Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 6


Mwanamuziki Roma Mkatoliki akamatwa akiwa studio

$
0
0

Rapa Roma Mkatoliki ambaye hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Usimsahau mchizi' amekamatwa na kupelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana.

Katika taarifa iliyotolewa na msanii Prof. Jay ambay pia ni mbunge wa Mikumi inasema msanii huyo alikamatwa jana akiwa studio.

Prof. Jay ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na kijana mmoja wa kazi walikamatwa jana wakiwa studio za Tongwe Records.

"Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za Tongwe Records majira ya saa moja usiku na wamemchukua Roma, Moni na kijana wa kazi na pia wamechukua computer ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi" aliandika Prof. Jay

Mpaka sasa bado hajafahamika wasanii hao wamekamatwa na nani na kwa kosa gani, na pia bado haijafahamika wamepelekwa wapi. 

Lakini watu kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.

Nape Nnauye Kuanika Ukweli Wote Jumamosi Hii

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kuwa Jumamosi April 8, 2017 atakuwa jimboni kwake ambapo atazungumza na wapiga kura wake kuwaeleza ukweli wa mambo yaote yaliyotokea.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Nape Nnauye amendika kuwa, “Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi hii tar 8/4/17.”

Nape  aliondolewa kwenye nafasi hiyo wiki chache zilizopita baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi ya Saa 24 aliyoiunda kufuatia Kituo cha Clouds TV kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Nape aliahidi kupeleka ripoti hiyo kwa wakuu wake ambao ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais John Pombe Magufuli ambapo siku iliyofuata Rais alitengua uteuzi wake na kumteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape.

Spika wa Bunge Aagiza Polisi kumkamata Mbunge Halima Mdee......Mbowe nae Katakiwa Kufika Kamati ya Maadili Kujieleza

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.

Pia Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo akituhumiwa kutukana bunge kufuatia uchaguzi huo  wa EALA. 

Mwingine anayetarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka leo ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Pastory Mnyeti ambaye ameitwa na kamati hiyo  na anatakiwa kufika leo.

==>Msikilize Spika Ndugai akitoa maagizo hayo

Rais Dkt Magufuli Akutana Na Balozi Wa Israel Mhe. Yahel Vilan, Ikulu,jijini Dar Es Salaam Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalumu toka kwa Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu uliowasilishwa kwake na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na  Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan baada ya kutana naye kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017
PICHA NA IKULU

Tanzania Yang'ara viwango vya FIFA, imepanda Kwa nafasi 22

$
0
0
Tanzania imepaa kwa nafasi 22 hadi nafasi ya 135 kutoka nafasi ya 157 kati ya mataifa 211 katika viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa na FIFA leo Aprili 6, 2017.

Hivi karibuni, Tanzania katika mechi za kalenda ya FIFA, iliwashinda Botswana na Burundi katika michezo miwili tofauti zilizofanyika Machi, mwaka huu.

Katika viwango hivyo vipya vya mwezi April, Brazil imeishusha Argentina kileleni na kukamata usukani rasmi wa dunia, huku Argentina ikishuka hadi nafasi ya pili na Ujerumani imebaki katika nafasi yake ya 3.

Katika ‘top ten’, mataifa yanayofuata ni Chile, Colombia, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, Uswisi na Hispania inakamata nafasi ya 10

Barani Afrika Misri  inaongoza ikiwa nafasi ya 19 ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya 30, Cameroon nafasi ya 33,  Burkina Faso nafasi ya 35, Nigeria nafasi ya 40 na Congo DR nafasi ya 41 ikiwa mbele ya Tunisia kwa nafasi moja

Kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda bado inaongoza ikiwa imepanda kwa nafasi mbili hadi nafasi ya 72, ikifuatiwa na Kenya nafasi ya 78, Rwanda nafasi ya 117,  Ethiopia nafasi ya 124,  Tanzania nafasi ya 135 na Burundi imeshuka kwa nafasi mbili hafasi ya 141.

Wengine ni Djibouti ambayo iko nafasi ya 194 huku Eritrea na Somalia zikiwa mkiani kabisa katika nafasi ya 206

Spika Wa Bunge Job Ndugai Atoa Nafasi ya Mwisho CHADEMA

$
0
0
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetoa nafasi ya pili na ya mwisho kwa ajili ya mchakato wa kuwapata wawakilishi wawili wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Akitoa taarifa yake bungeni leo , Spika wa Bunge hilo Job Ndugai amesema hadi sasa nafasi hizo bado ni za CHADEMA na atahakikisha haki hiyo wanaipata na kwamba Katibu wa Bunge atatoa taarifa ni lini mchakato huo utafanyika.

Katika hatua nyingine, Ndugai ametoa tahadhari kwa chama hicho kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa utaratibu wa kupatikana kwa wawakilishi wa Tanzania kupitia vyama vya upinzani, hivyo endapo wasipotumia nafasi hiyo, atatumia mamlaka aliyonayo kutangaza utaratibu mwingine ili Tanzania isikose wawakilishi katika nafasi hizo.

