Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mchungaji Rwakatale Amshukuru Rais Magufuli Kwa Kumteua kuwa Mbunge Viti Maalumu

$
0
0
Mchungaji  Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto  lililopo Mikocheni B,  Assembles of God, Dk. Getrude Rwakatale, amemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumkumbuka na kumteua katika nafasi ya ubunge wa Viti Maalumu.

Dk, Rwakatale alitoa shukrani  hizo Dar es Salaam jana wakati alipozungumza katika kanisa hilo wakati wa ibada ya Sikukuu ya Pasaka.

“Leo (jana) tunasherehekea kumbukumbu ya kufufuka kwa mwokozi wetu Yesu  ambaye alitufia pale msalabani,… Pasaka ya mwaka huu ni yangu, Mungu ameniona.

“Nina furaha ya mwili na roho kwa sababu Yesu amefufuka na pia Mungu amenirudisha bungeni, Mungu amejibu maombi yetu, tulifunga siku tatu na ile ya mwisho akajibu,”  alisema Mchungaji Rwakatale.

Alisema ana kila sababu ya kumshukuru Rais Dk. Magufuli kwa sababu  wapo wanawake wengi ambao angeweza kuwachagua na kuwapa nafasi hiyo.

“Nakishukuru pia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kunikumbuka, wapo wanawake wangapi lakini leo mlima wa moto katikati ya maombi, Mungu ametenda,” alisema.

Dk. Rwakatale alitumia ibada hiyo kuwaomba msamaha watu aliowakosea huku akiwasihi waungane naye kumshukuru Mungu katika maombi.

“Katika Luka 24:1-9 tunasoma habari kuhusu ufufuko wa Yesu, tumezoea makaburini huwa kuna habari mbaya lakini kwa Yesu ilikuwa tofauti, ilikuja habari njema.

“Alitangaza msamaha hata alipokuwa msalabani basi naomba mnisamehe nilipokosea maana na mimi ni mwanadamu,”  alisema.

Aprili 14, mwaka huu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),  kupitia kwa Mkurugenzi wa tume hiyo, Ramadhan Kailima ilitangaza jina la Mchungaji Rwakatale kuwa mbunge baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupeleka jina lake.

 Tume ilipitia  fomu zake na kuridhika kuwa mteule huyo ana sifa za kuwa mbunge akichukua nafasi ya Sophia Simba ambaye alivuliwa uanachama na chama chake.

Machi 11, mwaka huu, Sophia Simba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) alivuliwa uanachama kwa madai ya ukiukwaji wa maadili ya chama hicho na hivyo kumfanya kukosa sifa ya kuendelea kuwa mbunge kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.

Marekani: Hatuna Muda wa Ziada wa Kuvumilia Vitisho vya Korea Kaskazini

$
0
0
Mshauri wa Rais Donald Trump wa masuala ya usalama, Herbert Raymond McMaster amesema kuwa Marekani na China zinaelekea kupoteza uvumilivu dhidi ya Korea Kaskazini inayoendelea na vitisho vya silaha za Nyuklia.

McMaster amesema makubaliano yanayojitokeza dhidi ya tabia ya vitisho vya Korea Kaskazini kwa sasa yanaijumuisha China. 

Amesema kuwa kuna makubaliano ya kimataifa, ikiwemo China kuhakikisha tabia hii haiendelei, kwani kumekuwa na majaribio ya makombora ya hivi karibuni yanayoonyesha tabia ya vitisho ya Korea Kaskazini hali ambayo hawataivumilia zaidi.

Amesema kuwa Rais Trump ameweka wazi kuwa Marekani na washirika wake hawatokubali kuona utawala wa vitisho dhidi ya silaha za nyuklia.

Korea Kaskazini imefanya jaribio la uzinduzi wa makombora ya masafa ya mbali, hata hivyo lilikwama, ambapo Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence amefika Korea Kusini saa chache baada ya jaribio hilo.

Akizungumza katika kambi ya jeshi, Pence amesema anawahakikishia kuwa chini ya uongozi wa Rais Trump ushirika wa  Marekani  Korea Kusini haujawahi kuwa na nguvu lakini kwa msaada wa jeshi hilo na Mungu uhuru utaendelea kuimarika katika rasi ya Korea bila vitisho vyovyote

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya April 18

Bajeti Tano Za Wizara Zitakazopata Wakati Mgumu Bungeni

$
0
0
Wakati Bunge likiendelea na vikao vyake mjini Dodoma, wizara tano zinatarajia kujikuta kwenye wakati mgumu mijadala ya hotuba zao za bajeti itakapowadia kutokana na matukio ya hivi karibuni.

Wizara ambazo bajeti zake zinaweza kuibua mijadala mizito
ni Wizara ya Elimu; Tamisemi; Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Mambo ya Ndani; na Wizara ya Nishati na Madini.
 
Wizara ya Elimu inatarajiwa kukumbwa na mjadala kutokana na kutochukua hatua zozote tangu kuibuka kwa tuhuma za kughushi vyeti dhidi ya ofisa mmoja mteule wa Rais.
 
Tangu tuhuma hizo zilipoibuka, si Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) wala Wizara ya Elimu iliyoibuka kuzungumzia suala hilo.Wizara hiyo inaendesha uhakiki wa vyeti vya elimu kwa watumishi wa umma.
 
Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako, ambaye amekuwa akisisitiza uhakiki huo, amekuwa kimya katika suala la vyeti vya ofisa huyo.
 
Mteule huyo wa Rais aliingia katika sakata hilo baada ya kuwatuhumu na kuwangaza wanasiasa, viongozi wa dini, wasanii na wafanyabiashara kuhusika katika matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
 
Tangu tuhuma hizo zitolewe dhidi yake, hajawahi kukiri wala kukanusha.
 
Mjadala mwingine unaotarajiwa kuibukia wizara hiyo ni sera ya utoaji wa elimu bure. 

Hivi karibuni Taasisi ya Haki Elimu imetoa taarifa inayoonyesha changamoto za utoaji wa elimu bure ikionyesha mafanikio hafifu.
 
Mijadala itakayoibuka katika Wizara ya Elimu inaweza kufanana na mijadala itakayotokea Wizara ya Tamisemi inayosimamiwana George Simbachawene inayosimamia wakuu wa mikoa na wilaya.
 
Hii inatokana na wakuu hao kuwaweka ndani watendaji kwa makosa ya kinidhamu kinyume cha Sheria ya Utumishi wa Umma inayoeleza bayana mamlaka za kuchukua hatua dhidi ya watendaji.
 
Katika mijadala iliyoibuka awali, mbunge wa Muheza, Adadi Rajab alishauri wakuu wa mikoa na wilaya kuelimishwa kuhusu uchukuaji hatua na matumizi ya Sheria ya Tawala za Mikoa na Wilaya.
 
Adadi aliyewahi kuwa kamishna wa polisi na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), alisema suala la ukamataji ni taaluma inayosomewa.

Simbachawene pia ana kibarua cha kufafanua kuhusu changamoto za utoaji elimu bure.
 
Hali kama hiyo inaweza kuibuka katika bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo kwa sasa inaongozwa na Dk Harrison Mwakyembe.
 
Suala la waziri wa zamani, Nape Nnauye kutishiwa bastola na askari kanzu wakati akienda kuzungumza na waandishi wa habari linaweza kuibua mjadala wa uhuru wa habari na kujieleza.
 
Dk Mwakyembe ana kibarua kigumu cha kufafanua kuhusu kukamatwa na kutekwa kwa wanamuziki, na hasa Ibrahim Mussa maarufu kama Roma Mkatoliki.
 
Roma, akiwa na wasanii wenzake, walitekwa na watu wasiojulikana wakiwa katika studio ya Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam na baada ya siku mbili, walipatikana.
 
Habari za watu waliowateka na mazingira ya kuachiwa huru zimekuwa na utata na hakuna aliyeweka bayana hadi sasa.
 
Akichangia katika mjadala wa hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu wiki iliyopita, mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia alihoji sababu za Dk Mwakyembe kuhudhuria ambao Roma alikuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusu kutekwa kwake.
 
Hoja ya Nkamia aliyewahi kuwa naibu waziri wa wizara hiyo katika awamu ya nne, ilikuja huku baadhi ya wabunge wakiibana Serikali iwajibike kwa matukio ya utekaji.
 
Hata hivyo, Dk Mwakyembe alijibu hoja hiyo ya Nkamia kuwa alikuwa Maelezo kwa kuwa ndiyo ofisini kwake.
 
Kabla ya tukio hilo la Roma, Elibariki Emmanuel, maarufu kwa jina la Ney wa Mitego, alikamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kutoa wimbo wa “Wapo” unaoelezea kuwepo kwa watu tofauti, akiwemo kiongozi mwenye vyeti vya kughushi na kuhoji sababu za “mtumbua majibu” kutolitumbua “jipu jipya mjini”.
 
Hata hivyo, Rais Magufuli aliagiza aachiliwe na auboreshe wimbo wake kwa kuongeza watu wenye sifa nyingine. 

Katika muendelezo huo, matukio ya utekaji, ukamataji na mauaji dhidi ya viongozi wa vijiji, watendaji na askari wa Jeshi la Polisi, yanampa kibarua kigumu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba.
 
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete alimtaka Waziri Mwigulu kutoendelea kukalia kimya matukio ya utekaji, lakini siku chache baadaye polisi nane waliuawa katika shambulizi la aina yake lililotokea Kibiti mkoani Pwani.
 
