Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Simu yamponza binti aliyejirusha baharini

$
0
0
Msichana mmoja (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa mika 16 na mwanafunzi wa kidato cha 3 huko Zanzibar, juzi alijitosa baharini katika eneo la Chumbe kutoka katika boti ya Azam Marine Kilimanjaro V.

Msichana huyo aliyekuwa akisafiri na mjomba wake kutoka Dar es salaam kwenda Unguja alijirusha baharini majira ya saa 5 na kuokolewa na mabaharia wa boti hiyo ndani ya muda mchache.

Wanafamilia wa binti huyo waishio eneo la Kikwajuni Unguja walieleza kuwa kabla ya kutoroka kwa binti huyo, walimkuta na simu ambayo hawakufahamu alikoipata. Kutokana na utaratibu wa familia hiyo ya kutoruhusu simu kwa watoto, walimnyang’anya simu hiyo na kumtaka aeleze alikoitoa vinginevyo watampeleka Polisi. Binti huyo alikasirishwa na kitendo hicho ndipo alipofanya uamuzi wa kutoroka.

Mama mdogo wa binti huyo alieleza kuwa walimtafuta binti huyo bila mafanikio ndipo walipoamua kuipekua simu aliyokuwa akiitumia na kukuta namba ya kijana mmoja iliyokuwa imetumiwa mara nyingi. Walipowasiliana na kijana huyo kumuuliza anafahamiana vipi na yule binti, alijibu kuwa walijuana kupitia mtandao wa ‘facebook’ lakini hawajawahi kukutana kwa kuwa binti anaishi Zanzibar na kijana anaishi Dar es Salaam.

Alisema walimpa taarifa kijana huuyo kuwa binti yao ametoroka na hajulikani alikokwenda, hivyo kumwomba kusaidiana kuhakikisha wanampata akiwa salama.

“Kwa kweli kijana huyo alikubali kutoa ushirikiano na akawa anawasiliana na binti yetu na kumuleza kuwa yuko Dar es Salaam na amehifadhiwa na dereva teksi baada ya kukosa msaada wa eneo analotaka kwenda ambako ni kwa bibi yake anayeishi Mburahati, Dar es Salaam” alisema

Alisema aliwasiliana na dereva huyo aliyemuhifadhi binti yao na kuambiwa kwamba amesharipoti katika serikali ya mtaa anoishi kuwa amemuokota binti huyo bandarini , Dar es salaam baada ya kukaa kwa muda mrefu bila ya kupata msaada.

Mama mdogo ambaye ndiye aliyemlea binti huyo tangu akiwa mdogo alieleza kwamba mama mzazi wa  binti huyo anaishi Muscat, Oman, na alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kupata taarifa kuwa binti yake amejitupa baharini wakati akitokea Dar es Salaam baada ya kusakwa kwa siku kadhaa na hatimaye kupatikana.

Naye mjomba wa binti huyo ambaye ndiye aliyekwenda Dar es Salaam kumchukua, alieleza kuwa wakiwa ndani ya boti binti alilalamika kuwa anajisikia vibaya, hivyo anahitaji kwenda kukaa kwenye veranda ya boti ili apunge upepo. Wakatoka kwenda kwenye veranda nje ya boti hiyo.

Wakiwa wamekaa binti huyo alimtaka mjomba wake kumpatia kitambaa cha kufunika uso ‘nikabu’ na baibui avae ili kuepuka usumbufu wakati wa kushuka kwani muda wa kufika Zanzibar ulikuwa umekaribia.

Mjomba alipogeuka upande wa pili ili kuvichukua vitu hivyo  katika begi, ndipo ghafla msichana huyo alijitosa ndani ya bahari.

“Nilipiga yowe baada ya kuangalia na kumwona. Tulishirikiana na mabaharia wa boti hiyo  ili kumwokoa na ndani ya muda mchahe tulifanikiwa”  alisema

Wanafamilia wa binti huyo walisema binti huyo alikuwa na tabia nzuri tokea alipokuwa mdogo, na mara nyingi alipendelea kukaa ndani. “Hatujui kwa nini amliamua kufanya uamuzi huo”

Aidha daktari Suleiman Abdul, Mratibu wa huduma za afya Hospitali ya Kidongo Chekundu alikotibiwa msichana huyo, alisema wanaendelea na uchunguzi wa afya ya akili ya msichana huyo na kuwataka wanafamilia yake kutokuzungumzia chochote kuhusu tukio hilo na waendelee kushirikiana nae vizuri ili kuona maendeleo ya afya yake.

Jibu la Wema Sepetu baada ya Harmorapa kumtamani kimapenzi

$
0
0
Muigizaji na kada wa CHADEMA, Wema Sepetu  amemtaka msanii asiyekaukiwa matukio mitandaoni Harmorapa kuacha mara moja kumtumia kama ngazi katika  kutafuta riziki zake bali amuheshimu kama dada na msanii mwenzake.

Wema amecharuka katika mtandao wake wa instagram  leo ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii huyo anayetamba na ngoma ya 'Kiboko ya mabishoo' kutangaza kuwa anampenda msanii huyo na kwamba anaumizwa na jinsi watu wanavyomuumiza kimapenzi.

