Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Aomboleza Kifo Cha Mzee Ndesamburo, Atuma Salamu Za Rambirambi

$
0
0
“Kwa masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31 Mei, 2017 katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa za kistaarabu”

Hii ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo, Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na kifo hicho.

Mhe. Rais Magufuli amesema alifanya kazi na Marehemu Philemon Ndesamburo wakati wote wakiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wote walishirikiana, kutaniana na anamkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake bungeni kupigania mambo yenye maslai kwa wananchi wa jimbo lake la Moshi Mjini.

Mhe. Dkt. Magufuli ameitaka familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo na wote waliguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu na amemuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
31 Mei, 2017

Uamuzi wa serikali baada gazeti la TanzaniaDaima kuchapisha habari ya uongo

Mwili wa Ndesamburo wafanyiwa uchunguzi

$
0
0
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Bazil Lema amesema mwili wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Moshi mjini Phillemon Ndesamburo unafanyiwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo chake cha ghafla.
 
Lema amesema Ndesamburo alifika ofisini kwake asubuhi kama ilivyo kawaida yake lakini aliugua ghafla mnamo saa nne asubuhi.
 
Bazil alisema baada ya Ndesamburo kujisikia vibaya, alichukuliwa na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC na wakati madaktari wanakifanya jitahada za kumpa matibabu alifariki dunia.
 
“Baada ya mwili kufanyiwa uchunguzi taarifa rasmi kuhusu kifo chake zitatolewa na uongozi wa chama pamoja na familia,” amesema
 

Zitto Kabwe Amlilia Ndesamburo

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe ametuma salamu za rambi rambi kwa wanachama wa Chadema  baada ya kuondokewa na kiongozi wake mkubwa, Philemon Ndesamburo.

 Pia Zitto amempa pole, mtoto wa marehemu Ndesamburo, Lucy Owenya kwa kumpoteza baba yake.

Zitto ameandika katika ukurasa wake wa Facebook leo na kusema; “Ni msiba mkubwa kwa watu wa Kilimanjaro na hasa Moshi Mjini ambapo Mzee Ndesa Pesa alikuwa mwakilishi wake Bungeni kuanzia Mwaka 2000 mpaka Mwaka 2015. Kilimanjaro imepoteza mtu ambaye aliweka maslahi ya mkoa wake mbele kuliko kitu kingine chochote.”

Zitto amesema msiba wa Ndesamburo ni mkubwa kwa wanaChadema ambacho alikuwa Mwenyekiti wake wa  Mkoa tangu chama kimeanzishwa mpaka mauti yalipomkuta.

 “Huwezi kutaja maendeleo ya Chadema kwa nchi yetu bila ya kutaja jina la mzee Ndesamburo. Nimepata bahati ya kufanya naye kazi kwa karibu, naweza kutamka bila wasiwasi kwamba ni mmoja wa watu waliokipenda chama chake kwa dhati kabisa,” amesema

Kadhalika Zitto anaendelea kummwagia sifa Ndesamburo akisema Tanzania ina faidi matunda ya vyama vingi kwa sababu ya kazi kubwa aliyofanya Mzee Ndesamburo.

“Nawapa pole Sana watoto, wajukuu na vitukuu vya Mzee Ndesamburo. Mzee wetu aliishi maisha yake na ameacha ' legacy ' yake. Najua maumivu yenu lakini tupo wengi tunaoumia nanyi. Mungu awavushe kwenye mtihani huu mkubwa. muwe wamoja na mshikamane.” Amesema na kuongeza:

“Poleni sana ndugu zangu wa Chadema kwa kupotelewa na kiongozi wenu na kiongozi wetu pia.  Poleni sana wana Moshi Mjini na wana Kilimanjaro wote. Poleni Sana Watanzania.pumzika kwa Amani Philemon Kiwelu Ndesamburo. Hiyo ni njia yetu sote. Amina.”

Gazeti La Tanzania Daima Lakiri Kukosa Umakini, Laomba Radhi

Rais Magufuli afanya uteuzi wa Naibu Magavana wawili wa Benki Kuu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Mei, 2017 amefanya uteuzi wa Naibu Magavana wawili wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha (Economic and Financial Policies – EFP).

