nafasi ya mwisho ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Jumamosi, Wenger aliambia BBC kwamba shutuma na uokosoaji aliokumbana nao msimu huu ni wa “kufedhehesha” na kwamba hatawahi kuusahau kamwe maishani.

Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari kwa wakazi wa ukanda wa pwani

$
0
0
Mamlaka ya hali ya hewa imetoa tahadhari  kubwa kwa wakazi wa ukanda wa pwani kuwa kutakuwepo na upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya bahari ya Hindi.

Aidha, katika Maeneo yanayotarajiwa kukumbwa na hali hiyo ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Katika taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo, imesema kuwa kunatarjiwa kuwepo na upepo mkali wa kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayozidi mita 2 baharini hivyo watumiaji wote wa bahari wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa.

Hata hivyo, hali hiyo inasababishwa na msukumo wa upepo wa kusi unaotokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda pwani hivyo kusababisha hali hiyo kutkea.

Habari zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 31


Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 31, 2017

$
0
0
Fuatilia hapa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayoendelea Mjini Dodoma leo Mei 31, 2017. 

Bofya hapa kutazama

Atiwa Mbaroni kwa kutumia nguo za Jeshi la JWTZ kutapeli

$
0
0
Na Tiganya Vincent, Tabora
Mkulima mmoja Kitangili mkoani Shinyanga Francis Martin Kilalo (31) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kufuatia kukutwa na sare na vifaa vingine vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambavyo anatuhumiwa kuvitumia kupateli nakuwadanganya kwa kuchukua fedha kutoka kwa vijana wanaotafuta nafasi yakujiunga na Jeshi hilo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mtafungwa alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi kwake juu ya hatua mbalimbali walizochukua katika kupambana na uhalifu mkoani humo.

Alisema kuwa Polisi walifanikiwakumukamata mtuhumiwa huyo katika Hoteli ya JM iliyopo Wilayani Igunga akiwa na sare mbalimbali za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) zikiwa na cheo cha Koplo ambavyo ni pamoja na kofia tatu, begi, sweta, buti jozi moja, magwanda na mikanda mitatu.

Mali nyingine zilikamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni pamoja na fomu za likizo, fomu za kujaza vijana wanaotaka kujiunga na Jeshi hilo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa Sheria na hiari na mihuli zenye nembo inayofanana na Jeshi hilo.

Kamanda Mtafungwa alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa akitumia nyaraka na sare za Jeshi hilo kuchukua fedha kwa kuwadanganya na kuwatapeli wananchi mbalimbali kwa kudai atawatafutia ajira katika majeshi ya Kujenga Taifa na la Wananchi.

Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo pia alikutwa na barua kutoka Serikali za mitaa za Dar es salaam na gari aina ya Toyota Starlet yenye namba za Usajili T633 ARF ambalo wanaendelea kuchunguza uhalali wa umiliki wake na ambalo mtuhumiwa alikuwa akilitumia na kuwafanya baadhi ya wananchi wamuamini kuwa atawasaidia kupata nafasi katika majeshi.

Aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo  na barua za maombi ya watu yakuomba kujiunga na Jeshi, Fomu za Matibabu za Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na kalaya Vyeti vya kumaliza elimu ya Sekondari vya baadhi ya watu.

Kufuatia tukio hilo alitoa witokwa waananchi waliowahi kutapeli ndani na nje ya Mkoa wa Tabora kujitokeza katika vituo vya Polisi ili waweze kutoa ushahidi utakasaidia kuonyesha ni jinsi gani walivyumizwa na mtuhumiwa huyo .

Kamanda Mtafungwa alisema kuwa Polisi inaendelea kushirikiana na JWTZ ili iweze kubaini sare na vifaa hivyo alivipata wapi , kwa lengo lipi na ni nani aliyompatia ili wahusika wote waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria kwa hatua zaidi.