Aidha mwanadada huyo amemtaka msanii huyo kupigana jinsi atakavyoweza kulifikisha jina na muziki wake juu pasipo kumtumia yeye kama njia na kuongeza ni kumvunjia heshima mbele ya familia, chama, marafiki pamoja na mpenzi aliyenaye.

"Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi siyo wa aina hiyo". aliandika Wema.

Katika kuonesha kuwa muigizaji huyo amekerwa na kauli ya Harmorapa, ameongeza kwamba  "Do u think na mimi ni wa aina hiyo? Usinidharaulishe.... Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one butan not for you and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako lets stop there"
Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi sio wa aina hiyo. Usiiharibu image yangu niliyoipigania muda wote, usiniharibie heshima yangu ninayoijenga sasa ktk chama changu CHADEMA, usiniharibie kwenye familia yangu, marafiki zangu na usiniharibie kwa niliye nae. Ni utoto na ujinga kuposti kila uchao picha za wanawake eti wanakutaka au unatoka nao *DO U THINK NAMI NI WA AINA HIYO?* Usinidharaulishe.... Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one but *AM NOT FOR U* and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako *LETS STOP THERE*
A post shared by Wema Sepetu (@wemasepetu) on

Rais Magufuli Aapisha Makatibu Wakuu, Mabalozi Na Kamishna Wa Tra Ikulu, Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha viongozi aliowateua kushika nyadhifa mbalimbali.

Hafla ya kuapishwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Dkt. Magufuli amemuapishwa Dkt. Leonard Douglas Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Prof. Kitila Alexander Mkumbo ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Dkt. Ave Maria Emilius Semakafu ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mhe. Baraka Haran Luvanda ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

Mhe. Sylvester Mwakinyuke Ambokile ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Dkt. Ave Maria Semakafu kuwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es salaam April 5,2017

Bw. Charles Edward Kichere ameapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Aidha, Viongozi hao wamekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Katibu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Waziri Yahaya Kipacha.

Akizungumza baada ya kuapishwa kwa viongozi hao, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapongeza kwa kuteuliwa kushika nyadhifa hizo na amewataka kufanya kazi kwa kutanguliza maslai ya Taifa na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

“Tutawapa ushirikiano wote mtakaouhitaji ili kufanikisha kazi zenu lakini na nyinyi msituangushe, Bw. Kichere tunakutegemea ukaimarishe ukusanyaji wa mapato pale TRA na pia ukawaambie maafisa wako na mameneja wa mikoa waache kutoa kauli za kuigombanisha Serikali na wafanyabiashara, wakusanye kodi kwa kufuata sheria na taratibu na pia wawe na lugha nzuri.
 
“Prof. Kitila Mkumbo tunategemea utaongeza msukumo kutatua matatizo ya maji, utasaidia kufanikisha kampeni ya kumtua Mama ndoo ya maji, Watanzania wapate maji safi na salama” amesema Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Video: Maneno ya Prof. Kitila Mkumbo baada ya kuapishwa na Rais Magufuli Leo

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 05 Aprili, 2017 amewaapisha viongozi aliowateua kushika nyadhifa mbalimbali.

Hafla ya kuapishwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Moja ya viongozi walioapishwa ni Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Prof. Mkumbo aliyekuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mmoja wa wanachama wa chama cha ACT Wazalendo, baada ya kuapishwa aliongea maneno machache akimshukuru Rais Magufuli kwa kuuona umuhimu wake na kumteua kuwa katibu katika wizara hiyo.

Aidha amemuhakikishia Rais kuwa ataifanya kazi yake kwa weledi mkubwa na taifa litarajie matokeo makubwa katika utendaji wake.

“Kazi yetu na jukumu letu kubwa ni kuhakikisha kuwa sera ya umwagiliaji tunaitekeleza” alisema.

Vilevile aliongeza kuwa katika maisha yake yote akiwa mhadhiri, amekuwa ni mtu wa kuhoji maswali mbalimbali kwa serikali ili kuhakikisha kuwa wanafanya kazi yao kwa weledi.

“Maisha yangu yote mpaka hapa nilipo nimetumia muda wangu mwingi kuhoji na kuuliza maswali hasa kwa serikali. Nimepata fursa sasa ya kushiriki kikamilifu, badala ya kuhoji nina kazi ya kujibu maswali ya serikali. Mh rais nakuahidi kuwa nitajibu hoja mbalimbali za serikali”  alisema.

Viongozi wengine walioapishwa leo ni pamoja na Dkt. Ave Maria Emilius Semakafu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Baraka Haran Luvanda kuwa Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Sylvester Mwakinyuke Ambokile kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na Bw. Charles Edward Kichere kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Hapa chini ni video ya Prof. Kitila Mkumbo akiongea Ikulu jijini Dar es salaam leo mara baada ya kuapishwa na Mh. Rais Magufuli.

Mbowe: CCM Hawawezi Kutuchagulia Viongozi Wetu

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe amekitaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuacha kuwachagulia viongozi.

Kauli hiyo imekuja baada ya jana bunge kupiga kura za hapana kwa wagombea wa CHADEMA ambao walipaswa kuwa wawikilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki na kusema wapende wasipende nafasi hizo mbili za CHADEMA zipo pale pale, huku akitangaza kuwa chama hicho kitakwenda mahakamani kudai haki.

