Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kauli ya Mwigulu Nchemba baada ya kutembelea eneo walilouawa askari 8

$
0
0
WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi,Mwigulu Nchemba,amesema hawatokubaliana na mtandao,kundi ama mtu anaehusika na kugharimu maisha ya askari ama wananchi wasio na hatia.

Aidha amebainisha kwamba kilichombele kwa sasa ,wanaendelea kuhakikisha kuwa wanarudisha silaha zinazochukuliwa katika matukio mbalimbali ya mauaji ya askari na kuendelea na mapambano na wahalifu hao.

Nchemba ameyasema hayo jana  ,wilayani Kibiti,mkoani Pwani,na kumtaka mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo kupambana na matukio ya mauaji yanayoendelea katika baadhi ya wilaya mkoani hapo.

Waziri huyo wa mambo ya ndani ,alieleza kwamba,amepokea taarifa ya kuuwawa kwa askari nane wilayani Kibiti  kwa mshituko mkubwa .

Nchemba aliwaomba watanzania kwa kipindi hiki wawe watulivu wakati jeshi la polisi likiendelea kukabiliana na mambo hayo.

“Hii ni changamoto kwa wizara ya mambo ya ndani kuanza upya kuboresha mbinu zake za ki intelensia zinazoendana na mazingira ya sasa kwa mahitaji ya sasa”alisema.

Alibainisha kwamba,ni ngumu kuingia akili kwa watu wachache kuuwa hovyo askari ambao ndio walinzi wa raia na mali zao

“Kuna jambo lipo nyuma limejificha ambalo mwisho wake umefika kwani hatutoweza kulifumbia macho”alisisitiza.

Nchemba aliomba jamii iendelee kulinda amani ya nchi na kuheshimu askari polisi ambao wapo kwa ajili ya kuwalinda katika usalama wao.

Rais Magufuli Aaahidi kuwatumbua wenye vyeti feki Serikalini

$
0
0
Rais Magufuli leo wakati akizindua majengo ya Hostel za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) amefunguka na kusema sasa anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wanatumia vyeti vya kufoji.

Rais Magufuli amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kila sekta hivyo sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika kazi na kutenda haki katika jambo hilo.

"Naisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wana vyeti vya kufoji ili niifanyie kazi" alisema Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli ameitaka Taasisi ya TCU kuacha kuwapangia wanafunzi vyuo bali wanafunzi wanapaswa kuwa huru kuchagua aina ya vyuo ambavyo wao wanataka kwenda na kusema kwa kufanya hivyo itatoa nafasi kila chuo kuwa na wanafunzi wa kutosha huku wanafunzi pia wakienda kusoma sehemu ambazo wao wanahitaji kwenda kusoma na si kuwapangia.

"Mtu amefaulu ana sifa zake anataka kuja kusoma Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam afaidi mabweni ya Magufuli analazimishwa kupelekwa kwenye ka chuo ambako wala hakana jina hata ukitafuta kwenye mtandao hakaonekani, akasome pale wakati hawana hata mabweni na saa zingine hata walimu hawana, tunawatesa watoto hawa na saa zingine wakuu wa vyo vile wamekuwa na tabia ya kwenda kwenye uongozi wa TCU ingawa sina ushahidi wapangiwe idadi wa wanafunzi wanaowataka kwenye vyuo hivyo, sifahamu wanapangiwa kwa rushwa lakini wapo pia kuna ushahidi na baadhi ya viongozi wa vyuo fulani fulani waliofunga safari kwenda TCU kwa ajili ya kuomba wapangiwe wanafunzi au kutoa shukrani, au hata kwenda kuwasalimu tu" alisema Rais Magufuli

Mabweni Mapya ya UDSM Yaliyozinduliwa na Rais Magufuli Yatachukua Wanafunzi 3,840

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, Jumamosi hii amefanya uzinduzi wa mabweni mapya ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.

Rais Magufuli amesema kukamilika kwa mabweni hayo ya kisasa ndani ya kipindi chini ya miezi minane ni ishara kuwa Tanzania inaweza. “Tukiamua tunaweza tukafanya watu wakaona miujiza,” amesema.

Ameongeza kuwa wapo watu walibeza kuwa shilingi bilioni 10 zisingeweza kukamilisha ujenzi huo na kwamba hawakumiani kuwa yasingeweza kujengwa na Watanzania. Ameshauri kuwa mafanikio hayo yawe vifundisho kwa viongozi wa serikali kutotoa tenda kwa wakandarasi wa nje zenye gharama kubwa na kuwaacha wale wa ndani.

Kwa upande mwingine Rais amesema mabweni hayo yatalipiwa kwa shilingi 500 pekee, tofauti na 800 kwa mabweni mengine. Mabweni hayo yana uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,840.

Awali akizungumza kwenye uzinduzi huo, makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala alissema mabweni hayo yana vitanda 1,920 vya double decker, makabati 1,920, shelves za vitabu 1,920, meza, 1,920, viti 3,840 magodoro 3,840.

“Tutahakikisha kuwa huduma zote muhimu kama vile cafeteria ya chakula, maduka kwaajili ya mahitaji mbalimbali, zahanati, salon, kituo cha polisi na nyinginezo vinapatikana hapa hapa,” alisema Profesa Mukandala.

Aliongeza kuwa ujenzi wa cafeteria umeshaanza na ikikamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kwa wakati mmoja. Amehakikisha kuwa chuo kimejipanga kuhakikisha kuwa mabweni yanatunzwa na tayari wameshampata msimamizi mkuu aliyepewa mafunzo maalum ya muda mfupi.