“Ikumbukwe kuwa maamuzi haya ya kuwatenganisha wabunge wa upinzani kwa  kuangalia vyama vyao ni maamuzi ya Spika, tukumbuke mabunge yaliyopita maspika wenzangu hawakufanya hivyo, waliwaweka wabunge wote wa upinzani kwenye kundi moja, mimi nikasema twende na demokrasia hii ya wawili, ambayo katika kufanya hivyo, mimi yuleyule,....tuendelee....... Hatuwezi kukubali nchi yetu ikose uwakilishi nchi yetu ikatekwa nyara kwa sababu fulani fulani". Amesema Ndugai

Pia Ndugai amewatoa hofu watanzania kuwa hawatakosa uwakilishi kwa kuwa anajua cha kufanya. "Tutatoa nafasi ya pili, lakini baada ya nafasi ya pili, tunajua hatua itakayofuata, nawahakikishia watanzania kwamba hawatakosa nafasi katika bunge hilo”

Katika uchaguzi uliofanyika juzi, Bunge hilo liliwachagua wajumbe 7 kati ya 9 waliohitajika, huku wagombea wawili wa CHADEMA  Ezekiah Wenje na Lawrence Masha wakikataliwa kwa kupigiwa kura za hapana.

Taarifa Toka IKULU: Rais Magufuli Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa EU, Roeland Van de Geer na Balozi wa Israel, Yahel Vilan.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Aprili, 2017 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe. Roeland Van de Geer na kuushukuru umoja wa nchi hizo kwa kutoa msaada wa Euro Milioni 205 sawa na takribani Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo hapa nchini kwa kipindi cha miaka 4 kuanzia mwaka huu.

Mhe. Rais Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo kumethibitisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya na kwamba pamoja na kutoa fedha hizo umoja huo unatarajia kutoa fedha nyingine kiasi cha Euro Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuendeleza viwanda, kilimo na uzalishaji wa nishati.

“Nimefurahi sana kwamba uhusiano na ushirikiano wetu unajikita kushughulikia mambo ya msingi kwa Watanzania, nakuhakikishia kuwa fedha mnazotoa zitatumika vizuri na zitatoa mchango mkubwa katika maendeleo yetu” amesema Mhe. Dkt. Magufuli.

Nae Mhe. Balozi Roeland Van de Geer amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi wake mzuri na dhamira yake ya kujenga uchumi na kusimamia utawala bora ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, na pia amemuahidi kuwa nchi wanachama wa umoja huo zitaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Tanzania.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan na kumhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Israel hususani katika masuala ya uwekezaji, biashara, utalii na uboreshaji wa huduma za kijamii.

Mhe. Rais Magufuli amesema ili kufanikisha dhamira hiyo Tanzania imefungua ubalozi nchini Israel na amemuomba Mhe. Yahel Vilan kupeleka ujumbe kwa Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu kuwa Tanzania itafurahi kuona Israel inafungua ubalozi wake hapa nchini.

“Naamini uhusiano na ushirikiano wetu utaongeza manufaa zaidi kwa nchi zetu na watu wake, nimefurahishwa sana na taarifa kuwa watalii wataanza kuja kwa ndege moja kwa moja kutoka Tel Aviv Israel na hivi karibuni ndege yenye watalii zaidi ya 200 itakuja nchini kwetu, nawakaribisha sana watalii na wawekezaji kutoka Israel” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Mhe. Balozi Yahel Vilan pamoja na ujumbe wake amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa wamefurahishwa na ziara waliyoifanya hapa nchini iliyowawezesha kukutana na viongozi mbalimbali na ameahidi kuwa Serikali ya Israel itajenga jengo la wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Mkoani Dodoma kuanzia mwishoni  mwa mwaka huu.

Mhe. Balozi Yahel Vilan amemhakikishia Mhe. Rais Magufuli kuwa Israel itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania kwa kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa viwanda, kilimo na kuimarisha huduma za matibabu kwa wananchi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Aprili, 2017

Bungeni: Serikali Yafuta Tozo Za Mazao Ya Chai, Pamba Na Kahawa- Majaliwa

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imefuta baadhi ya tozo katika mazao ya pamba, chai na kahawa ambazo ni kero kwa wakulima ikiwemo ya sh. 450,000 iliyokuwa inatolewa na kila kiwanda cha kuchambua pamba kwa ajili ya kuchangia mbio za Mwenge.

Amesema tozo nyingine iliyofutwa kwa zao la pamba ni ada ya vikao vya Halmashauri za Wilaya ambayo ni sh. 250,000, ambapo katika zao la chai kodi ya moto na uokoaji imeondolewa na kwenye zao la kahawa, ada ya leseni ya kusindika kahawa ya Dola za Marekani 250 imefutwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 6, 2017) katika hotuba yake ya mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2017/2018 Bungeni mjini Dodoma.

Amesema kufutwa kwa tozo hizo ni utekelezaji wa ahadi ya Serikali kwa wakulima nchini ili kuwapunguza kodi, tozo na ada mbalimbali zinazochangia kuwapunguzia faida.

“Serikali pia imeboresha mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kuanzisha utaratibu wa wazi wa ununuzi wa mazao kupitia minada na katika msimu wa mwaka 2016/2017 kwenye zao la korosho, utaratibu huo umechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa bei ya korosho kwa kilo kutoka sh  1,200 hadi sh 3,800, bei ambayo haijawahi kufikiwa katika historia ya zao la korosho nchini,” amesema.

Amesema mfumo huo wa stakabadhi ghalani na utaratibu wa minada umeongeza ushindani na kuvutia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi hususan nchi ya Vietnam na nchi nyingine kuja wenyewe kununua korosho badala ya kutegemea soko la India pekee.

Waziri Mkuu amesema katika mwaka 2017/2018, Serikali itaendelea na uchambuzi wa kina wa kodi, tozo na ada zilizobaki katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kwa lengo la kuziondoa au kuzipunguza ili kumwezesha mkulima kunufaika zaidi na jasho lake na kuongeza mapato ya Halmashauri.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema Bunge lilipitisha Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016, ambayo ni muhimu katika kuimarisha usimamizi na uwajibikaji katika Sekta ya Habari nchini, ambapo Kanuni za Sheria hiyo  zimeandaliwa na tayari zimeanza kutumika.

