Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mzee aliyebuni na kuchora Nembo ya Taifa apatiwa matibabu na Serikali

$
0
0

Serikali ya imelazimika kumuhamishia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mzee Francis Maige Ngosha aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Amana kwa kipindi cha siku moja kwaajili yakupatiwa matibabu zaidi.

Akitoa tamko la serikali Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Khamisi Kigwangalla amesema mzee huyo ambaye ni mmoja wa wachora Nembo ya Taifa amesema wameamua kumuhamishia katika hospital hiyo ya Taifa Muhimbili ili kufanyiwa uchunguzi wa kina na wataalamu wa magonjwa mbalimbali ili kubaini na kutibiwa.

Dkt. Kigwangalla amesema serikali itahakikisha inampa tiba kamili na malezi kwa kuzingatia haki ya kuishi ya binadamu na kuthamini mchango wa wazee na waasisi wa taifa.

Kwa upande wake daktari bingwa wa magonjwa ya dharura kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga amesema wanasubiri majibu ya vipimo wanavyomchunguza na pindi watakapobaini tatizo atapatiwa matibabu yake.

Kwa upande wake Francis Maige Ngosha ambaye ni mmoja wa wachora Nembo ya Taifa ameishukuru serikali na jami iliyokuwa ikimlea kwa miaka yote bila malipo.

Bomu Laua Polisi Watano Kenya

$
0
0
Jeshi la Polisi nchini Kenya limepoteza Askari wake watano baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa barabarani katika mji wa Liboi karibu na mpaka na Somalia.

Polisi hao wameuawa na shambulio lililotokea katika eneo ambalo Polisi wengine wanne waliuawa katika shambulio kama hilo lililotekelezwa na kundi la Alshabab hivi karibuni.

Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab ambao makao yao makuu ni Somali, wameendelea kufanya mashambulio kadhaa nchini Kenya katika siku za hivi karibuni, wakiitaka Serikari ya Kenya kuondoa majeshi yake yanayofanya kazi katika vikosi vya AMISOM.

AUDIO: Tetemeko Laua Polisi Mmoja Mwanza na Kujeruhi Wanafunzi Watatu

$
0
0
Tetemeko la ardhi lililotokea katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita na Kagera, limesababisha kifo cha askari WP Koplo Joyce Jackson wa Kituo cha Polisi Misungwi.

Mbali ya kifo hicho, pia limejeruhi watu watatu wakiwamo wanafunzi wa Shule ya Sekondari Igokelo na mahabusu mmoja.

 Tetemeko hilo lililotokea jana saa 6:55 mchana na kudumu kwa muda wa dakika moja, limesababisha taharuki kubwa katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na kwa baadhi ya wananchi wa mikoa ya Mwanza na Kagera ambao walilazimika kukimbilia ofisi zao kwa hofu ya kuangukiwa na majengo.

Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka kutaja jina  amesema walikuwa  wamepumzika nje ya Kituo cha Polisi Misungwi,  baada ya kutokea tetemeko la ardhi na Koplo Joyce alidondoka chini na kupoteza fahamu.

Alisema walimsaidia kumkimbiza hospitali, lakini wakati wanamfikisha alikuwa tayari amefariki dunia.

“Joyce alianza kazi jana, baada ya kumaliza likizo ya uzazi. Alijifungua kwa njia ya upasuaji na ameacha kichanga, alikuwa pia  anasumbuliwa na shinikizo la damu (presha),” alisema shuhuda huyo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi, Dk. Marcelina Kiemi, alithibitisha kupokea mwili wa Koplo Joyce na majeruhi ambao ni wanafunzi wa Shule ya Sekondari Igokelo na mahabusu mmoja.

“Baada ya kutokea tetemeko la ardhi, nimepokea mwili wa askari polisi wa kike Joyce Jackson ambaye alikuwa tayari amefariki dunia,” alisema Kiemi.

Dk. Kiemi, alisema majeruhi watatu; Anna Habi (18) mwanafunzi wa kidato cha nne, Mathayo Ndalahwa (15) kidato cha kwanza kutoka Shule ya Sekondari ya Igokelo na mahabusu Mathias Simoni (22) mkazi wa Kijima, wamelazwa na wote hali zao zinaendelea vizuri.

 Mwalimu wa Shule ya Sekondari Igokelo, Adela Sakoma, alisema wakati tetemeko hilo linatokea walikuwa darasani, ndipo wanafunzi walianza kukimbizana kutoka nje kupitia mlangoni ili kunusuru maisha yao.

Alisema baadhi yao walijeruhiwa na kuwakimbizwa hospitalini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alithibitisha kutokea kifo cha Koplo Joyce.

Alisema kwa muda sasa, Koplo Joyce alikuwa akisumbuliwa na tatizo la presha.

“Huyu WP Koplo Joyce alikuwa na tatizo la presha, wakati tetemeko linatokea wakiwa wanatoka nje, alianguka ghafla. Wenzake walimsaidia na kumkimbiza hospitalini na walipomfikisha tayari alikuwa amepoteza uhai,” alisema Kamanda Msangi.

==>Msikilize Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi akiongea hapo chini

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya May 27

Wafanyakazi wa Mochwari Watiwa Mbaroni kwa Kuiba Kete 32 za Dawa za Kulevya

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amefunguka kuwa wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala wameiba jumla ya kete 32 za dawa za kulevya zilizokuwa kwenye mwili wa Raia wa Ghana aliyefariki dunia akiwa katika nyumba ya wageni.

Kamanda Sirro amesema wahudumu hao wanne wote wamekamatwa na kukiri kwamba  baada ya kifo cha raia huyo wa Ghana aliyefariki ndani ya 'Red Carpet' iliyopo Sinza Dar es Salaam walipasua mwili wa raia huyo na kutoa kete hizo kisha kuziuza, na kuongeza wametaja watu ambao wamewauzia ambao nao wamekamatwa na wapo chini ya ulinzi wa polisi

"Yule Mghana ambaye alikutwa amefariki dunia tarehe 14/ 03/ 2017 kwenye nyumba ya wageni ya 'Red Carpet' na alichukuliwa na kupelekwa mochwari Mwananyamala lakini inaonekana wale wahudumu wali[pata taarifa kuwa ule mwili una dawa za kulevya, kimsingi walikula njama wakampasua na kutoa kete 32 za madawa ya kulevya na baada ya kuyapata waliyauza hayo madawa" alisema Sirro

Kamanda Sirro aliendelea kusema kuwa mpaka sasa wanawashikilia watu wanne ambayo wamehusika katika jambo hilo.

"Mpaka sasa tunawashikilia watu wanne ambao wanakiri kupasua mwili huo ambao ni wahusika wakuu na ni wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala lakini tumekwenda mbali zaidi baada ya kufanya upasuaji wamemuuzia nani naye amekatwa pia na anaeleza kuwa alinunua hayo madawa, lakini pia naye alichukua na kumuuzia mtu mwingine anayefahamika kwa jina la Ally Nyundo, huyu Nyundo tulishamkataga na kumpeleka kwa Mkemia Mkuu yeye alionekana ni mtumiaji, kimsingi tuna hao watuhumiwa wanne na huyo wa tano aliyekamatwa sasa tunaandaa jalada" alisisitiza Sirro

Wahujumu uchumi walitaka kumhonga Rais Magufuli Bilioni 300, uchunguzi Makinikia

$
0
0
Ikiwa imepita siku mbili tangu Rais John Magufuli kueleza kuwa kwa sasa nchi iko katika vita ya uchumi na kwamba ana majina ya watu waliotaka kuingilia na kuharibu uchunguzi wa Kamati Maalumu aliyoiunda ili kuchunguza thamani na viwango vya madini vilivyomo kwenye mchanga wenye madini (Makinikia) katika makontena 277 yaliyozuiliwa kusafirishwa nje ya nchi, ili kupoteza ushahidi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole Mei 25, 2017 aliibuka na kudai kuwa kuna wahujumu uchumi walitaka kumhonga kiasi cha Bilioni 300 Rais Magufuli, ili kusitisha zoezi la uchunguzi huo, huku akihoji masilahi wanayopata watu wanaofanya biashara ya kusafirisha makinikia hayo nje ya nchi.

