Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Ataja Sababu za Kumfukuza kazi Profesa Ntalikwa

$
0
0
Rais wa John Magufuli ameeleza sababu kwa nini alimfukuza kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa.

Rais Magufuli amesema kuwa alichukua uamuzi huo kutokana na Profesa huyo kueleza Kamati ya Bunge kiasi ambacho kilikuwa kipo kwenye makontena ya dhahabu ambacho hakikuwa sawa.

Profesa Ntalikwa alifutwa kazi na Rais Magufuli siku chache baada ya kufanya ziara ya kushtukiza bandarini lakini hakubainsha iwapo kuna uhusiano kati ya ziara hiyo na kufutwa kwake Ntalikwa.

Watu Wawili wanaodaiwa ni wapenzi wauawa kwa kuchomwa moto Arusha

$
0
0
Watu wawili wanaodhaniwa ni wapenzi,  wameuawa kwa kuchomwa moto baada ya kufungwa kamba wakiwa kitandani, katika  tukio lililotokea eneo la Whiterose lililoko kata ya Kiranyi wilayani Arumeru mkoani  Arusha.

Mamia ya watu wamejitokeza  kuzunguka nyumba lilipotokea tukio hilo baada ya kuona moshi ukitoka katika moja ya chumba na kuonekana miili ikiwa imeteketea kwa moto.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo amesema tuki hilo limetoke jana, Jumanne saa 3.00 asubuhi

Amesema aliyekutwa amefariki ni  Maurine Urio (32)  pamoja na rafiki yake huyo ambaye hajaweza kutambulika kutokana na kuungua sana.

“Tumepata taarifa asubuhi hii kuwa kuna nyumba inaungua na polisi pamoja na zimamoto walifika eneo la tukio na kukuta watu hao wameshapoteza maisha wakiwa juu ya godoro ambako mwanaume alionekana kabla ya kuchomwa alifungwa kamba miguu na mikono ili kuzibitiwa,”amesema.

Mkumbo amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru huku wahusika wa tukio hilo wakiwa wanatafutwa.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Ilkiurei iliyoko kata ya Kiranyi, Onesphory Chami amedai kuwa tukio hilo linahusishwa na wivu wa mapenzi.

Breaking News: Rais Magufuli avunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na pia kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wake kwa kushindwa kusimamia vyema sekta ya madini.

Mbali na kuchukua hatua hiyo, Rais Magufuli ameviagiza vyombo husika pia kuwachukulia hatua watendaji wa TMAA na Wizara ya Nishati na Madini waliohusika kuisababishia hasara serikali kutokana na mchanga wa madini uliokuwa ukisafirishwa kwenda nje.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akipokea taarifa kuhusu ripoti ya ukaguzi wa mchanga wa madini wa makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini.

“Bodi ya TMAA nimeivunja kuanzia leo. Mkurugenzi Mtendaji wa TMAA anasimama kazi kuanzia leo lakini vyombo vya dola ambavyo vipo hapa muanze kuwafuatailia wafanyakazi wa TMAA waliohusika na mlolongo wote ili hatua za kisheria zianze kuchukuliwa” alisema Rais Dkt Magufuli.

Lakini wakati huo huo Rais Magufuli ameikosoa Wizara ya Nishati na Madini kwa kushindwa kuisimamia vizuri TMAA ambayo ipo chini yake, na hivyo kuisababishia serikali hasara kubwa kutokana na usafirishwaji wa mchanga nje ya nchi.

Breaking News: Rais Magufuli atengua uteuzi wa Waziri wa Nishati, Prof. Muhongo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo kuanzia leo tarehe 24 Mei, 2017.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadaye.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Barua ya Prof. Muhongo kwa Rais Magufuli

Isome hapa ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini iliyowasilishwa kwa Rais Magufuli

$
0
0
Isome hapa ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini iliyowasilishwa kwa Rais Magufuli

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya May 25


Acacia Waipinga Ripoti Iliyowasilishwa Kwa Rais Magufuli kuhusu Madini........ Watoa viwango vyao vya madini kwenye mchanga

$
0
0
Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia imetoa taarifa kwa umma na kueleza kuwa kamati iliyofanya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini imepotosha juu ya uwepo wa viwango mbalimbali vya madini kwenye mchanga.