“Natoa wito kwa wadau wa sekta ya habari kuzingatia sheria na kanuni hizo ili kuimarisha weledi katika tasnia ya habari. Aidha, nashauri wadau wa habari kujikita zaidi katika kuandika na kutangaza habari za masuala ya maendeleo na uchumi ili kuwasaidia wananchi kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda na kuboresha huduma za kijamii,” amesema.

Pia Waziri Mkuu amevikumbusha vituo vya televisheni kuweka wakalimani wa lugha katika vituo vyao. Amesema katika mwaka 2017/2018, Serikali itaendelea kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu shuleni na vifaa vya kufundishia.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kwamba Serikali imeendelea kutoa huduma pamoja na kuongeza upatikanaji wa haki na fursa kwa watu wenye ulemavu na katika kutimiza azma hiyo, amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa Kamati za Watu wenye Ulemavu zinaanzishwa katika ngazi za Mikoa, Wilaya, Mitaa na Vijiji.

Pia Serikali imeanzisha kampeni za kupinga unyanyapaa na vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye ualbino katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Simiyu, Kagera, Tabora, Kigoma, Mara, Mbeya, Katavi na Rukwa na kampeni hiyo itaendelea nchi nzima.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S.L.P 980, DODOMA
ALHAMISI, APRILI 6, 2017.

Bungeni: Billioni 1.5 Zatolewa Mikopo Kwa Vijana.

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana imetoa mikopo yenye thamani ya Shillingi Billioni 1.5 kwa vikundi vya vijana 129 katika Halmashauri mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akitoa hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato  na matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.

“Serikali inaendelea na azma yake ya kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu”’ Alisisitiza Mhe. Majaliwa.

Aidha , Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia mapato yake ya ndani zimetoa Shillingi Billioni 4.6 ikiwa ni mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi vya vijana 2,356 na hatua hizi zimekwenda sanjari na utengeji wa maeneo maalum yenye jumla ya ekari 85,603 kwa ajili ya shughuli za vijana za Kilimo, biashara ndogo ndogo, burudani na michezo.

Katika mwaka 2017/2018, Serikali itaendelea kusimamia Halmashauri zote nchini kutenga asilmia 5 ya mapato yao kwa ajili ya vijana na asilimia 5 kwa wanawake.

Bungeni: Waajiri Na Waajiriwa Zingatieni Sheria Za Kazi Kuondoa Migogoro Kazini: Majaliwa

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wito kwa waajiri na waajiriwa wote nchini kuzingatia Sheria za kazi na kuimarisha uhusiano katika kazi ili kutumia muda mwingi kufanya kazi badala ya kutatua migogoro kazini.

Ameyasema hayo alipokuwa akitoa hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.

“Niwaombe waajiri na waajiriwa kuzingatia Sheria za kazi tupunguze migogoro kazini ili tuweze kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufanya kazi” alisisitiza Mhe. Majaliwa.

Ameongeza kuwa Serikali imefanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 58 ya migogoro ya kikazi inatokana na kutozingatiwa kwa taratibu za kuachishwa kazi kwa waajiriwa.

Amezitaja Sekta zinazoongoza kwa migogoro ya kazi kuwa ni Usafirishaji,ujenzi,ulinzi,binafsi,elimu,huduma za Hotel na Viwanda.

Katika kupunguza migogoro mahali pa kazi Serikali imefanya kaguzi na kusimamia uundwaji wa Mabaraza ya Wafanyakazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi imeendelea kutimiza wajibu wake wa kusuluhisha migogoro ambapo katika kipindi cha Julai  hadi Februari  2016 jumla ya migogoro 8,832 ilisajiliwa na kati ya hiyo migogoro 3,319 sawa na asilimia 37.6 ya migogoro iliyosajiliwa imesuluhishwa.

Waziri Mkuu Bungeni: Kasema Serikali Imeunganisha Shule 417 Kwenye Mtandao Wa Intaneti........Kasema Serikali haina mzaha na rushwa , Awataka mabalozi watangaze fursa za utalii

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Viettel ya Vietnam inatekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano vijijini ambao umefanikisha kuweka miundombinu ya mtandao wa intaneti kwenye shule 417 hapa nchini.

Amesema mradi huo ambao unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2015-2017,  umewezesha pia ofisi za Halmashauri za Wilaya 123, Hospitali za Wilaya 74, Vituo vya Polisi vya Wilaya 131 na Ofisi za Posta 68 kufikiwa na mtandao huo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 6, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2016/2017 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake ukiwemo Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018

Waziri Mkuu amesema katika mwaka 2016/2017, baadhi ya kazi zilizofanyika kwenye sekta ya mawasiliano ni pamoja na ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; Mradi wa Anuani za Makazi na Postikodi; na kuanzisha huduma ya kituo cha Jamii Centre kitakachorahisisha utoaji wa huduma muhimu katika kituo kimoja. Huduma hizo ni kulipa pensheni, ankara na huduma za kibenki.

“Sekta ya mawasiliano inatekeleza Programu ya Miundombinu ya Kikanda ambayo inahusisha Mradi wa Shule Mtandao (e-school), Mradi wa Video Conference ambao unahusisha ununuzi, usimikaji na ufungaji wa vifaa vya TEHAMA katika mikoa 26 na taasisi za Serikali,” amesema.

