Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali yatoa Ofa ya Bure Siku 3 Kwa Watanzania Kutembelea Mbunga za Wanyama

$
0
0
Serikali imetangaza kuanzia June 2 hadi 4, 2017 Watanzania wataingia bure katika Mbuga na Hifadhi za Wanyama nchini kote ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Tanzania ambayo yatafanyika kitaifa Butiama mkoani Mara.

Waziri wa Mazingira na Muungano January Makamba amesema tayari utaratibu umeshafuatwa ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na TANAPA kuwa katika siku hizo tatu Watanzania wataingia bure katika Mbuga na Hifadhi za Wanyama.

Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kitaifa yanatarajiwa kufanyika June  5 mwaka huu Butiama Mkoani Mara huku kukitarajiwa kuwa na mijadala mbalimbali itakayojadiliwa kuhusu utunzaji wa mazingira.

Akizungumza na wanahabari  jana, waziri wa wizara hiyo, January Makamba  alisema lengo la kupeleka maadhimisho hayo Butiama ni kumuenzi Nyerere ambaye alikuwa mwanamazingira namba moja nchini sanjari na kukumbuka mchango wake katika masuala ya uhifadhi wa mazingira nchini.

Kwa mujibu wa Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli Mkoani Tanga, kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu nchini ni utunzaji wa mazingira na maendeleo ya viwanda.


Korea Kaskazini Yarusha Kombora Kuelekea Japan

$
0
0
Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa mafupi, ambalo ni la tatu kurushwa na taifa hilo katika kipindi cha wiki tatu.

Kombora hilo aina ya Scud lilipaa umbali wa kilomita 450 (maili 280) kabla ya kuanguka katika maeneo ya bahari ya Japan, hatua iliyoifanya Japan kulalamika vikali.

Wachambuzi wanasema jaribio hilo ni ishara kwamba Korea Kaskazini inapiga hatua katika kuunda makombora yanayoweza kubeba mabomu.

Korea Kaskazini imeendelea kukiuka azimio la Umoja wa Mataifa linaloizuia kufanya majaribio yoyote ya makombora au silaha za nyuklia, na imeongeza kasi na idadi ya majaribio hayo katika miezi ya karibuni.

Kikosi cha Jeshi la Marekani katika Bahari ya Pasifiki kimesema kombora hilo lilirushwa kutoka Wonsan, Korea Kaskazini na lilipaa kwa karibu dakika sita kabla ya kuanguka.

Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga amewaambia wanahabari kwamba kombora hilo lilianguka katika eneo la bahari lililo kati ya visiwa vya Sado na Oki nchini Japan, katika eneo la pamoja la kiuchumi la visiwa hivyo viwili.

Msemaji wa Jeshi la Korea Kusini amesema kombora hilo lilipaa juu hadi kilomita 120 angani, na tathmini inaendelea kubaini “idadi hasa ya makombora yaliyorushwa,” ishara kwamba huenda nchi hiyo ilirusha zaidi ya kombora moja.

Jaribio hilo la kombora limetekelezwa siku moja baada ya vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini kusema nchi hiyo ilifanyia majaribio mfumo mpya wa kudungua ndege za kivita, na kutoa picha za kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un alishuhudia majaribio hayo.

Live Kutoka Ikulu: Rais Magufuli akimuapisha Simon Sirro kuwa IGP

$
0
0
Tazama moja kwa moja kutoka Iluku muda huu, leo Mei, 29, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha rasmi Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), kufuatia uteuzi wake uliofanyika jana Mei 28, 2017.

Kabla ya uteuzi huo, Sirro alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam. 

Bofya hapo chini kutazama

Godbless Lema Amuomba Rais Magufuli Alivunje Jiji la Arusha

$
0
0
Sakata  la madalali kuendelea kukusanya kodi za Halmashauri ya Jiji la Arusha kutoka kwa wapangaji wa vibanda vinavyomilikiwa na jiji hilo, limezidi kuchukua sura mpya huku, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), akimwomba Rais Dk. John Magufuli kuunda tume ya uchunguzi au avunje halmashauri.

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya hivi karibuni kikao cha Baraza la Madiwani katika Jiji la Arusha kupitisha azimio la kodi za vibanda vilivyojengwa stendi ndogo mjini Arusha kutakiwa kulipia halmashauri moja kwa moja na si kupitia madalali.

Jana  Lema alisema kwa muda mrefu kumekuwa na hali ya kutoheshimiwa kwa maazimio yanayotolewa na Baraza la Madiwani jambo ambalo halileti picha nzuri kwa jamii.

Alisema jiji liliingia mkataba wa miaka 10 na waliojenga vibanda hivyo tangu mwaka 1994 na baada ya hapo vitarudi chini ya umiliki wa halmashauri ya jiji lakini tangu wakati huo hadi sasa kumekuwa na kutoelewana na Serikali imekuwa ikikosa mapato yake.

“Tunajua huenda ni mkakati maalumu unaofanywa na Mkurugenzi wa Jiji (Athuman Kihamia) kupitia Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Mrisho Gambo).