==>Hii ni taarifa yao

By Brad Gordon | Chief Executive Officer | Acacia Mining PLC

Response to this morning’s Press Conference and presentation of the First Presidential Committee’s report on the export of metallic mineral concentrates to the President of Tanzania.

Many of you would have seen this morning’s press conference held at State House at which the First Presidential Committee presented its findings on its investigation into the export of gold/copper concentrates.

The Committee has stated that Acacia has not fully declared all of the minerals contained in the concentrate that it exports and the directive halting the export of metallic mineral concentrates remains in place.

We do not agree with the Committee’s findings which state that the value of minerals within the concentrates in the containers currently at the Dar-es-Salaam port is more than 10 times the amount we declare. We are confident in the accuracy of our declarations which are checked and verified by SGS, which is one of the world’s largest testing companies. The concentrate we produce has some small variances, and each container has different declared quantities of concentrate, but we firmly believe that each container contains on average around 3,000kg of copper, 3 kg of gold and 3 kg of silver. Together, these metals are worth an average of Tsh300 million per container.

We are also a listed company with our accounts being audited extensively by PWC, which verifies that we are fully transparent in everything we do. The revenues we state in our audited accounts match the amount of gold that we declare we produce and sell. If the amount of gold in our concentrates was in line with the Committee findings, then it implies that both Bulyanhulu and Buzwagi would produce more gold than any other mine in the world. Sadly this is not the case.

I appreciate that when events like today happen it creates uncertainty and makes people question who to believe. I want to reassure you that Acacia fully declares everything of commercial value that we produce. We also pay all appropriate royalties and taxes on all of the payable minerals that we produce and that the exporting of the concentrate takes place in full compliance with Tanzanian law and the legal agreements that we have with the Tanzanian Government.

Whilst we have listened to today’s presentation and seen a transcript of the press conference, until we receive a copy of the full report it is difficult to comment on or reconcile the specific numbers and values attributed to Acacia’s metallic mineral concentrates by the Committee, but I repeat, we believe in the numbers we declare.

Whilst we await the report I will respond to one question about royalties that has been raised among the workforce. Under the mining act the Government receives royalties of 4% of the minerals of commercial value namely gold, silver and copper contained in the concentrates. Acacia has always paid the royalty and there is a robust audit trail to demonstrate this. Whilst there are other minerals contained in the concentrate, these are of no commercial value. This is due to the small quantities and the cost to extract them exceeds their value, and so no royalty is due.

Obviously today has been a difficult day for everyone at Acacia. I can assure you that we are doing everything we can to ensure that all of our stakeholders believe in the integrity of Acacia. We have fully declared everything that we produce and have done so since Barrick first entered Tanzania over 15 years ago. We have not cheated the country that we operate in and whose people make up 96% of our workforce. Please continue to work safely as that is the most important thing and I will continue to provide you with updates and hopefully clarity as we move through the coming weeks.

FULL VIDEO: Hotuba ya Rais Magufuli Wakati Akikabidhiwa Taarifa ya Uchunguzi wa Mchanga wa Madini

$
0
0
Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli amepokea taarifa ya uchunguzi wa mchanga wa madini mbalimbali uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini nchini.

SBL yatoa zawadi ya gari aina ya Heicher ya shs 50m/- kwa msambazaji bora

$
0
0
Dar es Salaam, Mei 24, 2017-Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetoa zawadi ya gari aina ya Heicher  lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa MM Group,  ambaye ni msambazaji wa kanda aliyeibuka msambazaji anayeongoza  katika kipindi cha kwanza cha nusu mwaka  huu wa fedha 2017.

Kampuni ya MM Group ambayo  ina makao yake  wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi iliwashinda wasambazaji wengine 85 walioshiriki kwa ajili ya kupata zawadi hiyo  ya kipekee.

Akiendesha  hafla hiyo ya makabidhiano  iliyofanyika katika makao makuu ya SBL Temeke, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo  alimpongeza mshindi  huku akithibitisha kujikita kwa kampuni  hiyo ya bia katika kutambua  juhudi zinazofanywa na wateja wake  katika kuunga mkono ukuaji kwa kampuni.