Prof Mukandala alimshukuru Rais Magufuli kwa namna alivyojitolea kuhakikisha mabweni hayo yanakamilika kwa kufuatilia kwa ukaribu kila hatua za ujenzi wake.

“Hili ni jambo kubwa sana na historia itaandikwa kwa herufi za dhahabu,” alisema.

Aliongeza kuwa wizara tatu zimehusika kwenye ujenzi wa mabweni hayo ambazo ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Mawaziri wote wa wizara hizo Dr. Hussen Mwinyi, Profesa Makame Mbarawa na Profesa Joyce Ndalichako walikuwepo.

Korea Kaskazini: Tumejiandaa Kwa Vita na Marekani

$
0
0
Kukiwa na wasiwasi kwamba Korea Kaskazini inakaribia kupata ufanisi wa kukamilisha silaha za Kinyuklia, Marekani imepewa onyo la kutoanzisha uchokozi dhidi ya nchi hiyo kwani ipo tayari kulipiza kisasi kwa mshambulio ya Kinyuklia.

”Tuko tayari kulipiza kisasi na mashambulio ya Nyuklia kwa mbinu zetu dhidi ya shambulio lolote la Kinyuklia”.

Taarifa hiyo imetolewa wakati Rais wa nchi hiyo, Kim Jong-un alipohudhuria gwaride la heshima katika mji mkuu wa Pyong yang katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya babu yake, marehemu Kim II-Sung, ambaye ni mwanzilishi wa taifa hilo.

Mtu ammoja anayedaiwa kuwa na uwezo mkubwa katika nchi hiyo amesema kuwa wamejiandaa kwa vita kamili. “tumejiandaa kwa vita kamili” amesema

Aidha, katika gwaride lililofanyika, vifaa vilivyoonyeshwa kwa mara ya kwanza vilikuwa ni makombora ya masafa marefu yanayoweza kwenda kwa takriban kilomita 1000 na nyingina nzito ambapo wachanganuzi wa vifaa vya kijeshi pia wamesema kuwa kuna makombora mawili mapya yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine, lakini haijulikani iwapo yamefanyiwa majaribio. 

Mrema Amuomba Rais Magufuli Kuiangalia Upya Bodi Ya Parole

$
0
0
Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Bodi ya Parole  Augustino Mrema amesema kuna changamoto nyingi sana katika kuendesha bodi hiyo na kumuomba Rais Dr John Pombe Magufuli  kumwezesha ili atimize majukumu yake.

Akizungumza  kupitia kipindi maalum cha Radio UFM (ya Azm Tv),Mrema amesema kuwa anaiomba serikali kuiangalia upya bodi hiyo kuhusu hali ya wafungwa nchini na mchakato wa kuwatoa wafungwa walio katika hatua za kisheria za Parole.

Mrema amesema , anaukumbusha umma kuwa kila mtu ni mfungwa mtarajiwa na serikali haiwezi kufanya mambo yote hivyo watanzania wakiwa na utamaduni wa kuyasaidia magereza yetu itasaidia  kupata angalau virago kwa ajili ya wafungwa. 

Aliongeza kuwa utaratibu wa Parole ni mchakato unaohitaji gharama hivyo bodi yake inajitahidi kupata fedha ili kufanikisha  majukumu yao.

Akizungumzia hali ya kisiasa nchini, Mrema amesema kuwa viongozi waliopo madarakani na wale waliomaliza muda wao kufanya kazi pamoja na Rais ikiwemo na kumpa ushauri utakaojenga nchini na sio kumbeza kama watu wanavyofanya.

Watanzania waache kukosoa kazi za Rais na kuacha kuandika mabaya yake kwani siku hizi mtu akiongelea kitu kibaya ndite anaonekana anafaaa lakini kitu hicho kinajenga taswira mbaya na zaidi hata katika Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere aliongea mambo mazito  lakini hakuna chombo cha habari kilichoandika.

Mrema  amesema, katika wazalendo wa nchi hii yeye ni mmoja wao kwani anafanya kazi hiyo pasipo kujali mshahara ama posho yoyote pia alitumia nafasi hiyo kumuomba radhi Rais mstaafu wa awamu  ya tatu Mhe Benjamini William Mkapa kwa makosa aliyowahi kumfanyia katika kipindi chake kwa kumsingizia kuwa aliiba Tshs Milioni 900,  akasema ule ulikuwa ni mpango wa makusudi ingawa walipoenda mahakamani alishinda.

Miili Ya Askari 8 Waliouawa Mkoani Pwani Yaagwa Jijini Dar.......Mwigulu Nchemba Atangaza Kiama, IGP Atoa Onyo kwa Wanaoshabikia Mitandaoni

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewatangazia kiama watu wote waliohusika kuwaua askari polisi nane Kibiti wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari hao jijini Dar es Salaam leo asubuhi Mwigulu alisema watu hao watakamatwa wote na kufikishwa kwenye mkono wa sheria. 

"Kitendo hiki cha mauaji kilichofanyika dhidi ya askari wetu hakivumiliki hata kidogo waliohusika tutawatafuta na kuwakamata" alisema Mwigulu.

Aliwaomba wananchi wa maeneo husika kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwapata wahusika wa tukio hilo. 

Katika hatua nyingine Mwigulu ameitaka wizara husika kuhakikisha inatoa fidia kwa ndugu wa askari hao na majeruhi badala ya kuchukua muda mrefu kuitoa.