Pia, Waziri Mwigulu atakuwa na kazi nzito kutokana na kutotolea tamko vitendo vya utangazaji na ukamataji wa raia vilivyofanywa na mteule wa Rais kwa kuwalenga watu maarufu, wakiwamo wanasiasa, wafanyabiashara na wasanii walitajwa.
 
Mbali na masuala ya usalama, hatua ya Rais Magufuli kukamata makontena ya mchanga wenye madini katika bandari ya Dar es Salaam, nalo linatarajiwa kuzua mjadala bungeni.
 
Mbali na kukamata mchanga huo, Rais Magufuli amemsimamisha kazi katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justine Ntalikwa saa chache baada ya kujibishana na ujumbe wa Spika Job Ndugai uliotembelea bandarini kushuhudia makontena yenye mchanga wa shaba.
 
Suala hilo lilishaanza kuibua mjadala kutokana na hatua ya kuzuia ghafla mchanga huo, inayoonekana inaweka mazingira yasiyo rafiki kwa wawekezaji ambao walishangia mikataba na Serikali kwa kutumia sheria za nchi.
 
Umoja wa wachimbaji wadogo uliiomba Serikali kuuachia mchanga huo kwa sababu unasafirishwa kwa kufuata utaratibu.
 
Tayari Rais Magufuli ameshaunda kamati mbili za wataalamu kuchunguza mchanga huo na kutoa mapendekezo.
 
Tangu mjadala wa mchanga huo uanze, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo hajatoa kauli yoyote

Mkatabawaziri : Dawa Asilia InayoTibu Na Kuponyesha Kabisa Maradhi Ya Bawaziri Kwa Namna Ya Kipekee.

$
0
0
Kutokwa  na  kinyama  ama  uvimbe  kwenye sehemu  ya  haja  kubwa  ni  tatizo  linalo  wakabili mamilioni  ya watu  duniani.
Tatizo  hujulikana  kwa  Kiswahili  kama  Bwaziri,  katika  lugha  za kisukuma  na  kinyamwezi  huitwa  “Man’gondi” na  katika  lugha  ya  kiingereza  hujulikana  kama  Hemorrhoids.

AINA  ZA  BAWAZIRI : Kwa mujibu  wa  tafiti mbalimbali  za  kitaalamu, zipo  bawaziri  za  aina  mbili, bawaziri  ya  ndani  na  bawaziri  ya  nje. Kwa  kawaida  mtu  huweza  kuwa  na  moja  wapo kati  ya  aina  hizo   na  wakati  mwingine, mtu  mmoja  anaweza  kuwa  na  bawaziri  za  aina  zote  mbili  kwa  wakati  mmoja.

NINI  HUSABABISHA  BAWAZIRI ?

Mpaka   sasa  wataalamu  bado  hawaja  baini  chanzo  halisi  cha  tatizo  la  bawaziri. Hata  hivyo  tafiti  mbalimbali za  kitaalamu  zinabainisha  mambo  kadhaa  yanayo  changia  kutokea  kwa  tatizo  la  bawaziri.
Mambo  hayo  ni  pamoja  na :

i. Kukosa  choo  kwa  muda  mrefu
ii. Kuharisha  kwa  muda  mrefu
iii.Kukaa  kwenye  choo  kwa  muda  mrefu
iv. Kukaa  kwa  muda  mrefu
v. Unene  na  uzito  kupita  kiasi: Tafiti  mbalimbali  zina onyesha  kuwa, asilimia  kubwa  ya  watu wenye  tatizo  la  unene  na  uzito  ulio zidi, huwa  katika  hatari  kubwa  ya  kupatwa  na  tatizo  la  bawaziri.

vi. Ujauzito :  Tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu  zinaonyesha  kuwa, asilimia  kubwa  ya  wanawake  wajawazito  huwa  katika  hatari  ya  kupatwa  na  tatizo  la  bawaziri, sababu  ikiwa  ni  kuongezeka  kwa  shinikizo  ndani  ya  mfuko  wa  uzazi.

vii. Kutofanya  mazoezi  kwa  muda  mrefu

viii. Kutotumia  vyakula  vyenye  nyuzi nyuzi

ix. Sababu za  kinasaba : Tafiti  zinaonyesha  kuwa, wapo  watu wanao  patwa  na  bawaziri, kwa  sababu  za  kijenetiki

NINI  DALILI  ZA  BAWAZIRI ?
Dalili  kuu  za  bawaziri  ni  pamoja  na  kutokwa  na  kinyama  ama  uvimbe  kwenye  sehemu  ya  haja  kubwa, kukosa  choo, kupatwa  maumivu makali  sana  wakati  wa  kujisaidia  au wakati  unatembea  na  wakati  mwingine  maumivu  huendelea  hata  ukiwa haupo katika  matendo  yaliyo tajwa   hapo  juu. Dalili  nyingine  ni  pamoja na  kuhara  damu  ama  kutoa  kinyesi  chenye  damu.

JINSI  YA  KUJIKINGA  USIPATWE  NA  BAWAZIRI :
Kujikinga  usipatwe  na  bawaziri, unashauriwa
i. Kujenga  tabia  ya  kuwa  unakula  vyakula vyenye  nyuzi nyuzi ( fibre) kwa wingi
ii. kula  matunda  kwa wingi
iii. Kunywa  maji mengi
iv. Fanya  mazoezi  ya  mwili  mara  kwa  mara
v. Usikae   maliwatoni kwa  muda  mrefu
vi. Usiruhusu  unene  na  uzito  kubwa.

TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  LA  BAWAZIRI :
Zipo  dawa   mbalimbali  za  asilia  ambazo  zina  tibu  na  kuponyesha  kabisa  maradhi  ya  bawaziri.  Baadhi  ya dawa  hizo  ni  pamoja  na Lufwambo  ama Ufwambo,  Mkomavikali, Nun’ganun’ga  au  Mchicha  Pori,  Zumanguku, Luwawa  na  Mkatabawaziri.

Kati  ya  dawa  zilizo  orodheshwa  hapo  juu, dawa  ya  Mkatabwaziri inakubalika  zaidi  kwa  sababu  kuu  mbili, kwanza  ni  ufanisi  wake  katika kutibu  maradhi  ya  bawaziri  na  pili  ni  namna inavyo  tumika  katika  tiba  ya  bawaziri.

Wakati  dawa  nyingine  za  kutibu  maradhi  ya  bawaziri, zinatumika  kwa  mgonjwa  kunywa  au  kupaka.  Mkatabawaziri  yenyewe  inatumika  kwa  namna  ya  kipekee  sana.

JINSI  MKATABAWAZIRI  INAVYO  TUMIKA  KATIKA  TIBA  YA  MARADHI  YA  BAWAZIRI.
Mgonjwa  anatumia  kunywa  halafu  anatumia  kujifukiza  mvuke  wa dawa  ya  mkatabawaziri.  Katika  kujifukiza, dawa  hii  huchemshwa  kisha  huwekwa  kwenye  ndoo halafu  mgonjwa  anakalia  juu  ya  ndoo  ili  mvuke  wa  dawa  hii  uweze  kufika  kwenye  sehemu  iliyo  athirika  ( sehemu  yenye  bawaziri ).

Zoezi  hili  hufanyika  mara  mbili  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  ishirini  na  moja   mfululizo.

Ufanisi  wa  tiba  hii  ni  mkubwa  sana. Mgonjwa  huanza  kuona  mabadiliko  ndani  ya  siku  saba  na  baada  ya  siku  ishirini  na  moja  tatizo  la  bawaziri  linakuwa  limekwisha  kabisa  na  mgonjwa  anakuwa  amepona  kabisa  tatizo  la  bawaziri.

Tiba  hii  imemsaidia  na  kumponyesha  kila  alie  itumia. Kama  umesumbuliwa  na  maradhi  ya  bawaziri  kwa  muda  mrefu  na  umehanganika  kutafuta  tiba  bila  mafanikio, basi  jaribu  kutumia  tiba  ya  Mkatabawaziri, ili uweze  kuondokana  na mateso  ya  tatizo  la  bawaziri.

JINSI  DAWA  ASILIA  YA  MKATABAWAZIRI  INAVYO PATIKANA.

Kupata  dawa  ya  Mkatabawaziri, fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST.
 
TUNAPATIKANA UBUNGO  JIJINI  DAR  ES SALAAM,  JIRANI  NA  SHULE YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING, NYUMA  YA JENGO  LA  UBUNGO  PLAZA.
 
Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766  53 83  84.

Kwa  wateja  waliopo  jijini  Dar  Es  Salaam, ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  dukani kwetu  Ubungo, tunayo  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  walipo  ( HOME & OFFICE  DELIVERY )
Kwa wateja  waliopo  mikoani , tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  mabasi  mbalimbali.

Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti.
 
Kwa  wateja  waliopo  NAIROBI na  MOMBASA , tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  usafiri wa  magari mbalimbali.
 
Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

Na  kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  tiba mbalimbali  za  asili, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu:
 

Je, Umeathiriwa na Punyeto Kiasi cha Kushindwa Kurudia Tendo la Ndoa???.....Bofya Hapa Kupata Tiba, Pia Tuna Handsome Up ya Kuongeza Maumbile

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETIC ni kampuni inayotoa bidhaa ORIGINAL zenye matokeo mazuri bila kemiko wala madhara yoyote. Pata punguzo la bei kwa bidhaa hizi. 
 