“Wakati tunapongeza  mchango wa MM Group kwa kuongoza na kushika nafasi ya juu  katika kipengele chake kulikomwezesha kupata zawadi hii, tunatambua pia  kazi nzuri inayofanywa na  wasambazaji wengine, wateja na hali kadhalika wadau wetu. Kupitia uungwaji mkono huu wa dhati, SBL imekua katika uzalishaji  na kufikia kiwango cha juu  katika sekta ya uzalishaji bia  ndani   ya nchi na hata katika ukanda wa Afrika Mashariki,” alisema Tayo.

Akitoa wito kwa wasambazaji wengine wa SBL kuiga mfano wa MM Group, Tayo aliwahahakishia washirika wa SBL kibiashara wakiwamo wasambazaji na wateja kwamba SBL itaendelea kuwaenzi na kusikiliza mahitaji yao.

“Tunawashukuru wadau wetu wote kwa kuzingatia kwamba  wamekuwa pamoja nasi katika katika safari yetu ndefu na ya mafanikio kibiashara”, alibainisha Tayo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika, wakati akiishukuru SBL kwa zawadi hiyo,  aliwapa changamoto wasambazaji wengine kuendesha na kuenenda na ukaribu wa SBL kwa kufanya kazi kwa bidiii ili kufuzu kwa ajili ya tuzo kama hiyo.

“Naishukuru sana SBL  kwa kuheshimu ahadi yake  na kunituza gari hili Heicher. Hili gari ni zana  muhimu katika biashara yangu ambayo itaniwezesha kukuza shughuli zangu za usambazaji wa bidhaa za SBL,” alisema Bw Joseph Chanika kwa bashasha.
Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo (wa kwanza kushoto) akimkabidhi nyaraka za gari aina ya Heicher  lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika,  ambaye ni msambazaji wa kanda aliyeibuka msambazaji anayeongoza  katika kipindi cha kwanza cha nusu mwaka  huu wa fedha 2017.wanaoshuhudia katikati ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy ,na Baraka Kilimba Meneja Mauzo Baraka Kilimba na mwishoni ni Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha
Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo Akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu zawadi ya msambazaji bora ambapo MM Group kutoka Mpanda aliibuka mshindi ,kulia kwake ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy na kushoto kwake ni Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika,mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo wa kutangaza mshindi mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.
Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa kutangaza mshindi wa shindano la msambazaji bora ambapo MM Group toka Mpanda aliibuka mshindi ,anayefuatia katikati ni Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo na mwishoni kulia ni ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy ,mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika akijaribu gari lake mara baada ya kukabidhiwa baada ya kuibuka kama msambazaji bora ,Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari aina ya Heicher  lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

" Wasukuma Tutaziloga Ng'ombe Zetu Ili Mtakaokula Mvimbe Matumbo" - Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku

$
0
0
Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Musukuma amesema hawezi kumsifia hata kidogo Prof. Jumanne Maghembe, Waziri wa Maliasili na Utalii kwani yeye na watu wake wa Wizara wanafanya mambo ya ajabu hasa kwa watu wa Kanda ya Ziwa.

Musukuma anasema watu wa Wizara ya Maliasili wamekuwa wakiuza ng'ombe za watu jamii ya wasukuma na kuzipiga mnada kwa dili kwa lengo la kujinufaisha wenyewe, hivyo mbunge huyo amesema wasukuma wameamua kuwa wataziroga ng'ombe zote ili wanaokula ngo'mbe hizo Dar es Salaam wavimbe matumbo.

"Napata shida sana kujiuliza labda sisi watu wa kanda ya ziwa labda tulikuja kwa bahati mbaya Tanzania hii, mbona yanayofanyika Kanda ya Ziwa hayafanyiki Kanda ya Kaskazini wakati nao wana mapori, Waziri ametoa siku tatu tukamatiwe ng'ombe kwa kisingizio kwamba ni ng'ombe za Wanyarwanda wakati huo huo watumishi wake wanaowaingiza Wanyarwanda wanawaambia toeni ng'ombe, mnaenda kukamata ng'ombe za Wasukuma halafu unazipiga mnada na mnada wenyewe unavyopigwa ni wa dili" alisisitiza Musukuma