 "Naomba fidia kwa askari hawa tuliowapoteza wakitumikia taifa itolewa haraka bila kucheleweshwa" aliongeza Mwigulu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu alisema watuhumiwa wote waliohusika kufanya mauaji hayo ni lazima watafikiwa na mkono wa dola. 

Alisema wananchi wa eneo hilo wanawafahamu wahusika hivyo amewaomba washirikiane na polisi ili kuwapata vinginevyo nguvu itatumika.

Alisema linapotokea tukio kama hilo kuna baadhi ya watu wamekuwa wakishabikia kupitia mitandao ya kijamii hivyo akatoa onyo kuwa watakao bainika na wao watakamatwa kwa kutenda kosa.

Askari waliopoteza maisha katika tukio hilo la kinyama wametajwa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kaagiza Mkurugenzi wa Kampuni ya 4×4 Tanzania Limited akamatwe

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema timu aliyoiunda ichunguze tuhuma za ubadhirifu kwenye Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) imekamilisha kazi yake na imebaini madudu mengi zaidi.

Machi 16, 2017, Waziri Mkuu aliivunja Bodi ya WETCU pamoja na Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) kwa sababu ya kushindwa kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma. 

Alimuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora awakamate viongozi wanne wa pamoja na kufunga ofisi za chama hicho hadi uchunguzi wa fedha za chama hicho utakapokamilika.

Waziri Mkuu ambaye amefanya ziara ya siku moja mkoani Tabora, ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Aprili 15, 2017) wakati akizungumza na wajumbe zaidi ya 300 wa mkutano wa wadau wa zao la tumbaku katika ukumbi wa Kiyungi mwana Isike, mjini Tabora.

“Nilikuja Tabora mara ya kwanza ili kuchukua hatua za dharura na leo nimekuja kuendelea na mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuwezesha kilimo cha tumbaku kiwe na tija kwa wakulima na ndiyo maana niliomba wakulima, wanunuzi wa tumbaku, vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) na viongozi wa Serikali wawepo kwenye mkutano huu,” amesema.

Akitoa mrejesho juu ya uchunguzi uliofanywa na timu aliyoiunda, Waziri Mkuu amesema WETCU haikuwa na kitengo cha ununuzi kwa zabuni.
 
“Waliunda kampuni inayoitwa FDTU (Flu and Dark Tobacco Union) ambayo ni Umoja wa Wenyeviti wa Union zote za Tumbaku nchini ambayo ilipewa kazi zote za ununuzi wa pembejeo na hela walikuwa wanagawana,”amesema.

“Tumefanya ufuatiliaji hadi katika benki lakini kwenye akaunti hakuna hela mpaka sasa. Tumeangalia chanzo cha fedha za union zenu na kubaini hakuna fedha zinazotoka FDTU kwenda WETCU,” ameongeza.

Akifafanua kuhusu kashfa ya ununuzi wa gari aina ya shangingi lenye namba za usajili T181 DEN ambao ulifanywa kinyume na maazimio ya mkutano mkuu, Waziri Mkuu amesema viongozi wa WETCU walitumia zaidi ya sh. milioni 220 kuzidi kiwango kilichoidhinishwa na Mkutano Mkuu cha kununua gari lenye thamani ya sh. milioni 40.

“Gari walilolinunua ni la mwaka 2008 na siyo la mwaka 2015 kama taarifa zinavyoonesha. Lilikwishatumika kwa kilometa zaidi ya 95,000 lakini likarekebishwa hadi kubakiza kilometa 16,000 ili lionekane ni jipya,… maana yake wamekula fedha nyingi sana na ni lazima tuwachukulie hatua za kisheria kwa sababu wamekula fedha, wamenunua gari lililotumika na siyo maamuzi ya mkutano mkuu.”

Waziri Mkuu ameagiza Mkurugenzi wa kampuni ya 4×4 Tanzania Limited, Bw. Faraz Yaseen naye akamatwe na kuhojiwa ni kwa nini alihusika na kuuza gari la mwaka 2008 lakini akabadilisha nyaraka ili lionekane ni la mwaka 2015.

Akitoa ufafanuzi kuhusu uuzaji wa hisa za WETCU, Waziri Mkuu amesema chama hicho kilikuwa na hisa milioni 36 ambapo kilitoa milioni sita ili ziuzwe na zikapatikana sh. bilioni 2.520 na ndiko huko walitoa fedha za kununulia gari na vifaa vya ofisi kwa sh. milioni 49.

“Walichukua hisa 100,000 na kuziuza na wakapata sh. milioni 250 lakini fedha hizo hazikuwekwa kwenye akaunti ya chama. Hisa zilizobakia, ambazo ni milioni 30, walishaanza mchakato wa kuuza hisa milioni 28. Je mliahsatoa kibali Wamempatia cheti halisi cha hisa hizo wakala Zani Security ili auze hisa hizo bila kuomba kibali cha Mkutano Mkuu,” amesema.

“Kwa vile hawakupata idhini ya Mkutano Mkuu, na wala hawakufuata taratibu, kanuni na sheria, kuanzia leo nimesitisha mauzo ya hisa hizo na kirudishwe Tabora mapema iwezekanavyo. Mrajisi fuatilia Zani Securiy warudishe kile cheti kinachowapa dhamana ya kuuza hizo hisa.”

Waziri Mkuu amesema, kwa vile WETCU ina madeni mengi katika benko za CRDB na NMB, viongozi wa chama hicho waliamua kufungua akaunti mpya za fedha za kitanzania na dola za Marekani kwenye benki ya EXIM. Walifungua akaunti ya muda maalum na kuweka huko fedha ambazo zilishalisha faida ya zaidi ya sh. milioni 14 katika kipindi cha miezi mitatu.