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Yamungu Kayandabila alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazina anachukua nafasi iliyoachwa na Dkt. Natu E. Mwamba ambaye amemaliza muda wake.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Bernard Yohana Kibese kuwa Naibu Gavana anayeshughulikia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha (Financial Stability and Deepening – FSD).

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Bernard Yohana Kibese alikuwa ni Mtaalamu wa Uchumi na Fedha wa BOT na anachukua nafasi iliyoachwa na Lila H. Mkila ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
31 Mei, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya June 1

Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli leo wakati akizindua Mfumo wa serikali wa ukusanyaji kodi kwa njia ya Kieletroniki amewachana baadhi ya watumishi wake akisema wamekuwa wakiwaza mambo makubwa ambayo wanashindwa hata kuyatimiza.

Rais Magufuli amesema kuwa watumishi wengi wamekuwa si wabunifu katika kuangalia vyazo vya mapato ambavyo vinaweza kusaidia serikali kuingiza pesa nyingi lakini wao wamekuwa wakiwaza kuongeza bei ya pombe tu na kuacha vitu vingine ambavyo vingeweza kuongeza mapato kwa serikali kwa njia nyingine nzuri.

"Saizi watu wanahangaika na Machinga wakati tungeweza kutengeneza vitambulisho vya wamachinga na kila kimoja tukauza labda elfu kumi, Machinga akinunua kitambulisho hicho anatambulika na serikali na kinaeleza kuwa anapaswa kuwa wapi, je, ni shilingi ngapi tungezipata hapo kwa idadi wa wamachinga waliopo nchi nzima? Lakini watu wetu wao wanawaza kuongeza bei ya pombe tu, yaani tuna watu wa uchumi wengi lakini sijui hata wanafikiria nini " alisema Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli alisema hata tabia ya watu kukwepa kulipa kodi inasababishwa na mipango mibovu akitolea mfano kuwekwa bei juu ya kodi ya majengo jambo ambalo linafanya watu wengine kushindwa kulipa kodi hiyo na serikali kupoteza mapato.

"Watu wetu hawa hata kwenye kodi ya majengo unakuta wameweka mtu alipe milioni mbili sasa hizo pesa wananchi wanazipata wapi? Ndiyo maana wanakwepa kodi sababu hawana pesa hizo lakini kama wangeweka labda elfu kumi, ishirini mpaka hamsini halafu wenye maghorofa labda laki mbili ungeona kila mtu angekimbilia yeye mwenyewe kulipa kodi, kwa nyumba zote zilizopo Tanzania tungepata shilingi ngapi? Lakini wameweka pesa kubwa na hawazipati sababu watu hawalipi hawana hizo pesa" alisisitiza Rais Magufuli

Katika hatua ya mwisho Rais Magufuli aliyaomba makampuni ya simu nchini yawe mfano wa kuingwa na ikiwezekana yawe ya kwanza kabisa kujiunga katika mfumo huu mpya wa ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kieletroniki kwani mfumo huu una manufaa kwa wawekezaji na Watanzania kwa ujumla.

Bendera ya CHADEMA Kupeperuka Nusu Mlingoti

$
0
0
Kufuatia kifo cha mmoja wa Waasisi wa CHADEMA, Mzee Philemon Ndesamburo Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji, ametoa maelekezo kwa watendaji nchi nzima kupeperusha bendera nusu mlingoti

Mashinji ametoa maelekezo hayo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam na kusema bendera zinapaswa kupeperushwa nusu mlingoti hadi mwili wa kiongozi huyo utakapopumzishwa katika nyumba yake ya milele.