Mbunge huyo aliendelea kuelezea namna watu wa Wizara ya Maliasili wanavyofanya minada hiyo huku wakiwaumiza wafugaji

"Yaani ng'ombe 600 unaambiwa ulete milioni tatu halafu wanatoa watu wao wa Ubungo sasa hapo nikupongeze kwa sababu gani? Tunajua mipango inayoendelea kwenye wizara yako na niliwapigia kabisa watumishi wako, wananiambia mliipenda wenyewe kwa kauli yake kama Mwenyekiti wa Chama kesho yake akapiga ng'ombe za watu mnada yaani ng'ombe 500 zinauzwa milioni tatu" alisema Musukuma

Joseph Msukuma aliendelea na msimamo wake

"Nataka nikwambie sisi Wasukuma sasa tumeamua na ninazungumza uelewe tutaziroga hizo ng'ombe mtavimba matumbo mnaozila huko Dar es Salaam, haiwezekani kwanini wanunuzi watoke Dar es Salaam peke yake yaani leo siku ya mnada watu wametoka na malori Pugu wamejuaje kama wanakuja kushinda kwenye minada. Mnatukamatia ng'ombe hivi hii serikali imekosa sehemu ya kukusanya hela mpaka mkanyang'anye ng'ombe za wafugaji haiwezekani Mh. Maghembe"

Kafulila Afunguka Baada Ya Profesa Muhongo Kutumbuliwa

$
0
0
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu David Kafulila ameibuka na kutoa ya moyoni baada ya maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli baada ya kupokea ripoti ya Kamati Maalum kuhusiana na uchunguzi wa makontena 272 ya makinikia yaliyokuwa  tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi .
 
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Kafulila ameandika yafuatayo,
  1. Naipongeza Kamati kwa kazi iliyotukuka iliyojaa majaribu ya rushwa kubwa kwani kampuni nyingi madini, mafuta na gas duniani zina sifa hiyo kama alivyopata kusisitiza Profesa Joseph Stirglitz gwiji la uchumi na utandawazi duniani.
  2. Zaidi hatua aliyo chukua Rais kuhusu uharamia huu katika sekta ya madini inapaswa kuungwa mkono na kila mzalendo kwani imekuwa hoja ya upinzani na kila mzalendo kwa miaka mingi iliyoishia kubezwa na kupuuzwa.
  3. Rais asiishie kutaka uchunguzi kufanywa dhidi ya watumishi katika sekta ya madini tu, nchi hii imeoza, uchunguzi ufanywe mpaka ndani ya Idara ya Usalama na vyombo kama TAKUKURU kwani mafisadi hawa waliweka mfumo mzima mfukoni kwa kujenga mahusiano na baadhi ya wanausalama na vyombo vingine vyeti kiuchunguzi.
  4. Namshauri Rais aboreshe Idara ya Usalama kwa kuwa na kitengo cha ujasusi wa kiuchumi (Economic Intelligency) kitakachoweza kumudu kukabiliana na uharamia ktk utoroshaji utajiri wa nchi (illicits flows) kwani nchi inavuja kwa miaka mingi na mtandao wa uharamia huu uliweka sehemu kubwa ya mfumo mfukoni.
  5. Kuna haja yakutazama Katiba yetu upya ili ikibainika hata Rais kama alihusika na ufisadi afikishwe kwenye mkondo wa sheria kwani nchi nyingi za Africa zimeoza kwa ufisadi kuanzia Ofisi Kuu, huko ndio vinatoka VIMEMO kuruhusu uharamia wa namna hii. Ni Ushauri wangu kwa Rais aruhusu mchakato wa Katiba ili pamoja na mambo mengine tuangalie mfumo wa Ofisi Kuu kama moja ya chanzo cha uozo na uharamia huu.
  6. Ni vema Mheshimiwa Rais akatambua kwamba kampuni hizi za kimataifa zinaiba duniani kote ikiwemo Ulaya na Marekani, isipokuwa huku kwetu zinaiba zaidi kutokana na sera duni, sheria dhaifu, mifumo ya usimamizi dhaifu na udhaifu wa wanaopewa nafasi kwa ujumla. Kukabili tatizo hili lazima kutazama kwa mapana na kutengeneza mfumo madhubuti.
  7. Mwisho nimshauri Rais kwamba pamoja na kuchukua hatua hizi za kisheria za ndani, azifikishe kampuni hizi kwenye Mahakama za Kimataifa (Arbitration court) kama inavyo tamkwa kwenye mikataba ili kuzidai fidia kwa miaka yote ya Mikataba yao.
Mitambo na mali zao zishikiliwe mpaka kesi itapomalizika. Na hili lisisomeke kwamba nikukimbiza wawekezaji bali nikukabili uharamia wa utoroshaji rasilimali ambao hata sheria zakimataifa zinapiga vita. Hili ni muhimu sana. Umma una paswa kusimama pamoja dhidi ya uharamia huu!

