MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
Rahab akamtazama raisi Praygod na kumkumbatia, wote wakajikuta wakimwagikwa na machozi, jambo lililo wafanya makachero wengine kuwa katika hali ya simanzi iliyo changanyikana na furaha.
Gafla Rahab akaanza kuisikia milio ya risasi masikioni mwake, alipo nyanyua kichwa chake akawaoa makachero walio mpiga risasi kwenye handaki. Macho yake gafla yakabadilika na kuzidi kuwa mekundu, akamsukuma raisi Praygod pembeni na kumrukia kachero mmoja aliye mpiga risasi, akambwaga chini na kuanza kuliminya koo la kachero aliyeanza kutapatapa akijitahidi kuutoa mkono mmoja wa Rahab ulio mkaba shingoni
ENDELEA
Kwa haraka makachero wakaanza kumtoa Rahab juu ya mwili mwa kachero anaye kabwa koo. Japo ni wanaume wa nguvu ila kijasho kilianza kuwamwagika kutoka na jinsi Rahab anavyo washinda nguvu.
Zoezi la kumtoa Rahaba likafanikiwa. Japo kachero aliye nusurika kuyaonja mauti hali yake kidogo ni mbaya. Hapakuwa na mtu aliye weza kuelewa ni kitu gani ambacho kimepata mke wa raisi. Kila mmoja akatokea kumuogopa sana Rahab, hata raisi Praygod mwenyewe hakusubutu kumsogelea karibu mke wake.
“Madam”
Priscar aliita kwa mara nyingine tena ila safari hii hakudhubutu kusogea karibu na Rahab, aliye geuza shingo yake na kumgeukia na kumtazama. Gafla Rahab akapoteza nguvu za miguu na kuanguka chini, akapoteza fahamu.
***
Japo Eddy ana uwezo wa kupambana ila si kwa idadi kubwa ya vijana wa Kijapan walio mzinguka na kumuweka kati huku kila mmoja wao akiwa na silaha ya kisu mkononi mwake.
Vijana hao wanao onekana ni wahuni wa mtaani wakatulia wakimtazama Eddy, huku baadhi yao wa nyuma wakianza kumpisha kiongozi wao akisogea mbele taratibu. Kiongozi wao ni jitu moja refu lililo jazia misuli kifuani mwake pamoja na mikononi, kwa kimo cha Eddy anamfikia mtu huyo maeneo ya kifuani na kumlazimu Eddy kunyanyua sura yake juu ili kuweza kumtazama vizuri mtu huyo.
“Wewe ni NSS(Nation Securty Service)?”
Kiongozi wao huyo alimuuliza Eddy kwa kingereza, huku likikunja kunja vidole vyake vilivyo komaa.
“Hapana”
“Umefwata nini wewe mbwa mweusi?”
Eddy akatabasamu kisha akapiga hatua moja mbele kulisogelea jitu hilo karibu kabisa na sehemu alipo simama.
“Nimekufwata wewe mbwa Malaya wa kike”
“Nini……..!!!”
Jibu hilo likamkasirisha jamaa huyo, akamshika Eddy maeneo ya mabegani, akamnyanyua juu kama futi tano na kumsukumia chini. Wapambe wake wakataka kumvamia Eddy ila likawazuia ili apambane mwenyewe.
Eddy akapunguza uzito wa koti alilo livaa, akabakiwa na tisheti nyeusi iliyo mbana vizuri mwilini mwake na kulichora vizuri umbo lake la mazoezi. Akarudi hatua mbili nyuma, akavuta kasi ya kulivamia jitu hilo. Hata kabla hajalifikia akarudishwa na teke zito la kifua lililo mrusha kurudi alipo toka.
Wapambe wa jitu hilo hawakusita kushangilia kwa kitendo alicho kifanya mkuu wao. Eddy akajizoa zoa chini alipo anguka akajipanga tena kwa mashambulizi, akalitazama jitu hilo kuanzia chini hadi juu, kisha akakunya ngumi na kujiweka sawa.
Jitu hilo likaanza kurusha makonde ambayo Eddy alijitahdi kuyakwepa kwa maana endapo konde moja kitampata mwilini mwake ni sawa yeye akimpiga jitu hilo ngumi sehemu moja ya mwili si chini ya kumi tena mfululizo.