"Chama kitashiriki katika msiba huu kwa heshima zote kumuenzi mmoja wa waasisi wa siasa za mabadiliko ya kweli na Uhuru wa kweli nchini, msiba huu ni msiba wa CHADEMA, ni msiba wa Watanzania, ni msiba wa Taifa letu kutokana na mchango mkubwa wa Mzee wetu kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa nchi yetu, Mhe. Ndesamburo ndiye aliyekifadhili Chama kwa mara ya kwanza kwa kukipatia ofisi eneo la Kisutu jijini Dar es salaam" amesema Dkt. Mashinji

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 2

Binti wa Miaka 21 Atiwa Mbaroni kwa kuchoma moto nyumba sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Singida,linamshikilia mkulima mkazi wa Mitunduruni mjini hapa, Mariamu Juma (21), kwa tuhuma ya kuchoma nyumba moto na kuteketea pamoja na mali zote zilizokuwemo.
 
Kwa mujibu wa kamanda Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Debora Magiligimba, kitendo hicho kimechangiwa na wivu wa kimapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda Magiligimba,alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 30 mwaka huu saa 11.40 jioni, huko maeneo ya Mwenge tarafa ya Mungumaji Manispaa ya Singida.

Akifafanua, alisema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alienda kwenye nyumba aliyopanga mpenzi yake Benardo Mabula, ambayo inamilikiwa na Omari Hamisi (35) katika maeneo ya Mwenge mjini hapa.

“Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi  umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo, ni wivu wa kimapenzi. Mtuhumiwa Mariamu alipoingia kwenye chumba cha rafiki yake wa kiume (Mabula),aliwasha moto kwa kiberiti kwa lengo la kuchoma vifaa vya mpenzi wake,” alisema na kuongeza;

“Lakini  moto huo ulisambaa vyumba vyote vya nyumba hiyo na kuteketeza kila kitu.Hadi sasa thamani ya nyumba na mali iliyoteketea, bado haijafahamika.”

Kamanda huyo alisema kuwa baada ya uchunguzi kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili. Mpenzi wa mtuhumiwa Mariamu,amefanikiwa kutoroka na kukimbilia kusikojulikana.

“Jeshi la Polisi mkoani hapa,linatoa wito kwa wananchi wote hasa familia zenye migogoro ya ndoa,wafike ofisi zetu za dawati la jinsia na watoto zilizopo kila wilaya, ustawi wa jamii na viongozi wa dini, ili waweze kusikilizwa matatizo yao, badala ya kujichukulia sheria mkononi,” alisema Magiligimba.

Katika hatua nyingine, Kamanda huyo alisema vikongwe  wawili  wamefariki dunia papo hapo, baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba iliyojengwa kwa tofali za tope na kuezekwa kwa bati.

Magiligimba alisema vikongwe hao na watu wengine, walikuwa kwenye nyumba hiyo, kushiriki mazishi ya Mwajuma Mwendo aliyefariki Mei, 28 na kuzikwa kesho yake.

Aliwataja vikongwe  hao kuwa ni Nzitu Mkumbo (80) mkulima kwa kijiji cha Mwangeza ambaye alivunjika miguu yote na mkono wa kushoto.Mwingine ni Kimwana Kingu (90) mkulima wa kijiji cha Mazangila, ambaye alivunjika mguu wa kulia na kujeruhiwa vibaya mguu wa kushoto. Vijiji hivyo vipo wilaya ya Mkalama.

 Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Fatma Alli (70), Zena Ntoga (40), Kimwana Mohammed (70), Gyoli Kingu (45), Habiba Hussein (40) na Sophia Mashimba (50).

Alisema chanzo cha tukio hilo ni uchakavu wa nyumba hiyo iliyoanguka baada kupigwa na  upepo mkali na kusababisha ukuta wa ndani uliotenganisha chumba na sebule, kuanguka.

“Jeshi la polisi mkoa wa Singida,linatoa wito kwa wananchi wote wawe na utaratibu wa kukarabati nyumba zao mara kwa mara.Pia tunawashauri wapande miti kwa wingi kuzunguka maeneo ya makazi yao,” alisema kamanda Magiligimba.

Lowassa aeleza sababu za kutokuvaa sare za CHADEMA

$
0
0
"Si kweli kuwa sivai sare cha CHADEMA, hata nilipokuwa CCM nilikuwa nashona shati la rangi moja ama kijani au njano kisha naweka nembo maalumu ya chama, vivyo hivyo hata CHADEMA naweka nembo maalum.