“Ninamuagiza Mrajisi wa Vyama vya Ushirika kupitia COASCO (Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika) ya Tabora afuatilie benki ya EXIM hapa Tabora ili kubaini ni akina nani walikuwa wakifanya miamala hiyo,” amesema,

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama; Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba; Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wenyeviti wa Halmashauri za mkoa huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA,
JUMAMOSI, APRILI 15, 2017

Habari Zilizopp Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya April 16


Rais Magufuli Ashiriki Ibada ya Pasaka Kanisa la Africa Inland Church Magomeni Dar

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli katika Ibada ya Pasaka katika wa Kanisa la Afrika Inland Church Pastorate ya Magomeni  Mapipa jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa hilo la la Afrika Inland Church Pastorate ya Magomeni Mapipa  jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada ya Pasaka.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Kanisa la Afrika Inland Church Pastorate ya Magomeni Askofu Charles Salala mara baada ya kuzungumza Kanisani hapo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 17

Waziri Nchemba Atoa ONYO Kwa Wanaotumia Dini Kufanya Uhalifu

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mwigulu Nchemba, amewaonya waumini wa dini mbalimbali nchini kutotumia mwamvuli wa dini kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo kudhuru maisha ya wengine, huku akitangaza kulegeza masharti ya usajili wa nyumba za ibada

Waziri Mwigulu ametoa onyo hilo jana  alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la Pasaka lililofanyika  katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ambapo alisema serikali haitawavumilia watu wa aina hiyo.

Katika hotuba yake fupi Waziri Mwigulu alisema serikali inatambua uhuru wa kuabudu iliyoutoa kwa wananchi wake na inaunga mkono kazi nzuri inayofanyika kupitia ibada, lakini uhuru huo usikwaze wengine, na wala usivunje sheria.

Alisema "Ucha Mungu Siyo Udini", hivyo ni sahihi kwa waumini kumcha Mungu kwa kiwango wanachopenda lakini si kuwashikia silaha watu wengine ili wajiunge na dini zao.

“Wale ambao watatumia misimamo iliyopitiliza kudhuru maisha ya watu wengine, serikali itasimama na kuwahesabia kuwa ni waovu na tutashughulika nao kama wahalifu wengine” Alisema Mwigulu

Katika hatua nyingine, Waziri Nchemba ameagiza taasisi zilizo chini ya wizara yake kulegeza masharti ya usajili wa nyumba za ibada, badala ya kuwapa njia ngumu kwani nyumba hizo ni muhimu kwa ajili ya kumuombea Rais Magufuli na taifa kwa ujumla

"Nimeelekeza watu wangu kuwa waelekezeni watu wanaotaka kusajili nyumba za ibada watimize masharti na muwasajili, hatuwezi kuweka masharti magumu ya kusajili nyumba za ibada halafu tukaweka masharti rahisi ya kusajili bar na kumbi za disco" Alisisitiza Mwigulu

Aliwataka waumini wa dini mbalimbali kuendelea kuliombea taifa, huku akiwapongeza kwa kazi nzuri ya maombi waliyoifanya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

"Endeleeni kuliombea taifa letu, wana maombi mkishaomba, mambo yakawa mema, watu huwa hawakumbuki kama mlisugua magoti… hata wakati wa uchaguzi mliomba ndiyo maana tukapita salama wakati kuna watu walitaka kuona Tanzania inayojidai kuwa na amani, itakuwaje.....

"..Wakati ule walikuwa wameandaa magari ya washawasha na mabomu ya machozi lakini nilipofika wizarani nilikuta yale magari yapo hayakutumika pamoja na mabomu, kazi mlishamaliza wana maombi"

Waziri Mwigulu pia alitumia nafasi hiyo kuwahakikishia wasanii wa nyimbo za injili kuwa serikali itafanya kila iwezalo kulinda maslahi ya kazi zao, huku akipongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli ya kuwaletea maendeleo wananchi licha ya kupingwa na baadhi ya watu na kutolea mifano ujenzi wa reli ya kisasa, ununuzi wa ndege, elimu bure  na mengine.

Askofu: Rais, majipu unayotumbua ni madogomadogo...... Tunakuunga Mkono na Tutazidi Kukuombea

$
0
0
Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli jana  Sikukuu ya Pasaka, waliungana na Waumini wa Kanisa la Africa Inland – Tanzania Dayosisi ya Pwani Pastorate ya Magomeni kusali Ibada ya Pasaka.

Katika Ibada hiyo Askofu wa Kanisa la Africa Inland – Tanzania Baba Askofu Charles Salalah aliongoza maombi ya kumuombea Mhe. Rais Magufuli ili aendelee kutekeleza majukumu yake ya kuiongoza nchi vizuri na alimpongeza kwa kazi kubwa ya kurekebisha mambo yote yasiyofaa nchini ikiwemo kuwaondoa viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya na kufuja mali za umma.

“Mhe. Rais unafanya kazi kubwa ya kutumbua majipu, majipu unayoyatumbua wewe ni majipu madogomadogo yaliyotokana na jipu kuu ambalo ni dhambi za mwanadamu, na jipu hili lilitumbuliwa na Bwana Yesu, kwa hiyo sisi Wakristo wenzako na waumini wengine tunakuombea sana na tunakuunga mkono katika kazi hii nzito ya kutumbua majipu haya madogomadogo ya watumishi hewa, mishahara hewa, mikopo hewa na mengine mengi” alisema Askofu Charles Salalah.