"CHADEMA tutakwenda kuitafuta haki pengine, kama taifa tungetegemea kupata wawakilishi na tuwe tumemaliza uchaguzi huu wa kuwapata wawakilishi wetu kwenye Bunge la Afrika Mashariki, lakini ndiyo kwanza kwa matokeo haya na kwa utaratibu huu wa upindishaji wa sheria za uchaguzi, tutakwenda mahakamani, tutaitafuta haki hii mahali pengine" alisema Freeman Mbowe

Mbali na hilo kiongozi huyo amesema ni jambo lisilowezekana kwa chama kimoja kuwapangia wapinzani 
 
"Ni aibu kwa taifa kwamba chama kimoja kinataka kutafuta na kupitisha mgombea wa chama kingine cha upinzani, haiwezekani na haikubaliki, Spika amevunja kanuni za Bunge, sheria hazikuheshimiwa, ubabe umetumika lakini kwetu sisi ni sehemu ya mchakato wa demokrasia tutaendelea kuitafuta haki yetu". Alisema Mbowe

Kuhusu nafasi zao, Mbowe amesema, "Nafasi mbili za Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki wapende wasipende ni za CHADEMA, tutakaa tutashauriana, hawawezi kueleza sababu za msingi za kuwakataa wagombea wetu. Kwa sababu wagombea wetu wana sifa, lakini tunajua huu ni mkakati wa CCM , Rais anahusika, Waziri Mkuu anahusika na viongozi wao wanahusika. Wanatumia Sheria gani kutuchagulia wapinzani wawakilishi wetu katika Bunge la Afrika Mashariki?" Alihoji Mbowe. 

Dkt. Boniface ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI)

Mbasha Asimulia Jinsi Flora Alivyomsaliti na Kuzaa Nje ya Ndoa

$
0
0
Muimbaji wa nyimbo za injili madam Flora (Zamani Flora Mbasha) amekiri kupata mtoto nje ya ndoa yake na aliyekuwa mume wake Emmanuel Mbasha ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za injili. Imefahamika.

Hilo limefichuliwa leo na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha, alipokuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV .

Ishu hiyo imeibuka baada ya mmoja kati ya watu waliouliza maswali, kumtaka Mbasha kunyoosha maelezo kuhusu mtoto wa pili wa Flora kama ni wake ama la, na ndipo Mbasha akaweka wazi kuwa mtoto yule si wake, na Flora mwenyewe alishakiri suala hilo.

Mbasha amesema kuwa, Flora alikiri suala hilo hivi karibuni wakiwa katika harakati za kuachana kwa mujibu wa sheria mahakamani, ambapo ilipofika wakati wa kutaja idadi ya watoto aliozaa naye, Flora alimtaja mtoto mmoja pekee ambaye ni Elizabeth (akiwa ni mtoto wao wa kwanza)

"Yule mtoto siyo wangu, hata katika hati ya mashitaka ya kuachanishwa na mahakama, yeye mwenyewe Flora kwa mkono wake akiwa na wanasheria wake, aliandika kwamba kwa kipindi chote ambacho aliishi na mimi alibahatika kupata mtoto mmoja pekee ambaye ni Eliza, kwahiyo mpaka hapo unajua kabisa kwa hapa imeshakula kwangu, ni kitu ambacho kinauma sana, lakini kila mtu na ujasiri wake" Alisema Mbasha.

Kuhusu uamuzi aliouchukua baada ya kuthibitishiwa hilo, Mbasha amesema "Nilipojua siyo wa kwangu nilikaza moyo, nikasema basi Mungu ana makusudio yake, lakini kama ningeichukulia kibinadamu, ningeushangaza ulimwengu na dunia"

Kuhusu uwezekano wa kurudiana na Flora, Mbasha amesema kuwa yeye na Flora mapenzi yao yalishakwisha kutokana na mwenza wake huyo kuamua kuanza maisha mapya na kumuacha yeye.

Wakati akijibu moja ya swali kutoka kwa shabiki aliyetaka kujua ni jambo gani lililopelekea yeye kuachana na mkewe Flora Mbasha ndipo hapo Mbasha alifunguka na kusema yeye hajamuacha mkewe, bali mkewe ndiye alimuacha yeye kwa kumsaliti na mtu mwingine kwa sababu za kimaslahi na tamaa kutokana na umaarufu uliowafanya waweze kuonana na watu wengi wenye uwezo wa kila aina kifedha ikiwemo viongozi wa serikali na wafanyabiashara.

"Mimi siwezi kusema nilimuacha mke wangu, bali mwenzangu tayari alikuwa na maisha mengine yaani tayari alikuwa na njia zake na alishakuwa amefanya maamuzi na kuamua kwenda na njia ambayo yeye aliona ni sahihi na kuendelea na maisha yake. Hivyo alinisaliti kwa sababu ya maslahi na kwenda kwingine ambako anaona ni sehemu sahihi kwake" alisema Mbasha

Msanii huyo anakiri kuwa kitendo hicho kilimuumiza sana na kumtesa lakini yeye alimtumaini na kumuomba Mungu kwani hakutaka kuvuta bangi, au kunywa pombe ili kuondokana na 'stress' bali alimuomba Mungu na Mungu alimsaidia kupita katika kipindi hicho kigumu.