"Na jambo kubwa hapa ni kuwa, nisihukumiwe kwa kuvaa au kutokuvaa sare za CHADEMA lakini kwa matendo yangu."

Hayo ni maneno yaliyotolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Ngoyai Lowassa alipokuwa akijibu swali la mtangazaji wa kituo cha Azam Tv, Charles Hillary aliyetaka kujua kwanini havai sare za CHADEMA katika matukio mbalimbali kama ilivyokuwa CCM.

Lowassa alienda mbali na kusema kuwa, sare si jambo kubwa sana kwani mtu anaweza kuvaa sare na bado akawa si mmoja wenu. Unaweza kukuta mtu kavaa nguo za kijani lakini kiukweli moyoni si wa CCM

Aidha, Lowassa alisema, alipomaliza Chuo Kikuu alikwenda jeshini na kwa muda wote huo alikuwa akivaa magwanda, hivyo alishavaa vya kutosha, na umri wake kwa sasa si wa kuvaa tena.

Alipoulizwa kama uamuzi wa kutokuvaa sare ni mbinu ya mwaka 2020 aweze kupata kuungwa mkono na wanachama wa CCM na CHADEMA, alicheka kisha akasema kuwa, kama ni mbinu basi anaamini itafanyakazi.

Mazishi Ya Ndesamburo Kufanyika Kwa Siku Mbili Mfululizo

$
0
0
Na Dixon Busagaga

MAZISHI ya Mbunge mstaafu wa jmbo la Moshi mjini na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Philemon Ndesamburo Kiwelu (82) yanataraji kufanyika kwa siku mbili mfululilizo huku watu zaidi ya laki 2 wakitaraji kushiriki katika mazishi hayo.

Shughuli nzima za mazisihi zinataraji kufanyika June 5 na sita katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi kabla ya kuhitimishwa siku ya Jumanne kwa ibada itakayoanzia kanisani na kumalizikia nyumbani kwa marehemu.

Hatua ya maziko ya Ndesamburo kufanyika kwa siku mbili inatokana na uwepo wa idadi kubwa ya marafiki wa familia kushiriki katika maziko hayo ya kihistoria yatakayotanguliwa na kutoa heshima za mwisho ,shughuli zilizopangwa kufanyika katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichodumu kwa zaidi ya saa nne ,Msemaji wa Chadema katika maandalizi ya mazishi hayo Amani Golugwa amesema uamuzi huo unatokana na kutoa nafasi kwa watu mbalimbali kutoa heshima za mwisho kwa Ndesamburo.

“Tumekua na kikao na wanafamilia viongozi wa chama na mashaurizano kuhusiana na msiba huu ,tumekuwa na watoto wa marehemu ,walikuwepo wachungaji na viongozi wa chama ,kimsini tumekubaliana mazishi ya mze wetu Ndesamburo yatafanyika kwa siku mbili mfululizo”alisema Golugwa.

Kutakuwa na siku mbili za maombolezi,siku ya jumatatu mwezi huu tutakuwa na state funeral (mazishi ya kitaifa) siku ambayo tutafanya kumbukizi ya maisha yake na tunataraji kuwa na idadi kubwa sana ya watu”alisema Golugwa.

Kwa upande wake msemaji wa familia ambaye pia ni motto mkubwa wa marehemu Ndesamburo,Sindato Ndesambur o alisema vikao mbalimbali vinaendelea kwa ajili ya maandalzi ya mazishi na kwamba yanataraji kutanguliwa na maandamano.

“Kama unavyoona bado tunaendelea na vikao kwa sasa ,kuona namna gani tunaweza kumuaga mzee wetu kwa heshima aliyojijengea kwa wakazi wa Moshi na taifa kwa ujumla “alisema Sindato.

Alisema wanatazamia kupokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi zikiwemo taasisi mbalimbali za kidini,kiserikali pamoja na wafanyabiashara watakao shiriki katika shughuli nzima ya mazishi .