“Ni wazi huu ni  mkakati wa kudhoofisha halmashauri ambazo zipo chini ya upinzani hasa Chadema ili zionekane zimeshindwa kusimamia rasilimali ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

“Kutokana na hali hii ninamwomba sana Rais Dk. John Magufuli, kama aliweza kuunda tume na ikachunguza suala la mchanga wa dhahabu na akawafukuza kina Acacia basi afanye hivyo na kwa jiji la Arusha na kama itaonekana vinginevyo avunje Baraza la Madiwani nasi tutarudi mtaani na kuwa madiwania wa wananchi kuliko kutoheshimiwa maamuzi ya vikao.

“Mtu amejenga kibanda miguu mitatu kwa mitano tangu mwaka 1994 anakusanya kodi je hadi leo hajarudisha fedha zake? Kuna nini kinachoendelea na kwanini madiwani wanadharauliwa? Nakuombas Rais Magufuli tupia jicho lako Arusha,” alisema Lema

Mbunge huyo alikwenda mbali na kudai kwamba wapo baadhi ya viongozi wa Serikali wamekuwa wakiandaa mikakati kwa kushirikiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  yenye lengo la kudhofisha maeneo yanaongozwa na wapinzani.

“Tunaona wazi huu huenda ni mkakati wa kudhofisha upinzani kwani hata kauli ya CCM kupitia kwa Katibu Mwenezi wake, Humphrey Polepole kwamba viongozi wa Serikali kupelekwa kwenye maeneo ya upinzani. Kauli hii aliitoa akiwa Arusha na kilio chetu hiki tumekifikisha hadi kwa Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene naye anajua kila kitu,” alisema

Alisema suala la malipo hayo awali wafanyabiashara walikubaliana na uamuzi wa jiji lakini baada ya kuteuliwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Arusha ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa, Mrisho Gambo aliingia suala hilo na kumpa maagizo kwa kuwakingia kifua watu waliojenga vibanda hivyo.

Polisi Kigambano Wadaiwa Kumuua Mwanafunzi

$
0
0
Askari  wa Jeshi la Polisi, Kituo cha Kigamboni wanadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi tumboni, mwanafunzi wa Chuo cha cha Uvuvi Mbegani, Bagamoyo Boniventure Kimali (25), wakimtuhumu kuwa ni jambazi.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa 3:30 usiku wa kuamkia juzi huko Kigamboni Vijibweni, nyumbani kwa kaka wa marehemu aitwaye, Naftan Barampami ambaye alikuwa akiishi naye.

Akisimulia jinsi ilivyokuwa, Barampami alisema usiku huo wakiwa bado wapo nje ya nyumba yao huku kila mmoja akiendelea na shughuli zake ndogo ndogo na wengine wakiwa wamejipumzisha, ghafla walishangaa kusikia milio ya risasi zilizopigwa mfululizo.

“Tulishtuka, milio hiyo ilitokea upande wa uwanjani ambapo ni jirani na nyumbani kwetu, tuliogopa kila mtu ilibidi atafute namna ya kujiokoa, tulikimbia, mimi nilikimbilia ndani, Boni alikimbia kuelekea nyuma ya nyumba yetu,” alisema.

Alisema akiwa ndani ya nyumba yake alisikia mtu akilia huku akiwasihi watu waliokuwa wamemzingira wasimuue.

“Ikabidi nisogee jirani zaidi na dirisha, nikakaa kwa utulivu na kuangalia nje kupitia dirishani kilichokuwa kikiendelea, ghafla nilimsikia Boni akilia kwa uchungu huku akiugulia maumivu, kumbe walikuwa tayari wamempiga risasi,” alisema.

Alisema askari wote walikuwa wamevaa kiraia, marehemu alikuwa akiendelea kuwasihi wasimuue huku akiwasihi wamuwahishe hospitalini kwani alikuwa akisikia maumivu makali.

“Aliwaomba wampekele hospitali na watujulishe ndugu zake lakini hawakumsikiliza, punde alifika mwenzao ambaye alishtuka na kuwaeleza wenzake wamefanya kosa kwani waliyempiga risasi si jambazi ambaye walikuwa wanamtafuta,” alisema.

Alisema japo alitamani kutoka nje ili akamsaidie ndugu yake lakini alihofia maisha yake kwani mmoja wa askari hao alionya asitokee mtu yeyote katika eneo hilo.

“Niliogopa mno, ikabidi nibaki pale pale dirishani nikifuatilia, nilihofu iwapo nisingetii amri hiyo na kutoka nje na mimi wangenipiga risasi,” alisema.

Barampami  alisema akiwa dirishani hapo, alimshuhudia yule askari aliyefika katika eneo hilo akichukua simu yake na kuwasiliana na wenzake ambao aliwataka wawahishe gari haraka katika eneo hilo.

“Lilipofika, walimchukua marehemu wakampakiza ndani ya gari hilo na kuondoka naye, wakati huo alikuwa bado anaugulia maumivu,” alisema.

Alisema baada ya muda kupita eneo hilo lilikuwa shwari akatoka nje na baadhi ya ndugu zake na kwenda kituo kidogo cha Polisi Vijibweni.