Kuhusu kuoa tena, Mbasha amesema hana mpango wa kuoa kwa kuwa hajapata mtu wa kuoa, hivyo ameamua kubaki 'single boy'

Katika hatua nyingine amesema hawezi tena kwenda wala kuhudhuria ibada katika Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima baada ya kukosana na mtu mmoja ambaye hajamuweka wazi, na kwamba sasa amerudi kwenye kanisa lake la zamani, la EAGT.

Jela miaka minne kwa kufukua kaburi la albino Mbeya

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Mbeya imewahukumu watu wawili kila mmoja kifungo cha miaka minne jela na kulipa faini ya Sh2.3 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa kula njama na kufukua kaburi la marehemu aliyekuwa na ulemavu wa ngozi (albino). 

Washtakiwa hao wakazi wa Mbalizi walifukua kaburi la Sister Sisara (38) aliyefariki dunia mwaka 2008 na kuzikwa katika Kijiji cha Mumba, Kata ya Ilembo wilayani Mbeya.

Hakimu Rashid Chaungu aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Jonas John (28) na Hazore Ezekia (33). Akitoa hukumu, Chaungu alisema Mahakama imeridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka uliowasilisha mashahidi watano. 

Alisema katika kosa la kwanza kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka miwili jela na kulipa faini ya Sh1 milioni. 

“Katika shtaka la pili, kila mmoja atalipa faini ya Sh1 milioni na kutumikia kifungo cha miaka miwili jela. Kwa sababu ya maelezo ya mashahidi wa upande wa mashtaka mlisababisha usumbufu kwa familia, mtailipa Sh300,000 kila mmoja,” alisema Chaungu. 

Awali, walipopewa fursa ya kujitetea kabla ya adhabu kutolewa, John alisema amelelewa katika mazingira ya uyatima na ana familia, hivyo aliomba asamehewe.

Ezekia alidai ni mgonjwa mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na anatumia dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo, na kuomba asamehewe. 

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Bernadetha Thomas aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo. 

Baada ya hukumu kutolewa, Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (Tas), mikoa ya Songwe na Mbeya, Claud Mwakyoma aliiomba jamii ishirikiane na vyombo vya dola kuwafichua watu wenye imani potofu za kuamini kuwa viungo vya binadamu vinaleta utajiri badala yake wafanye kazi halali. 

Bonventura Mwalongo ambaye ni mjumbe wa kamati ya kushughulikia changamoto za albino nchini, alisema chanzo cha matukio hayo ni ramli chonganishi zinazofanywa na baadhi ya waganga wa jadi. 

Katibu wa Tas, William Simwali ambaye ni kaka wa marehemu Sisara, alisema Serikali inatakiwa kusimamia zuio la waganga wa jadi kujitangaza kwa kuweka mabango. 


Utafiti Waweka Hadharani Mafanikio na Kasoro za Elimu Bure Nchini

$
0
0
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Haki Elimu unaonesha kuwa fedha za ruzuku kwa ajili ya elimu bure zinazopelekwa mashuleni hazizingatii idadi ya wanafunzi kama ambavyo inapaswa kuwa jambo ambalo limekuwa likiwapa wakati mgumu walimu wakuu mashuleni.

Akitoa matokeo ya utafiti kuhusu mpango wa serikali wa kutoa elimu bure Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, Bw. John Kallaghe amesema asilimia 95 ya walimu wakuu waliohojiwa walikiri kuwa fedha za ruzuku wanazopata hazitoshi na kushauri serikali ifanye jitihada za makusudi kuhakikisha inapeleka fedha hizo kwa wakati na kwa kuwashirikisha na wadau wa maendeleo.

Bw. Kallaghe amesema uchambuzi wa tafiti umeonesha kuwa baadhi ya shule zenye wanafunzi wachache zinapata fedha zaidi kuliko shule zenye wanafunzi wengi hali inayoashiria kutokuwa na mpangilio mzuri wa utoaji ruzuku hiyo.

Utafiti huo ulifanyika katika wilaya 7 zilizowakilisha kanda nchini nazo ni Korogwe Muleba Tabora M, Njombe , Mpwapwa, Kilosa na Sumbawanga, na kuonesha kuwa asilimia 93 ya fedha za ruzuku zilizotarajiwa shuleni zilifika.

Kwa upande wake mmoja wa watafiti wa ripoti hiyo Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. Richard Shukio, amesema japo sera ya elimu bila malipo imesaidia kuongezeka kwa uandikishaji wanafunzi hasa wa darasa la kwanza, serikali ichukue hatua za makusudi kushughulikia changamoto zilizopo za elimu.