Mapema jana vilio na Simanzi vilitawala chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ,wakati familia ya Marehemu  Ndesamburo  ikiongozwa na mtoto wake wa  Pili ,Lucy Owenya kushudia mwili wa mpendwa wao ukiwa umehifadhiwa.

Wakati kifo cha Mzee Ndesamburo kinatokea ,Lucy Owenya alikuwa akihudhuria vikao vya  Bunge la 11 ,vikao vya  Bajeti  ambapo alipata nafasi ya kuchangia mjadala wa bajeti ya wizara ya fedha kabla ya kupokea taarifa rasmi ya kifo cha Ndesamburo ambaye pia ni mfanyabiashara mashuhuri.

Majira ya saa 11:45 familia ilifika katika hospitali ya rufaa ya KCMC huku Mbunge wa jimbo la Rombo ,Joseph Selasini akisimamia zoezi la kuomba kuona mwili wa marehemu Mzee Ndesamburo ili kujiridhisha kama kweli baba yao amelala mauti.

Philemoni Ndesamburo atakumbukwa na mengi hasa katika siasa za mageuzi ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2015 akiwa ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro alisaidia kupatikana kwa madiwani wengi katika baraza la madiwani wa manispaa ya Moshi.

Ndesamburo maarufu kama Ndesa Pesa ametumia muda wake mwingi katka siasa na biashara ,amefariki dunia wakati akitaka kukabidhi mchango wake kwa meya wa jiji la ARUSHA ,Kalist Lazaro kwa ajili ya familia za watoto wa shule ya msingi ya Lacky Vicent waliofariki katika ajali ya gari Wilayani  Karatu mkoani Arusha.

Mwisho.

Ndugu na Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya Viongozi wa Chadema wakishiriki katika kikao hicho.
Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo.
Baadhi ya Wabunge wakishiriki katika kikao hicho.
Baadhi ya wanandugu wa familia ya marehemu Ndesamburo.


Kampuni za Simu Mtegoni.....Rais Magufuli Aiagiza TCRA Kuzifuta Zisizojisajili DSE

$
0
0
Rais John Magufuli ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufuta kampuni za simu za mkononi zote ambazo hazitaki kujiandikisha katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Aidha, amezitaka kampuni mbalimbali kujisajili katika mfumo wa ukusanyaji kodi za serikali kwa njia ya kielektroniki, aliouzindua jijini Dar es Salaam jana, mfumo unaosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 

“Tulipitisha sheria kwamba makampuni ya simu yote lazima yasajiliwe kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, wamesuasua weee, wamezunguka …TCRA msitoze faini, futeni hizo kampuni,” alisema Rais Magufuli na kuongeza kuwa faini ambayo imewekwa na TCRA ni ndogo, hivyo kampuni hizo haziogopi.

Alisema kituo hicho kilichoanza kazi Oktoba mwaka jana, mwitikio wa kujiunga sio mkubwa, ambapo ni kampuni tatu pekee ambazo zimejiunga na alihimiza zingine kujiunga. 

Rais Magufuli alisema kwa kutumia kituo hicho, makusanyo ya kodi hayatakuwa na malalamiko tofauti na huko awali kulikuwa na malalamiko kwa wakusanya kodi na pia walipa kodi wakidai kuongezewa viwango.

“Tulikuwa tukitumia makusanyo ya kodi ya mtu na mtu na huyo mtu inategemea uaminifu wake, wapo ambao sio waaminifu wanapokwenda kwa wateja wanawakadiria makadirio ya juu na pia walipakodi kudanganya wanachopata,” alisema Rais Magufuli. 

Rais Magufuli alisema mwarobaini wa malalamiko hayo ni mfumo huo, ambao ni mashine zinakokotoa na kwamba hakuna mwingilio wa mtu katika hesabu.