Amesema Serikali imekamilisha ujenzi wa kituo cha kuhifadhi taarifa na mifumo ya Serikali (Government Data Centre) ambacho lengo lake ni kuimarisha usalama wa mifumo na taarifa unaoenda sambamba na uhakika wa upatikanaji wa taarifa za Serikali katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa viwanda, Waziri Mkuu amesema Serikali inahamasisha wawekezaji wa ndani na nje kujenga viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ili kujenga uchumi wa viwanda, na kwamba inatoa kipaumbele kwenye viwanda vile vinavyotumia malighafi zinazopatikana hapa nchini, vinavyotoa ajira kwa watu wengi na vinavyozalisha bidhaa zenye soko hapa nchini na nje ya nchi.

“Katika kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu kwenye uchumi wa viwanda, Serikali inahamasisha zaidi sekta binafsi ya hapa nchini pamoja na mashirika ya umma kujenga viwanda. Jitihada hizo zimewezesha mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF, PPF, LAPF, GEPF, PSPF na NHIF kuanza kufufua, kuendeleza na kujenga viwanda vipya vipatavyo 27 katika maeneo mbalimbali nchini,” amesisitiza.

Ameyataka mashirika ya umma yahakikishe kwamba mipango yao inaendana na utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa ambao dhima yake ni kujenga uchumi wa viwanda.

Akizungumzia kuhusu juhudi za Serikali kupambana na rushwa, Waziri Mkuu amesema Serikali inapambana na rushwa kwa nguvu zake zote na haina mzaha wala uvumilivu na vitendo vya rushwa.

“Hatua zilizochukuliwa kupambana na rushwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani Novemba, 2015 zimetambuliwa na mashirika ya Kimataifa yanayojishughulisha na tafiti kuhusu masuala ya rushwa duniani. Taarifa ya Shirika la Transparency International kwenye utafiti wake kuhusu mtazamo wa rushwa mwaka 2016, imeonesha kuwa viwango vya rushwa vinaendelea kupungua hapa nchini,” amesema.

Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017, Serikali iliweza kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 9.75 kutokana na operesheni zilizofanywa na TAKUKURU,

“TAKUKURU imefanya uchunguzi wa majalada 306 ya tuhuma za rushwa na kupata kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini kuendelea na mashtaka kwa majalada 104. Katika kipindi hicho, TAKUKURU iliendesha kesi 674 zikiwemo kesi mpya 182, ambapo katika kesi 97 watuhumiwa walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo au kulipa faini. Kesi 407 zinaendelea kusikilizwa mahakamani,” amesema.

Amesema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaendelea na mapambano dhidi ya rushwa hususan katika eneo la ukusanyaji mapato ya Serikali, kudhibiti matumizi ya fedha za umma, malipo hewa, matumizi mabaya ya fedha za ushirika na kuimarisha ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Serikali imefungua balozi mpya sita katika nchi za Algeria, Israel, Korea Kusini, Sudan, Qatar na Uturuki. Amesema Balozi hizo zina kazi ya kuendeleza juhudi za kuitangaza Tanzania kama nchi yenye vivutio vingi vya utalii na rasilimali zinazoweza kutumika kuvuta uwekezaji kutoka mataifa hayo ikizingatiwa utulivu na amani iliyopo nchini.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S.L. P. 980,
DODOMA,

ALHAMISI, APRILI 4, 2017.

Hotuba Ya Mhe. Waziri Mkuu Aliyoitoa Leo Bungeni

$
0
0

UTANGULIZI

  1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa Hoja kwamba kutokana na taarifa zilizowasilishwa leo katika Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI zilizochambua Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2016/2017 na Mwelekeo wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018. Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Bunge lako Tukufu limeondokewa na Wabunge wenzetu, Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani – CCM na Mheshimiwa Dkt. Elly Marko Macha, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum – CHADEMA. Pia, Taifa lilimpoteza Mheshimiwa Samwel John Sitta aliyekuwa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, nchi yetu imekumbwa na majanga na maafa yaliyosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali. Ninaomba Mwenyezi Mungu awajalie nafuu ya haraka wale wote waliopata majeraha, na kuwapumzisha kwa amani wale waliopoteza maisha, Amina! Ninatoa pole kwa familia za wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki. Pia ninatoa pole kwa Mheshimiwa Aida Khenani aliyepata ajali ya kugongwa na pikipiki wakati akitoka Bungeni. Tunamuombea apone haraka na aweze kurejea Bungeni ili kuendelea na majukumu yake.