1.HANDSOME UP ni kifaa kinachoongeza maumbile ya kiume  kwa 99% kwa size uipendayo wewe na kuimarisha misuli ya uume kwa @170,000/= tuu. 
 
2.MEN GELY kupaka. Hii inaongeza kwa wastani wa inch 6.5 na inapatikana kwa @120,000/=.  
 
3. MAX MAN 2. Ni vidonge kwa ajili ya nguvu ambavyo vinasaidia sana hata kwa watu wenye kisukari na waliokua wakifanya sana masturbation. Pia huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa @130,000/=tu.     
 
Tupo DAR ES SALAAM  kariakoo na kinondoni kanisani.

Kwa mawasiliano zaidi piga  0759029968 au 0659618585.
Popote ulipo utapata huduma zetu.
 
Follow us
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
 
     Bidhaa zetu zote ni garantii na unapewa risiti
              Karibu

Jeshi la Magereza Lajitosa Kujenga Viwanda Vya Sukari na Viatu

$
0
0
Wakati Taifa likijielekeza kwenye ujenzi wa Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati, Jeshi la Magereza nchini linatarajia kujenga upya kiwanda chake cha viatu cha Karanga na kuanzisha kiwanda kipya cha sukari katika Gereza la Mbigiri mkoani hapa.
 
Awali, Kiwanda cha Karanga kilichopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kilishindwa kuendelezwa.
 
Ili kufanikisha hilo, tayari Shule ya Sekondari ya Bwawani inayomilikiwa na jeshi hilo imeanzisha mtalaa wa masomo ya sayansi ili kuandaa vijana wa kufanya kazi viwandani. 

Kamishna wa Utawala na Fedha wa Magereza, Gaston Sanga alisema mikakati hiyo inalenga kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kutilia mkazo ukuaji wa uchumi kupitia viwanda.
 
Alisema taaluma inayotolewa shuleni hapo itakwenda sambamba na mahitaji ya wataalamu watakaotumika katika viwanda hivyo.
 
“Tumeona tuanzishe mchepuo wa masomo ya Sayansi yaani CBG (Kemia, Bailojia na Jiografia) kuanzia mwakani katika shule yetu ya Bwawani,” alisema kamishna huyo.
 
Alifafanua kuwa wameanzisha masomo hayo ili kupata wataalamu wengi watakaovisaidia viwanda vya jeshi na vingine vilivyopo nchini.
 
Kamishna Sanga alisema katika kuimarisha na kujenga upya kiwanda cha viatu na kile cha sukari, wanashirikiana na mifuko ya hifadhi za jamii ya PPF na NSSF.
 
Kuhusu Shule ya Sekondari ya Bwawani, alisema maendeleo ya kitaaluma yanategemea miundombinu ya madarasa, maabara, maktaba na ubora wa afya ya mwanafunzi.
 
Alipongeza jitihada zinazofanywa za kukamilisha kuendeleza miradi mbalimbali katika shule hiyo ili kuboresha maendeleo ya kitaaluma.
 
Pia, alisema ni vyema wazazi wawe mstari wa mbele kulipa ada kwa wakati ili kuwaruhusu wanafunzi kurudi shule mapema na walimu waweze kwenda sambamba na mitalaa iliyopo.
 
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga ambaye pia ni mkuu wa sekondari ya Bwawani, alisema pamoja na jitihada za ujenzi wa nyumba mbili za walimu kwa mfumo wa kujitolea na madarasa mawili, bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa jengo la utawala na nyumba za watumishi.

Habari ya Waziri Mwakyembe Yaliponza Gazeti la Mwanahalsi

$
0
0
Katika toleo namba 387 la Jumatatu April 17-23, 2017 gazeti la MwanaHalisi katika ukurasa wake wa kwanza lina habari isemayo:“Mwakyembe: Maisha Yangu Yako Hatarini.”  

Habari hiyo inadai kuwa Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hayuko huru na maisha yake bado yapo hatarini, taarifa ambayo imemshtua na kumhuzunisha sana Waziri kwa uzushi, ulaghai na uzandiki uliopitiliza.
 
Mwandishi wa habari hiyo amedai kufanya mahojiano na Dkt. Mwakyembe nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma Alhamisi iliyopita, na amenukuu kile anachodai ni Waziri kueleza wasiwasi kuhusu usalama wa maisha yake, kitu ambacho hakikutokea.
 
Tunapenda kuutaarifu umma kuwa, habari hiyo ni ya uongo na ya kutunga. Mhe. Dkt. Mwakyembe hajafanya mahojiano yoyote na mwandishi yeyote katika siku na mahali palipotajwa sembuse mwandishi husika wa gazeti la MwanaHalisi ambalo Mhe. Mwakyembe ana kesi nalo Mahakama Kuu kwa kumzushia habari za uongo alipokuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
 
Wakati Serikali ikitafakari hatua za kuchukua kwa uandishi wa aina hii, tasnia ya habari inaendelea kukumbushwa kuzingatia weledi na maadili hasa wakati huu ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya 2016, tasnia ya habari imepewa hadhi ya kuwa taaluma kamili.


Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime

$
0
0
MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara, amewataka wanachi wilayani Tarime, kuachana na uwindaji haramu, badala yake watumie fursa zilizopo kukuza vipato vyao iii kuondokana na umasikini katika ngazi ya familia. 

Pia, amewataka wananchi hao watumie fursa hizo kuwekeza katikamiradi na biashara mbalimbali katika maeneo jirani na Hifadhi ya Mbuga ya Serengeti, itakayowawezesha kuwaingizia vipato. 

Waitara alitoa wito huo mjini Tarime, juzi, alipokutana na baadhi ya wananchi na kubadilishana nao mawazo, wakati akielekea nyumbani kwake kijiji cha  Itiryo kusherekea sikukuu ya Pasaka. 

Alitoa ushauri kwa watu wenye nia ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ya uzalishaji mali wilayani humo, watumie nafasi hiyo iii kukuza na kuendeleza mji waTarime na wilaya hiyo kwa ujumla.
 
Alisema awali, wilaya hiyo ilikuwa na sifa mbaya nchini na kimataifa, kutokana na kuzuka kwa mapigano ya koo za makabila ya Wakurya na Waluo, yaliyochochewa na wizi wa mifugo. 

Waitara alisema ipo haja kwa jamii inayoishi kando ya Hifadhi ya Serengeti, kuthamini rasilimali za wanyamapori kuwa ni miongoni mwa tunu za taifa na hakuna budi kuzitunza na kuzilinda kwa ajili vizazi vya sasa na vijavyo. 

"Ni muhimu jamii yetu itambue kuwa, wanyama waliopo ni wetu kwa faida yetu na taifa la leo na vizazvijavyo. Kuendekeza uwindaji haramu kunasababisha hasara kubwa dhidi ya rasilimali hiyo, hivyo ni muhimu jamii yetu ikatumia fursa zilizopo katika utalii ili kunufaika nazo," alisema. 

Kuhusu miradi ya kijamii inayoibuliwa na vijiji na kisha kupitishwa na kamati za maendeleo za kata, kama vipaumbele vyao vya kutekelezwa na Hifadhi ya Mbuga ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), alisema utekelezaji wake utasubiri kutokana na bajeti ya hifadhi hiyo.

Mauaji ya polisi yamtoa machozi mhubiri kanisani

$
0
0
MHUBIRI wa Kanisa la IEACT lililoko Manispaa ya Shinyanga, Eliamani Kisanaga, amebubujikwa na machozi kutokana na vitendo vya kinyama vinavyoendelea hapa nchini vya kuuawakwa polisi.

Kutokana na hali hiyo, aliwashauri Watanzania kumrudia Mungu kwa kuishi kwa kupendana kama alivyoagiza katika vitabu vitakatifu. Mhubiri huyo alitokwa na machozi wakati wa Misa ya Pasaka, iliyofanyika juzi, kwenye kanisa hilo. Pia alitumiafursa hiyo kuwaaga waumini wa kanisa hilo kuwa anahama. 

"Tuishi kama Kristu kwa kuiga matendo yake, tusijiite Wakristu tu bila matendo, huko ni kujidanganya kwani hakuna kitabu kinachohubiri kuua, hiyo ni njia ya shetani. Tunakokwenda Watanzania wenzagu ni kwenye laana,"alisema. 

Aliongeza: "Nchi yetu katika sura ya kimataifa, tulikuwa na sura nzuri ya amani na upendo, lakini ghafla yakaanza mauaji ya vikongwe, mauaji ya walemavu wa ngozi, dawa za kulevya na leo tunaua askari wetu wanaotulinda, tunakwenda wapi?" 

Pia, aliwataka Wakristo kuishimaisha mema na kuwa mfano kwa watu wengine ambao si wakristo

Mchungaji Amfananisha Rais Magufuli na Nabii Mussa

$
0
0
RAIS Dk. Jonh Magufuli amefananishwa na Nabii Mussa wa kwenye Biblia, aliyekuja kuwaokomboa wana wa Israel kutoka Misri. 

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mchungaji wa Kanisa la IEACT la mjini Shinyanga, David Mabushi, alipokuwa akizungumza na mwandishi, baada ya Misa ya Pasaka, alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu mustakabali wa taifa. 

"Mimi na kanisa langu tunamuunga mkono kwa kazi zote anazofanya kwa kusaidia rasilimali zote za nchi hii ill ziwanufaishe Watanzania. Huyu ni kama Mussa aliyekuja kuwakomboa wana wa Waisraeli," alisema Mabushi. 