==>Baadhi ya dondoo za matokeo ya utafiti huo
  1. Wakuu wa shule wanakubali kuwa elimu bure imepunguza mzigo kwa familia maskini.
  2. Elimu bure imewaongezea walimu mzigo wa kufundisha na wanataka nyongeza ya malipo kwa majukumu ya ziada.
  3. Nusu ya wazazi wamesema kwamba licha ya kuondolewa kwa ada bado wanaendelea kuchangia michango mbalimbali shuleni.
  4. Gharama anazoingia mzazi ni zaidi ya mara kumi ya kiwango cha shilingi 6,000 kwa mwanafunzi kinachotolewa na Serikali kuendesha shule.
  5. Mzazi mwenye mtoto katika shule ya sekondari ya bweni hutumia kiasi shilingi 250,000 katika mwaka wa kwanza.
  6. Asilimia 95 ya shule zilizoshiriki wamesema kiasi cha pesa kilichopelekwa hakikidhi mahaitaji ya shule
  7. Asilimia 93 ya kiasi cha fedha za ruzuku kilichotarajiwa kilifika shuleni.
  8. Elimu bure mesaidia kuondoa migogoro kati ya walimu na wazazi kwa sasa kwani watoto hawarudishwi tena nyumbani kuchukua michango
  9. Zaidi ya asilimia 80 ya washiriki wamesema kuwa elimu bure imewapunguzia wazazi mzigo wa michango ya mara kwa mara.
  10. Kufutwa kwa ada ya shule sio kigezo cha ongezeko la wanafunzi kutoka katika familia zilizotengwa na zenye mazingira magumu
  11. Wakuu wa shule wanne kati ya watano wanaamini kuwa elimu bure italeta madhara katika maendeleo ya taaluma ya mwanafunzi
  12. Mwalimu mmoja kwa kipindi cha elimu bure anafundisha wanafunzi 164 ukilinganisha na uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 99 mwaka 2015.

Je, Umeathiriwa na Punyeto Kiasi cha Kushindwa Kurudia Tendo la Ndoa???.....Bofya Hapa Kupata Tiba, Pia Tuna Handsome Up ya Kuongeza Maumbile

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETIC ni kampuni inayotoa bidhaa ORIGINAL zenye matokeo mazuri bila kemiko wala madhara yoyote. Pata punguzo la bei kwa bidhaa hizi. 
 
1.HANDSOME UP ni kifaa kinachoongeza maumbile ya kiume  kwa 99% kwa size uipendayo wewe na kuimarisha misuli ya uume kwa @170,000/= tuu. 
 
2.MEN GELY kupaka. Hii inaongeza kwa wastani wa inch 6.5 na inapatikana kwa @120,000/=.  
 
3. MAX MAN 2. Ni vidonge kwa ajili ya nguvu ambavyo vinasaidia sana hata kwa watu wenye kisukari na waliokua wakifanya sana masturbation. Pia huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa @130,000/=tu.     
 
Tupo DAR ES SALAAM  kariakoo na kinondoni kanisani.

Kwa mawasiliano zaidi piga  0759029968 au 0659618585.
Popote ulipo utapata huduma zetu.
 
Follow us
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
 
     Bidhaa zetu zote ni garantii na unapewa risiti
              Karibu

Wavuvi 53 Zanzibar waliozama waokolewa

$
0
0
Watu 53 wanaosadikiwa kuwa wavuvi wamenusurika kifo baada ya boti yao kukumbwa na dhoruba na kuzama baharini eneo la Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Hasina Ramadhan Tawfiq alisema boti hiyo inafahamika kwa jina la Advantage na watu hao waliokolewa, na baada ya matibabu katika hospitali za Tumbatu na Kivunge waliruhusiwa kurejea makwao. 

Hasina alisema taarifa za tukio hilo walizipata juzi jioni baada ya kuokolewa kwa mmoja wao na meli ya Azam Link iliyokuwa ikitokea Pemba kwenda Unguja na kuwa boti hiyo ilizama saa nne asubuhi. Kamanda huyo alisema jitihada za uokoaji zilifanywa na vikosi vya KMKM, ZMA na Polisi. 

Mvuvi aliyeokolewa, Khatib Khamis ambaye ni mkazi wa Mtoni alisema chanzo cha tukio hilo ni upepo mkali ulioambatana na mawimbi yaliyosababisha chombo chao kupinduka. Alisema kabla ya tukio hilo walikuwa wanatokea Mtoni kuelekea Kisiwa cha Tumbatu kuvua.

Kamanda Sirro Awataka Watuhumiwa wa Dawa za Kulevya Wajisalimishe

$
0
0
Watu waliokuwamo kwenye orodha ya kuhojiwa kuhusu dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo Kikuu cha Polisi lakini hawakufika, wametakiwa kuripoti haraka. 

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro bila kutaja idadi alisema jana miongoni mwao wamo walioorodheshwa kwenye orodha iliyokabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga. 

“Niwaombe wote waliopokea wito wa polisi waje wahojiwe kwa sababu mtu akija mwenyewe ni tofauti na akisubiri nguvu ya dola kutumika kumkamata,” alisema Siro.

Wafaransa watua kuwekeza umeme

$
0
0
Zaidi ya kampuni 40 kutoka Ufaransa zipo nchini kuwekeza kwenye umeme utakaosambazwa vijijini. 

Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema jana kuwa, kampuni hizo zimekuja kwa majadiliano na sekta za umma kuhusu namna ya kuwekeza. 

Alisema wanaosimamia uwapo wa kampuni hizo ni Wizara ya Mambo ya Nje na Maendeleo ya Kimataifa ya Ufaransa chini ya Wakala wa Biashara wa nchi hiyo na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD). 

Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Fedha wa Korea Kusini, Song Eon-Seog amesema wametoa Dola 88 milioni za Marekani kusaidia uboreshaji wa mazingira kwa nchi za Afrika ikiwamo Tanzania.