“Vita ziko za aina nyingi, ziko zile tunazopigana kwa silaha mtu na mtu, na nchi na nchi, lakini sasa ziko vita za kiuchumi, ni mbaya zaidi zinalenga kuturudisha nyuma.Wahujumu uchumi hawapigani na rais, bali wanapigana na maisha ya wananchi wa Tanzania, tukiwa wamoja tutashinda vita hii, wako watu wanaipinga vita hii yenye dhamira njema, huu si wakati wa kutofautiana ni wakati wa kusimama kumshinda adui,” alisema.

Polepole aliyasema hayo, wakati akitoa wito kwa wananchi, kumuunga mkono Rais Magufuli katika kipindi hiki kigumu kwani nchi iko katika vita mbaya ya uchumi ambayo wahujumu uchumi wamelenga kupigana na maisha ya watanzania na kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

“Kuna watu walitaka kumhonga rais bilioni 300 ili kusitisha uchunguzi. Walitaka kuhonga bilioni 300 kwa ajili ya kusitisha uchunguzi huo, hivi wao wanapata fedha kiasi gani? Lakini rais akawatolea nje, akasema subirini uchunguzi ukamilike. Tusiamame naye na hakika tutashinda na historia itaandikwa kwamba tulisimama katika kulinda urithi wetu,” amesema.

Katika hatua nyingine, Polepole aliwajibu baadhi ya wanansiasa wanaoikosoa CCM kutokana na viongozi wake waliopita kutunga na kupitisha sheria za madini ambazo zinatetea masilahi ya wawekezaji kuliko nchi, kwa kusema kuwa viongozi walioko sasa ni tofauti na waliopita, na kwamba serikali iliyoko madaraka itarekebisha sheria hizo.

“Tumehujumiwa sana, tumedhurumiwa sana mali za watanzania ambazo tumezirithi kutoka kwa mababu zetu na tuna dhamana ya kuhakikisha zinawafikia watoto wa watoto wetu,” alisema.

Ofa: Jipatie Riwaya Kali ta U KILL ME toka kwa Mtungi Eddazaria

$
0
0
OFA KABAMBE YA MWEZI HUU WA RAMADHANI.

Jipatie PUNGUZO KUBWA la asilimia 85% la kitabu cha AIIISSII U KILL ME(Season One) kwa sh 15000 badala ya sh 50000.
Sifa ya kitabu
1.Kina episode 200 sawa na kurasa 889
2.Ni story iliyo andikwa kwa ustadi wa hali ya juu.
3. Imezingatia, furaha, huzuni, msisimko, upandeo kwa ujumla ni story itakayo kupa buruni itakayo kuancha mdomo wazi.

AIIISSII U KILL ME
Dany kijana ambaye anaigia kwenye matatizo makubwa kutokana na penzi lake juu ya bosi wake mkuu wa idara ya upelelezi K2. Matatizo yanayo pelekea kila kitu kuharibika kwenye maisha yake na kujikuta akipoteza mfumo mzima wa maisha yake. Jitihada zake za kuyarudisha maisha yake kwenye mfumo wa kueleweka kunamfanya aonekane gaidi wa dunia. Je nini kitakacho endelea. Ungana nami kwenye kisa hichi cha kusisimua na kuburudisha kilicho andaliwa nami muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa

KITABU HICHI NINAKIUZA KUPITIA MTANDAO WA WHATSAPP 0657072588 au EMAIL eddazariaM@gmail.com Au zungumza nami 0657072588 au 0768516188

Acacia Wataka Uchunguzi Huru Mchanga Wa Dhahabu......Watishia Kuchukua Hatua Kuhakikisha Hawapati Hasara

$
0
0
Kampuni ya Acacia imesema ripoti kuhusu mchanga wa dhahabu aliyopewa Rais John Magufuli Jumatano ya wiki hii imejaa upotoshaji wa hali ya juu na imependekeza kufanyika kwa uchunguzi mpya ambao ni huru ili kuweza kupata ukweli.

Katika taarifa yake ya jana, Kampuni ya  Acacia, yenye makao makuu jijini London, Uingereza, imesema kwamba, imejaribu mara kadhaa kuomba nakala ya ripoti hiyo nzima pamoja na utaratibu wa kuchukua sampuli kwenye uchunguzi huo, lakini mpaka sasa haijapewa.

“Kwa kuzingatia data tulizo nazo kwa zaidi ya miaka 20 ambazo tunaweza kuzitoa kwa ajili ya uchunguzi zaidi, hatuwezi kukubaliana na matokeo ya Tume. Data hizi ni data ambazo zimechambuliwa na kuandaliwa na Watanzania, wataalamu pamoja na taasisi za kimataifa na zimekuja na matokeo yanayofanana.

“Data hizi huru ambazo zinaweza kuthibitika zimeonyesha kuwa dhahabu kwenye mchanga ni chini ya asilimia moja ya kumi ya kiwango ambacho kimetajwa na ripoti ya tume. Kama data za ripoti ya tume zingekuwa kweli, Bulyanhulu na Buzwagi zingekuwa ndiyo wazalishaji wakubwa wa dhahabu duniani. Kutokana na upotoshaji huu, tunaamini tathmini mpya ambayo ni huru inahitajika,” inasomeka sehema ya Acacia kwa umma. 

Zaidi ripoti hiyo inaeleza kuwa, Acacia imekuwa ikilipa mrahaba ambao ni asilimia 4 kwa mujibu wa makubaliano kati yake na Serikali pamoja na sheria za Tanzania na kuongeza kuwa, pamoja na kuwa kweli kuna baadhi ya aina nyingine za madini kama chuma, sulphur, rhodium na mengineyo kwenye mchanga, aina hizo hazina thamani kibiashara na kampuni hiyo haipati mapato yoyote kutokana nayo.

Kampuni hiyo imesisitiza kuwa, imekuwa ikilipa mrahaba kwa mujibu wa sheria kwa madini wanayoyazalisha na kusema kuwa, katazo hilo la kusafirisha mchanga kutoka migodi hiyo miwili inaifanya kampuni hiyo kupoteza zaidi ya shilingi bilioni 2.2 kila siku, huku ikisisitiza itachukua hatua zote kuhakikisha haiendelei kupata hasara.

Taarifa hiyo ya jana imekuja zikiwa zimepita siku mbili baada ya kampuni hiyo kutoa taarifa nyingine ya kukosoa ripoti ya uchunguzi wa makinikia ambayo imewasilishwa kwa Rais.

Kupitia taarifa hiyo, Acacia ilidai kuwa, haijaona nakala ya ripoti hiyo ambayo inaonyesha kuwa kiwango cha madini kilichopo kwenye makinikia yanayoshikiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam ni mara kumi zaidi ya kiwango kilichoainishwa kwenye data zilizowasilishwa awali.