PONGEZI NA SHUKRANI

  1. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Makamu wa Rais na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi wao. Sisi tunaowasaidia tunajivunia uongozi wao mahiri, uzalendo uliotukuka na dhamira njema waliyonayo kwa Watanzania.
  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017, Bunge lako Tukufu limepokea na kuwaapisha Wabunge wapya watano, ambao ni Mheshimiwa Abdallah Majura Bulembo (Mb.), Mheshimiwa Anne Killango Malecela (Mb.), Mheshimiwa Juma Ali Juma (Mb.), Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) na Mheshimiwa Salma Rashidi Kikwete (Mb.). Ninawapongeza sana Waheshimiwa Wabunge wapya kwa heshima waliyoipata ya kujumuika nasi kwenye Bunge hili. Kama ilivyo ada, tutatoa ushirikiano unaotarajiwa kwa Waheshimiwa Wabunge hawa ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi na tija. Kipekee, ninampongeza Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Pia ninatumia nafasi hii kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote walioteuliwa kuingia kwenye Bunge la Afrika Mashariki, Makatibu Wakuu wapya walioteuliwa na Mheshimiwa Rais yaani Profesa Kitila Alexander Mkumbo, Dk. Leonard Akwilapo, Maimuna Tarishi na Dk. Ave Maria Semakafu. Nawapongeza sana wote walioteuliwa kushika nyadhifa hizo.
  1. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuwashukuru Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kazi kubwa ya kupitia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara, Mikoa, Wakala, Idara za Serikali zinazojitegemea na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Ninawashukuru kipekee sana Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria inayoongozwa na Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa, Mbunge wa Rufiji; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini kwa kutoa mchango mkubwa wakati wa maandalizi ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Pia, niwapongeze Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kuongoza kwa umahiri mkubwa Kamati zao wakati wa kupitia makadirio ya sekta zote. Maoni na ushauri wao umesaidia sana kuboresha Makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa mafungu yote.
  1. Mheshimiwa Spika, niruhusu pia niwashukuru Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wakuu wa Idara, Mashirika na Taasisi zote za Serikali kwa ushirikiano wanaoendelea kunipa katika kutekeleza majukumu yangu. Aidha, ninawashukuru Wafanyakazi wote wa Serikali na Taasisi zake chini ya Uongozi wa Katibu Mkuu Kiongozi, kwa kukamilisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/2018.
  1. Mheshimiwa Spika, kipekee, ninamshukuru Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama (Mb.), Mbunge wa Peramiho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu); Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde (Mb.), Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana) kwa ushirikiano wao mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha, ninamshukuru Mheshimiwa Dkt. Abdallah Possi aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kazi kubwa aliyofanya wakati akiitumikia nafasi hiyo. Ninamtakia kazi njema kwenye jukumu lake  jipya la kuiwakilisha Tanzania nchini Ujerumani. Vilevile, ninawashukuru wafanyakazi wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu, chini ya Uongozi wa Makatibu Wakuu, Dkt. Hamisi H. Mwinyimvua; Bwana Eric F. Shitindi na aliyekuwa Katibu Mkuu Bwana Uledi A. Mussa kwa ushauri wao wa kitaalam kwangu na kwa Waheshimiwa Mawaziri.
  1. Mheshimiwa Spika, ninazishukuru pia nchi marafiki, Taasisi na Mifuko ya Fedha Duniani, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Madhehebu ya Dini na Mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kujenga uchumi wa nchi yetu. Misaada na mikopo iliyopatikana kwa wakati imechangia kutekeleza miradi ya maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
  1. Mheshimiwa Spika, ninapenda kutumia fursa hii kuwashukuru kwa dhati wananchi wa Jimbo la Ruangwa kwa kuendelea kuniunga mkono na kuielewa vizuri dhamana ya Kitaifa niliyonayo ya kusimamia utendaji wa Serikali katika sekta zote na kuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni. Mwisho ninaishukuru familia yangu hususan mwenza wangu mpendwa, Mary na watoto wetu kwa upendo, dua na kuendelea kunitia moyo ili nitekeleze kwa ufanisi zaidi majukumu yangu ya Kitaifa. Asanteni sana!

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 7

Mke auawa na Mumewe kwa Imani za Kishirikina

$
0
0
Mtu mmoja katika kijiji cha Solwe wilayani Kwimba mkoani Mwanza anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kutokana na imani za kishirikina.

Tukio hilo limetokea tarehe 5/04/2017 saa 5 asubuhi ambapo mtu huyo anayefahamika kwa jina la Kumalija Kondolo Basu anadaiwa kumchoma mke wake na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani na shingoni upande wa nyuma na kupelekea kifo chake papo hapo.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikuwa akiishi na mkewe nyumbani kwake kijiji cha Bagadu wilayani Magu lakini hivi karibuni alikwenda kwa wakwe zake wilayani Kwimba kuwasalimia  yeye pamoja na mkewe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alibaki nyumbani na mkewe kwani wengine walikuwa  wamekwenda gulioni  kwasababu ilikuwa siku ya gulio.

Kwa mujibu wa Kamanda Msangi, inadaiwa kuwa baada ya mtuhumiwa kuona wanafamilia hawapo ndipo alimchukua mkewe na kuingia naye ndani na kisha kutekeleza kitendo hicho.

Amesema wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa kumakamata mtuhumiwa.

Amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo amekamatwa na yupo katika mahojiano na jeshi la polisi, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani

Spika wa Bunge akutana na Rais wa TLS, Tundu Lissu

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu walipofika na Ujumbe kutoka TLS kumtembelea ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akizungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu na ujumbe wake walipomtembelea ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu akimueleza jambo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai alipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu akimuonesha kitabu chenye nyaraka kadhaa za Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai alipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akipokea kitabu chenye nyaraka kadhaa za Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS)kutoka kwa Rais wa chama hicho Mhe.Tundu Lissu wakati viongozi wa Chama hicho walipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.

Wabunge wachachamaa, wapinga vikali matumizi ya Faru Fausta

$
0
0
Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameibuka na kupinga vikali gharama za matumizi ya Faru Fausta aliyepo katika Hifadhi ya Ngorongoro, na kuongeza kuwa gharama hizo haziendani na uhalisia.

Mjadala huo uliibuka mara baada ya Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul (Chadema) kuuliza swali kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe kuhusu mipango ya Serikali kwa Faru huyo.

Aidha, akijibu swali hilo, Prof. Maghembe amesema kuwa Faru huyo anatumia gharama kubwa za matunzo kwa sababu ni mzee na huwa anaugua mara kwa mara.

“Hivi sasa utafiti unafanyika kwa kumtumia Faru Fausta juu ya namna ya kuishi na wanyama wa aina hiyo ili waweze kuishi maisha marefu, ni kweli kufanya hivi ni gharama kubwa sana,”amesema Prof. Maghembe.