“Pale tuliuliza kama walikuwa wamemfikisha hapo, askari tuliyemkuta alituambia walielekea Kituo Kikuu cha Polisi Kigamboni, tukaenda huko,” alisema.

Alisema walipofika walipokewa na baadhi ya askari waliowakuta ambao waliwaeleza ndugu yao alikuwa amepelekwa Hospitali ya Vijibweni kwa matibabu.

“Tukaenda hadi huko lakini daktari mmoja alituambia hawakumpokea na kumuhudumia kwani hawakuwa na maelezo yaliyojitosheleza, tukarudi Kigamboni lakini awamu hii hatukupewa ushirikiano kama awali, tulipewa amri tusisogee katika eneo hilo,” alisema.

Alisema waliwasiliana na ndugu zao kuwaeleza hali waliyoikuta akiwamo ndugu yao Daudi Gwelenza ambaye anafanya kazi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

“Tuliwataka wajaribu kupita katika hospitali mbalimbali kumtafuta hasa Muhimbili, ndipo Gwelenza akaenda pale chumba cha kuhifadhia maiti,” alisema.

Gwelenza alisema alipofika hapo alielezwa kuna mwili ambao umefikishwa na askari wa Kigamboni, aliruhusiwa kuuona ndipo akakuta ni ndugu yake huyo.

“Nilimuangalia sura nikakuta ni yeye, nikamwangalia tumboni kweli alikuwa amepigwa risasi eneo la kushoto tumboni, alikuwa na mchanga mwingi wa bahari inaonesha huenda aliburuzwa, nilisikitika mno sikuweza tena kuendelea kuangalia tena,” alisema.

Aliongeza “Lakini nishangaa kwanini katika maelezo yaliyoandikwa juu ya taarifa ya marehemu hawakuandika kwamba amepigwa risasi, waliandika tu amepigwa na waliandika hajulikani jina lake, yaani kama vile walimuokota mahali akiwa ameuwawa.

Katika eneo hilo kulipatikana maganda mawili ya risasi yenye namba 311 (10) na 10 (77).

Msemaji wa familia, Goodluck Kimali ambaye ni kaka wa marehemu, alisema kitendo kilichofanywa na askari hao hakivumiliki.

“Kwa mujibu wa majirani na mashuhuda wa tukio hili, wanasema angewahishwa hospitalini asingepoteza maisha, kwanini hawakumuwahisha huko, kwanini walimpiga risasi tumboni na si mguuni ili asiwakimbie, kwa sababu hakuwa na silaha yoyote, kwanini walimuua,” alihoji.

Alisema tangu kutokea kwa tukio hilo hakuna askari yeyote aliyefika nyumbani hapo kukagua, kujiridhisha juu ya kile walichokuwa wakimtuhumu marehemu.

“Hatujamuona askari hata mmoja kukagua, kwanini hawajafika kufanya ukaguzi, hii inamaanisha wanajua walichokifanya, kitendo hiki hakivumiliki, Tanzania ni nchi ya amani, askari anapaswa kulinda raia na mali zake, lakini imekuwa kinyume chake,” alisema.

Alisema ingawa wanafuatilia kwa ukaribu suala hilo hata hivyo hawaoni kama kweli watasaidiwa kupata haki ya ndugu yao.

“Kuna urasimu mwingi nauona, tunaomba watupe mwili wa ndugu yetu tukampumzishe, maana hata tukisusa na kuwaachia hawawezi kurejesha uhai wake, lakini vitendo hivi vikomeshwe, sisi tunavumilia lakini ipo siku raia watachoka,” alisisitiza.

Alisema watakapokabidhiwa mwili huo, wanatarajia kuusafirisha wakati wowote hadi kijijini kwao Mwayeye, Wilaya ya Buligwe mkoani Kigoma kwa ajili ya maziko.

Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti wa Chuo cha Mbegani, Ambaksye Simtoe alisema tukio hilo limewashtua kwani marehemu alikuwa kijana mtulivu, msikivu na mpole.

“Alikuwa anasoma kozi ya Uchakataji Samaki, Ubora na Masoko, ngazi ya Diploma, mwaka wa tatu, Juni, mwaka huu angehitimu masomo yake.

“Alikuwa yupo field (mafunzo kwa vitendo) katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri, tumesikitika mno, kifo chake kimekuwa cha ghafla hatukutarajia kama ipo siku haya yatatokea,” alisema.

PICHA: Kamanda Sirro Aapishwa Rasmi Kuwa IGP Mpya

$
0
0
Rais John Magufuli amemuapisha mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro aliyeteuliwa jana kuchukua nafasi ya Ernest Mangu.

Hafla hiyo imehudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri wa Mambo ya Ndani , Mwigulu Nchemba na makamishna mbalimbali wa jeshi hilo.
 
Sirro baada ya kuapishwa amekula kiapo cha maadili mbele ya Rais Magufuli kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake mapya.