Jipatie Riwaya ya Kusisimua ya Am Not A Doctor Toka Kwa Mtunzi Makin Eddazaria

$
0
0
UNAANZAJE KUKOSA KITABU HICHI CHA KUSISIMUMUA #AM NOT A DOCTOR
Jipatie nakala ya kitabu hichi kupitia WHATSAPP 0657072588 au EMAIL eddazariaM@gmail.com kwa kiasi cha sh 10000/=TUUU

Kupitia kitabu hichi kitakufundisha mambo mengi sana hususani jinsi ya kufanikiwa kutoka ZERO to HERO. Usikose kitabu hichi kwa kweli. Karibu sana

AM NOT A DOCTOR
'Kila mtu kwenye maisha ana ndoto, ila si kila binadamu anaweza kuitimiza ndoto yake. Pesa, na mali walizo nazo wazazi wa Erick zinwapa jeuri ya kuhitaji mtoto wao aweze kufanya kile wanacho kitaka wao ila, Erick mwenyewe ana ndoto ambayo hakuna mzazi wake au mtu mwengine anaweza kuimini anaweza kuifanikisha. Mateso, majeruhi na maumivu mengi anayo yapitia kwenye kutimiza anacho kihitaji yanamkatisha tamaa mara tu baada ya mwanamke anaye mpenda kuliko kitu chochote kumuacha njiani kutoka na usaliti.
Je Erick peke yake atafanikiwa, ungana nami kwenye story hii ya kusisimua kutoka kwa mimi muandishi wako Eddazaria G.Msulwa

Kwa maoni na ushauri wasiliana nami kwa simu no 0657072588 au 0768516188 Utazungumza na mimi muandishi wako Eddazaria G.Msulwa moja kwa moja. KARIBUNI SANA

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 26


Watu 4 wafariki kwa kufukiwa na kifusi Geita

$
0
0
Watu wanne wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya Nyamalinde kijiji cha Sobola nje kidogo ya wilaya ya Geita, mkoani Geita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo limetokea  jana majira ya saa mbili asubuhi katika machimbo hayo yanayomilikiwa na wananchi licha ya kuwa tayari yalishapigwa marufuku kuendelea kwa kazi hiyo.

Mponjoli amesema tukio hilo limetokea baada ya watu 7 kuingia ndani ya mgodi huo, lakini muda mfupi baadaye kifusi kikawaangukia na kusababisha vifo vya watu wanne kati yao huku watatu wakitoka salama licha ya kuwa na majeraha.

Amewataja watu waliopoteza maisha kuwa ni pamoja na Robert Kazegemwa, Jeremia Emmanuel, Makenya Mwita na Julius Timotheo.

Waliojeruhiwa ni pamoja na Mashaka Samuel, Justine Safari na Maneno Lusika ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Katoro.

Katika tukio lingine, jana majira ya saa 7 mchana tetemeko dogo la ardhi limetikisa katika mkoa wa Geita ambapo licha ya kutokuwa na madhara yoyote, limezua taharuki katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika shule ya sekondari Nyang'wale.