Gharama za matunzo ya Faru Fausta kwa mwezi ni shilingi milioni 64, kiasi ambacho kiliwashtua baadhi ya wabunge na kutaka muongozo zaidi wa kupata taarifa za kina zaidi.

Hata hivyo, kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi ya Ngorongoro, Dkt. Fredy Manongi amesema kuwa Faru Fausta ni Mzee na ana umri wa miaka 54, hivyo alipokuwa porini alikuwa akishambuliwa na Fisi kitendo ambacho kilimsababishia vidonda vingi.

Aliyekuwa kiongozi wa Freemason Tanzania, Sir Andy Chande afariki dunia

$
0
0
Aliyekuwa  Kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy’ Chande, amefariki dunia.

Sir Chande amekuwa mwanachama wa Freemason kwa takribani miongo sita tangu ajiunge na umoja huo mwaka 1954.

Kiongozi huyo alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7, 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini mkoani Tabora.

Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii jana asubuhi.

Kulingana na taarifa hizo, kiongozi huyo alifariki dunia jijini Nairobi, Kenya alikokuwa akitibiwa.

Kiongozi huyo aliwahi kueleza kuwa alijiunga na Freemason Oktoba 25 mwaka 1954 baada ya kupitia usaili.

Aliwahi pia kutunga kitabu alichokiita kwa jina la ‘A night in Africa –journey from Bukene’ (usiku wa Afrika – safari kutoka Bukene).

Katika miaka ya 1950 ndipo alieleza kuanza kutambua kuwa Freemason  ipo katika msingi wake, ikiwa ni pamoja na sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu kiimani na kumfanya awe anavyopaswa kuwa.

Aliwahi kuelezea kanuni tatu kubwa za Freemason ikiwa ni pamoja na kumtaka mtu kuwa mkweli na mwenye maadili ambayo hasa Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili ili mwanachama awe mzuri.

Ngazi ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia sanaa na sayansi ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo katika maisha.

Ngazi ya tatu alisema kuwa unafundishwa namna ya kufurahia maisha kwa kiwango chake cha juu kwa kufuata kanuni hizo na mwisho ni upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli.

Katika masha yake aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Shaaban Robert.

Akiwa kwenye Jumuiya ya Freemason katika uhai wake, Sir Chande aliwahi pia kukutana na viongozi mashuhuri nchini kama vile Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, marais wastaafu, Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Hata hivyo kutokana na fikra zilizojengeka katika jamii, Freemason ilikuwa ikiogopwa na kutajwa tajwa na watu vibaya, mojawapo ikiwa ni kupata utajiri kwa njia isiyo ya kawaida.

Hata hivyo, hadi sasa dhana hiyo inaendelea na hakuna lililo wazi katika hili, huku katika mitandao ya kijamii kila mmoja akijadili jumuiya hiyo kadiri anavyoifahamu au kuisikia.

Histora yake
Sir Chande alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.

Alifika Tanzania mwaka 1950, alihamia Dar es salaam 1953 na kukutana na watu wengi wa bandarini, shirika la reli na mashirika mbalimbali aliyofanyia kazi.

Katika simulizi zake kadhaa, Sir Chande alisema alikutana na watu wengi ambao walikuwa wanahudhuria vikao vya Freemason, akaanza kuulizia na akajifunza mambo kadhaa kuhusu watu hao.

Wakati huo, hao watu hawakuwa huru kuzungumzia Freemason kama alivyofanya Sir Chande, hasa kabla ya vita ya pili ya dunia.

Sir Chande alisema wakati huo Freemason ilikuwa imegawanywa makundi tofauti, katika hospitali, shule, na mashirika mbalimbali na kulikuwa na kundi maalumu kwa ajili ya matajiri na wafanyakazi wakubwa wa Serikali. Ukiangalia vizuri wengi wao walikuwa ni wazungu na baadhi ya Wahindi.

Kundi la kwanza lilikuwa linaongozwa na watu wa Scotland, makundi mawili yaliyofuata yalikuwa yanaongozwa na Waingereza na kundi la nne lilikuwa linaongozwa na Wahindi ambalo ndilo Chande alilojiunga nalo. Ilimchukua miaka miwili kukubaliwa kujiunga na Freemason.

Aliapishwa rasmi mwaka 1954 akiwa na umri wa miaka 28. Kumbuka kwamba masharti ya kujiunga ni lazima uwe na umri kuanzia miaka 21.

Baada ya hapo ndipo alipanda cheo na kupewa nafasi ya kuongoza kundi au tawi la Freemason katika nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.

Akajiunga na miradi tofauti ya Freemason nchini Uingereza yakiwemo hoteli za kifahari pamoja na kupewa jukumu la kujenga hoteli mpya ya Freemason nchini Ghana kwenye Mji wa Khumasi ambayo ni ya kifahari.

Hoteli nyingine ya kifahari aliyoisimamia ujenzi wake iko Zambia.

Sir Chande anakumbukwa sana kwa kuanzisha shule ya msingi ya Viziwi Buguruni, Dar es Salaam, moja ya taasisi ambazo alizipa kipaumbele mno hadi anaingia kaburini.

Sir Andy Chande alistaafu kama kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki mwaka 2005 baada ya kuifanyia kazi kwa miaka 19, akawa hahudhurii mikutano ya nchi hizi, lakini akishiriki ile ya Uingereza kwa sababu alikuwa akiendelea kufanya kazi na mashirika ya huko.
 
Freemason ni nini?
Freemason ni taasisi kongwe, kubwa na inayotambulika kote duniani.