Kwa msingi huo, uongozi wa Acacia ulisema kuwa unaendelea kusubiri nakala zaidi za ripoti hiyo kwa ajili ya kutolea ufafanuzi.

Kutana Maajabu ya NGWIZUKULU KARORE Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

$
0
0
Kutana Maajabu ya NGWIZUKULU KARORE Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..

Ngwizukulu karore ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa mwenye Uzoefu wa Miaka 19 na Ametembea Zaidi ya Nchi 43 Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
Je unasumbulia na Mapenzi..?
 
(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na Ngwizulu Karore Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.
 
Je Unasumbuliwa na Madeni?
Umepotelewa na Mali au Kudhulumiwa?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
Wasiliana na Ngwizukulu karore Kwa Majibu ya Maswali yako..
Anasafisha Nyota na Kutoa Pete za Bahati kuendana na Nyota yako.
 
Kupandishwa Cheo na Heshima Mahala pa Kazi.
Wanaotaka Kuwa Maarufu na Kujulikana.
pia Utapewa Nguvu ya Kujilinda na Mali zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara..
Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.
 
Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.)Humaliza Kesi za Muda mrefu ndani ya siku 14 tu.
 
Anatoa NDAGU Zisizokuwa na Masharti(Mali Bila Mashrti) Kwa maelezo Zaidi wasilina nae kwa
 
Whatsapp+255 654 876 841
Call .. +255 759 084996

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya May 28

SORRY MADAM -Sehemu ya 64 & 65 (Destination of my enemies)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
Akafungua vioo vya dirishani, akachungulia chini, akashusha pumzi na kuanza kuutoa mguu wake wa kushoto kwenye sehemu ulipo kanyaga mguu wake wa kulia, lengo lake alihitaji kwenda katika dirisha linalo fwata kwa kupita katika kijinjia hicho. Phidaya alipo hakikisha kwamba ameshikilia vizuri, akaanza kutambaa kuelekea kwenye dirisha la chumba cha pili, ila kabla hajafika akajikuta akigeuka na kuangalia chini, kizunguzuku kikali kikamshika na kujikuta akipepesuka, mikono na miguu yake vikapoteza muhimili na kujikuta akianza kuelea hewani na kwenda chini kwa kasi kali, kitendo kilicho shuhudiwa na watu wengi waliopo chini, kila mmoja alishangaa kuona mwanamke huyo akianguka kutokea gorofa ya kumi kuja chini.

ENDELEA
Macho ya watu wengi yakashuhudia jinsi Phidaya anavyokuja kwa kasi chini, wakamshindikiza kwa macho yao hadi kwenye swimming poolm, lililo jaa maji liliopo chini usawa wa sehemu ambayo Phidaya aliangukia.

Vijana wawili wenye asili ya kiarabu pamoja na Rahab ambaye alikuwa ameketi pembezoni mwa swimming pool hilo akipunga upepo wakajitosa kwenye maji, kila mmoja akiwa na lengo la kwenda kumuokuoa msichana huyo. Kwa pamoja wakajikuta wakimtoa kwenye maji, kidogo Rahab akaonekana kustushwa na msichana huyo. Kutokona ni mwanamke mwenzake Rahab akaanza kumpulizia hewa, Phidaya mdomoni mwake kumpa pumzi ya ziada kutokana kuanguka kwake kumemfanya kuzimia.

Haikuchukua muda Phidaya akastuka, huku akihema, macho yake yakatua kwa Rahab aliye muinamia, akashangaa kumuona Rahab kwa maana ni mtu anye mfahamu, ila bado hakujua ni sehemu gani ambayo aliweza kumuona mwanamke huyo.
Wahuduu wa Hoteli pamoja na meneja wa hotelo hiyo wakafika baada ya kujulishwa na wateja wao kwamba kuna tukio la ajabu limetokea, katika hoteli yao, wakakuta Phidaya akiwa amefunikwa na taulo, kubwa ili kutoa ubaridi mwilini mwake na mwili nzima unamtetemeka kwa woga.

“Yupo vizuri mpeni hewa musimzunguke”
Rahab alizungumza huku akiwasogeza watu waliopo katika eneo hilo, hapakuwa na mtu aliye weza kuamini kwamba mwanamke huyo anaweza kupona, hii ni kutokana na umbali mrefu alio weza kutoka hadi chini alipo angukia.
”Mama uaitwa nani?”
Meneje alimuuliza Phidaya, aliye mtazama kwa macho makali, yalio jaa wekundu ulio sababishwa na kulia sana.
“Kwa sasa hayupo sawa, labda badae anaweza kuzungumza”
“Kuna huduma ya dharura labda tuweze kumuwahisha hospitalini.”
“Hilo pia linaweza kusaidia”

Ikaletwa gari ya wagonjwa, Phidaya akaingizwa kwenye gari, huku Rahab akiomba na yeye kwenda, akakubaliwa, kutokana na msaada wake walio weza kuufanya kwa binti huyo. Haikuwachukua muda mwingi sana wakawa wamefika hospitalini, ila kabla Phidaya hajaingizwa katika chumba cha matibabu, akamuomba Rahab kuweza kuwasiliana na mtu aliye weza kumtajia namba yake.
“Huyo ni nani?”
“Ni mlinzi wangu”
“Yupo wapi?”
“Yupo Japani”
“Anaitwa nani?”
“Lee Si”
Phidaya alipo maliza kuzungumza hayo, kitanda alicho lalia kikasukumwa ndani ya chumba hicho kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa mwili wake.

***
“Lee Si nina mazungumzo na wewe”
Shamsa alizungumza huku akiufunga mlango wa Lee Si, baada ya kuugonga kwa muda kasha ukafunguliwa. Lee Si, akavaa tisheti yake kisha na kuelekea chumbani kwa Shamsa, akamkuta akiwa amekaa na Sa Yoo wakimsubiria, sura za wasichana hao zilimuonyesha Lee Si, kwamba wana maswali mengi juu yake.

“Nimefika”
Sa Yoo, akamkata jicho Lee Si kisha akamtazama Shamsa ambaye muda wote alikuwa akifikiria jambo la kuzungumza.
“Kwa nini unatuzunguka?”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Lee Si usoni
”Kivipi madam?”
“Tuambie madam yupo wapi, ikiwa wewe kama mlinzi wake ni lazima utatambua kuna kitu kinacho endelea, la sivyo tutakuripoti polisi na utatuambia ukweli kuhusiana na sehemu alipo mama yangu”

Lee Si, akatabasamu kwa dharau kicha akamtazama Shamsa kuanzia chini hadi juu. Dharau ya Lee Si, ikamfanya Sa Yoo, kuachia msunyo mkali, huku akilitoa na yeye jicho lake kubwa fulani kumpandisha na kumshu Lee Si juu hadi chini.
“Hata mukinipeleka polisi, munahisi nitawekwa ndani? Siku ambayo mulikwenda kununuliwa nguo mimi nilikuwepo? Kama jibu ni hapana basi tambueni kwamba sifahamu alipo madam, na mimi nikama nyinyi sote hatujui ni wapi alipo”

“Shamsa unaona dharau zake nilizo kuambia, huyu ni lazima atakuwa anafahamu”
Sa Yoo, alizungumza huku akichukua mto mdogo wa kochi na kumrushia, Lee Si, na kumbamiza nao wa uso. Lee Si, akanyanyuka kwa hasira akamfwata Sa Yoo, sehemu alipo simama, kwa lengo la kumuadhibu kwa kitendo alicho kifanya ila kabla hajamfikia, akazuiliwa na Shamsa aliye simama kwa haraka.
“Unataka kufanya nini?”