Akizungumza katika Ibada hiyo Mhe. Rais Magufuli aliwashukuru Wakristo wa Kanisa la Africa Inland na waumini wa madhehebu mengine ya dini kwa kuendelea kumuombea na ameomba maombi hayo yaendelee, na pia waiombee nchi iendelee kuwa na amani, umoja, mshikamano na watu wachapa kazi.

TCRA Yatoa Somo kwa Wanafunzi Vyuoni

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini na wananchi kutumia huduma za mawasiliano kwa faida, badala ya kuzitumia kujiburudisha pekee.
 
Mhandisi wa Masafa wa TCRA, Francis Mihayo alisema hayo hivi karibuni wakati wa kongamano la vyuo vikuu kujadili matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha. Mihayo alisema kumekuwa na matumizi yasiyo sahihi ya mitandao hasa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambao baadhi wameingia matatani kutokana na kuTOzingatia sheria.
 
Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho, John Semindu alisema wameamua kuandaa kongamano hilo ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kujifunza matumizi sahihi ya na kujiepusha kusambaza ujumbe wenye lengo la kusababisha uvunjifu wa sheria. 

Semindu alisema kutokana na kukua kwa huduma za mawasiliano nchini na duniani, ni watu wachache wanaotumia huduma hizo zaidi ya kuwasiliana.
 
“Tunatakiwa twende mbali zaidi ya kuwasiliana na kutumiana ujumbe kutufanya tucheke, bali tunaweza kutumia huduma za Tehama kujiajiri na kuajiri wengine ni eneo muhimu katika kurahisisha kazi na kuchochea ubunifu ambao ndiyo msingi wa maendeleo,” alisema Semindu.
 
Richard Gwele, kutoka Taasisi ya Smart Education na Mwangaza Jafar ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, walisema elimu zaidi inapaswa kutolewa ili kuepusha matumizi yasiyo sahihi hasa kwenye mitandao ya jamii.
 
Gwele alisema iwapo wanafunzi watatumia mitandao vizuri itawasaidia kupata kujisomea mambo mbalimbali hasa yanayotokana na mabadiliko ya teknolojia duniani.
 
Alisema wanafunzi hawajatumia hata nusu ya mitandao katika kujielimisha, hivyo wanatakiwa kubadilika.

Eka 17 za mashamba ya Bangi zafyekwa

$
0
0
Polisi Mkoa wa Arusha wameteketeza eka 17 za mashamba ya bangi katika Kata ya Kisimiri, wilayani Arumeru.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema mashamba hayo yalitekelezwa wakati wa msako maalumu.
 
Mkumbo alitoa onyo kwa wananchi wanauzunguka Mlima Meru ambao wamekuwa wakilima bangi kwa kisingizio kuwa, polisi hawawezi kufika.
 
“Kuna mtindo wa kulima bangi milimani hasa Mlima Meru, tunasema tutaendelea na msako kubaini wote wanaohusika,” alisema.
 
Aliwataka viongozi wa mitaa na madiwani kuwa makini na kudhibiti kilimo hicho haramu kwenye maeneo yao. Kamanda Mkumbo alisema kwa sasa umeanzishwa mtindo wa baadhi ya wananchi kuchanganya bangi na mazao mengine ili kupoteza ushahidi.
 
“Wanachokifanya sasa wanachanganya miche ya mazao na bangi, kwa hiyo inakua pamoja tutaendelea na msako huo kila kona lengo ni kuhakikisha kunakuwa na ukomo wa kilimo hicho cha dawa za kulevya mkoani hapa,” alisema Mkumbo.

Wazee Muheza Wamlilia Rais Magufuli Mgao Wa Chakula

$
0
0
Wazee wanaoishi katika kambi ya makazi ya waathirika wa ukoma ya Misufini wilayani Muheza, wamemuomba Rais John Magufuli kuwaongezea mgawo wa chakula kwani wanachopata hakitoshelezi.
 
Walitoa ombi hilo juzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha Tumbo wakati walipokabidhiwa mbuzi, mchele na mafuta ya chakula ikiwa ni zawadi iliyotolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka.
 
Mwenyekiti wa wakazi wa kambi hiyo, Bakari Salim alisema mgawo wa makopo mawili ya sembe ambayo wamekuwa wakipewa kila mmoja kila wiki hautoshelezi.
 
Akijibu maombi hayo, Tumbo aliahidi kuyafikisha kwa wahusika na kwamba ana imani yatapokelewa na kufanyiwa kazi.
 
Alitoa wito kwa wadau na taasisi nyingine kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwalea wazee hao.

Wanawake CUF Washtuka Kutumiwa

$
0
0
Jumuiya ya Wanawake wa CUF (Juke- CUF) imewataka wanawake nchini kukataa kushirikishwa au kuwa sehemu ya utekelezaji wa mipango miovu dhidi ya chama hicho.
 
Mwenyekiti wa Juke-CUF, Fatma Abdulhabib Ferej alisema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa mwishoni mwa wiki iliyopita ikimuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
 
Chama hicho kipo kwenye mgogoro wa uongozi kati ya katibu mkuu huyo na Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.
 
Ferej alisema si busara kwa mwanamke kujiingia katika kundi ambalo kwa makusudi linaonekana kwenda kinyume na utaratibu wa sheria uliopo kuhusu vyama vya siasa nchini.
 
Alisema Juke-CUF ipo tayari kukilinda chama hicho kwa gharama yoyote na kwamba, itasimamia na kutekeleza maagizo yatakayotolewa na CUF.
 