Pamoja na kwamba shirika hili katika muundo wake wa sasa lilianzishwa mjini London, Uingereza mwaka 1717, lakini historia yake inaelezwa kurudi nyuma katika karne ya 14.

Limekuwa likitajwa kwa kila aina ya minong’ono kiasi kuwa baadhi ya matapeli wamekuwa wakiitumia fursa hiyo kujinufaisha, ikiwamo kutoa matangazo ya kualika watu kujiunga wakilenga kukusanya fedha za ada kwa minajili ya kuwafanya wanachama hao tarajiwa kuwa tajiri, wenye nguvu na ushawishi.

Licha ya marehemu Chande na viongozi wengine duniani kuizungumzia kwa uzuri, lakini bado Freemason inabakia fumbo tata miongoni mwa watu wengi duniani wakiwamo Watanzania.

Kwa mujibu ya vitabu vya historia, Freemason kama neno linavyojieleza kwa Kiingereza, awali lilikuwa kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kwa maneno mengine.

Walikuwa wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki katika zama za kati.

Mejengo mengi ya kale kama vile makanisa, mji wa Rome, Washington DC ilisanifiwa na kujengwa na mafundi hawa ndiyo maana mengi yna alama zao.

Lakini pia vitabu vya historia vinaeleza waashi hawa kutokana na uaminifu wao, walikabidhiwa masuala ya utunzaji fedha za asasi mbalimbali kubwa hasa benki na Kanisa Katoliki.

Wakati wakijenga mahekalu, pia walitengeneza mahandaki ya kuhifadhi fedha na kuzikia.

Utaalamu wao wa ujenzi ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza kupotelea humo ndani usiweze kutoka tena.

Kwa sababu ya kuwa waashi, alama zao kubwa ni vifaa vya ujenzi kama vile pima maji.

Ikatokea kipindi ambapo hawa Freemason wanadaiwa kuasi na kuanza kujishirikisha na mambo ya nguvu za giza, utoaji kafara watu na ushirika na shetani.

Wengine wanasema walianza kuiba fedha za Kanisa Katoliki, lakini ukweli halisi haujulikani.

Kutokana na sababu hizi na nyingine ambazo ni siri kati ya Kanisa na Freemason, wakafukuzwa kutoka ukatoliki.

Ndiyo sababu ambayo inaelezwa kutokuwapo kwa maelewano kati yao na Wakatoliki pamoja na imani nyingine duniani.

Wakatoliki walianzisha shirika jingine badala ya Freemason lijulikanalo kama Jesuits.

Hata hivyo, Freemason ya sasa inaelezwa tofauti na viongozi wake wengi duniani, akiwamo marehemu Sir Chande.

Inajieleza kama taasisi ya kirafiki na kifamilia inayounganisha wanaume wenye tabia nzuri wa dini tofauti, wenye kuchangia imani moja katika ubaba wa Mungu na undugu duniani.

Utamaduni wa Freemason unaanzia wakati wa ujenzi wa hekalu la Mfalme Solomon na sherehe zake za kirafiki hutumia kazi za uashi kuashiria somo la maadili na ukweli.

Uanachama wa Freemason hauingiliani na imani ya mtu, familia au ajira yake na hivyo ni kundi lisilo la kidini wala kisiasa ambalo linakaribisha watu wa imani zote kwa malengo ya kuleta ustawi katika jamii.

Katika miaka ya 1990, Freemason ilipata changamoto kubwa nchini Kenya baada ya Rais, Daniel arap Moi kuunda tume kuchunguza watu wanaoabudu shetani, ambayo moja ya majukumu ya tume yalikuwa kuichunguza Freemason.

“Nilifika mbele ya tume hiyo mara mbili na katika nyakati tofauti kama Mkuu wa Freemason Afrika Mashariki. Nilitoa ushahidi kuhusu kazi tunazozifanya,” alikaririwa Sir Chande akisema wakati huo.

Ijapokuwa tume hiyo haikutoa majibu ya kazi waliyokabidhiwa na Rais Moi, inasemekana ilisafisha tuhuma zilizoelekezwa kwa Freemason.

“Nafurahi kusema kwamba tuhuma zile zilisafishwa zaidi na Rais aliyefuata baadaye, Mwai Kibaki ambaye katika moja ya hotuba zake, alisema Freemason imetoa mchango mkubwa sana nchini Kenya,” Sir Chande aliwahi kukaririwa akisema.

VIDEO: Mke wa Mwanamuziki, Roma Mkatoliki akielezea tukio kutekwa kwa Mumewe na jitihada alizozichukua.

$
0
0
Mke wa Roma Mkatoliki, Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Ivan, amedai yeye pamoja na ndugu zake wameshazunguka kila sehemu bila mafanikio kumtafuta mume wake ambaye ametekwa usiku wa Jumatano hii akiwa studio za Tongwe Record Masaki jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari jana jioni, Nancy alisema mara ya mwisho kuzungumza na Roma ilikuwa juzi saa kumi na mbili jioni.