Shamsa alimuuliza kwa sauti ya msisitizo huku akimtazama Lee Si usoni mwake, Lee Si akamsukumia Shamsa pembeni, akamzaba kibao kizito Sa Yoo, aliye baki akishangaa. Kitendo hicho kikamkera sana Shamsa, akanyanyuka na kumtandika kofi zito Lee Si, aliye mtolea macho makali Shamsa, akataka kurusha ngumi, ila simu yake, ikaita, akaitoa kwa haraka mfukoni mwa suruali yake, kabla hajatazama ni nani aliye piga simu hiyo, akastukia Sa Yoo, akimpiga teke kwenye mkono alio shika simu, ikaangukia pembeni.
Lee Si akamrukia Sa Yoo kwenye kochi kabla hajampiga kofi, tayari Shamsa Alisha jiachia, na kumrukia, akamuangusha chini na kuanza kumtandika ngumi mfululizo.

Lee Si hakukubali kuona anapigwa na msichana huyo alicho kifanya ni kujigeuza, akampiga Shamsa ngumi moja aliyo izuia kwa mikono yake miwili, Sa Yoo, katika kuzungusha zungusha jicho lake, akaiona simu ya Lee Si, ikiita, hakutaka kuujali ugomvi huo alicho fanya ni kuishika simu hiyo na kuipokea.
“Haloo”
Sa Yoo, alizungumza huku akikimbilia bafuni na kuwaacha Shamsa na Lee Si wakiendelea kupigana
“Unazungumza na Rahab Praygod ninatumaini kwamba wewe ndio Lee Si”

Sa Yoo, ikabidi kuitoa simu hiyo sikioni na kuitazama namba hiyo akagundua kwamba si namba ya Japan. Akili yake ikafanya kazi haraka haraka na kujibu kwamba yeye ndio Lee Si.
“Kuna taarifa ambayo bosi wako Phidaya ameniambia nikujulishe, kwa sasa yeye yupo nchini Misri barani Afrika na yupo hospitalini kwa uchunguzi zaidi wa madaktari hii, ni baada ya kujaribu kufanya jaribio la kutaka kujiua”
Sa Yoo, akauziba mdomo wake kwa wasiwasi mwingi, akionekana kustushwa na habari hiyo.
“Alooo unanisikia?”
Rahaba alizungumza baada ya kuona mtu anaye zungumza naye amekaa kimya.

“Nakusikia, amelazwa hospitali gani?”
Rahab akalitaja jina la hospiali aliyo lazwa Phidaya, kisha akamuaga Lee Si, kutokana na kumaliza mazungumzo yake aliyo kuwa ameagizwa na Phidaya. Sa Yoo, akatoka bafuni na kurudi sebleni, akamkuta Lee Si, akiwa anavuja damu puani huku amelala sakafuni na Shamsa amesimama pembeni yake huku amekunja ngumi na kufura kwa hasira.
“Vipi?”
Sa Yoo, alimuliza Shamsa huku akiwa amemkodolea macho Lee Si, anaye jizoa zoa kunyanyuka.

“Siwezi pigana na wazembe mimi”
Shamsa alizunguza huku akiondoka karibu na Lee Si, aliye kaa kitako sakafuni akiwa haamini kwamba umahiri wake wa kupigana ameweza kuchezea kichapo ambacho hakukitarajia kabisa kutoka kwa binti huyo ambaye kwa mara ya kwanza alimchukulia binti wa kawaida.
“Nenda chumbani kwako na usije ukarudia”
Kwa haraka Sa Yoo akaituma kwa namba ya simu kwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu yake, namba ambayo ilipiga kwenye simu ya Lee Si, kisha akaifuta na kumrushia Lee Si simu yake.

“Besti hiyo puaa ilivyo kaa”
Sa Yoo alimtania Lee Si baada ya kumuona pua yake ikiwa kidogo kama imepinda, huku damu zikiendelea kumwagika. Baada ya Lee Si kutoka chumbani hapo, na Sa Yoo kuhakikisha kwa kuchungulia mlangoni kwamba Lee Si ameingia chumbani kwake akamuelezea Shamsa kila kitu alicho kizungumza kupitia simu ya Lee Si.
“Huyo mtu amesema kwamba anaitwa nani?”
“Rahab Praygod”
Jina la Rahab Praygod halikuwa ngeni masikioni mwake, ila hakuhitaji, kuliwekea maanani kwa maana majina duniani yananafanana isitoshe kwamba mtu mwenyewe aliye ipiga simu hiyo yupo nchini Misri.
“Inabidi tuondoke”
“Sawa tuanze kufwatilia maswala ya viza”
“Poa”

***
Macho ya Sabogo yaliweza kuwakumbuka Shamsa na Sa Yoo, ambao amewaona wakiwa wamesimama kwenye ofisi za shirika moja la ndege. Kutokana alisha elezwa na Black Shadow kuhusiana na binti huyo kwamba ni mwanae hakuona haja ya kuendelea kuwatazama. Akatembea kwa mwendo wa haraka hadi walipo, akamgusa Shamsa begani na kufanya Shamsa kugeuka na Sa Yoo pia kugeuka. Wote wakaonekana kumshangaa, Sabogo kwani ni jitu refu kwenda juu, na wote vimo vyao wanamfikia kiunoni.
“Ninaweza kuzungumza na nyinyi?”
Sa Yo alikubali kwa kutingisha kichwa kutokana na woga ulio mvaa gafla. Wakatoka hapo dirishani na kwenda kukaa nje ya uwanja huo wa ndege ambapo kuna mgahawa

“Naamini kwamba munanifahamu?”
“Hapana”
Sa Yoo alijibu kwa haraka sana hata kabla Shamsa kujibu.
“Mimi ni meneja wa Black Shadow ninaimani kwamba wote munamjua, ninaitwa Sabogo”
“Ahaaa wewe ndio yule ambaye ulituletea tiketi za kukaa VIP?”
“Ndio mimi haujakosea”
Furaha ikamuingia Shamsa, akaona ni bahati kubwa sana kuonana na mtu huyo kwa maana ndoto za kukutana na mpenzi wake ambaye ni Black Shadow, zinaanza kufufuka upya.

“Black Shadow yupo wapi?”
“Yupo na ninaimani pia atakuwa na furaha kuonana na nyinyi”
“Ninakuomba utupeleke sasa hivi”
Shamsa alizungumza huku akimshika, mkono Sabogo.
“Kwa mchana huu ninaimani itakuwa ni ngumu labda kwa usiku”
“Hata iwe saa nane ya usiku mimi nipo tayari kuonana naye”
“Sawa kuna sehemu nitawahitaji muje, ila hakikisheni kwamba munakuja nyinyi wawili peke yenu tu”
“Sawa”

Sabogo akaawachia namba za simu, hata wazo la kwenda Misri, barani Afrika, wakaliweka kando kwanza, moyo wa upendo juu ya Black Shadow, ukarudi kwa upya kabisa moyoni mwa Shamsa. Siku hiyo furaha ikamjaa tele moyoni mwake, hata kumbukumbu alizo ambiwa na Phidaya kwamba Black Shadow ni baba yake ziliteketea. Hakutaka kuzipa uzito wa aina yoyote kutokana anaamini kwamba Black Shadow ni mwanaume mwengine kabisa na Eddy ni mwanaume mwengine kabisa.