Ferej alisema mgogoro huo umepandikizwa makusudi ili kufifisha mafanikio ya CUF yaliyopatikana katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015.

Mke wa Roma Mkatoliki Afunguka kuhusu tukio la mume wake kutekwa

$
0
0
Mke wa msanii Roma Mkatoliki, Nancy Mshana amefunguka kwa mara ya kwanza toka mume wake alipotekwa na kupatikana na kuwashukuru Watanzania ambao walikuwa pamoja na yeye katika kipindi kigumu.

Mrembo huyo ametumia maneno ya kwenye Biblia kutoka katika kitabu cha Yeremia kufikisha ujumbe wake kwa watu ambao wamemfanyia ubaya mume wake na kusema kuwa na wao watakutwa na mabaya hayo.

“(Yeremia 30:16-17) Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.Ameen” Alinukuu mke wa Roma Mkatoliki.

Mbali na hilo Nancy alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wote ambao wamesimama na wao katika kipindi hiki kigumu.

“Ahsanteni wote mliosimama na sisi katika kipindi kigumu tulichopitia !! Mungu awabariki sana” aliandika Nancy.

Msanii Roma Mkatoliki bado anaendelea na matibabu kufuatia tukio lake la kutekwa na kuumizwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Nape: Nikisema Ukweli naonekana Mkoroni, Ila haya Nimeyashuhudia Mwenyewe

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa ya moyoni kwa kusema kila anapokumbuka shida wanazozipata wananchi humfanya aonekane mkorofi kwa kuwa anasema ukweli.

Nape amebainisha hayo, kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter huku akiwa ameambatanisha na picha ambayo inaonesha wananchi jinsi wanavyopata tabu kuvuka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili kwa kupita ndani ya maji hayo.

“Niliyashuhudia maisha haya mikoani kwa miezi 38, nadhani ndiyo nikiyakumbuka naonekana mkorofi !! iko haja kama Taifa kuangalia vipaumbele vyetu”. Ameandika Nape

Maaskofu Walaani Mauaji ya Polisi na Utekaji Wananchi

$
0
0
Matukio ya utekaji watu na kupotea kwenye mazingira yasiyoeleweka pamoja na mauaji ya   polisi wanane mkoani Pwani, ni baadhi ya mambo yaliyotawala katika mahubiri ya mkesha na ibada za Sikukuu ya Pasaka katika maeneo mbalimbali nchini.

Maaskofu, wachungaji na mapadri wa makanisa mbalimbali katika ibada zao, walitumia muda mwingi kuzungumzia matukio hayo na kutahadharisha kuwa ni ishara mbaya ya kuporomoka kwa amani nchini.  

Viongozi hao wa dini wanayatazama matukio hayo kwa sura mbili, kwamba yanafanywa na binadamu walio hai na binadamu wafu ingawa ni hai.

Askofu Amani-Moshi
Katika mahubiri yake, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi mkoani Kilimanjaro, Isack Amani, alisema vitendo vya utekaji nyara, biashara ya binadamu, mauaji ya askari, ubakaji na ulawiti na mengine yanayofanana na hayo, ni dalili ya amani na utulivu wa nchi kupotea.

Akihubiri katika ibada ya Pasaka iliyofanyika kitaifa katika Kanisa la Askofu la Kristo Mfalme, mkoani Kilimanjaro, Askofu Amani alisema vimekuwapo vitendo vingi vya uhalifu vinavyoendelea kutokea nchini yakiwamo mauaji ya ukatili ya askari, utekaji nyara na unyanyasaji wa raia, hali inayoonyesha  kupotea kwa amani na utulivu nchini.

“Sasa majambazi wamefikia hatua ya kuua askari, hii ni ishara mbaya na wapo baadhi yetu wanashangilia. Inaonyesha kwamba ni makundi mabaya ya uhalifu tuliyo nayo kwenye jamii.

“Kwa lugha nyingine tunaweza kusema tunahitaji msaada kwa sababu hali si nzuri na inatishia amani, umoja na utulivu wetu.

“Amani na utulivu ni vitu ambavyo vinapaswa kuchochewa kama moto ila sasa naona mambo hayako sawa. Ni lazima wananchi pamoja na Serikali yetu tubadilike, tuichochee amani yetu,” alisema Askofu Amani.

Alisema pia kwamba kuendelea kufanyika biashara haramu ya binadamu ni jambo jingine linaloonekana kuchangia kuongezeka vitendo vya uhalifu.

“Biashara haramu ya biandamu huliingiza taifa lolote kwenye maafa mengi ya uhalifu kwa vile  watu wamekuwa wanakodishwa na kufanya uhalifu. Hivyo basi, ni lazima Watanzania tubadilike na kuishi maisha yenye staha.

“Mauaji ya vikongwe na watu wenye ualbino, ushirikina, chuki, ubinafisi na kulipiza visasi ni baadhi ya mambo yanayoonekana kuidhoofisha nchi, hivyo ni lazima Serikali na wananchi wabadilike kulinda amani na utulivu.

“Wananchi tuungane na Serikali kulaani mambo yote ya uhalifu yanayoendelea nchini, tuliombee taifa letu ili wananchi tuwe na umoja katika kupambana na matendo ya uhalifu na uovu wote, na mkumbuke amani ya taifa letu ipo mikononi mwetu,”alisema.

Askofu huyo aliwataka wanasiasa wote nchini,  waache ubinafsi kwa kufanya kazi za kuimarisha vyama vyao pekee na badala yake watumie muda huo kuwaletea wananchi wao maendeleo.