Alisema miongoni mwa mambo, ambayo Watanzania walikuwa wanalalamikia ni mikataba ya migodi na mchanga unaosombwa kupelekwa nje ya nchi, ambayo kwa sasa yameanza kushughulikiwa. 

"Hivi sasa kazuia na kuunda tume mbili. Moja ya wataalamu wa kujua kilichomo ndani ya mchanga na nyingine ina wachumi na wanasheria watakaoangalia mikataba inasema nini," alisema. 

Pia, aliwakumbusha Watanzania kauli ya Baba wa Taifa, aliyoitoa siku za nyuma kuwa, mali ya nchi hii haiozi, ataiweka mpaka wasomi waje. 

Hata hivyo, mchungaji huyo alielezea kusikitishwa kwake na kushuka kwa maadili ya watoto wanaotumia mitandao kuangalia mambo machafu, badala ya kuitumia kujifunza. 

Kuhusu mauaji ya askari, alisema anaungana na serikali kulaani mauaji hayo. 

"Naiomba serikali itunishe misuli na kuhakikisha wale wote waliohusika na mauaji hayo, wanapatikana na kufikishwa mahali panapohusika," alisema.

Askari wa JWTZ auawa kwa kuchomwa visu na vibaka

$
0
0
ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), MT 94293, aliyefahamika kwa jina la Tekeli Israel (29), ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani na watu wanaodaiwa kuwa ni vibaka. 

Akithibitisha kuuawa kwa askari huyo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa nne usiku, wakati marehemu, ambaye ni mkazi wa Mbaunda, alipokuwa akitoka kula chips. 

Alisema marehemu wakati akitoka baa ya Tarakea kwenda nyumbani kwake, alipofika eneo la Tarakea Super Car Wash, mtaa wa Simanjiro, kata ya Sombetini, asikia kelele za mtu akiomba msaada. 

Kamanda Mkumbo alisema mtu aliyekuwa anapiga kelele za kuomba msaada alifahamika kwa jina la Tumkislai Abdallah, ambaye alikuwa akiporwa simu ya kiganjani na vibaka. 

"Baada ya marehemu kufika eneo la tukio na kubaini kuwa ni vibaka, aliamua kupambana nao, lakini kwa bahati mbaya walimjeruhi kwa visu na mmoja wao alimchoma nacho kifuani,"alisema. 

Kwa mujibu wa Kamanda Mkumbo, wananchi kwa kushirikiana na polisi, walifanikiwa kumtia mbaroni kibaka mmoja, aliyefahamika kwa jina la Dickson Moses(19), maarufu kwa jina la 'Tukai', mkazi wa Olmatejoo, ambaye alimchoma kisu marehemu. 

Alisema baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na polisi, aliwataja wenzake watatu, ambao walifanikiwa kutoroka na kwamba, polisi wanawasaka popote pale walipo. 

"Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linawataka watuhumiwa watatu, ambao majina yao tunayo, waliokuwa na Tukai kwenye tukio la mauaji ya mwanajeshi huyo, kujisalimisha mara moja kwani mkono wa serikali ni mrefu utawatia nguvuni popote pale walipo," alisisitiza. 

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Ally Omaiy, alisema walimuona marehemu kwenye baa ya Tarakea, ambako alikula chispi kisha akaondoka. 

Alisema dakika chache baadaye, walisikia kelele za mtu anaomba msaada na baada ya kufika eneo la tukio, walimkuta marehemu akipambana na vibaka hao na ghafla walimuona ameanguka chini. 

Alisema baada ya kuanguka, vibaka hao walianza kukimbia, lakini wananchi kwa kushirikiana na madereva wa bodaboda, waliwakimbiza na kufanikiwa kumkamata mmoja wao. 

"Marehemu alipambana na vibaka hao kwa ajili ya kumsaidia Abdallah asiporwe simu, lakini kwa kuwa vibaka walikuwa wanne, walimzidi nguvu na mmoja alifanikiwa kumchoma marehemu kisu cha kifuani na kufariki dunia," alisema. 

Shuhuda mwingine, ambaye ni rafiki wa karibu wa marehemu (Jina linahifadhiwa), alisema marehemu alikuwa anajiandaa kwa ajili ya safari ya kwenda Darfur. 

"Marehemu alikuwa rafiki yangu wa karibu, tunaishi jirani hapa Mbauda, tulishirikiana kwa mambo mengi, licha ya mimi kuwa raia wa kawaida na aliniambia ameshakamilisha taratibu zote za kikosini na kwamba, alikuwa anajiandaa kwa ajili ya kwenda Darfur," alisema. 

Mwili wa marehemu Israel, umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hosptali ya Mkoa ya Mount Meru, ukisubiri taratibu za kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Mbeya kwa maziko.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Agundua Madudu 5 Mirandi ya Ujenzi NSSF

$
0
0
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini kasoro katika mambo matano baada ya kufanya ukaguzi wa hesabu za Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Ripoti ya CAG imekuja wakati wakurugenzi sita, mameneja watano na mhandisi mmoja wakiwa wamesimamishwa kazi tangu Julai mwaka jana kupisha uchunguzi.
 
Ripoti hiyo iliwasilishwa bungeni Aprili 13 mwaka huu, ikiwa ni siku chache tangu CAG, Profesa Mussa Assad aikabidhi kwa Rais John Magufuli.
 
Kasoro zilizobainika katika mfuko huo ni kiwango cha chini cha ukaliwaji wa majengo, usimamizi na udhibiti wa mikopo ya vyama vya ushirika vya akiba na mikopo, udhaifu katika uwekezaji wa ardhi.
 
Ripoti hiyo inabainisha kasoro katika Shamba la Dungu na mradi wa uwekezaji Tuangoma na kasoro nyingine ni katika mkataba wa mshauri katika ununuaji wa Pan Africa Energy Limited kwa Sh551.61 milioni.
 
Ripoti inaonyesha kuwa NSSF imewekeza kwa kiasi kikubwa katika majengo ya kupangisha kwa wateja kama vile hoteli, kampuni, watu binafsi na kutumia sehemu nyingine ya majengo hayo kama ofisi zake.
 
Imegundulika kuwa, kiwango cha upangaji katika majengo tisa ya uwekezaji kilikuwa chini ya kusudio la kiwango cha soko cha asilimia 80. Ripoti inaonyesha kuwa kiwango cha upangaji kilikuwa kati ya asilimia 0 na 43.
 
Rasilimali hizo za uwekezaji katika majengo zinajumuisha hoteli ya Mwanza, Kigoma, jengo jipya la biashara la Old Moshi -Arusha, jengo jipya la biashara la Kaloleni (Arusha), jengo jipya (Kahama), Njiro (Arusha), jengo kubwa la kibiashara Kilimanjaro, Mafao House (Ilala) na jengo kubwa la kibiashara la Morogoro.
 
Mbali na hali hiyo CAG amebaini kuwa NSSF ilisimamisha kutoa mikopo kwa wanachama wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo Juni, 2016 ili kuimarisha usimamizi na kuhakikisha kuwa kuna ukusanyaji wa marejesho ya mikopo.
 
Hata hivyo, mikopo iliyotolewa kabla ya kusimamisha utoaji, ilikuwa na mapungufu ikiwamo mikopo ya Sh1 bilioni iliyotolewa kwa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo zaidi ya kiwango cha ukomo.
 
Ripoti inaonyesha NSSF ilitoa Sh21.3 bilioni kwa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Bunge (National Assembly Saccos) na Sh2.2 bilioni kwa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Jumuiya ya Ndugumbi (Ndugumbi Community Saccos).
 
Utoaji huo wa mikopo ulizidi kiwango cha ukomo kwa Sh1 bilioni, lakini menejimenti ya NSSF ilieleza kwamba mikopo kwa wanachama wa Bunge ilitolewa kama mpango maalum wa kuvutia wanachama wapya kwenye mfuko.
 
Pia, kuna vyama vya ushirika vya akiba na mikopo vilivyopewa zaidi ya asilimia 50 ya mali zote ilizonazo.
 
Pia, CAG ameeleza kuwa ushuru wa stempu ulikuwa haujalipwa kwa vyama vinne vya ushirika ambavyo vilipewa mikopo.
 
Vyama hivyo ni Masoko Madogo Madogo ambacho hakijalipa Sh500 milioni, Ngima (Sh500 milioni), Mafanikio (Sh490 milioni) na Mount Meru (Sh260 milioni).
 
Udhaifu uliogundulika kwenye Uwekezaji wa Ardhi
Kwa mujibu wa CAG, taarifa za fedha za NSSF zilionyesha kuwa iliwekeza kwenye viwanja (Benki ya Ardhi) kwa thamani ya Sh97.2 bilioni, lakini imebainika kuwepo na mapungufu katika ununuaji na uwepo wa ardhi zilizonunuliwa.
 
Ripoti inaonyesha kulikuwa hakuna mipango na upembuzi yakinifu kuhalalisha sababu za kuwekeza katika rasilimali kinyume na aya ya 3.3 ya Sera ya Uwekezaji ya NSSF ya mwaka 2012 inayolitaka shirika hilo kuwekeza rasilimali zake katika miradi inayolipa zaidi ili kuweza kunufaisha wanachama wake.

“Sikuweza kupata hati ya umiliki ya viwanja/mashamba vinne kwa sababu vipo katika mzozo wa umiliki.  Viwanja hivi vilikuwa ni Nunge Beach kilichopo Bagamoyo chenye ukubwa ekari 67.35, kiwanja namba 146/4 Barabara ya Old Moshi kilichopo Halmashauri ya jiji Arusha, Clement Mabina Farm Bugando Magu na kiwanja namba 98 Barabara ya Nyerere (Pugu) Temeke chenye mita za mraba 8,825,” inaeleza ripoti ya CAG.
 