Kamanda Sirro: Tumemkamata Aliyemuua Mpenzi Wake na Kumweka Kwenye Jaba la Maji

$
0
0
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata mtuhumiwa Musuguri David (29) anayedaiwa kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa kumchinja kisha mwili wake kuwekwa katika jaba la maji kisa wivu wa mapenzi maeneo ya Kibamba.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa hilo mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kumfumania aliyekuwa mpenzi wake wakiwa chumbani na mwanaume mwingine ambaye hata hivyo mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka.

Alieleza kuwa baada ya kifanikisha adhima yake mtuhumiwa huyo ya mauaji aliwatumia ndugu wa marehemu ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu (sms) akitumia namba ya simu ya marehemu akisema;

“Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani” ameeleza huku akisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine Sirro amesema wamewakamata raia watatu wa kigeni kutoka Afrika Kusini wakiwa na vipande viwili vya meno ya vinavyokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 45 na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ambao walikamatwa Machi 28 mwaka huu maeneo ya Upanga Dar.

Sirro ameeleza kuwa upelelezi juu ya watuhumiwa hao bado unaendelea ili kubaini kama walikuwa wanamiliki nyara hizo za serikali kihalali na mawasiliano kati ya Idara Maliasili yanaendelea.

Serikali Yatia saini Mkataba Wa Ushirikiano Wa Anga

$
0
0
Serikali ya Tanzania na Uganda zimesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano (BASA), katika usafiri wa anga utakaowezesha nchi hizo kutoa huduma bora za anga na kufungua fursa za kibiashara kwa wananchi wake.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo jijini Arusha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema mkataba huo utaruhusu ndege za nchi hizo mbili kutua na kuruka bila vikwazo vyovyote katika nchi hizo.

"Naamini ushirikiano huu utaboresha huduma zinazotolewa na Mamlaka za usafiri wa Anga na hivyo kuongeza viwango vya usalama wa usafiri huu", amasesema Prof. Mbarawa.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa, amesisitiza kuwa mkataba huo ni muendelezo wa ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Uganda na hivyo kuchochea maendeleo ya uchumi kwa raia wa nchi hizo.

Ushirikiano wa Tanzania na Uganda ni sehemu ya mkakati wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuwezesha wananchi wake kunufaika na fursa za kijamii, kiuchumi, kiusalama na kiutamaduni.

Waziri Mkuu Majaliwa Awakaribisha Wa Israel Kuwekeza Nchini

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Israel waje nchini kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya  kilimo.

Ametoa kauli jana (Jumatano, Aprili 5, 2017) alipokutana na Balozi wa Israel nchini Tanzania, Mheshimiwa Yahel Vilan, Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Tanzania na Israel ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri kwa muda mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.

Pia Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa Israel kuitembelea Tanzania kama watalii kwa sababu kuna fursa nyingi za utalii ukiwemo mlima wa Kilimanjaro na mbuga nyingi zilizosheheni wanyama.

Kwa upande wake, Balozi Vilan  ameipongeza Serikali kwa utendaji wake, ambapo amesema viongozi wa makampuni 50 kutoka nchini Israel wanatakuja nchini mwaka huu kushiriki katika jukwaa la biashara na uchumi kati ya Tanzania na Israel.

Amesema mbali na kushiriki katika jukwaa hilo, pia viongozi wa makampuni hayo watapata fursa ya kuangalia maeneo mbalimbali ya uwekezaji nchini.

Pia Balozi Vilan amesema Serikali ya Israel itaimarisha kitengo cha wagongwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hicho.

Mashahidi 30 Kutoa Ushahidi Kesi ya Mauaji ya Dr. Mvungi

$
0
0
Mashahidi 30 wa upande wa mashtaka wanatarajiwa kutoa ushahidi Mahakama Kuu katika kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi. 

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita alisema hayo jana alipowasomea washtakiwa Msigwa Matonya, Mianda Mlewa, Paulo Mdonondo, Longishu Losingo, Juma Mayunga na John Mayunda wanaokabiliwa na kesi hiyo maelezo ya mashahidi walioshuhudia tukio hilo na vielelezo ambavyo vitatumika wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo. 

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakili Mwita alisema watakuwa na vielelezo 13 ikiwamo ramani ya tukio na ripoti ya daktari kuhusu kifo cha Dk Mvungi. 

Washtakiwa hao wanadaiwa Novemba 3, 2013 katika eneo la Msakuzi Kiswegere lililopo wilayani Kinondoni walimuua kwa kukusudia Dk Mvungi.

Mbunge ataka Zanzibar ipewe fedha na Tanzania Bara ili ilipe Deni la umeme

$
0
0
Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Jaku Hashimu Ayoub ametaka makusanyo ya kodi na tozo mbalimbali za Serikali yapelekwe Zanzibar ili kulipia deni la umeme. 

Jaku alisema hayo wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, ambapo alisema kuna kodi zinazolipwa Tanzania Bara, lakini hazipelekwi Zanzibar kwa ajili ya kusaidia maendeleo ikiwamo kulipia deni hilo.

 Mbunge aliyedai kuwa na ushahidi juu ya kauli yake hiyo na kwamba yupo tayari kuutoa, alisema fedha hizo ni muhimu zikapelekwa ili zisaidie ulipaji wa malimbikizo ya deni la umeme. 