Diamond Platinumz atahudhuria MAZISHI ya aliyekuwa mume wa mkewe? .....JIBU Liko Hapa

$
0
0
==> Mwanamuziki,Diamond Plantinumz  alikuwa  nchini Kenya kwa ajili ya tamasha la Koroga ambalo lilifanyika jana  Jumapili Mei 28

==> Diamond aliwahutubia wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi na kuzungumzia kifo cha aliyekuwa mme wa mkewe wa sasa, Ivan Ssemwanga

==> Ssemwanga alifariki akiwa amelazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo
****
Mwanamuziki, Diamond Plantinumz amezungumzia kifo cha aliyekuwa mme wa mkewe ,Zari Hassan ambaye alifariki juma lililopita akipokea matibabu katika hospitali moja Afrika kusini.

Akizungumza akiwa katika chuo kikuu cha Nairobi Ijumaa Mei 26, Diamond alisema kuwa Zari anapitia wakati mgumu ikizingatiwa kuwa alizaa watoto watatu na Ssemwanga .

Aidha ,Diamond alisema kuwa hangekosa kwenda Kenya kuhudhuria tamasha la Koroga kwa sababu alikuwa tayari amewaahidi Wakenya kwamba angeenda kabla ya msiba huo kutokea.

Diamond alisema atahudhuria mazishi ya mwenzake,Ssemwanga.

"Kwa kweli umekuwa ni wakati mgumu kufutilia mbali mualiko huu. Nimeongea na mke wangu akanielewa. Nikimaliza hapa nitaenda Uganda kwa sababu ya mazishi," Diamond alisema.

Marehemu Ivan Ssemwanga alikuwa amemuoa Zari Hassan ambaye kwa pamoja walikuwa na watoto watatu wa kiume kabla ya kutalakiana kisha Zari akaolewa na Diamond.

Video: IGP Simon Sirro ataja kipaumbele chake cha kwanza kwa Jeshi la Polisi

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Nyakoro Sirro amesema kuwa lengo lake kubwa baada ya kukabidhiwa wadhifa huo mpya ni kuhakikisha kuwa uhalifu unapungua na anaimani kubwa kuwa atafanikiwa kwa sababu wananchi ambao ni wema ni wengi kuliko ambao ni majambazi.

Simon Sirro ameyasema hayo leo mara tu baada ya kupandishwa cheo na kuwa Inspeka Jenerali wa Jeshi la Polisi na kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi akichukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, IGP Sirro amewaomba wananchi kutoa ushirikiano ili wafanikiwe kutokomeza uhalifu kwa sababu wahalifu wanaishi ndani ya jamii, hivyo Polisi peke yao hawatafanikiwa.

“Ombi langu kwa Watanzania, ili tuweze kuishi kwa amani na utulivu, ni vizuri sana wakatoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi. Naamini kabisa tutaweza kwa sababu hawa wahalifu ni wachache na sisi ni wengi, kwa hiyo umoja wetu ule ni lazima tutashinda” amesema IGP Sirro wakati akihojiwa na maafisa wa habari wa Ikulu.

Mbali na kuomba ushirikiano huo kwa raia, IGP Sirro ametoa onyo kwa wahalifu kuwa, siku zote uhalifu haulipi, na ukiung’ang’ania sana, utasababisha ukaiacha familia yako.

Msikilize hapa chini IGP Sirro akizungumza;

Diamond: Sitaki Tiffah awe msanii, naogopa ataliwa sana na Wanaume

$
0
0
Diamond Platnumz amefunguka kwa kudai kuwa hataki mtoto wake wa kike Tiffah awe msanii kwa madai akiwa msanii atatembea kimapenzi na wanaume wengi.

Muimbaji huyo amedai mtoto wake huyo akiwa msanii, wanaume wengi watamiminika kumtaka kimapenzi.

“Mtoto wangu wa kiume ningependa awe msanii lakini mtoto wangu wa kike sitaki awe msanii, watamla sana,” alisema Diamond weekend iliyopita  akiwa katika kipindi KTN nchini Kenya. 

“Mtoto akiwa msanii watu wanaomjua wanakuwa wengi, watu wanaokujua wakiwa wengi na kutongozwa kunakuwa kwingi, sasa watanipa presha,”

Aliongeza,“Ukiwa mwanaume lijali na ukiwa kwenye nafasi kama yangu lazima wataliwa. Nilikuwa kwenye kutafuta tafuta, mpaka nilivyompata Zari na kweli nimetulia,”

Muimbaji huyo Jumanne hii anatarajia kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa Zazi, Ivan aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika Kusini kwa ugonjwa wa moyo.

Nape Awaponda Wabunge Wanaoisifia Serikali kwa Kila Kitu

$
0
0
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amefunguka na kusema wabunge wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanaishauri na kuikosoa serikali ni watu ambao wana mapenzi mema na Rais na serikali yake kuliko wanao sifia kila kitu.

Nape Nnauye amedai wabunge ambao kazi yao ni kusifia kila kitu hata kama kuna mapungufu hao hawana mapenzi ya kweli kwa Rais Magufuli na serikali kiujumla na kudai yeye anaitumia nafasi yake vizuri kutoa ushauri kwa serikali kupitia bunge sababu ndiyo njia sahihi aliyonayo kwa sasa.