Kadri jinsi jitu hilo lilivyo zidi kurusha ngumu ndivyo jinsi Eddy alivyo zidi kujitahidi kumkwepa hadi jitu hilo likaanza kuchoka, na jasho jingi likaanza kumwagika. Ikawa ni kazi kwa Eddy kujipatia maujiko kama wasemavyo watoto wa mtaani. Kwa maana alizitambua sehemu zenye udhaifu kwa jitu hilo. Ngumi iliyo komaa kwa mazoezi makali ya miezi mingi ya nyuma, ikaanza kutua kwenye viungio vya mikono vya jamaa huyo.
Kila lilipo jaribu kurusha ngumu ili mradi amfikie Eddy, ila ndivyo jinsi lilivyo zidi kupiga sehemu ya viungio vya mikono yake hadi ikafikia hatua likashindwa kabisa kurusha mikono yake. Likamlazimu kutumia mateke, ila hali ikawa ni hiyo hiyo, kila alipo rusha teka basi alijikuta akipigwa teke kwenye viungio vya miguu yake, taratibu likaanza kuyumba. Wapambe wake wakajikuta wakikaa kimya wengi wao wakiwa hawaamini kwamba kiongozi wao ndio huyo anaye pigika kama mtoto mdogo. Kwa mwili mkubwa wa jamaa hili likajikuta likipiga magoti yote mawili chini, huku likiwa limeorojeka twipwili tipwili.
“Ahaaaaa”
Jamaa hilo lilijikuta likipiga mayowe, huku likifumba macho, baada ya kuiona ngumu nzito ikija kuharibu pua yake. Likasubiria kwa sekunde kadhaa ngumi hiyo kutua kwenye pua yake ili isambaratike, ila haikuwa hivyo, taratibu likafumbua macho na kukutana na ngumi hiyo ikiwa imemsogelea karibu kabisa na uso wake.
“Nikubamize?”
Jitu hilo likatingisha kichwa huku woga mwingi ukiwa umemjaa, Eddy akaishusha ngumi yake, wapambe wote wakawa kimya wakikosa cha kuzungumza. Taratibu jitu hilo likainamisha kichwa chini likaishiria kwamba limemkubali Eddy. Wapambe wake nao wote wakapiga magoti na kuinamisha vichwa vyao chini wakimpa heshima Eddy.
Eddy akatabasamu kisha akaelekea alipo libwaga koti lake, akaliokota na kulikung’uta vumbi kisha akalivaa vizuri. Akaanza kupita katikati yao kabla hajawamaliza akasikia sauti ikimuita.
“Heei usiondoke kiongozi”
Jitu lile lilimsemesha Eddy kwa heshima kubwa.
“Kama hutojali tunakuomba tulifahamu jina lako”
Eddy akageuka na kulikukuta jitu hilo likisaidiwa na wapambe wake kunyanyuka kutoka chini.
“Unahitaji kulijua jina langu?”
“Eddy alizungumza huku akilifwata jitu hilo”
“Ndio”
Lilizungumza kwa kuto kujiamini sana.
“Black Shadow ndio jina langu”
“Mimi naitwa Sabogoo. U…uu unakwenda wapi?”
“Sina makazi popote mimi ninaishi”
“Basi twende kwangu ni jirani na hapa”
Sabogoo alizungumza huku akiachia tabasamu pana dharau zote alizo kuwa nazo zimeyanyuka kama barafu, heshima ikachukua nafasi yake juu ya Eddy.
***
Kazi ya kumbembeleza Sa Yoo, ilichukua masaa kadhaa, hadi akaukubali ukweli kwamba bibi yake kipenzi amefariki dunia. Kwa tamaduni za Kijapan, endapo kunatokea msiba basi nyumbani kwamfiwa ama ndugu wa mfiwa. Kutaandaliwa sehemu maalumu ambayo watu watahudhuria kumpa pole mfiwa huku picha kubwa ya marehemu iliyo pambwa kwa maua pamoja na kuwashiwa ubani pembei yake. Ikiwa katika eneo hilo.
Hivyo ndivyo ilivyo kuwa kwa Sa Yoo. Alirudi nyumbani akiwa ameongozana na Shamsa pamoja na dakari. Shamsa akajikuita akiwa na majukumu ya kuwa karibu sana na Sa Yoo. Urafiki wao wa muda mfupi tu, walijikuta kila mmoja akimpenda mwenzake hadi baadhi ya watu ambao ni watu wa karibu na Sa Yoo, wakabaki wakiwa wanamshangaa Shamsa kwani hawakujua ni wapi ametoke na ni nani katika familia ya Sa Yoo. Kwani Shamsa aliketi jirani kabisa na Sa Yoo na kila sehemu ambayo Sa Yoo alikwenda basi Shamsa yupo nyuma yake.