Ripoti hiyo inaeleza kuwa mfuko uliingia mkataba na Halmashauri ya jiji la Mwanza kwa ajili ya kununua viwanja 692 (viwanja 405 eneo la Kiseke na 287 Bugarika) kwa Sh1.89 bilioni.
 
Hata hivyo, ni viwanja 156 tu vilielekezwa Kiseke; wakati hakuna kilichoelekezwa upande wa Bugarika.
 
Pia, imesema kulikuwa na shamba namba 113 lililonunuliwa kwa Sh1.26 bilioni lililopo Mapinga, katika Manispaa ya Kinondoni lenye ukubwa wa hekta 127, lakini ni hekta 58 tu zilizokuwa zimetengwa na kufanyiwa kazi.
 
Ununuaji Pan Africa Energy
Dosari nyingine katika ripoti hiyo ni mkataba wa NSSF na Yakubu and Associates Chambers uliosainiwa Februari 12, 2016 kwa lengo la kutoa huduma ya ushauri ili kuwezesha kupatikana kwa mshirika Kampuni ya Pan Africa Energy Limited kwa ada ya utaalamu ya Sh551.61 milioni kwa ajili ya matumizi ya ziada na kodi za ndani.
 
Ripoti hiyo inaeleza mshauri huyo hakuwa na uzoefu uliohitajika kama ilivyoelekezwa kwenye hadidu za rejea iliyohitaji uzoefu wa mali zisizohamishika za ndani na mambo ya mazingira, ushauri wa kodi za ndani na nje na leseni na kanuni za mfumo wa hydrocarbon.
 
Pia, iligundulika kuwa Kampuni ya Yakubu and Associates Chamber ndiyo iliyokuwa imesajaliwa mwaka huohuo wa kukaribisha zabuni na hivyo washauri hawakuwa na uzoefu na mazingira ya ndani.
 
Mshauri alitakiwa kukagua taarifa ya uchunguzi iliyoandaliwa chini ya mkataba namba NSSF/CS/20/2014-2015 ulioingiwa Desemba 11, 2014 kwa ajili ya kutoa huduma ya ushauri katika ununuzi wa Kampuni ya Pan Africa Energy Limited. 
 
Kanuni iliyotumika ambayo ni namba 257(2)(a) ya Kanuni za Manunuzi ya Umma ya mwaka 2013 (PPR, 2013), haikuwa sahihi.
 
Mkataba ulikuwa umeisha muda wake tangu Aprili 26, 2016, lakini uliongezwa muda kupitia kanuni namba 111(1) ya Kanuni za Manunuzi ya Umma ya mwaka 2013 (PPR, 2013) inayomruhusu ofisa masuuli kuongeza muda wa mkataba na kuelezea sababu ya kufanya hivyo.
 
Ripoti ya CAG inasema mshauri aliwasilisha bili namba 01031604 ya Machi 1, 2016, lakini mpaka kufikia Oktoba 7, 2016 malipo yalikuwa hayajafanyika.
 
Kutokana na kasoro hizo, CAG ameeleza kuwa NSSF haikufuata vigezo vya kuchagua mshauri kama vilivyoainishwa kwenye Kanuni za Manunuzi ya Umma na Hadidu za Rejea (ToR) zilizoandaliwa na Bodi ya Wadhamini.
 
Pia, ameishauri menejimenti ya mfuko huo kuvunja au kusimamisha mkataba kwa kuwa mshauri hakuwa na uzoefu wa kutosha kufanya kazi hiyo.
 
Shamba la Dungu, Tuangoma 
Ripoti ya CAG inaeleza kuwa NSSF iliingia mikataba yenye thamani ya Sh165.4 bilioni kwa ajili ujenzi wa kijiji cha kisasa katika shamba la Dungu na Tuangoma Kigamboni katika Manispaa ya Temeke Dar es Salaam. Mfuko ulikuwa umeshaingia gharama ya Sh73.4 bilioni.
 
CAG anaeleza kuwa miradi ya mfuko huo ilitekelezwa bila kufanya upembuzi yakinifu ambao ungeipa menejimenti uhakika wa uwekezaji. Kwa sababu hiyo CAG ameshindwa kupata misingi na vigezo vilivyoshawishi maamuzi ya menejimenti kuwekeza, malengo ya uwekezaji na mipango ya kurudisha fedha zilizowekezwa.
 
Kutokana na hali hiyo, NSSF iligundua kuwa sehemu ya ardhi ya shamba la Dungu ilikuwa inamilikiwa na Shirika la Nyumba Taifa (NHC), hivyo baadhi ya ujenzi ulihamishiwa Tuangoma.
 
Hata hivyo, menejimenti haikuweza kutoa nyaraka za ununuzi wa viwanja vya Tuangoma na kama vilikuwa vina ukubwa sawa, vinauzika kwenye soko na kiwango cha kurudisha uwekezaji kama ilivyo kwa Dungu.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Aibua Ubadhirifu wa Kutisha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

$
0
0
UBADHIRIFU wa kutisha unaohusisha mabilioni ya fedha, umefichuliwa kwenye Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ukihusisha uongozi, wafanyakazi, watoa huduma na wazabuni. 

Wanaodaiwa kuhusika na utafunaji wa mabilioni hayo, walitumia mabadiliko mapya ya usajili wa vitambulisho, yaliyoigharimu serikali kupitia manunuzi yasiyo na tija huku wadanganyifu wakitumia mianya iliyopo kujinufaisha wenyewe kinyume na taratibu. 

Kutokana na hali hiyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad, aliagiza wale vote waliohusika na ubadhirifu na udanganyifu wa mabilioni ya fedha, wachukulie hatua kali. 

"Ukaguzi umejiridhisha kwamba, uongozi, wafanyakazi, watoa huduma na wazabuni wameshiriki kwa namnamoja au nyingine katika ubadhirifu na udanganyifu kwenye matumizi ya fedha katika mradi wa kuboresha vitambulisho vya taifa,"alisema.
 
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)    imeonesha ubadhirifu katika eneo la usajili na utambuzi ambako Sh bilioni 1.2 zililipwa kwa huduma za bima kupitia dalali wa Bima M/s Aste Insurance Brokers Company Limited. Kiasi hicho kililipwa zaidi ya gharama halisi isivyostahili.

Huduma hizi zilipaswa kugharimu Sh milioni 450.2, lakini mamlaka ililipa Sh bilioni 1.7. CAG alibaini kuwa dalali huyo wa bima, alitumia akaunti za biashara katika kupokelea fedha za malipo ya bima ya Sh bilioni 1.7 badala ya akaunti ya amana isivyostahili.

Kwa hali hiyo, CAG amependekeza kampuni ya uwakala wa bima irejeshe Sh bilioni 1.2 zilizolipwa zaidi isivyostahili; na hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya Astery Ndege na kampuni hii kwa kufanya udanganyifu na kujipatia fedha kutoka mamlaka. 

Ubadhirifu mwingine alioutaja ulikuwa ni manunuzi ya bima ya vifaa vya usajili na magari yaliyotumika katika mradi wa vitambulisho vya Taifa ya jumla ya Sh milioni 494, yaliyofanyika bila kukihusisha Kitengo cha Manunuzi.

CAG pia ameshauri hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya watumishi waliohusika katika udanganyifu, uliobainishwa na kutozingatia sheria za manunuzi ya umma na kuisababishia Mamlaka gharama zisizo na tija sanjari na kuhakikisha kuwa wahusika wanafidia hasara iliyopatikana, kisha kuhakikisha udhibiti wa vifaa. 

Uhakiki wa leja za mafuta, pia ulibaini kuwa lita 1,110 za mafuta ya dizeli yenye thamani Sh milioni 2.2 zilitumika kwa shughuli zisizo za Mamlaka.

Pia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilikopa Sh milioni 455.3 kutoka NIDA kwa ununuzi wa magari manne mwaka 2014, ambazo hadi ukaguzi unafanyika Oktoba 2016 fedha hizo hazikuwa zimerejeshwa. 

Uhakiki wa fomu zenye ‘Barcode’ zilizotengenezwa kupitia mpiga chapa binafsi M/s MFI Solution, ulibaini kuwa fomu 7,762,907 zenye thamani ya Sh bilioni 2.5 zilizopokelewa na mamlaka hazikutumika.

Kadhalika, ilibainika kuwa fomu 8,220,000 zenye thamani ya Sh milioni 519.6 zilizochapishwa tangu mwaka 2011/2012 hadi 2013/2014 hazikutumika; hivyo kutelekezwa katika stoo za TANITA. 

“Hali hii ilitokana na mamlaka kutokuwa na Mpangokazi, hivyo kuingia hasara ya Sh milioni 932.8,” ilisema ripoti hiyo.

Matengenezo ya magari 
Aidha, kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 mpaka 2015/2016, Mamlaka ilifanya matengenezo ya magari kupitia gereji binafsi yaliyogharimu Sh bilioni 1.3. 

Nida pia ilifanya matengenezo yaliyogharimu Sh bilioni 1.1 yaliyofanyika na kulipwa na Mamlaka bila kufanyika ukaguzi unaothibitisha kuwapo kwa ubovu wa gari na mahitaji ya matengenezo husika.