"Kimsingi kazi kubwa ya Mbunge hasa wabunge wa CCM ni kuishauri serikali yake sisi tunaoshauri tunampenda zaidi Rais na tunaipenda zaidi serikali ifanye vizuri kuliko wale ambao watakuja na kusifu na kupongeza kwa kila kitu, hata pale wanaona kabisa hapa tungeweza kushauri na mambo yakarekebishika" alisema Nape Nnauye

Mbali na hilo Nape Nnauye amedai kuwa watu ambao wanashangaa yeye kuishauri serikali sasa kupitia bunge anasema hawafahamu pia alipokuwa kwenye Baraza la Mawaziri, alikuwa akifanya hivyo.

Wanaosafiri kati ya Tanzania na DRC kupimwa Ebola, Waziri Ummy aeleza hali ya ugonjwa huo nchini.

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Ally Mwalimu amesema mpaka sasa hakuna mgonjwa wa Ebola wala anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo nchini Tanzania huku Tsh. bilion 1.5 zikiwa zimetumika kuukabili ugonjwa huo
 
Ummy amebainisha hayo leo wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kusema wananchi wasiwe na hofu ila wanapaswa kuchukua tahadhari huku akisisitiza kuwa wameweka kifaa maalum 'register' ambacho kitawalazimu wasafiri wote kujaza wakiwa wanakwenda  katika nchi ya DRC na pindi wakiwa wanatoka huko kuingia nchini.

"Hadi sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ebola wala mwenye virusi Tanzania, tumechukua tahadhari katika mikoa yote inayopakana na nchi ya Congo DRC. Wasafiri wote wanaotoka DRC wakifika Tanzania lazima waandikishwe kimaalum ili kufuatiliwe kama huko alikotoka hali ikoje na kama hana virusi nyemelezi. Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kuwapima wasafiri wote kwenye mipaka yetu na Congo DRC" alisema Ummy.

Aidha, Ummy amesema serikali imeagiza mashine nne za nyongeza kutoka nje ya nchi ili kuongeza nguvu ya upimaji wa virusi vya ugonjwa huo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 30

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kupunguza tumbo, Kuongeza nguvu za Kiume na Mvi

$
0
0
(OFFER OFFER OFFER) NATURAL BEAUTY COSMETIC INAKUPATIA OFA YA PUNGUZO LA BEI KWA KILA BIDHAA PUNGUZO LA  %10 KWA MWEZI HUU WA RAMADHANI. 
 
PATA BIDHAA HIZI ZILIZOTENGENEZWA KWA MIMEA NA MATUNDA UFURAHIE MATOKEO MAZURI BILA KEMIKALI WALA MADHARA YOYOTE PIA NI GUARANTEE. Bidhaa tulizonazo÷
 
🍉🍓🍇🍅🍊🍒🍍🌴🍐🧀🧀🧀🧀🍅🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍐🍍🌳🍏🍐🌶🍉🍆🍆🍒.
Pata punguzo la bei kwa bidhaa hizi.
1. YODI PILLS _ Ni vidonge vya kuongeza hips na makalio @170,000/=
2. BOTCHO CREAM_ Ni dawa ya kupaka ya kuongeza shepu (hips na makalio) @150,000/=
3. BOTCHO MULT PLUS_ Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza shepu (hips makalio na mapaja) @200,000/=
4. PANNAMAS BREAST_ Ni dawa ya kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walio nyonyesha. Inapatikana kwa Tsh @120,000/=
5. DISCREET_Hii ni kwa ajili ya kuondoa mvi milele na zisiludi tena. @120,000/=
6. BODY BOOSTER_Ni dawa ya kuongeza mwili mzima na kukupa hamu ya kula vizuri. Inapatikana kwa Tsh @130,000/=
7. LEG BOOSTER_Ni dawa ya kuongeza miguu kuwa (Chupa ya bia) @120,000/=
8. HAIR GROWTH STIMULATOR_ Ni mafuta ya kulefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo. Yanapatikana kwa Tsh @100,000/=
9. MICRO COMPUTER_ Ni mkanda wa kupunguza tumbo na manyama uzembe. @170,000/=
10.HANDSOME UP ni kifaa kinachoongeza maumbile ya kiume  kwa 99% kwa size uipendayo wewe na kuimarisha misuli ya uume kwa @170,000/= tuu.
11.MEN GELY YA KUPAKA. Hii inaongeza kwa wastani wa inch 6.5 na inapatikana kwa @120,000/=. 
12. SHARK POWER. Hii pia ni kwa ajili ya kuongeza maumbile  wastani wa inch 7.5 inapatikana kwa @135,000/=.
15. MAX MAN 2. Ni vidonge kwa ajili ya nguvu ambavyo vinasaidia sana hata kwa watu wenye kisukari na waliokua wakifanya sana master blashion. Pia huongeza hamu ya tendo la ndoa inapatikana kwa @130,000/=
🌳🍉🍌🍅🍍🍐🍓🍆🍐🍒🍒🍓🍓🍑🍍🍍🍓🍓🍓🍍🍐🍐🍈🍉
Tupo DAR ES SALAAM  kariakoo na kinondoni kanisani.
Kwa mawasiliano zaidi piga  0759029968 au 0659618585. 
 