Msiba ukachukua siku kadhaa hadi kumalizika. Kutokana Shamsa alisha zoeana na Sa Yoo, ikawalazimu kuishi pamoja katika nyumba ambayo Shamsa amepangishiwa kwa ajili ya mapumziko yake. Furaha ya urafiki ikazidi kutawala kati yao, Sa Yoo akazidi kumtembeza Shamsa sehemu mbali mbali ndani ya Japan. Walitembelea sehemu nyingi za vivutio vya asili na vilivyo tengenezwa na binadamu.
“Hivi Shamsa huwa unapendelea kutazama mchezo wa mapambano?”
Sa Yoo alimuuliza wakiwa ndani ya gari lao wakirudi kutoka kwenye jengo la mauonyesho ya mashujaa walio pigana vita ya kwanza na yapili ya dunia.
“Ndio napenda kutazama”
“Basi leo usiku tutaelekea kwenye ukumbi mmoja unaonyesha mapambano ya ulingoni”
“Sawa ila hakuna fujo?”
“Hapana hakuna fujo kila kitu huko kina ulinzi wa kutosha. Tena ngoja tupitie kwenye ukumbi huo tununue tiketi mapema za kwenda kwenye maonyesho”
“Hakuna tatizo”
Ndani ya dakika kumi Sa Yoo akasimamisha gari kwenye moja ya ukumbi mkubwa wenye mapicha picha mengi ya mapambano yatakayo fanyika usiku wa siku hiyo. Idadi ya watu wanao nunu tiketi katika siku hiyo ni kubwa sana.
“Huyu BLACK SHADOW ni nani?”
Sa Yoo alimuuliza mmoja wa wauzaji wa tiketi baada ya kuona picha kubwa ya mpiganaji huyo, aliye valia kinyago cheusi usoni mwake na kuyaacha macho yake tu.
“Huyu ni mpiganaji mwengine mpya kabisa anazaminiwa na Sabogoo. Nasikia kwamba huyu jamaa ni mkali sana japo sijawahi kumuona na mimi”
Muuza tiketi huyo alizungumza kwa shauku iliyo zidi kuwatamanisha Sa Yoo na Shamsa. Wakanunua tiketi mbili za siti za mbele kabisa kisha wakaondoka kurudi nyumbani wanapo ishi kujiandaa kwa ajili ya usiku.
***
Eddy hakuwa na jinsi ikamlazimu kukubaliana na Sabogo kujiunga katika kikosi chake, ambacho mara nyingi kinajishuhulisha na maswala ya upambanaji wa ulingoni. Eddy kutokana anatafutwa na polisi wa Japani, ikambidi atumie kikundi hicho kama sehemu ya kujihifadhia huku akiendelea na upelelezi wake wa maeneo kuweza kutafuta sehemu ambayo alipaswa kwenda kukutana na mwalimu ambaye angeendelea kumfundisha mafunzo ya upiganaji.
“Ila kabla sijaingia ulingoni na kupambana inabidi tukubaliane mambo mawali”
Eddy alizungumza akiwa na Sabogo kwenye ndani ya ofisi zikiwa zimebakia siku chache kabla mashindano ya kumtafuta mpambanaji wa ulingoni ndani ya Japan hayajaanza.
“Mambo gani tena kiongozi”
“Nahitaji kwa kila pambano munilipe asilimia ishirini ya pesa ambayo nitashinda. Mbili nitahitaji kuwa na mavazi ambayo ni meusi na yenye kinyago cheusi sihitaji sura yangu kuweza kuonekana na watu wa aina yoyote”
“Hayo yote mawili hayana tatizo nakuahidi kiongozi kila jambo litakwenda vizuri, swala la mavazi kuna mwana mitindo nitamuita sasa hivi aje akupime kisha leo leo hii hii mambo yatakwenda safi”
“Sawa”
Sabogo akampigia simu mwanamitindo anaye tengeneza nguo za wapambanaji katika maonyesho hayo makubwa ndani ya Japan. Akaifanya kazi hiyo ndani ya masaa kadhaa ambapo nguo imare za Eddy zikamalizika kutengenezwa huku kinyago chake anacho kivaa kichwani mwake kikimkaa vizuri kabisa hadi mwenyewe akajikubali.
“Unaonekana vizuri kiongozi”
Sabogoo alimsifia Eddy baada ya kumuona akiwa amevalia mavazi hayo, yenye maandishi makubwa mngongoni BLACK SHADOW.