***
Furaha na amani ikamtoweka Madam Mery, hakujua maisha yake ya hapo mbeleni yatakuwa vipi, kwani adui yake namba moja ndio huyo amekalia kiti cha uraisi nchini Tanzania.
“Nitafanyeje?”
Ndio swali ambalo Madam Mery aliendelea kujiuliza kichwani mwake, akaendelea kuzunguka chumbani kwake, akitafakari, hakuhitaji siku hiyo kuonana na mtu wa aina yoyote hata wafanyakazi wake wa ndani. Kila alilo lifikiria alilipangua, kwani mpango wake aliona unafeli.

“Eddy, lazima nionane na Eddy ndio mtu pekee ambaye anaweza kuniunga mkono katika mpango wangu huu”
Madam Mery alizungumza huku akiifungua Laptop yake, akaanza kutafuta ni wapi alipo Eddy. Ripoti ya mwisho ambayo aliipata katika mtandao kwamba Eddy yupo Japani na nimuhalifu katika nchi hiyo anatafutwa.

Madam Mery hakuona haja ya kupoteza muda akakata tiketi kabisa kupitia mtandao, siku iliyo fwata akapanda ndege hadi Dar es Salaam, ambapo akakuta tiketi yake ikiwa tayari, akapanda ndege ya shirika la KLM na kuianza safari yake, ambayo ilimchukua masaa mengi kukaa angani.

Kitendo cha kutoka katika uwanja wa ndege akamshuhudia Shamsa akiwa na binti mmoja wakiingia kwenye gari ya kifahari na kuondoka.
Madam Mery hakuhitaji kuweka hisia za kwamba mtu aliye weza kumuona ni tofauti za Shamsa, kutokana binti huyo anamtambua vizuri sana na Alisha wahi kukaa naye na kumueleza siri nyingi kuhusiana na kikosi cha siri kinacho milikiwa na mzee Godwin baba yeka Eddy.

Madam Mery akamuomba dereva huyo kulifwata gari hilo kwa nyuma popote litakapo kwenda, dereva naye akafanya hivyo kama alivyo agizwa, gari hilo likafika kwenye moja ya hoteli mabinti hao wakashuka, Madam Mery naye akashuka na kumlipa dereva pesa yake akiamini kwamba atawakuta mapokezi Shamsa na huyo rafiki yake wa kijapani.

Hadi anaingia ndani hakuweza kuwaona, muhudumu mmoja akamkaribisha, bila kutaja haja yake, ya yeye kumfikisha hapo, ikamlazimu kuchukua chumba katika hoteli hiyo hiyo, akijipa moyo kwamba akiliona gari hilo basi Shamsa atakuwa amemuona na kama amemuona Shamsa basi Eddy hato kuwa mbali na atamueleza kila kitu kuhusiana na Tanzanani.
***
Sabogo, mara baada ya kurudi katika makao yake, kitu cha kwanza alicho kifanya akampigia simu Black Shadow na kumuomba aweze kukutana naye kwenye moja ya gorofa juu kabisa ya gorofa hilo zinazo pata gorofa, ishirini na tano.
“Kuna nini?”

“Kuna zawadi nimekuandalia”
“Sawa kaka”
Majira ya saa nne usiku, Sabogo akawa ndio mtu wa kwanza kuweza kufika katika eneo la gorofa hilo, akawaelekeza Shamsa na Sa Yoo, mara baada ya kupigiwa simu na wasichana hao. Haikuchukua muda sana Sa Yoon a Shamsa wakawa wamesha fika katika kilele cha gorofa hilo.
“Yupo wapi Black Shadow?”
Shamsa alimuliza Sabogo.
“Ninaimani kwamba yupo njiani”
Ikawalazimu wawe wavumilivu waendelee kumsubiria Black Shadow.
***
Katika kitu ambacho kilitoke kumkera na kumuudhi Lee Si ni kupigwa na Shamsa, bado hakuwa anaamini kwamba amechezea kichapo kikali kutoka kwa binti huyo. Moyoni mwake akajiapiza kuweza kumuua, iwe isiwe ni lazima awaangamize hususania cha umbea Sa Yoo. 

Rais Magufuli na Mkewe wamjulia hali mtoto aliyekuwa akila maziwa, mafuta na sukari

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2017 amewajulia hali wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Mwaisela iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuwashukuru Madaktari na Wauguzi kwa juhudi kubwa wanazofanya kunusuru maisha ya watu.

Mhe. Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wamewatembelea wagonjwa hao majira ya saa moja ya asubuhi wakitokea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ambako wamehudhuria ibada ya Jumapili.

Miongoni mwa wagonjwa waliojuliwa hali na Mhe. Rais Magufuli na mkewe ni Mzee Francis Maige Kanyasu (Ngosha) aliyelazwa katika chumba namba 310 na Mtoto Shukuru Musa Kisonga aliyelazwa katika chumba namba 312 ambaye hivi karibuni aliripotiwa kuugua ugonjwa usiofahamika uliosababisha aishi kwa kunywa mafuta ya kula, sukari na Maziwa.

Pamoja na kuwapa pole wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Mwaisela na kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali itaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo na changamoto zinazowakabili madaktari na wauguzi.

“Jamani, Madaktari tunawashukuru sana, mnafanya kazi nzuri, Madaktari wote nchini pokeeni pongezi zangu, sisi Serikali tutaendelea kuzikabili changamoto hizo na siku moja zitakwisha, kikubwa ni kumtanguliza Mungu mnapofanya kazi ya kuokoa maisha ya watu kwa juhudi kubwa, mnafanya kazi ya Mungu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwatembelea wagonjwa katika hospitali hiyo na amemhakikishia kuwa Madaktari tayari wamegundua magonjwa yanayowakabili Mzee Francis Maige Kanyasu (Ngosha) na Mtoto Shukuru Musa Kisonga na kwamba wanaendelea vizuri na matibabu.

Aidha, Prof. Museru amesema hospitali hiyo imepiga hatua kubwa ya kujenga uwezo wa kutibu magonjwa ambayo wagonjwa walilazimika kwenda kutibiwa nje ya nchi na hivyo kuokoa fedha nyingi za Serikali.

“Mhe. Rais hospitali yetu sasa imeanza kufanya upasuaji na kutoa tiba ya magonjwa ambayo yalilazimu wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, mfano hivi sasa tunatoa huduma ya kusafisha figo kwa wagonjwa takribani 250, na kuanzia mwezi Julai mwaka huu tutaanza kupandikiza figo.

“Huduma hii hugharimu kati ya Shilingi Milioni 60 na Shilingi Milioni 70 kwa mgonjwa mmoja anayekwenda kutibiwa nje ya nchi, lakini hapa nchini gharama zinashuka hadi Shilingi Milioni 21” amesema Prof. Museru.

Prof. Museru ameongeza kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili pia inajipanga kuanza kutoa huduma ya matibabu kwa watoto wenye matatizo ya usikivu ambao wapo hatarini kuwa viziwi na hivyo kuokoa fedha nyingi zinazotumika kuwatibu nje ya nchi, kutoka Shilingi Milioni 90 hadi Shilingi Milioni 30.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru pamoja na Dkt. Juma Mfinanga Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali katika hospitali hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto Shukuru alikuwa akidaiwa kuishi kwa kula Sukari, Maziwa na mafuta ya kula lakini hali yake imeimarika zaidi na kuanza kula vyakula vya kawaida. Katikakati ni Mama yake Shukuru Mwanahabibi Mohamed Mtei.

CHADEMA Wamkana Raila Odinga....Watangaza Kumuunga Mkono Uhuru Kenyatta

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza rasmi kumuunga mkono Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Kenya utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Msimamo huo umetolewa jana katika mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho unaofanyaki mjini Dodoma, ikiwa ni maamuzi ya Baraza hilo, na kutangazwa rasmi na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.