Pia kulikuwa na matengenezo yaliyogharimu Sh milioni 197.2, yaliyofanyika na kulipiwa na Mamlaka bila kufanyika ukaguzi wa awali wala ukaguzi baada ya matengenezo.

 Ripoti imeeleza kuwa ukaguzi ulibaini malipo ya Sh milioni 42.7 yalifanyika zaidi ya madai stahili kutokana na udanganyifu wa kuongeza tarakimu katika hati za madai na kutumiwa kwa hati moja ya madai zaidi ya mara moja katika malipo ya kuanzia mwaka 2012/2013 hadi 2015/2016.

Ajira za muda na za kudumu 
NIDA imegundulika kuwa ilikiuka sheria katika ajira za muda na za kudumu, zilizofanywa na mamlaka kuanzia mwaka 2012 hadi 2015, ambapo vibarua 1,071 walipatikana kwa kupigiwa simu bila kutangaza mahali popote kinyume na Sera ya mamlaka hiyo. Ukaguzi ulibaini kuwa NIDA iliomba kupatiwa vibarua kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Chuo cha Utumishi wa Umma wapatao 415.

Lakini baada ya kupatiwa vibarua hao, mamlaka haikuwatumia na kubainisha kwamba wangetumiwa siku za baadaye. Ripoti ilifafanua kuwa mamlaka iliamua kuajiri vibarua wengine wapatao 882 bila kutangaza mahali popote, tofauti na watumishi 415 ambao walikwishapatiwa. Pia Septemba 2015 Mamlaka iliajiri watumishi 213 licha ya kibali cha kuajiri kutoka Utumishi kuisha tarehe Aprili 2015.

NIDA pia inatuhumiwa kufanya malipo Sh milioni 16.6 ya kiinua mgongo kwa vibarua, kinyume na mkataba wa ajira ya muda na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004. 

Ubadhirifu mwingine uligundulika kwenye matumizi ya mafuta ya dizeli na petroli, yaliyonunuliwa na mamlaka yenye thamani ya Sh bilioni 2.3, yaliyotolewa kwenye magari na majenereta, ambapo hayakuthibitika matumizi yake kutokana na sababu mbalimbali.

CAG pia amebaini upotevu wa vifaa vyenye Thamani ya Sh milioni 93.7 katika stoo ya mamlaka. Ukaguzi umebaini kuwa hakukuwa na taarifa rasmi kutoka kwa mtunza stoo juu ya upotevu huo, licha ya kufahamu kuhusu upotevu wa vifaa hivyo. Vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 991.4 havikutumika tangu kununuliwa kwake katika vipindi tofauti kuanzia Machi 2013 hadi Oktoba 2016.

Udanganyifu mwingine ulifanyika katika ushindanishi wa wazabuni katika ununuzi wa vifaa vya TEHAMA. Nida ilifanya manunuzi ya Ipad zenye thamani Sh milioni 63.4 zilizonunuliwa kutoka kwa M/s Elite computers baada ya kuonekana kukidhi vigezo vya ushindani na kupewa zabuni saba (7) tofauti. Lakini taarifa za wazabuni ambao waliainishwa kuwa washindani katika zabuni hii, M/s Prudent Enterprise na M/s Morex General Enterprise zilighushiwa; na wazabuni hawa hawakuhusishwa wala kutoa nukuu za bei.

Upangishaji nyumba Mamlaka ilitoa zabuni ya kuipangisha Ofisi ya Mamlaka kwa Mary Mwema kupitia barua ya maombi ya tarehe 06.05.2012 ambapo tangazo la zabuni husika ni la tarehe 25.05.2012 baada ya tarehe ya kuomba.

 “Zabuni husika haikupitia Kitengo cha Manunuzi na haikuwa imeidhinishwa na Bodi ya Zabuni,” inasema ripoti hiyo. 

Pia ripoti ilifafanua kuwa mzabuni wa upangishaji wa jengo la ofisi ya John Masenga haukujumuishwa kwenye mchakato wa tathmini ya kitaalamu licha ya kukidhi vigezo.

Korea Kaskazini Yatoa Vitisho Vingine kwa Marekani

$
0
0
Wakati kukiwa na taharuki kati ya Marekani na Korea Kaskazini kuhusu matumizi na majaribio ya mabomu ya nyuklia yanayofanywa na nchi hiyo ya bara la Asia, imetoa msisitizo wa vitisho vingine.

Makamu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Han Song-ryol ameiambia BBC kuwa nchi hiyo haiogopi vitisho vya Marekani na kwamba wamejipanga kufanya majaribio ya makombora yake kwa mfumo wa kila wiki, kila mwezi na kila mwaka.

Alisisitiza kuwa vita kamili ya nchi hiyo itakuwa ni matokeo ya Marekani kuchukua hatua zozote za kijeshi dhidi yake.

“Kama Marekani inapanga mashambulizi ya kijeshi dhidi yetu, tutajibu kwa makombora ya nyuklia kwa namna yetu na njia yetu wenyewe,” Han anakaririwa na BBC.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence kuionya Korea Kaskazini kuwa muda wa kuivumilia umekwisha na kuwataka waache kuijaribu Marekani.

Pence alisema kuwa Korea Kaskazini haipaswi kumjaribu Rais Donald Trump akiwataka kuona mfano wa kipigo alichowashushia Syria na Afghanistan hivi karibuni.

Korea Kaskazini imeendelea na mpango wake wa kuandaa na kufanya majaribio ya mabomu ya nyuklia ingawa hatua hizo zimekuwa zikilaaniwa vikali na Umoja wa Mataifa.

Nchi hiyo imelenga katika kuhakikisha inatengeneza makombora yanayoweza kufika katika pande kadhaa za dunia ikiwa ni pamoja na Marekani.

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa mpango huo hautawezekana na tayari ameanza kutuma vikosi vya Marekani na Manuari za kivita katika ufukwe wa Korea.

Bungeni: Serikali Kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa Ili kuwasaidia Wasanii

$
0
0
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iko katika mchakato wa kuanzisha “Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa” ambao una dhima kubwa ya kusaidia kuinua kipato, kuongeza tija na weledi kupitia utaratibu wa upatikanaji fedha utakaowekwa ili kuwawezesha wasanii kuzalisha kazi bora za sanaa zenye kukidhi viwango vya masoko ndani na nje ya nchi.
 
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Annastazia Wambura ameeleza hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Maulid Said Mtulia aliyeuliza juu ya mpango wa serikali kuwaongezea vifaa, mitaji na menejimenti vijana walioamua kujiajiri katika sanaa mbalimbali kama vile maigizo, maonesho ya mitindo na michezo mbalimbali.

Vilevile Naibu Waziri Wambura, ameeleza kuwa katika kipindi ambacho mfuko wa maendeleo ya sanaa unaandaliwa, Serikali inashauri Halmashauri zote ziwasaidie vijana wanaojishughulisha na sanaa kwa kuwapa mikopo yenye masharti na riba nafuu kwa ajili ya mitaji kutoka kwenye asilimia 10 ya mapato ya kila Halmashauri kwa kuwa sanaa ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana kwa sasa.

SORRY MADAM -Sehemu ya 49 & 50 (Destination of my enemies)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

 ILIPOISHIA
Kwa bahati nzuri, Shamsa akamkuta Eddy akiwa tayari amemaliza kuoga na kuvaa nguo zake pamoja na kinyago chake. Eddy katika kumduwaa, Shamsa aliye mjia kwa kasi, ndani ya bafu hilo akiongozana na waandhishi wa habari. Akastukia Shamsa akimkumbatia kwa nguvu bila hata kusita Shamsa akaanza kumnyonye denda black shadow, huku waandishi wakifyatua kamera zao kupiga picha za kuweka kwenye magazeti yao.

ENDELEA
   Kitendo hicho kikampa Eddy kigugumizi, akataka kumuita Shamsa ila sauti haikutoka akajikuta akiugulia tu huku akijaribu kumtoa Shamsa mwilini mwake.
Mabaunsa na wapambe wa Sabogo wakawa tayari wamesha ingia ndani ya bafu. Mabaunsa wakambeba juu juu Shamsa aliye anza kupiga kelele za furaha.
“I love you black shadow”(Nakupenda black shadow)
Waandishi wa habari nao wakatolewa ndani ya bafu hilo. Akabaki Eddy na Sabogo.

“Hao ndio mashabiki kiongozi inabidi uwavumilie tu”
Eddy hakujibu kitu zaidi ya kubaki kimya, akimfikiria Shamsa.
‘Huyu mtoto amepatwa na nini?’
Alijiuliza swahi  hilo kichwani mwake.
“Kiongozi?”
“Mmmmmmm”
Eddy alistuka kutoka katika dibwi la mawazo mengi
“Huyu binti amekuumiza nini, tumchukulie hatua za kisheria?”
“Hapana muacheni, na kama inawezekana kesho nahitaji akae meza ya VIP”

“VIP tena! Au umesha mzimikia tukamlete upate naye burudani usiku mzima. Kwa maana anaonekana kama changudoa”
“Fanya kama nilivyo kuagiza kufanya”
Eddy alizungumza kwa sauti nzito hadi Sabogo mwenyewe akabaki kimya na kutingisha kichwa akimaanisha kwamba amemuelewa.
    Shamsa akamkuta Sa Yoo nje ya ukumbi, akamkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu rafiki yake huyo huku akishangilia kama ameokota kipande cha dhahabu barabarani.