Aidha, Kamanda huyo aliwaasa wananchi kuwa makini na matapeli wanaowadai fedha na kuwadanganya kuwa watawatafutia kazi katika Majeshi kwani vyombo hivyo vinaotaratibu wake ambao ndio unaotumika kuwapata vijana wanaojiunga kwa mujibu wa sheria na wale wahiari na sio kwa kuchangishwa fedha.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limefanikiwa kukamata watuhimiwa 17 kwa kukutwa na lita 205.25 za gongo wakati wa msako wa kukamata wa watumiaji na wauzaji wa bidhaa hizo haramu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora Mtafungwa alisema kuwa watuhimiwa watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zao wakati wowote. Aidha, alisema kuwa katika zoezi hilo pia Polisi ilifanikiwa kuteketeza ekari tano na nusu za mashamba ya zikiwana uzito wa kilogramu 220 yalikuwa yamelimwa katika Msitu wa Hifadhi wa Igombe wilayani Uyui.

Alisema kuwa jitihada za kuwasaka watuhumiwa wa mashamba hayo zinaendelea na kuwaomba wananchi wenye taarifa yawalipo wahusika walisaidie Jeshi la Polisi ili wahusika waweze kufikishwa Mahakama kujibu tuhuma zao.

Yeriko Nyerere Atiwa Mbaroni saa tisa usiku

$
0
0
Kada wa Chadema Yeriko Nyerere, amekamatwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi au usalama wa taifa  leo akiwa nyumbani kwake Kigamboni, Mbutu.

Taarifa iliyotolewa na Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob imeeleza kuwa Nyerere alikamatwa na watu hao ambao waliambatana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbutu.

“Nimepata taarifa kutoka kwa ndugu wa Yeriko ambao wamenipigia simu alfajiri leo. Wamesema amekamatwa saa tisa usiku na watu hao ambao walivalia kiraia.  Viongozi wa Chadema wanaelekea polisi kufuatilia kwa kina chanzo cha Yeriko kukamatwa,” amesema Jacob

Wizara ya Fedha yaliomba Bunge Sh 11.7 trilioni ......Isome hapa hotuba ya bajeti ya Wizara Hiyo 2017/18

$
0
0
Wizara ya Fedha na Mipango imeliomba Bunge iliidhinishie Sh11.757trilioni ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote tisa yaliyo chini ya Wizara hiyo.
 
Maombi hayo yametolewa jana na Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mpango, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaya hiyo, Bungeni Mjini Dodoma.
 
Dk Mpango alisema kuwa kati ya fedha hizo, Sh10.328trilioni  ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh1.429trilioni  ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
 
Alifafanua kuwa matumizi ya kawaida yanajumuisha Sh87.996bilioni kwa ajili ya mishahara, Sh778.6bilini kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC) na Sh9.4trilioni ni kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa na Huduma nyingine.
 
Pia katika fedha za matumizi ya maendeleo, Sh1.382trilioni  ni fedha za ndani na Sh46.1bilioni ni fedha za nje.

==>Isome hapa hotuba ya bajeti ya Wizara  Hiyo  hapo chini

Marekani yaanza kujipanga Kukabiliana na makombora ya Korea Kaskazini

$
0
0
Marekani imesema kuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika jaribio lake la kwanza la mtambo wa kutungua makombora ya nyuklia ya masafa marefu.

Mtambo huo wa ardhini umefungwa katika kambi ya kijeshi iliyopo Califonia kwaajili ya kujihami na vitisho ambavyo vimekuwa vikitolewa na maadui zake ikiwemo Korea Kaskazini.

Aidha, Pentagon imesema kuwa jaribio hilo limefanyika baada ya Korea Kaskazini kufanya majaribio yake ya makombora tisa ya masafa marefu mwaka huu hivyo kutishia usalama wa nchi hiyo.

“Mfumo huu ni mhimu sana kwa ulinzi wa taifa letu na jaribio hili ni uthibitisho mkubwa kwamba tuna uwezo wa hali ya juu wa kujilinda na kutetea usalama wa raia wetu,” amesema Mkurugenzi wa kitengo cha ulinzi wa makombora, Admirali Jim Syring.