Popote ulipo utapata huduma zetu.
                 Follow us
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
     Bidhaa zetu zote ni garantii na unapewa risiti
              Karibu

Baba Amkata Amkata Makalio Mwanaye

$
0
0
Mwanamume mmoja mkazi wa Ndofe wilayani Nyamagana mkoani Mwanza amemfanyia kitendo cha ukatili mtoto wake kwa kumkata na kisu sehemu za makalio kwa madai ya utoro shuleni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Nuhu James (50) anayedaiwa kumfanyia ukatili mtoto Ndalo Nuhu (14) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Igoma kwa kumfunga kamba miguuni na mikononi kisha kumchapa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baadaye kumkata na kisu sehemu za makalio, tukio analodaiwa kulifanya majira ya saa 11:00 alfajiri ya tarehe 25 Mei, 2017.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa aliaamua kumfanyia ukatili wa aina hiyo mtoto wake baada ya kugundua kwamba mwanaye ni mtoro shuleni.

Kamanda Msangi amesema baada ya mama wa mtoto alipoona ukatili anaofanyiwa mwanaye na hali yake kiafya kuzidi kubadilika alishindwa kuvumilia na arehe 28 Mei.2017 aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi

Kamanda Msangi ameendelea kusema kuwa polisi wapo katika upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi utakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani huku majeruhi akipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Ole MedeyeOle Medeye Ajitumbua mwenyewe Nafasi ya Kaimu Katibu Mkuu UDP

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha 'The United Democratic Party' (UDP) ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai ya kujipa fursa ya kuitumikia familia yake.

Ole Medeye ambaye alijiunga na UDP akitokea CHADEMA mapema mwaka jana, ametoa kauli hiyo jana katika barua aliyomuandikia Mwenyekiti wa chama hicho Mh. John Cheyo, huku akimshukuru kwa kumuani katika nafasi hiyo kwa kipindi chote.

"Napenda kukujulisha rasmi kwamba ili nipate muda wa kutosha kufanya shughuli za ustawi na maendeleo ya familia na jamii inayonitegemea nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi hiyo ya Katibu Mkuu kuanzia tarehe ya barua hii".Imesema sehemu ya barua hiyo

Mwanasiasa huyo amewahi kushika nyazifa mbalimbali ikiwemo Ubunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi kupitia CCM katika Bunge la 10 na kupitia nafasi hiyo aliweza pia kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika serikali ya awamu ya nne.

Mara baada ya kushindwa katika kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, aliamua kuhama chama na kujiunga na CHADEMA ambapo hakudumu sana licha ya CHADEMA kumpa nafasi ya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kisha alihamia UDP kabla ya kupewa nafasi ya Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho.


Mangu Awataka Wananchi Wampe Ushirikiano IGP Simoni Sirro

$
0
0
Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewataka wananchi kumpa ushirikiano IGP mpya, Simon Sirro katika kukabiliana na matukio ya uhalifu nchini hasa katika Mkoa wa Pwani.

Mangu aliyasema hayo jana  Ikulu jijini Dar es salaam baada ya Rais John Magufuli kumwapisha Sirro kuwa IGP mpya wa kuliongoza jeshi la polisi nchini.

Kuhusiana na hali inayoendelea mkoani Pwani, Mangu alisema "Sirro anafahamu anachotakiwa kufanya katika hilo, nimefanya naye kazi kwa karibu, ninachoomba ni askari na wananchi wote wampe ushirikiano"

Mangu ambaye anasubiri kupangiwa kazi nyingine alisema anamfahamu Sirro kama mchapakazi mzuri na ataweza kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na amani.

Sirro aliapishwa jana kuwa IGP, kabla ya uteuzi huo alikuwa kamanda wa polisi (RPC) katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Shinyanga. 

Baadaye alikwenda kitengo cha operesheni na mafunzo polisi makao makuu, kisha akahamishiwa kitengo hicho kanda maalumu ya Dar es Salaam kabla ya kuwa kamishna wa kanda hiyo.

OFA: Jipatie Kitabu cha Riwaya Kali ya President Wife Toka Kwa Mwandishi Makini Eddazaria

$
0
0
OFA OFA OFA OFA OFA YA PRESIDENT WIFE, IMERUDI TENA
 
JIPATIE KITABU CHA PRESIDENT WIFE kama BADO hujafahamu kitabu hichi ni muendelezo wa story ya SORRY MADAM(Destination of my Enemies) kwa SH 10000/= huku kitabu hicho kikiambatana na OFA ya kitabu cha HARD DAY bureee kabisa.