“Vipi nieleze umefanikiwa?”
“Ndio yaani ninafuraha achaa. NAKUPENDA BLACKKKK SHADOOOOOOWWWWWWWWW”
Shamsa alizungumza kwa sauti kubwa kama mwenda wazimu. Hata baadhi ya watui wakabaki wakimshangaa. Kutokana yupo nje ya ukumbi amboa mpiganaji huyo ametoka kuzichapa ulingoni muda mfupi ulio pita. Kila mtu akaamini kwamba binti huyo amechanganyikiwa kwa upendo kama wanachanganyikiwavyo wasichana wengine wanapo waonaga watu maarufu duniani.

  Njia nzima ndani ya gari Shamsa, aliendelea kumzungumzia black Shadow. Kumbukumbu ya jinsi alivyo mrukia black shadow na kumnyonya denda, zikawa zinamrudia rudia. Hadi ikafikia kipindi akaanza kuutathini mwili wa mpiganaji huyo, akiwa hana nguo.

 “Huli chakula?”
“Nimeshiba”
Shamsa alijibu huku akielekea chumbani kwake mara baada ya kufika katika nyuma wanayo ishi na Sa Yoo. Akaingia ndani kwake na kuufunga mlango kwa funguo. Haraka haraka akazivua nguo zake zote na kubaki kama alivyo zaliwa. Akasimama mbele ya kioo kikubwa cha kabati na kuanza kujichunguza huku akigeuka geuka akiliangalia umbo lake lililo jengeka vizuri.
“Mimi mzuri, kesho nawahi mapemaa ukumbini nimuone black shadow”
                                                                                                                   ***
   Ndani ya ndege ya kifahari aina ya Jet, Mzee Gdowin na John, pamoja na walinzi wao wawili. Waliendelea kuzungumza mambo mengi kuendelea kikundi chao ambacho kina watu wengi sana dunia. Ndege iliendelea kupasua mawingu kuelekea bara la Asia, ikitokea Amerika ya kaskazini. Ni safari ambayo imewachukua masaa mengi kadhaa, ila lengo na zumuni lao ni kwenda kuishuhudia fainali ya mapambano inayo endelea ndani ya Japani.

Wametokea kujikuta wakimpenda black shadow, mpiganaji mwenye ujuzi mkubwa sana katika maswala ya kupigana, wameona ni vyema wamchukue huyo ili awe miongoni mwa washirika wao ili kuzidi kujitanua kwenye kikuni chao.

Mara kadhaa wakajikuta wakitazama baadhi ya video za mapambano manne ya black Shadow. Ujuzi wao wa kupigana ulizidi kuwachanganya, na kutamani ndege hiyo iweze kufika katika muda mchache. Kwani wanahofia matajiri wengine duniani wanaweza kujitokeza na kumchukua black shadow katika mambo mbalimbali, ikiwemo uigizaji wa filamu.

“Mzee usiwe na hofu tutampata tuu. Nguvu ya kila kitu tunayo”
John alizungumza huku akimtazama Mzee Godwin anaye onekana kuwa na wasiwasi mwingi sana.
“Hawa marubani sijui wanaiendeshaje hii ndege, naona tunachelewa”
“Tutafika tu”
Masaa manne mbele teyeri wakawa wamefika nchini Japani, majira ya saa nne asubuhi. Wakapokelewa na mwenyeji wao ambaye moja kwa moja akawapeleka hadi kwenye hoteli moja ya kifahari.

“Pambano linaanza saa ngapi?”
Aliuliza mzee Godwin baada ya kupumzika kwa dakika kadhaa baada ya kufika hotelini.
“Saa nne usiku”
“Ahaa, hatuwezi kuonana na huyo black shadow muda huu kabla ya pambano?”
Mzee Godwin alimuuliza mwenyeji wao bwana Jackson Lee.
“Kusema kweli itakuwa ni ngumu kutokana black shadow yupo kwenye maandalizi ya pambano la usiku”
“Sawa kila kitu kiwekeni sawa, hata kesho muutaarifu uongozi wake kwamba ninahitaji kufanya naye kikao”
“Sawa mueheshimiwa”
                                                                                                 ***
   Kengele ya mlangoni ndio iliyo mkurupusha Sa Yoo. Akajizoa zoa kitandani kwake na kuiangalia saa yake ya ukutani na kukuta ni saa tano na dakika tano asubuhi. Akasimama na kujinyoosha mara kadhaa huku akipiga miyayo. Taratibu kwa wenge la usingizi akaanza kutembea kuelekea mlangoni. Akafika mlangoni na kuminya moja ya batani ambayo pembeni yake kuna kitivii kidogo cha ukutani kinacho muonyesha mtu aliyopo nje ya mlango. Akamuona kijana mmoja aliye valia tisheni yekundu na kofia nyekundu akiwa amesimama, huku mkononi mwake akiwa ameshika boksi.

Uvaaji wa kijana huyo ukamuashiria Sa Yoo kwamba huyo ni mlete mizigo kutoka katika kampuni moja kubwa ya kutuma mizigo ndani ya Japani. Akafungua mlango na kumtazama kijana huyo.
“Wewe ndio Ms Shamsa?”
“Hapana ila unaweza kusema shida yako”
“Kuna mzigo wake hapa nimeagizwa kuuleta kama yupo basi nahitaji kuweza kumuona”
“Umetokea wapi?”
“Madam kama wewe si muhusika basi, siwezi kukuambia kwamba unatokea wapi?”

“Mmmmmm”
Sa Yoo aliguna kisha akaanza kumuita Shamsa kwa sauti kubwa. Shamsa aliitikia baada ya muda akatoka akiwa amejifunga taulo akiashiria kwamba naye ndio kwanza anaamka.
“Kuna mzigo wako hapa”
Sa Yoo alizungumza huku akiondoka mlangoni na kwenda kujibwaga kwenye sofa na kujilaza kumalizia malizia usingizi wake.
“Naamini wewe ndio ms Shamsa?”
“Ndio”

“Kuna mzigo wako hapa kutoka kwa Mr Sabogo”
“Mr Sabogo ndio nani?”
Sa Yoo baada ya kusikia hilo jina akakurupuka na kukimbilia mlangoni akiwa katika sura ya furahja
“Humjui wewe Mr Sabogo, si yule mzamini wa black shadow”
Shamsa kusikia hivyo akawa kama mtu aliye changanyikiwa kwa haraka, akasaini kwenye karatasi maalumu ya kijana huyo kisha wakaagana naye kijana huyo na kuufunga mlango. Akaanza kulifungu boksi hilo. Macho yao wote yakatua kwenye ua zuri jekundu, linalo nukia vizuri, Sa Yoo akalitoa ndipo wakaziona tiketi mbili zilizo kuwa chini ndani ya boksi.

“VIP TIKETIIIIIII UUUUUUUUU”
Shamsa alizungumza huku akiruka juu kwa furaha, Sa Yoon aye akampokonya moja wote wakajikuta wakiruka ruka kwa kushangilia kupata mualiko huo kutoka kwa black shadow.
Kila mmoja akawa anaombea muda na masaa yaweze kukimbia kwa haraka ili wafike ukumbini kushuhudia pambano ambalo si kwasababu watu wanalipenda, ila Shamsa anampenda mpiganaji wa pambano huyo ambaye ni black Shadow

Majira ya saa mbili usiku Sa Yoo na Shamsa wakawa wamefika katika ukumbi wa mapambano. Kwa siku hiyo hawakupita katika lango wanalo pita watu wa kawaidia ila walipita katika lango la kuingilia katika viti maalumu vya watu wenye hadhi ya juu. Kila sehemu Shamsa alipo pita alitazamwa na watu kwani habari za yeye kumbusu black shadow, zilienea kwenye magazeti mengi. Kwa msaada wa muhudumu katika sehemu hiyo maalumu wakaonyeshwa viti vyao vya kukaa, ambavyo mbele yake kuna kioo kikubwa na kigumu kinacho onyesha pambano hilo kwa ukaribu zaidi kutokana na lensi ya mvutano iliyo tengenezwa kwenye kioo hicho.
“Munatumia kinywaji gani?”
Dada muhudumu aliwauliza, kila mtu akaseme kinywaji anachho kihitaji. Watu walizidi kumiminika katika ukumbi, kila mtu aliitafuta siti yake na kuweza kukaa kusubiria muda muafaka wa pambano hilo liweze kufika.

   Ulinzi mkali ukaimarishwa katika sehemu ya VIP, mzee Godwin na John ambaye muda wote maisha yake ni yakusukumwa kwenye kiti maalumu cha matairi. Wakaingi katika sehemu hiyo. Wakakaribishwa katika sehemu waliyo andaliwa, ambapo kuna wadada sita walio valia chupi aina ya bikini na sidiria wakiwa wamesimama, kwa ajili ya kuwapa huduma ya kuwachua chua miili yao pale watakapo kuwa wakiendelea kuliangalia pambano hilo.

Vipaza sauti vilivyomo ndani ya uwanja vilianza kutoa sauti ya kike ya mtangazaji wa pambano wa siku ya leo. Kelele zilizidi kurindima kila mahali, watu walikuwa kama wameingiwa na pepo la kushangilia kila walipo sikia jina la black shadow.

Wadada wengi walishika mabango yaliyo andikwa ujumbe tofauti tofauti wakionyesha hisia zao za kumpenda mpiganaji huyo, aliye jizolea umaarufu katika kipindi kifupi tu.
Macho ya Shamsa yakaendelea kutazama huku na kule, mara kadhaa alijaribu kuyapitia mabango ya wasichana waliyo yashika, akajikuta akiingiwa na woga pamoja na wivu wa kumkosa mpiganaji huyo katika swala zima la mapenzi.