Machi 9, mwaka huu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lilitangaza kuikatia umeme Zanzibar kutokana na limbikizo la deni la zaidi ya Sh275.38 bilioni. 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema wameipa siku 14 kuhakikisha kuwa inalipa deni hilo. Hata hivyo, siku chache baadaye Tanesco ilitangaza kulipwa Sh10 bilioni kama malipo ya awali ili isikate umeme visiwani humo.

 Awali, katika swali la msingi, Mbunge wa Magomeni (CCM), Jamal Kassim Ali alitaka kujua iwapo Serikali haioni haja ya kodi ya mishahara (paye) kwa wafanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) isikusanywe visiwani humo kwa ajili ya kusukuma maendeleo. 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mapato sura ya 66, kifungu cha 4(a) na (b), kodi za kampuni ni za Muungano na zinakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 

Pia, alisema hata kampuni ambazo zimesajiliwa Tanzania Bara lakini zinafanya kazi Zanzibar, kodi zake zinakusanywa Bara. 

Naibu waziri alisema iwapo kampuni itakuwa imesajiliwa Zanzibar na ikawa na matawi Tanzania Bara inatakiwa kulipa kodi yake Zanzibar.

Mgogoro wa CUF Ulivyoibua Mvurugano Katika Uchaguzi wa Wabunge ELA.....

$
0
0
Wakati wabunge saba kati ya tisa watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (Eala) wakipatikana juzi usiku, suala la wawakilishi wa upinzani limetawaliwa na hali ya kutoeleweka, huku ikibainika rasmi kuwepo kwa CUF “A” na CUF “B”.


Kikao cha juzi kilichotawaliwa na mjadala wa kikanuni kuhusu wawakilishi wa Chadema na CUF, kiliweka rekodi ya kuchukua muda mrefu baada ya kumalizika saa 7:00 usiku kikikipiku kikao kilichojadili sakata la uchotwaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow. 

Bunge lilichagua wanachama sita wa CCM kuingia Bunge la Afrika Mashariki, pamoja na mmoja kutoka CUF, ambaye amezua mjadala baada ya jina lake kukubaliwa na msimamizi wa uchaguzi licha ya kusainiwa na naibu katibu mkuu wa chama hicho badala ya katibu mkuu ambaye aliwasilisha jina jingine. 

Waliopitishwa ni Fancy Nkuhi, Happines Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngawaru Maghembe na Alhaj Adam Kimbisa kutoka CCM, wakati Habib Mnyaa, aliyekuwa amevuliwa uanachama na CUF, alichaguliwa pia kuingia kwenye chombo hicho. 

Hata hivyo, wanachama wawili walioteuliwa na Chadema kuwania ubunge wa Eala, Ezekiah Wenje, aliyepata kura 124 za ndiyo na 174 za hapana, na Lawrence Masha, aliyepata kura 124 za ndiyo na 198 za hapana, hawajaingia kwenye chombo hicho, kitu ambacho kimeifanya Chadema kuamua kwenda mahakamani. 

Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema jana kuwa uchaguzi huo ulikuwa ni batili kutokana na taratibu kutofuatwa. 

Pia, hoja ya kuwepo kwa CUF A na B iliyozungumziwa na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi huo imeibua mvurugano kwa chama hicho ambacho kimekuwa na mgogoro na mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba tangu alipojiuzulu mwaka juzi na kujirejesha mwaka jana.

CUF na pande mbili
 Katika uchaguzi huo uliofanyika bungeni mjini Dodoma, CUF ilipeleka wagombea wanne baada ya upande wa Profesa Lipumba kutuma majina matatu huku upande wa Maalim Seif ukipeleka jina moja.

 Majina yaliyopelekwa na upande wa Profesa Lipumba ni Mnyaa, Thomas Malima na Sonia Magogo huku upande wa Maalim Seif ukipeleka jina la Twaha Taslima. 

Kitendo cha Dk Kashililah kutangaza kukubali majina ya pande zote mbili, kilifanya wabunge waanze kuhoji sababu za ofisi ya Bunge kukubali kupokea majina ambayo hayajasainiwa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. 

Akihoji suala hilo, Lissu alisoma barua ambayo ofisi ya Bunge ilimwandikia Maalim Seif kuthibitisha kupokea jina la Taslima na kuandika kasoro ambazo zilionekana katika fomu, akisema huo ni uthibitisho kuwa Maalim Seif ndiye katibu wa chama hicho.

 Alihoji sababu za kupokea fomu za upande mwingine wakati Maalim Seif yupo. Spika John Ndugai alisema hana taarifa za mawasiliano hayo na hivyo kumtaka katibu atoe maelezo.

 “Nafikiri anachokisoma (Lissu) ni sahihi na tuliandika. Msingi wa andiko letu ulitokana na barua ya tarehe 28 Machi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi,” alisema Dk Kashililah wakati akitoa maelezo. 

 “Hatukuviandikia vyama kuviomba, tulitoa GN 376, vyama viliandika vikaomba. Mimi sikuvitambua, aliyevitambua vyama ni mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Ninayo orodha ya CUF “A” wamewasilisha kupitia kwa naibu katibu mkuu, na CUF “B” kupitia kwa katibu mkuu.

 “Mheshimiwa Spika ni vizuri tuelewane. Katika barua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndipo viongozi wawili wa CUF wanapokutana na wala si ofisi ya msimamizi wa uchaguzi. 