Kamanda Mponjoli amesema katika shule hiyo, wanafunzi walikuwa katika mitihani na ndipo walipokimbia kutoka darasani ili kujiokoa ambapo kutokana na msukumano, mwanafunzi mmoja alijeruhiwa lakini tayari amekwishapatiwa matibabu na yuko salama

Sakata la Mauaji Pwani: CCM yataka viongozi wenye dhamana Wajiuzulu

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimelaani vikali mauaji ya baadhi ya viongozi, raia na askari polisi, waliouawa kwa kupigwa risasi katika wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga mkoa wa Pwani, na kutoa pole kwa familia zilizoguswa na mauaji hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari  jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey  Polepole alisema chama hicho kwa niaba ya wananchi kinawataka viongozi wenye dhamana na usalama wa wananchi kujitafakari, huku akisisitiza kuwa ikiwa mauaji hayo yataendelea, chama hicho kitaielekeza serikali kuwachukulia hatua.

“Sasa imetosha, yeyote mwenye dhamana ajitafakari.Hatupendi kusema hali hii ikiendelea watu wawajibike, ingawa kuwajibika kwa sababu ya watu kupoteza maisha ni ustaarabu wa kiungozi. Viongozi wote na wenye dhamana mchukue hatua, sitaki tufike pahala niseme, CCM tutaielekeza serikali kuchukua hatua kwa walio na dhamana kwa kutowajibika katika majukumu yao,” alisema na kuongeza Polepole.

“Tunaamini demokrasia ya vyama vingi ni mshikamano tunahisi kama tumeachwa wenyewe, tumevunjika moyo sana , sielewi mshikamano wa kuweka Tanzania moja, unakuja wakati wa uchaguzi au kugawana ruzuku? tumesikitishwa, nimeona wenzangu wametingwa na kufanya siasa za madaraka kuliko siasa za maendeleo zinazohusu shida za watu wetu.”

Aidha, Polepole alisema anasikitishwa na ukimya wa vyama vya upinzani kuhusu mauaji hayo, ambapo ameeleza kipindi hiki vyama vyote pasina kujali itikadi za kisiasa vingeungana kutetea uhai wa wananchi wa maeneo hayo ambao ndiyo wapiga kura wao.  

Alisema CCM wangependa kuona vyama vyote kwa sasa vinaungana hasa katika kipindi hiki ambacho wananchi wana hofu na maisha yao kutokana na mauaji hayo lakini jambo hilo limekuwa tofauti kwa wapinzani wao kuwa kimya na kutoonyesha kuumizwa na mauaji hayo.

“Hakuna namna bora ya kuwahudumia wananchi kama kuwa na mshikamano, wale wananchi wakienda kwenye kura wanachagua vyama vyote, wale wenzetu wamekuwa kimya, wametusikitisha, na hata wale walioongea wamecheza maneno, tusicheze maneno wakati uhai wa wenzetu upo hatarini,

“Sisi kama Chama cha Mapinduzi tukikaa kimya tutakuwa hatuwatendei haki watanzania ambao wakati kama huu wanapitia wakati mgumu, ninawaomba viongozi wote wenye dhamana wachukue hatua,” alisema Polepole.

Ushauri wa Tundu Lissu Kwa Serikali Kuhusu Sakata la Madini kwenye Mchanga

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.

Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu

"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu

Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.

"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu

Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...

"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu

TCU Yatangaza Mfumo Mpya wa Kudahili Wanafunzi Vyuo Vikuu

$
0
0
Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Vyuo Vikuu nchini kwa mwaka wa masomo 2017/2018 watatumia mfumo mpya wa udahili tofauti na ule uliozoeleka wa kuchaguliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Haya yamebainishwa katika taarifa ya TCU iliyotolewa juzi  ambapo  imesema kuwa wanafunzi wote wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka  wa masomo 2017/2018 watatumia mfumo mpya ambao unawataka kwenda vyuoni moja kwa moja kuomba nafasi.

Hivyo,taarifa hiyo imewataka wanafunzi  waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka wa masomo 2017/2018 kuomba nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu moja kwa moja vyuoni kuanzia tarahe 22 Julai 2017 hadi 13 Agosti 2017.

Sifa za kujiunga kwa wanafunzi wote ni kama ifuatavyo…
==> Isome taarifa ya TCU hapo chini

Serikali Yawapa Ahueni Wananchi Kumiliki Ardhi ......Madalali Watangaziwa Kiama

$
0
0
Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema Serikali inatarajia kuandaa sheria itakayowabana madalali katika sekta ya ardhi.