“Huyu jamaa ni mtaalamu sana”
“Ndio maana nikaamua kumpa tenda yeye, na endapo utafanya vizuri basi nguo zako zinaweza kutengenezwa nyingi na kuuzwa kwa watu wa kila rika. Ukajikuta ukiingiza pesa nyingi sana”
“Kweli?”
“Ndio huku kwetu kila jambo zuri basi ni fursa ya kuingiza pesa”
“Basi nitahakikisha ninafanya kazi nzuri kadri ya uwezo wangu”
Siku iliyo fwata wakaelekea kwenye studio za kupigia picha ambapo, Eddy akapiga picha zipatazo mia moja, akiwa amevalia mavazi yake hayo, na picha hizo zikapelekwa moja kwa moja kwa waandaaji wa mashindano hayo makubwa kwa ajili ya matangazo.
Siku na masaa yuakakatika, watu wengi ndani ya Japan, wakiisubiria siku ya mashindano ya mapambano ya ulingoni. Vituo vingi vya redio na televishion, vikazidi kutangaza juu ya mashindano hayo ambayo yana zawadi kubwa kwa mshindi, ikiwemo mkanda wa dhahabu wenye dhamani ya dola za kimarekani milioni ishirini.
Watu wengi kutoka maeneo mbali mbali ya Japan wakaanza kuingia kwenye ukumbi mkubwa unao ingiza watui zaidi ya laki sita kwa wakati mmoja, tiketi nyingi sana ziliuzwa majira ya asubuhi na mchana, wengi wakiwa na hamu ya kwenda kumuona mpiganaji mpya black shadow, ambaye anadhaminiwa na mpiganaji mbabe Sabogo, ambaye amewashangaza watu wengi sana kuto kushiriki katika mapambano hayo, na kusimamisha mtu mwingine kabisa.
Kila mmtu alisikika akisema yake, wengine wakidai labda Sabogo amestafu kupigana, wengine wakidai labda ameishiwa kutokana na kupoteza pambano la fainali mwaka jana na mpinzani wake ajulikanaye Young Poo.
Eddy na wapamba wake Sabogo, wakaingia ndani ya jengo la mapambano, kupitia mlango wa nyuma ili asionekane na watu wengi akiwa amevalia mavazi yake ya kazi. Wakaelekea kwenye vyumba maalumu vya wapambanaji, wakakuta chumba chake kikiwa kimendaliwa vizuri na Sabogo akiwa na baadhi ya wadhamini wezake.
Akamtambulisha Black Shadow kwa wazamini wezake na kutoa majigambo mengi kwamba lazima mtu wake ataibuka mshindi na kuchukua mkanda, huku mamilioni ya dola ya ushindi yakiingia mikononi mwake.
“Kiongozi namba yako ya ushindani ni kumi na mbili”
Sabogo alimumbia Eddy huku akimpa kikaratasi mkoni mwake chenye namba.
“Sawa”
“Ukiingia usiwasikilize mashabiki, wewe hakikisha kwamba unacheza na mpinzani wako. Natambua mashabiki wako humu ndani ni wachache haswa ni hawa vijana wangu”
“Usijali kwa hili kila kitu kitakwenda poa”
“Nakuaminia”
***
Sa Yoo na Shamsa hawakupoteza muda baada ya kurudi nyumbani, wakaingia bafuni na kuoga kisha kila mmoja akavalia vazi ambalo anaona linaweza kumtoa kutona na umbo lake alilo jaliwa na Mungu. Kila mmoja alionekana kuwa katika hali ya kupendeza sana, walipo jitazama kwenye kioo kikubwa kilichomo ndani mwao kila mmoja alijikuta akimsifia mwenzake kwa alivyo pendeza.
Wakatoka hadi nje, ila Shamsa akarudi ndani alipo isahau simu yake. Akaingia chumbani kwake na kuichukua simu yake, akakuta pia wamesahau kuizimi tv kubwa iliyomo ndani ya chumba chao. Akiwa anaangaza macho yake huku na kule kuitafuta rimoti ya kuzimia tv hiyo, taarifa ya habari ikaonyesha picha ya Eddy kwamba bado anaendelea kutafutwa na polisi.
Mwili wa Shamsa ukawa kama umeingiwa na ganzi alipo isikia taarifa hiyo. Hakujua ni wapi alipo Eddy, hakujua ni kwa nini anazidi kutafutwa na polisi wa nchi ya Japani. Honi ya gari kutoke nje, ikamstua na kumtoa katika hali hiyo ya kujiuliza maswali mengi, kwa haraka akaizima tv na kutoka zake nje, akaingia ndani ya gari na wakaondoka zao.