“Mimi kama mke wa Roma mara ya mwisho niliwasiliana na mume wangu juzi saa kumi na mbili jioni, akaniambia anaelekea Tongwe Records kwajili ya kazi zake za kila siku. Baada ya hapo sikuwa nampata tena kwenye simu lakini nikachukulia ni kawaida tu simu imezima, nimekuja kuamka saa 7 nikapokea simu kutoka kwa rafiki yake akaniambia uko na Roma nikamwambia hapana alikuwa Tongwe, akaniambia kuna taarifa kwenye mitandanao na mimi nikaingia nikakuta hizo taarifa kama walizopata watu wengine,” alisema Nancy na kuongeza:

“Baada ya hapo nikaanza kutafuta watu wa kunisaidia, baadhi ya ndugu zangu wameangaika vituo vyote vya polisi Roma hayupo, hadi sasa hivi sifahamu yuko wapi, kwa ufupi sina ninachokijua wala ninachokifahamu. Jitihada zangu za kutafuta kwenye vituo vyote vya polisi nimemaliza,”

Alisema mume wake huyo hakuwai kumpatia taarifa yoyote kama anatafutwa na polisi wala ana tatizo na mtu yeyote.

Pia aliwaomba wadau mbalimbali pamoja na watanzania kwa ujumla kumuunga mkono katika jitihada za kumtafuta mume wake ambaye mpaka sasa hajulikani aliko.

Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro amesema kuwa wamezipata taarifa hizo na wanazifanyia kazi.

==>Msikilize hapo chini akiongea 

Mbowe Amshangaa Rais Magufuli Kwa Kumtumbua Nape Nnauye na Kumwacha RC Paul Makonda

$
0
0
Ikiwa  ni siku ya tatu ya Bunge la Bajeti, jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, limeanza kusikika ndani ya mhimili huo wa dola baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kuhoji ukimya wa Serikali juu ya tuhuma za vyeti feki, kumiliki mali nyingi zisizoendana na kipato chake yakiwamo magari ya kifahari ya aliowatuhumu kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya na matumizi mabaya ya madaraka.

Akizungumzia suala la vyeti, alisema Serikali inaendesha uhakiki wa watumishi wa umma ikiwamo vyeti vya taaluma jambo ambalo ni jema, lakini ni muhimu kazi hiyo ikafanywa kwa weledi bila kuathiri masharti ya Ibara ya 13 (1) ya Katiba ya nchi inayoonya ubaguzi wa aina yoyote kwa mtu yeyote bila kujali cheo chake, kabila lake, dini yake, elimu yake na hata jinsia yake.

“Wapo Watanzania wengi waliochukuliwa hatua baada ya kukutwa na vyeti feki, lakini cha ajabu Rais ameendelea kumkingia kifua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye anashutumiwa kutumia cheti ambacho si chake na kushindwa hata kuamuru uchunguzi wa jambo hilo ufanyike, ni kitendo cha kufedhehesha sana kwani kinawagawa Watanzania.

“Ubaguzi wa namna hiyo unalifanya kundi fulani kujisikia wanyonge na hawana haki na kundi jingine kujisikia wao wana haki zaidi ya wengine. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutenda haki katika zoezi hili la uhakiki kwani limeshaanza kuonyesha dalili za ubaguzi na upendeleo na linaweza kusababisha matabaka ya watu katika taifa,” alisema Mbowe.

Kiongozi huyo alisema kambi yake inaunga mkono vita ya dawa za kulevya, lakini hivi karibuni vita hivyo vilichukua sura mpya baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwataja hadharani watuhumiwa wa dawa za kulevya.

“Kitendo cha kuwataja watu hadharani bila ushahidi wowote, kilifanywa kibabe kwa kuwakejeli, kuwadhihaki na kwa uonevu mkubwa kwakuwa hakukuwa na ushahidi wowote na pia mahakama haikuhusishwa katika hatua za awali. Hii ina maana kwamba mkuu huyo wa mkoa aliamua kuwa hakimu kwa kutumia cheo chake kuchafua majina ya watu na haiba waliyoitengeneza kwa muda mrefu na kwa gharama kubwa.

 “Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshangazwa sana na kitendo cha Rais kuendelea kumkingia kifua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam katika matukio tofauti tofauti, huku ushahidi wa wazi ukionyesha matumizi mabaya ya madaraka na ukiukwaji wa haki za binadamu, umiliki wa mali ulio wa shaka, ikiwamo magari ya anasa ya wafanyabiashara aliowatuhumu kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, vitisho kwa vyombo vya habari, kuingilia uhuru wa habari nchini, matumizi mabaya ya rasilimali za nchi ikiwa ni pamoja na kufanya tafrija ya kutimiza mwaka mmoja kazini kwa kivuli cha kampeni ya kutokomeza dawa za kulevya.

 “Ni jambo la kusikitisha sana kuona Rais akimtoa kafara waziri wake kwa gharama ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Tunajiuliza kuna jambo gani lililojificha baina ya Rais na Mkuu huyu wa Mkoa? Tatizo la madawa ya kulevya si tatizo la mtu mmoja na wala halihitaji kufanywa kama vita ya mtu binafsi.

“Kambi Rasmi ya Upinzani inatambua Rais ana mamlaka ya kuteua na kutengua uteuzi, lakini hana mamlaka ya kumkingia kifua mtu yeyote pale anapovunja sheria za nchi, hata kama Rais ndie aliyempa dhamana. Hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani inawataka viongozi wote waliopewa dhamana kuheshimu utu na haki za kila raia.

“Ugomvi binafsi, kutofautiana kiitikadi, kiimani na hata kimtazamo kusimfanye yeyote mwenye dhamana kutumia mamlaka yake katika kumwonea mtu yeyote. Kama taifa tuna jukumu la kusimamia misingi ya utu na kuheshimiana.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inamtaka Mheshimiwa Rais kumchukulia hatua za kinidhamu Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam. Aidha, Rais aache ubaguzi katika uamuzi wa kinidhamu kwa baadhi ya viongozi wa umma, kwani hii ni kuwa na ‘double standard’ katika utekelezaji wa majukumu yake,” alisema mbowe.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images