"Mimi nieleze wazi. Kwani aliyepeleka jina la Mnyaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni nani? Na aliyepeleka jina la Taslima ni nani? Sasa mbona wote wameleta?” 

Hivi karibuni Profesa Lipumba alitangaza kumteua Sakaya kukaimu nafasi hiyo, akisema Maalim Seif hatii maagizo. Kwa mujibu wa katiba ya CUF, katibu mkuu huchaguliwa na mkutano mkuu wa chama. 

Akieleza utaratibu wa kuwathibitisha wagombea wa Eala, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Ramadhani Kailima alisema walipokea majina ya wagombea kutoka vyama vya siasa na kwa suala la CUF hawajui kuhusu mgogoro unaoendelea. 

“Sisi hatupitishi majina ya wag- ombea. Soma taarifa ya Spika kwenye GN (Gazeti la Serikali). Kazi yetu ni kuthibitisha wagombea. Mimi sijui kama kuna mgogoro CUF. Tena andika kwa wino mweusi kabisa,” alisema Kailima. 

“Sifa ya mtu kugombea ubunge ni lazima atokane na chama cha siasa na ni lazima awe raia wa Tanzania. Sasa kama amedhaminiwa na Maalim Seif au Lipumba, sisi hatujui kama kuna mgogoro.

“Mwenye jukumu la kusajili chama ni Msajili wa Vyama vya Siasa na akishasajili anawasiliana na taasisi nyingine. Kwa hiyo sisi tunaangalia uongozi alioutambua. Nec inaangalia sifa ya mtu kuwa mbunge, vyama vya siasa kama CCM, CUF Chadema ndiyo wanatuletea majina,” alisema Kailima. 

Alipoulizwa kuhusu katibu aliyetakiwa kutia saini za wagombea wa CUF, Kailima alisema Nec haifungwi na mgogoro uliopo.

 “Tume haifungwi, tunawasiliana na mwenyekiti au katibu. Mwenyekiti wa chama anawasiliana na mwenyekiti wa Tume na katibu mkuu anawasiliana na mkurugenzi wa uchaguzi,” alisema. 

“Ninyi si mliandika kuwa Magdalena Sakaya ameteuliwa kuwa kaimu katibu mkuu wa CUF na msajili akaridhia? Sisi tunawasiliana na huyo huyo pia. 

“Lipumba anawasiliana na mwenyekiti wa Tume na Maalim Seif anawasiliana na mimi mkurugenzi.” 

 Akizungumzia kuhusu wagombea watatu wa CUF, Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua, alisema alitia saini fomu zao kama kaimu katibu mkuu.

“Majina yalipelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuthibitishwa kisha yakapelekwa Idara ya Uhamiaji kuthibitisha uraia ndipo yakapelekwa kwa katibu wa Bunge,” alisema Sakaya. 

“Fomu zao nilitia saini mimi kama kaimu katibu mkuu kwa sababu katiba yetu inasema kama katibu mkuu hayupo, nafasi yake inakaimiwa na naibu katibu mkuu.” 

Bilioni 2 Zahitajika kusambaza gesi majumbani......Serikali yasema mradi utakamilika Julai, yafafanua mipango iliyopo

$
0
0
Bunge limeelezwa kuwa, Wizara ya Nishati na Madini inahitaji Sh2 bilioni kwa ajili ya kusambaza gesi majumbani katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani alisema jana kuwa, mradi wa usambazaji gesi unaweza kukamilika ifikapo mwezi Julai. 

Dk Kalemani alitaja kiasi kamili cha gesi kinachohitajika kwenye nyumba za watu katika mikoa hiyo ni mita za ujazo kati ya milioni tano hadi 10 ambazo uwezekano wa kupatikana ni mkubwa kwa kuwa gesi ipo ya kutosha. 

Naibu waziri huyo alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mtwara Mjini (CUF), Maftaha Nachuma aliyetaka kujua kiasi na gharama zitakazotumika kwa ajili ya usambazaji majumbani.

Katika swali la msingi, mbunge huyo alitaka kujua ni lini Serikali itasitisha usafirishaji wa gesi kutoka Mtwara kwenda Kinyerezi Dar es Salaam, ili wananchi wa Mtwara waweze kunufaika kwanza na ajira zitokanazo na uchakataji wa gesi hiyo asilia na kujenga viwanda.

Hata hivyo, naibu waziri alisema sera mpya ya nishati ya mwaka 2015 na Sera ya Gesi ya mwaka 2013 zinalenga kutoa fursa ya gesi asilia kuwanufaisha Watanzania wote, ikiwa ni pamoja na wananchi wa eneo inakopatikana rasilimali hiyo.

Alisema kuna miradi miwili inayosafirisha gesi asilia kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam. Dk Kalemani alisema mradi mmoja ni mpya unaosafirisha gesi kutoka Mtwara ambao ulikamilika mwaka 2015, huku mwingine ni wa Songas uliokamilika mwaka 2004 wakati gesi inayochakatwa Madiba, Mtwara inasafirishwa kwa bomba kwenda Mkuranga.

Alisema Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) inatekeleza mradi wa kuunganisha gesi hiyo katika Kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara ambacho kitahitaji takriban futi za ujazo 45 milioni.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images