“Wengine wote ambao hamjajiunga mfanye hivyo kwa hiari, mlipa kodi na mkusanya kodi mnatakiwa kuishi kwa raha na upendo,” alisema Rais Magufuli na kuongeza kuwa kama wafanyabiashara hao wanataka mpaka sheria ibadilishwe ndipo watii agizo hilo, serikali inaweza kupeleka muswada kwa hati ya dharura. 

“Najua mnaweza kufafuta visababu kama mnataka mpaka tubadilishe sheria bado Bunge linaendelea kule, tunaweza kufanya mabadiliko,” alisema na kuziomba kampuni hizo kushirikiana na serikali, isionekane kwamba serikali haitaki kushirikiana na wawekezaji kwa kuanzisha mfumo huu.

Aidha, alisema serikali hii inawapenda wawekezaji ndio maana inawawekea mazingira bora ya biashara sambamba na ukusanyaji kodi ulio sahihi. 

“Niwaombe ndugu zangu, na hii nawaomba kutoka moyoni mwangu tunahitaji kodi, nchi zote zinalipa kodi, ni lazima kila mmoja alipe kodi awe anataka au hataki,” alisema. 

Rais Magufuli aliziomba kampuni za simu pamoja na kampuni nyingine, kuingia katika mfumo huo ili kuwe na usawa katika ukusanyaji wa kodi.

Alisema anachukia wawekezaji pamoja na ubinafsishaji wa mali za umma wa hovyo, ambao hauna faida kwa nchi ambapo alisema kuna zaidi ya kampuni 197 zimekufa. 

“Naeleza yote haya ili muelewe serikali ninayoiongoza inataka nini, inataka kufanya biashara na wawekezaji ambao ni waaminifu, biashara yoyote lazima iwanufaishe na wenye nchi,” alisema.

Aidha, Rais Magufuli alizitaka wizara zote zisimamie kampuni kuingia katika mfumo huo, ambao utawasaidia pia katika biashara zao kujua mapato yao. 

“Hakuna mtu duniani anayependa kulipa kodi, hata enzi za Yesu, na walipa kodi katika enzi zote hawakupendwa, usitegemee wewe kamishna TRA, ZRA utapendwa, wewe kusanya tu,” alisema Rais Magufuli.

Alisema nchi inapoteza fedha nyingi kupitia mianya ya upotevu wa mapato, lakini serikali iliamua kujenga kituo hicho kwa lengo la kuhakikisha na kulinda usalama wa taifa na taasisi za serikali na kampuni binafsi pamoja na kuimarisha na kukuza sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano. 

“Kampuni ambazo zitatunza taarifa zao kwenye kituo hiki zitakuwa na uhakika wa usalama wa taarifa zao hata kama uharibifu wowote utatokea,” alisema.

Hotuba Ya Rais Magufuli Aliyoitoa Jana Wakati wa Uzinduzi wa Kituo Cha Cha Kuhifadhi Kumbukumbu (Data Centre)

$
0
0
Hotuba Ya Rais Magufuli Ktk Uzinduzi Kituo Cha Cha Kuhifadhi Kumbukumbu (Data Centre) 1 Jun 2017

Rwanda yataka kuchukua sehemu ya anga la Tanzania

$
0
0
Serikali ya Rwanda imeiliandikia barua Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) ikitaka kulidhibiti (control) eneo la Kati na Magharibi mwa anga la Tanzania.

Suala hilo limekuja wakati Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ikijitahidi kulirejesha eneo la anga la mashariki. Eneo hilo linalojumuisha Madagascar, Mauritius, Moroni na Kisiwa cha Mayotte ambalo kwa miaka 39 limekuwa likidhibitiwa na Kenya kutokana na sababu za kiusalama. ICAO iliipa Kenya eneo hilo ilidhibiti kutokana na Tanzania haikuwa na rada za ulinzi za kutosha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la THE CITIZEN la Alhamisi Juni Mosi, 2017, ICAO bado haijaijubu Rwanda ambayo ina rada mbili za kisasa kwa ajili ya ulinzi wa anga.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari alisema Tanzania kwa sasa inaweza kudhibiti anga lake lote kwa sababu ipo katika mchakato wa kununua rada nne mpya zenye thamani ya Tsh 61.3 bilioni.