Katibu Mkuu -TEC
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Padri Raymond Sabba, alisema taifa linatakiwa kuombewa ili kuondokana na matatizo katika kipindi hiki cha mashaka ili mambo yanayojitokeza yasiendelee kutokea.

Akihubiri wakati wa mkesha wa Pasaka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Dar es Salaam, Padri Sabba alisema kwa kiasi kikubwa yanayoendelea yanatakiwa kukemewa.

Alivitaja vitendo hivyo kuwa ni pamoja na mauaji ya kutisha, watu kutekwa nyara, ufisadi, uzembe wa viongozi, dawa za kulevya na kukosekana kwa haki.

"Tuliombee taifa katika kipindi hiki ambacho inawezekana kumekuwa na mashaka yakiwamo mauaji ya ajabu kwa watu wasio na hatia kama albino, vikongwe na kukosekana kwa haki.

“Kila mtu anapaswa kutambua kuwa hayo yote ni makaburi yanayopaswa kuondolewa kwa sababu hayampendezi Mungu kwa vile pia yanadhalilisha utu wa mtanzania.

“Wanaotenda matendo hayo  wakati mwingine si wapagani bali ni wenye dini wanaojitambulisha kuwa ni wakristo wakati matendo yao hayafai,” alisema Padri Sabba.

Aliwataka wakristo kuhakikisha wanaliombea taifa katika kipindi hiki ambacho kuna mashaka juu ya mambo mbalimbali ya kutisha yanayoendelea nchini.

Askofu Sylvester Gamanywa
Askofu wa Kanisa la BCIC lililoko Mbezi Beach, Dar es Salaam, Sylvester Gamanywa, alisema matukio yanayotokea nchiniyana sura mbili.

“Hayo yanafanywa na binadamu walio hai na binadamu wafu ingawa ni hai. Kwa kifupi, yanafanyika mambo ya ajabu na ya kusikitikisha na ya kuudhi wakati mwingine.

“Huwezi kutoa uhai wa binadamu kama kitu cha mchezo. Tumeshuhudia mauaji ya polisi waliouawa Kibiti na si hao tu wameshauawa wengi. Tusishangae hayo ni matendo ya watu waliokufa kiroho.

“Kwa mateso aliyoyapata Yesu, tungeweza kuua askari wote kwa mkupuo, lakini Yesu badala ya kuua, alisamehe.

“Unapoona watu wanafanya vituko, mfano wazee wanafanya zinaa na watoto waliowazaa, hao ni wafu, wamekufa kiroho.

“Mara nyingi kifo cha roho huanzia kwenye kinywa cha mtu ambako maneno yake yanaweza kutoa majibu kama ni hai au mfu.

“Kama mtu anatoa maneno ya chuki, fitina, uchonganishi ama kupandisha watu hasira, hizo ni dalili za mauti ndani ya kinywa chake,” alisema Gamanywa.

Alisema pia kwamba  licha ya kuwapo kwa mamlaka za dola nchini, bado mambo mengi yanayotendeka kwenye jamii yanadhihirisha mamlaka zimezidiwa kutokana na kuongezeka kwa maovu kuliko nguvu ya udhibiti iliyopo.

“Mfu wa roho yuko hai mwili, lakini utashi wa kufufuka ni hiyari yake mwenyewe. Majambazi, wazinzi, waongo na wachawi, wakiamua kusema Yesu fufua roho zetu tuwe viumbe wapya tutoke katika makaburi, wote wanaweza kufufuka na polisi wakakosa kazi,” alisema.

Askofu Gamanywa pia aliwashutumu baadhi ya viongozi wa dini kwa madai kuwa wamesahau wajibu wao na kufanya kazi ambazo hawajatumwa na Mungu.

“Sisi viongozi wa roho na hapa nawazungumzia wakristo, tunatarajiwa kuleta ufufuo wa roho za watu waliokufa, lakini tunafanya kazi nyingine ambazo hatujatumwa na Mungu.

“Matamko ya kukemea na kulaani ni staili ya wanasiasa, sisi tunayo mamlaka inatoka juu. Hivyo basi, maneno yetu yanatakiwa kuwa ni habari za ufufuo kwa wenye dhambi ambazo mamlaka za kawaida haziwezi kufanya bali Yesu pekee.

“Tukihubiri watu wakaacha maovu, watafanya kazi bila kusukumwa, wataacha kazi haramu na wataacha uvivu.

“Kama viongozi wa dini watashindwa kuwahubiria watu wakaacha kutenda maovu, basi kazi hiyo itakuwa imewashinda na itabidi wajiuzuru.

“Kama wewe ni mchungaji ama askofu halafu kuna watu wanaokufuata ibadani lakini bado ni waongo, wezi, wafitinishaji, ujue kazi imekushinda.

“Kabla hatujawaambia wanasiasa wajiuzuru, tunatakiwa tuanze sisi. Mimi natangaza sijiuzuru bali nitawaambia ukweli, kwamba Yesu Kristo amefufuka ni lazima umkubali na kumwamini ili ufufuke roho.

“We must speak the truth (lazima tuseme ukweli), hata kama kuna watu wana fedha nyingi na wanatoa sadaka kubwa ni lazima waambiwe ukweli,” alisema Askofu Gamanywa.

Askofu Mkuu KKKT
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo, alisema matukio ya utekaji yanajenga hofu ya kutoaminiana ambayo si nzuri na ni hatari kwa nchi.