“Anaye kuja kwenu kwa sasa ni   BLACK SHADOWWW”
Uwanja mzima ukasimama huku watu wakimshangilia. Eddy hakuamini kupata idadi kubwa ya watu wanao mshangilia, kila alipo pitisha macho yake huku na kule aliona baadhi ya watu wakiwa wamevaa mavazi kama yake. Akaanza kutembea kwa kujiamini kuelekea uwanjani. Hakusita kupita karibu na washabiki walio kaa karibu na njia ya kuelekea ulingoni. Akawapa mikono kuashiria kwamba anawapenda kama wanavyo mpenda.

   Akaingia ulingoni na kuendelea kuzunguka huku mkono wake mmoja wa kulia akiwa ameunyoosha juu, kwa ishara ya kuwasalimia watu. Muendesha shuhuli akamkaribisha Yong Po. Mashabiki wake nao wakasimama na kumshangilia mpiganaji huyo anaye sifika kwa kuweka rekodi ya kuwavunja vunja wapiganaji anao kutana nao. Hakuwa mwenye mwili mkubwa wa kutisha, ila sura yake iliyo komaa na yenye upara ulio kolezwa mafuta hadi unameta meta, ndivyo vilivyo mfanya Eddy ahofie kidogo. Ili kupoteza hofu hiyo ikambidi Eddy ashushe pumzi nyingi na kujiweka sawa huku akinyoosha nyoosha viungo vyake.

Muendesha shuhuli akatoka uwanjani na kuwaacha Eddy na mjapani huyo aliye komaa sana akionekana ni mpambanaji wa kipindi kirefu cha nyuma. Refarii akasimama katikati yao, akawapa sheria zinazo takiwa kufwatwa, alipo hakikisha kila mmoja ameelewa sheria hizo. Akaanzisha mpambano.

Young Po akaanza kuruka ruka huku akiichezesha miguu yake kwa kasi, jambo lililo mfanya Eddy kutazama miguu hiyo inavyo kwenda, kwani hakujua ni muda gani, mpinzani wake huyo atarusha teke. Kufumba na kufumbua Eddy akajikuta akiwa ameanguka chini, hakuelewa hata teke hilo la kifuani amepigwa muda gani.

   Eddy akanyanyuka kwa haraka na kupanga mashambulizi, akarusha ngumi kadhaa baadhi zikampata Young Po ila baadhi alizikwepa.  Yoong Po hakuwa nyuma, na yeye akaendelea kutupa mashambulizi ya kustukia kwani tayari alisha weza kumsoma Eddy kupitia mikanda ya video aliyo cheza jana. Alimgundua kwamba black Shadow ni mwepesi sana katika kukwepa, kurusha ngumi na mateke.

Pambano likazidi kufaana, watu walizidi kushangilia kila pale mmoja kati ya wapiganaji alivyorusha makonde kwa mwenzake.
Kila mmoja wa mashabiki hadi inatimu robo saa, hakuweza kujua mshindi ni nani kwani wapiganaji hao walijitahidi kila mmoja kufanya awezalo kuhakikisha kwamba anajibu makonde ya mwenzake.
Jasho likazidi kuwatirika wapiganaji, hata Shamsa mwenyewe, japo amekaakatika sehemu ambayo ina kiyoyozi cha kutosha ila naye jasho lilimwagika kila alipo shuhudia black shadow anapigwa.

    Shamsa akajikuta akiaanza kuingiwa na furaha moyoni mwake baada ya kuanza kuona black shadow anamzidi Young Po. Si Shamsa pekee bali hata mashabiki wa black shadow nao walianza kumshangilia. Mzee Godwin na John nao hawakuwa nyuma kumshangilia mpiganaji huyo waliye muhitaji kwa udi na uvumba. Yong Po alipigwa ngumi moja takatifu ya shingoni iliyo muangusha chini na kulala kifudi fudi.
Uwanja mzima ukanyanyuka kwa kushangilia, refarii akamsogelea Yong Po. Akainama na kumuuliza kama ana weza kuendelea na pambano.
“Nipatie”

Bungeni: Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama Kukutana Leo Kujadili Mauaji ya Polisi 8 na Raia

$
0
0
Mbunge wa Bukombe, Mhe. Dotto Biteko ametoa hoja ya kuahirishwa kwa shughuli za bunge ili Bunge liweze kujadili hali ya mauaji inayoendelea nchini ikiwemo mauaji ya askari polisi waliouawa na watu wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani. 

Hoja hiyo imeungwa mkono na wabunge kadhaa wakiwemo Cosato Chumi (Mafinga Mjini) na Amina Mollel (Viti Maalum)

Akitolea ufafanuzi hoja hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Mwigulu Nchemba amesema serikali inachukulia jambo hilo kwa ukubwa na uzito mkubwa.
 
“Kama ilivyotolewa kauli na Waziri Mkuu serikali inalichukulia mambo haya kwa uzito mkubwa na inawahakikishia wananchi matukio ya uhalifu yaliyotokea ndio yametupa chachu zaidi ya kupambana na matukio kama haya na pia tunawaomba wananchi watoe taarifa na wala wasiogope maana tuna mfumo bora sana wa kuwalinda watoa taarifa wote” Ameeleza Waziri Nchemba ambaye pia ametoa pole kwa familia za askari wote waliopoteza maisha wakiwa katika kazi ya kulinda wananchi na amani ya nchi.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai, amelieleza Bunge kwa kuwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama chini ya Mwenyekiti wake Balozi Adad Rajabu itakutana leo na mawaziri husika ili kupokea taarifa ya mambo haya ni vyema Bunge likatoa nafasi kwa kamati hiyo kukutana kwanza na kupokea taarifa hiyo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya leo Jumatano ya April 19

Wapinzani Wadai Wakurugenzi Waliotumbuliwa wanalipwa Milioni 480 kwa mwezi

$
0
0
Maoni ya upinzani ya wizara mbili, jana yaliibua hoja tofauti; ya kwanza ikidai Serikali inawalipa wakurugenzi 120 waliotumbuliwa Sh480 milioni, na ya pili ikikikishutumu kiti cha Spika kwa kuzuia mjadala wa wabunge kutishiwa maisha.

Katika sakata la kwanza, wapinzani walisema fedha za Serikali zinapotea kutokana na watumishi waliotumbuliwa au kuachwa katika uteuzi kuendelea kulipwa stahiki zao.

Msemaji wa kambi hiyo, Japhary Michael alisema wakati akitoa maoni kuhusu bajeti ya Tamisemi kuwa wakurugenzi hao wanalipwa mshahara wa Sh5.76 milioni kila mmoja kwa mwezi.

“Ikumbukwe kuwa wakurugenzi hawa bado wanalipwa mishahara yao pamoja na stahiki nyingine za kiutumishi kama nyumba, umeme, simu, matibabu na kadhalika. Wastani wa mshahara wa mkurugenzi ni Sh 3.8 milioni mpaka Sh4 milioni,” alisema.

Alisema wakurugenzi 120 wa zamani hawakuteuliwa kwa nafasi hizo katika Serikali ya Awamu ya Tano lakini bado wamo katika utumishi wa umma, na hata wale wapya walioteuliwa walitoka nje ya mfumo wa utumishi wa umma, wengi wao wakiwa makada wa CCM.

Alisema baada ya kutenguliwa kwa wakurugenzi hao 120 kutoka halmashauri mbalimbali nchini, walielekezwa kuripoti kwa makatibu tawala wa mikoa waliyotoka kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.

“Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa wakurugenzi hawa takribani wote wanahudhuria kwa makatibu tawala wa mikoa na kimsingi hawana kazi za kufanya,” alisema.

Alisema kambi hiyo inaishauri Serikali kuangalia upya sheria ya utumishi na ajira katika serikali za mitaa ili kuwe na utaratibu ambao mchakato wake utaanzia katika vikao kisheria vya halmashauri.

Michael, ambaye ni mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), alishauri Waziri ateue kutokana na orodha itakayopendekezwa na halmashauri baada ya watu kuomba ajira.

Katika sakata la pili, msemaji wa kambi ya upinzani bungeni anayehusika na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ruth Mollel alidai kiti cha Spika kilizuia mjadala wa wabunge kutishiwa maisha kwa mgongo wa kanuni za Bunge.

Suala hilo lilimfanya waziri husika, Jenista Mhagama kusimama na kutaka sentensi hiyo ifutwe kwa kuwa ilishaondolewa wakati kiongozi wa upinzani bungeni, Freeman Mbowe alipokuwa akisoma maoni yao kuhusu bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Lakini hoja hiyo ilipingwa na mbunge wa Iringa, Mchungaji Peter Msigwa aliyesema kuwa Katiba inawapa uhuru wa kusema maneno hayo.

Hata hivyo, Spika Job Ndugai alisema maoni hayo yaliandikwa na mtu ambaye haelewi taratibu za Bunge na hivyo kufuta sentensi hiyo.

Alihoji kama kuna mbunge aliyepeleka taarifa ya kutishiwa maisha.

Kuhusu hoja kwamba wapinzani wanadhibitiwa, Ndugai alihoji wanadhibitiwaje.

“Hivi kwa nini mnajiweka katika hali fulani ya kuona kwamba mnaonewa? Hivi unaonewa na nani kanuni ni za wote? Taratibu ni za wote hakuna mtu aliyedhibitiwa chochote,” alisema.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>