Akizungumzia uamuzi huo, Mbowe alisema sababu kuu ya uamuzi huo ni kugeukwa na mgombea wa muungano wa ODM Raila Odinga, ambaye chama hicho kilikuwa kikimuunga mkono mara zote.

Mbowe amesema "Kwa muda mrefu chama chetu kimekuwa kikimuunga mkono Raila Odinga achukue nafasi ya kuliongoza Taifa la Kenya. Mwaka 2015 ilipofika zamu yetu rafiki yetu Raila Odinga alitugeuka na kumuunga mkono adui yetu. Sisi kama Chama, safari hii tunamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na Umoja wa vyama vinavyounda JUBILEE".

Ikulu yaijibu Acacia kuhusu mchanga wa madini

$
0
0
Uamuzi wa Serikali kuhusu suala la usafirishaji wa mchanga wa madini, utategemea ripoti ya kamati ya pili iliyoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza suala hilo.

Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa ikiwa ni siku moja baada ya kampuni ya Acacia kuitaka Serikali kuunda kamati huru kuchunguza kiasi cha madini kwenye makontena yake 277 yaliyozuiwa bandarini.

Wiki iliyopita, Rais Magufuli alikabidhiwa ripoti na kamati ya kwanza iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma ambayo ilibaini kuwa makontena hayo yana tani 7.8 za dhahabu.

Pia, Acacia wanadai hawakupewa ripoti ya kamati hiyo licha ya kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi.

“Sijui chochote kuhusu hao Acacia kuomba iundwe kamati huru, lakini tunasubiri ripoti ya kamati ya pili iliyoundwa kuchunguza sakata hili wampelekee ripoti Rais,” alisema Msigwa.

Kamati ya awali iliyokuwa ikiongozwa na Prof. Mruma ambayo ilikabidhi ripoti yake Mei 24 mwaka huu ilionyesha kuwa kiwango cha madini yaliyomo kwenye makinikia hayo ni zaidi ya yale ambayo hujazwa kwenye makabrasha.

Mbali na kuonekana kiasi kuzidi, lakini kamati hiyo ilibaini pia kuna madini makakati (strategic metals) ambayo yamo kwenye makinikia hayo lakini hayakuwa yakitajwa na kampuni zinazosafirisha mchanga nje jambo lililosababisha serikali kupata hasara ya mabilioni.

Kwa upande wao Acacia, walipinga ripoti hiyo na kusema wao hutangaza kila kitu kwa mujibu wa sheria na kulipa tozo zote stahiki hivyo kuomba iundwe kamati huru kuchunguza upya kiasi cha madini kwenye mchanga huo.

CHADEMA Wamtupia Lawama Mkapa na Kikwete sakata la mchanga wa madini

$
0
0
Mwenyekiti  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, wanahusika na sakata la mchanga wa madini (makinikia) unaosafirishwa nje ya nchi.

Pia amesema Mkapa na Kikwete hawawezi kukwepa lawama juu ya mchanga huo kwa kuwa mikataba kati ya Serikali na wawekezaji wa migodi inayotajwa, ilisainiwa kwa nyakati tofauti wakati wao wakiwa madarakani.

Kauli hiyo aliitoa mjini Dodoma  jana alipozungumza katika mkutano wa Baraza Kuu la Chadema uliokutanisha wajumbe 332, kati ya 370 waliotakiwa kuhudhuria.

 “Kama kuna kitu kinaangamiza nchi, ni pale unapomwambia mfalme umevaa suti wakati unaona yuko uchi. Katika sakata hili la mchanga, sisi kama chama cha siasa, tumekaa na wataalamu wetu na kukusanya taarifa kwa sababu wengi wanalizungumzia kwa kauli tofauti,” alisema Mbowe na kuongeza: 

“Kwanza kabisa inabidi tuelewe kwamba mchanga wa madini umekuwa ukisafirishwa kwenda nje ya nchi kutoka kwenye migodi yetu miwili ya Bulyanhulu kuanzia mwaka 2001 na Buzwagi kuanzia mwaka 2008.

“Eleweni kwamba leseni za kusafirisha mchanga kwenda nje zilitolewa na Serikali hii hii ya CCM na katika mikataba hiyo, kunatambulika kuna madini mengine mbali na dhahabu katika migodi hiyo.

 “Pia makontena ya madini yanapokuwa bandarini kabla ya kusafirishwa, watu wa TRA, TMAA, lazima wahakiki makontena yenye mchango huo ili kujiridhisha na kilichomo.

“Wakati mikataba hii inasainiwa, Rais Dk. John Magufuli alikuwa kwenye Baraza la Mawaziri na pia Mkapa na Kikwete, wanayajua haya kwa sababu mikataba ilisainiwa wakati wao wakiwa madarakani kwa nyakati tofauti.

“Nasema hivyo kwa sababu enzi za Mkapa, mikataba mingi ya madini ilisainiwa na hata Kikwete alipokuwa Waziri wa Nishati, kuna mkataba aliusaini.

 “Kibaya zaidi, CCM wamekuwa wakitumia wingi wao vibaya bungeni kupitisha sheria mbovu kwa sababu hata mwaka 1997, Bunge lilipitisha kwa siku moja sheria mbili za madini chini ya hati ya dharura na mwaka 1998, Bunge lilipitisha sheria nyingine ya madini inaweka utaratibu wa uchimbaji wa madini na kuruhusu wawekezaji kutoa mrabaha wa asilimia tatu ingawa baadaye mrabaha huo ulibadilishwa na kuwa asilimia nne, huku sheria hiyo ikiruhusu mchanga usafirishwe kwenda nje ya nchi.

“Yaani, hata mikataba yetu inaruhusu wawekezaji kupewa misamaha ya madini wakati sheria haisemi hivyo. Kwa hiyo, kinachotokea sasa ni matokeo ya CCM kutufikisha tulipofika.”

Kutokana na hali hiyo, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kuna uwezekano mkubwa Kampuni ya Acacia inayomiliki migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ambako mchanga huo ulipatikana, ikafungua mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro.

“Jana nilikuwa nasoma Gazeti la Telegraph la Uingereza ambapo wanasema tatizo sio wawekezaji bali ni Waafrika wanaoingia mikataba ya uwekezaji na wanasema kwa mujibu wa mkataba wetu, mchanga sio mali ya Tanzania bali ni mali ya wawekezaji.

“Kwa hiyo, kinachoonekana sasa ni kwamba nchi inaingia katika mgogoro wa kidiplomasia na wawekezaji na kama wakiamua kwenda mahakamani, hatutashinda kesi kwa sababu mikataba tuliisaini vibaya.

“Kibaya zaidi, ni kwamba kesi haitakuwa Kisutu, Kinondoni, Mwanza au Kigoma, bali itafanyika huko huko kwao,” alisema.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alisema kwa kuwa uwezo wa Tanzania ni mdogo katika uwekezaji wa miradi mikubwa, Serikali inatakiwa kuwa makini kwa sababu si kweli kwamba wawekezaji wote ni wezi na pia si kweli kwamba wote ni waaminifu.

Akizungumzia hali ya kisiasa, Mbowe alisema katika uzoefu wao kisiasa, Serikali ya awamu ya tano ndiyo ngumu katika harakati zao kwa sababu Rais Magufuli anakandamiza demokrasia.