Rada hizo zitafungwa katika viwanja vikubwa vitano vya ndege ambavyo ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo Dar es Salaam, Abeid Amani Karume Zanzibar, Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro, Mwanza na Songwe.

Mdhibiti ameweka pia Radio yenye ‘Frequency’ za juu kabisa (VHF Radios) eneo la Mnyusi Tanga ambazo zimegharimu Tsh 389.9 milioni.

Tumejidhatiti katika kuhakikisha tunadhibiti eneo letu lote la anga tofauti na sasa ambapo tunadhibiti asilimia 25 pekee ya anga letu kitu ambacho si  hakikubaliki, alisema Johari.

Kushindwa kwa Tanzania kudhibiti eneo la kati na magharibi na kuiachia Rwanda, ina maana kuwa Tanzania itakosa mapato yote yanayotokana na eneo hilo.

Tanzania imekuwa ikipoteza Tsh 1 bilioni kila mwaka kwa kushindwa kudhibiti eneo la mashariki ambalo kwa sasa lipo chini ya Kenya.

Wema Sepetu abadilishiwa mashtaka katika kesi ya dawa za kulevya

$
0
0
Msanii wa filamu nchini na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu jana alisomewa upya mashtaka katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili yeye na wenzake pamoja na maelezo ya awali.

Wakili wa serikali, Constatine Kakula mbele wa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba alisema kuwa kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa kwa maelezo ya awali lakini aliomba kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka, ombi ambalo lilikubaliwa na hakimu hiyo.

Wakisomewa mashtaka upya, Wema Sepetu na wenzake wanakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kukutwa na kiasi kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa hizo.

Wakili wa serikali alidai kuwa Februari 4 mwaka huu katika makazi ya msanii huyo eneo la Kunduchi, Ununio walikuta msokoto mmoja wa bangi na vipisi vyenye uzito wa gramu 1.08. Aidha, Wema anatuhumiwa kuwa, Februari Mosi katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.

Watuhumiwa wakikana mashtaka yote na wakili wa serikali akawasomea maelezo ya awali. Katika maelezo hayo, wakili huyo anasema baada ya vitu hivyo kupatikana vilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kubainika kuwa ni bangi. Lakini pia Februari 8 Wema alipelekwa kwa mkemia na aligundulika kutumia bangi.

Wengine wanaoshtakiwa na Wema Sepetu ni wafanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa, Matrida Seleman Abbas ambao nao walikubali sehemu tu ya maelezo ya awali na kukana shtaka linalowakabili. Katika kesi hiyo, Wema Sepetu na wenzake wanatetewa na Wakili Peter Kibatala.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 14 mwaka huu.

Ushauri wa John Mnyika kwa Rais Magufuli

$
0
0
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika amefunguka na kumshauri Rais Magufuli jana bungeni na kusema Rais kabla ya kufikiria kuhusu makinikia alipaswa kufikiria kuhusu madini yanayochimbwa na kuchenjuliwa pasipo nchi kupata mapato.

Mnyika alisema hayo jana bungeni wakati akichangia katika bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ambayo imewasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/18 ambapo Waziri aliomba bunge liweze kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 998. 3 ili kutekeleza majukumu yake katika wizara hiyo.

"Rais kabla ya kufikiria makinikia, angefikiria kuhusu madini yanayochimbwa na kuchenjuliwa kwa ukamilifu hapa nchini lakini nchi haipati mapato yanayostahili" alisema John Mnyika

Lakini pia Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Madini ya Nishati na Madini, Dotto Mashaka Biteko aliitaka serikali kufuta leseni zote za madini ambazo hazifuati sheria na zinakiuka sheria ya madini na hazijatekelezwa kwa muda mrefu ili wapewe wachimbaji wadogo wadogo.