PRESIDENT WIFE
"Baada ya utawala wa mzee GODWIN na MANKA kutolewa madarakani na EDDY DODWIN, adui mkubwa wa Eddy, JOHN anachukua madaraka ya Mzee Godwin na kuapa ni lazima ataamuangamiza Eddy aliye kuwa rafiki yake wa kipindi kirefu toka wakiwa sekondari. Rahab anaongoza nchi huku kijana machachari Adrus akiwa mlinzi makini kuhakikisha maisha ya mke wa raisi yanakuwa salama, ila K2 na kaka yake wanajawa na uchu wa madaraka na kuhakikisha kwamba wanauangusha uongozi wa Raahab, ila Eddy anasimama kama ngao na kupigania uongozi wa Rahab je atafanikiwa"
 
Ungana nami muandishi wako Eddazaria G.Msulwa katika hadithi hii ya kusisimua

Ukihitaji kitabu wasiliana nami kupitia WhatsApp 06570725888. Email eddazariaM@gmail.com. Kwa watumiaji wa Facebook nanyi munaweza kukipata kupitia inbox zenu kwa jina la @StoryZaEddy-tz  Kwa maelezo zaidi wasiliana nami moja kwa moja kwa simu namba 0657072588 au 0768516188

KARIBUNI SANA NA NINAWATAKIA MFUNGO MWEMA WA RADHAN

Hisa za ACACIA zapungua bei kwa asilimia 32% kwenye soko la DSE

$
0
0
Kupungua kwa bei za hisa za kampuni ya ACACIA kwa asilimia 32.7, na UCHUMI 28.6% na JHL 17.8% kumetajwa kuwa sababu ya kupungua kwa ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa Sh. Trilioni 1.5 kutoka Shilingi Trilioni 19.9 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 18.4 wiki iliyoishia tarehe 26 Mei 2017.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Miradi na Masoko wa DSE Patrick Mususa, pia alisema mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia Mei 26, 2017 yamepungua kutoka thamani ya Sh. Bilioni 29.5 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 2.9, kutokana na mauzo ya hati fungani 7 za serikali zenye thamani ya bilioni 3.8 kwa jumla ya gharama ya bilioni 2.9.

kwa upande wa viashiria,Mususa alisema“Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepungua kwa pointi 171 kutoka pointi 2,288 hadi pointi 2,117 kutokana na kupungua kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni. Wakati Kiashiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimeongezeka kwa pointi 6 kutoka pointi 3,357 wiki iliyopita hadi pointi 3,363 wiki hii.”

“Sekta ya viwanda imeendelea kubaki kwenye pointi 4,228 wiki hii. Sekta ya huduma za kibenki na kifedha  wiki hii imeongezeka kwa pointi 17 kutoka pointi 2,551 hadi pointi 2,568 kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za CRDB kwa asilimia 2.7%.Sekta ya huduma za kibiashara wiki hii imeendelea kubaki kwenye pointi 2,969,” alisema.

Pia, Mususa alisema thamani ya mauzo ya hisa imepungua kutoka Sh. Bilioni 8 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 2.6 wiki hii.

Hata hivyo, Mususa alieleza kuwa, idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeongezeka kutoka hisa Milioni 1.1 hadi hisa Milioni 2.2, hali kadhalika mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa Bilioni 13 kutoka Shilingi Trilioni 7.056 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.069 wiki hii. kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za CRDB (2.7%).

Serikali yatolea ufafanuzi tangazo la ajira za walimu mitandaoni

Mchanga wa Madini Walivuruga Bunge....... Tundu Lissu na Godbless Lema Wanapinga Kitendo cha Serikali Kuuzuia

$
0
0
Mchanga  wa dhahabu uliozuiwa katika makontena Bandari ya Dar es Salaam, umezua mjadala bungeni baada ya wabunge wa CCM na Chadema kupingana juu ya uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli kuyazuia kusafirishwa nje ya nchi.

Hayo yalitokea jana wabunge walipokuwa wakichangia hotuba ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje, Kikanda na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2017/18, iliyowasilishwa na Waziri Balozi Augustine Mahiga.

Wakichangia bajeti hiyo, wabunge wawili wa Chadema, Tundu Lissu (Singida Mashariki) na Godbless Lema (Arusha Mjini), walisema uamuzi wa Rais Magufuli utalisababishia taifa hasara na kuwafukuza wawekezaji wa nje.

Naye Lema alisema amepata taarifa kwamba wamiliki wa mgodi wa Acacia ambao makontena yao yamezuiwa, wamefungua kesi katika Mahakama ya London, Uingereza, kulalamikia uamuzi huo wa Serikali.

“Katika hatua ya kulinda rasilimali ya nchi, ni mwendawazimu anayeweza asipongeze, lakini lazima tujue ni namna gani unalinda rasilimali hizo bila kuligharimu taifa.

“Wote tunafahamu taifa letu lina mgogoro na Acacia Minning ambao kwa sura ya kwanza, mgogoro huo unajenga hisia za siasa ndani ya nchi na sura ya pili ya mgogoro huo unapunguza kasi ya wawekezaji wa nje kuja kuwekeza nchini.

“Leo (jana) tunapongeza alichokifanya Rais, tuelewe wakati Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe anaanza sera ya kunyang’anya watu mashamba na kuwakandamiza wawekezaji, alipigiwa makofi na watu wake kama ambavyo sisi tunapiga makofi leo.

“Matokeo yake leo Zimbabwe hawana noti yao, hawana fedha yao na ni taifa ambalo halina ‘identity’.