Kwa mujibu wa Mbowe, alisema serikalini kuna baadhi ya viongozi wanaamini njia pekee ya kuwaweka madarakani ni kuvunja sheria na kuminya demokrasia, jambo ambalo wamelivumilia kwa muda mrefu na kuwafanya viongozi hao waamini Chadema ni waoga.

Alitoa mfano wa matukio aliyosema ni uminywaji wa demokrasia nchini ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa, kukamatwa kwa wanasiasa wa upinzani na kufikishwa mahakamani bila sababu na kupotea kwa kada wa Chadema, Ben Saanane.

 “Awamu hii ya tano ni ngumu sana kisiasa, lakini pia inatoa fursa kwetu kwa sababu wananchi wana maisha magumu kweli kweli kuliko Serikali yoyote katika nchi yetu.

“Rais lazima ajue kwamba matendo yake yanaathiri Watanzania milioni 50 na ajue sisi tunahitaji pia aliyeko madarakani alete amani kwa sababu nchi ni yetu sote.

“Kwa kifupi, nchi yetu kwa sasa haiko salama, kisiasa, kiuchumi na wala kijamii, kwa sababu kila mmoja anashuhudia jinsi watu wanavyouawa Rufiji na Mkuranga.

“Pamoja na hayo, eleweni kwamba haki haipatikani kwa kuombwa bali kwa mapambano. Kwa hiyo, lazima katika kikao chetu hiki tutoke na uamuzi mgumu ili watawala wa nchi hii waelewe salama ya nchi ni kusimamia haki kwa watu wote na sio kwa wana CCM peke yao, kama mbwai na iwe mbwai,” alisema Mbowe.

Askofu Gwajima Afunguka Mazito Sakata la Madini Katika Mchanga

$
0
0
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefunguka na kusema Watanzania tumerogwa kwani tuna kila kitu ambacho kinaweza kutufanya kuwa mbele kimaendeleo lakini siku zote tumekuwa nyuma.

Mchungaji Gwajima amesema hayo leo wakati akitoa mahubiri yake kwenye kanisa lake na kusema Watanzania wamerogwa kwani wanapenda sana maandamano na vitu visivyo na msingi kuliko kufanya kazi, anasema Tanzania ina vitu na mali nyingi

"Ukitaka kuingoza Tanzania lazima uwe na moyo wa mwendawazimu maana watu wake wamerogwa mpaka wamerogeka, ni nchi ya waliorogeka tu unaweza kwenda kusaini mikataba ya madini, nenda kasaini mkataba wa madini Japan au Kenya uone, sisi Tanzania Watanzania tunauza ubuyu na karanga mzungu anabeba kila kitu, sisi tumerogwa. Tanzania ina mito mingi yenye maji lakini maji yanakwenda tu, watu hawalimi" alisema Gwajima

Mbali na hilo Gwajima amempa tano Rais Magufuli kwa kitendo chake cha kuzuia makontena ya madini na kusema ni hatua nzuri na Rais ashikirie hapo hapo

"Hata kama tulisaini mikataba ya kufa mtu sawa tu Rais ashikirie hapo hapo hakuna kuruhusu makontena mpaka wazungu macho yao yawe mekundu, kama hatujawa tayari kuchimba madini tuyaache kwanza, wapo wanaosema sijui tutashitakiwa, sijui mikataba itatubana ondoka na makaratasi yako hapa yale madini ni ya kwetu, mwanasiasa unayetaka kulia ulie tu na ufe madini hakuna kwenda" alisema Gwajima

Breaking News: Rais Magufuli Amuondoa Ernest Mangu......Amteua Simon Sirro Kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2017 amemteua Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Kabla ya Uteuzi huo IGP Simon Sirro alikuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

IGP Simon Sirro anachukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa IGP Simon Sirro ataapishwa kesho Jumatatu tarehe 29 Mei, 2017 saa 3:30 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Mei, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 29

Jinsi Kitambi Kinavyopatikana na Jinsi Kinavyoondolewa na Dawa ya Mkataa Kitambi

$
0
0

Kitambi  ni  ile  hali  ya  tumbo  kuwa kubwa  na  kuchomoza  kwa  mbele  na  wakati mwingine  kufikia  hatua  ya  kunin’ginia.
JINSI  KITAMBI  KINAVYO  PATIKANA
Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati  ya bilioni 50  hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili wa binadamu.

 Kwa wanawake  seli hizo  zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye  nyonga, kiunoni na kwenye makalio.

Kwa upande  wa  wanaume seli  hizo zinapatikana  sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia.

Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:

i.Njia  ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi

ii.Na  njia  ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

SABABU ZA KUPATA KITAMBI
Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika  mwili  wa  mwanadamu, hali  inayo  sababishwa  na  mtu  kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.

VYAKULA  VINAVYO  CHANGIA KULETA  KITAMBI

Vyakula vinavyochangia  kuleta  kitambi ni  pamoja  na :
i.Vyakula  vyenye  mafuta  mengi  kama  vile  nyama nyekundu  (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama  ya  kuku  wa  kizungu  ( iwe  ya  kuchemsha, kukaanga  ama  kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi ya kukaanga kwa  mafuta  (chips) pamoja  na  pizza.

ii.Vyakula vyenye wanga mwingi kama  vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate  mweupe.

iii. Vyakula  na  vinywaji  vyenye  sukari  nyingi  iliyo  ongezwa( added  sugar ), kama  vile  soda  na  keki.

iv. Vyakula  vilivyo  tengenezwa  kwa  ngano  na  sukari kama  vile  keki, skonzi, chapatti, maandazi, mkate  mweupe  nakadhalika

v. Pamoja  na  vinywaji  vilivyo  tengenezwa  kwa  kutumia  ngano  kama  vile  bia  za  aina  mbalimbali  na  kadhalika.

Vyakula  vilivyo  tajwa  hapo  juu, vikitumiwa  bila  kuzingatia  kanuni  za  mlo  kamili, huchangia  kuleta  tatizo  la  kitambi.

vi. Sababu nyingine ni  kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na  viungo(  physical  exercises  )  kwa  muda  mrefu.

JINSI YA KUJUA KAMA UNA KITAMBI
Kitambi kinaweza kuonekana kirahisi kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya vipimo vya kiuno(waist) na nyonga (hips).

Mzingo wa kiuno ukiwa >102 cm au 40  kwa wanaume na >88 cm au 35  kwa wanawake, na uwiano wa kiuno na hips(Waist-Hip Ratio) ikiwa >0.9 kwa wanaume na >0.85 kwa wanawake.

BMI ya 30 au zaidi inaashiria 'Obese' uzito kuzidi kiasi. Kuwa na mzingo uliozidi kawaida ni kiashiria hatari cha matatizo ya kimetaboliki, kuliko hata cha BMI.

Kipimo kingine cha kitambi ambacho kimeonyesha uwezo zaidi kuliko BMI katika kutabiri uwezekano mkubwa wa magonjwa ya moyo ni Index Of Central Obesity(Waist-To-Height Ratio-WHtR) ambapo uwiano ukiwa sawa na 0.5 au zaidi, hii ikimaanisha mzingo wa kiuno angalau ni nusu ya kimo cha mtu.

Kipimo kingine ni Body Volume Index, kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.

MAMBO  YANAYO  MUWEKA  MTU  KATIKA  HATARI  YA  KUPATWA  NA  KITAMBI
Tumekwisha  ona  hapo  juu jinsi  kitambi  kinavyo  patikana  na  vyakula  pamoja  na  sababu  nyinginezo  zinazo  sababisha  kutokea  kwa  kitambi, sasa  tutazame  mambo  yatakayo  kufanya  uwe  katika  hatari  ya  kupatwa  na  kitambi.

Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za kitaalamu, mambo  yafuatayo  huwaweka  watu  katika  hatari  kubwa   ya  kupatwa  na  kitambi :

1. Ulaji  mbovu  wa  chakula; Ulaji  mbovu  wa  chakula  ni  ulaji  usio  zingatia  kanuni  za  mlo  kamili. Hapa  mtu  hufululiza  kutumia  chakula  cha  aina  fulani  pekee  bila  kuzingatia  aina  nyinginezo  za  chakula.  Mfano; mtu  anaweza  kuwa  anakula  mlo  ufuatao :

Asubuhi :  Mchemsho  ama    supu  ya  ng’ombe , chapatti  tatu  na  soda  moja.  Mchana :   Ugali  nyama  choma anashushia  kwa  maji  na  soda.

Jioni :  Mchemsho  wa  kuku  na  bia  mbili  nakuendelea.

Usiku  :  Chips  mayai  au  chips  kuku  au  chips  mishikaki  na  bia.

Mtu  huyu  akiendelea  na  utaratibu  huu  kwa  muda  mrefu, ni  lazima  atapatwa  na  kitambi.

2. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  mafuta  mengi

3. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye wanga  mwingi  

4.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  sukari  iliyo  ongezwa ( added  sugar  ).

5.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vya  ngano.

6.Ulaji  mfululizo  wa   vinywaji  vyenye ngano  na  sukari.

7.Kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na viungo  ( physical  exercises  ).

Mhusika  anapokuwa  katika  makundi  yote  yali yotajwa  hapo  juu, hali  huwa  mbaya  zaidi. 

NJIA ZA KUONDOA KITAMBI
Kuwa  na  kitambi  ni  lugha  ya  mwili  ( body-language )  inayo  leta  ujumbe  kwako  kwamba  “ Mwili    wako  haupo  salama  tena “

Kama  una  kitambi   maana  yake  una  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini, mwili  wako  unatumika  kuhifadhi  mafuta  usiyo  yahitaji.

Hali  hii  kitabibu  imaanisha  kwamba, ogani  nyinginezo  zilizomo  ndani  ya  mwili  wako  zinao gelea  kwenye  mafuta( fats  )  yasihotika  yaliyomo ndani  ya  mwili  wako,  jambo  linalo  kuweka  katika  hatari  kubwa  sana  ya  kushambuliwa  na  magonjwa  hatari  kama  vile  shinikizo  kubwa  la  damu, kiharusi  na kisukari  na  kwa kutaja  machache.

Hivyo  basi  ili  kuondokana  na  hatari  hiyo, yakupasa   kupambana  kuondoa  hayo  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini  mwako.

NJIA  ZA  KUONDOA  KITAMBI.
Unaweza  kuondokana  na  kitambi  kwa  kufanya  diet  pamoja  na  mazoezi ya  mwili  na  viungo.

Vilevile  unaweza  kuondoa  kitambi  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  dawa  asilia  ya  kuondoa  kitambi  na  kuondoa  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

DAWA   ASILIA  YA  KUONDOA  KIAMBI  NA  MAFUTA  MWILINI.
Hii  ni  njia  ya  uhakika  kabisa  ya  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

 Unaweza  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  DAWA  ASILIA   IITWAYO YA  MKATAA  KITAMBI.

 Dawa   hii  ni  ya asili  kabisa
“  Pure  Herbal “, ambayo  haijachanganywa  na  kemikali  yoyote, haina  side  effect kwa  mtumiaji  na  inaondoa  kabisa  tatizo  la  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

JINSI  DAWA  YA  MKATAA  KITAMBI  INAVYO  FANYA  KAZI.
1.Huyeyusha  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

2.Husaidia  kupunguza  hamu  ya  chakula.

3.Inazuia  kutengenezwa  kwa  seli  za  mafuta  ( fat cells  ) katika  mwili  wa  mwanadamu. Unapokula  chakula  chenye  mafuta  mengi, dawa  hii asilia  hupambana  kuyafanya  mafuta  hayo  yasitengeneze  seli  za  mafuta  mwilini  mwako. Hali  hii  huuepusha  mwili  wako  kuhifadhi  mafuta   yasiyo  hitajika  mwilini.

4. Husaidia  kupunguza  uzito wa mwili  kwa  haraka  sana  endapo  itatumika  pamoja  na  diet  ya  kabechi.

UFANISI  WA  DAWA.
Ufanisi  wa  dawa  hii  ni  wa  asilimia  mia  moja. Dozi  ya  dawa  hii  hutumika  kwa  muda  wa  siki  ishirini  na  moja.

MATOKEO  YA  DAWA:
Dawa  hii  huondoa  kabisa  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

BEI  YA  DAWA :
Dawa  hii  inaoatikana  kwa  kiasi  cha  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU  (Tshs. 50,000/=)

MAHALI  TUNAPO  PATIKANA.
Tunapatikana  jijini  DAR  ES  SALAAM, katika  eneo  la  UBUNGO  karibu  na  SHULE  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

KWA  WATEJA  WASIO  WEZA  KUFIKA  OFISINI  KWETU.
Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu  Tabata, tunao  utaratibu  wa  kuwafikishia  dawa  mahali  popote  walipo  ndani  ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  DAR  ES  SALAAM.
Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  Dar  Es  salaam, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  MABASI.

Kwa  wateja  wa  ZANZIBAR  tunawatumia  dawa  kwa njia  ya  boti.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  NCHI:
Kwa  wateja  wa  nje  ya  nchi, tunatumia  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA : 0766  53 83 84

TUTEMBELEE:

Wanawake Wawili Wauawa Kwa Kukatwa Katwa Mapanga Tabora

$
0
0
Wanawake  wawili wilayani Igunga mkoani Tabora wameuawa kikatili kwa kukatwa na mapanga na watu wasiojulikana huku mmoja akikatwa kiganja cha mkono wa kulia.

Mtendaji wa Kata ya Tambalale, Salumu Kitindi alimtaja aliyeuawa kuwa ni Elizabeth Charles (45), mkulima wa kijiji cha Tambalale, kata hiyo ya Tambalale, Tarafa ya Nsimbo.

 Kitindi alisema watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwa mama huyo ambaye kwa sasa ni marehemu usiku kisha kuingia ndani na kumshambulia kwa mapanga hadi kupoteza uhai wake ambapo baada ya kufanya mauaji hayo walikata kiganja cha mkono wa kulia kisha kuondoka nacho kusikojulikana.

Naye Mtendaji wa Kata ya Mwisi, Issa Omary alisema katika kata yake, mwanamke Suzana Alex (24) mkulima mkazi wa Kijiji cha Busomeke, Tarafa ya Simbo ameuawa kwa mapanga kwa kukatwa sehemu mbalimbali za mwili wake huku mumewe, John Matheo (27) akijeruhiwa vibaya ambapo amelazwa Hospitali Misheni ya Ndala iliyoko Nzega.

Aidha, Omary alibainisha kuwa watu hao walifika katika mji huo saa saba usiku ambako walivunja mlango na kuingia ndani kisha kuanza kuwakata kwa mapanga wanandoa hao na kusababisha Suzana kuuawa papohapo kisha kuondoka bila ya kubeba kitu chochote.

Mkuu wa Wilaya ya Igunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo, John Mwaipopo alithibitisha kuuawa kwa akinamama hao na kueleza kuwa Jeshi la Polisi Igunga linaendelea na msako wa kuwabaini waliohusika na mauaji hayo huku akitoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na mauaji kuacha mara moja.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images