Makamu wa Rais kufanya ziara rasmi ya siku tatu mkoani Mara

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kufanya ziara rasmi ya siku tatu kuanzia tarehe 05 Juni, 2017  Mkoani Mara.

Kwa mujibu wa ratiba ya Mkoa, Mhe Samia atatembelea Wilaya ya Tarime, katika Kituo cha Afya cha Nyamwaga kinachojengwa na wananchi kwa msaada wa Mgodi wa Acacia North Mara.

Pia, Mhe. Makamu wa Rais atapata fursa ya kutembelea Bonde la Mto Mara kunakokusudiwa kuanza kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari.  Mchana siku hiyo hiyo atafanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Bisarwi; katika eneo hilo kunakusudiwa kujengwa kiwanda cha sukari.

Aidha tarehe 6/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais ataenda Wilaya ya Serengeti ambapo ataweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Wilaya; mchana atafanya Mkutano wa Hadhara katika Uwanja wa Mbuzi, Mugumu mjini.

Tarehe 7/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais atakuwa Musoma ambapo ataweka jiwe la msingi kwenye barabara ya km. 9.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Musoma. Pia atatembelea kiwanda cha Samaki cha Musoma Fish Processors (T) Ltd na kufanya Mkutano wa Hadhara katika uwanja wa Mukendo Musoma Mjini.

Hii ni mara ya kwanza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa na ziara rasmi Mkoani Mara.

Godbless Lema: Yeriko Nyerere amekamatwa au ametekwa?

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema ameuliza swali je, Yeriko Nyerere amekamatwa au ametekwa?
 
Lema ameuliza swali hilo katika ukurasa  wake wa Twitter leo na kuongeza: “Msiogope. Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. "
 
Yeriko anayefahamika kuwa ni kada wa Chadema, amekamatwa leo saa tisa alfajiri na watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi akiwa nyumbani kwake, Kigamboni, Mbutu.
 
Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amethibitisha kukamatwa kwa Yeriko.

Breaking News: IGP Simon Sirro Kaongea na Waandishi wa Habari kwa Mara ya Kwanza na Kutangaza Dau la Milioni 10

$
0
0
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro kwa mara ya kwanza amefanya mazungumzo maalum na wanahabari jijini Dar es Salaam na kutangaza dau nono la Sh10 milioni kwa atakayetoa taarifa kuhusu mauaji ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga. 

“Niwaambie ukweli kuwa katika hili, maneno yatakuwa machache lakini vitendo vitakuwa vingi zaidi,” amesema katika mkutano huo.

Pia IGP Sirro amewatangazia kiama madereva wa bodaboda na kuwataka kuacha kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi.

“Huu ni wakati wa kutii utawala wa sheria bila shuruti na nimeshaongea na makamanda wa polisi nchi nzima,” amesema 


==>Msikilize hapo chini akiongea

Waziri Mwakyembe Atuma Salamu Za Rambirambi Kifo Cha Mzee Kanyasu aliyechora nembo ya Taifa

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Serikali itaenzi michango yote ya wasanii wakongwe hapa nchini.

Ameyasema hayo kufuatia kifo cha mzee aliyebuni nembo ya taifa, Mzee Francis Kanyasu maarufu kwa jina la ‘Ngosha’ aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwaajili ya kupatiwa matibabu.

“Tutaendelea kuwa karibu na familia ya marehemu Mzee Francis Kanyasu, kwani katuachia alama kubwa sana na mchango wake katika Taifa utakumbukwa milele”, amesema Dkt. Mwakyembe.

Hata hivyo, katika kushiriki msiba huo, Mwakyembe atawakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza ambapo atakuwa akiiwakilisha Serikali.

Breaking News: Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) afariki dunia

$
0
0
Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema) Philemon Ndesamburo amefariki dunia ghafla leo, wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi.
 
Katibu wa Chadema, Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa wataendelea kutoa taarifa zaidi juu ya kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe.
 
Taarifa zaidi kuhusu kifo cha Ndesamburo zitaendelea kukujia.

Taarifa ya Bunge kuhusu kifo cha Mbunge Mstaafu, Philemon Ndesamburo

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images