“Katika suala hili ni muhimu mumshauri Rais kwa sababu  gharama za uamuzi wake ni kubwa, ikizingatiwa Acacia leo wamekwenda mahakamani London na kwa hali ya kawaida, taifa hili litaingia kwenye gharama kubwa kama tulivyoingia kwenye minofu ya samaki,” alisema Lema.

Tundu Lissu alisema amekuwa akipinga sera mbaya za uwekezaji tangu mwaka 1999 na kwamba uamuzi alioufanya Rais Magufuli si mzuri na ataupinga kama ambavyo amekuwa akipinga sera zote ambazo zimelifikisha taifa pabaya.

Alisema uamuzi wa kuzuia makontena hayo unalichafua taifa kimataifa na kuwaogopesha wawekezaji wa nje.

“Suala siyo Acacia watafanya nini, suala ni watu wote tunaohusiana nao kwenye uchumi kama Wachina ambao ndiyo taifa kubwa duniani kwa uwekezaji watafanya nini.

“Fikiria, Jumuiya ya Ulaya, Japan na Marekani watafanya nini kwa sababu ya kuwanyang’anya mchanga wa dhahabu Acacia.

“Sisi tunazungumza masuala ya diplomasia ya uchumi wakati hatujui lolote kuhusu diplomasia ya uchumi, ndiyo maana tunafanya haya tunayoyafanya. Kwa hiyo, waziri nakuomba usikubali hizi kelele kwa sababu hivi sasa nchi yetu ina hali mbaya kwenye diplomasia.

“Tulichokifanya ni makosa katika sheria, mikataba ni makosa kwa mujibu wa sheria za mataifa. Kwa taarifa yenu, gharama tutakazolipa katika jambo hili ni kubwa kuliko huo mchanga wa Acacia.

“Tutakuwa na kesi kama Zimbabwe, tusishabikie uamuzi uliofanyika kwa sababu tu umefanywa na Rais,” alisema Lissu.

Hatua hiyo ilimfanya Mnadhimu Mkuu wa Serikali, Jenister Mhagama, aombe mwongozo kwa mwenyekiti wa Bunge kutokana na lugha kali aliyokuwa akitumia mbunge huyo (maneno hayo makali hatukuyaandika).

Akijibu mwongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, alimtaka Lissu afute maneno hayo makali, jambo ambalo alilikubali ingawa alisisitiza kupingana na uamuzi wa Rais Magufuli.

Wabunge wa CCM nao waliamua kujibu mapigo kwa kusema uamuzi uliofanyika ni sahihi kwa kuwa nchi ilikuwa ikiibiwa.

Mbunge wa Viti Maalumu, Juliana Shonza, aliwashamnbulia Lema na Lissu akisema hawaaminiki kwa kuwa walikuwa wakimsema vibaya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa ni fisadi, lakini alipohamia Chadema wakampigia kampeni wakati wa Uchaguzi Mkuu.

“Wewe Lissu na Lema, mlikuwa mkimsema vibaya Lowassa ni fisadi, alipokuja kwenu mkaanza kumsafisha. Je, huo siyo uamuzi mbaya?

“Yaani nyie kila kinachofanywa na Serikali mnaponda kwa sababu mmejipa vyeo vya mtoto wa kambo. Eleweni nchi hii inahitaji Rais kama Magufuli, nyie wenzetu endeleeni kutetea wezi, sisi tumeshawazoea.

“Tunamuomba Mheshimiwa Rais aendelee kuchapa kazi, nyie wenzetu muendelee kulalamika, sisi hapa kazi tu,” alisema Shonza.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba, alisema uamuzi uliofanywa na Rais Magufuli ni sahihi na utaigwa na mataifa mengine duniani.

Alisema kuna haja ya Watanzania kushirikiana katika uamuzi huo kwa masilahi ya taifa.

Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi, aliwatoa hofu Watanzania kwa kusema kama Acacia watakwenda mahakamani, Serikali itakwenda pia kwa kuwa jambo hilo linawezekana.

“Tutabishana hapa kutafuta umaarufu kwa sababu kama ni mahakamani tutakwenda pia. Hata mtu wa kawaida ukimwambia jambo hilo alilofanya Rais atakuunga mkono na nawaomba tusipinge kila kitu kwa sababu ya itikadi zetu,” alisema Chumi.

Wengine waliounga mkono uamuzi wa Serikali huku wakitaka Watanzania washirikiane katika jambo hilo, ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mary Mwanjelwa, Ester Mahawe na Rose Tweve.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, aliwataka wabunge wasishabikie suala la wawekezaji hao kwenda mahakamani kwa sababu wakienda huko hawataishtaki CCM bali wataishtaki Tanzania.

“Nawaomba waheshimiwa wabunge muiunge mkono Serikali katika jambo hili kwa masilahi ya Taifa, nchi ikishtakiwa, haitashtakiwa CCM.

“Kilichofanyika hakina makosa kwa mujibu wa sheria kwa sababu mkataba una kipengele kinasema unaweza kupitiwa upya baada ya miaka mitatu, kwa hiyo nawaomba tushirikiane,” alisema Masaju.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images