“Mambo haya yanahitaji uthibitishisho, hivyo ni vema uchunguzi ufanyike na ikithibitika hatua zichukuliwe kwa sababu yanazidi kuwatia hofu watu,” alisema.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gavile, alisema mauaji ya askari wanane yaliyotokea wiki iliyopita mkoani Pwani, yanasikitisha na watu wanatakiwa wafunge kwa ajili ya kuliombea taifa.

Akitoa salamu za Pasaka katika Usharika wa Kanisa Kuu mkoani hapa, Askofu Gavile alisema kazi ya wakristo si kulalamika bali ni kumgeukia Mungu na kumuomba   aliepushe Taifa dhidi ya matukio ya utekaji, mauaji na mengine.

“Kazi ya wakristo si kulalamika mtaani kama ilivyo kwa mataifa mengine bali kazi yao kubwa ni kufunga na kuomba kwa ajili ya taifa.

“Tuendelee kuliombea taifa na Mkoa wa Iringa, tuseme Mungu yatosha kuendelea kusikia matukio ya ajabu ndani ya nchi yetu,” alisema Askofu Gavile.  

Naye Askofu mstaafu wa Dayosisi hiyo, Dk. Owdenburg Mdegella, aliwataka Watanzania kuacha kupoteza muda kujadili mambo yasiyo ya msingi badala yake wajikite kujenga nchi.

Askofu mstaafu wa Kanisa la Pentekoste (FPCT) mkoani Singida, Dk. Paulo Samweli, alitoa rai kwa madhehebu ya dini nchini, kuliombea taifa  liweze kuondokana na umwagikaji wa damu kwa Watanzania wasio na hatia wakiwamo  polisi.

Akihubiri katika ibada ya Pasaka  katika Kanisa la Pentekoste mkoani humo, Dk. Paulo alisema mauaji ya polisi wanane Kibiti, Pwani hayavumiliki na kila mtanzania anapaswa kuyakemea yasijirudie.

Dk. Paulo alisema jukumu la polisi ni kulinda Watanzania wa madhehebu yote na wasiokuwa na dini na mali zao.

“Tukianza kuwaua kwa ukatili namna hii, nani atatulinda?  Wewe ukimuua   polisi  ujue wazi kuwa unajiua wewe mwenyewe bila ya kujijua.

“Unyama huu haukubaliki mbele ya Mungu na kwa Watanzania wote, tuungane kuukomesha.

“Watu wasipofanya maombi vitendo hivyo vinaweza kusambaa sehemu mbalimbali nchini na matokeo yake nchi haitakalika tena.

“Shughuli za kumwabudu Mungu kwa uhuru mpana kama ilivyo hivi sasa zitakuwa ni ngumu na kujiletea maendeleo nako kutakuwa ni shida kutokana na kuwapo   viasharia vya uvunjifu wa amani,” alisema Askofu Dk. Paulo.

CCM Yatoa Onyo kwa makada wake Wanaolalamika Baada ya Kutumbuliwa na Rais

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na kukemea vikali kauli zinazotolewa na viongozi au makada wa chama hicho wambao wametenguliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika nafasi zao mbalimbali walizokuwa wakishikilia.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga aliyasema hayo juzi akizungumza Mjini Iringa katika mkutano na wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyomo mkoani humo ambao ni wananchama na pia viongozi wa chama hicho katika ngazi ya matawi na kata.

Lubinga aliwataka makada hao walioteuliwa na kisha kutemwa na Rais Dkt Mwagufuli ambaye pia ni Mwenyeketi wa CCM Taifa, kuacha kulalamika na kupiga kelele badala yake wakubiliane na mabadiliko hayo kwa nia ya kuheshimu maamuzi ya Ikulu kwa uamuzi uliochukuliwa dhidi yao.

Licha ya kuwa kiongozi huyo hakutaja majina ya viongozi aliowataka kuheshimu maamuzi ya Ikulu, lakini ni dhahiri kuwa miongoni mwa waliolengwa ni Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Moses Nnauye ambaye alitenguliwa katika nafasi yake aliyokuwa ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nafasi aliyoitumikia kwa kipindi cha miezi 15.

Nape alitenguliwa katika nafasi hiyo ikiwa ni saa chache tu tangu alipopokea ripoti ya kuvamiwa kwa kituo cha Clouds Media Group ambapo ripoti hiyo ilithibitisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ndiye aliyehusika katika tukio hilo.

Nafasi ya Nape ilichukuliwa na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison George Mwakyembe ambaye naye nafasi yake ikajazwa na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Prof. Palamagamba Aidan John Kabudi ambaye ni mbobezi katika taaluma ya sheria.

Mwingine ambaye licha ya kuwa hakuenguliwa na Rais moja kwa moja lakini alionyesha kutoridhishwa na mchakato wa kuenguliwa kwake ndani ya CCM ni aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji. Yeye alienguliwa alipotaka kugombea kwa mara ya pili, na tangu hapo amekuwa akilalamika kwa madai  kuwa njia zilizotumika hazikuwa za haki.

“Rais anapoteua kiongozi na kumpa dhamana ni kwamba anaona kuwa unahitajika, lakini inapofika mahali amekuondoa ujue mazingira yale huwezi kuyamudu na anakuokoa ili usipate laana. Baadhi ya viongozi wameondolewa madarakani, lakini wamebaki wakilalamika mitaani ovyo.”  alisema Kanali Lubinga.

Lubinga alisema kuwa chama hicho sasa kimejikita kuhakikisha kuwa kinarejesha nidhamu na uwajibikaji ndani ya chama na serikali ili viongozi wote waliochaguliwa na kuteuliwa wafanye kazi kwa maslahi mapana ya taifa na wananchi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images