"Leseni zote ambazo zinakiuka sheria ya madini ikiwa pamoja na kutotekelezwa kwa muda mrefu zifutwe na kupewa wachimbaji wadogo wadogo na wachimbaji wa kati kwa kuwa wameonyesha nia ya dhati ya kuendeleza sekta hiyo" alisema Biteko

Raila Odinga Amwangukia Lowassa

$
0
0
Mgombea urais wa Kenya kwa tiketi ya umoja wa vyama vya upinzani wa NASA, Raila Odinga ameweka wazi ombi lake kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa kuhusu mchakato wa uchaguzi huo.

Amesema kuwa Lowassa pamoja na Rais John Magufuli waliochuana kwenye uchaguzi mkuu uliopita ni marafiki zake, na kuwaomba wote wamuunge mkono kwenye uchaguzi huo.

Ombi la mwanasiasa huyo mkongwe wa Kenya na Waziri wa zamani wa nchi hiyo limekuja siku chache baada ya Lowassa kuweka wazi kuwa atamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta ili aendelee kuitawala nchi hiyo.

“Mimi na familia yangu tunamtumikia Mungu lakini vilevile kwa dhati kabisa sisi wana Monduli tunamuunga mkono Uhuru Kenyatta kwenye mbio za Urais nchini Kenya. Naomba nitamke wazi na dunia yote ijue kuwa sisi tunampenda Uhuru Kenyatta naye anatupenda, kwa hiyo tunamuunga mkono kwa kuwa tunaamini ana uwezo wa kuwaunganisha Wakenya na Watanzania,” alisema Lowassa alipotembelewa na wabunge wanawake kutoka Kenya, nyumbani kwake Monduli takribani mwezi mmoja uliopita.

Lowassa ana ushawishi kwa kiasi fulani kwenye uchaguzi huo kwa kuwa ni kiongozi mkuu wa Wamasai (Leigwanan) katika ukanda wote wa Afrika Mashariki.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo pia kimeweka wazi kuwa kitamuunga mkono Kenyatta kwa kuwa kinaridhika na namna alivyofanya kazi hususan kuruhusu demokrasia nchini kwake.

Hata hivyo, msemaji wa vyama vya upinzani nchini Kenya, Philip Etale alisema kuwa Odinga ni rafiki wa Lowassa na Magufuli na kwamba asingependa urafiki huo upotee kwa sababu za kisiasa.

“Odinga aliweka bayana wakati wa kampenzi za uchaguzi wa Tanzania kuwa anawaunga mkono wote na kutaka mgombea bora ashinde. Kama ODM tunaamini katika demokrasia na tusingependa wakati wowote ule, tupoteze marafiki zetu kwa sababu ya siasa,” huo ulikuwa ni ujumbe wa Etale

Kenya inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Agosti 8 mwaka huu, uchaguzi ambao unatajwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi kwani katika uchaguzi uliopita, Kenyatta na Odinga walizidiana kwa kiasi kidogo cha kura.

Waziri Mkuu Awatuliza Wabunge Sakata la Madini ya Mchanga ( Makinikia)

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji wa madini nchini kuondoa hofu ya kukosa haki zao kwani kamati ya pili iliyoagizwa kufanya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini (makinikia) bado haijakamilisha kazi yake.

 Waziri Mkuu alisema hayo jana wakati akijibu swali la mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka, lililohoji kuhusu taswira ya Tanzania kimataifa hasa katika uwekezaji wa madini.

Majaliwa aliwataka wawekezaji wa madini kuondoa hofu kwa kuwa  kamati ya pili iliyoundwa kuangalia athari za kisheria, kisiasa na kimataifa kuhusu sakata la mchanga wa madini bado haijatoa ripoti yake.

“Watanzania wengi walikuwa na hofu, hata wabunge wengi katika serikali hii ya awamu ya tano mmekuwa mkizungumzia sakata la mchanga wa madini, lakini niwatoe hofu,  Rais John Magufuli alifanya hayo kwa nia njema ya kulinda rasilimali za Taifa,” amliema

Waziri Mkuu aliwataka wawekezaji wa madini kuondoa hofu kwa kuwa  serikali itazingatia ushauri kutoka sekta nyingine kabla ya kuchukua hatua katika  sakata hilo la mchanga wa madini.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images