Amesema lengo la sheria hiyo ni kuwabana madalali hao ambao wamekuwa wakiuza ardhi katika siku za mapumziko kutokana na sababu wanazozijua wao.

Lukuvi aliyasema hayo bungeni jana alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2017/18.

“Wizara hii itatunga sheria ya kuwadhibiti madalali wanaowaonea wananchi kwa kuuza nyumba siku za sikukuu na weekend. Hao kiama chao kinakuja kwa sababu tutawatungia sheria na tutawatambua kwa sifa zao kisheria.

“Hata wenye maeneo makubwa mijini, lazima tutaanza kuwatambua na kuwatoza kodi hata kama hawajayapima.

“Utakuta mtu anamiliki ekari 30 mjini, zote hizo za nini, utafika wakati tutawazuia kuuza maeneo hayo kwa sababu wanaiibia Serikali,” alisema Lukuvi.

“Katika hilo, Serikali imejipanga kuhakikisha kila ardhi iliyopo nchini, inapimwa na kutumika kwa usawa na haki kama ilivyokusudiwa kwani kuna watu wanatakatisha fedha zao kupitia sekta ya ardhi,” alisema Lukuvi.

Kuhusu utoaji wa miliki za ardhi, alisema wizara yake itaendelea kushirikiana na halmashauri na sekta binafsi kuhakikisha kila ardhi inapimwa na kumilikishwa.

“Katika mwaka wa fedha 2016/17, wizara iliahidi kuandaa hatimiliki za ardhi 400,000 na kutoa hati za hakimiliki za kimila 57,000.

“Hadi kufikia Mei 15 mwaka huu, wizara imetoa hatimiliki za ardhi 33,979 na imeratibu uandaaji wa hati za hakimiliki za kimila 35,002 na pia wizara imeandaa vyeti vya ardhi za viijiji 505.

“Lakini, katika mwaka wa fedha 2017/18, wizara yangu kwa kushirikiana  na halmashauri nchini, itaandaa hatimiliki za ardhi 400,000, vyeti vya ardhi ya vijiji 1,000 na kutoa hati za hakimiliki za kimila 57,000.

“Ili kuwawezesha wananchi wengi kupata hatimiliki za ardhi, wizara inakusudia kupunguza tozo ya mbele ambayo hutozwa wakati wa kumilikisha kutoka asiliia 7.5 mpaka asilimia 2.5 ya thamani ya ardhi.

“Kwa hiyo, natoa wito kwa halmashauri zote nchini, kuhakikisha zinamilikisha viwanja vyote vilivyopimwa na kuandaa hati ili wananchi waweze kuwa na miliki salama,” alisema Lukuvi.

Wakati huo huo, alisema wizara yake itaendelea kuhakiki viwanja na mashamba nchini ili kubaini ukiukwaji wa masharti ya umiliki .

Pamoja na hayo, alisema baada ya kufanya uhakiki siku zilizopita, wizara yake imeshabatilisha miliki za viwanja 227 na mashamba 17 kutokana na ukiukwaji wa masharti. Viwanja na mashamba hayo, viko katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Iringa, Kagera na Morogoro.

Naye Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alimtaka Waziri Lukuvi atakapoanza kuchukua hatua kwa waliokiuka sheria za ardhi, asiangalie itikadi za kisiasa na badala yake kila mmoja achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu mradi wa viwanja 20, 000 jijini Dar es Salaam, aliitaka Serikali ifanye uhakiki wa viwanja hivyo ili kujua uhalali wa viwanja hivyo.

Pia, alitaka sheria za kimila za umiliki wa ardhi zinazowakandamiza wanawake, alitaka ziangaliwe upya ili wanawake nao wawe na haki ya kumiliki ardhi kama walivyo wanaume.

Naye Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka (CCM), alitaka migogoro ya ardhi inayohusisha wananchi na maeneo ya jeshi, itatuliwe haraka ili wananchi waishi kwa amani.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma (CUF), alilalamikia bei ya nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na kusema zinauzwa kwa bei kubwa ingawa viongozi wa shirika hilo wamekuwa wakisema zinauzwa kwa bei ndogo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images